Wednesday, 17 May 2023

WAZIRI DKT MABULA ATAKA MADALALI WENYE WELEDI NA STAHA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ilipomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma tarehe 16 Mei 2023. Kulia ni Katibu Mkuu Eng. Anthony Sanga.

**************

Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kuhakikisha madalali wanaoteuliwa wanapata mafunzo na wenye weledi wanaoweza kufanya kazi kwa staha.

Dkt Mabula alisema hayo tarehe 16 Mei 2023 alipokutana na Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya Ardhi, Nyumba na Wilaya ilipokwenda kumtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Kamati hiyo ambayo iko chini ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliundwa tarehe 27 Disemba 2021 kwa mujibu wa wa kifungu cha 2&3 cha sheria ya Mahakama za migogoro ya ardhi sura 216.

"Ni vizuri madalali mtakaowateua waonekane ni wale waliopata mafunzo na wenye weledi na wanaoweza kufanya kazi kwa staha, hilo nalo ni zuri zaidi" alisema Dkt Mabula.

"Unaenda kutekeleza amri ya mahakama halafu unachukua vitu unarusha huko hiyo hapana, tunatambua ni amri ya mahakama lakini basi ifanyike kwa staha siyo kujivurugia kwa sababu ni dalali, tusingependa kuingia kwenye historia ya kuanza na madalali walioteuliwa kwa kanuni mpya na kupigiwa kelele" àlisema Dkt Mabula.

Aidha, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametaka madalali walio na leseni za utekelezaji kutoenda moja kwa moja kwenye tukio bila kupita ofisi za utawala wa eneo husika na kutaka madalali wakati wa utekelezaji kupita kwa Mkuu wa Mkoa. Wilaya wilaya au Afisa Tarafa kutegemeana na utaratibu utakaowekwa ili kazi ifanyike na baraka za utawala.

" Kumekuwa na changamoto hiyo mara nyingi sana, dalali anapata kazi anaamkia site anaenda kuvunja nyumba mimi nisingependa yatokee kwa style hiyo ni vizuri kupita kwa DC akaona hukumu yenyewe au amri ya mahakama na kujiridhisha ingawa hana namna ya kubadilisha lakini akawa na taarifa nini kinaenda kufanyika" alisema Dkt Mabula.

Akigeukia suala la wito wa mahakama, Waziri Mabula ametaka kujua sheria inasemaje kwa mtu anayepelekewa wito na kukosekana mara moja au mbili nyumbani kwake.

"Nisingependa malalamiko yatokane na madali walioteuliwa halafu mtu akose haki kutokana na kutopata wito au nyaraka iliyotoka mahakamani na taratibu nyingine zikaendelea ni vizuri kuangalia utaratibu mzuri wa kuhakikisha mhusika amefikiwa na kama hakufikiwa utaratibu upi unatumika ili walau afahamishwe kile kinachoendelea vinginevyo tunatumia madalali badala ya kupunguza changamoto zinakuwa zinaendelea" alisema Mabula.

Majukumu makuu ya Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya ardhi ni kufanya uteuzi wa Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya ardhi, Kusikiliza na kuamua madai ya utovu wa nidhamu dhidi ya madalali na wasambaza nyaraka wa mabaraza ya ardhi pamoja na kuunda na kusimamia kamati ndogo za kusimamia Madalali na Wasambaza Nyaraka katika ngazi za mikoa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifuatilia mchango wa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya Ardhi na nyumba ya wilaya (hayupo pichani) alipokutana nao jijini Dodoma tarehe 16 Mei 2023. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Eng. Anthony Sanga.

Baadhi ya Wakuu wa idara wa wizara ya ardhi wakiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wakiwa katika kikao na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 16 Mei 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Eng. Anthony Sanga. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

KATAMBI AELEZEA NAMNA SERIKALI INAVYOWAWEZESHA VIJANA WA SKAUTI


Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ametaja mikakati ya serikali ya kuwawezesha vijana wa Skauti nchini ikiwamo mafunzo ya fani kupitia programu ya kukuza ujuzi nchini.

Katambi ameyasema hayo Mei 17, 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Asha Abdullah Juma.

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji mkakati wa serikali wa kuwawezesha kimaendeleo vijana wa skauti nchini.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema kama ilivyo kwa vijana wengine wote wa Tanzania wakiwamo vijana wa skauti ambao wapo kati ya miaka 15 hadi 35, Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania imeendelea kutekeleza program mbalimbali.

Amesema program hizo ni pamoja na klabu za skauti katika shule za msingi na sekondari ambapo vijana hupatiwa mafunzo ya ujasiri, kutatua matatizo katika jamii, kujitolea na uzalendo.

Vilevile, amesema vijana wa skauti ni miongoni mwa vijana ambao hunufaika na programu mbalimbali zinazosimamiwa na Serikali ikiwa ni pamoja na fursa za mikopo yenye masharti nafuu ili kuanzisha miradi ya uzalishaji mali inayowawezesha kujiajiri pamoja na mafunzo ya fani mbalimbali kupitia programu ya kukuza ujuzi nchini.

Share:

Tanzia : ASKOFU DKT. JOHN KANONI NKOLA AFARIKI DUNIA




Aliyekuwa Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola amefariki dunia leo asubuhi Jumatano Mei 17,2023 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugandp Jijini Mwanza.


Taarifa zaidi tutakuletea.

R.I.P Askofu Nkola
Share:

MAADUI WAPAGAWA KWA ULINZI NILIONAO NYUMBA YENYE MAUZA UZA

Ninazijua shida nilizopitia kwenye yumba za kupanga, raha yake ni kuwa unatembea na nyumba yako mfukoni yaani unahama wakati wowote ule unapoitwa wewe mpangaji, ila mambo mengi sana kwenye nyumba zetu za kupanga zinatusumbua sana.

Kabla sijahamia Mwasanga Majengo Mapya mwanzoni nilikuwa ninaisha Ilemi ambapo sijawahi kuwa na afadhali hata usiku mmoja, ni tukio baada ya tukio ninashukuru pale palikuwa na mlinzi wa kuangalia mali lakini wenye mji wenyeji wangu vikongwe hawakuisha kunisumbua kila nilipopanda kitandani kusinzia.

Mara tatu mfululizo nimekuwa ninalala kitandani chumbani na nguo lakini asubuhi ninaamkia sebuleni tena nikiwa uchi wa mnyama.Hili nikafikiria pengine huwa nalala huku natembea nikaamua kuwa nafunga mlango wa chumbani na kufuri halafu kutengesha vyombo kusudi nikifungua nisikie niamke lakini halikuisha likaendelea.

Awamu mbili tofauti nimekuwa ninaamka nimekatwa nywele zangu kichwani na kiasi kwenye sehemu za siri hili ndilo likanifumbua macho nimtafute shemasi wa kanisa na kumpa mualiko aje kunifanyia ibada nyumba shida zinazonikabili usiku zikome kabisa.

Mtumishi akaja akaniombea na maji ya baraka tukamwaga kila kona ya  nyumba ninayoishi nikaamini hii itakuwa kiboko yao lakini wapi usiku wake nilipolala kuamka hali ikawa ndio nimewachokoza wenyeji wangu wa mtaa niliamka nikiwa nimechanjwa chale mwili mzima kuanzia nyuma ya shingo mpaka kwenye magoti ya miguuni.

Sasa nikaamua niwaambie wazazi wangu na ndugu zangu juu ya hali ninayoipitia wao kwa ufahamu wakaniambia nimtafute ostadh yoyote mwenye jina asome kisomo wakifikiri ni jini ndilo lilikuwa linanifanyia tabia za mtindo huo.

Nikafanya hivyo akaja msomaji wa kisomo akasoma kisomo kisha tukapeana pongezi na pole za shughuli usiku wake walikuja tena asubuhi nikaamka nikiwa ninaa alama za viganja kwenye shingo kana kwamba kuna mtu alikuwa ananikaba .

Uvumilivu ukanishinda nikaamua nitafute nyumba nihame pale palikuwa pana matukio yasiyoisha, nilipomwambia rafiki yangu dalali Charles akaniambia kuwa hali kama hizo huwa zipo kwenye kila nyumba hakuna nyumba nitakayohamia iwe salama bila shida yoyote ile.

Msimamo wangu wa kuhama ukawa juu nikasema lazima nihame lakini kwa bahati mbaya kipindi hicho nyumba za kupanga hazikuwa rahisi kupatikana na zilizopatikana zilikuwa gharama ya kodi iko juu kidogo.Dalali akaniambia nivumilie miezi iliyobaki akiwa ananitafutia nyumba lakini pia akanishauri kama sitojali nimtafute daktari BAKONWGWA kwenye namba zake za whatsapp +243990627777.

Kwa shida ambazo nilikuwa nimekwisha kuzipitia haraka haraka nikamtafuta na yeye daktari akaaamua kakufanya kulingana na hali yangu alinipa dawa ya kujitengeneza na kuondoa mizindiko yaliyowekwa na wakaaji wengine kabla yangu kwenye hiyo nyumba ambayo ilinipasa nitumie kwa siku mmoja tu.Usiku wake baada ya dawa nililala usingizi wa mmoja kwa mmoja bila shida zozote zile.

Sikutarajia kama itakuwa rahisi sana lakini kwa tiba zake daktari iliwezekana kila mara nikikumbuka hayo mpaka ulipofika wakati wa mimi kuhama niliwaacha majirani wakishangaa ni ulinzi gani nimeutumia kwenye maboma yao nakushukuru sana daktari bakongwa wa https://bakongwadoctors.com .


Share:

Tuesday, 16 May 2023

WANAWAKE WANAOTOKA FAMILIA ZA KICHUNGAJI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KIUCHUMI


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joab Ndugai.

Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Anglikana Tanzania (UMAKI) Margareth Ndonde amewataka wanawake wa familia za kichungaji kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo kujihusisha  ili kuepuka kuwa tegemezi na  kuwatwisha  mzigo waamini.

Amesema hayo kwenye Uzindizi wa mradi wa maendeleo ya Kanisa na Jamii uliyofanyika Chuo cha Theolojia cha Mt Philip's Kongwa mkoani Dodoma unaotekelezwa katika vijiji kumi kwa ukanda wa Hogoro na Zoissa.

Katibu huyo amesema ikiwa Wanawake hao watakubali kujibidiisha wataongeza ustawi kwenye  familia zao na kuwa bora zenye kujitegemea na kuwa mfano kwa wengine.

"Kwenye familia zetu imezoeleka tunapenda kuwa tegemezi,ni wakati wetu Sasa kuukataa umaskini Kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na  kujenga mahusiano mema na majirani ili kuimarisha amani na upendo katika jamii,"amesisitiza.

Naye Spika wa bunge aliyemaliza muda wake Job Ndugai ametumia nafasi kuitaka jamii kuwekeza kwenye miradi  mbalimbali ya maendeleo na kueleza kuwa huko nyuma ilikuwa ni changamoto kupata huduma kwa wakati tofauti na hivi sasa ambapo wamesogezewa kwa ukaribu.

Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa amesema Serikali imewekeza  miundombinu ya maendeleo vijiji vingi vya wilaya hiyo ya Kongwa vina umeme,shule,vituo vya afya na barabara zenye kupitika kirahisi kwa kipindi chote na kuimarisha mawasiliano ya simu na hivyo kirahisisha maendeleo.

"Hili la mawasiliano ya mitandao vijiji vingi vilikuwa hakuna mawasiliano,lakini kwa hivi sasa serikali imeadhimia kujenga minara 10 yenye uwezo mkubwa na wananchi wanaenda kuondokana na kero ya kukosa mawasiliano"amesema.


Naye Kanoni Ndatila amesema,"Tunamshukuru mbunge kupitia serikali yetu ndani ya kipindi chake tumeona jitihada ambazo zimefanyika ikiwemo miundombinu ya elimu afya umeme kilimo ma barabara ambazo hivi sasa zinapitika kwa muda wote"amesema.

Share:

MAFUTA HAYA YAMENIPA UTAJIRI KATIKA BIASHARA YANGU

Kuna wakati biashara huwa ngumu sana, wakati mwingine waweza unakosa wateja kwenye biashara yako, unatakiwa kujua kuwa maadui huwa wamewekeza ili kuona biashara yako haiendelei wakati wote.

Nilikuwa mfanyabiashara katika eneo la River Road, Nairobi ambapo nilifanya biashara ya kuuza vitabu, nilimiliki duka kubwa la vitabu, kando yangu kulikuwa na wafanyabiashara wengine waliofanya biashara mbalimbali zikiwemo za magendo.

Wakati ule biashara yangu haikuwa inafanya vizuri kabisa kwani hata wakati mwingine nilienda nyumbani bila hata ya kupata chochote kile.

Biashara zingine zilizokuwa kando yangu zilikuwa zimenawiri sana kwani walipata mapato mengi na watu walifurika katika biashara zao, nilijaribu kuweka mabango ya kuwavutia wateja lakini jitihada zote hazikufua dafu.

Nilijitia moyo na kujiambia moyoni kwamba hii ni changamoto tu, hivyo biashara ile itakuja kuwa kubwa siku za mbeleni, lakini siku zilivyokuwa zinazidi kwenda mambo yalizidi kuwa magumu kwangu.

Niliwatembelea baadhi ya wataalam wa mitishamba na kunifanyia tiba zao za asili na kuniahidi mambo yatakuwa sawa, lakini yote sikuweza kufanikiwa kabisa, mambo yaliendelea kubaki vilevile. 

Katika zile harakati za kutafuta suluhisho, nilikutana na Oliphia ambaye alikuwa ni rafiki wangu wa dhati na ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara mashuhuri. Alikuwa na biashara ya Hoteli, alinieleza siri ya mafanikio yake katika biashara.

Aliniambia kuwa African Doctors walimpa dawa ambayo iliweza kukinga biashara yake na husda za maadui zake, alisema bila kufanya hivyo ni vigumu sana kuja kupata mafanikio ya kibiashara.

Siku iliyofuatia nilifunga safari hadi kwenye Ofisi za African Doctors ili kupata usaidizi, alinihoji na hapo akaniambia kuwa mahasidi wangu kwenye biashara walikuwa wamepanda vitu ambavyo vilizuia kuimarika kwa biashara yangu.

Alinipa mafuta ambayo nilipaka kwenye mlango wa biashara yangu ili kuondoa nguvu za vitu vile, nilirejea jijini na kufanya jinsi nilivyoshauriwa.

Siku tatu baadaye nilianza kupata matokeo, duka langu la uuzaji wa vitabu lilipata wateja wengi zaidi kuwahi kutokea, magari yalifurika kwa wingi kwa ajili ya ununuzi wa vitabu kwenye duka langu.

Kwa kweli yale mafuta ambayo African Doctors alinipa yalikuwa yenye mwamko mpya katika maisha yangu, badaye nilifungua maduka zaidi ya uuzaji wa vitabu na biashara kuchanganya sana.

African Doctors ana uwezo wa kutibu magonjwa kama vile kifaduro, kifua kikuu, kaswendee n.k, anasuluhisha migogoro ya mashamba na kukuwezesha kushinda kesi kotini kwa muda unaotaka.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.



Share:

HUAWEI AIMS TO USE ITS  “4T”  TECHNOLOGIES TO ENABLE AN ENERGY LANDSCAPE TRANSITION OF 'FROMENERGY CONSUMER TO SUSTAINABLE ENERGY PRODUCER AND ENABLER'



President of Huawei Sub Saharan Africa ,Leo Chen

Huawei has successfully held the FusionSolar Forum 2023 at the sidelines of the Africa Solar Show 2023 last week in Johannesburg. Industry associations,sector organisations, industry leaders and experts gathered to share industry trends and insights and presented innovative solutions and best practices which will contribute to the development of the industry on the continent.

Leo Chen, President of Huawei Sub Saharan Africa, said that the quest for global carbon neutrality, energy security, and commercial value are driving the rapid development of a new international energy industry. The urgency of Africa’s own transition is being accelerated by power shortages and rising energy prices.Leo Chen indicated that in facing these challenges, Huawei as a leading ICT company, can be part of the solution. “With a heavy investment in R&D, we’ve developed the most comprehensive set of technologies in ICT, and this forms our unique advantage.”

He said that by integrating power electronic and digital technologies, Huawei’s ‘4T’ (WatT, HeaT, BatTery, and BiT) technologies, which refers to Huawei’s innovations in the field of power electronics,thermal management, power storage, and Cloud and AI, can enable the traditional solar energy industry to be more efficient and more intelligent.

“The application of our “4T” technologies, will also effectively accelerate Africa’s energy transition toward the direction of ‘4D’, which is Decarbonisation, Digitalisation, Decentralisation, and Democratisation,” he said.

Huawei’s full-scenario smart PV solutions not only can provide solutions to utility-scale large plants, but also to energy storage facilities, commercial and industrial (C&I) rooftops, residential rooftops, data centres, and smart microgrids in rural areas. By doing this, more flexible energy generation solutions that are close to the point of use can be applied and the transmission and distribution setup can be minimised, thus saving costs and losses. Through this approach, power consumers can be transformed into power producers, which helps to achieve better power resilience for users and the whole society.

South Africa’s Electricity Minister Dr. Kgosientso Ramakgopa gave a keynote address at the forum, and commended Huawei for the role it is playing in infrastructure development in Africa and in greening South Africa’s energy systems. “Huawei is bringing technological advancements and innovations that help us keep pace with the developed and industrialised countries in the global north,” he said.

He indicated that his role as the electricity minister involves working with the private sector, including Huawei, to address the power deficit issue and boost a digital and sustainable future for South Africa.

He said, “The South African government is looking for blended financial facilities for the funding of alternative energy installations, making it more accessible to more people. At the same time, the government will also broaden the flow of participation by upskilling people in the technology of renewable energy systems.”

Chen Guoguang, President of Huawei Smart PV Product Line said that, with Huawei’s innovative solutions, it has achieved a very impressive carbon footprint globally. “By the end of 2022, Huawei Digital Power has helped our customers to offset 340 million tons of CO2 emissions, roughly the same as planting 470 million trees,” he said.

John van Zuylen, CEO of AFSIA(Africa Solar Industry Association), presented on the rapid adoption of solar technologies on the African continent, where almost every country now has some solar capacity. With power storage options becoming more accessible and more affordable, AFSIA predicts that Africa will soon outstrip other regions in its use of solar power supply. Huawei technologies currently power 25% of the world’s PV capacity, and so the company is well positioned to play a growing role on the continent.

In her presentation, CEO of the SAPVIA(The South African Photovoltaic Industry Association), Dr Rethabile Melamu, stressed the need to skill young South Africans to participate and take full advantage of the huge opportunities in this industry. “Huawei’s skills development initiative is incredible and we are partnering with them to make sure we get more young people skilled and accredited for the sector,” she said.

In addition, industry players also shared their experiences. For example, Bui Power Plant in Ghana shared the latest insights into PV and energy storage trends in their organisations and how Huawei technologies are contributing to their success.

In Conclusion, Leo Chen expressed Huawei’s commitment to Africa. He said, working with various partners, “over the past two decades, Huawei has brought ubiquitous connectivity to Africa. In the next two decades,Huawei is aiming to bring ubiquitous green power to the continent.”
Share:

MHE.KATAMBI: THAMANI YA UWEKEZAJI WA MIFUKO YA HIFADHI JAMII IMEFIKIA TRIL.14/-




Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (Mb) akijibu swali Bungeni leo tarehe 16 Mei, 2023, jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi amesema hadi kufikia Juni 30, 2022 thamani ya uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ilikuwa imefikia Sh.Trilioni 14.04.

Mhe.Katambi ameyasema hayo Mei 16, 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Halima Mdee.

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji tangu kuanzishwa kwa Mifuko hiyo ni kiasi gani cha fedha kimewekezwa na kila Mfuko na nini faida na hasara za uwekezaji huo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi amesema kiwango hicho ni kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulikuwa umewekeza Sh.Trilioni 6.03, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Sh.Trilioni 7.49 na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Sh.Bilioni 521.94.

Ametaja faida za uwekezaji huo kuwa ni kulinda thamani ya michango ya wanachama na kuhakikisha Mifuko inakuwa endelevu ili kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kulipa mafao.

“Aidha, uwekezaji huu huchangia pia kuongeza ajira, mapato ya Serikali kupitia kodi na kuchochea shughuli za uchumi,”amesema.

Hata hivyo, amesema kama ilivyo katika uwekezaji wowote kuna vihatarishi amabavyo vinaweza kusababisha hasara kwa baadhi ya uwekezaji, ambapo mifuko imevifanyia kazi kwa mujibu wa miongozo ya uwekezaji katika mifuko inayotolewa na Benki kuu ya Tanzania (BOT).
Share:

MWENYEKITI UVCCM TANGA ATEMBELEA MRADI WA BBT KATIKA CHUO CHA MLINGANO MATI MUHEZA ATOA NENO

 



MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM) Ramadhan Omary kulia akiwa na jembe akishiriki kulima na vijana kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mohammed Kawaida wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM)  Ramadhan  Omary kushoto akiangalia namba vitalu vya miche vilivyopandwa na vijana  kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa  Mohammed  Kawaida wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).


Na Oscar Assenga, MUHEZA 



MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM)  Ramadhan  Omary leo aliongoza  ziara ya kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Tanga kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa  Mohammed  Kawaida kutembelea Chuo cha Kilimo (Mati Mlingano )ambacho ni Miongoni mwa Vituo vya Mradi wa jenga kesho yako iliyo bora (BBT).

Katika ziara hiyo  aliwataka  vijana kuitumia fursa hiyo ya uwepo wa chuo hicho kwa manufaa yao binafsi na jamii inayowazunguka kwasababu serikali imetumia gharama kubwa kujenga kwaajili ajili ya kuwanufaisha na kuwaajiri Vijana kwenye sekta ya Kilimo,

"Mradi huu wa BBT ni moja kati ya miradi iliyotupa heshma kubwa vijana tuufanyeni kwa kwa ustadi na uaminifu mkubwa"Alisema Omary 

Mwenyekiti hiyo alitumia fursa hiyo kushauri uongozi wa chuo kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wakulima wa maeneo ya hayo na maeneo ya karibu kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima wa Maeneo hayo na kuweza kukuza kilimo bora kwa jamii inayokuzunguka,

"Mkoa wetu unafursa nyingi za kilimo kaimu mkuu wa chuo angalieni namna chuo hiki kitaweza kuwanufaisha vijana/ jamii inayo wazunguka ili tuwe na kilimo chenye tija"Alisisitiza Omary 

Aidha katika hatua nyengine Omary aliwataka  Makada wa CCM na Vijana wa Chuo cha Mati Mlingano kwa niaba ya vijana wote wa Tanga kuwa namna pekee ya Kumlipa  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.Samia  kuyasema mazuri anayoyafanya na kuyatangaza mema anayoyafanya kwa Watanzania wote kiujumla kwani ameyafanya mengi kwa ajili ya Watanzania.


"Kwa kweli sisi kama vijana katika mkoa wa Tanga tunapongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu hivyo kama vijana lazima tuzitangaze kazi hizo tusiishie kusema mama anaupiga mwingi "Alisema Mwenyekiti huyo 

"Lakini pia tumuombe Mungu atujalie viongozi wengi mithili ya Bashe kwa sababu unamuona kabisa anaguswa na changamoto za vijana na jamii ya Kitanzania"Alisema 

Share:

TBS YATEKETEZA SHEHENA YA BIDHAA HAFIFU ZA VIPODOZI NA CHAKULA MKOANI MWANZA


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

SHEHENA ya bidhaa mbalimbali vikiwemo vipodozi vyenye viambata vya sumu zenye uzito wa tani sita zimeteketezwa baada ya kuondolewa sokoni kutokana na kutokidhi matakwa ya viwango.

Bidhaa hizo zimeteketezwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika dampo ya Buhongwa Jana, jijini Mwanza baada ya kukamatwa kwenye mikoa sita ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo, Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown alitaja bidhaa zilizoteketezwa mbali vipodozi vyenye viambata vya sumu kuwa ni pamoja vyakula vilivyokwisha muda wa matumizi.

Kwa upande wa vipodozi vilivyoteketezwa, Brown alisema vilipigwa marufuku kutumika nchini kutokana na kuwa na madhara ya kiafya kwa watumiaji ikiwemo kusababisha kansa.


Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa shirika la viwango Tanzania pale wanapokumbana na bidhaa wanazotilia mashaka vikiwemo vipodozi vilivyozuiwa katia soko la Tanzania, kwani shirika hilo lipo kwa ajili ya kulinda walaji na kuhakikisha wanapata bidhaa kulingana na thamani ya fedha zao

Aidha, alitoa mwito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuangalia muda wa mwisho wa matumizi kwenye vifungashio vya bidhaa wanazotaka kununua ili kuepuka kununua bidhaa zilizoisha muda wake wa matumizi ambazo zinakuwa na madhara kiafya.
Share:

Monday, 15 May 2023

USHINDI RAHISI MERIDIANBET KASINO

 


Sloti ya Wild Hot 40         

Sloti ya Hot Wild 40 inakuja na bonasi ya mzinguko ya bure kama ukishinda, Jackpot za aina 3 huku ukiwinda ushindi wako kwa njia rahisi, yote haya yanawezekana kama ukicheza kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

 

Moja kati ya mchezo ambao unakupa matumaini ya kuongeza hela kwenye dau lako uliloweka ni sloti ya Wild Hot 40 kutoka kasino mtandaoni, inakuhakikishia ushindi mkubwa kwa kuwa ina Jackpot 3 za ushindi ambazo ni GoldPlatinum na Diamond

 

Jinsi ya Kucheza Sloti ya Wild Hot 40

Sloti hii ya Wild Hot 40 inayopatikana Meridianbet kasino ya mtandaoni, inasifika kwa uchezaji wake rahisi haswa katika muundo wa alama za matunda na muundo wa kolamu 5 na mistari 40 ya malipo.

 

Matunda hayo ni NdiziTufaa (Apple) na Strawberry ambapo ukipata alama hizi 5, utapata mara 2.5 ya dau uliloliweka. Ukipatia alama 5 za Kengele, unarudishiwa mara 5 ya dau uliloliweka. Ukipatia alama ya namba 7 za bahati, utapata mara 10 ya dau uliloliweka. Ukipatia alama 5 za Wild, utarudishiwa mara 25 ya dau uliloweka wakati ukipatia alama 5 za Scatter utarudishiwa zaidi ya mara 500 ya dau lako. 

 

Kubwa Zaidi ni kwamba Sloti hii kutoka kasino ya mtandaoni inakuja na  chaguo la Gamble ambalo litakuletea mara 2 ya faida uliyoipata kwenye ushindi wako. 

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko 50 ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.



Share:

SERIKALI YATHIBITISHA HAKUNA MWANANCHI ALIYENYANYASWA WALA MIFUGO ILIYOPORWA KATIKA SAKATA LA MBARALI

Na John Mapepele.

Serikali imesema hakuna mwananchi aliyenyanyaswa kijinsia, wala mifugo ya mwananchi yeyote (Ng’ombe 250) kuporwa au taarifa ya mtu yeyote kutaka kujinyonga pia hakuna uthibitisho wa vitendo vya wanawake kuvuliwa nguo na Askari wa Uhifadhi katika tukio la Askari wa TANAPA kuwaondoa ndani ya Hifadhi ya Ruaha Wananchi watano (5) wilayani Mbarali katika Mkoa wa Mbeya kama ilivyoelezwa hivi karibuni Bungeni na Mbunge wa jimbo hilo wakati alipoomba Mwongozo kwa Mhe. Spika akiomba Bunge lihairishe mjadala ili kujadili suala hilo kama dharura.

Akiwasilisha taarifa ya Serikali bungeni leo Mei 15, 2023 kuhusu tukio hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema ni kweli kuwa Mei 6 mwaka huu, Askari wa TANAPA wakiwa katika doria za kawaida walifika katika Kijiji cha Mwanavala na helikopta katika maeneo yaliyopo ndani ya Hifadhi ya RUAHA ambapo ni sawasawa na KM 20 ndani ya hifadhi ya TANAPA kutoka ulipo mpaka ambalo ni eneo la hifadhi lisiloruhusiwa Wananchi kuingia kwa kuwa ni karibu na Mto RUAHA ambao ni sehemu ya chanzo cha kupeleka maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Ameongeza kuwa Askari husika wakiwa katika doria za kawaida walibaini ujenzi wa maboma mawili mapya ya mifugo ndani ya hifadhi ya RUAHA kinyume cha Sheria ambapo katika harakati za kutaka kuwakamata watuhumiwa, Wananchi hawa, waliongia kijinai na kinyume cha Sheria katika eneo la Hifadhi walizuia kutiwa nguvuni kwa kurusha mawe, fimbo, mishale na silaha nyingine za jadi na kusakizia mbwa askari wa Jeshi la Uhifadhi kwa lengo la kuwadhuru askari hao.

“Miongoni mwa silaha za jadi zilizorushwa zilitishia usalama wa Askari Jeshi la Uhifadhi waliokuwa katika kazi yao halali ya uhifadhi na kupelekea kitako cha bunduki aliyokuwa nayo askari kuvunjika. Nguvu waliyotumia askari kujilinda ilipelekea majeraha kwa Wananchi hao na askari Jeshi kulazimika kuwadhuru mbwa waliowasakizia kwa hofu ya kulinda maisha yao.” Amesisitiza Mhe.Mchengerwa

Ameongeza kuwa baada ya mivutano hiyo Wananchi wote waliopata majeraha walipelekwa hospitali na walipatiwa matibabu ambayo yaligharamiwa na TANAPA na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida pamoja na kwamba tukio husika limetokea ndani ya hifadhi, Wizara iliona ni busara kutoa pole ya shilingi milioni moja kwa kila mwananchi aliyeathirika na tukio hilo.

“Ikumbukwe mbele ya Bunge lako tukufu kuwa eneo lilipotokea tukio hili ni karibu na eneo yalipotokea mauaji ya Askari wa Uhifadhi Ndugu Yusti Matei na askari wa Wanyamapori wa Vijiji Ndugu Isaya Mwambe miaka michache iliyopita. 

Takwimu za Wizara zinaonesha kwamba Askari wa Jeshi la Uhifadhi 15 wameuwa na wengine 51 wamejeruhiwa na Wananchi wavamizi ndani ya Hifadhi mbalimbali nchini wakiwa wanatekeleza majukumu yao.” Amefafanua, Mhe. Mchengerwa

Aidha, Mhe.Mchengerwa amesema Askari wote waliohusika na tukio hilo waliandikishwa maelezo Polisi kufuatia maelekezo ya Serikali na maelekezo yake. Kufuatia tukio liliojitokeza Wilayani Mbarali Serikali imetoa maelekezo sita.

Akisoma maelekezo hayo Mhe. Mchengerwa amesema Askari wote wa uhifadhi nchini watumie weledi wao katika kudhibiti uvamizi kwenye hifadhi badala ya kutumia nguvu kupita kiasi katika utekelezaji wa himasheria, ambapo amesisitiza kuwa ni pamoja na kuwakamata na kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya Sheria ili Sheria ichukue mkondo wake.

Aidha amesema tukio la Mbarali limetokea ndani ya Hifadhi ya Ruaha takriban kilomita10 baada ya mpaka mpya wa hifadhi na kilomita 20 ndani ya mpaka wa zamani karibu kabisa na Mto Ruaha ambao ndio mto tegemezi unaozalisha maji yanayotegemewa katika Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo Serikali kupitia kodi za wananchi inatumia zaidi ya Trilioni 6.5 kulijenga, lakini pia ndio mto tegemezi wa maji ya kunywa lakini na chanzo cha maji katika mito mbalimbali nchini.

“Hii inadhihirisha kwamba wananchi hao waliingia ndani ya hifadhi kimakosa, bila kufuata taratibu za kisheria. Eneo hili halina ruhusa ya kulima wala kufuga, wala mapito ya wananchi na hii ni kwa kuzingatia hali halisi ya uwandani kama nilivyoeleza hapo juu sambamba na kulinda maeneo oevu ili mito iweze kurejesha mikondo yake ya asili ya mitiririko yake ya maji kama nilivyoeleza.” Ameelezea Mhe. Waziri.

Amewasihi wananchi kufuata sheria na taratibu zote za maeneo yaliyohifadhiwa kisheria kwa maslahi ya watanzania wote kwa ujumla wa vizazi vya sasa na baadaye pia ameendelea kuwasihi Waheshimiwa Wabunge, kusaidia katika kutoa elimu kuhusu umuhimu wa maeneo haya yaliyohifadhiwa.

Amewataka Wahifadhi wote nchini kuwawashirikisha viongozi wa Chama na Serikali katika kutatua migogoro kati ya wananchi na maeneo ya hifadhi ikiwemo kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo; lakini watambue kwamba wananchi ni wahifadhi namba moja hivyo waboreshe mahusiano baina yao na wahifadhi wananchi na kila kiongozi wa uhifadhi katika eneo lake atapimwa kwa namna anavyoshirikiana na wananchi katika maeneo yao ambapo amesisitiza wakaimarishe mahusiano yao na wananchi na vijiji vinavyopakana na hifadhi.

Pia Wahifadhi wote nchini waendelee kuimarisha doria, kuweka alama za mipaka, kuweka mabango na kulima mkuza ili kudhibiti uvamizi katika maeneo ya hifadhi kwa mustakabali wa nchi yetu ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mifugo, kufua umeme na kilimo hususan programu za umwagiliaji.

Ameiagiza TANAPA kuanza ujenzi wa Rangers Post (kituo cha Askari wa Uhifadhi) ili kuimarisha ulinzi katika eneo la Hifadhi ya Ruaha Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa amesema katika kupata suluhisho la kudumu la migogoro katika hifadhi hii kongwe iliyoanzishwa mwaka 1910 iliyojulikana kwa jina la hifadhi ya Saba, mwaka 1946 ilibadilishwa jina na kuitwa RUNGWA na mwaka 1964 Mwalimu Nyerere aliporidhia iitwe RUAHA, Serikali inakusudia kumega eneo la hifadhi lenye ukubwa wa takribani hekta 34,000 ili zitumike kwa shughuli za maendeleo ya wananchi ambapo Wananchi wa Vijiji husika watajipangia mpango bora wa matumizi ya ardhi.

Aidha Serikali itaondoa ekari 900 ili zitumike kwa shughuli za malisho. 

Wiki hii Serikali itakamilisha uthamini wa mali za wananchi katika baadhi ya maeneo ya Kijiji cha Mwanavala ili taratibu zingine za fidia ziendelee.

 Vilevile napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa Serikali imekamilisha uwekaji wa vigingi katika mpaka mpya wa hifadhi ya Ruaha.

Amesema kwa sasa Serikali inakamilisha mchakato wa kuandaa rasimu ya Tangazo la Serikali (Government Notice – GN) jipya la Hifadhi ya Taifa Ruaha na mara taratibu husika zitakapokamilika Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali italeta Azimio Bungeni ili kupata ridhaa ya Bunge kama ilivyo kwa mujibu wa sheria na hatimaye kuwasilishwa GN hiyo kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua stahiki.
Share:

PROGRAM YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI AFDP KUBORESHA MAZINGIRA YA UVUVI KILWA.


Mhandisi Erick Isack aliyesimama, akizingumzia namna ambavyo programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi, itakavyoboresha sekta ya uvuvi mkoani Lindi.
Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu na Wizara ya Fedha, wakiangalia dagaa walioanikwa katika kichanja cha kienyeji, katika kata ya  KILWA Kivinje,wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo yatakayoteleza programu ya KILIMO na UVUVI (AFDP) mkoani Lindi Leo.
Picha ikionesha washiriki wa Kikao cha ugeni kutoka programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) wataalam na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya KILWA,wakati Ujumbe huo ulipotembelea maeneo yatakayoteleza programu hiyo mkoani Lindi
Mtaalamu wa masuala ya Lishe na Jinsia Bi. Irene Mbando, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizingumzia namna ambavyo Programu Hiyo itakavyohusisha masuala ya Lishe na jinsia.
 Picha ikionesha Dagaa walioanikwa chini, katika kata ya KILWA Kivinje mkoani Lindi.
Kulia Bw. Robert Lee mtaalam wa Uvuvi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo Duniani (IFAD) akijadili jambo na Bw. Richard Abila mtaalamu wa Ufugaji wa viumbemaji  kutoka IFAD.
Mfanya biashara wa dagaa,katika kata ya KILWA kivinje Wilayani KILWA, Mkoani Lindi akianika dagaa katika chanja ya kienyeji, ambapo programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) Itaenda kuwajengea chanja za kisasa.


Na; Mwandishi Wetu - KILWA

IMEELEZWA kuwa, Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi AFDP inategemea kwenda KUBORESHA MAZINGIRA na maisha ya wavuvi wilayani Kilwa Mkoani Lindi.

Hayo yamesemwa mapema Leo tahehe 15 Mei 2023, Mkoani Lindi na Mtaalamu wa masuala ya mazingira wa mradi huo, Mhandisi Erick Isack kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakati Ujumbe wa Programu hiyo ulipokuwa katika Ziara ya kikazi Mkoani hapo.

Mhandisi Isack amesema programu hiyo itasaidia kujenga kiwanda Cha kuchakata samaki katika maeneo ya bandari ya uvuvi KILWA Masoko na ghala la kutunzia samaki. Sambamba na hilo programu hiyo pia itaenda kujenga vichanja vya kisasa vya kukaushia dagaa katika kata ya KILWA Kivinje.

Kwa Upande wake mtaalam wa masuala ya Lishe na jinsia Bi. Irene Mmbando alisema, programu itazingatia ushiriki wa jinsia zote ikiwa wanawake watashiriki Kwa asilimia sitini (60%) na Asilimia arobaini (40%) vijana.

Aliongeza Kwa kusema kuwa Mradi huo unalenga kufika kaya laki mbili na sitini ambazo zitahusika katika kilimo, uvuvi na ufugaji wa viumbemaji.

Akizingumzia masuala ya Lishe, mtaalamu huyo Alisema programu hiyo inakwenda kuzingatia maswala ya Lishe katika kaya husika.

Awali akiongea katika mazungumzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya KILWA Bw. Eston Mngilangwa alisema, programu hii imezingatia mazingira halisi ya maeneo husika "Kwa upande wangu naona kama Lindi tumependelewa, tumeletewa miradi sita, programu hii tunaipokea Kwa mikono miwili, Tunashukuru sana, tunawahakikishia kuwa Mradi huu utaenda kuleta matokeo chanya, tumeshafanya maandalizi kwenye kila eneo,kama itatokea Kuna mahala tumekosea itakuwa ni suala la uelewa tuu." Alibainisha Mkurugenzi Huyo.

Ujumbe huo kutoka Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi, inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,  uliohusisha wataalam kutoka IFAD, Wizara MIFUGO NA UVUVI, FEDHA na Wizara ya Kilimo itaendelea na ziara yake ya kikazi kisiwani Zanzibar wiki hii.

= MWISHO =
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger