Friday, 24 November 2023

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI TAWI LA KIZUMBI SHINYANGA!! WAMSHANGAZA MENEJA WA HALOTEL 'KICHUO BONANZA'


Na Amo Blog Shinyanga

Tamasha la michezo la "Kichuo Bonanza" lafanyika katika uwanja wa michezo wa Ushirika na wanachuo wa MoCU waibuka na ushindi katika michezo yote.


Bonanza hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Halotel kwa kushirikiana Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) limewakutanisha wanachuo wa mwaka wa wWanza na mwaka wa pili na wa tatu ikiwa ni sehemu ya kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho cha MoCU .

Timu hizo zimeshindana katika michezo ya mpira wa miguu (wanaume na wanawake), mpira wa pete na mpira wa wavu.

Akizungumza na Wanachuo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo kikuu cha ushirika Moshi Tawi la Kizumbi Beatrice Karia amemshukuru meneja wa kampuni ya Halotel kwa kudhamini bonanza hilo huku akiwataka wanachuo wa mwaka wa kwanza kudumisha umoja na mshikamano baina yao na wanachuo waliowakuta katika chuo hicho maana kufanya hivyo kutasaidia kuchochea maendeledo ya chuo hicho.

Naye meneja wa Kampuni ya Halotel Mkoa wa Shinyanga, Frank Mashauri amewataka wanachuo kuendelea kufanya mazoezi huku akiwashauri kutumia mtandao wa Halotel kwa kununua vifurushi vitakavyowawezesha wao kujisomea na kujifunza mambo mbalimbali yatakayosaidia kuinua kiwango cha taaluma maana wanazo ofa za wanachuo zinazo patikana kwa bei nafuu.
Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa pili na wa tatu wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakishangilia ushindi zawadi ya mbuzi kutoka halotel baada ya kuwafunga wanachuo wa wa mwaka wa kwanza katika mchezo wa mpira
wa Netiboli


Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakionyesha umwamba wao wakati wa kuvuta kamba.
Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga baada ya kuwanyoosha Wanachuo wa mwaka wa pili kwa kichapo cha magoli mawili kwa moja .
Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa pili chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga baada ya kukubali kunyooshwa na Wanachuo wa mwaka wakwanza kwa kukubali kichapo cha magoli mawili kwa moja .
Wafanyakazi chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakiendelea kufurahia burudani.
Mwakilishi wa Mkurugenzi chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Beatrice Karia akizungumwa na wanachuo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Chuo hicho wakati wa bonanza .
Mwakilishi wa Mkurugenzi chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Beatrice Karia katikati akizungumza na wanachuo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Chuo hicho Kulia akiwa ni Meneja Wa kampuni ya Halotel mkoa wa Shinyanga Frank Mashauri.
Meneja wa kampuni ya Halotel mkoa wa Shinyanga Frank Mashauri akizungumza
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakionyesha vipaji vyao katika ukumbi wa chuo hicho.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakionyesha vipaji vyao katika ukumbi wa chuo hicho.
Mmoja wa wana chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga akionyesha kipaji chake katika ukumbi wa chuo hicho.
Viongozi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakifurahia burudani mbalimbali katika ukumbi wa chuo hicho.
Viongozi wa Serikali ya wanachuo wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakifurahia burudani mbalimbali katika ukumbi wa chuo hicho.
Wanachuo wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakitoa burudani mbalimbali katika ukumbi wa chuo hicho.
Wanachuo wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakifurahia burudani mbalimbali katika ukumbi wa chuo hicho.
Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa Kwanza wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakicheza mchezo wa Vollebo katika uwanja wa mpira wa Volebo.
Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa pili na watatu chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakicheza mchezo wa Vollebo katika uwanja wa mpira wa Volebo.
Viongozi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakifurahia burudani katika uwanja wa mpira wa Volleyball
Viongozi wa Serikali ya wanachuo wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakifurahia burudani uwanjani.
Wanachuo wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakijiunga na huduma za Halotel kutoka kwa mawakala wa kampuni hiyo.

Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa pili na watatu chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakicheza mchezo wa Vollebo katika uwanja wa mpira wa Volebo.
Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa pili na watatu chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakicheza mchezo wa Vollebo katika uwanja wa mpira wa Volebo.
Timu ya Wanachuo wa Mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakicheza mchezo wa Vollebo katika uwanja wa mpira wa Volebo.
Viongozi wa Kampuni ya Halotel wakikabidhi zawadi kwa wasdhindi wa michezo mbalimbali.
Viongozi wa Kampuni ya Halotel wakikabidhi zawadi kwa wasdhindi wa michezo mbalimbali.




































Share:

RAFIKI ZANGU WALIONIIBIA GARI WAKUTANA NA MAMBO MAZITO!

Imepita miaka sita tangu gari langu aina ya Toyota Hilux  lipotea, nilijaribu juu chini kulitafuta lakini wapi, halikupatikana, nakumbuka vizuri jinsi kisa hicho kilitokea.

Nlikuwa nafanya kazi na kampuni moja maarufu sana nchini nikiwa kama mfanyikazi wa kawaida hadi nilipopandishwa daraja hadi nikawa Meneja.

Baada ya kupandishwa daraja na mshahara wangu uliongezeka hivyo nikaamua kununua gari kwa ajili ya kwenda kazi kwa sababu nilikuwa nimechoka kupanda matatu na hata kutembea.

Kwa kweli rafiki zangu wengine hawakurahia mafanikio yangu, ila baada ya miezi kadhaa rafiki zangu wengine wakawa wananikodi gari langu na kwenda nalo sehemu mbalimbali.

Siku moja nilichelewa kutoka kazini kwa vile kwangu nyumbani ni mbali niliamua kupitia njia ya mkato ili nifike haraka sikujua ilikuwa siku ambayo gari langu lingeibiwa.

Nilipokuwa napita njia ile niliona gari lingine likinifuata nyuma, ghafla gari langu liligongwa kutoka upande wa nyuma, niposimama walitoka watu wanne wakiwa na slaha na kuniagiza nishuke na niwape ufunguo wa gari. Niliposita kuwapa nilizabwa makofi na kichapo kikali ndipo nilipopoteza fahamu, na hapo ndipo gari langu lilipotea.

Nilipopata fahamu nilijikokota hadi nyumbani nisijue nianzie wapi nimalizie wapi, siku ilifuatia nikapiga ripoti kwa polisi ili wanisaidie kutafuta gari langu Lililopotea.

Kuna siku mmoja nilikuwa napitia mambo kadha kwenye mtandao wa kijamii ndipo nikapata namba ya African Doctors, nilikuwa na hofu lakini nilijikaza na kuwapigia, walinitoa hofu na kunifanyia dawa zao ambazo zilikuja kufanikisha kupatikana kwa gari langu.

Baada ya siku kama mbili hivi, nikiwa nyumbani walikuja rafiki zangu ambao ninafanya nao kazi, walipiga magoti huku wakiniomba msamaha kwamba ni wao ndio waliochukuwa gari langu na wamelirejesha. Walisema waliyaona mambo yasiyo ya kawaida na yaliyowatatiza maishani mwao!. 

Mara tu gari la polisi lilifika kuwachukuwa, nawashukuru sana African Doctors kwa kunisaidia kupatikana kwa gari langu, pia kumbuka wanatibu magonjwa kama kifua kikuu, saratani ya mapafu, kisonono na mengine mengi.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com

Mwisho.


Share:

WAZIRI MKUU AJIONEA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA NSSF

#Ni katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ambayo yanaenda sambamba na elimu ya hifadhi ya jamii

NA MWANDISHI WETU ARUSHA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alitembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa, katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha 2023 yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Mkoani Arusha.

Wiki ya Fedha 2023, imebeba kauli mbiu isemayo 'Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo Kiuchumi' ilizinduliwa na Waziri Mkuu, tarehe 22 Novemba, 2023.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele alimueleza Mhe. Waziri Mkuu huduma zinazotolewa katika banda hilo ambazo zinaenda sambamba na elimu ya fedha kwa upande wa kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao kwa upande wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Lulu alisema NSSF inatumia fursa hiyo kuwakumbusha baadhi waajiri wa sekta binafsi kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati ili kuepusha usumbufu kwa wanachama pindi wanapotoka kwenye ajira kwa mujibu wa sheria ambapo elimu hiyo inaenda pamoja na elimu ya fedha kwa kuwajengea uelewa wanachama wake na jamii kutambua mambo muhimu yanayoweza kuwaendeleza kiuchumi.

Vilevile, Lulu alimueleza Mhe.Waziri Mkuu kuwa NSSF inatumia fursa ya Wiki ya Huduma za Fedha kuendelea kutoa elimu kwa wananchi waliojiajiri wenyewe wakiwemo wakulima, wafugaji, mama lishe, bodaboda kujiunga na kuchangia NSSF kwa ajili ya maisha yao ya sasa na baadaye.

Alisema Mfuko unaendelea kutatua kero mbalimbali za wanachama na wadau wake kwa kuboresha huduma kupitia mifumo mbalimbali ya TEHAMA ambapo kupitia mifumo hiyo wanachama wanaweza kupata taarifa zao popote walipo bila ya kulazimika kufika katika Ofisi za NSSF.

Naye, Furahisha Wabanu, Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa wa Arusha, aliwakaribisha wananchi wote kutembelea banda la NSSF kwa ajili ya kupata huduma zote zinazotolewa na Mfuko ikiwemo elimu ya hifadhi ya jamii, kujiunga na kupata kadi zao papo hapo, kupata taarifa zao za michango na kupata elimu kuhusu uwekezaji.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger