Monday, 14 August 2023

IJUE SHERIA: HILI NDILO KOSA LA UHAINI

 



Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (1) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania au popote, atakuwa ametenda kosa la uhaini iwapo ataamua:

* Kujaribu kumuua Rais

* Kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, ambaye anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo yafuatayo, atakuwa ametenda kosa la uhaini:

* Kusababisha kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia Rais


* Kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano


* Kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au


* Kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kubainisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi au machapisho au kwa kitendo chochote cha siri kinachojionyesha cha hali yoyote

Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (3) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano, atakuwa ametenda kosa la uhaini kwa:


* Kuwa na  mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko


* Anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au


 * Anabeba silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia, kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano


Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (4) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, atakuwa ametenda kosa la uhaini kwa kuonesha nia ya kumsaidia adui wa Jamhuri ya Muungano kwa kufanya kitendo chochote kinacholenga au kinachoweza kutoa msaada kwa adui huyo, au kuingilia kwa maelekezo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, au kuzuia operesheni ya Majeshi ya Ulinzi au Jeshi la Polisi, au kuhatarisha maisha, ana hatia ya kosa la uhaini.


⚠️ Adhabu ya kosa la uhaini ni kifo


✒️  Kanuni hii ya adhabu ni kwa mujibu wa Sheria ya Uhaini Namba 2 ya mwaka 1970

Share:

RAIS MWINYI AIPONGEZA BENKI YA CRDB KWA KUIMARISHA AFYA NCHINI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Benki ya CRDB kwa juhudi inazozionyesha kuboresha afya nchini na kuzitaka kampuni nyingine binafsi kujitoa ili kuongeza nguvu kwani mahitaji ni makubwa.

Rais Mwinyi ametoa pongezi hizo kwenye kilele cha CRDB Bank Marathon kilichofanyika leo Agosti 13 katika viwanja vya The Green vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuwashuhudia washindi wakiondoka na mamilioni ya zawadi baada ya kuonyesha kasi kubwa kuliko wakimbiza upepo wengine zaidi ya 7,000 waliojitokeza na kushiriki.

Akieleza mchango wa CRDB Bank Marathon kwenye sekta ya afya, Rais Mwinyi amesema ni mkubwa na unagusa pande zote za muungano kwa kuwawezesha wasio na uwezo wa kugharimi amatibabu yao pamoja na kuimarisha miundombinu.

“Fedha zinazokusanywa kutoka kwa washiriki wa mbio hizi za hisani zinaelekezwa kwenye matibabu ya Watoto wenye matatizo ya moyo pamoja na wanawake wenye ujauzito hatarishi. Mwaka huu fedha hizi zitajenga kituo cha afya kule Zanzibar, huu ni mchango mkubwa unaowagusa Watanzania wengi. Nawaomba wadau wengine nao waone namna wanavyoweza kushirikiana na serikali kuboresha huduma za afya,” amesema Rais Mwinyi.

Hata kuratibu mbio hizi zilizokusanya shilingi bilioni moja zitakazoelekezwa kwa walengwa waliokusudiwa mwaka huu, Rais Mwinyi amesema kulihitaji ushiriki wa watu wenye nia moja na akaipongeza kampuni ya Sanlam Insurance ambayo ndio mdhamini mkuu wa mwaka huu.

“Benki ya CRDB inashirikiana na washirika wake kufanikisha mbio hizi. Niwapongeze kampuni ya Sanlam ambao niliwaona ikulu kule Migombani Zanzibar. Homgereni Sanlam kwa kuwa sehemu ya mchango huu mkubwa kwa jamii,” amepongeza Rais.

Akieleza namna mbio za CRDB Bank Marathon zinavyoigusa jamii, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kwa misimu mitatu iliyotanguliwa, fedha zilizokusanywa kutokana na usajili wa washiriki na zile zilizochangwa na washirika, zimewagusa watu wengi.

“Mwaka 2020 wakati tunaanza, zaidi ya watu 4,000 walishiriki na kufanikisha kukusanya shilingi milioni 200 zilizofanikisha upasuaji wa moyo kwa watoto 100 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), pamoja na programu ya utunzaji mazingira ya pendezesha Tanzania,” alsema.

Aliongeza kuwa mwaka 2021 kulikuwa na washiriki 5,000 na jumla ya shilingi milioni 350 zilikusanywa ambazo zilitumika katika upasuaji wa moyo kwa watoto wengine 100 na kujenga Kituo cha Mawasiliano Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Alifafanua kuwa mwaka jana, jumla ya shilingi milioni 470 zilikusanywa kutoka kwa washiriki 6,000 ambazo zilitumika katika gharama za matibabu ya wagonjwa watoto 100 JKCI na wanawake wenye ujauzito hatarishi na walio na maradhi ya fistula katika Hospitali ya CCBRT.

Kutokana na mafanikio hayo, Nsekela amesema msimu huu wa nne wa CRDB Bank Marathon una malengo makuu manne ambayo ni kujenga kituo cha afya ya mama na mtoto visiwani Zanzibar, kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo, kuchangia matibabu ya wanawake wenye ujauzito hatarishi na wanaougua fistula pamoja na kuendelea programu ya pendezesha Tanzania kwa kuimarisha bustani za Zanzibar ikiwamo Bustani ya Jamhuri, Bustani ya Migombani-Botanic Garden, Bustani ya Tenga-Mnazi Mmoja, Bustani ya Mbele ya Ikulu Migombani pamoja na Njia Nne za Michenzani.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba alisema mafanikio ya mbio wanazoziratibu waliyoyapata ndani ya miaka mitatu iliyopita yamevuka mipaka kwani katika mwaka wa pili tu zilitambulika kimataifa na Chama cha Usajili na Upimaji wa Mbio za Kimataifa (AIMS) na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa Riadha (World Athletics).

“Hii si tu imekuwa ni heshima kwa Benki yetu lakini pia ni heshima kwa nchi yetu. Kwa utambulisho huu wa kimataifa, mbio za CRDB Bank Marathon zinavutia wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni hivvo kuzifanya kuwa sehemu ya kutangaza utalii wa nchi yetu,” alisema Warioba.

Warioba alisema kuwa mafanikio ya mbio za mwaka huu yamechangiwa na wadau kadhaa wanaoshirikiana na Benki ya CRDB ambao ni kampuni ya Sanlam Insurance, Alliance Life Insurance, Clouds Media Group Jubilee Allianz & Life Insurance, Heritage Insurance, Britam Insurance, Strategis Insurance, A1 Outdoor, Gardaworld, Mwananchi Communications, IPP Media, Sahara Media, Softnet, BEVCO, Hyatt Regency, na Spik & Span.

Afrika Mashariki wagawana zawadi
Zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi 100 zilizotolewa kwa washindi wote walioshiriki kilomita 42, kilomita 21, kilomita 10 na kilomita tano pamoja na kilomita 65 kwa waendesha baiskeli zilikwenda kwa wawakilishi kutoka karibu mataifa yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kwenye kilomita 42 (full marathon), Jakline Juma wa Tanzania na Moses Menginch wa Kenya waliongoza makundi yao hivyo kuondoka shilingi milioni 10 walizoshinda huku nafasi ya pili ikienda kwa Paskalia Chipkorir wa Kenya na Jonathan Akankwasa walizawadiwa shilingi milioni 5 na Nancy Cheptegei wa Uganda na Rashid Muna wakiondoka na shilingi milioni 2, baada ya kushika nafasi ya tatu.

Kwenye mbio za kilomita 21 (nusu marathon), Watanzania waling’ara katika makundi yote mawili, yaani wanawake na wanaume baada ya Magdalena Crispin na Josephat Joshua kuongoza. Nafasi ya pili ilikwenda kwa Atalena Napule Gasper wa Sudan na Nangat Willy wa Kenya huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Failuna Matanga wa Tanzania na Panuel Mkingo wa Kenya.

Ceclia Panga, Transfora Musa na Neema Kisuda waliwaongoza wanawake kukimbia kilomita 10 huku Shuemery Mohamed, Josephat Tiophil na Jonas John wakifanya hivyo kwa wanaume. John Msigwa, Danidi Kisoni na Justine Mbegu walikuwa moto wa kuotea mbali kwa wavulana waliokimbia kilomita tano.





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi akimvalisha medali ya kushiriki mbio za hisani za CRDB Bank Marathon Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance Life Assurance, Byford Mutimusakwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Neema Mori. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba, Waziri wa Habari, Vijana na Michezo Zanzibar, Tabia Mwita, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt Pindi Hazara Chana na Mke wa Rais Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi.











Share:

Sunday, 13 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 14,2023































Share:

ALLY SALIM AIBEBA SIMBA SC IKIICHARAZA YANGA SC


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

GOLIKIPA wa Simba SC, Ally Salim Khatoro ameibuka shujaa (The hero) baada ya kudaka penalti tatu kwenye mchezo wa Fainali ya mashindano ya Ngao ya Jamii 2023 dhidi ya Yanga SC kwenye dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Katika mchezo huo, Simba SC wameibuka kidedea kwa jumla ya mikwaju ya penalti 3-1 dhidi ya mtani wao Yanga SC baada ya sare ya 0-0 kwenye dakika 90’ za mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki lukuki wa soka kwenye dimba hilo la Mkwakwani.

Changamoto ya mikwaju ya penalti ilifuata baada ya sare hiyo tasa kwenye dakika hizo 90’. Simba SC walianza kupiga mkwaju wao wa penalti kupitia kwa Kiungo wao, Mzamiru Yassin Selemba ambaye alimpoteza maboya Golikipa wa Yanga SC, Djigui Diarra.

Yanga SC walipiga mkwaju wao wa kwanza kupitia kwa Stephane Aziz Ki ambaye alipiga vizuri mkwaju huo na kuweka wavuni akimuacha Golikipa Ally Salim hana la kufanya. Simba SC walipiga mkwaju wao wa pili kupitia kwa Saido Ntibazonkiza ambaye alikosa kwa Diarra kupangua vizuri.

Kiungo Khalid Aucho alikosa mkwaju wa penalti wa pili baada ya Ally Salim (The hero) kudaka na kuuficha kabisa mpira wa Aucho uliopigwa upande wake wa kulia. Simba SC nao walikosa mkwaju wa tatu baada ya Moses Phiri kuupeleka juu ya lango mpira. 

Mkwaju wa tatu wa penalti wa Yanga SC uliopigwa na Kiungo Pacôme Zouzoua ambaye alikosa kwa mkwaju wake kupanguliwa na Ally Salim. Penalti ya nne ya Simba SC ilipigwa na Mshambuliaji Onana Essomba Willy ambaye alipata kwa kumuacha Kipa Diarra hana la kufanya.

Mlinzi wa kulia wa Yanga SC, Kouassi Attohoula Yao alikosa mkwaju wa nne ambao ulipanguliwa tena na Ally Salim. Mkwaju wa ushindi kwa upande wa Simba SC ulipigwa na Mshambuliaji Jean Baleke ambaye alimuacha Diarra hana la kufanya kudaka mkwaju huo.

Mchezo wa awali wa kusaka nafasi ya tatu wa Ngao ya Jamii uliisha kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars kwenye huo huo wa CCM Mkwakwani.

 Katika mchezo huo mabao ya Azam yalifungwa na Washambuliaji Prince Dube kwenye dakika ya 1’ na Abdul Suleiman Sopu dakika ya 42’.


Share:

TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA- DKT MABULA

Na Munir Shemweta, Ludewa

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (MNEC) Dkt Angeline Mabula amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutangaza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ili yaweze kufahamika kwa wananchi.
Dkt Mabula ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema hayo tarehe 11 Agosti 2023 alipotembelea ofisi ya CCM wilaya ya Ludewa na kuzungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho akiwa katika ziara yake mkoa wa Njombe.

Alisema, wakati serikali ya awamu ya sita ikifanya mambo makubwa ya kuwaletea watanzania maendeleo, viongozi pamoja na wanachama wa CCM katika ngazi mbalimbali wana jukumu la kutangaza mafanikio yaliyofanywa na serikali inagoongozwa na Raisi Samia Suluhu Hassa.

"Chama kitangaze mafanikio ya serikali na ninyi viongozi wa ngazi mbalimbali mnalo jukumu hilo ambapo Rais wetu Samia Suluhu Hassa ameonesha kuwajali wananchi kwa ujenzi wa madarasa, zahanati pamoja na kuanzizsha shule mpya, hayo ni mafanikio makubwa" alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Mjumbe huyo wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, yote yanayofanywa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kiasi kikubwa yamemgusa kila mtu kutokana na kulenga huduma za jamii.

Dkt Mabula pia amegusia miradi mikubwa ya kimkakati kama vile Bwawa la Mwalimu Nyerere pamoja na reli ya mwendo kasi kuwa ni miradi inayokwenda kuipaisha Tanzania ambapo amesema hata mchakato wa bandari unaoendndelea sasa utakapokamilika unaenda kuwa wa aina yake.

Aidha, amekitaka chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa kuangalia fursa za uwekezaji katika miradi mbalimbali na kutolea mfano wa Liganga na Mchuchuma kuwa chama kinaweza kuwekeza katika eneo hilo ili kukiwezesha kutekeleza majukumu yake bila kutegemea misaada.

"Ni vizuri chama kikaangalia fursa zinazopatikana, kama hapa mnao mradi wa Liganga na mchuchuma mnaweza kuomba vitalu na kuwekeza ili chama kiwe na nguvu na kujisimamia chenyewe jambo litakalowafanya kuheshimika na kama huwezi kujisimamia siyo vizuri". alisema Dkt Mabula.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Angeline Mabula akiwasili ofisi za CCM wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe wakati wa ziara yake mkoani humo mwishoni mwa wiki. Kulia kwa Dkt Mabula ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Angeline Mabula akizungumza kwenye kikao na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho wilayani Ludewa mkoa wa Njombe mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wakimpokea Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Dkt Angeline Mabula alipotembelea ofisi za chama hicho mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Dkt Angeline Mabula alipotembelea ofisi za chama hicho wilayani Ludewa mwishoni mwa wiki.

Share:

JE, UNA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU?, DAWA HII ITAKUSAIDIA SANA!


Kutokana na mtindo wa maisha kubadilika sana ulimwenguni kutokana na ukuaji wa teknolojia, watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kuvimba kwa miguu.

Mimi ni miongoni mwa watu walioteswa sana tatizo hilo kwa zaidi ya miaka minne, nilitumia dawa za kila namna lakini sikuweza kupona hadi kusema huu ni ugonjwa wangu sasa, inanibidi nijifunze jinsi ya kuishi nao tu licha maumivu niliyokuwa napitia.

Jina langu ni Sofia kutokea Eldoreti hapa nchini Kenya, kuna siku niliamka na kukuta miguu yangu imevimba ghafla lakini sikuweza kujua sababu ni nini hasa.

Nilijua ni hali tu ya kawaida na  baada ya muda itaweza kupotea, hata hivyo haikuwa kama ambavyo nilitarajia kwani hali iliendelea kuwa mbaya zaidi hadi kuanza kutembea kwa shida.

Hatimaye niliamua kwenda Hospitali kupata tiba, nilitumia dawa za huko kwa muda mrefu bila matokeo ya aina yoyote ile, hali yangu ya kuvimba miguu iliendelea kunitesa sana.

Baadhi ya rafiki zangu walinishauri niende kwa waganga wakienyeji wakanicheki kama kuna majini nimetupiwa, nilifanya hivyo lakini wataalamu wale walikula fedha zangu bila kupata suluhisho.

Wengi walikuwa wanasema kuna mtu kaniloga hivyo nitoe fedha ili waweze kuniondolea shida hiyo lakini kwa bahati mbaya hakuna hata mmona aliweza kunisaidia kama ambavyo nilitarajia.

Pona yangu ilikuja siku moja ambapo nilisikia kwenye redio kuna mtu anaitwa African Doctors anaweza kunisaidia kushinda ugonjwa huo kwa kutumia dawa zake za mitishamba.

Nilisafiri hadi ofini kwake ambapo nilipokelewa vizuri kabisa na kupatiwa dawa ambayo iliniponya moja kwa moja ugonjwa huo ambao ulinitesa kwa miaka mitano.

Tangu wakati huo nimekuwa hata nikiwashauri watu wenye magonjwa sugu kwenda kwa African Doctors ambaye kwangu naona ni mtaalamu wa tiba za mitishamba namba moja hapa duniani.

 Kumbuka African Doctors  ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Pia anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha, kifafa, upungufu wa nguvu za kiume, kuvimba miguu, kaswende, vile vile anawezesha wanawake kubaba ujautizo, wanaume kutungisha mimba n.k.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger