Thursday, 11 May 2023

WANAFUNZI WAWILI WAFA KWA AJALI YA ROLI NA WENGINE ZAIDI KUJERUHIWA







Na Dotto Kwilasa, DODOMA 

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma, Dk. Ernest Ibenzi amethibitisha kupokea miili ya wanafunzi wawili wa shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi mkoani Dodoma waliokufa katika ajali ya lori aina ya Canter lenye namba T519 DSY walilokuwa wamepanda kupinduka wakati wakiwa safarini kwenda kwenye kambi ya michezo ya Umiseta.

Akizungumza na waandishi wa habari Dk.Ibenzi pia amethibitisha kupokea majeruhi  31 wanaohusishwa na ajali hiyo na kwamba wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa.

“Majira ya saa 7:30 tulipokea majehi hao wanafunzi kutoka shule ya sekondari Mpalanga na wanne kati yao wamefanyiwa upasuaji na wengine walikuwa na majeraha madogo ya majera wanaendelea vizuri”amesema Dk. Ibenzi

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya Rufaani ya mkoa wa Dodoma wameeleza chanzo Cha ajali hiyo kuwa ni  mwendokasi .

Amani Yobwa, mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Mpalanga, alisema walipanda usafiri huo kwenda kushiriki michezo ya Umiseta ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika katika kijiji cha Magaga.

“Tulipakiwa kwenye gari lile asubuhi ili kuwahi michezo ya Umiseta lakini tulipofika katika kijiji cha Chidilo kuna eneo kuna kona kali dereva alipokata kona gari likapoteza mwelekeo na kupinduka na kusababisha wenzetu wawili kufa na sisi kujeruhiwa’alisema Yobwa

Magreth Masinga mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo alisema sababu za ajali hiyo ni mwendo kasi na tatizo kubwa ni aina ya gari walilotumia ambalo siyo kwa ajili ya abiria.

“Kama tungepanda gari la abiria kusingekuwa na shida kama hii kwani alipokata kona wanafunzi waliyumba na kulala upande mmoja na kusababisha kupinduka kwa gari hivyo tunaomba magari ya mizigo yasitumike kubeba abiria”alisema Masinga

Mmoja wa wazazi wa wanafunzi waliopata ajali hiyo Manase Matonya, alisema wanaiomba serika kwenye matukio mbalimbali ya wanafunzi kuacha matumizi ya magari ya mizigo kwa ajili ya kubeba abiria.

“Siku hizi hata minadani abiria hawapandi magari ya mizigo lakini tunashangaa leo watoto wetu kupanda gari la mizigo kwa ajili ya kwenda kwenye michezo ya Umiseta”alisema

Aidha,taarifa iliyotolewa na uongozi wa wilaya ya Bahi inasema kuwa ajali ya gari hilo imetokea kijiji cha Chidilo majira ya saa 5 Asubuhi Kata ya Mpalanga,Tarafa ya Chipanga.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa gari ilikuwa aina ya canter ilikuwa imebeba jumla ya wanafunzi 46 wakitokea Mpalanga Sekondari kwenda Magaga Sekondari kwenye michezo ya Umiseta.

“Wanafunzi wawili wa kike wamefariki dunia hapohapo majina yao ni Neema Yohana Hoya (17) kidato cha tatu mkazi wa Chidilo na Magreth Juma (19)  mkazi wa Nholi na wanafunzi 31 wamepelekwa hospitali ya Rufaani Dodoma kwa matibabu zaidi na wengine 14 wamepatiwa matibabu zahati ya Mpalanga”inasema sehemu ya taarifa hiyo


  




---------- Forwarñded 
Share:

JINSI NILIVYOWEZA KUWA MWANASOKA TAJIRI KENYA

Ukweli ni kwamba kila mtu hutaka ndoto yake maishani itimie ili aweze kuwa na maisha mazuri hapo baadaye, bila hivyo, huwa ni vigumu mtu kuwa na amani maishani kwani mara nyingi kushuhudia kuishi nje ya ndoto zako ni jambo lenye kuumiza sana.

Nilikuwa kijana ambaye nilizaliwa katika familia ya walalahoi kwenye kauti ya Migori, Kenya, ndoto yangu ilikuwa ni kuwa mwanasoka maarufu nchini, hiyo ilikuwa ndio talanta yangu hasa.

Nilivutiwa na wachezaji kama vile Mbwana Samatta wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa barani Ulaya, wazazi wangu walinitia moyo kwani pia walifahamu kuwa iwapo ningefaulu kwenye soka maisha yao pia yangebadilika.

Nilianza kufuatilia usajili wa wachezaji katika vilabu mbalimbali nchini na kila mara nilitemwa wakisema kuwa sikuwa na uwezo, hii ilikuwa ni mojawapo ya changamoto zilizonifanya kukaribia kukata tamaa.

Kadiri siku zilipoenda ndipo ndoto yangu ya kuwa mchezaji maarufu zilikuwa zinapotea, marafiki walinicheka kwani wengi wao walisema sikuwa na kipaji ingawa mimi nilijiamini sana kuwa nina uwezo huo.

Baba yangu siku moja alinieleza kuna tovuti (www.african-doctors.com) inaweza kunisaidia kufikia ndoto zangu kwani watu wengi wameweza kusaidika kupitia tovuti hiyo. Nilipitia kila kitu katika tovuti hiyo na kubaini kuna watu wengi wameweza kupata mafanikio kupitia wao, African Doctors.

Nilikusanya fedha ya nauli kwani nilitaka kufika katika Ofisi za African Doctors pande za Nakuru ili nipate usaidizi wao kwani ndoto yangu ya kuwa mwanasoka maarufu ilikuwa inanisumbua sana.

Kwa kweli African Doctors alinitabiria kuwa kipaji changu kilikuwa ni kucheza kabumbu, nilishangaa alivyojua lakini akanieleza kuwa ana uwezo huo.

Siku tatu baada ya kutoka kwa African Doctors, nilipata nafasi ya kuichezea klabu moja ya ligi ya Kenya, nilicheza kwa muda wa miezi nane hivi. Maisha yangu pamoja na wazazi wangu yalianza kubadilika kwa kasi, baada ya muda mchache nilipata klabu China na hapo nililipwa mshahara mzuri tu.

Kumbuka African Doctors wanasuluhisha mizozo ya ndoa, migogoro ya mashamba n.k, wanatibu magonjwa kama kisukari, kisonono, presha, upungufu wa nguvu za kiume na mengineo.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:

MAKALLA ARIDHISHWA NA UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI KIBAMBA





Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa maji katika jimbo la Kibamba baada ya ziara ya mtaa kwa mtaa kwenye Kata ya Kwembe na Kibwegere na kujionea upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi baada ya kuwepo changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa maji.

Mhe. Makalla amesema lengo la ziara hii ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan la kufuatilia na kujiridhisha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wanaoishi pembezoni ya miji.

"Nipo hapa kutekeleza agizo la Mhe. Rais Mama Samia Suluhu la kupita, kukagua na kuona ni kwa namna gani wananchi wanapata huduma ya maji. Nimeridhishwa na hali niliyoikuta niwapongeze DAWASA kwa kazi nzuri vile mnavyotuandikia kwenye ripoti ndio vitu tunaviona vimetekelezeka hakikisheni huduma inakua endelevu na kila mwananchi aliyeomba huduma anaipata." amesema Mhe. Makalla.

Akitoa taarifa fupi ya upatikanaji huduma kwa eneo la Kibamba, Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA-Kibamba Ndugu Elizabeth Sankere amesema ndani ya Kata ya Kwembe na Kibwegere changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji kwa ilichangiwa na sababu za kijiographia ya eneo na vilevile ongezeko la watu ambapo ilipelekea miundombinu kuzidiwa na kutokidhi mahitaji ya wananchi huku akibainisha kwa sasa huduma inapatikana kwa asilimia 90 baada ya jitihada zilizofanywa na Serikali kupitia DAWASA ambapo miradi imefanyika na inaendelea kufanyika kwa maeneo yaliyobaki kupata huduma.

"Kwa upande wa ofisi ya DAWASA Kibamba tunahudumia kata tano zenye wateja 25,000 na hali ya upatikanaji maji kwenye kata hizo ni asilimia 90. Tumefanikiwa kuwa na mtandao wa mabomba wa zaidi ya kilomita 200,000 kwa eneo lote tunalolihudumia"aliongeza

"Kwa maeneo yaliyokuwa na changamoto hapo awali, Mamlaka ilipeleka miradi ya kuongeza mtandao wa maji na jitihada zinaendelea kwa maeneo yaliyobaki" amesema Ndugu Elizabeth

Naye, Ndugu Joyce Kijumbe Mkazi wa Mji mpya Kwembe ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwaondolea adha ya maji iliyokuwepo katika mtaa wao kwa mda mrefu hali ilyowapelekea kuingia gharama kubwa kupata huduma ya maji

"Kwa kweli tunamshukuru Mhe. Rais Mhe. Samia Suluhu ametuheshimisha sisi wanawake tumepitia shida kubwa lakini sasa tunafuraha maji yapo, tunafanya kazi zetu kwa raha na gharama imepungua pia" ameeleza Ndugu Joyce


Share:

TRA YAENDESHA KAMPENI YA TUWAJIBIKE, YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA, WANUNUZI WA BIDHAA...."UKINYWA BIA, SODA DAI RISITI"

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga imefanya ukaguzi kwa wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya TUWAJIBIKE inayolenga kuwakumbusha na kuwahimiza wafanyabiashara kuwajibika katika kutoa risti halali za EFD na wateja wa wafanyabiashara kuhakikisha wanapata risiti sahihi.


Ziara hiyo imefanyika leo Mei 11,2023 Mjini Shinyanga ambapo TRA Mkoa wa Shinyanga imekutana na wafanyabiashara na wateja wa wafanyabiashara na kuwasisitiza umuhimu wa utoaji risiti na kudai risiti.


Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Ndessa amesema Kampeni ya Tuwajibike ni Kampeni ambayo imeanzishwa na TRA na kuzinduliwa rasmi Mei 3,2023 na itakuwa endelevu na imepangwa kutekelezwa kote nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa TRA.

“Kampeni ya Tuwajibike ina malengo makuu mawili ambayo ni kuwakumbusha na kuwahimiza wafanyabiashara kuwajibika katika suala ya utoaji wa risiti halali za EFD kwa kila bidhaa wanazouza na huduma wanazozitoa lakini pia inawakumbusha na kuwahamasisha wanunuzi ambao ni wateja wa wafanyabiashara kuwajibika kwa kuhakikisha wanadai risiti halali za EFD pamoja na kuzikagua ili kujiridhisha kuwa risiti hiyo inakidhi vigezo vyote muhimu vya risiti halali ya EFD ili pesa wanazolipa na risiti iwe sahihi kwa kiwango walicholipa”,amesema Ndessa.

Amevitaja vigezo vikuu vinavyoonesha kuwa risiti halali ya EFD ni jina la muuzaji,tarehe na muda halisi ya mauzo, kiasi/gharama halisi ya pesa iliyonunuliwa bidhaa au huduma pamoja na TIN na jina la mnunuzi

Amefafanua kuwa TRA imeamua kuhimiza na kusimamia suala la wafanyabiashara kutoa risiti sahihi wanapouza bidhaa au kutoa huduma na wanunuzi kudai risiti kwa malipo halali waliyoyafanya hali ambayo itasaidia sana katika kuhakikisha mapato ya serikali kuu yanafika katika mfuko sahihi.


“Kumetokea kawaida ya aidha wafanyabiashara kutoa risiti pungufu au kutotoa risiti kabisa na wanunuzi kutodai risti hii inamaanisha kwamba uwezekano mkubwa wa pesa ya serikali kutofika kule inakoelekea”,amesema Ndessa.


“Kampeni ya Tuwajibike inahusu biashara na huduma zote hivyo itahusisha biashara zote nchini ila mkazo zaidi utawekwa katika maeneo korofi zaidi katika utoaji wa risiti za EFD kama vile eneo la usafirishaji wa vifurushi au vipeto vinavyokwenda mikoani kwa usafiri wa mabasi. Eneo jingine ni kumbi za starehe ikiwemo baa na kumbi za muziki. Ukinywa bia au soda dai risiti”,amesisitiza Meneja huyo wa TRA Mkoa wa Shinyanga.


Amesema hatua za kisheria zitakazochukuliwa kwa mujibu wa sheria ya adhabu ya makosa katika matumizi ya mashine za EFD ambapo mfanyabiashara atayebainika kutokutoa risiti halali ya EFD au kufanya udanganyifu wowote ule atatozwa faini ya kuanzia shilingi 3,000,000/= hadi shilingi 4,500,000/= au kifungo kisichozidi miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja.


“Kwa mnunuzi atakayebainika kufanya manunuzi bila ya kudai risiti halali ya EFD atatozwa faini ya kuanzia shilingi 30,000/= hadi shilingi 1,500,000/=”,amesema Ndessa.


“Ombi langu kwa watanzania kwa lengo la tuwajibike, kitu ambacho ni endelevu tunawashauri kwa kila anayefanya biashara ahakikishe anatoa risiti na kama kuna tatizo lolote awasiliane na TRA haraka iwezekanavyo na mnunuzi ahakikishe anadai risiti kwa malipo sahihi aliyofanya ili kuepuka adhabu inayoweza kuipata kwa kutodai risiti”,amesema.

"Tunapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara wote kuwajibika kwa kutoa risiti halali za EFD bila ya kushurutishwa na wanunuzi kudai risiti halali za EFD kwa kila manunuzi watakayofanya ili kuepuka usumbufu usio wa lazima na wakati huo huo kuisaidia serikali kutimiza malengo yake kuwaletea wananchi maendeleo na kukuza uchumi wan chi yetu. Tuwajibike”, ameongeza Ndessa.


Kwa upande wake, Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Mkoa wa Shinyanga, Estomih Mossi amesema njia inayotumika kuendesha kampeni ya Tuwajibike ni pamoja na kufuatilia utoaji risiti halali za EFD nchi nzima na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofuata sheria katika utoaji wa risiti halali za EFD kama vile kutokutoa risiti ya EFD, kutoa risiti yenye mapungufu, kutumia risiti moja ya kushinikiza mizigo kadhaa, kufanya biashara ya kuuza risiti pasipokuwa kwa watu wengine ambao hawana mashine za EFD na mnunuzi kutokudai risiti baada ya kununua bidhaa au huduma.


Nao baadhi ya Wafanyabiashara akiwemo Adonikamu Kweka na Manka Geofrey Mushi wamesema hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wafanyabiasha kutumia mashine za EFD huku wakieleza kuwa utoaji risiti pia unasaidia sana katika kutunza kumbukumbu za mauzo.


Kwa upande wao wanunuzi wa bidhaa akiwemo Moyo Bunzali na Khamis Kasole wamesema pindi mfanyabiashara anapotoa risiti na mnunuzi kudai risiti inasaidia katika kukusanya kodi za serikali kwa halali na kwamba ukikwepa risiti maana yake unaiibia serikali.

Wasiliana na Kituo cha Huduma kwa MlipaKodi kwa namba za bure 0800 750 075 au 0800 780 078 au 0800 110 016 . Pia anaweza kutumia ujumbe kwa njia ya WhatsApp namba 0744 233 333 au kutumia barua pepe kwenda huduma@tra.go.tz au kwenye mitandao ya kijamii.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Ndessa akielezea kuhusu Kampeni ya Tuwajibike inayoendeshwa na TRA inayolenga kuwakumbusha na kuwahimiza wafanyabiashara kuwajibika katika kutoa risti halali za EFD na wateja wa wafanyabiashara kuhakikisha wanapata risiti sahihi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Ndessa akielezea kuhusu Kampeni ya Tuwajibike inayoendeshwa na TRA inayolenga kuwakumbusha na kuwahimiza wafanyabiashara kuwajibika katika kutoa risti halali za EFD na wateja wa wafanyabiashara kuhakikisha wanapata risiti sahihi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Ndessa akielezea kuhusu Kampeni ya Tuwajibike inayoendeshwa na TRA inayolenga kuwakumbusha na kuwahimiza wafanyabiashara kuwajibika katika kutoa risti halali za EFD na wateja wa wafanyabiashara kuhakikisha wanapata risiti sahihi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Faustine Cosmas Ndessa akielezea kuhusu Kampeni ya Tuwajibike inayoendeshwa na TRA inayolenga kuwakumbusha na kuwahimiza wafanyabiashara kuwajibika katika kutoa risti halali za EFD na wateja wa wafanyabiashara kuhakikisha wanapata risiti sahihi.

Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga wakikagua risiti ya bidhaa alizokutwa nazo mwananchi aliyekuwa anasafirisha magodoro ambapo mwananchi huyo alikutwa na risiti halali ya bidhaa alizopewa kuzisafirisha.
Msafirishaji mizigo akielezea umuhimu wa kudai risiti wakati wa kununua bidhaa wakati maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga walipomsimamisha kukagua kama ana risiti ya bidhaa alizonunua ambapo mwananchi huyo alikutwa na risiti ya bidhaa alizopewa kuzisafirisha
Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Mkoa wa Shinyanga, Estomih Mossi akizungumza wakati wa ukaguzi wa risiti kwa wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa Mjini Shinyanga
Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye duka la mfanyabiashara Adonikamu Kweka wakati wakiendelea kukagua risiti za bidhaa
Mfanyabiashara Adonikamu Kweka (kulia) akionesha risiti ya bidhaa alizouza. Kushoto ni Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Mkoa wa Shinyanga, Estomih Mossi
Mfanyabiashara Adonikamu Kweka akielezea umuhimu wa kutoa risiti
Maafisa wa TRA wakiondoka kwenye duka la Mfanyabiashara Adonikamu Kweka
Mfanyabiashara Manka Mushi akielezea umuhimu wa kutoa risiti
Mnunuzi wa bidhaa Moyo Bunzali  akielezea umuhimu wa kudai risiti
Waafisa wa TRA wakiwa katika duka la Mfanyabiashara Emmanuel Lazaro
Mnunuzi wa bidhaa Khamis Kasole akielezea umuhimu wa kudai risiti
Bango likiwa nje ya Kumbi ya Starehe maarufu  The Dees's Lounge Mjini Shinyanga inayohamasisha kudai risiti
Maafisa wa TRA wakikagua risiti katika Kumbi ya Starehe maarufu  The Dees's Lounge Mjini Shinyanga 
Maafisa wa TRA wakikagua risiti katika Kumbi ya Starehe maarufu  The Dees's Lounge Mjini Shinyanga 
Maafisa wa TRA wakikagua risiti katika Kumbi ya Starehe maarufu  The Robi's Bar & Grill Mjini Shinyanga 
Maafisa wa TRA wakikagua risiti katika Kumbi ya Starehe maarufu  The Robi's Bar & Grill Mjini Shinyanga 
Share:

GGML KILI CHALLENGE - 2023 KUKUSANYA BILIONI 2 KUDHIBITI VVU/UKIMWI

Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa harambee ya uchangiaji wa fedha za kudhibiti maambukizi ya VVU/ Ukimwi kupitia kampeni hiyo ya GGM Kili Challenge kwa mwaka 2023. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu pamoja na wadau wengine waliohudhuria hafla hiyo.
Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa harambee ya uchangiaji wa fedha za kudhibiti maambukizi ya VVU/ Ukimwi kupitia kampeni hiyo ya GGM Kili Challenge kwa mwaka 2023.

NA MWANDISHI WETU
KAMPENI ya GGML Kili Challenge inayoratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) mwaka huu inatarajiwa kukusanya dola za Marekani milioni moja sawa na Shilingi za kitanzania bilioni 2.3.


Fedha hizo ambazo hukusanywa kila mwaka, hulenga kuchangia juhudi za serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia malengo ya sifuri tatu yaani kupunguza kabisa kwa kufikia asilimia sifuri ya maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa pamoja na sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI.


Hayo yamebainishwa jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo katika hafla ya uzinduzi wa harambee ya uchangiaji wa fedha hizo kupitia kampeni hiyo ya GGM Kili Challenge kwa mwaka 2023.


Mbali na kuishukuru Serikali kwa kuunga mkono kampeni hiyo iliyoasisiwa mwaka 2002, Shayo alisema wakiwa wadau wa mapambano haya ya UKIMWI na VVU, GGML imepokea msaada ambao uliiwezesha Kili Challenge kupiga hatua kubwa hadi kufikia kuwa mfuko wa kimataifa, wenye kushirikisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.


“Mwaka huu tumekuja tena kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, hivyo GGM kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) tunawakaribisha sana wadau wetu na makampuni mbalimbali kuchangia na kushiriki kampeni hii.


“Kipekee tunapenda kutambua ushirikiano wa baadhi ya makampuni na taasisi mbalimbali ambazo tayari zimeshajitokeza kuchangia mfuko katika mwaka huu wa 2023. Nina imani wadau waliojitokeza leo watatusaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya kukusanya bilioni 2.3,” alisema.


Alisema VVU/UKIMWI bado ni tatizo kubwa nchini kwani takwimu za maambukizi mapya ya VVU haziridhishi, hususani kwa makundi maalum wakiwemo vijana.


Awali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu aliipongeza GGML na TACAIDS kwa kuendelea kuutumia mlima Kilimanjaro kama kivutio kinachotumika kukusanya fedha kwa ajili ya mwitikio wa VVU na UKIMWI.
Alisema jambo hilo limechangia kwa kiasi kikubwa katika kuutangaza mlima huo maarufu duniani, na hivyo kuongeza idadi ya watalii.

“Nakaribisha mawazo, ushauri kutoka kwenu na wadau wengine wa jinsi ya kuboresha zaidi kampeni hii,” alisema.


“Natoa wito kwa watu binafsi, mashirika, taasisi na makampuni mengine kuiga mfano wa GGML kwa kujitoa zaidi kuchangia rasilimali za mwitikio wa VVU na UKIMWI nchini, hususan katika kipindi hiki ambapo michango ya wahisani kutoka nje ya nchi inaendelea kupungua kwa sababu mbalimbali,” alisema.


Zoezi hilo la kupanda mlima linatarajiwa kuanza tarehe 14 Julai na kushuka tarehe 20 Julai mwaka huu.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 11,2023




















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger