Saturday, 20 May 2023

KAMATI YA UTEKELEZAJI WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI YABAINI MADUDU UJENZI WA MADARASA NA VYOO SHULE YA MSINGI MSUFINI


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini imeeleza kusikitishwa na matofali yanayotumika kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya Msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga kwamba ziko chini ya viwango.

Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ikitembelea na kukagua ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule hiyo leo Jumamosi Mei 2023, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Fue Mrindoko amesema kamati hiyo imebaini matofali hayo hayana kiwango kwani mengine wameyaona yakiwa na matope/udongo unaopukutika.


"Matofali haya hayana kabisa kiwango na ujenzi unaendelea sasa hatuelewi next (baadaye) itakuwaje katika madarasa na vyoo hivi vinavyojengwa...si yatabomoka kabla ujenzi haujaisha??", amesema Mrindoko.


"Kutokana na matofali haya kuwa chini ya kiwango tunaona kabisa tutajenga mara mbili...Niwaombe sana wanaohusika wafahamishwe haraka, haiwezekani matofali yapo chini ya kiwango namna hii halafu ujenzi unaendelea...Hayana kiwango kabisa, pembeni kuna saruji ndani kuna udongo unamong'onyoka kwa vidole...Kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini imeona Matofali haya haya kiwango kabisa, yaondolewe hatuwezi kujenga mara mbili", ameongeza Mrindoko.

Mrindoko amewashukuru walimu wa shule hiyo kuona mapungufu ya matofali hao na kutoa taarifa mapema ili kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza hapo baadaye.


“Tumesikitishwa kuona matofali haya yanayotumika yapo chini ya kiwango. Tunaziomba mamlaka zinazohusika zije kukagua ujenzi huu na kuangalia namna ya kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. CCM haiwezi kukubali fedha zinazotolewa na serikali zitumike vibaya”,ameongeza Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi.


Akisoma taarifa ya ujenzi huo Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Msufini kata ya Ndala , Godfrey Oscar Jebele amesema madarasa hayo matatu na matundu matatu ya vyoo yanajengwa kupitia mradi wa BOOST na umeanza Mei 15,2023 ukiwa na gharama ya shilingi 84,600,000 (Milioni 84.6).

“Changamoto iliyopo katika ujenzi huu ni kwamba mafundi wanalalamika kuwa tofali zinazotumika baadhi zinakuwa na changamoto kwani zinapukutika”,amesema Jebele.


Diwani wa kata ya Ndala Zamda Shaban amesema haiwezekani mradi huo uharibiwe hivyo atahakikisha changamoto hiyo inatatuliwa.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wakiangalia matofali yanayotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akiangalia matofali yanayotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Matofali yanayotumika katika ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Matofali yanayotumika katika ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Matofali yanayotumika katika ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wakikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wakikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga ukiendelea
Diwani wa kata ya Ndala Zamda Shaban  akizungumza wakati Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini ikifanya ziara kwenye kata hiyo
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza katika kata ya Ndala
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza katika kata ya Ndala
Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Msufini kata ya Ndala , Godfrey Oscar Jebele (kulia) akikabidhi taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule hiyo kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko 
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Share:

SERIKALI YAJIPANGA KUTOA ELIMU BORA ZAIDI ITAKAYOSAIDIA VIJANA KUSONGA MBELE



Na Woinde Shizza ,ARUSHA

Serikali imejipanga kutoa elimu bora zaidi na ambayo itawasaidia vijana kusonga mbele lengo likiwa kuhakikisha kuwa kile kinachofundishwa kwa wanafunzi kinaendana na wazalishaji wa bidhaa pamoja na watoaji wa huduma, ili vijana wanapotoka vyuoni elimu waliyopata iweze kuwasaidia.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ambayo inasimamia wizara ya elimu Mh. Husna Sekiboko akiongea katika uzinduzi rasmi wa maonesho ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, yaliyoandaliwa na NACTVET

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati wa uzinduzi rasmi wa maonesho ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, yaliyoandaliwa na NACTVET, ambapo alisema kuwa serikali imejipanga kuwasaidia vijana kupata elimu bora ya Ujuzi ambayo itawasaidia kujiendeleza kiuchumi binafsi na Taifa kwa ujumla.


Aidha alisema kwa kutimiza hilo serikali imejipaga kujenga vyuo vya veta 64 katika wilaya na Chuo kimoja kikubwa cha Veta katika mkoa ,wanaongeza uwezo mkubwa sana wa kufundisha vijana katika vyuo hivyo yote hayo not kuhakikisha vijana wanapotoka shuleni elimu aliyoipata ikamsaidie huko mtaani.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiongea mara baada ya kuzinduzi rasmi wa maonesho ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, yaliyoandaliwa na NACTVET,

Kwa upande wa mwenyekiti wa NACTIVET Prof. John Kondoro, alisema kuwa sasa hivi Kama serikali inayovyofanya kupitia mitaala pamoja na sera ya mafunzo ,wao wameanza mapema lakini wanaunga mkono serikali kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaopita katika vyuo vyao wanakuwa tayari ni mahiri lakini pia wanaonyesha nini wanafanya kwa kutumia mikono yao ,ni ujuzi gani walio nao ,ni sekta gani wanapokwenda na wanakubaliwaje na soko.


Naye makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ambayo inasimamia wizara ya elimu Mh. Husna Sekiboko alipongeza jitihada za serikali lakini pia alipongeza wizara kwa sababu wameamua kupindua elimu nakuipeleka zaidi katika elimu ya vitendo ili vijana waweze kujiajiri.


"Na mtakumbuka watanzania wote inatokana na wimbi kubwa la vijana wengi kukosa ajira ,sasa profesa mkenda sasa anatamani kijana anapo hitimu awe na ujuzi dhahiri kwa akili ya kwenda kumudu maisha yake", alisema Husna.


Alisema wao kama wabunge kazi yao kubwa ni kuhakikisha Kama kutakuwa na Sheria ,kanuni taratibu zozote ambazo zinatakiwa ama kurekebishwa au kuanzishwa ili kuhakikisha kwamba wizara ama serikali inatekeleza vizuri jukumu hilo wao wapo tayari kufanya hivyo.


Maonesho ya NACTVET yanaendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, maonesho yaliyoanza Tarehe 16 mei na yanatarajiwa kufungwa Rasmi Tarehe 22 mai 2023.
Share:

PROF. BISANDA: UMRI SI KIKWAZO KUPATA ELIMU


Jamii ya Watanzania imetakiwa kuachana na dhana ya kuwa umri ukisogea basi hakuna tena fursa ya kujiendeleza katika elimu ya juu.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda, alipotembelea banda la maonesho la chuo hiki May 19, 2023 katika maonesho ya pili ya Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

“Dhana ya kusema kuwa ukiwa mzee huwezi tena kupata nafasi ya kusoma elimu ya juu kwa sasa imepitwa na wakati, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tunatoa fursa kwa marika yote bila kubagua umri na shughuli zao haziwezi kufa au kusimama kwa sababu zozote za kishule kwani wanasoma na huku wanaendelea na shughuli zao za kila siku.” Amesema Prof. Bisanda.

Aidha, alisisitiza kuwa kinachoangaliwa katika kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni ukamilifu wa vigezo vinavyotakiwa katika kujiunga na elimu ya juu pekee kwani kwa mfumo wa elimu hii hata asiyeweza kujongea anaweza kumudu kusoma.

Akithibitisha hilo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika programu ya msingi (Foundation Program), Ndg. Felix Ringo, mwenye umri wa miaka 55 licha ya kuwa umri wake umesonga na kubanwa na majukumu mengi ya kimaisha bado ameweza kujiunga na chuo hiki na dhamira yake ni kufika mbali kitaaluma katika umri huo.

“Kwa umri huu nilionao nimebanwa na mambo mengi nisingeweza kujiendeleza kupitia elimu za kukaa darasani, kupitia chuo Kikuu Huria cha Tanzania nimepata fursa adhimu kabisa na nina shauku kubwa ya kusoma hadi kufikia ngazi za juu za usomi. Nimeanza mwaka huu na ninajiandaa na mitihani ya majaribio hivi karibuni.” Amesema Ndg. Ringo.

Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko, Dkt. Mohamed Maguo, amefafanua kuwa dhima halisi ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ilikuwa ni kuwainua kielimu watumishi na watu waliokosa fursa ya kuhudhuria elimu za darasani kutokana na kubanwa na majukumu mbalimbali ya kimaisha. Hivyo, hata wale wanaohisi umri wao umeanza kuwatupa mkono, chuo hiki ni sehemu pekee yenye fursa ya wao kupata elimu ya juu ambayo wanahisi walishaipoteza.


Share:

Friday, 19 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 20,2023

















]
Share:

JAJI MAHAKAMA KUU ATOA NENO USALAMA WA WAFANYAKAZI NA MIUNDOMBINU YA SERIKALI


Mkaguzi wa usalama wa mifumo ya umeme wa OSHA, Mhandisi Maria Ndaskoy akifanya ukaguzi wa mifumo ya umeme katika jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Morogoro.
Meneja wa OSHA Ofisi ya Kanda ya Pwani, Mhandisi, George Chali (kushoto) akizungumza na watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Morogoro, wakati wa kikao cha kutoa mrejesho wa ukaguzi uliofanywa na OSHA katika ofisi na maeneo mbalimbali ya jengo hilo.
Mkaguzi wa afya na mazingira ya kazi wa OSHA, Bw. Renatus Qalqal akifafanua namna sahihi ya matumizi ya kiti cha egonomia katika ofisi wakati akitoa mrejesho wa ukaguzi uliofanywa na OSHA katika jengo hilo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro.
Mkaguzi wa usalama wa umeme wa OSHA, Mhandisi Maria Ndaskoy akifafanua jambo kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro, Mhe.Jaji. Paul Ngwembe wakati akitoa mrejesho wa ukaguzi wa mifumo ya umeme uliofanywa na OSHA katika jengo la Ofisi hizo.

****************

Na Mwandishi Wetu

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro, Mhe. Paul Ngwembe, ametoa wito kwa viongozi wa Taasisi mbali mbali za umma kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kuhakikisha kwamba miundombinu iliyowekezwa na serikali katika Taasisi zao pamoja na usalama wa wafanyakazi vinalindwa.

Ametoa kauli hiyo mara baada ya kuhitimishwa kwa zoezi la ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Mkoani Morogoro ambao umefanyika sambamba na mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya usalama na afya watumishi wa Mahakama hiyo.

“Kwa kipindi cha hivi karibuni serikali imewekeza fedha nyingi sana katika ujenzi wa Ofisi bora za Mahakama hapa nchini na zaidi ya hapo serikali imejenga Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki (Integrated Justice Centres) zenye mahakama za ngazi zote kuanzia Mahakama ya Mwanzo pamoja na ofisi mbali mbali za wadau wote wa Mahakama wakiwemo Mawakili wa Kujitegemea zipatazo sita (6) nchi nzima. Hivyo, sisi kama viongozi tunatambua umuhimu wa kuhakikisha kwamba uwekezaji huu wa serikali unatunzwa ipasavyo ili miundombinu hiyo iweze kutumika kwa kipindi kirefu zaidi,” ameeleza Mheshimiwa Ngwembe na kuongeza kuwa:

“Jambo hili ndilo limetufanya sisi kuona kuna haja ya kushirikiana na wenzetu wa OSHA ambao ndio wataalam wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili kuweza kupata ushauri endelevu katika kulinda afya za wafanyakazi pamoja na miundombinu yote muhimu katika Ofisi zetu za Mahakama.”

Aidha, Kiongozi huyo Mkuu wa Mahakama Kanda ya Morogoro amebainisha kwamba Ofisi yake itaendelea kushirikiana na OSHA katika kuhakikisha kwamba ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya pamoja na mafunzo kwa watumishi wa Mahakama unakuwa endelevu na unafanyika katika Ofisi zote za Mahakama katika kanda husika.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amewapongeza Viongozi wa Mhimili wa Mahakama kwa kutambua umuhimu wa kulinda miundombinu bora ya Ofisi za Mahakama kupitia utekelezaji wa taratibu zote muhimu za utunzaji wa majengo ikiwemo kuhakikisha majengo hayo yanakuwa na mifumo madhubuti ya usalama na afya.

“Ninaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu bora ya Ofisi za Mahakama nchini jambo ambalo litafanikisha azma yake ya kuharakisha utoaji wa haki kwa wananchi kupitia chombo hiki muhimu cha Mahakama. Aidha, pongezi hizi ziwaendee viongozi wa Mhimili wa Mahakama kwa kutambua thamani ya uwekezaji huo na kushirikiana nasi ili kuhakikisha kwamba uwekezaji huo unabaki salama wakati wote. Lengo la kaguzi za OSHA sio tu kumlinda mfanyakazi lakini vile vile ni kulinda uwekezaji ili kuwa na uzalishaji endelevu na wenye tija,” amesema Kiongozi huyo Mkuu wa Taasisi ya OSHA.

Lilian Kombe, Mfanyakazi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Morogoro ambaye alishiriki mafunzo yalitolewa na Wakaguzi wa OSHA mara baada ya kuhitimisha ukaguzi wao, amesema wamejifunza mambo mengi kuhusu afya na usalama wao wanapokuwa kazini ikiwemo usalama wa mifumo ya umeme pamoja na masuala ya kiegonomia.



OSHA ni Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) yenye jukumu la kulinda nguvukazi ya Taifa pamoja na rasilimali nyingine zilizowekezwa katika sekta ya umma na binafsi. Miongoni mwa mambo yaliyotazamwa na OSHA katika ukaguzi huo ni pamoja na usalama wa mifumo ya umeme, mashine na zana kufanyia kazi, masuala ya kiegonomia pamoja na ukaguzi wa afya na mazingira ya kazi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger