Friday, 3 November 2023

JK, HICHILEMA WAENDELEA KUSULUHISHA MGOGORO LESOTHO


Na Mwandishi Maalumu. 

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameungana na Rais Haikande Hichilema wa Zambia kukutana na Viongozi mbalimbali wa Ufalme wa Lesotho kama sehemu ya mchakato wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa na kiusalama uliopo katika Ufalme wa Lesotho. 

Viongozi hao wawili wapo nchini Lesotho kutekeleza maagizo ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ya kuusaidia Ufalme huo kukamilisha mchakato wa kutafuta amani ya kudumu katika Ufalme huo ambao haujawahi kupata amani ya kudumu tangu ulipopata uhuru hadi sasa. 

Rais Hichilema ameongoza ujumbe huo kama Mwenyekiti wa sasa wa Ogani ya Utatu ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika).  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameambatana naye kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la SADC (POE) ambapo ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuongoza timu ya usuluhishi wa mgogoro huo wa Lesotho. 

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamepata fursa ya kuonana na Mfalme Letsie III wa Lesotho, Waziri Mkuu wa Nchi hiyo Mhe. Samuel Makane pamoja na Viongozi wa Vyama vya Upinzani nchini humo. 

Katika Mkutano wao na Waziri Mkuu Sam Matekane Viongozi hao walipokea taarifa ya Serikali ya Ufalme huo katika kutekeleza mchakato wa kupitisha Bungeni muswada wa mabadiliko ya kudumu unaoaminika na wengi kuwa ndiyo muarobaini wa kudumu wa changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo. 

Waziri Mkuu huyo alielezea nia ya dhati ya Serikali yake kusimamia na kuhakikisha kuwa muswada huo unapitishwa kama inavyotarajiwa na wengi. 

Aidha, katika kikao na Viongozi wa Umoja wa Upinzani Viongozi hao walipata fursa ya kusikiliza masuala ambayo upande wa Upinzani wanaamini ni vyema yakafanyiwa kazi ili mchakato huo uweze kukamilika kwa kuzingatia maoni ya wadau wote.

Kwa upande wao, Rais Hichilema na Rais Mstaafu Kikwete walitumia fursa ya kukutana na Viongozi hao kusisitiza umuhimu wa pande zote zinazohusika katika kutafuta suluhu ya kudumu nchini humo kutanguliza maslahi mapana ya Ufalme wa Lesotho ili kukamilisha mchakato huo uliofikia katika hatua nzuri ya majadiliano. 

Aidha, walisisitiza haja ya pande zote husika kuwa na mtizamo wa kufanya maridhiano ya kisiasa hususan katika masuala magumu wanayoshindwa kufikia muafaka ili kuepusha kuurefusha mchakato huo bila sababu za msingi.

Share:

Thursday, 2 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 3,2023

Share:

TIMU YA RIADHA YA BARRICK NORTH MARA YAITANGAZA TANZANIA MASHINDANO YA CAPE TOWN MARATHON

Kapteni ya timu ya Barrick North Mara Runners Club, Sarah Cyprian, akifurahi baada ya kumaliza mbio za kilometa 42.2 za CapeTown Marathon zilizomalizika nchini Afrika ya Kusini Karibuni.
Kapteni ya timu ya Barrick North Mara Runners Club, Sarah Cyprian, akifurahi baada ya kumaliza mbio za kilometa 42.2 za CapeTown Marathon zilizomalizika nchini Afrika ya Kusini Karibuni.
Kapteni ya timu ya Barrick North Mara Runners Club, Sarah Cyprian, akifurahi baada ya kumaliza mbio za kilometa 42.2 za CapeTown Marathon zilizomalizika nchini Afrika ya Kusini Karibuni.
Wachezaji wa timu ya Barrick North Mara Runners Club, wakifurahia baada ya kumaliza mbio ndefu za kilometa 42.2 katika mashindano ya Cape Town Marathon yaliyomalizika hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini
Wachezaji wa timu ya Barrick North Mara Runners Club, wakifurahia baada ya kumaliza mbio ndefu za kilometa 42.2 katika mashindano ya Cape Town Marathon yaliyomalizika hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini
Timu ya riadha ya Barrick North Mara Runners Club, inayoundwa na wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara, baada ya kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani sasa imezidi kuchanja mbuga na kushiriki mashindano ya Kilometa 42.2 ya Sunlam Cape Town Marathon yaliyomalizika nchini Afrika ya kusini karibuni ambapo pia imepata fursa ya kuitangaza Tanzania katika mashindano hayo.

Kapteni ya timu hiyo, Sarah Cyprian,ameeleza kuwa wachezaji wote wa timu hiyo wako vizuri na wameweza kushiriki mbio hizo za umbali mrefu na kumaliza,na kudai kuwa wamefurahi kushiriki katika mashindano hayo makubwa ya riadha ya kimataifa na kuitangaza Tanzania.

Alisema katika mashindano hayo ambayo yamewakutanisha wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali wamejifunza mambo mengi na anaamini wameanza kupata uzoefu utakaowawezesha kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa watakayoshiriki siku za mbele.

Sarah alieleza kuwa timu ya riadha ya Barrick North Mara Runners Club, ilianzishwa mwaka 2016 na inajumuisha wakimbiaji 66,miongoni mwao Wanaume wapo 53 na Wanawake 13.

Alisema baadhi ya mashindano ambayo klabu hiyo imeshiriki ameyataja kuwa ni Kilimanjaro International Marathon -Moshi, Capital City Marathon -Dodoma(ilitoa mshindi wa tisa wa umbali wa kilometa 21 ) , Serengeti Migration marathon 21km-Mugumu, Serengeti Safari Marathon 21km-Lamadi na Lake Victoria Marathon -Mwanza (ilitoa mshindi wa 4 kwa wanawake umbali wa kilometa 21).

Mashindano makubwa ambayo timu hiyo imeshiriki na kung’ara ameyataja kuwa ni Kilimanjaro International Marathon ambapo ilishiriki mbio za kilometa 21 na kilometa 42.Kwa mbio hizo za masafa marefu ya kilometa 42 klabu iliwakilishwa na yeye mwenyewe. (Sarah Cyprian).


Akielezea siri ya mafanikio ya klabu Sarah alisema “Kampuni ya Barrick inayo sera mathubuti katika kusaidia wafanyakazi kwenye upande wa michezo. Kwanza kwa kuwa na miundo mbinu ya mazoezi kama gym, swimming pool, uwanja wa mpira wa miguu , uwanja wa mpira wa kikapu pamoja na uwanja wa mpira wa pete. Pia inatoa vifaa na nyenzo mbalimbali za kufanyia mazoezi, vilevile kugharamia huduma zote tunapoenda kwenye mashindano nje”.


Aliongeza kusema kuwa Kampuni pia kupitia kitengo cha Afya na Usalama huwa inaandaa mashindano ya ndani kwa kushindanisha idara mbali mbali hii ni kama njia moja wapo yakuweza kuweka vizuri afya za mwili na akili za wafanyakazi wawapo kazini.


Kuhusu ni jinsi gani wanaweza kutenga muda wa kazi na muda wa kufanya mazoezi Sarah alisema “ Kila mtu ana masaaa 24 katika siku.Klabu ya North Mara Runners huwa tunatenga muda wa saa moja katika siku kufanya mazoezi.Mazoezi hayo huwa tunafanya jioni mara baada ya kutoka kazini,na mara chache ratiba zinapokuwa zinabana jioni huwa tunafanya mazoezi saa kumi alfajiri kabla ya kwenda kazini”.


Kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo katika mazoezi na kushiriki mashindano alisema kulingana na majukumu ya kazi huwa kuna wakati ni vigumu wote kwenda kushiriki mashindano, lakini huwa wanajitahidi kutoa wawakilishi kwa ajili ya kushiriki mashindano, na kampuni huwa inawaunga mkono wakati wote.


Akitoa maoni kuhusu maendeleo ya tasnia ya mchezo wa mbio za marathon nchini alisema katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwitiko mkubwa katika mchezo wa mbio na kushauri kuwa ni vizuri kuanza maandalizi mapema kwa vijana wadogo ili kuweza kuwa na washiriki wengi katika mbio za kimataifa.Aliongeza kusema kuwa kuna wakimbiaji wengi wenye vipaji nchini kwa sasa ambao wanashiriki mashindano ya marathon mbalimbali yanayoandaliwa nchini.


Sarah, alitoa wito kwa jamii kujitahidi kutenga muda hata nusu saa kwa siku kufanya mazoezi. “Mazoezi yanasaidia kuimarisha afya ya akili na mwili. Pia mazoezi yanasaidia kuweza kujikinga na magonjwa yasioambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na unene wa kupindukia”alisema.


Kuhusu malengo ya baadaye ya klabu hiyo alisema “Kauli mbiu ya club yetu ni ‘We run for fun and healthy’ hivyo basi bado tunajukumu la kuhimiza wafanyakazi wengi zaidi kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zetu, kwani mazoezi pia yamekuwa yakituweka vizuri kiakili hata kuweza kutimiza majukumu yetu kazini kwa ufanisi zaidi.Lakini pia kuweza kushiriki zaidi katika marathoni za kimataifa.”


Share:

TAMASHA LA WANAWAKE NA UTALII KUFANYIKA NOVEMBA 17 JIJINI ARUSHA ,WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJUA FURSA ZA UTALII ZINAZOPATIKANA KWENYE HIFADHI


Mwenyekiti wa Tamasha lijulikanalo Kwa jina la wanawake na Utalii festival Nangasu Werema akiwaonyesha waandishi wa habari tuzo ambayo Rais Samia Suluhu ameishinda baada ya filamu yake ya The Royal Tour kuonyeshwa nchini India ambapo mara baada ya kushinda mwenyekiti huyo alikabidhiwa kwa ajili ya kumletea Rais Samia Suluhu Hassan
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sanaa Sana Design LTD kampuni ambayo inayohusisha wanawake wenye ulemavu Iren Filex akiongea na waandishi wa habari juu ya vitu watakavyovionyesha katika Tamasha hilo la wanawake na Utalii festival
L
Mwenyekiti wa Tamasha lijulikanalo Kwa jina la wanawake na Utalii festival Nangasu Werema akiongea na waandishi wa habari juu ya Tamasha la wanawake linalotarajiwa kufanyika Novemba 17,2023 katika kituo cha mikutano cha AICC Tamasha lijulikanalo kama wanawake na Utalii festival uku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa waziri wa maliasili na Utalii
Na Woinde Shizza,Arusha


Waziri wa Mali asili na utalii Anjela Kairuki anatarajiwa kufungua tamasha la Wanawake festival litakalofanyika Novemba 17 jijini Arusha ambalo litalenga kuwezesha kufikia idadi ya watalii milioni Tano ifikapo mwaka 2025


Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha mwenyekiti wa tamasha hilo Nengasu Werema amesema kuwa wameamua kuunga serikali mkono katika jitiada za kutangaza utalii.


Alisema kuwa wao kama wanawake watafanya tamasha hilo ambalo litashirikisha wanawake na wadau wa utalii kwa pamoja ili Wanawake waweze kushiriki kwenye sekta ya utalii.


"Tunataka kutangaza na kukuza sekta ya utalii kwani mada kubwa ya festival hii ni kuangalia namna ambavyo Wanawake wanaweza kujihusisha katika sekta ya utalii ambayo itawezesha kukua kwa uchumi wa Tanzania na wa mtu mmoja mmoja",aliongeza.


Aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na tuzo mbali mbali ambazo zitatolewa kwa Wanawake vinara wa utalii lakini pia wataweza kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo ya hifadhi ya taifa ngorongoro na na hifadhi ya Tarangire.


Kwa upande wake afisa uhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa Tarangire Jully Bede aliwapongeza Wanawake hao kwa kuandaa tamasha hilo na kuahidi kuwapa ushirikiano ikiwemo kuwaeleza Wanawake fursa zilizopo kwenye hifadhi.


Naye Mkurugenzi wa Wanawake na utalii Mercy Michael alisema kuwa lengo la wao kuandaa tamasha hilo ambalo litashirikisha wanawake walioko kwenye sekta ya utalii ni kuhamasisha Wanawake kuunga mkono sekta ya utalii kuwekeza katika sekta hiyo na hatimaye kuweza kuongeza pato la taifa.
Share:

PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI (AFDP) YASAIDIA WAKULIMA KUKABILIANA NA ATHARI ZITOKANAZO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.





Mtaalamu wa Masuala ya Ufuatilia na Tathmini Bw. Bernard Ulaya kutoka katika Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akizungumza wakati Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo (IFAD) Ulipotembea Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Nchini Mkoani Arusha (TOSCI).
Mtaalamu wa masuala ya Lishe na Jinsia kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bi. Florence Munyiri akizungumza mbele ya wataalamu hawapo katika picha, mara Ujumbe huo kutoka IFAD ulipotembelea Taasisi ya Tafiti za Mbegu za Kilimo (TARI) Seriani Arusha.

Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD),na wataalamu wakiwa katika kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Missaile Albano Musa, kabla ya Ujumbe huo kuanza ziara ya kutembelea baadhi ya Taasisi za Kilimo zinazotekeleza Programu ya kuelendela Kilimo na Uvuvi (AFDP) Mkoani humo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Missaile Albano Musa,na Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD),na wataalamu kabla ya Ujumbe huo kuanza ziara ya kutembelea baadhi ya Taasisi za Kilimo zinazotekeleza Programu ya kuelendela Kilimo na Uvuvi (AFDP) Mkoani humo.



NA; MWANDISHI WETU – ARUSHA


Imeelezwa kuwa, Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) imesaidia wakulima katika kufahamu na kutumia njia bora za kilimo cha kisasa zitakazowapelekea kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi.

Akizungumza wakati Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo (IFAD)ulipotembelea kituoni hapo Novemba 1 mwaka huu , Mtafiti kutoka Taasisi ya Tafiti za Mbegu Nchini (TARI) tawi la Seriani Arusha Bw. Shida Nestory amesema, Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi zake za Tafiti za Kilimo, (TARI) Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI) na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar, umesaidia wakulima katika kufahamu na kutumia njia bora za kilimo cha kisasa.

TARI Seriani Mkoani Arusha inatekeleza kupitia zao la maharage na Mahindi ambapo kwa mazao yote mawili mradi umewasiaidia kuwafikia wakulima ambapo mabwana shamba wanapewa mafunzo ya namna ambavyo wakulima wawaweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kupitia teknolojia mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya aina za mbegu mbazo zinaweza kustahimili kwenye maeneo ya ukame.

“Tari inawaelimisha wakulima juu ya matumizi ya teknolojia ya kuvuna maji na kuwa na uhakika wa kulima katika misimu tofauti na matumizi ya mbegu bora ambazo zinaweza kukinzana na magonjwa.” Alisisitiza

Kwa Upande wake Mtaalamu wa masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka katika Programu hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Bw. Bernard Ulaya alisema, Lengo la Timu hii ya IFAD kufanya ziara katika taasisi hizo ni kuangalia maendeleo ya program, mafanikio, changamoto zilizopo ili kama kuna maeneo yanayoweza kuboreshwa yaboreshwe.


“katika kituo cha Seriani program imeweza kuwasaidia kuwa na kitalu Nyumba mbacho kitaweza kuwasiaidia katika tafiti zao za kuweza kuzalisha mbegu mama na mbegu kwa matumizi ya wakulima.” Alifafanua


Wageni hao kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) pamoja na wataalam watatembelea maeneo hayo ya Kilimo katika Mikoa ya Arusha, Manyara Tabora, Morogoro na Dodoma kwa Upande waTanzania Bara Pamoja na Sekta ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu katika baadhi ya mikoa ya Unguja na Pemba.
Share:

Wednesday, 1 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 2,2023

Share:

TANZANIA YAPATA HESHIMA YA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 24 WA KAMISHENI YA AFRIKA YA MISITU NA WANYAMAPORI



Na Mwandishi Wetu, Arusha

Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa masuala ya wanyamapori, kilimo na misitu.

Akiongea na waandishi wa habari leo mara baada ya kufungua mkutano wa 24 wa Kamisheni ya Afrika ya Misitu na Wanyamapori (AFWC24) na wiki ya Nane (08) ya Misitu na Wanyamapori Afrika (AFWW8) jijini Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii mh. Angellah Kairuki amesema hiyo ni heshima kubwa kwani kati ya nchi 53 ambazo ndio wanachama wa kamisheni hiyo, nchi 40 zimetuma wawakilishi wake .


“Hadi sasa tuna washiriki takriban 300 , lakini wapo pia wengine ambao watashiriki kupitia njia ya mtandao. Tunaamini watanufaika lakini hasa sisi Watanzania. Wataalam kutoka serikalini wanao simamia masula haya, tutakuwa pia na majadiliano mahususi kuhusiana na biashara nzima ya hewa ukaa” ,amesema Mhe. Kairuki.


Ameongeza kuwa Wadau wa mkutano huo watajadili soko lililopo pamoja na fursa zinazopatikana ambapo ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa kuendelea kufanya majadiliano na wawekezaji wa biashara ya hewa ya ukaa.


Wakati huo huo, Mhe. Kairuki amesema Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Wanyamapori Tanzania (2007), inayotaka uhifadhi wa wanyamapori na makazi yao pamoja na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori nchini.


“Utekelezaji wa sera hiyo umewezesha mtandao wa maeneo ya hifadhi Tanzania kukua na kufikia Hifadhi za Taifa 21, Eneo 1 la Hifadhi, Mapori ya Akiba 29, Mapori Tengefu 25, Maeneo 22 ya Hifadhi za Wanyamapori” ,amesema.


Katika hatua nyingine , Kairuki amesema Tanzania ilishinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa Kongamano la 50 la Apimondia litakalofanyika Jijini Arusha mwaka 2027,hivyo amewakaribisha wadau hao kuhudhuria mkutano huo.


"Kongamano la Apimondia linatarajiwa kuleta washiriki wapatao 6,000. Ningependa kuchukua fursa hii kuwakaribisha katika Kongamano hili muhimu la Apimondia. Wageni hao mara baada ya mkutano huo watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyopo jijini Arusha na vile vilivyopo nje ya jiji la Arusha”,  amesisitiza.


Naye Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa mkutano wa 24 wa Kamisheni ya Afrika ya Misitu na Wanyamapori (AFWC24) na wiki ya Nane (08) ya Misitu na Wanyamapori Afrika (AFWW8), Prof. Dos Santos Silayo amesema, lengo la Mkutano huo ni kubadilishana uzoefu wa pamoja ili waweze kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya misitu na nyuki.


“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu hassan kwa kuridhia mkutano kufanyika Jijini Arusha. Mkutano una matokeo chanya katika sekta ya utalii, misitu Pamoja na sekta ya wanyamapori hapa nchini hapa nchini”, amesema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger