Sunday, 17 September 2023

GST YATAKIWA KUWA KINARA WA TAARIFA ZA MADINI NA HUDUMA BORA ZA MAABARA



Kupitia utekelezaji wa muelekeo mpya ujulikanao kama Vision 2030, Serikali yaweka mkakati wa kuifanya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) kuwa kinara wa upatikanaji na utoaji wa taarifa za madini na pia huduma bora za maabara.

Hayo yamesemwa leo tarehe 17 Septemba, 2023 Mkoani Morogoro na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde alipokuwa akifunga kikao kazi cha Menejimenti ya GST ambacho kilikuwa mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan wakati akizungumza na wakuu wa Taasisi za umma Jijini Arusha na kupitia muelekeo mpya wa Wizara wa VISION 2030: Madini ni Maisha na Utajiri


"Nchi yetu imegawanywa katika QDS 322, ambapo QDS moja ina eneo la kilometa za mraba 2916. Ni asilimia 16 pekee ya eneo lote nchini ndilo limefanyiwa utafiti wa jiofizikia kwa teknolojia ya kisasa ya kurusha ndege yaani High Resolution Airborne Geophysical Survey.

Sote tunaona kwamba iwapo tukiweza kufanya utafiti wa eneo hata kwa asilimia 50 tu, namna ambavyo sekta ya madini inakwenda kulinufaisha Taifa letu kwa kuchangia zaidi kwenye ukuaji wa uchumi.

Mh. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan , ameonesha dhamira ya dhati ya kuikuza sekta ya madini ili iongeze mchango zaidi kwenye Pato la Taifa la Nchi yetu.

Taasisi hii inategemewa kwa taarifa za awali za muelekeo wa miamba, hivyo tunakwenda kuifanya kuwa kinara wa taarifa na takwimu za madini nchini,sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wake ili kukidhi mahitaji ya dunia ya leo na pia kuimarisha maabara yake kwa vifaa vya kisasa”Alisema Mavunde.

Awali, akitoa maelezo ya utangulizi, Afisa Mtendaji Mkuu wa GST, Dkt. Mussa Budeba alieleza kuwa kikao kazi hicho ni matokeo ya Mkutano wa Mhe. Rais alipokutana na Wenyeviti na Watendaji wa Taasisi za Serikali ambapo alielekeza Taasisi zijiwekee mikakati ya kujiendesha kwa tija na faida na kupunguza utegemezi kutoka Serikalini.

Vilevile, mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye ni Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga alibainisha kwamba pamoja na masuala mengine kikao kazi hicho kililenga pia kuongeza ari ya kazi, ushirikiano baina ya watumishi kwa kufanya kazi kwenye Timu ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mh. Rebecca Nsemwa alishukuru kwa GST kuchagua kufanyia kikao Morogoro na kuiomba GST kuuweka Mkoa wa Morogoro kwenye mkakati wao kwani wanao utajiri mkubwa wa madini.


Share:

NAIBU WAZIRI BYABATO AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA BIASHARA WA JAMAICA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wakili Stephen Byabato(Mb) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina John Smith pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China unaofanyika jijini Havana nchini Cuba.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea kuridhishwa kwao na hali ya uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Jamaica na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi ili kuimarisha uhusiano huo.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Byabato amemuelezea Mhe. Smith kuwa Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri uliopo na kuongeza kuwa kuna haja ya kuhakikisha uhusiano huo wa kidplomasia unaimarishwa na kufikia hatua ya juu.

Amemhakikishia utayari wa Serikali ya Tanzania kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Jamaica katika maeneo yatakayozinufaisha pande zote mbili.

Pia amemuelezea nia ya Tanzania ya kupanua wigo wa maeneo ya ushirikiano na kuingiza sekta za uchumi wa bluu, biashara na uwekezaji.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina John Smith alisema pamoja na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania, Jamaika inaiomba Tanzania kuiunga mkono katika nafasi mbili inazogombea kimataifa katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Bahari (IMO) na Kamati ya Urithi wa Dunia iliyoko chini ya UNESCO.
Share:

DAWA HII IMENIPONYA UGONJWA WA KIFUA KIKUU!


Licha ya matangazo mengi katika vyombo vya habari kuwa Kifua Kikuu (TB) ni ugonjwa unaotibika kwa urahisi na watu wasione aibu kwenda Hospitalini, kwani hali hiyo kwangu ilikuwa ni tofauti kabisa.

Nadhubutu kusema hivyo kutokana baada ya kupata maradhi ya TB nilitumia dawa kwa kipindi kirefu bila mafanikio yoyote, zaidi nilipata nafuhu lakini baada ya muda hali ilirejea kuwa mbaya zaidi.

Kwa majina ni Dulla, nilikuwa nafanya kazi katika mgodi wa dhahabu kwa miaka zaidi ya 10, mazingira ya mgodi na matumizi ya vifaa  duni vya kufanyia kazi ni moja ya sababu za kuugua ugonjwa wa TB kwani hata marafiki zangu wengi walikumbwa na ugonjwa huo.

Kabla sijaanza kuumwa, mara kadhaa nilikuwa naona watalaamu wa afya wakija eneo letu la kazi na kutupatia semina pamoja na ushauri namna ambavyo tutaweza kuwa salama kiafaya.

Sikuwahi kifikiria siku moja nami nitaweza kuugua ugonjwa huo kwani katika familia yetu hakuna mtu mwenye histoaria hiyo, na pengine kwa vile nilikuwa mzima na kusikia nguvu ya ajabu katika mwili wangu sikuwa na shaka kabisa.

Nilianza kuwa na wasiwasi pale ambapo kila mara nilikuwa nakohoa kikozi kisichoisha, niliona ni hali ya kawaida lakini kadiri siku zilivyozidi kusonga ndivyo ambavyo mambo kwangu yalizidi kuwa magumu.

Hatimaye niliamua kwenda Hospitali kupima kujua ni kipi hasa nimenisibu, na ndipo nilionekana kuwa ni ugonjwa wa TB, nilianza dozi mara moja na kuachana na kazi ya mgodini kama ambavyo nilishauriwa na wataalumu.

Nilitumia dawa zile kwa miezi kadhaa hadi zikaisha lakini sikuweza kupona kabisa, hata nilipopatiwa aina nyingine ya dawa sikuweza kupona hali iliyonipa sana msongo wa mawazo.

Ghafla siku moja nikiwa nimeketi kibarazani lilinijia wazo kuwa nitafute dawa wa TB mtandaoni, katika kusoma huku na kule ndipo nikakutana na mtu anaitwa African Doctors kupitia tovuti yake ambayo ni www.african-doctors.com na kuweza kusoma huduma zake.

Bila kusita nilichukua namba yake ambao ni +254769404965 na kuanza kuwasiliana naye, nilimsimulia kuhusu tatizo langu na jinsi ambavyo limekuwa likinitesa. Alinitoa hofu kuwa dawa zake zimekuwa zikiwasaidia wengi ukanda wa Afrika Mashariki hivyo nitapona kabisa.

Nilifunga safari na kufika ofisini kwake, alinipokea vizuri sana na kunipatia tiba asilia ambayo naweza kusema ndio hasa imekuja kukomboa maisha yangu na hadi sasa ni mzima wa afya.

Kwa muda mfupi nilipoanza kutumia dawa za African Doctors hali yangu ya kiafya iliimarika sana kiasi kwamba nikasema ningebaini hilo mapema ningekuwa nishapona na kuendelea na shughuli zangu. Asante sana African Doctors.

Kumbuka African Doctors ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Pia anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha, kifafa, upungufu wa nguvu za kiume, kuvimba miguu, kaswende, vile vile anawezesha wanawake kubaba ujautizo, wanaume kutungisha mimba n.k.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

Tanzia : NUMPELE MULUNGU AFARIKI DUNIA




Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WATANZANIA 12000+ WALIOITWA USAILI WA KAZI TRA SEPTEMBA 2023

Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA MAPYA YA WATUMISHI WALIOAJIRIWA LEO KUTOKA UTUMISHI

Share:

Saturday, 16 September 2023

WAZIRI TAMISEMI: SERIKALI IMETOA KIBALI CHA AJIRA 43000 AFYA NA ELIMU ,DIPLOMA NA CHETI WAKUMBUKWA



Na ripota,Maswayetu blog 

Leo Mapema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya ziara katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ,Mtwara.

Rais Samia ameanza kusalimiana na wananchi wa halmashauri ya Mji Nanyamba,ambapo baada ya hapo alielekea Wilaya Ya Tandahimba na kufanya mkutano wa hadhara.

Baada ya mkutano wa Tandahimba alielekea wilaya ya Newaala,ambapo katika salamu za Mawaziri, Waziri wa Tamisemi Mh.Mchengerwa Ametanagza kuwa Rais ametoa kibali cha kuajiri watanzania wenye diploma,cheti na digrii zaidi ya 43000 ambapo atazitangaza siku sio nyingi.

Hivyo amewataka vijana wajiandae kuomba na kwenda kuwatumikia watanzania.

Mwisho.

Share:

IAA YADHAMIRIA KUFANYA MAKUBWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

 


Na Mwandishi wetu Arusha 

Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka leo tarehe 15 Septemba 2023 ametoa rasmi ripoti ya utendaji kazi ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kueleza mipango na mikakati ya mwaka mpya wa fedha 2023/2024.


Akizungumza na waandishi wa habari leo katika kampasi ya Arusha, Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa IAA imepata mafaniko makubwa kutokana na juhudi wanazozifanya ikiwemo; kuboresha mazingira ya kujifunzia (Miundombinu), kuongeza mitaala mipya ambayo mpaka sasa imefikia 71 kwa ngazi zote kwa mwaka wa masomo 2023/2024.



Aidha, ameongeza kuwa IAA imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 10,342 mwaka 2021/2022 mpaka 13,716 kwa mwaka 2022/2023, ongezeko hilo likienda sambamba na ongezeko la mapato ya ndani kutoka bilioni 15 mwaka 2021/2022 mpaka kufikia 2022/2023. 


Katika hatua nyingine Prof. Sedoyeka ameeleza kuwa IAA inaendelea kuweka jitihada katika kuhakikisha inakuwa na wataalam (wahadhiri) wa kutosha ili kuendana na ongezeko la wanafunzi; ambapo mpaka sasa jumla ya watumishi 52 wanasoma shahada ya uzamivu (PhD) katika Vyuo Vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi na watumishi Tisa (09) wanasoma  shahada ya uzamili (Masters)



Kuhusu ushirikiano na wadau Profesa Sedoyeka amesema IAA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ambapo kwa mwaka 2022/2023 imeanzisha rasmi ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kutoa mafunzo kwa kozi mbli za Shahada ambazo ni Bachelor Degree in Cyber Security, Bachelor Degree in Security and Strategic Studies na Kozi mbili za Shahada ya Uzamili ambazo ni Master of Information Security na Master of Arts in Peace and Security Studies.


Sanjari na hili ameongeza kuwa Chuo kitaendelea kuongeza mitaala kulingana na mahitaji ya wakati na kuboresha iliyopo kuendana na mahitaji ya Taifa na soko la ajira ili wataalam watakaondaliwa na Chuo cha Uhasibu Arusha waweze kuwa chachu katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi kwa jamii na Taifa kwa ujumla.


Prof. Sedoyeka ameishukuru serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ambayo ina mchango mkubwa katika maendeleo ya chuo, katika kuhakikisha IAA inatoa elimu bora kwa jamii ya Watanzania.


Vile vile, Prof Sedoyeka amefafanua mipango mikakati waliyonayo kwa mwaka mpya wa fedha ambayo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kimkakati cha TEHAMA, kukamilisha ujenzi wa baadhi ya majengo ya madarasa na hosteli za wanafunzi katika kampasi ya Arusha, kukamilisha ujenzi wa Kampasi ya Babati na Dodoma, pamoja na ujenzi wa kampasi mpya ya Songea.

Share:

KATAMBI KUTIMIZA NDOTO YA MAGDALENA BUJA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kushoto) Septemba 15 , 2023 akiangalia futi kamba nundu anayoitumia Mwanafunzi asiyeona Magdalena William Buja (wa kwanza kushoto) alipotembelea Chuo cha Ufundi na Marekebisho ya Watu wenye Ulemavu Yombo Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Tungi Mwanjala

Na, Mwandishi wetu. Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amejitolea kutimiza ndoto ya Mwanafunzi Magdalena William Buja (23) mwenye ulemavu wa kutoona kwa kumsomesha na kugharamikia matibabu yake ili kutimiza ndoto yake ya kuwa Mwalimu.

Mwanafunzi huyo mwenye ulemavu huo anasoma katika Chuo cha Ufundi na Marekebisho ya Watu wenye Ulemavu Yombo Dar es Salaam alipata ulemavu huo akiwa kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo.

Hayo yamejiri Septemba 15, 2023 Mhe. Katambi alipotembelea Chuoni hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya Chuo hicho ambapo amesema atahakikisha mwanafunzi huyo anafanyiwa vipimo ili kubaini chanzo cha ulemavu wake.

Amesema majibu ya vipimo yatabainisha kama anaweza kurudi katika hali yake ya awali ama kuendelea na hali hiyo ambapo madaktari watashauri fani anayoweza kusoma ili amsomeshe kuanzia sekondari hadi Chuo Kikuu.

Akitoa neno la shukrani Mwanafunzi huyo, amemshukuru Mhe. Katambi kwa ujio na Uongozi wa Chuo kwa kumfundisha kushona nguo licha ya ulemavu alio nao.

Share:

RAIS SAMIA AFURAHISHWA UTENDAJI KAZI BANDARI YA MTWARA,AAHIDI KUONGEZA BAJETI KUBORESHA MIUNDOMBINU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na ufanisi wa kiutendaji katika Bandari ya Mtwara hasa baada ya maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika katika Bandari hiyo.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Maboresho wa Bandari hiyo, Rais Dkt. Samia amesema Maboresho makubwa yaliofanyika Bandarini hapo yameleta ufanisi zaidi na kuufungua Kiuchumi Mkoa wa Mtwara na Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Ameongeza kuwa Serikali yake itaendelea kuongeza Bajeti ya kuboresha miundombinu ya Bandari ili kuvutia zaidi Wateja, Wadau Wafanyabiashara wa Usafirishaji kuzitumia Bandari zetu.

Vilevile, Rais Dkt. Samia amesema Serikali yake imejiandaa kusafirisha korosho kupitia Bandari ya Mtwara, hivyo ametoa wito kwa Wananchi kujiandaa kuiunga mkono Serikali kwa kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za Bandari.

Rais Dkt. Samia pia ametoa rai kwa Watumishi wa Bandari ya Mtwara kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili Bandari hiyo ifikie kiwango cha Bandari ya Dar es Salaam.

Miradi iliyotekelezwa kama sehemu ya maboresho ya utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara ni pamoja na ujenzi wa Gati moja la nyongeza lenye urefu ww mita 300, ujenzi wa mita ya kupimia mafuta ili kuhakikisha mafuta yanayoshushwa katika Bandari ya Mtwara yanapimwa, ujenzi wa sehemu ya kuhifadhi Makasha na ukarabati wa ghala na vifaa vya kuhudumia mizigo Bandarini.

Katika mwaka wa Fedha wa 2022/2023 TPA kupitia Bandari zake zote Nchini imehudumia Jumla ya Shehena Tani Milioni 24.899 ambapo Bandari ya Dar es Salaam ni Kinara kwa kuhudumia Shehena Tani Milioni 21.461 ikifuatiwa na Bandari ya Mtwara iliyohudumia Shehena Tani Milioni 1.62.

📍Bandari ya Mtwara

🗓️ 15 Septemba,2023

Share:

KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA WIPO





TANZANIA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MRADI WA HAKIMILIKI NCHINI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (kushoto) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia kulinda hakimiliki za Ubunifu duniani -WIPO Bw. Daren Tang ( Kulia) makao makuu ya Shirika hilo Mjini Geneva, Uswisi, tarehe 13 Septemba,2023. 

Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ulinzi wa haki miliki za ubunifu na ushirikiano wa kimataifa ambapo Dkt. Abdallah amemshukuru Bw. Tang kwa ushirikiano Mkubwa ambao WIPO imekuwa ikiutoa, ikiwemo ushauri wa kitaalamu kuhusu uanzishwaji wa Sera ya Taifa ya haki miliki na ubunifu Tanzania bara, kuanzishwa kwa sera ya haki miliki na ubunifu Zanzibar na kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini Tanzania. 

Bw. Tang ameipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mradi wa hakimiliki nchini

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 16,2023




Share:

Thursday, 14 September 2023

TASAC YATOA ELIMU KWA UMMA KATIKA MAONESHO YA KONGAMANO LA WIKI YA PILI YA UFUATILIAJI (U&T) 12-15 SEPTEMBA 2023 ARUSHA - AICC


Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanikiwa kutoa elimu kwa umma ikiwa ni moja ya  ya Taasisi za Kiserikali zinazoshiriki maonesho yanayoendelea katika Kongamano la Wiki ya Pili ya Ufuatiliaji (U&T).

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya AICC jijini Arusha yalianza tarehe 12 Septemba na kilele chake ni tarehe 15 Septemba, 2023. 

TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu kazi  na majukumu inayoyatekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.

Wadau wote mnaalikwa kutembelea banda la TASAC katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger