Monday, 18 September 2023

BENKI YA NMB YAENDESHA WARSHA YA SIKU YA WALIMU KAHAMA… ‘NMB KIMBILIO SALAMA KUEPUKA MIKOPO KAUSHA DAMU’



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Benki ya NMB imeendesha Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kutambua mahusiano mazuri yaliyopo kati ya walimu na Benki ya NMB, kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya Benki hiyo pamoja na kuwapa fursa ya kutoa maoni na mapendezo ya namna gani wanaweza kunufaika zaidi na huduma za Benki ya NMB.


Warsha hiyo imefanyika leo Jumatatu Septemba 18,2023 Mjini Kahama ikiongozwa na kauli mbiu ‘Mwalimu Spesho – Umetufunza Tunakutunza’ ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.


Kupitia warsha hiyo walimu wamejifunza masuala ya Kibenki ikiwemo mikopo,bima,amana na huduma mbalimbali za NMB zitakazowasaidia kupanua uwezo wao kiuchumi na kujenga utamaduni wa kuweka akiba ili kukidhi mahitaji ya dharura pindi yanapojitokeza.


Akizungumza wakati wa Warsha hiyo, Julius Chagama ameipongeza Benki ya NMB kwa kuandaa Warsha ya Siku ya Walimu akisema jitihada hizo za Benki ya NMB ni nzuri na zinaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Watanzania walio wengi wanajumuishwa katika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua vipato vyao na uchumi kwa ujumla.

“Nawapongeza sana NMB kwa bidhaa za akiba na mikopo inayolenga mahitaji ya kila makundi ya wateja kama walimu na jamii kwa ujumla. Tunawapongeza kwa kujali mahitaji ya wafanyakazi kwani mikopo hii imekuwa msaada sana katika kukidhi mahitaji mbalimbali katika ngazi ya familia n ahata kufanikisha maandalizi yao kwa Maisha ya baadae pale wanapostaafu”,amesema.
Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Katika hatua nyingine, Chagama amewahamasisha walimu na watumishi wengine wa serikali watumie taasisi rasmi zinazotoa mikopo rasmi ikiwemo Benki ya NMB ili kuepukana na mikopo umiza ‘Kausha Damu’ inayotolewa kwenye makampuni binafsi ambayo imekuwa ikiwaathiri zaidi walimu.

“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imekuwa ikipokea kesi nyingi za migogoro kati ya walimu na wakopeshaji wa makampuni binafsi. Walimu wamekuwa waathirika wakubwa wa mikopo umiza ‘kausha damu’, unakuta mwalimu kakopa, anamaliza deni lakini bado anaendelea kukatwa pesa zake. Benki hii ya NMB inaenda kutuweka katika mikono salama ya mikopo salama. Watumishi tumieni Benki ya NMB kupata mikopo rasmi”,ameongeza Chagama.
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Kahama

“Natoa rai kwa Benki ya NMB kuzidi kuboresha huduma kwa wateja hasa walimu ili idadi yao iweze kuongezeka jambo ambalo litawapa fursa nyingi zikiwemo kukopa ili wawe na amani wanapokuwa kazini na kuongeza tija kwenye maeneo yao ya kazi. Pia endeleni kubuni bidhaa, huduma na program nyingi si kwa ajili ya walimu tu, hata kwa watumishi na wafanyakazi wa kawaida waweze kumudu”,ameongeza Chagama.


Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Seka Urio amewashukuru Walimu kwa kuendelea kuwa wateja wazuri huku akiwahamasisha kupata mikopoyenye masharti nafuu kupitia benki ya NMB.

“Leo tumekutana na walimu zaidi ya 250 kutoka Halmashauri ya Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama katika Warsha ya Siku ya Walimu ili kuwaonesha kwa kina na upana fursa zinazotolewa katika Benki ya NMB. Tulizindua mpango huu mwaka 2022 ili kuwaonesha walimu namna ya kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuepukana na mikopo umiza na kuhakikisha Benki ya NMB inaendelea kuwa suluhisho kwa watanzania”,amesema Urio.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Seka Urio.

“Benki ya NMB inatoa mikopo yenye masharti nafuu. Walimu ni miongoni mwa wateja wetu wengi,na ni kundi ambalo limekuwa kundi lengwa kwa mikopo umiza na wamekuwa waathirika wakubwa wa mikopo ya kausha damu, kausha maji kutokana na kwamba wamekuwa wakikopo kwenye makampuni binafsi na kutozwa riba kubwa na masharti magumu hali inayosababisha kuwa na msongo wa mawazo ‘Stress’ kuhusu mikopo hiyo”,ameongeza Urio.

Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya NMB kutoka Makao Makuu, Isaac Mgwassa amesema Benki ya NMB ni benki ya Kwanza miongoni mwa taasisi nyingi za fedha nchini kufikiria kuandaa siku maalumu kwa ajili ya walimu lengo likiwa ni kuwafikia walimu zaidi ya 9000 nchini hivyo itaendelea kuwatunza walimu kwa masuluhisho mbalimbali ya kifedha.


Kwa upande wao, walimu waliopata mafunzo hayo akiwemo Tegemeo Severiani, Levina Kassim na Regina Mbozu wameishukuru Benki ya NMB kwa kuandaa warsha hiyo ambayo imekuwa fursa nzuri kujua namna gani wanaweza kupata huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa unafuu, uharaka na ufanisi lakini pia kuepukana na mikopo umiza ambayo imekuwa ikisababisha walimu wapunguze ufanisi wa kazi zao.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB leo Jumatatu Septemba 18,2023 . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Seka Urio akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Seka Urio akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya NMB kutoka Makao Makuu, Isaac Mgwassa akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya NMB kutoka Makao Makuu, Isaac Mgwassa akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Kaimu Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Sadick Juma Kigaile akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Afisa Elimu Halmashauri ya Msalala, Hajra Mmkoki akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Godfrey Mkumbo akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Godfrey Mkumbo akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Godfrey Mkumbo akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Godfrey Mkumbo akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Godfrey Mkumbo akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Godfrey Mkumbo akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Huduma za Kibenki zikitolewa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Huduma za Kibenki zikitolewa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Mwalimu akijaza fomu kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Huduma za Kibenki zikitolewa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Picha ya kumbukumbu meza kuu 
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu

Picha ya kumbukumbu meza kuu na walimu
Picha ya kumbukumbu meza kuu na wafanyakazi wa Benki ya NMB

Picha ya kumbukumbu meza kuu na wafanyakazi wa Benki ya NMB
Picha ya kumbukumbu meza kuu na wafanyakazi wa Benki ya NMB

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

DAWASA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UONDOSHAJI MAJITAKA PSSSF


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo Mhe.Kitila Mkumbo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Uondoshaji Majitaka wa PSSSF, Sinza - Kijitonyama unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA).

Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe.Mkumbo ameipongeza DAWASA kwa kutekeleza mradi huo kwa ufanisi na amewataka kuongeza nguvu kwa kuweka bajeti ya kutekeleza miradi ili kuondoa adha ya uchafuzi wa Mazingira.

Amesema ni wakati muafaka wa DAWASA kuweka mkakati madhubuti wa kutekeleza miradi ya Majitaka ili kuondokana na uchafuzi wa Mazingira kwenye maeneo korofi ikiwemo Sinza.

"Changamoto iliyopo sasa kwenye maeneo ya Sinza ni uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na utiririshaji hovyo wa majitaka kwenye maeneo ya makazi ya watu". Amesema

Nae Mwakilishi wa Kaimu Afisa Matendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Modesta Mushi ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi unalenga kunufaisha kaya zaidi ya 200 za mitaa ya Sinza pamoja na hospitali ya Sinza Palestina.

"Tumejipanga kikamilifu kukamilisha mradi huu mwezi wa kumi, kwa kuwa inatekelezwa usiku na mchana, niwasihi wananchi kuacha kutupa taka ngumu kwenye miundombinu hii kwa kuwa inasababisha kuziba na kuchelewesha ukamilishwaji wa mradi," amesema Mhandisi Modesta.

Ameishukuru PSSSF kwa kutoa ushirikiano wa utekelezaji wa mradi huu unaoleta manufaa ya afya kwa pande zote.

Kwa upande wake Meneja wa Miradi PSSSF Mhandisi Marko Kapinga amesema kuwa mradi huo una manufaa makubwa kuanzia kwa wapangaji wa jengo la PSSSF pamoja na wakazi wanaozunguka jengo hilo na utapunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa ya mlipuko.



Share:

WAZIRI GWAJIMA AMWAKILSHI RAIS SAMIA MAREKANI KWENYE JUKWAA LA KIZAZI CHENYE USAWA




Na WMJJWM- New York, Marekani

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amemwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa kipindi cha Kati cha Jukwaa la Kizazi chenye usawa (Mid Point) uliofanyika Septemba 17, 2023 jijini New York nchini Marekani.

Katika mkutano huo, Tanzania imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ahadi za nchi katika kuelekea Usawa wa Kijinsia ambapo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliahidi kuwa kinara katika eneo la HAKI na USAWA wa KIUCHUMI.

Hadi sasa jitihada zilizofanywa na Tanzania katika kutekeleza ahadi hizo ni pamoja na kuundwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inayoweka kipaumbele eneo la usawa wa kijinsia na kuteuliwa kwa Kamati ya Taifa ya Ushauri yenye wajumbe 25 wa sekta mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar inayoongozwa na Mhe. Angella Kairuki, Waziri wa Maliasili na Utalii.

Jitihada nyingine ni kuundwa kwa Programu ya Kizazi chenye Usawa Tanzania (Tanzania Generation Equality Programme - TGEP) inayotekelezwa na Wizara za kisekta kwa miaka mitano (5) Julai 2021/22 hadi Juni 2025/26 yenye mkakati wa kuleta mabadiliko ya ubora wa maisha ya wanawake na wasichana kwa kuimarisha Haki na Usawa wa Kiuchumi pasipo kuwaacha nyuma wanaume na wavulana kwa kuwajengea uelewa ili waweze kushiriki kwenye maendeleo ya Taifa.

Aidha, uteuzi wa maafisa viungo ngazi zote wanaosimamia utekelezaji wa haki na usawa wa kiuchumi kwenye maeneo yao na kuitambua Siku ya Wanawake Duniani sambamba na kushirikiana na Wadau kushughulikia changamoto za wanawake kama ilivyobainishwa katika Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na Mpango wa Mkakati wake wa mwaka 2005, Maazimio ya Ulingo wa Beijing, Ajenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda ya Maendeleo ya Bara la Afrika 2063.

Waziri Dkt. Gwajima katika mkutano huo ameambatana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Riziki Pembe, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Mgeni Hassan Juma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya utekelezaji wa Ahadi za nchi kwenye Jukwaa la Kizazi chenye Usawa Mhe. Angellah Kairuki.

Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekalaghe, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar Abeda Rashid Abdullah na wataalamu mbalimbali.

Wakati huo huo ujumbe wa Tanzania umekutana na Mkurugenzi wa UN Women Dkt. Sima Bahous, ambaye ameipongeza Tanzania katika utekelezaji wa GEF na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo.
Share:

Sunday, 17 September 2023

GST YATAKIWA KUWA KINARA WA TAARIFA ZA MADINI NA HUDUMA BORA ZA MAABARA



Kupitia utekelezaji wa muelekeo mpya ujulikanao kama Vision 2030, Serikali yaweka mkakati wa kuifanya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) kuwa kinara wa upatikanaji na utoaji wa taarifa za madini na pia huduma bora za maabara.

Hayo yamesemwa leo tarehe 17 Septemba, 2023 Mkoani Morogoro na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde alipokuwa akifunga kikao kazi cha Menejimenti ya GST ambacho kilikuwa mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan wakati akizungumza na wakuu wa Taasisi za umma Jijini Arusha na kupitia muelekeo mpya wa Wizara wa VISION 2030: Madini ni Maisha na Utajiri


"Nchi yetu imegawanywa katika QDS 322, ambapo QDS moja ina eneo la kilometa za mraba 2916. Ni asilimia 16 pekee ya eneo lote nchini ndilo limefanyiwa utafiti wa jiofizikia kwa teknolojia ya kisasa ya kurusha ndege yaani High Resolution Airborne Geophysical Survey.

Sote tunaona kwamba iwapo tukiweza kufanya utafiti wa eneo hata kwa asilimia 50 tu, namna ambavyo sekta ya madini inakwenda kulinufaisha Taifa letu kwa kuchangia zaidi kwenye ukuaji wa uchumi.

Mh. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan , ameonesha dhamira ya dhati ya kuikuza sekta ya madini ili iongeze mchango zaidi kwenye Pato la Taifa la Nchi yetu.

Taasisi hii inategemewa kwa taarifa za awali za muelekeo wa miamba, hivyo tunakwenda kuifanya kuwa kinara wa taarifa na takwimu za madini nchini,sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wake ili kukidhi mahitaji ya dunia ya leo na pia kuimarisha maabara yake kwa vifaa vya kisasa”Alisema Mavunde.

Awali, akitoa maelezo ya utangulizi, Afisa Mtendaji Mkuu wa GST, Dkt. Mussa Budeba alieleza kuwa kikao kazi hicho ni matokeo ya Mkutano wa Mhe. Rais alipokutana na Wenyeviti na Watendaji wa Taasisi za Serikali ambapo alielekeza Taasisi zijiwekee mikakati ya kujiendesha kwa tija na faida na kupunguza utegemezi kutoka Serikalini.

Vilevile, mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye ni Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga alibainisha kwamba pamoja na masuala mengine kikao kazi hicho kililenga pia kuongeza ari ya kazi, ushirikiano baina ya watumishi kwa kufanya kazi kwenye Timu ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mh. Rebecca Nsemwa alishukuru kwa GST kuchagua kufanyia kikao Morogoro na kuiomba GST kuuweka Mkoa wa Morogoro kwenye mkakati wao kwani wanao utajiri mkubwa wa madini.


Share:

NAIBU WAZIRI BYABATO AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA BIASHARA WA JAMAICA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wakili Stephen Byabato(Mb) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina John Smith pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China unaofanyika jijini Havana nchini Cuba.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea kuridhishwa kwao na hali ya uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Jamaica na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi ili kuimarisha uhusiano huo.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Byabato amemuelezea Mhe. Smith kuwa Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri uliopo na kuongeza kuwa kuna haja ya kuhakikisha uhusiano huo wa kidplomasia unaimarishwa na kufikia hatua ya juu.

Amemhakikishia utayari wa Serikali ya Tanzania kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Jamaica katika maeneo yatakayozinufaisha pande zote mbili.

Pia amemuelezea nia ya Tanzania ya kupanua wigo wa maeneo ya ushirikiano na kuingiza sekta za uchumi wa bluu, biashara na uwekezaji.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina John Smith alisema pamoja na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania, Jamaika inaiomba Tanzania kuiunga mkono katika nafasi mbili inazogombea kimataifa katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Bahari (IMO) na Kamati ya Urithi wa Dunia iliyoko chini ya UNESCO.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger