Sunday, 13 August 2023

WANANCHI WA KIJIJI CHA KILOLELI - KISHAPU WAHAMASIKA UJENZI WA MATUNDU YA VYOO

Na Mwandishi wetu _ Malunde 1 blog

WANANCHI wa kijiji cha Kiloleli halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga wamefanikiwa kuanzisha ujenzi wa matundu 24 ya vyoo na chumba kimoja cha kujistiri wanafunzi wa kike wakati wa hedhi na kuondoa changamoto iliyokuwa ikiwakabili shuleni hapo.

Ujenzi huo umetokana na wanakituo cha taarifa na maarifa waliojengewa uwezo na Mtandano wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuibua changamoto zinazowakabili katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu,Afya na Maji.

Wakiongea na waandishi wa habari waliofika katika kijiji hicho jana tarehe 12/08/2023 kuona mafanikio ya wananchi ambayo yaliibuliwa na wanakituo cha taarifa na Maarifa kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto shuleni.

Mwanakituo cha taarifa kijiji cha Kiloleli Helena Makele amesema wanafunzi wamekuwa wakijisaidia vichakani baada ya matundu ya vyoo manane kujaa na hayatoshelezi kwa wanafunzi waliopo hivyo wakahamasishana wao na baadaye kulipeleka kwenye mkutano wa hadhara wananchi wakakubali kuchangia fedha.

Mwanakituo cha taarifa na Maarifa kutoka Kiloleli Joseph Solea amesema waliona changamoto kubwa ni kukosa matundu ya vyoo maana yaliyopo yalikuwa yamejaa wakajadiliana , wakahamasisha  jamii ikakubali kuanza kutoa sh 1000 na kuchimba shimo kwa kujitolea na wakaona haitoshi wakarudi tena kuchangia sh 2000 wanafunzi wakihitaji huduma wanajitafutia mahali popote.

Mkazi wa kijiji cha Kiloleli Martha Ngwelu amesema waliibua ujenzi wa vyoo kutokana na vyoo vyenye matundu manane kujaa na havikutosheleza kutokana na idadi ya wanafunzi hivyo waliitishwa mkutano wa hadhara na kukubaliana kuanzisha ujenzi huo.

“Hamasa ilitoka kwa wanakituo cha taarifa na maarifa baada ya wao kuanzisha harambee ya mchango na kutoa sh 50,000 na mifuko ya Saruji mitano lakini sisi mara nyingi tulikuwa tukiliongelea kwenye mikutano ya hadhara bila mafanikio wao wametuhamasisha vyoo vimeanza kujengwa”amesema Ngwelu..

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Msingi Kiloleli Juliana Petro amesema shule hiyo ina wanafunzi 997 changamoto iliyopo ni ukosefu wa matundu ya vyoo na wanafunzi wanapitwa na masomo kwa kushelewa chooni sababu ya matundu yaliyokuwepo yamejaa na machache na sasa wanajisaidia vichakani.

“Matundu 24 ya vyoo yaliyojengwa yatasaidia kuondoa changamoto iliyokuwepo awali kulikuwa hakuna chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike sasa kimewekwa jamii imeanza kupata uelewa kwani uwiano unaotakiwa wanafunzi 25 tundu moja kwa wakiume na wa kike wanafunzi 20 tundu moja”amesema Juliana Petro.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kiloleli Kuhwema Mshala amesema changamoto zilizokuwepo shuleni matundu ya vyoo yalikuwa hayatoshi na yamejaa wakaamua kuwaita vituo vya taarifa na maarifa na wananchi wakazungumza kwenye mkutano wa hadhara na kukubaliana kituo cha taarifa na maarifa kutoa sh 50,000 na mifuko ya Saruji mitano.

“Wananchi walikubaliana kuchangia sh 2000 tukanunua nondo na Saruji na kujenga bamba na wananchi wakachimba tena karo na kuleta mchanga nguvu kazi na kikao cha Maendeleo ya kata (WDC) walitoa mifuko 30 ya Saruji na matofali yakavyatuliwa kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo”

Mashara amesema serikali ya kijiji ilitoa sh 600,000 na Sungusungu walitoa sh 500,000 na ujenzi ukaanza na wanaiomba serikali waongeze fedha waweze kupaua lakini wakiona wanachelewa watajitahidi wakamilishe wenyewe.

Mtendaji wa kijiji Nicholaus Mzirai amesema halmashauri ya kijiji hicho wamepata sh Millioni 1.3 zitokanazo na ushuru wa zao la pamba na wamefanya matumizi ya sh 500,000 kwaajili ya uendelezaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo na michango ya wananchi ilipatikana sh 700,000.
Choo cha zamani shule ya msingi Kiloleli.

Matundu ya vyoo cha zamani shule ya msingi Kiloleli.







Mkazi wa kijiji cha Kiloleli Martha Ngwelu Akizungumza na waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kiloleli Kuhwema Mshala Akizungumza.

Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Kiloleli Juliana Petro akizungumza.

Vyoo vipya  vyinavyojengwa shule ya msingi Kiloleli.


Vyoo vipya  vyinavyojengwa shule ya msingi Kiloleli.

Mtendaji wa kijiji Nicholaus Mzirai akizungumza na waandishi wa habari.







Share:

MSEVENI ATUPWA JELA MIAKA 30 , KUCHAPWA VIBOKO 10 KWA KUMBAKA MTOTO WAKE "ALIMLEWESHA"


Na MWANDISHI WETU MALUNDE 1 BLOG

Mkazi wa Mtaa wa Nyasubi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga Mseveni Mchele Derefa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, viboko 10 na faini ya Shilingi milioni 1 na Mahakama ya Wilaya ya Kahama baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 12.


Hukumu hiyo imetolewa juzi na Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Edmund Kente baada ya kuridhika na Ushahidi uliotolewa na Jamhuri ambao umethibitisha kosa hilo, pasipo kuacha shaka kuwa Mseven alitenda kosa hilo.


Amesema Mahakama imemtia hatiani kwa mujibu wa kifungu namba 130 kifungu cha 1, 2 (e) na 130 (1) vya Kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marejeo ya Mwaka 2022 ambapo Mseveni atatumikia kifungo cha Miaka 30 jela viboko 10 na faini ya Shilingi milioni moja.

Alifafanua kuwa Mahakama imetoa adhabu hiyo kwa Mseven ili iwefundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hizo kwenye jamii ambao wanatekeleza matukio ya ukatili kwa watoto huku wakijua vitendo hivyo vipo kinyume cha Sheria.

Awali akisoma Shauri hilo la jinai namba 135 la Mwaka 2023 Wakili wa Serikali aliyekuwa anasimamia shauri hilo, Jukael Jairo aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa Mseveni ili iwe fundisho kwake na kwa wazazi wengine wanaotekeleza matukio ya ukatili kwa watoto wao.

Naye Mseven katika utetezi wake aliiomba Mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa madai kuwa anafamilia ya watoto watano wanaomtegemea, hoja ambayo ilitupiliwa mbali na Mahakama na kupatia adhabu hiyo.

Ikumbukwe kuwa Mseveni alituhumiwa kutenda kosa hilo Aprili 15 Mwaka huu kwa kumbaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 12 Mwanafunzi darasa la saba shule ya Msingi Nyasubi kwa kumlaghai kwa kumpatia Chipsi na Kinywaji kilichochanganywa na Kilevi akimwambia ni dawa ya kutibu tatizo la UTI.

Kitendo hicho alikuwa akikifanya baada ya mke wake kusafiri kwenda mkoani Morogoro kumpeleka mtoto wake kwenye Matibabu na kumwachia binti huyo nyumbani huku taarifa za kufanyiwa ukatili huo zilitolewa na Majirani waliokuwa wakisikia kelele za binti kuingiliwa na Baba yake nyakati za usiku.

soma pia:
Share:

MBUNGE UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA KATA YA DUGA JIJINI TANGA

 








*Atembelea Kituo Cha Afya Duga 
*Afungua Shina la Wakereketwa 
•Afungua Ofisi ya CCM  kata CCM ya duga .
     
Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu leo tarehe 12/8/2023 amefanya ziara kata ya Duga. Katika ziara hii mbunge ametembelea kituo Cha Afya duga kukagua utoaji wa huduma ambapo amepongeza watumishi kwa kutokuwa na kifo hata kimoja cha mama mjamzito na watoto wachanga. Mhe Ummy amesema kuwa Rais Samia atatoa gari ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya Kituo cha Afya Duga. 

Aidha Mh Ummy amemtaka Mganga Mkuu wa Jiji  kusimamia kwa karibu upatikanaji wa Dawa katika Kituo hicho. Mhe Ummy pia ameutaka Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kufanya ukarabati wa paa la Kituo hicho ili kuepusha madhara kwa wananchi. 
  
Pia Mhe Mbunge  alifungua shina la vijana wa CCM lililopo mtaa wa Magomeni Kirare na  kutoa shilingi milioni 1 kuwaunga mkono vijana hawa na kuahidi kuwatengenezea  turubai moja (tent) .

Pia Mhe Ummy amefungua Ofisi ya CCM kata ya Duga na   kusema ataendelea kujitolea kwa ajili ya Chama. Awali Mhe mbunge amenunua meza 3 na viti 7 kwa ajili ya ofisi hiyo.

Mwisho mbunge Ummy alitembelea makazi ya wazee duga ambayo ni kawaida yake kila mara kuenda eneo hilo au kutuma wasaidizi  wake kuwaona wazee hao na kuwapatia vyakula.

Katika ziara hiyo, Mhe mbunge aliambatana na viongozi wa chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Tanga wakiongozwa na Mwenyekiti Meja  mstaafu Hamisi Bakari Mkoba, Mkuu wa wilaya ya Tanga, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe Shillow na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Simon
 
Imetolewa na :
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tanga Mjini
12/8/2023
Share:

Saturday, 12 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 13,2023

























Share:

WANANCHI KITOBO MISENYI WAANZA KUPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA



Na Mariam Kagenda _ Kagera

Wakazi zaidi ya 5000   wa  kata ya Kitobo wilaya ya  Missenyi mkoani Kagera wameondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama baada ya serikali kutekeleza mradi wa maji Kitobo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 802.

Wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi huo Meneja wa Ruwasa wilaya ya Missenyi Mhandisi Andrew Kilembe amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa January 18 mwaka 2022.

Mhandisi Kilembe amesema kuwa mradi huo umekamilika Juni 30 mwaka huu na kaya 102 kati ya kaya 973 na Taasisi 7 zimeunganishiwa huduma ya maji majumbani na zoezi la kuunganisha linaendelea.


Miundombinu ya mradi iliyojengwa ni pamoja na tenki la maji lenye ujazo wa lita 135000,tenki dogo lenye ujazo wa lita 50000, vituo 10 vya kuchotea maji , nyumba ya mtambo1 na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilo mita 27.1 .

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 Abdalla Shaib Kaim ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa namna inavyoendelea kuisaidia jamii kwa kuondokana na  changamoto ya maji.

Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wameshukuru kuletewa mradi huo kwani walikuwa wanaancha shughuli za uzalishaji na kwenda kufata huduma ya maji.
Share:

MBUNGE BYABATO ATOA MSAADA WA MAJIKO YA GESI KWA MAMA LISHE, TV KWA WAFANYABIASHARA SOKO KUU BUKOBA


Na Mariam Kagenda - Bukoba

Katika jitihada za kuhakikisha anarudisha shukrani kwa wananchi waliomchagua mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato ametoa msaada wa Television 6 kwa wafanyabiashara wa soko kuu la Bukoba na majiko 28 ya gesi kwa mama lishe.


Mhe. Byabato amekabidhi Television pamoja na majiko ya gesi Agosti 11, 2023 na kuwasha Television hizo jambo ambalo litawasaidia wafanyabiashara wa soko hilo kutopitwa na habari za matukio mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi.


Akizungumza na wafanyabiashara hao amesema kuwa amenunua Television hizo ikiwa ni shukrani zake kwa wafanyabiashara wa soko kuu na kuhakikisha hawapitwi na taarifa ya habari, mpira na hotuba za viongozi wa Kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na matukio mengine yanayoendelea ndani na nje ya nchi.


Ameongeza kuwa Television hizo wanaweza kuzitumia kuangalia vipindi vya bunge pamoja na vipindi mbalimbali cha kuelimisha jamii juu ya maswala ya afya,elimu na kilimo.


Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali akiwemo mstahiki Meya na madiwani .


Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko kuu wamemshukuru Mhe. Mbunge Stephen Byabato kwa kuona umuhimu wa kupeleka Television katika soko hilo na kuomba afikishe salamu zao za shukrani na pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan.


Share:

KATAMBI: UWANJA WA KWARAA KUTUMIKA KILELE CHA MWENGE WA UHURU



*Ataka mkandarasi akamilishe kwa wakati


Na: Mwandishi Wetu - MANYARA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amemuagiza mkandarasi anayejenga uwanja wa mpira wa Kwaraa kumaliza kwa wakati ili kutumika katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.


Mhe. Katambi ametoa maelekezo hayo Agosti 11,2023 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwanja huo kuelekea kilele cha mbio hizo za zitakazohitimishwa Oktoba 14, 2023.


Aidha, amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo ni mpango wa Serikali katika kuwasongezea karibu viwanja vya michezo wananchi wa Mkoa wa Manyara lakini pia utakautumika kwenye kilele hicho.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Lazaro Twage amemhakikishia Naibu Waziri kuwa kuwa watamsimamia mkandarasi ili ujenzi huo ukamilike ndani ya muda uliopangwa.


Katika ziara hiyo, Mhe. Katambi amekagua pia Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro -Manyara itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa, uwanja wa stendi ya zamani itakapofanyika wiki ya vijana na kukagua maendeleo ya vijana wa halaiki katika Shule ya Sekondari ya kutwa ya Babati.


Share:

MERIDIANBET WAMEKUJA NA MZIGO WA KUTOSHA MSIMU HUU

Kampuni kubwa ya ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na kaulimbiu mpya msimu huu mpya wa soka barani ulaya wa “Meridianbet Mzigo wa Kutosha” ambao unamaanisha kuwa pesa zipo kibao wewe bashiri utapata kiasi chochote ambacho utakuwa umeshinda.

EPL mechi zipo kibao ambazo zinaweza kukupatia mkwanja wa maana kabisa huku mechi ya mapema itakuwa ni kati ya Arsenal ambaye atakuwa nyumbani dhidi ya Nottingham Forest . The Gunners amepewa ODDS ya 1.18 huku mgeni akiwa na 13.72. Nani kuondoka na ushindi? Bashiri sasa mechi hii.

Mechi nyingine kali pale Uingereza itakuwa ni kati ya vijana wa Eddie Howe Newcastle dhidi ya Aston Villa huku mechi ya mwisho kuonana mwenyeji alipoteza mechi hiyo akiwa ugenini. Leo yupo nyumbani. Je anaweza kulipiza kisasi?

Meridianbet Msimu Mpya Mzigo wa Kutosha

Huku ukiendelea kubfanya ubashiri wa mechi kumbuka kuna michezo ya kasino kama vile, Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao ya kupiga pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Pata mizunguko 50 ya bure kucheza sloti na michezo ya kasino ya mtandaoni ukijisajili na Meridianbet. Jisajili kupitia link hii

ODDS KUBWA machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu kinapatikana Meridianbet ingia sasa na ufanye ubashiri wako uweze kutimiza ndoto zako za kuwa bingwa. Pia kuna michezo ya kasino ya mtandaoni ambayo inatolewa na Meridianbet. Ingia www. Meridianbet.co.tz.

Keshokutwa sasa Cheslea watkipiga dhidi ya Liverpool huku timu hizi msimu uliopita walipokutana hakuna mabaye alikuwa mbabe kati yao huku The Blues wakiwa na msimu mbaya sana baada ya kumaliza nafasi ya 12 kwenye msimamo. ODDS ya ushindi amepewa Klopp akiwa na 2.40, na mwenyeji ana 2.79. Beti yako unaipeleka wapi?

Pale LALIGA sasa nayo itaanza kutimua vumbi leo ambapo hapo kesho mabingwa watetezi Barcelona watakuwa ugenini kukiwasha dhidi ya Getafe huku wakihitaji pointi 3 muhimu waweze kuanza msimu vizuri. Wakati wapinzani wao wakubwa Real Madrid wao watcheza dhidi ya Athletic Bilbao. Ancelloti na vijana wake wana ODDS ya 2.16 kwa 3.23, beti yako unaipeleka kwa nani?

 Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

Mechi nyingine ya kusisimua pale Hispania itakuwa ni kati ya Villarreal dhidi ya Real Betis na mechi mbili za msimu uliopita, Betis aliondoka na pointi 4. Je Nyambizi wa Njano atakubali na msimu huu kupoteza pointi hizo au atapindua meza?

Ndugu mteja endelea kubeti na Meridianbet huku ukisubiri mechi za ligi zote kurejea wiki ijayo na kwasasa odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

Tukitoka hapo tunaenda moja kwa moja mpaka kule LIGUE 1, na Mabingwa watetezi wa ligi hiyo PSG watakuwa pale Parc des Princes kumenyana dhidi ya Lorient. Paris wana kocha mpya ambaye ni Luis Enrique. Je mabingwa hawa ambao hawana Messi na Mbappe wataanzaje?

Marseille atamualika Reims hii leo kusaka pointi tatu za maana kujifua kwaajili ya kucheza michuano ya Ulaya. Je nani kuondoka na alama zote mechi hii?

NB: Habari njema kwako, Meridianbet imesikia ombi la wengi imekuja na Jackpot kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindi atajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#

#MERIDIANBET MSIMU MPYA, MZIGO WA KUTOSHA


Share:

Tanzia : MWENYEKITI WA ZAMANI WA SIMBA SC AYOUB CHAMSHAMA AFARIKI DUNIA

 

Ndugu Soud Ayubu Chamshama
wa Chang'ombe Dar es salaam 
Anasikitika kutangaza kifo cha Baba 
Yake mzazi,  Mzee Ayubu Salehe Chamshama, 
Kilichotokea tarehe 11 Agosti 2023
nchini India alikokuwa kwa matibabu.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 15 Agosti 2023 kijijini kwao Kilole, Lushoto, Mkoani TANGA.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe Maduka Mawili Dar es salaam.

Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa na marafiki popote pale walipo.

Enzi za uhai wake Marehemu Chamshama alishika nyadhifa mbalimbali. Alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni ya Tanzania Tea Blenders, vilevile alihudumu kwa muda mrefu kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC na pia alikuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
Share:

WAZIRI MABULA AHIMIZA MATUMIZI YA KLINIK ZA ARDHI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wilayani Ludewa wakati wa ziara yake katika mkoa wa Njombe tarehe 11 Agosti 2023. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva na kushoto ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba.

***************

Na Munir Shemweta, WANMM LUDEWA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewaelekeza watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuhakikisha wanakuwa na kliniki za ardhi kama ilivyoelekezwa na wizara yake ili kutatua changamoto za sekta ya ardhi.

Dkt Mabula ametoa maelekezo hayo tarehe 11 Agosti 2023 wilayani Ludewa mkoa wa Njombe kufuatia kupokea malalamiko mbalimbali kuhusu changamoto za sekta ya ardhi katika mkutano wa hadhara akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe.

Katika mkutano huo, wananchi walimlalamikia waziri Mabula kuwa, wamekuwa wakipata usumbufu kutoka kwa watendaji wa sekta ya ardhi katika mambo mbalimbali yanayohusiana na sekta ya ardhi jambo linalowafanya kushindwa kupata huduma stahiki ikiwemo hati milki.

‘’Wananchi wengi katika wilaya ya Ludewa hatuna hati milki za ardhi, tukikosa hati miliki maisha yetu yako hatarini maana tunaweza kunyang’anywa viwanja wakati wowote’’ alisema mkazi wa Ludewa Cosmas Sanga

Mkazi mwingine Herman Luoga alisema, mbali na kupimiwa mashamba kwa ajili ya kupatiwa hati za kimila lakini pamoja na kufuatilia mara kwa mara ofisi za ardhi kwenye ofisi za ardhi katika halmashauri ya wilaya ya ludewa wameshindwa kupata majibu hadi sasa.

‘’Jambo ambalo ningependa watumishi wa sekta ya ardhi wafanye ni kuwa na klinik za ardhi ambazo wizara yake imeziekeleza kufanyika nchi nzima’’ alisema Waziri wa Ardhi Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kupitia klinik za ardhi watumishi wa sekta ya ardhi watatoka ofisini kwenda kwenye kata na kuweka vikao kwa ajili ya kusikiliza hoja, changamoto na kero za sekta ya ardhi kutoka kwa wananchi na wanaposikiliza lazima watoe majibu papo hapo kwa kuwa wao ndiyo wataalamu wa sekta hiyo.

Alisema, katika maeneo hayo wanaweza kukaa siku moja ama mbili kutegemeana na uhitaji wa eneo husika na kuongeza kuwa, kliniki hizo za ardhi zinatakiwa kuzungukia kata zote za halmashauri ambapo alisisitiza kuwa ya watendaji hao kabla ya kwenda eneo husika lazima watangaze ama kutoa taarifa mapema siku watakayokwenda.

‘’Kwa sababu wakati mwingine changamoto hakuna isipokuwa elimu, mtu haelewi kwa nini amiliki ardhi kwa nyaraka, mtu hajui akitaka kupimiwa aanzie wapi na mwingine amevamiwa katika eneo lake hajui afanye nini’’ alisema Dkt Mabula.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe ambapo alitembelea wilaya za Njombe, Makete pamoja na Ludewa ambapo mbali na kuzungumza na watumishi wa sekta ya ardhi pamoja na wananchi wa wilaya hizo alikabidhi hati milki kwa wananchi waliokamilisha taratibu za kupatiwa hati.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe Victoria Mwanziva akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula (kushoto) tarehe 11 Agosti 2023. Kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ludewa Gilbert Sandagila na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias.


Sehemu ya wananchi wa Ludewa mkoani Njombe wakiwa katika mkutano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula uliofanyika wilayani humo tarehe 11 Agosti 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsalimia mlemavu mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi wa Ludewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo tarehe 11 Agosti 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipokea zawadi ya mbuzi aliyopewa na wananchi wa Ludewa kama zawadi baada ya kufanya ziara katika wilaya hiyo tarehe 11 Agosti 2023. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpongeza mmoja wa wananchi wa Ludewa aliowakabidhi hati katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo tarehe 11 Agosti 2023. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva.

(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

Friday, 11 August 2023

TRA YAKANUSHA BODA BODA KUTOZWA KODI




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger