Wednesday, 19 July 2023

PROF. MKENDA ASISITIZA TAASISI ELIMU YA JUU KUFANYA MAPITIO YA MITAALA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akizindua rasmi Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezitaka Taasisi za Elimu ya Juu nchini kuendelea kufanya mapitio ya Mitaala iliyopo kwa kuzingatia miongozo iliyopo ili kuendana na mabadiliko ya soko la Ajira.

Prof. Mkenda ametoa Rai hiyo wakati akizindua rasmi Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo yanaongozwa na kauli mbiu isemayo Kukuza Ujuzi Nchini Kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi Imara na Shindani.

"Kauli mbinu ya Maonesho haya inaakisi hali halisi na matarajio ya Watanzania. Sisi kama Taifa tunaendelea na mchakato wa mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na Mitaala ya Elimu na Mafunzo kwa ngazi zote". Alisema Prof. Mkenda

Amesema Serikali inatambua kuwa Elimu ya Juu ni Elimu ya Kimataifa, kwa kuzingatia hilo amevisisitiza Vyuo Vikuu kuendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali duniani ili kujenga mahusiano yenye tija kuwawezesha Watanzania kupata maarifa na ujuzi.

"Leo tumeweka sahihi ya mashirikiano ya kielimu kati ya Tanzania na Serikali ya Hungary, ambapo kutakuwa na ufadhili wa Wanafunzi kwenda kusoma nchi hiyo, vile vile Tanzania itatoa ufadhili wa Wanafunzi wao kuja kusoma hapa nchini, ili kuvifanya Vyuo Vyetu kuwa vya Kimataifa kwa kupokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali duniani, na hatimae kutoa wahitimu wenye Ujuzi na stadi za maisha " alieleza Prof. Mkenda.

Aidha Prof. Mkenda amezitaka Taasisi hizo kuhakikisha zina buni program mpya zitakazoendana na wakati pamoja na kuimarisha au kuanzisha mahusiano yenye tija baina yake na Taasisi za utafiti pamoja na sekta binafsi na kuweka utaratibu wa kuendeleza Teknolojia na kuhamasisha matumizi yake ili kuongeza kasi ya Maendeleo ya kijamii.

Awali akizungumza kuhusu Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa amesema jumla ya Taasisi 83 za ndani na Nje ya nchi zimeshiriki ukilinganisha na Taasisi 75 zilizoshiriki Maonesho kwa mwaka uliopita.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila,akizungumza wakati wa Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa,,akizungumza wakati wa Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.






Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Share:

NDERIANANGA AWATAKA WATANZANIA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA

 




Na Mathias Canal, Moshi-Kilimanjaro

Mbunge wa Viti maalumu Mhe Ummy Nderiananga ambaye pia ni Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akiwa katika ziara mkoani Kilimanjaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa imani kubwa aliyompatia ya kumteua kuwa Naibu Waziri.

Akizungumza Katika mkutano na wananchi uliofanyika katika kijijini kwao Lotima ambapo ndipo alipozaliwa katika Kata ya Makuyuni ambapo ameeleza umuhimu wa shule za kata katika kuimarisha elimu nchini kwani zimeongeza chachu ya mafanikio kwa wananchi ambapo ametolea mfano yeye ambaye alisoma katika shule hizo.

Amesema kuwa Rais anafanya kazi usiku na mchana hivyo watanzania wanapaswa kumtia moyo na kumuunga mkono ili aweze kufikia dhamira ya kuwaletea maendeleo endelevu.

"Mhe Rais Samia ana upendo mkubwa na wana Kilimanjaro na sisi wanamakuyuni tumeona upendo wake, tumeona kujali kwake na kuthamini kwake" Amekaririwa Mhe Nderiananga.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Kimei amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo utengenezaji wa barabara ya Himo-Makuyuni kwa kiwango cha lami ambayo imeshaanza kutengenezwa.

Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo utarahisisha huduma za kijamii ikiwemo usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe Kisare Makori ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Kwa miradi mingi ya maendeleo katika Wilaya ya Moshi.



Share:

Tuesday, 18 July 2023

SERIKALI, ABBOTT FUND KUIMARISHA SEKTA YA USTAWI WA JAMII


Kaimu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju akizungumza jambo wakati wa Ziara ya bodi ya Mfuko wa Abbott katika makao ya Taifa ya kulelea watoto Kikombo Jijini Dodoma.
Rais wa Mfuko wa Abbott Melissa Brotz akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa mabinti washonaji wa nguo kutoka katika karakana ya Makao ya Taifa ya kulea watoto Kikombo wakati walipotembelea makao hayo, Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Huduma za uhandisi akishiriki zoezi la upandaji Mti wakati wa Ziara ya shirika hilo lilipotembelea makao ya Taifa ya kulea watoto ya Kikombo Jijini Dodoma.
Kikundi cha Ngoma ya Watoto kutoka Makao ya Taifa ya kulea Watoto Kikombo, kikitoa burudani wakati wa kuhitimishwa kwa ziara ya bodi ya Mfuko wa Abbott ilipotembelea makao hayo, Jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na mfuko wa Abbott (Abbott Fund) wa nchini Marekani imekubaliana kuimarisha Makao ya kulea watoto mkoa wa Dar es Salaam hasa upande wa maktaba.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya rais wa mfuko huo Melisa Brotz yenye lengo la kujionea maendeleo ya shughuli walizoshirikiana na Serikali kupitia Wizara zilivyotekelezwa hususani makao ya Taifa ya watoto Kikombo jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju ameushukuru mfuko huo kwa ushirikiano na Serikali katika kuboresha miundombinu na hali ya makazi ya taifa ya kulea Watoto.

"Mfuko wa Abbott umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Tanzania, Wizara tumejipanga kuhakikisha inafanikiwa, nawaomba kuendelea kufadhili makao haya ili kupunguza changamoto ya usafirishaji kwa kuwezesha upatikanaji wa Basi pia kuungana na Serikali katika kuwezesha ujenzi wa Makao ya Watoto ya Jijini Dar es salam" amesema Mpanju.

Kwa upande wake Melisa Brotz amesema amefurahishwa na Stadi za kazi, Elimu ya ufundi stadi, Mtindo wa elimu na Maisha wa makao hayo na kuahidi kuwezesha kuongeza miradi na kufadhili ujenzi wa kituo cha ustawi wa jamii cha Dar es salam. Pia kuhakikisha upatikanaji wa vitabu vya Kiingereza na Kiswahili kwa maktaba ya makao ya kukea watoto jijini Dar es salaam.

Makao ya Taifa ya kulea Watoto Kikombo ni mpango wa kusaidia programu za watoto wanaoishi katika mazingira magumu Tanzania Bara kwa ushirikiano na mfuko wa Abbott. Makao hayo yana maeneo ya shamba, karakana, hosteli za Watoto, madarasa na makataba, ambayo mfuko umekua ukiyaimarisha.
Share:

WAKALA WA CRDB SHINYANGA MJINI AKABIDHIWA ZAWADI YA PIKIPIKI KWA KUKIMBIZA SANA MIAMALA


Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akikabidhi nyaraka za pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB imetoa zawadi ya Pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura anayefanya shughuli za Uwakala Ngokolo Mitumbani Mjini Shinyanga kutokana na kuwahudumia wateja wengi zaidi.

Akizungumza leo Jumanne Julai 18,2023 wakati wa kukabidhi Pikipiki hiyo, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amesema katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa huduma ya CRDB Wakala, benki ya CRDB imetenga zawadi mbalimbali ikiwemo kamisheni za fedha, bodaboda, bajaji na gari kwa ajili ya kuwazawadia mawakala wake watakaowahudumia wateja wengi zaidi kwa kipindi cha miezi minne mfululizo ijayo.


"Benki ya CRDB inampongeza sana Mr & Mrs Charles Zacharia Wambura kwa kuwa mfano bora wa Mawakala wanaofanya kazi vizuri. Bwana Charles Zacharia Wambura amekimbiza sana miamala. Tunakupongeza sana kwa ushindi huu",amesema Wagana.


Ameeleza kuwa kutokana na umuhimu wa Mawakala, benki ya CRDB imekuja na kampeni ya kuwazawadia mawakala watakaotoa huduma kwa wateja wengi zaidi ambapo Kampeni hiyo imeanza mwezi Aprili na itafanyika kwa muda wa miezi mitano na zawadi nyingi zitatolewa ambazo ni Kamisheni/bonasi, pikipiki 40, Bajaji 5 na mshindi wa jumla atapata Gari jipya aina ya Toyota Alphard.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

"Lengo la kutoa zawadi hizi ni kuwapa Motisha Mawakala wetu, sisi tunaamini Mawakala ni sehemu ya Benki ya CRDB kwa sababu wanafanya mambo yote yanayofanyika ndani ya Benki ya CRDB ikiwemo kuweka fedha, kutoa fedha,kufungua akaunti, malipo ya serikali na hivi karibuni tumeongeza jukumu jingine la kukata bima",amesema Wagana.

"Kwa hiyo Mawakala wa CRDB wanatusaidia sana na wanafanya kazi kubwa ndiyo maana tukiwa tunaadhimisha miaka 10 ya CRDB Wakala tumeona tusiwaache hivi hivi tukaja na hizi zawadi ili iwe chachu kwa Wakala wetu wanaokimbiza miamala",ameongeza Meneja huyo wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Tabora, Geita na Kigoma.


Kwa upande wake, Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa amesema huduma ya CRDB Wakala iliyoanzishwa mwaka 2013 na kutokana na umuhimu wa Mawakala ndiyo maana wameanzisha Kampeni hiyo ili kuwashukuru na kutambua mchango wao mkubwa ambao umefanikisha kuifikisha CRDB wakala kwa miaka 10.


"CRDB Wakala imekuwa ikikua mwaka hadi mwaka, hivyo tukiwa tunatimiza miaka 10 tumeona Mawakala wetu tusiwaache hivi hivi ndiyo maana tukasema Miaka 10 pamoja hatukuachi hivi hivi. Tunaangalia Wakala gani amefanya miamala mingi lakini pia amefungua akaunti nyingi. Mshindi wetu huyu wa leo Charles Zacharia Wambura aliyepata zawadi ya pikipiki siyo tu ameshinda Shinyanga bali ameshinda kati ya mikoa minne ya Shinyanga, Tabora, Geita na Kigoma. Tunampa pikipiki hii mpya, kadi ina jina lake na hatumpangii matumizi",amesema Kidagaa.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney ametumia fursa kuwasihi Mawakala wa Benki ya CRDB kuchangamkia Kampeni ya 10 na kitu kwa kufungua akaunti nyingi na kufanya miamala mingi zaidi.

"CRDB tunasema Mchongo kama wote kwa Wakala wetu, Mchongo upo Mtaani kwako! .Tuungane kusherehekea miaka 10 ya huduma ya CRDB Wakala kwa kushiriki promosheni hii ya 10 na kitu. Wakala unachotakiwa kufanya ni kukimbiza miamala uwezavyo ya wateja wako, walipie bili, wakatie Bima na kuwafungulia akaunti za Al-Barakah na akaunti nyingine ujiongezee nafasi ya kushinda Kamisheni hadi zaidi ya mara 3, Gari jipya aina ya Toyota Alphard, Bajaji 5, bodaboda 40",amesema Mneney.


Akipokea zawadi ya Pikipiki Wakala wa Benki ya Charles Zacharia Wambura akiwa na mkewe wanayeshirikiana naye kufanya kazi ya Uwakala Mary Festo Bukumba ameishukuru Benki ya CRDB kwa kutambua mchango mkubwa wanaotoa kwenye benki hiyo huku wakiahidi kuendelea kukimbiza miamala zaidi na kufungua akaunti nyingi zaidi.


Kwa upande wake, Wakala wa Benki ya CRDB Grace Joliga amempongeza Wakala huyo kwa ushindi akisema " Tulikuwa tunajua ni Stori tu au CRDB wanatoa zawadi kwa kujuana, lakini kumbe ni kweli wanatoa zawadi kwenye kwa wanaofanya vizuri, hii ni motisha nzuri na sisi wengine tunajitahidi kuhakikisha tunaongeza kasi".

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga leo Jumanne Julai 18,2023 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Muonekano wa pikipiki iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga leo Jumanne Julai 18,2023 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga. 
Muonekano wa pikipiki iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga leo Jumanne Julai 18,2023 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga. 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga
Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga
Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akikabidhi nyaraka za pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akifuatiwa na Mke wa Charles Zacharia Wambura (Mary Festo Bukumba). Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akikabidhi funguo za pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akifuatiwa na Mke wa Charles Zacharia Wambura (Mary Festo Bukumba). Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney
Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura na  mkewe Mary Festo Bukumba wakiwa wamepanda pikipiki waliyopatiwa zawadi na Benki ya CRDB kwa kukimbiza sana miamala na kufungua akaunti nyingi. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney  akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana
Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura  akitoa neno la shukrani baada kukabidhiwa pikipiki na Benki ya CRDB, kulia ni mkewe Mary Festo Bukumba. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney  akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana
Mke wa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura  bi. Mary Festo Bukumba akitoa neno la shukrani kwa benki ya CRDB
Wakala wa Benki ya CRDB Grace Joliga akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB, Mawakala wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura
Wafanyakazi wa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura wakipiga picha ya kumbukumbu
Mke wa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura  bi. Mary Festo Bukumba akiwa amepanda kwenye pikipiki iliyotolewa na Benki ya CRDB

Picha  zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Share:

JINSI YA KUCHEZA MCHEZO WA KASINO-HOT SHOTS MINES


Hii ni kwa wapenzi wa michezo isiyo ya kasino kama vile kubashiri mubashara na kucheza bahati nasibu, ni mchezo wa Hot Shots Mines. Huu ni mchezo wa mkakati wa awamu ambao ni mzuri kwa wapenzi wa soka na michezo ya kasino ya mtandaoni, mchezo huu wa Hot Shot Mines unachezwa kwenye uwanja wa soka katika msitu wa kuvutia.

 

Hot Shot Mines una vyumba 25, kazi yako ni kuvifungua moja baada ya jingine. Ogopa sana kadi nyekundu, hufanya kutomaliza zamu yako. Kadri unavyofungua masanduku zaidi, ndivyo unavyopata zawadi/ushindi zaidi.

 

Hatua ya Kucheza Hot Shots Mines Kasino ya Mtandaoni.

 

Unapoucheza huu mchezo wa kasino ya mtandaoni ya Meridianbet unapaswa kuchagua kadi moja, mbili, tatu, tano, saba, kumi, au kumi na tano nyekundu. Idadi ya Kadi nyekundu unazozidi kuchagua, ndivyo dau la ushindi linavyozidi kuongezeka na malipo kuwa makubwa zaidi.

 

Ushindi Na Malipo

Hot Shots Mines kutoka kasino ya mtandaoni ya Meridianbet una matoleo tofauti kulingana na idadi ya kadi nyekundu utakazo chagua, Malipo kwa kila toleo la mchezo ni kama ifuatavyo:

 

Toleo la Kadi moja nyekundu:
Kwa toleo hili la uwepo wa kadi moja nyekundu uwanjani utapata;
Mara 5.9x ya dau lako ukicheza vyumba 21,
Mara 7.85x ya dau lako ukicheza vyumba 22,
Mara 11.8x ya dau lako ukicheza vyumba 23,
Mara 23.5x ya dau lako ukicheza vyumba 24,

Toleo la Kadi mbili nyekundu:
Kwa toleo hili la uwepo wa kadi mbili nyekundu uwanjani utapata;
Mara 28.2x ya dau lako ukicheza vyumba 21,
Mara 47x ya dau lako ukicheza vyumba 22,
Mara 94x ya dau lako ukicheza vyumba 23,
Mara 282x ya dau lako ukicheza vyumba 24.

Toleo la Kadi tatu nyekundu:
Kwa toleo hili la uwepo wa kadi tatu nyekundu uwanjani utapata;
Mara 38.7x ya dau lako ukicheza vyumba 17,
Mara 62x ya dau lako ukicheza vyumba 18,
Mara 109x ya dau lako ukicheza vyumba 19,
Mara 217x ya dau lako ukicheza vyumba 20.

Toleo la Kadi tano nyekundu:

 

Kwa toleo hili la uwepo wa kadi tano nyekundu uwanjani utapata;
Mara 39x ya dau lako ukicheza vyumba 12,
Mara 63.5x ya dau lako ukicheza vyumba 13,
Mara 109x ya dau lako ukicheza vyumba 14,
Mara 200x ya dau lako ukicheza vyumba 15.

Toleo la Kadi saba nyekundu:
Kwa toleo hili la uwepo wa kadi saba nyekundu uwanjani utapata;
Mara 39.5x ya dau lako ukicheza vyumba 09,
Mara 70.5x ya dau lako ukicheza vyumba 10,
Mara 132x ya dau lako ukicheza vyumba 11,
Mara265x ya dau lako ukicheza vyumba 12.

Toleo la Kadi kumi nyekundu:
Kwa toleo hili la uwepo wa kadi kumi nyekundu uwanjani utapata;
Mara 16.7x ya dau lako ukicheza vyumba 05,
Mara 33.3x ya dau lako ukicheza vyumba 06,
Mara 70.5x ya dau lako ukicheza vyumba 07,
Mara 158x ya dau lako ukicheza vyumba 08.

 

Toleo la kumi na tano nyekundu:
Kwa toleo hili la uwepo wa kadi kumi na tano nyekundu uwanjani utapata;
Mara 18.1x ya dau lako ukicheza vyumba 03,
Mara 57x ya dau lako ukicheza vyumba 04,
Mara 200x ya dau lako ukicheza vyumba 05.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.

 


Share:

KUPITIA UCHUMI WA BLUU WANANCHI WANAWEZE KUJIONGEZA KIPATO

MBUNGE wa Jimbo Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Taasisi ya Tanga Yetu kupitia ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation katika Jiji la Tanga kushoto ni Mwakilishi wa Botnar Tanzania Dkt. Hassan Mshinda
MBUNGE wa Jimbo Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Taasisi ya Tanga Yetu kupitia ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation katika Jiji la Tanga kushoto ni Mwakilishi wa Botnar Tanzania Dkt. Hassan Mshinda



MKURUGENZI wa Kampuni ya V.J Mistry& Co.Ltd inayojenga Forodhani ya Tanga Jitesh Jethwa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa ziara hiyo
MKURUGENZI wa Kampuni ya V.J Mistry& Co.Ltd inayojenga Forodhani ya Tanga Jitesh Jethwa kulia  akimuonyesha maeneo mbalimbali  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa ziara hiyo


Na Oscar Assenga, TANGA


MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema kuwa kupitia fursa ya uchumi wa bluu wananchi wa Jiji la Tanga wataweza kujiongezea fursa ya shughuli za kiuchumi ikiwemo kujiongezea kipato kupitia fursa za ufugaji na kilimo kupitia bahari.

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya aliyasema hayo wakati alipotembelea miradi inayotekelezwa na Taasisi ya Tanga Yetu kupitia ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation katika Jiji la Tanga huku akiwashukuru kwa kukubali ombi lake kutekelezwa miradi hiyo ambayo itasaidia kukuza uchumi wa bluu.

Miradi hiyo ni ya uvuvi, kilimo cha mwani, jongoo bahari na unenepeshaji wa kaa pamoja na ufugaji wa samaki, kuku na kilimo cha mbogamboga katika kata za Tongoni, masiwani, Tangasisi, Usagara na Central.

Aidha Botnar foundation pia wamefadhili miradi ya Afya, Elimu na kujenga Forodhani ya Tanga.

Katika miradi hiyo jumla ya fedha zilizotumika hadi sasa ni kiasi cha shilingi bilioni 5.65 zimetumika ambayo kwa asilimia kubwa zimewasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

Alisema kutokana na umuhimu wa uchumi wa bluu katika kukuza uchumi wa wananachi hivyo Jiji hilo limejipanga kuwa kinara katika uzalishaji wa majongo bahari, unenepeshaji wa kaa pamoja na kilimo cha mwani kwa kutumia fursa ya bahari iliyopo kwenye Ukanda wa Pwani.

Alisema kwa sababu mkoa wa Tanga una eneo kubwa la bahari na tayari mafanikio yamekwisha kuyaona hivyo tumejipanga kuongeza uzalishaji Ili tuweze kuwa vinara wa kutumia fursa za uchumi wa buluu Kwa maendeleo ya watu wetu sambamba na nchi kupata mapato yake”amesema Waziri Ummy.

Alisema kutokana na uwepo wa fursa wanapaswa kulikumbatia zao la mwani kwa sababu ni zao ambalo kilimo chake sio kigumu zaidi na faida yake ni kubwa.

“Mimi kama Mbunge wa Jimbo la Tanga nitashirikiana na wadau Botnar Foundation kuendeleza kilimo cha mwani kikubwa tuwape elimu na ujuzi wananchi hususani wanawake ikiwemo kuwapa vitendea kazi ambayo vitasaidiaa kufanya vizuri katika kilimo cha Mwani na kutafuta masoko”Alisema Mbunge Ummy.

Aidha alisema kwamba amejipa kazi maalumu ya kutangaza mazao makubwa matatu Tanga mjini kutokana na kwamba wanataka mwambao wa Tanga uwe maarufu kwa kuzalisha mazao ya Mwani,Majongoo Bahari na kunenepesha kaa.

Alisema kwamba hayo mazao matatu amevutiwa nayo na kama watawekeza kwenye uchumi wa bluu utasaidia watu wengi sana kupata kipato na hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Lakini niwahaidi kwamba nitafatuta kiwanda cha mwani ili wakiweke kwenye Jiji la Tanga hivyo niwahamasishe watu wengi walime mwani na nimewaomba botnar watusaidie hivyo wananchi tusikate tamaa mapema mwani utalipa hivyo tujitume kulima”Alisema Mbunge Ummy

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwakilishi wa Botnar Tanzania Dkt. Hassan Mshinda amemuhakikishia Mbunge Ummy kuwa Botnar itaendelea kushirikiana nae na Halmashauri ya Jiji la Tanga katika kutatua kero za maendeleo kwa wakazi wa Tanga Mjini hususan vijana na watoto.


Share:

SERIKALI YATEKELEZA MIRADI KWA KISHINDO CHIKUYU-MANYONI



Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mheshimiwa Dkt. Pius Chaya ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Wilaya kupitia mwa mtendaji kata ya Chikuyu kuboresha miundombinu ya barabara ya kuingilia katika mnada wa Mwiboo kutokana na hali yake kuwa hairidhishi.


Dkt. Chaya ameyasema hayo Julai 17 , 2023 wakati alipofanya ziara katika kata ya Chikuyu vijiji vya Mwiboo, Chilejeho, Mtiwe na Chikuyu iliyokuwa na dhima ya kufanya mikutano ya hadhara, kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi hao.


"Hii barabara haipo chini ya TARURA inatakiwa ikarabatiwe na Halmashauri, Mtendaji wa kata kila mnada unakuja kukusanya Mapato lakini hamuikumbuki ili hali ndiyo inayowapa kipato, wakati wa mvua magari hayaingii hapa, Nakuagiza kwa Mkurugenzi wako wa Wilaya tunampa mpaka mwezi wa kumi mwaka huu atume timu yake ifanye tathmini na kutenga fedha kwaajili ya kuweka vifusi kwenye hiyo barabara"  Dkt. Chaya.


Akiwa katika mwendelezo wa ziara yake suala la Skimu za umwagiliaji ikaonekana kuwa changamoto kwa wananchi hao ndipo Mbunge huyo akatoa siku saba kwa Mtendaji wa kata ya Chikuyu awe ametoa majina ya wakulima wenye mashamba ya skimu.

Kuhusu mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Ameagiza viongozi wanaohusika kutekeleza mpango huo kuhakikisha wanaandikisha majina ya walengwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ili kuchukua hatua zitakazowanufaisha walengwa hao.


Aidha ametoa rai kwa walimu na uongozi wa shule kuwa ni marufuku kumtoa mwanafunzi darasani kama mzazi hajatoa mchango na ikiwezekana iundwe kamati ya wazazi ya kufuatilia michango hiyo na siyo waalimu kwani itakuwa ni njia rahisi ya kuwafikia wazazi hao.


"Kuanzia leo ni marufuku kumrudisha mtoto nyumbani kama hajatoa mchango" ,Dkt. Chaya.


Dkt. Chaya katika mikutano yake hakuacha kuishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji w miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Jimbo la Manyoni Mashariki.


Hata hivyo Mbunge huyo ataendelea ataendelea na Ziara mpaka atakapomaliza kutembelea kata zote zote 19 zilizomo Jimboni humo ambayo itaambatana na Mikutano ya hadhara.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger