Wednesday, 22 March 2023

BENKI YA TADB, HEIFER INTERNATIONAL WAENDESHA MKUTANO WA WADAU SEKTA YA MAZIWA SHINYANGA


Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga ukiendesha wa HEIFER International na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Shirika la HEIFER International wameendesha Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.

Mkutano huo umefanyika leo Machi 22, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa maziwa pamoja na viongozi wa Serikali wakiwamo maofisa ugani, huku Mgeni Rasmi akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme.

Akizungumza kwenye Mkutano huo Mratibu wa Mradi wa wasindikaji na wazalishaji wa maziwa Tanzania TI3P kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Joseph Mabula, amesema benki hiyo ilianzishwa kwa ajili ya kuleta maendeleo katika Sekta ya Kilimo na kuhakikisha nchi ina jitosheleza katika suala zima la upatikanaji wa chakula pamoja na kusaidia wakulima wadogo kuondokana na uzalishaji wa kujilimu bali wafanye na kilimo biashara.

Amesema Benki hiyo iliona kuna fursa katika Sekta ya Maziwa kwamba kumekuwapoa na mwamko wa watu ambao wanahiji kunywa maziwa ambayo ni salama na pia matumizi ya maziwa yanapunguza utapiamlo kwa watoto na kuimarisha afya na pia Sekta hiyo inaiunua kipato cha wafugaji.

Amesema zaidi ya 80 ya wafugaji wanaozalisha maziwa ni wafugaji wadogo hivyo wakaona ni vyema wawaendeleze. na hatimaye kuja na mradi wa kuendeleza Sekta ya ndogo ya Maziwa, Mradi ambao ni shirikishi wa wasindikaji na wazalishaji wa maziwa Tanzania (TI3P) ambao ulizinduliwa mwaka jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao ni wa miaka mitatu.

“Mradi huu umelenga zaidi kutatua changamoto ambazo zinawakabili wasindakaji wa maziwa ili mwisho wa siku wanufaike na Mnyororo wa thamani katika Sekta ya Maziwa, na unatekelezwa katika maeneo mawili ya Kanda ya Ziwa pamoja na Zanzibar,”amesema Mabula.

Aidha, amesema mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na wadau wa HEIFER International ambao ni wataalam na wanauzoefu mkubwa katika Sekta ya Maziwa na wametenga dola milioni 40 ambazo zitaingia katika kuinyanyua Sekta hiyo ya maziwa na kupewa wafungaji fursa ya kokopa kupitia vikundi,”ameongeza.

Naye Mwakilishwa wa Mkurugenzi Mkazi wa HEIFER International Nyamate Musobi ambaye ni Afisa Uendeshaji, amesema kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo wapo Kanda ya Ziwa kutekeleza mradi Shirikishi wa wasindikaji na wazalishaji wa maziwa na wanauzoefu mrefu tangu mwaka 1974, na wamekuwa wakifanya kazi sana Nyanda za juu Kusini na Kaskazini.

Amesema na sasa wamekuja kutekeleza mradi huo Kanda ya Ziwa eneo ambalo halijaendelezwa ambalo limekuwa na changamoto katika uzalishaji, miundombinu ya ukusanyaji wa maziwa hata masoko ya maziwa Kanda ya Ziwa ipo chini, hivyo kupitia mradi huo wamekuja kuleta mabadiliko.

“HEIFER tumejulikana kwa mradi wa kopa Ng’ombe lipa Ng’ombe, moja wapo la Shirika ambalo limesaidia watanzania kuwa na Ng’ombe wengi wa maziwa na tulileta Ng’ombe zaidi ya Laki Mbili na tumechangia uzalishaji mkubwa wa maziwa,”amesema Nyamate.

Amesema pia katika mchango wao wa kukuza Sekta ya Maziwa waliweza kuwaweka wafugaji pamoja kwenye vikundi na kuendeleza Tasnia ya Ushirika na kuunda vyama vya Ushirika zaidi ya 60 na wamefanya kazi za vyama vya ushirika zaidi ya vyama 119 huko walipotoka.

“Katika utekelezaji wa mradi huu tutakuwa na majukumu makubwa matatu, na jukumu la kwanza ni kuhakikisha wafugaji tunawaweka pamoja, kuwajengea uwezo kuanzia kwenye vikundi ili wapate mafunzo mbalimbali na kuongeza uzalishaji, kuwasaidia ziwe taasisi za kibiashara kwa kushirikiana na tume ya maendeleo ya ushirika, kuwaunganisha na wanunuzi mbalimbali, na kuboresha miundombinu ya ukusanyaji wa maziwa,”amesema Nyamate.

Katika hatua nyingine amesema kipindi wanafanya tathimini kabla ya kufanya utekelezaji wa mradio Kanda ya Ziwa ushiriki wa akina mama katika kunufaika na Mnyororo wa Thamani wa Maziwa upo chini sana, na kubainisha changamoto waliyoibaini akina mama hawana Rasilimali za Mifugo na kupitia mradi huo wataona namna ya kusaidia akina mama kupata Rasilimali hizo kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambao ndiyo watekelezaji wakuu wa mradi na kushirikiana pia na Halmashauri kupitia Ofisi za Maendeleo ya Jamii.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo wa Shinyanga, amesema mradi huo utaleta chachu ya mabadiliko na kuongeza uzalishaji na ukusanyaji wa maziwa katika vituo Rasmi pamoja na kuongeza pato la wafugaji wadogo na taifa kwa ujumla.

Amesema Sekta ya Maziwa ina mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya Mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na kutaja mchango huo kuwa ni kuimarisha upatikanaji wa lishe bora kwa watoto, kuboresha afya za wananchi, kupunguza umaskini kwa wafugaji, kupunguza uingizwaji wa maziwa kutoka nje ya nchi, na kuongeza makusanyo ya Serikali sababu Sekta hiyo inachangia asilimia 2.3 ya pato la taifa.

Ametaja faidi zingine ni kuchochea ukuaji wa Sekta ya Viwanda vya kusindika maziwa kutokana na uwepo wa malighafi.

Aidha, ametoa maelekezo ya msisitizo katika kukuza Sekta hiyo ya Maziwa kuwa Halmashauri zihakikishe zinatenga maeneo ya kwa ajili ya malisho, kuimarisha miundombinu ya maji na uchibwaji wa mabwawa, Majosho pamoja na Maofisa ugani kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa.

Amesema halmashauri ziendelee kuhamasisha unywaji wa maziwa Maofisini na kushirikiana na TAMISEM kuendeleza mpango wa unywaji wa maziwa shuleni ikiwamo kupitia mikataba na wasindikaji wa maziwa na kusambaza maziwa kwenye shule zote zilizopo katika maeneo yao.

Afisa uzalishaji wa Maziwa kutoka Bodi ya Maziwa Deogratias Buzuka, amewataka Wanachi watumie maziwa ambayo yamesindikwa kuwa ndiyo yapo salama, na wakitumia maziwa ambayo hayapita kwenye mfumo Rasmi ni kujitafutia magonjwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Mratibu wa Mradi wa TI3P kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Joseph Mabula akielezea mradi huo kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Maziwa.
Afisa Uendeshaji Mradi wa HEIFER International Nyamate Musobi akielezea utekelezaji wa mradi wa TI3P kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania TADB.
Mratibu wa Mradi wa TI3P kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Joseph Mabula akiwasilisha maelezo ya Tasnia ya Maziwa Tanzania kwenye Mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Afisa Tathimini na ufuatiliaji kutoka HEIFER International Willifaston Ntoroma akiwasilisha jinsi ya utekelezaji wa Mradi.
Afisa Uzalishaji wa Maziwa kutoka Bodi ya Maziwa Deogratias Buzuka akizungumza kwenye Mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Maziwa.
Meza Kuu wakiwa kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga (kulia) Beda Chamatata, akiwa na Afisa Uendeshaji wa HEIFER International Nyamate Musobi kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, (kushoto) akiwa na Afisa Uendeshaji Mradi wa HEIFER International Nyamate Musobi wakifuatilia mawasilisho na uchangiaji wa mada kwenye Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa kikiendelea mkoani Shinyanga.
Washiriki wakiwa kwenye kikao cha Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga kikiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye kikao cha Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada kumalizika kwa Mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Maziwa mkoani Shinyanga.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Share:

WAZIRI MABULA ATAKA UPANDAJI MITI KWA WANAOMILILISHWA ARDHI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Handeni mkoani Tanga alipokwenda kukabidhi hatimilki za ardhi wakati wa ziara ya siku moja katika halmashauri ya Mji wa Handeni na kijiji cha Msomera tarehe 22 Machi 2023. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando.

Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando akizungumza wakati Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipokwenda kukabidhi hati milki za ardhi wilayani Handeni mkoani Tanga tarehe 22 Machi 2023. Kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Handeni Mashaka Mugeta

Sehemu ya wananchi wa Handeni waliojitokeza kukabidhiwa hati milki za ardhi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula tarehe 22 Machi 2023.




Waziri wa Ardhi Nyimba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati milki ya Ardhi pamoja na mche wa mti mkazi wa Handeni Doto Bakari alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo tarehe 22 Machi 2023.

Afisa kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) akitoa elimu ya upandaji miti kwa wananchi wa handeni waliokabidhiwa hati milki za ardhi na Waziri wa Ardhi Nyimba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula tarehe 22 Machi 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

*****************************

Na Munir Shemweta, WANMM HANDENI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi waliokabidhiwa hati milki za ardhi wilayani Handeni mkoani Tanga kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao ikiwa ni moja ya sharti lililopo katika hati ya ardhi.

Dkt Mabula ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Machi 2023 wilayani Handeni Mkoani Tanga wakati akikabidhi hati milki za ardhi kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni.

Amesema, katika kuhakikisha maeneo wanayomilikishwa yanakuwa na utunzaji mzuri wa mazingira wizara yake imeona ije na sharti la kuwataka wanaomilikishwa kupanda miti mitano katika eneo wanalomilikishwa ili kutunza mazingira.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi hukata miti kwa visingizio vya matumizi mbalimbali jambo linalosababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali.

Amebainisha kuwa, iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa dhidi ya uharibifu huo wa mazingirs kuna hatari ya vizazi vijavyo kukumbwa na ukame ama majira ya mvua kubadilika badilika.

"Tunahitaji kutunza mazingira katika maeneo yetu kwa kupanda miti ya matunda ili tupendezeshe mandhari ya maeneo yetu" alisema Dkt Mabula.

Aidha, Waziri Mabula amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao namna bora ya kupanda miti na kuitunza kwa lengo la kuwajenga kiakili kuhusiana na utunzaji wa mazingira.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wananchi waliokabidhiwa hati kuhakikisha wanafuata masharti ya umiliki ardhi ikiwemo kulipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka kuwa na malimbikizo makubwa ya madeni.

Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando alimueleza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuwa, wilaya yake imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuhakikisha inatatua kero za wananchi ziliwemo zile za ardhi na moja ya mikakati iliyopo ni kuwa na kliniki inayozunguka kwa lengo la kutatua kero za wananchi.
Share:

JARIBU BAHATI YAKO NA SLOTI YA BOOK OF ESKIMO

Ilizanza kama hadithi tamu na ya kusisimua kutoka kwa mtaalam Knud na mara ghafla ikageuka uhalisia, ni kutoka simulizi za Knud zinakuletea uhalisia wa mchezo wa Book of Eskimo ambao unapatikana kwenye Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet kwa kushirikia na Expanse Studio.


 

Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakurejesha kwenye simulizi za mabingwa kuhusu juhudi zao za kushinda kirahisi, moja ya kitu kizuri kutoka Sloti ya Book of Eskimo ni mchezo unaokupa nafasi ya kushinda kirahisi ni uwezo wako tu wa kuvumilia baridi unapokua mchezoni ndio kitu pekee kinachoweza kukupatia ushindi.

 

Sloti ya Kasino ya Mtandaoni ya Book of Eskimo na Ubora Wake

 

Sloti ya the Book of Eskimo ni sloti ya kasino ya mtandaoni imeandaliwa vyema na Studio za Expanse, unayoweza kuipata kwenye kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet.

 

Mchezo huu umetengenezwa kwa ubora ikiwa na mandhari ya kwenye baridi, ambayo ingekuhitaji kuwa na nguo za joto kidogo kuweza kufurahia kuwepo kwako eneo hilo.

 

Thamani ya ushindi was loti hii unaipata kwenye alama mbalimbali, huku alama za barafu za herufi A, K na Q zikiwa na ushindi mdogo zaidi, huku alama zingine zikiwa ni alama za kukusaidia wewe kuiepuka baridi, ukiwa kwenye mazingira hayo zikikusogezea ushindi mkubwa.

Sloti hii inalipa vyema kwa mistari 5, 3 na 10 ya malipo, ambayo Inaweza kukuvusha kwenye kipindi cha barafu na kukupa ushindi.

 

Unaweza kufurahia ofa nyingi sana ndani ya mchezo huu kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, wakati ukiwa karibu na ushindi wa jackpot mbali mbali za kasino. Tembelea kasino ya mtandaoni ya Meridianbet kujaribu mchezo huu na michezo mingine mingi uwe moja ya mabingwa wengi wa kila siku.

 

Share:

UGONJWA ULIOUA WATU WATANO KAGERA NI 'MARBURG'


Serikali imetangaza mpaka sasa ugonjwa ulioripotiwa Machi 16, 2023 kutoka Wilayani Bukoba mkoani Kagera umejulikana kuwa ni virusi vya 'Marburg'' na hadi wakati huu tayari umekwishaua watu watano huku walioathirika wakiwa ni 8 na watatu kati ya hao wanaendelea na matibabu.

Akizungumza na Wanahabari, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kwamba ugonjwa huu ambao kwa mara ya kwanza uligundulika huko Mji wa Marburg chini Ujerumani.

Akizungumzia kuhusu uambukizaji wa ugoonjwa huo, Waziri amesema "Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine ambapo, kama utashika maji maji pale ambapo pana uwazi au mtu ana michubuko ama kidonda, na maji maji hayo yanaweza kuwa Damu, mate, mkojo, machozi yatokayo kwa maiti ama kwa mgonjwa mwenye dalili ya ugonjwa huo".

Mpaka sasa Serikali imedhibiti ugonjwa huo kusambaa kutoka nje ya wilaya, na kwamba tangu wagonjwa huo waliporipotiwa Bukoba mpaka sasa haujavuka kwenda sehemu nyingine.

Aidha ameeleza kwamba baadhi ya dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kuumwa kichwa, kuharisha, kuishiwa nguvu, kutoka damu sehemu za mwili zilizo wazi.

Mbali na hayo, Waziri Ummy ameweka wazi kuwa Ugonjwa huo hauna tiba mahsusi isipokuwa mtu atatibiwa kutokana na dalili atakazo kuwa nazo.

Hata hivyo Waziri huyo amesisitiza Ugonjwa huo sio tishio kwa kuwa unaweza kudhibitika na kwamba mpaka sasa serikali inawatazama kwa makini watu 161 ambao kwa namna moja ama nyingine walipata kushirikiana moja kwa moja na waathirika wa ugonjwa wa Marburg.

Aidha Shirika la Afya duniani (WHO) imeeleza kwamba ugonjwa huu si mara ya kwanza kutokea Afrika na kwamba miaka kadhaa nyuma umeshawahi kutokea katika nchi jirani ya Uganda.

Chanzo - EATV 
Share:

UGANDA YAONESHA NIA UWEKEZAJI MIRADI YA UMEME NCHINI

 



Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Col Mwesigye Fred (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Wizaya ya Nishati, Athumani Mbuttuka( wa tatu kushoto), Kamishna Msaidizi Maendeleo ya umeme, Mhandisi Styden Rwebangila(kushoto) na wawekezaji kutoka Uganda kuhusu kuwekeza katika mradi wa umeme, Machi 21, 2023.u
 

 Na Zuena Msuya, Dodoma

Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania pamoja na wawekezaji kutoka nchini humo kuhusu kuwekeza katika mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Lindi, Masasi, Tunduru na Songea.

Mazungumzo hayo yamefanyika Machi 21, 2023 katika ofisi za Wizara ya Nishati mkoani Dodoma na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Kamishna Msaidizi Maendeleo ya umeme, Mhandisi Styden Rwebangila na wawekezaji kutoka Uganda.

Wawekezaji hao wamemueleza Makamba kuwa wanataka kuwekeza katika mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa Msongo mkubwa wa Kilovolti 400 wenye urefu wa Kilometa 222.3 kutoka Lindi, Masasi hadi Songea.

Wawekezaji hao watawekeza kwa kusanifu, kutafuta fedha, kujenga na kuendesha njia hiyo na kuikabidhi baada ya muda uliopangwa.

Hata hivyo Makamba ameridhia wawekezaji hao kuwekeza katika mradi huo na kusema kuwa huo ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele kwa taifa.

Vilevile amewaagiza wawekezaji hao kutana na Shirika la Umeme nchini Tanzania na maafisa wa Wizara ya Nishati ili kujadiliana na kuona njia bora ya kutekeleza katika mradi huo kwa kuangalia sheria, taratibu na kanuni za uwekezaji katika miradi ya umeme.

Aidha Wawekezaji hao pia wameonyesha nia ya kutaka kuwekeza katika mradi wa umeme wa jua katika Kisiwa cha Mafia wenye megawati 5 kwa gharama ya Dola za Kimarekani 11.64.

Hata hivyo Waziri aliwaeleza wawekazaji hao kuwa serikali imeshapa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 5 kutoka Wakala wa Maendeleo wa Ufaransa (AFD) na kwamba iko katika mazungumzo ya AFD kuongeza fedha Zaidi.

Kwa upande wake Balozi wa Uganda nchini Tanzani, Col. Mwesigye Fred ameishukuru Serikali ya Tanzania, kwa kukubali wawekezaji kutoka nchi Uganda kuwekeza katika miradi ya umeme.

Amesema hayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili ulioasisi na viongozi wakuu.

 




Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba(kulia) akiwa mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Col Mwesigye fred (kushoto) na wawekezaji kutoka Uganda 
Share:

DC MKUDE ATOA MAAGIZO ULIPWAJI FIDIA WAATHIRIKA TOPE LA MGODI WA ALMASI MWADUI

 

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi kupasuka kwa bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui afanya kikao na uongozi wa Mgodi huo kufuatilia hatua za ulipwaji fidia wananchi,

Na Ofisi ya habari Kishapu.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkunde ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi kuvunjika kwa kingo za bwawa la maji tope katika mgodi wa almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) uliopo Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, amefanya kikao na uongozi wa mgodi huo ili kufahamu hatua ya ulipaji wa fidia waliyofikia tangu kupasuka kwa bwawa hilo Novemba 7 mwaka jana.

Awali akitoa taarifa wakati wa kikao hicho, Afisa Uhusiano wa Mgodi huo Benard Mihayo, amesema tayari timu yao imeshafanya tathimini na kubaini waathiriwa wanaostahili kulipwa fidia na kujengewa nyumba kufuatia tope la mgodi huo kuharibu makazi na mashamba ya wakazi wa Vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo Kata ya Mwadui Luhumbo kwa kufunikwa na tope.

“Tathimini imefanyika na kubaini makundi yanayostahili kulipwa fidia kuwa ni pamoja na wamiliki wa ardhi, wapangaji, waliokuwa wamekodisha mashamba pamoja na waliopoteza mifugo na tayari tumeanza ulipaji wa fidia na mpaka sasa ulipaji upo Asilimia 18 na wahanga wengine tunaendelea kuwafungulia akaunti za benki ili tuweze kuwalipa stahiki zao,” amesema Mihayo.

Kwa upande wake Meneja wa Mgodi huo, Ayoub Mwenda ameishukuru tume ya madini na Serikali kwa kuendelea kuwapa ushirikiano katika kuhakikisha waathiriwa wote wanalipwa fidia kwa kuzingatia sheria na miongozi ya Serikali.

“Tunaishukuru tume ya madini kwa kuendelea kushirikiana nasi ambapo Machi 6 mwaka huu tumepata kibali cha kuendelea kujenga bwawa jipya la Tope hadi sasa ujenzi umefika asilimia 25 na kufikia Julai 2023 tutakuwa tumekamilisha na uzalishaji kuendelea," amesema Mwenda.

Aidha, Mhe. Mkude ameupongeza uongozi wa mgodi huo kwa hatua waliyofika na ameahidi kutoa ushirikiano kila muda kuhakikisha waathirika wa tope wanapata stahiki zao na kuagiza hadi kufikia Machi 31 mwaka huu Waathirika wote wawe tayari wameshalipwa fidia.

“Jitahidini kulisukuma kwa haraka ili waathiriwa waliobakia wapate fidia hadi kufikia tararehe 31 Machi 2023 Waathirika wote wawe wameshalipwa, na mimi nitashirikiana nanyi kila mkihitaji msaada kutoka ofisini kwangu," amesema Mhe. Mkude.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger