Sunday, 19 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 19 , 2023

 


 
   
Share:

Saturday, 18 November 2023

WASTAAFU WAASWA KUZINGATIA NIDHAMU YA FEDHA BAADA YA KUSTAAFU

 


Na Mwandishi Wetu; Morogoro

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Kitengo cha Ukuzaji Tija imetoa mafunzo ya kujiandaa na maisha baada ya kustaafu kwa watumishi wanaotarajiwa kustaafu na kuwaasa kuwa na nidhamu ya fedha na waangalifu kwenye miradi watakayowekeza.

Akifunga mafunzo hayo ya siku tano kwa watumishi hao kutoka Takukuru, Dawasa, Rita, Feta na Chuo cha Ustawi wa Jamii, Novemba 17, 2023 Mjini Morogoro, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali wa Ofisi hiyo, Leonard Mchau amesema watumishi wanapostaafu wamekuwa wakihamasishwa kutumia mafao yao kuwekeza kwenye miradi isiyo na tija na kusababisha mafao kupukutika.


Aidha Mkurugenzi Mchau ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa Wastaafu kupata fursa ya kupata mafunzo hayo yenye kaulimbiu ‘Kustaafu Sio Mwisho wa Maisha.’

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija wa Ofisi hiyo, Yohana Mdadi ameeleza kuwa kitengo hicho kina wajibu wa kutoa na kuratibu mafunzo hayo na kuwashukuru wastaafu kwa kushiriki kupata elimu muhimu ya kujiandaa kustaafu.

Naye, Mshiriki kutoka DAWASA, Poncean Muyaga ameishukuru serikali kwa kuwezesha kupata mafunzo hayo na kwamba elimu waliyoipata itawasaidia kuondoa hofu na kujiandaa katika uwekezaji wenye tija.

Share:

TBS YATOA LESENI NA VYETI VYA UBORA 145 KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga akikabidhi leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam

**************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa vyeti na leseni 145 kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 17,2023 wakati wa Zoezi hilo lililofanyika katika Ukumbi wa TBS Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga amesema kuwa kati ya vyeti hivyo, vyeti vya ubora wa mifumo (system certification) vilivyotolewa ni sita (6) na Leseni zilizoongezewa bidhaa (Licence extension) ni 13.

Aidha, Bw. Msasalaga amesema kuwa leseni na vyeti 60 ambayo ni sawa na asilimia 43 vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo.

“Vyeti na leseni zilizotolewa ni za bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vilainishi, vitakasa mikono, vifaa vya umeme, vifaa vya makenika, vibebeo pamoja na vifungashio”. Amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa Jukumu la usajili wa vyakula, vipodozi na majengo limetokana na marekebisho ya sheria ya Viwango yaliyofanywa na sheria ya fedha ya mwaka 2019, na kwa mabadiliko hayo, ‘hakuna bidhaa ya Chakula au vipodozi itakayoruhusiwa katika soko la Tanzania kama haijasajiliwa au kuthibitishwa ubora wake na TBS’ [The Finance Act, section 17 (a) (m)].

“Kwa kipindi cha kuanzia mwezi June mpaka Novemba 2023 tumekwisha sajili majengo -1003- ya biashara na ya kuhifadhia bidhaa za vyakula na vipodozi. Pia kwa kipindi hicho tumeweza kusajili bidhaa 906 za vyakula na vipodozi”. Amesema Bw. Msasalaga

Hata hivyo amewataka wazalishaji wa bidhaa kuzalisha bidhaa zenye Ubora kabla ya kuingiza sokoni ambapo itawasaidia kulinda soko lao kitaifa na kukuza wigo wao wa biashara kutokana na kuwa na alama ya ubora na kulinda afya ya mlaji.

“Unapokua na alama ya ubora ya TBS wateja wetu watapata imani zaidi kwa bidhaa zetu tunazozizalisha na kwa kuwa imani ya walaji inaongezeka utaona zitakubalika sokoni na utapata faida ya Ushindani na utapeleka bidhaa yako yoyote ndani ya Afrika mashariki." Amesema

Kwa upande wake Mjasiriamali wa bidhaa za Choya, Bi.Elizabeth Mtei ameishukuru TBS kwa kuwapatia leseni bure kama wajasiriamali wadogo ambayo imewaongezea wigo wa kuuza bidhaa zao nje ya mipaka ya nchi na amewashauri wajasiriamali wengine kujitokeza TBS kukaguliwa bidhaa zao ili watanue fursa yao kibiashara.

Naye Afisa Masoko wa Kilimanjaro Cable,Bw.David Tarimo amewaasa Watanzania kuamini bidhaa zinazozalishwa katika Viwanda vya ndani kwani TBS na Serikali imewaamini na kuwapatia leseni.

Katika kipindi cha mwaka 2023 TBS ilitwaa tuzo ya Shirika Bora la udhibiti barani Afrika, ambayo imechagizwa na usimamizi mzuri na udhibiti katika kuhakikisha bidhaa ina viwango na ubora unao stahili.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga akikabidhi leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga akikabidhi leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga akizungumza katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wadau na wazalishaji wa bidhaa nchini wakiwa katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam

( PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share:

WIZARA YA NISHATI KUBORESHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - KAPINGA

 



*Nishati Safi si anasa, kaya zote kufikiwa*

Wizara ya Nishati imelenga kuboresha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kutokana na umuhimu wa afya za Watanzania na Mazingira. Inakadiriwa Watanzania zaidi ya asilimia 80 wanatumia  vyanzo vya nishati ya kupikia  ambavyo si salama na vyenye madhara ya kiafya, kiuchumi na kimazingira. 

Akimuwakilisha Mgeni rasmi  Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko,  wakati wa kukabidhi hundi za takribani Shilingi Bilioni 9 za Kitanzania fedha za ruzuku zinazofadhiliwa  na Nchi za Umoja wa Ulaya (EU)  kupitia mfuko wa *CookFund* kwa wajasiriamali 44 wanaojihusisha na Mradi wa Nishati Safi ya Kupikia leo Novemba 17, 2023. 

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema, jitihada zinazofanyika zitasaidia kupunguza utegemezi wa Nishati zisizo safi na kuunga mkono jitihada za  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alihimiza uwepo wa programu endelevu za matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia zinalenga kusaidia Wananchi na kujikwamua katika hali za kiuchumi.

"Kwa kweli kwa niaba ya Wizara tunapenda kuwapongeza  Umoja wa Ulaya (EU), kwa mradi huu kabambe wa kuboresha na kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia, lakini vilevile mradi ambao unachagiza maendeleo katika Sekta ya Nishati nchini," amesema Kapinga. 

Aidha, ameongeza kuwa programu hiyo ni muhimu kwa Wizara na washirika kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Wizara ya fedha ambao kwa pamoja wameendelea kuboresha mnyororo wa thamani kutokana na umuhimu wa Nishati safi ya kupikia kwa ustawi wa Taifa. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Nchi za Umoja wa Ulaya (EU) Cèdric Merel amesema, suala la Nishati safi ya kupikia lisichukuliwe kuwa ni la anasa na kwamba hitaji hilo lifikie kila kaya bila kujali hali ya kipato kwani inasaidia kuokoa muda, ni rahisi kutumia na inalinda mazingira. 

"Maono ya Serikali ni kuhakikisha inafikia lengo lake la asilimia 80 ya Watanzania kutumia Nishati Safi ya kupikia mpaka ifikapo mwaka 2033, nishati hii safi ya kupikia pia ipatikane kwa urahisi, na kwa ufanisi na kwa gharama nafuu," Cèdric Merel

Awali, Meneja Mradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la (UNCDF), Emmanuel Muro amesema, utekelezaji wa mradi huo umeingia mwaka wa pili na unalenga kupunguza athari za uharibifu wa mazingira na kwamba asilimia 80 ya Watanzania wanahama kutoka katika matumizi ya nishati isiyo safi na kuwataka wadau kuendelea kutoa ushirikiano ili kufanikisha lengo. 

Mradi huo wa Nishati Safi ya kupikia  unafadhiliwa na Nchi za Umoja wa Ulaya (EU), ukitekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali (UNCDF), kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) chini ya usimamizi wa Wizara ya Nishati.

Hafla hiyo ya utoaji wa hundi kwa wajasiriamali wa Nishati Safi ya Kupikia (44) imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga, Mkuu wa Nchi za Umoja wa Ulaya  (EU) Cèdric Merel, Wataalam kutoka (UNCDF) na Wizara ya Nishati.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 18,2023

]
Share:

Friday, 17 November 2023

OFISI YA WAZIRI MKUU KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO KUWEZESHA VIJANA NCHINI




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Bw. Mark Schreiner (kushoto) walipokutana katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (Unicef), Elke Wisch (kushoto) walipokutana katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akieleza jambo wakti wa kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemaja akieleza jambo wakti wa kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Bw. Mark Schreiner akieleza jambo wakati wa kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) walipokutana katika Ofisi ya NSSF, Benjamin Mkapa Tower, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2023.



Na, Mwandishi Wetu: Dar es Salaam

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuwezesha vijana kutumia fursa za kiuchumi kujiletea maendeleo.

Amesema hayo, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipokutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango na Maendeleo (UNDP) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (Unicef) nchini.

Aidha, Waziri Ndalichako ameeleza kuwa Ofisi hiyo itaendelea kukuza ushirikiano na Wadau hao wa Maendeleo maendeleo katika kuendesha programu na miradi ya uwezeshaji maendeleo ya vijana sambamba na kuimarisha ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

Vile vile, Prof. Ndalichako amepongeza wadau hao kwa namna wanavyoendelea kuchangia jitihada za Serikali za kuinua na kuimarisha ustawi wa maendeleo ya vijana kupitia Programu na miradi mbalimbali inayotekeleza hapa nchini. Sambamba na hayo amewahakikishia kuwa wadau hao Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amehamasisha wadau hao kuwezesha vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kupata ujuzi utakaowasaidia kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kujikwamua kiuchumi.

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja amemshukuru Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kwa namna shirika hilo lilivyojitoa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika mkoani Manyara, mwaka huu 2023.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka katika ofisi hiyo.
Share:

MWENYEKITI WA BODI YA NISHATI VIJIJINI AAGIZA MIRADI YOTE IKAMILIKE KABLA YA DESEMBA 2023





Na Veronica Simba-REA


Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika Wilaya za Nachingwea, Nanyumbu, Masasi na Tandahimba kukamilisha miradi yao ifikapo Desemba 31, mwaka huu.

Pia amewaelekeza kuhakikisha ubora, weledi na kukamilika kwa wakati miradi yote wanayoisimamia ili wananchi wapate huduma kwa muda uliopangwa.

“Nishati ni kila kitu, usalama, uchumi, siasa, afya na maeneo mengi, hivyo, jukumu la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni kuhakikisha kuwa wanawapatia wananchi umeme ili waweze kutimiza malengo yao,” amesema Balozi Kingu.

Amesema hayo katika kikao chake na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya nishati vijijini katika Mkoa wa Mtwara ambapo amewataka watendaji wa REA na TANESCO kuwafuatilia kwa karibu kuhakikisha kuwa lengo la kuvifikia vijini vyote ifikapo Juni 30, 2024 linafikiwa.

Wakandarasi hao , NAMIS Corporate na Central Electrical International Co, wametakiwa kuongeza nguvukazi na upatikanaji wa vifaa kwa wakati ili ifikapo Novemba 30, 2023 vijiji vyote walivyopangiwa kimkataba viwe vinawaka umeme.

Amewaagiza kutumia vifaa vinavyozalishwa  na kupatikana katika viwanda vya ndani ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi na kuagiza nje vile tu ambavyo havipatikani nchini.

Ametaka kikao cha tathmini kifanyike Desemba Mosi mwaka huu  na wakandarasi hao na kuona kama wako katika muda uliopangwa na endapo kuna changamoto waone namna bora ya kuzitatua kwa pamoja.

Pia amewataka Wakandarasi kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa kazi zao kila wiki ili kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amempongeza Balozi Kingu kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Rais Samia katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi na kuongeza kuwa anaamini kwa sifa yake ya uchapakazi, REA itaendelea kupata matokeo chanya zaidi.

Kanali Ahmed amesema anatamani kuona wananchi wote wa vijijini wanafikiwa na umeme kama ilivyodhamiriwa na Serikali ili waweze kuboresha maisha yao na kwamba hana shaka kuhusu kutimia kwa jambo hilo ikiwa wote wanaohusika watashirikiana.

Awali, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika Mkoa wa Mtwara, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Jones Olotu alisema hadi sasa, vijiji 384 kati ya 785 vimekwishafikishiwa huduma ya umeme na kwamba kazi inaendelea ili kukamilisha vijiji vyote.

Mhandisi Olotu ambaye ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, amesema Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (R3-R2) ambao ni mojawapo ya miradi inayoendelea kutekelezwa mkoani humo unalenga kufikisha umeme katika vijiji vyote 401 na kwamba Wakandarasi wanaendelea na kazi hiyo.

Aidha, ametaja miradi mingine inayoendelea kutekelezwa mkoani humo kuwa ni pamoja nan a Mradi wa Vijiji Miji, Mradi wa kupeleka umeme kwenye migodi midogo ya madini, maeneo ya kilimo, vituo vya afya na pampu za maji pamoja na Mradi wa Ujazilizi.

“Hadi kufikia Novemba 15 mwaka huu, REA imewasha umeme katika vijiji 193 kati ya 401 ambavyo vilikuwa havina umeme kwa Mkoa wa Mtwara wakati Mradi wa R3-R2 unaanza kutekelezwa Julai, 2021.”

Mhandisi Olotu ameongeza kuwa, vijiji 208 vilivyobakia vitafikishiwa umeme kabla ya Juni 2024.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger