Friday, 19 May 2023

DKT MPANGO AVUTIWA NA UBUNIFU WA PROGRAMU YA IMBEJU KATIKA KUCHOCHEA UJUMUISHI WA KIUCHUMI NCHINI

Arusha. Tarehe 18 Mei 2022 - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ameipongeza Benki ya CRDB pamoja na taasisi yake ya CRDB Bank Foundation kwa ubunifu iliokuja nao kupitia programu ya IMBEJU ambapo amesema ni wenye manufaa makubwa kwa Taifa.


Dkt. Mpango amesema hayo wakati wa uzinduzi wa semina maalum ya elimu ya fedha na uwekezaji kwa wanahisa wa Benki ya CRDB pamoja na umma iliyobeba kaulimbiu ya “Ushirika wa Benki ya CRDB na Serikali kuwezesha Vijana na Wanawake” iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).


Katika semina hiyo iliyoambatana na maonyesho ya biashara changa za vijana, Dkt. Mpango ameshuhudia bunifu za baadhi ya vijana zinazoendelezwa kupitia programu ya IMBEJU. Dkt. Mpango amepongeza akisema semina hiyo pia ni fursa kwa vijana kuonekana na wawekezaji.
“Nimefurahi kuona mmewaalika vijana wenye biashara changa pamoja na wanawake katika semina hii. Kwa kufanya hivi mmewapa fursa ya kuonekana na wawekezaji watarajiwa kwani naamini wapo wanahisa ambao wanaweza kuwekeza katika hizi biashara zao kama ambavyo wamewekeza katika Benki ya CRDB,” amesema Dkt. Mpango.


Dkt. Mpango pia amepongeza jitihada za Benki ya CRDB kushirikiana na Serikali kuyawezesha makundi ya kiuchumi bara na visiwani kupitia programu hiyo ya IMBEJU na kwamba sio mara ya kwanza kwani benki hiyo inashirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoa mikopo isiyo na riba kupitia programu ya INUKA na Uchumi wa Bluu.


Aidha, Dkt. Mpango aliipongeza Benki ya CRDB kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yaliyoshuhudia benki hiyo ikiendelea kutengeneza faida inayoiwezesha kutoa gawio kwa wanahisa wake.
“Nimefurahisha kusikia mwaka huu Bodi ya Wakurugenzi imekuja na pendekezo la ongezeko la asilimia 25 la gawio kwa kila hisa. Wanahisa wa Benki ya CRDB mnastahili kutembea kifua mbele kwa ongezeko hili,” ameongezea Dkt. Mpango huku akibainisha kuwa Serikali nao itanufaika na ongezeko hilo kwani ina hisa ndani ya Benki ya CRDB.


Dkt. Mpango ametumi anafasi hiyo kuziomba taasisi za fedha na bennki za biashara nchini kupunguza riba ya mikopo kama ilivyofanywa kwenye kilimo ambako baadhi zinatoa mikopo hiyo kwa asilimia 9.


“Naamini riba hiyo inaweza kushuka zaidi ya hapo. Punguzeni riba pia kwenye sekta nyingine mfano wachimbaji wadogo wa madini, wafugaji na wakulima. Riba kubwa ni kati ya sababu zilizolifanya Jiji la Dar es Salaam kushika nafasi ya 500 kati ya majiji 1,000 duniani katika kukuza biashara ndogo tofauti na majirani zetu Kenya ambao jiji lao la Nairobi lilikuwa miongoni mwa majiji 160 bora katika ripoti hiyo yam waka 2022,” aemesema Dkt. Mpango.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alimweleza Makamu wa Rais kuwa dhamira ya benki hiyo ni kuifanya programu ya IMBEJU kuwa endelevu ndio maana wanashirikiana na wadau mbalimbali ili kuwafikia vijana na wanawake wengi zaidi.


“Tunaamini mafanikio ya programu hii yapo katika ushirikiano, ndio maana tangu mwanzoni tulianza kwa kushirikiana na wenzetu wa COSTECH (Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia) na ICTC (Tume ya TEHAMA) na hivi karibuni tumesaini mkataba na Shirika la Care International,” amesema Nsekela akiainisha kuwa mpaka sasa vijana 709 na wanawake zaidi ya 4,000 wameshanufaika na programu hiyo.


Nsekela amebainisha kuwa lengo la kuijumuisha programu ya IMBEJU katika semina ya wanahisa wa benki hiyo ni kuwaonyesha kwa vitendo mwelekeo wa mkakati mpya wa Benki ya CRDB wa miaka mitano kuanzia mwaka 2023 – 2027 ambao umejikita katika kuleta mageuzi thabiti katika biashara ya benki hiyo kupitia huduma, bidhaa na programu bunifu katika soko.
Mwaka huu, Benki ya CRDB imepata leseni ya kutoa huduma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na leseni ya kampuni tanzu ya CRDB Insurance. Nsekela amesema kwa hatua hiyo, Benki sasa inatoa huduma katika nchi tatu ambazoni Tanzania, DRC na Burundi ambako ilifungua tawi miaka 10 iliyopita.


“Tunayo CRDB Bank Foundation ambayo imejikita kuwahudumia vijana na wanawake. Kwa hatua zote za kimkakati tunazozichukua, tunaamini miaka michache ijayo, ufanisi wetu utaongezeka hivyo kuongeza thamani ya uwekezaji wa wanahisa wetu,” amesema Nsekela.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay amesema ikiwa benki ya kizalendo inayomilikiwa na Watanzania kwa zaidi ya asilimia 80, wanajivunia kuendelea kuwekeza katika ubunifu uliochangia kukua kwa thamani ya uwekezaji wa wanahisa wake ikiwamo Serikali.
Katika semina hiyo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwamo faida za kuwekeza katika hisa. Dkt. Laay aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji katika hisa husasan za Benki ya CRDB ili nao wanufaika na gawio nono ambalo limekuwa likitolewa na benki hiyo kila mwaka.


Dkt Laay pia alitumia fursa hiyo kuwaalika wanahisa wa Benki ya CRDB kuhudhuria Mkutano Mkuu utakaofanyika kesho katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) na kupitia mtandao. “Mkutano utaanza saa 3 asubuhi, watu wa mtandaoni wataweza kujiunga kupitia link https://escrowagm.com/crdb/login.aspx au kupitia SimBanking App,” amesema Dkt. Laay.


Benki ya CRDB imeweka mwongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yake ya www.crdbbank.co.tz, mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter, na maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa wanahisa wote.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kyaro Assistive Tech, Colman Ndetembea inayozalisha vifaa vya usaidizi kwa ajili kusaidia watu wenye ulemavu, wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa ya Benki ya CRDB ambayo mwaka huu imebeba ujumbe wa uwezeshaji wa vijana na wanawake kupitia program ya IMBEJU. Wengine pichani ni kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mweneykiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa ya Benki ya CRDB ambayo mwaka huu imebeba ujumbe wa uwezeshaji wa vijana na wanawake kupitia program ya IMBEJU, uliofayika leo kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Foundation, Tully Esther Mwamapa akizungumza wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa ya Benki ya CRDB ambayo mwaka huu imebeba ujumbe wa uwezeshaji wa vijana na wanawake kupitia program ya IMBEJU, uliofayika leo kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Share:

KIKWETE AIPONGEZA GGML KUENDELEZA KAMPENI YA KUDHIBITI UKIMWI, AKUSANYA BILIONI 1.6



Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko (kushoto kwake) wakimkabidhi hundi ya Sh milioni 100 Mwenyekiti wa Mfuko wa Udhamini wa kudhibiti UKIMWI -ATF, Carorine Mdundo(wa tatu kushoto) zilizotolewa na Kampuni ya GGML kupitia Kampeni ya GGML Kili Challenge. Wengine wanaoshuhudia kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo na Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong.

NA MWANDISHI WETU
JUMLA ya Dola za Marekani 700,000 (sawa na Sh bilioni 1.6) zimepatikana katika uzinduzi wa harambee Ya kampeni ya GGML Kili Challenge iliyoongozwa na Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kwa lengo la kukusanya Sh bilioni 2.3 fedha zitakazotumika kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi.

Kampeni hiyo iliyoasisiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ilianzishwa mwaka 2002 na kufikia makundi mbalimbali yaliyo katika maeneo hatarishi kwenye janga hilo.

Akizunguma katika harambee hiyo iliyofanyika jana tarehe 18 Mei 2023 jijini Dar es Salaam, Dk. Kikwete aliipongeza GGML na TACAIDS kwa ushirikiano walioufanya na kuanzisha kampeni hiyo inayounga mkono jitihada za Serikali kudhibiti maambukizi ya VVU/ UKIMWI.

“Endeleeni kuitangaza GGM Kili Challenge kwa kupitia mabalozi mbalimbali na celebrity (watu maarufu) ili kampeni hii iwe jambo linalozungumzwa duniani,” alisema.


Tanzania bila UKIMWI, inawezekana! Msemo huo ulikuwa wa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.

Dk. Kikwete alisema Serikali yenyewe haiwezi kutokomeza janga la Ukimwi bila kuwepo kwa ushirikiano kati yake na sekta binafsi ili kuhakikisha katika kipindi cha miaka saba iliyosalia kufikia 2030, hakuna kifo chochote kitokanacho na janga hilo.

“Hamasa inatakiwa kuendelea kutolewa kwa ukubwa kwa sababu tumetoka mbali, tumepunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi kutoka 72,000 mwaka 2016 hadi 54,000 mwaka 2021,” alisema na kuongeza kuwa;

“Tatizo bado ni kubwa, suala la msingi tuhakikishe fedha zinazokusanywa kupitia kampeni ya GGM Kili challenge zinawafikia walengwa husika.”

Akizungumzia katika kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong mbali na kuishukuru Serikali kwa kuunga mkono kampeni hiyo, alisema wakiwa wadau wa mapambano hayo ya UKIMWI na VVU, GGML imepokea msaada ambao uliiwezesha Kili Challenge kupiga hatua kubwa hadi kufikia kuwa mfuko wa kimataifa, wenye kushirikisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.

Alisema kampeni hushirikisha wapanda mlima Kilimanjaro kwa njia ya miguu na njia ya baiskeli ili kuhamasisha jamii kuchangia fedha za kutunisha mfuko wa mapambano ya Ukimwi pamoja na juhudi za kutokomeza maambukizi ya janga hilo.

Kwa upande wake Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo amesema tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo makundi mbalimbali yamefaidika ikiwa kuazishwa kwa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu - Moyo wa Huruma kilichopo Geita.

Alisema katika kundi la kwanza la watoto waliolelewa kwenye kituo hicho sasa wamefikia elimu ya chuo kikuu ikiwamo wawili ambao wanasomea udaktari.

Alisema pia wameanzisha vituo vya maarifa katika maeneo hatarishi kwa maambukizi ya VVU, Manyoni na Segera ambavyo vinatoa elimu kuhusu VVU/ Ukimwi kwa madereva wa malori ya masafa marefu kwani pia ni kundi hatarishi kwa janga hilo.

“Chochote ambacho mtatoa au mlichowahi kutoa kinalenga kufikia sifuri tatu yaani kupunguza kabisa kwa kufikia asilimia sifuri ya maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa pamoja na sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko alisema fedha zinaokusanywa hupelekwa pia kwa asasi zisizo za serikali zinazoendeleza mapambano dhidi ya VVU/ Ukimwi.

Alitolea mfano kuwa kwa mwaka 2019/2020, jumla ya Sh milioni 550 zilitolewa kwa asasi hizo 20 huku nane kati yake zikiwa zinaongozwa na wanaoshi na VVU.

Alisema mapambano dhidi ya VVU bado yanahitaji hasa ikizingatiwa misaada kutoka nje imepungua hivyo juhudi za Watanzania na wadau wengine zinahitajika ili kufikia malengo yaliyoweka na Serikali kufikia sifuri tatu mwaka 2030.

Katika harambee hiyo GGML walitoa dola za Marekani 500,0000.
Zoezi hilo la kupanda mlima linatarajiwa kuanza tarehe 14 Julai na kushuka tarehe 20 Julai mwaka huu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Hamis Nderiananga (kulia) akimkabidhi zawadi maalumu Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake muhimu katika kampeni ya GGML Kili Challenge ambayo ilianzishwa na Kampuni ya GGML mwaka 2002 kwa kushirikiana na TACAIDS kwa lengo la kutokomeza VVU/ UKIMWI.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (kushoto) akimkabidhi zawadi Rais mstaafu Jakaya Kikwete kutokana na mchango wake kwenye Kampeni ya GGML Kili Challenge iliyoanzishwa na kampuni hiyo mwaka 2002 kwa kushirikiana na TACAIDS. Jana Alhamisi Kikwete ameshiriki katika uzinduzi wa harambee ya kampeni hiyo kwa mwala huu jijini Dar es salaam.
Share:

NILICHEZEWA NISITUNZE PESA MFUKONI

Ninafanya kazi nzuri kwenye shirika lisilo la kiserikali la kusaidia watoto yatima, wazee na wale waote wasio jiweza Dodoma huko shirika letu linaitwa Diamanda Foundation sio kongwe sana lina kama miaka kumi sasa tangu tulizinduwe,tunategemea kupokea misaada kwenye mashirika mbalimbali, serikalini , na taasisi nyingine zote zinazoguswa na huduma yetu tunayoitowa hapo ofisini.


Mshahara wangu ni mzuri unakidhi familia na kuiendesha vizuri bila ya changamoto yoyote ile. Ninaye mke na watoto wawili wa kiume bado ni wachanga na hawasomi wanashinda nyumbani na mama yao .Shirika hili nililifunguwa mimi na rafiki yangu Remmy na lilipokuwa tukaajiri wenzetu kadhaa sasa linazaidi ya wafanyakazi thelathini ambao wote wanafurahishwa na ufanyaji wetu wa kazi na malipo yetu pia.

Kwa muda ambao nimefanya kazi ningekuwa nimefahamu daktari BAKONGWA mapema nisingekuwa mtu wa kulia shida tena kama wengine au angalau ningezijuwa tovuti zake https://bakongwadocotors.com  tu mimi nisinge jutia muda ambao nimeupoteza kipindi chote cha ufanyaji wangu wa kazi pale ofisini kwetu.

Hali yetu ya familia ni ya kawaida sana tumepanga nyumba ambayo kwa nyuma ina majirani wasioishi pale na mara kadhaa huwa hawaonekani kabisa zaidi ya wiki mbili mpaka tatu bila ya taarifa zozote.Kila ninapopokea mshahara nazingatia sana familia na kumpatia mke wangu kwa kuwa yeye ndiye mama wa nyumbani ninamuacha afanyemipango ya matumizi na kiasi kingine kina chobaki ninakitunza humohumo ndani.

Jambo la kushangaza ni kila mara ninapotenga fedha ya kumpatia mama watoto kiasi kingine kinachobaki ni kikubwa lakini huwa sielewi kimetumikatumika vipi au kimeenda wapi – yaani huwa yanajitokeza matumizi na mahitaji ambayo hayakuweko kwenye malengo wala sikuyatarajia kabisa siku hizo za usoni mwetu.

Mara ya mwisho kabla ya kuligundua hili ni pale nilipompatia mke wangu fedha za matumizi kisha baada ya hapo mtoto akaumwa ghafla na sikuwa hata na senti yoyote ile mfukoni na ukiangalia ni siku mbili tu zimepita toka siku ya kupokea mshahara ipite, nusura nimpoteze mwanangu kwa kushindwa kutunza pesa ilikuwa ni msululu wa madeni kwangu.

Nikawashuku wale waliokuwa majirani zetu kuwa walikuwa wanafanya chuma ulete kwangu au chochote kilicho jihusisha na upooteaji na matumizi yasiyo na malengo kwenye pesa zangu.Nikaamua kuleta mchungaji kwangu afanye ibada ya pamoja na sisi kama familia hilo lilikwisha lakini bado pesa zangu hazikuonekana zilikwisha hovyohovyo bila ya mipangilio.

Sasa majirani zangu walihama lakini bado hali yangu ni ileile pesa zangu hazikai na wala matumizi yake hayaonekani, nikaamuwa kuhamanyumba labda nitapata aahuweni ila bado hakuna kilichokwenda sawa kwangu.Nikiwa mwenye hali ya kuonesha kushindwa na kuridhika na mateso yale nikapewa ushauri na Remmy nimtafute daktari bakongwa kwenye nambari zake za whatsapp +243990627777 naye atanisaidia, nilifanya hivyo .

Daktari alipopata taarifa zangu akafanya utaalamu wake kisha akagunduwa kuwa kuna watu upende wa marafiki zangu hawapendi wamafinikio na walikuwa wamenifunga nisikae na pesa na ndio kila wakati yalikuja matumizi yasiyo ya msingi akanipa dawa yangu na familia tukatumia sasa maendeleo ya kiuchumi ninayaona nina miliki hata kigari cha kutembelea asante sana daktari.


Share:

Thursday, 18 May 2023

MCHENGERWA ATOA WITO KWA BALOZI KUSHIRIKIANA NA MAWAKALA WA UTALII KULETA WAGENI


Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa waheshimiwa mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kushirikiana na makampuni ya mawakala ya utalii katika nchi husika kuwaleta watalii nchini ili kuifikia azma ya kuwaleta watalii milioni tano ifikapo 2025 na kukuza uchumi wa nchi.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Mei 18, 2023 wakati akisoma hotuba yake kwenye mkutano maalum wa kibiashara baina ya makampuni makubwa duniani ya watalii kutoka nchini China na wadau wa utalii nchini jijini Arusha alipokuwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Anderson Mutatembwa.




Amempongeza Balozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na wadau wengine kuratibu ujio wa mawakala hao na kutoa wito kwa mabalozi wengine kuiga mfano huo.

Amefafanua kuwanchi ya China ni soko la kimkakati la utalii kwa Tanzania kwa kuwa ni miongoni mwa nchi yenye watalii wengi ambao Tanzania inapaswa kunufaika nalo

Akitolea mfano amesema kuwa nchi ya China inatoa takribani watalii milioni 155 kwa mwaka kwenda sehemu mbalimbali duniani lakini ni watalii 33000 kutoka china ndiyo wanaotembelea Tanzania kwa mwaka.




Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini China wameandaa program maalum hii inayolenga kuwavutia watalii wengi kutoka China kuja kutembelea Tanzania.

Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine program hiyo itahusisha masuala ya mafunzo ya utamaduni, masuala ya lugha, mifumo mbalimbali ya kurahisisha malipo wakiwa nchini, vyakula vya kichina na namna ya kujitangaza.

Aidha, amesema program hiyo itawasaidia watalii kutoka China kufurahia utalii wa Tanzania, pia kuratibu safari za kitalii ikiwa ni mwendelezo wa program ya Royal Tour iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Waziri Mchengerwa amesema mawakala hao ikiwa ni kundi lenye ushawishi mkubwa kwenye mnyororo wa thamani wa utalii duniani litasaidia pia kufungua milango ya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya utalii hapa nchini.

Amewapongeza wadau mbalimbali wa utalii nchini ambao wameshirikiana na Serikali katika kuratibu ujio huu wa mawakala hao huku akisisitiza kuwa kwa sasa Serikali itaongoza katika kufanya kushawishi badala ya kubaki nyuma kama na kuacha kazi hiyo kufanywa na wadau pekee.




Amesema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo havipatikani katika sehemu nyingi duniani hivyo ina kila sababu ya kuweka mikakati mizuri ili kuwavutia watalii na wawekezaji ili waje nchini na kuleta fedha za kigeni.

“Ninaamini taifa letu ni taifa la kipekee, taifa ambalo lina vivutio vingi ambavyo mataifa mengi hayana na yanatamani kuwa katika nafasi kama yetu, pia vivutio vyetu ni vivutio ambavyo sehemu nyingi ya dunia havipo na ndiyo maana katika takwimu za UNESCO tunaongoza katika nafasi za juu kabisa. “amesisitiza Mhe. Mchengerwa.




Amewahakikishia mawakala hao kuwa tayari Serikali imeshaainisha maeneo ya uwekezaji katika hifadhi na kwamba imeandaa mazingira rafiki yatakayowezesha kufanya biashara na kupata faida.

Mara baada ya mkutano huu mawakala hao ambao wameambatana na vyombo vikubwa habari 6 kutoka nchini China wataembelea maeneo ya Hifadhi ili kuona vivutio vya utalii kabla ya kurejea nchini China mwishoni mwa mwezi Mei 2023.
Share:

SERIKALI KUENDELEA KUWEZESHA UWEPO WA MAJUKWAA YA WAFANYAKAZI


Na Mwandishi Wetu-MOROGORO

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imesema itaendeea kuwezesha uwepo wa majukwaa ya wafanyakazi ili kuhakikisha yanatoa nafasi ya wafanyakazi kujadili masuala yao.

Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri chini ya Ofisi hiyo, Pendo Berege ameyasema hayo Mei 17, 2023 katika mafunzo ya watendaji wa vyama vya wafanyakazi, waajiri na Shirikisho la vyama hivyo yaliyofanyika mkoani Morogoro yaliyolenga kukumbushana wajibu na majukumu katika utekelezaji wa katiba na kanuni za vyama.

Amesema ataendelea kushirikiana na vyama vya wafanyakazi ili kuhakikisha vyama hivyo vinatekeleza majukumu kwa weledi na bila kuingiliwa na kuwa majukwaa ya kujadili mambo yao.

Amesema katika sherehe za Mei Mosi serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ilielekeza vyama vya wafanyakazi kuhakikisha vinawasilisha masuala ya wafanyakazi serikalini hivyo majukwaa hayo ni kiunganishia ycha kushughulikia maslahi ya wafanyakazi.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya ametoa rai kwa Msajili wa vyama hivyo kuwasilisha ombi la ada ya uwakala serikalini isiingiliwe na watu serikalini ili kuondoa changamoto zinazojitokeza.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Chama Cha Waajiri (ATE), Leonard Mapha, ameshauri kuendelea kuwepo kwa mijadala yenye manufaa na kuwa na mikataba bora mahali pa kazi ili kuweka wazi matarajio yao baina ya mwajiri na mwajiriwa.
Share:

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA BENKI YA CRDB KWA KUTOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI KUIMARISHA USALAMA KWA WATALII JIJINI ARUSHA


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa (wa pili kushoto) akiwa katika pikipiki zilizokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha kwa ajili ya kusaidia katika doria na kuimarisha ulinzi na usalama kwa watalii. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya Arusha, Felician Mtahengerwa (wa kwanza kulia), na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

======== ======== =========


Arusha Tarehe 18 Mei 2023 - Serikali imeipongeza Benki ya CRDB kwa kutoa msaada wa pikipiki 15 kwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha ili kuimarisha doria zitakazoongeza usalama kwa watalii wanaokuja nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Utalii na Maliasili, Mohamed Mchengerwa alipopokea pikipiki hizo zenye thamani ya TZS 40 milioni kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia kilichopo jijini hapa.
Waziri amesema sekta ya utalii ina umuhimu mkubwa katika uchumi na maendeleo ya wananchi nchini kwani ndiyo inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni, ikiwa ya pili kwa kuchangia kwenye Pato la Taifa (GDP), na ya tatu kwa kutoa ajira.


“Ripoti za Benki Kuu Tanzania (BOT) zinaonyesha sekta ya utalii inaendelea kuimarika baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO-19. Mapato yatokanayo na utalii kwa Machi yalifikia Dola za Marekani bilioni 2.787 ikilinganishwa na dola milioni 885 kipindi kama hicho mwaka 2021. Katika mwezi huo, jumla ya watalii 1,574,630 waliingia nchini,” amesema Mchengerwa na kuongeza huku akipongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Samia katika kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Royal Tour.


“Kipeeke kabisa naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa msaada huu wa pikipiki 15 ambao Benki yetu ya CRDB imeutoa kwa kituo chetu hichi. Pikipiki hizi zitawawezesha askari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Askari watakabiliana haraka na dharula jambo litakalosaidia kuimarisha usalama kwa watalii na kuifanya nchi yetu kuwa kivutio kikubwa hivyo wageni wengi kuja kuitembelea.”
Mwaka 2020, sekta ya utalii ilichangia asilimia 10.6 kwenye pato la taifa ila kiasi hichi kilishuka hadi asilimia 5.7 mwaka 2021 kutokana na athari za UVIKO-19 hivyo kuilazimu Serikali kuchuku ahatua za makusudi kuifufua kwa kufuata taratibu za Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanya matangazo kimataifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe kurekodi filamu ya ‘The Royal Tour.’


Ili kuhakikisha usalama wa watalii wanaokuja nchini, Serikali ilianzisha kitengo maalum cha utalii na diplomasia kwa ajili ya kuwahudumia watalii na wanadiplomasia wanaofika nchini kutalii ama kuwekeza kwa haraka.


Kwa kuwa jiji la Arusha ndio kitovu cha utalii nchini, kituo hicho kimejengwa huko na askari wake walipewa mafunzo ya ziada ndani na nje ya nchi juu ya namna bora ya kuhudumia watalii. Vituo vingine vidogo vimefunguliwa katika wilaya za Arumeru, Karatu, Monduli na Longido.
Akikabidhi pikipiki hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa amani, utulivu na usalama katika maendeleo ya nchi kiuchumi, kijamii na kisiasa hivyo ni jukumu la jamii nzima kushiriki kuuimarisha.


“Pamoja na kuwepo hali ya amani na utulivu nchini, bado baadhi ya matukio ya uhalifu hujitokeza kama vile vile uporaji wanaofanyiwa raia hata watalii wanaokuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini. Ili Jeshi la Polisi litekeleze majukumu yake kwa ufanisi linahitaji vitendea kazi vya kutosha,” amesema Nsekela.


Mkurugenzi huyo amesema wanayo furaha kubwa kukabidhi pikipiki hizo ili kuwasaidia askari kukimbizana na wahalifu wanaowapora watalii au kusafirisha mihadarati hivyo kuharibu sifa njema za jiji hili la kitalii.
“Tunaamini matumizi sahihi ya pikipiki hizi yatasaidia kudhibiti uhalifu jijini hapa na tunaahidi tutaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kupunguza baadhi ya changamoto zinazokwamisha ufanisi wake ili nchi yetu iendelee kuwa salama kwa biashara na uwekezaji,” amesema Nsekela.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Edith Swebe, amesema jitihada zinazoendelea kuutanga utalii wa Tanzania umelifanya Jiji la Arusha kupokea wageni wengi wanaoongeza haja ya askari polisi kuwapo katika kila eneo.
“Tunachokifanya sasa hivi ni kusimamia mradi wa utalii salama ambao unahitaji askari kuwapo kila walipo wageni. Pikipiki hizi tunazozipokea zitasaidia kuwafikisha askari kwenye maeneo ambako magari hayawezi kufika kwa urahisi zikiwamo barabara nyembamba. Jeshi la Polisi linaaminimazingira salama ni kivutio cha utalii,” amesema Edith ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu.


Hata hivyo, ameiomba Serikali na wadau wengine wa utalii kuliwezesha jeshi hilo kupata pikipiki nyingine 10 zitakazofanya kata zote 25 za Jiji la Arusha kuwa na pikipiki moja ya doria itakayosaidia utekelezaji wa mradi wa utalii salama.









Share:

MSHINDI WA TZS 20,000,000/= ATAMBULISHWA MERIDIANBET


­­­­­Kila mtu na bahati yake Meridianbet hakuna masuala ya nyota yako imefifia au oga maji ya bahari kuondoa nuksi, iko hivi kucheza na kushinda kasino ya mtandaoni ni rahisi, kuwa moja ya mabingwa na Wafalme wa Meridianbet kila unapocheza kasino.

 

Kutoka uswahilini Temeke Mtoni kwa Aziz Ali, Meridianbet imempata milionea aliyecheza kasino ya mtandaoni kwa dau dogo tu lililompeleka kwenye Jackpot kabambe ya ushindi.

 

Mwamba anasema kwamba ameifahamu Meridianbet kasino ya mtandaoni kwa muda wa miaka 4 na amekuwa akicheza sana sloti na michezo mingi, moja kati ya michezo aliyocheza na kumpa utajiri ni Piggy Party.

 

“Nimeifahamu Meridianbet kasino ya mtandaoni kwa miaka 4, na kila nikicheza nilikuwa nashinda pesa ndogo kuanzia Laki Moja lakini hatimaye bahati imenidondokea mimi kwa kushinda TZS Milioni 20,000,000/= Mshindi kutoka Kwa Aziz Ali.

 

Meridianbet kasino ya mtandaoni ina michezo/sloti mingi ya ushindi na kila siku washindi wengi wanatangazwa, kama hujashinda leo basi endelea kucheza mara kwa mara huenda nawe kesho ukawa Milionea.

 

Kubwa kuliko ni kwamba kila unapojisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko 50 ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.

 

NB: Sloti ya Piggy Party ina mistari 11 ya ushindi, kuna chaguo la Gamble kuongeza ushindi wako kama unahitaji, kubwa Zaidi kila unapocheza unaingia kwenye Jackpot ambayo inatoa mamilioni ya hela.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger