Tuesday, 5 December 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 5, 2023

 

Magazeti ya leo
 

Share:

Monday, 4 December 2023

WIZARA YA AFYA YAJIDHATITI KUTOA HUDUMA BORA KWA WAHANGA WA MAFUTIKO


Na Mwandishi wetu,Manyara.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Afya mapema leo Disemba 4, 2023 wamewasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kuona hali ya utoaji huduma na kutoa pole kwa majeruhi 11 wa maafa ya mafuriko yaliyotokea katika mji wa Katesh Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara ambao wamelazwa katika Hospitali hiyo.

Dkt. Mollel amesema kuwa Wizara ya Afya imejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za matibabu ili kuokoa maisha ya watu, amesema kuwa hadi sasa Hospitali zote ndani ya Mkoa wa Manyara zimepokea na kuhudumia majeruhi 93 na wote wanaendelea vyema na matibabu.

Dkt. Mollel amesema kuwa Wizara ya Afya imeratibu upatikanaji wa timu za Madaktari kwa ajili ya kuongezea nguvu katika Hospitali za Mkoa wa Manyara ili kuweza kutoa huduma bora na kwa haraka zaidi kwa majeruhi ambapo amebainisha kuwa madaktari hao wametoka katika Mikoa ya Arusha, Dodoma na Singida.

“Huduma zinatolewa vizuri, hakuna kilichokosekana na wagonjwa wanaendela vyema na matibabu, kila kitu kinaenda vizuri kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza jana". Amesema Dkt. Mollel.

Mapema leo asubuhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sengida amesema kuwa idadi ya vifo vya watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko yaliyotokea imeongezeka kutoka watu 47 hadi kufikia 49 baada ya kupatikana kwa miili mingine miwili.

Hapo baadae Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kufika katika Mkoa wa Manyara kujionea hali ya maafa, kutembelea na kutoa pole kwa majeruhi pamoja na kufanya kikao na watendaji katika kushughulikia maafa ya Katesh.

Share:

MAPOROMOKO YA MATOPE HANANG' YAUA WATU 47, RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE



Na John Walter-Manyara

Juhudi za kuwaokoa watu waliokwama kwenye Matope zimeendelea Vijiji vya Katesh na Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara baada ya Mafuriko kuyakumba maeneo hayo na kusababisha vifo vya watu 47 na wengine 85 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga watu zaidi wanahofiwa kufukiwa na matope baada nyumba na makazi yao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo kutoka Mlima Hanang’.

Eneo kubwa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi na Katesh ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya ya Hanang’.

Nyumba za watu zimezingirwa na mafuriko na miti iliyosombwa na mafuriko kutoka sehemu ya Mlima Hanang yamesababisha barabara ya Katesh kwenda Singida kushindwa kupitika kwa muda.
Wakazi wa Hanang’ wamesema hawajawahi kushuhudia hali kama hiyo na kwamba kwao hilo ni janga kubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia tukio hilo na kuzitaka mamlaka zote zihamishie nguvu wilayani Hanang kutoa msaada wa haraka.
Share:

Sunday, 3 December 2023

DIT-MWANZA YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)-Kampasi ya Mwanza, imeadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kutoa semina elekezi kwa wanafunzi.

Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wanafunzi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo ukatili wa  kijinsia na namna ya kupinga vitendo hivyo.

Awali mwenyekiti wa dawati la njisia DIT-Mwanza, Bi,Consolata Ndimba ambaye pia ni mkufunzi chuoni hapo ameeleza  kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kujenga uwezo, uelewa na ushiriki wa kila mwanajamii katika kupinga ukatili wa kijinsia.

"Sisi viongozi wa dawati la njisia hapa DIT -Mwanza tumeona ni vyema tutumie fursa hii ya maadhimisho ya siku 16 kwa kutafuta wawezeshaji wa masuala mbali mbali ya kijinsia ili wawapatie mafunzo na stadi za maisha zitakazowasaidia kutimiza malengo yao wakiwa chuoni na hata baada ya kumalizia masomo yao, ilikusudi kila mwanafunzi aweze kujua nini chakufanya pindi anapokutana na kadhia hizi.'"amesema Bi,Ndimba.

Wakizungumza baadhi ya wanafunzi waliohudhuria mafunzo hayo, Grace Semule na Samwel Joshua  wamesema mafunzo yote yaliyotolewa yatawawezesha kujitambua pamoja na kuweka malengo yao ya masomo mbele zaidi na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zao.

Meshack Samwel ni moja wa wawezeshaji  katika maadhimisho hayo na daktari bingwa wa magojwa ya afya ya akili kutoka hospitali ya rufaa sekou Toure Jijini Mwanza amewahimiza wanafunzi kujitambua ili kuepukana  na madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao.

Naye mhadhiri na mwakilishi wa Mkurugenzi wa DIT  Kampasi , Bwana,Shija Mbitila amesema "Taasisi ya DIT Mwanza  inaungana na taasisi nyingine kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kutoa mafunzo elekezi, tukijua  madhara yanayotokana na ukosefu wa utambuzi kuhusu masuala hayo ni makubwa.

aidha Mbitila ameongeza kuwa "wanafunzi wetu kupitia mafunzo waliyopata yatawasaidia  kujitambua zaidi na kushiriki kupinga vitendo hivyo".

Taasisi ya DIT Kampasi ya Mwanza inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa semina hiyo ikiwa na lengo la kuwawezesha wanafunzi kutimiza ndoto zao za kitaaluma bila vikwazo vitokanavyonna vitendo vya kikatili.


Share:

WAZIRI PINDI CHANA ASISITIZA UADILIFU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO



Waziri Wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana akizungumza Disemba 3,2023 jijini Dodoma ,wakati akizindua Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, yanaongozwa na kauli mbiu ya ‘’Mapambano Dhidi ya Rushwa ‘’Zingatia Maadili, Utu, Uhuru na Haki kwa Watu Wote kwa Maendeleo Endelevu’
Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma Bw. Joseph Mwaiswelo akizungumza Disemba 3,2023 jijini Dodoma ,wakati wa uzindua Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, yanaongozwa na kauli mbiu ya ‘’Mapambano Dhidi ya Rushwa ‘’Zingatia Maadili, Utu, Uhuru na Haki kwa Watu Wote kwa Maendeleo Endelevu’

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri Wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana amesema uwepo wa vitendo vya rushwa inaifanya Serikali kushindwa kutekeleza ipasavyo jukumu lake la kuwahudumia wananchi ipasavyo na kusababu miradi ya maendeleo kushindwa kufanyika au kufanyika kwa kiwango cha chini kutokana na fedha zinazotengwa kutekeleza miradi hiyo, kuingia katika mikono ya watu wachache.


Balozi Chana ametoa kauli hiyo Disemba 3,2023 jijini Dodoma ,wakati akizindua Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ambapo amesema serikali kupitia TAKUKURU imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili kukabiliana na ubadhirifu ikiwemo rushwa.


"Serikali yetu imekuwa ikifanya juhudi kubwa, kudhibiti rushwa nchini na ninyi nyote ni mashahidi kwa kuwa mlimsikia Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiielekeza TAKUKURU kufanya ufuatiliaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili kukabiliana na ubadhirifu ikiwemo rushwa. Vita hii bado ni kubwa hivyo, nasi wanahabari tujitahidi kutumia vizuri kalamu zetu katika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kushiriki kwa vitendo katika kukataa na kufichua vitendo vya rushwa,"amesema Balozi Chana


Waziri huyo ameongeza kuwa Maadhimisho ya mwaka huu yanaadhimishwa sambamba na maadhimisho ya miaka 75 ya Tamko la Haki za Binadamu (‘’Universal Declaration of Huma Rights’’ ,tamko hilo tangu kutangazwa kwake tarehe 10 Desemba,1948 limeweka msingi wa mikataba mingine ya Haki za binadamu ambayo imefuata. Ni tamko ambalo limeainisha haki za kiraia, kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi.


Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeliweka Tamko hili katika Katiba zao ambapo Tanzania ni ibara ya 9 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kwamba Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu.


"Tunapoadhimisha Siku hii muhimu ya Maadili na Haki za Binadamu ni jambo muhimu tukumbuke kuwa tunapaswa kutekeleza wajibu wetu kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na hivyo, kuepuka kuathiri haki za binadamu kwa kushiriki rushwa. Wakati mwingine haki hizi za binadamu huathiriwa na tabia za baadhi ya watendaji wasio waadilifu ambapo rushwa huwa kigezo cha mtu kupata haki ya msingi,"ameeleza Balozi Chana


Akitoa taarifa kuhusu shughuli mbalimbali zitakazofanyika kuelekea kilele cha Maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU),Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma Bw. Joseph Mwaiswelo amesema kuwa Desemba 4,2023 kutakuwa na Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Juhudi dhidi ya Rushwa ambapo mada maalum itawasilishwa na kujadiliwa katika jukwaa hilo ambalo ni matarajio kuwa litachangia kuimarisha misingi ya uwajibikaji na uadilifu katika sekta ya umma na sekta binafsi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa .


Mwaiswelo amesema shughuli ya tatu iliyopangwa kufanyika wakati wa maadhimisho hayo ni kuwa na Wiki ya Huduma kwa Umma itakayoanza tarehe 5 hadi tarehe 10 Desemba, 2023 katika viwanja ya Nyerere, maarufu Nyerere Square ambapo wiki hiyo itatumika kutoa huduma mbalimbali ikiwamo elimu kuhusu majukumu ya Taasisi zitakazoshiriki, kujibu maswali au kutoa ufafanuzi kwa wananchi na huduma za afya.


Kilele cha Maadhimisho ya mwaka huu itakuwa Disemba 10, 2023 katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma na yanaongozwa na kauli mbiu ya ‘’Mapambano Dhidi ya Rushwa ‘’Zingatia Maadili, Utu, Uhuru na Haki kwa Watu Wote kwa Maendeleo Endelevu’. Kauli mbiu hii imekuja wakati muafaka kwani inatufanya tutafakari kwamba ili tupate maendeleo lazima tuzingatie maadili, utu, uhuru na haki za binadamu kwa watu wote ambayo ni masuala ya msingi sana kwa ustawi wa taifa letu na watu wake.
Share:

WAFANYAKAZI WA BARRICK BULYANHULU WASHIRIKI MBIO ZA ZERO MALARIA

Baadhi ya washiriki wakifurahi baada ya kumaliza mbio hizo

****
Wafanyakazi wa Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, uliopo halmashauri ya wilaya ya Msalala, Mkoani Shinyanga, mwishoni mwa wiki wameshiriki mbio za zenye urefu wa kilomita tano, kumi na 21 zilizoandaliwa na mgodi huo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kuhamasisha kutokomeza ugonjwa wa Malaria yenye kauli mbiu ya ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI ,WEWE NA SISI SOTE.

Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa karibuni tayari imewafikia wananchi wa kata za wilaya ya Msalala, ambao pia wamegawiwa vyandarua huku mikakati ya kupulizia dawa za kuua mbu majumbani na kwenye mazalio ya mbu zikiwa zinaendelea.

Afisa Raslimali Watu Mwandamizi wa Barrick Bulyanhulu,Renatus Malawa, akiongea na washiriki wa mbio hizo
Washiriki wakiwa katika ya pamoja baada ya kupewa medali za kushiriki
Baadhi ya washiriki wakikimbia
Baadhi ya washiriki wakikimbia
Washiriki wakipewa medali za ushiriki
Washiriki wakipewa medali za ushiriki
Washiriki wakipewa medali za ushiriki
Washiriki wakipewa medali za ushiriki
Washiriki wakipewa medali za ushiriki
Washiriki wakipewa medali za ushiriki
Washiriki wakipewa medali za ushiriki


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger