Saturday, 15 July 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 15,2023














Share:

Friday, 14 July 2023

TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA AGRF 2023

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu Mkutano wa AGRF 2023.
Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Zaidi ya washiriki 3000 wanaojihusisha na mnyororo wa thamani wa Mifugo na chakula wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa sekta ya Mifugo na uvuvi (AGRF-2023) ifikapo September 5-8,2023 Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Julai 14,2023Jijini hapa,Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdalla Ulega amesema Tanzania inaenda kuwa mwenyeji wa mkutano huo hivyo Ushiriki wa wadau wa kisekta watanufaika na fursa zitakazopatikana ikiwemo kukutana na wafanyabiasha mashuhuri na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali hali inayotazamwa kufungua milango ya uwekezaji na mashirikiano kibiashara.

"Lengo ni kuwezesha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu kuingia kwenye ufugaji na uvuvi na kuwa na uwezo wa kusafirisha Mifugo hai nje ya nchi na kuitangaza nchi,ili kurahisisha hayo Serikali inaendelea kuboresha utaratibu wa upatikanaji wa vibali vya kusafirisha Mifugo na mazao yake nje ili kuleta unafuu kwa wafugaji,"amesisitiza

Waziri Ulega amesema mkutano huo utatoa fursa ya kuongeza uzalilishaji na kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kuuza ziada ya mazao na kufafanua kuwa kwa sasa biashara ya nyama imeshamiri na kuuza tani 12,000 kwa mwaka sawa na Dola za marekani milioni 51 ambapo kabla ya hapo Tanzania iliuza tani 1600 pekee .

"Lazima tufuge Kwa malengo,wafugaji wanapaswa kuelewa kuna kuishi na kuku na kufanya biashara ya kuku, tuingie kwenye kufuga mifugo biashara na sio kuiishi na Mifugo kama wengi wanavyofanya huko vijijini,"amesema na kuongeza;

"Sisi kama Serikali tulianzisha mkakati wa mashamba darasa Kwa halmashauri 44 zenye Mifugo Kwa kuanzisha mashamba zaidi ya 100 Ili kuwaonesha wafugaji kuwa inawezekana kulima,kuvuna na kuhifadhi Kwa faida zaidi,hii itaenda sambamba na urasilimishaji wa Kilimo cha majani na uhifadhi wa ardhi,pomoja na kuwa na Ranchi za asili,"amesisitiza

Waziri huyo pia ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wadau kuandaa taarifa za Kampuni zao kwa ufasaha ili iwe rahisi kujitangaza na kuvutia wawekezaji,wafadhili na kuongeza wigo wa biashara zao.
Share:

KAMPUNI YA JAMBO YAKABIDHI JEZI KWA TIMU YA SOKA YA WANAWAKE 'MWAMVA FDC QUEENS' MICHUANO YA WRCL JIJINI MWANZA

Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media (kulia) akikabidhi jezi kwa ajili ya Timu ya Soka ya Wanawake Mwamva FDC Queens. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Timu ya Mwamva FDC Queens Mwalimu Aisa Mariki akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo na Nahodha wa Timu ya Mwamva FDC Queens, Mwajab Athuman.

Na Elizabeth Hassan & Kadama Malunde - Shinyanga
Kampuni ya Jambo Food Products imekabidhi Jezi seti mbili zenye thamani ya shilingi 500,000/= kwa Timu ya Soka ya Wanawake Mwamva FDC Queens ya Mjini Kahama mkoani Shinyanga ambayo inashiriki katika Ligi ya Mabingwa wa mikoa kwa wanawake (Women Region Competition League- WRCL)  jijini Mwanza.


Hafla hiyo imefanyika leo Julai 14, 2023 katika kiwanda cha Kampuni ya Jambo Food Products mjini Shinyanga ambapo mkurugenzi wa Timu ya Mabingwa wa Mkoa wa Shinyanga ya Wanawake 2023 'Mwamva FDC Queens' Mwalimu Aisa Mariki amesema mchango huo wa jezi ni motisha kubwa katika mashindano hayo ya ligi ya mabingwa wa mikoa yatakayoanza kutimua vumbi Julai 16, 2023 katika viwanja vya Alliance School Jijini Mwanza.

"Tunaishukuru sana Kampuni Jambo Food Products kwa kutushika mkono kwa kutupatia jezi hizi, Kampuni hii imekuwa ikitusaidia mara kwa mara kwa vitu mbalimbali na imekuwa mdau mkubwa wa michezo",amesema Mariki.


Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo ameishukuru Kampuni ya Jambo Food Products imekuwa mdau mkubwa sana katika kusaidia sekta ya michezo katika mkoa wa Shinyanga na kwamba msaada huo utaleta hamasa kwa wachezaji hao wa timu ya wanawake mkoani Shinyanga.


Kwa upande wake Nahodha wa Timu ya Mwamva FDC Queens, Mwajab Athuman amesema watapambana ili kuendelea kuwatia moyo wadau wa soka ikiwemo Kampuni ya Jambo Food Products kwa kuhakikisha timu wanaipandisha daraja.


Akikabidhi jezi hizo, Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media amesema Kampuni hiyo ilipokea ombi kutoka Chama cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) kuunga mkono timu hiyo hivyo kutokana na utamaduni wa Kampuni hiyo kusaidia jamii inayowazunguka ndiyo maana wametoa jezi hizo ili timu hiyo ikazitumie kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa.
Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media (kulia) akikabidhi jezi kwa ajili ya Timu ya Soka ya Wanawake Mwamva FDC Queens. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Timu ya Mwamva FDC Queens Mwalimu Aisa Mariki akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo na Nahodha wa Timu ya Mwamva FDC Queens, Mwajab Athuman.
Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media (wa pili kulia) akikabidhi jezi kwa ajili ya Timu ya Soka ya Wanawake Mwamva FDC Queens.
Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media (wa pili kulia) akikabidhi jezi kwa ajili ya Timu ya Soka ya Wanawake Mwamva FDC Queens.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo akizungumza wakati Kampuni ya Jambo Food Products ikikabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens
Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo akizungumza wakati Kampuni ya Jambo Food Products ikikabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens
Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media  akizungumza wakati Kampuni ya Jambo Food Products ikikabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens

Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Chrispin Kakwaya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Michezo Jambo Media akizungumza wakati Kampuni ya Jambo Food Products ikikabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens
Mkurugenzi wa Timu ya Mwamva FDC Queens Mwalimu Aisa Mariki akizungumza wakati Kampuni ya Jambo Food Products ikikabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens
Nahodha wa Timu ya Mwamva FDC Queens, Mwajab Athuman akizungumza wakati Kampuni ya Jambo Food Products ikikabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens
Picha ya kumbukumbu baada ya Kampuni ya Jambo Food Products kukabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens
Picha ya kumbukumbu baada ya Kampuni ya Jambo Food Products kukabidhi jezi kwa Timu ya Mwamva FDC Queens
Share:

WIZARA YA MADINI - ASANTENI SANA KWA KUSHIRIKI PAMOJA MAONESHO SABASABA 2023


Share:

MWENYEKITI MWENZA WA BARAZA LA MAWAZIRI AONGOZA MKUTANO WA PILI WA KAMISHENI YA BONDE LA MTO SONGWE


Waziri wa Maji Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Mawaziri Bonde la Mto Songwe Mhe. Jumaa Aweso ameongoza Mkutano wa pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe.

Waziri Aweso ambaye ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyeji ameshirikiana na Mwenyekiti mwenza wa Kamisheni kutoka Malawi Waziri wa Maji Mhe. Abida Sidik Mia ambapo kwa pamoja wameongoza mkutano huu wa siku moja ukijadili maendeleo ya pamoja ya ushirikiano katika kamisheni ya Bonde la Mto Songwe , kujadili na kupitisha makadirio ya Bajeti, kujadili maendeleo na undeshaji wa Kamisheni, na na dhima kuu na lengo maalum la mkutano huu ambalo ni maandalizi ya ujenzi wa bwawa la kuhifadhi Maji, Mto Songwe kwaajili ya kuzuia mafuriko, matumizi ya Binadamu, shughuli za kilimo, pamoja na kuzalisha Nishati ya Umeme ikiwa wajumbe wamekubaliana mchakato wa kutafuta fedha na hatua za ujenzi ziendelee.

Mkutano huu umewajumuisha Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe kutoka Malawi na Tanzania wanaotokana na Sekta 5 kwa nchi zote mbili ikiwa ni pamoja na Maji, Nishati, Ardhi, TAMISEMI, na Kilimo. Mkutano umeudhuliwa na Waziri wa Ardhi na Makazi Mhe Angelina Mabula, N/Waziri wa TAMISEMI Mhe Deogratius Ndejembi, N/Waziri wa Kilimo Mhe Anthony Mavunde na N/Waziri wa Nishati Mhe Stephen Byabato.
Kutoka Malawi ni Mhe. Matola Ibrahim, Mhe. Oweni Chumanika, na Mhe. Deus Gumba.
Share:

NSSF YATENGENEZA FAIDA YA ZAIDI YA TRILIONI 1.01 MWAKA 2021/22 KWA HESABU ZILIZOKAGULIWA


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba

*Yasema mafanikio hayo yamechangiwa na Serikali ya awamu ya sita kuvutia wawekezaji

Na MWANDISHI WETU

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umepata faida ya zaidi ya shilingi trilioni 1.01, kulingana na hesabu zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika mwaka wa 2021/22, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema.


Amesema sambamba na hilo pia mapato yatokanayo na uwekezaji nayo yameongezeka na kufikia shilingi bilioni 745. “Hii haijawahi kutokea katika historia ya NSSF” amebainisha Mkurugenzi Mkuu wakati akitoa tathmini yake baada ya kupokea taarifa ya watendaji wa Mfuko walioshiriki kuhudumia wanachama na wananchi kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofikia kilele Julai 13, 2023.

Mshomba ametaja sababu za mafanikio hayo kuwa ni pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye mara tu baada ya kuingia madarakani alikuja na mpango  wa “Kuifungua Nchi” akilenga kuwaalika wawekezaji kuja kuwekeza nchini lakini pia kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania kupitia filamu ya “The Royal Tour”.

“Kichocheo kikubwa ni Mheshimiwa Rais alivyoweza kuwavuta wawekezaji, kumekuwa na ongezeko kubwa la waajiri na waajiriwa, suala zima la uchangiaji limeongezeka, vipato vya wafanyakazi vimeongezeka na haya yote yamechangia kuongeza michango na kufanya kipato cha Mfuko kutokana na uwekezaji kuongezeka pia.” alifafanua  Mshomba

Alisema sababu nyingine ni juhudi kubwa zilizowekwa na Mfuko katika kuboresha mifumo ya TEHAMA ambayo imesaidia kuboresha utoaji wa huduma.

“Kulingana na Mpango wetu wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao unaishia Juni 2026, thamani ya Mfuko itafikia zaidi ya trilioni 11.5, na yote haya yanatokana na msukumo wa kuongeza waajiri na waajiriwa wanaochangia katika Mfuko lakini pia kazi nzuri inayofanywa na Mfuko.” alifafanua.

Kwa sasa thamani ya Mfuko wa NSSF ni trilioni 7.1, hivyo Mkurugenzi Mkuu  amewahimiza  Watanzania hususan kutoka sekta binafsi  kujiunga kwa wingi ili kujenga maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Aidha, Mshomba amesema NSSF imepewa jukumu la kushughulika na sekta isiyo rasmi.


“Tunakamilisha taratibu za mwisho na tunaamini tukiweza kuwa na uchangiaji katika sekta isiyo rasmi, basi NSSF itazidi kupaa zaidi na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi hii.” alisema

Alisema idadi kubwa ya Watanzania wako katika sekta isiyo rasmi na wakiweza kujumuishwa kwenye mpango huo wa taifa litakuwa limefanikiwa kuondoa umaskini nchini.

“Kama ninavyosema siku zote hifadhi ya jamii iko kwa ajili ya kuwahudumia wananchama hasa kwa lengo la kuwaondolea umaskini pale wanapokoma kufanya kazi.” Alifafanua.

Kuhusu ushiriki wa NSSF katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Bw. Mshomba amesema wanachama zaidi ya 2,400 wametembelea na kuhudumiwa katika banda hilo kwa siku zote za Maonesho.

“Kumekuwa na mabadilio chanya ukilinganisha na mwaka jana, Wanachama wetu wamehudumiwa kwa kupatiwa elimu, usajili wa Wanachama, umuhimu wa kuwasilisha Michango kwa wakati na kuondoa kero mwanachama anapostaafu, elimu katika masuala ya uwekezaji, Mafao yatolewayo na Mfuko ambayo yanafikia saba lakini pia masuala ya Uwekezaji.” alifafanua.

Kuhusu Uwekezaji,  Mshomba amesema wamebaini kuwa watu wengi wamevutiwa na eneo hilo.

“Kuna maeneo ambayo wanachama wetu wanaweza kufaidika moja kwa moja tunajenga nyumba na kuuza, au kupangisha kwa wateja.Hivyo aliendelea kwa kutoa rai kwa Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za NSSF.



Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba ametembelea banda namba 13 la ushirikiano baina ya NSSF na PSSSF kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko na kufurahishwa na huduma zote ambazo zilikuwa zinatolewa  katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ yaliyofungwa na Mhe. Dkt. Husaein Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, tarehe 13 Julai2023, katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akizungumza na mwanachama aliyetembelea katika banda la Mfuko, ambapo alimueleza kuwa pamoja na kuwa mwanachama wa sekta binafsi lakini bado anaweza kuchangia kwa hiari kupitia sekta isiyo rasmi kwa kuwa ina manufaa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akizungumza jambo na mwanachama William Matee, aliyejiunga na huduma ya NSSF Taarifa Mobile App, ambapo sasa anaweza kutazama michango yake bila kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.



Matukio katika picha
Share:

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA 47 YA SABASABA

Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka Kidedea kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) Jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa tuzo na  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ally  Mwinyi ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho hayo. 


Akielezea Tuzo hiyo ya Banda bora na mashuhuri upande wa Wizara na Taasisi, Mwenyekiti wa Maonesho ya Saba Saba Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Filex John, amesema ni Matokeo chanya ya Uongozi mzuri wa Wizara hiyo pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Watumishi wa Wizara hiyo ya utoaji huduma kwa Kiwango cha juu kwa wote waliofika kwenye Banda hilo. 

Bw. John amewashukuru wadau  na wananchi  wote waliojitokeza kupata huduma kwenye Banda hilo la Maliasili, pamoja na ushirikiano waliotoa katika kuhakikisha Maonesho hayo yanakuwa na Mafanikio Makubwa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger