Wednesday, 22 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 22,2023











Share:

Tuesday, 21 November 2023

TRAVELING BY BUS JOHANNESBURG, SOUTH AFRICA TO TANZANIA



Exciting news for Tanzanian travelers! Mkombe Luxury Bus, a Tanzanian company with its base in Johannesburg, South Africa, has introduced a convenient and comfortable travel solution. Now, individuals can easily journey by bus from Dar-Es-Salaam to Johannesburg, South Africa using the new buses provided by Mkombe Luxury Bus.


This innovative transport option is set to simplify trips between Tanzania and South Africa. Travelers have the opportunity to utilize the services of Mkombe Luxury Bus for their journeys. The fare for a one-way trip stands at 350,000 Tanzanian Tshs. Alternatively, travelers can opt for a round-trip fare of Tsh 700,000 (seven hundred thousand Tanzanian Tshs). To facilitate ticket booking, Mkombe Luxury Bus has established offices on Shekilango Street in Dar-es-Salaam. Additionally, tickets can be obtained through What's App at +27604749717

This travel option allows Tanzanian and South African travelers to transit through Zambia, experience the majestic Victoria Falls in Zimbabwe, and finally arrive in Johannesburg, South Africa. The entire journey takes approximately three days to complete. Mkombe Luxury Bus stands as a patriotic company that aims to enhance the ease of travel to and from South Africa. Moreover, the company offers luggage transportation services, ensuring a hassle-free experience for passengers.


The buses themselves are equipped with amenities that guarantee a pleasant journey. Passengers can expect amenities such as a toilet, TV, and WiFi internet access throughout the entirety of the trip. Mkombe Luxury Bus not only provides transportation but also offers a unique and enjoyable travel experience.

For Tanzanians embarking on this transportation adventure, Mkombe Luxury Bus presents an outstanding travel opportunity. With their comprehensive services and commitment to quality, Mkombe Luxury Bus has become a significant player in the realm of Tanzanian-South African travel. Traveling with Mkombe Luxury Bus is not just a journey; it's a testament to the dedication and advancement of Tanzanian tourism. keep in touch or booking What's App at +27604749717


Share:

"WANANCHI MKOA WA MARA KUTOYUMBISHWA NA WAPINZANI, PUNDA HASIFIWI KWA MARINGO BALI MZIGO ALIOUBEBA"

Na, Deborah Munisi


"Kama yupo mtu anayeipinga CCM ni wivu wake binafsi kwasababu katika sekta ya maendeleo inatekeleza kwa kasi, msiyumbishwe na kelele za wapinzani, kufuatia maendeleo haya CCM ina kila sababu ya kutembea kifua mbele"

Ni kauli ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Patrick Chandi wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nyasho, Musoma Mjini Mkoa wa Mara Novemba 21, 2023 ikiwa ni mwendelezo wa Ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa inayoongozwa na mwenyekiti huyo ambaye ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara.


Akihutubia wananchi hao amewataka kutoyumbishwa na kelele za wapinzani kwani maendeleo wanayoyaona kwasasa yametokana na msingi bora wa chama tawala wa kuwajali na kuwathamini wananchi wake kwa zaidi ya miaka 60 baada ya ukoloni.


"Punda hasifiwi kwa maringo bali kwa mzigo mzito alioubeba, kwasasa tukiwa na uhitaji wa huduma za afya tunazipata bila tabu yoyote, na hili suala la katiba iliyopo inawazuia kuoa?, msidanganyike hawana jambo zuri la kuwaeleza, Chama tawala kimewahudumia kwa zaidi ya miaka 60 na wakoloni hawakutuachia maendeleo bali maendeleo hayo yamepatikana ndani ya chama Cha Mapinduzi CCM", amesema Chandi

Kwa upande wake Mwita Waitara Mbunge wa Tarime vijijini amewaasa wananchi wa Mkoa huo kuunga viongozi wao mkono ili kukuza maendeleo badala ya kuyadidimiza kwa kutafuta wagombea wao mfukoni na kama ni suala la uchaguzi kila mtu ataonyesha alichokifanya.

"Tunataka siasa tulivu, Hakuna mbunge anayeweza kugawa sukari na matumizi kwenye familia zetu anachokifanya ni kutekeleza majukumu ya kijamii ambayo yanamgusa kila mwananchi na endapo akigundua kuna wagombea wameandaliwa pembeni anaenda Bungeni mwili tu huku akili inabaki jimboni, akirudi anakuja kujibu mapigo na hapo maendeleo lazima mchelewe" ,amesema Mhe. Waitara

Suala la wapinzani nalo akasema “Uchaguzi ujao kila mtu atakula alikopeleka mboga, wameanza kuhaha walianza na bandari, sasa wanaimba katiba, tutakuja na wao watakuja kila mtu aseme na kuonyesha alichofanya, barabara ni mwendo wa kuteleza, kule Tarime kwenda Serengeti, shule za mchepuo wa sayansi nchi nzima, miradi ya kimkakati ya maji mkoani Mara, wapeni salaamu hao watoa taarifa, Mara ni mkoa wa kiumeni, watajua hawajui CCM ndo habari ya mjini,”amesema Waitara.


Naye Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Vedatus Mathayo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani maendeleo Jimboni humo yametekelezwa kwa asilimia mia moja ikiwemo huduma za afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara huku utekelezaji wa soko na kusambaza umeme wa REA kwa wananchi wasio na umeme mchakato unaendelea.

"Suala la miundombinu ya barabara hivi karibuni zinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, na kabla mwezi huu haujaisha mkandarasi anatarajiwa kuingia site kwaajili ya kuingiza umeme wa REA kwa kila mwananchi", amesema Mbunge huyo.

Awali akiwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Musoma mjini uliofanyika katika ukumbi CCM Mkoa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma mjini kimemkabidhi cheti Patrick Chandi (MNEC) na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara kwa kuchaguliwa kwa kura za kishindo na kwa kazi nzuri anazoendelea kuzifanya za kuimarisha chama na jumuia zake.


Hata hivyo katika ziara hiyo Chandi amepokea na kusikiliza kero za wananchi na wanachama na kuzitatua na nyingine zikatolewa maelekezo kwa lengo kuzitafutia uvumbuzi, ambapo miongoni mwa kero zao zilikuwa ni Migogoro ya ardhi, Uvuvi haramu, ‘kikokotoo’ kisicho rafiki kwa watumishi, kadi ya bima ya kutodhamiwa, Mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutotibiwa kama Ilani ya CCM inavyoelekeza.
Share:

SIMBACHAWENE AITAKA TAKUKURU KUSIMAMIA MALALAMIKO YA RUSHWA NCHINI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene. 

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Rashid Hamduni. 

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene, amekiri kuwa bado yapo malalamiko mengi ya wananchi kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika ofisi za umma hali inayosababisha wengi wao kushindwa kuzifikia huduma wanazozihitaji.

Simbachawene, aeleza hayo leo November 20,2023 jijini hapa, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).

Amesema bado yapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwepo kwa rushwa katika taasisi mbalimbali hali ambayo inasababisha wananchi kukosa huduma ambazo wanazihitaji.

“Bado suala la rushwa ndogondogo ni tatizo sana kwa wananchi wetu na huko ndiko yapo malalamiko mengi ya watu kutokana na rushwa hiyo kuwanyima fursa ya kupata huduma.

“Huduma hizo ni pamoja na elimu ngazi za chini kati hadi vyuo vikuu, lakini pia huduma za afya,kodi na leseni ambako kumewekwa utaratibu mgumu na ukilitimba katika utoaji wa huduma ili tuu watu watoe rushwa ndipo wahudumiwe”amesema Simbachawene

Aidha, amesema kutokana na hali hiyo kila taasisi inatakiwa kutengeneza mkataba wa huduma kwa wateja na TAKUKURU iwe nao kama sehemu ya kufuatilia utekelezaji wake.

“Tukitoka tuu hapa tukaenda pale hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma General tukajificha mahali na kuangalia namna shughuli zinavyoendelea kama ni muhudu au daktari atakuwa anatoa huduma bora tutaona na kama kuna muhudumu ambaye atakuwa hatoi huduma bora tutabaini hivyo hizi rushwa ndogondogo zinakera sana wananchi kuliko hata hizi za ubadhirifu wa mabilioni ambayo wao hawayaoni”amesisitiza Simbachawene. 

Kadhalika, amesema TAKUKURU, inapaswa kuendeleza kushughulikia watu wote ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa nchini bila kuangalia hali zao.

“Lazima tuwashughulikie watu wote wanaojihusisha na rushwa nchini zipo rushwa zinaoekana kabla ya kukamilika kwa miradi lakini zipo ambazo zinaanza kuonekana baada ya miaka mitatu tangu kukamilika kwa mradi hivyo wahusika wote wanatakiwa kukamatwa na kuhojiwa hata kama watakuwa wamestaafu”alisema

Amesema hali hiyo itasaidia kukomesha tabia amabzo zimeluwa zikifanywa na watumishi wa umma kujihusisha narushwa na kuhama kituo cha kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Rashid Hamduni alisema, mkutano huo ni wa siku tatu ambapo lengo lake ni kujadili mafaniko na changamoto kwa mwaka uliopita ili kuzipatia suluhu.

Amesema katika kipindi cha mwaka uliopita taasisi hiyo, imeokoa kiasi cha Sh. bilioni 171.9 ambazo zingeingia mifukoni mwa watu kama TAKUKURU, isingefanya oparesheni mbalimbali kwenye miradi ya umma.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 21,2023

Share:

Monday, 20 November 2023

MOTO WATEKETEZA BWENI LA WANAFUNZI CHUO CHA KIISLAMU MULEBA



Na Mariam Kagenda - Muleba

Moto umeunguza vifaa vyote vya wanafunzi wa chuo cha Kiislamu cha Umaru Ibn Khatwabi kilichopo kata ya Muleba wilayani Muleba mkoani Kagera wakati wanafunzi hao wakiwa msikitini.

Mkuu wa  wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga amesema kuwa taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha moto huo ulioanza alfajiri ya jana kimetokana na hitilafu ya umeme katika bweni la wanafunzi wa chuo hicho.

Dkt. Nyamahanga amesema kuwa hakuna mwanafunzi yeyote aliyedhurika   kwani wakati moto huo unatokea walikuwa msikitini ambapo vitu vilivyoungua ni magodoro 69 na vitanda pamoja na vifaa vyote vya wanafunzi.

Amesema kuwa mpaka sasa serikali kwa kushirikiana na mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Dkt Oscar Ishengoma Kikoyo wamefanikiwa kutoa magodoro 69 pamoja na mablanketi 69 ambapo amewahimiza wadau wa maendeleo kuendelea kutoa msaada kwa watoto hao kwani vifaa vyao vyote vimeungua.

Naye mkuu  wa chuo hicho Hassan Juma amesema kuwa chuo hicho ni cha kidini ambacho kinatoa mafunzo ya dini ya Kiislamu kwa watoto wa kiume ambapo kina jumla ya wanafunzi 69 na baada ya moto huo kutokea wanafunzi wote wako salama.

Ameongeza kuwa wanafunzi hao wamehamishiwa kwenye jengo jingine kwani hata paa za bweni zimeungua hivyo linatakiwa kukarabatiwa.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger