Thursday, 16 March 2023

BUNGE LA AFRIKA LATUMA SALAMU ZA POLE VIFO VYA WATU 250 KUFUATIA KIMBUNGA FREDDY NCHINI MALAWI NA MSUMBIJI

Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira na Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu 250 waliofariki kufuatia Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Afrika Kusini

Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) limetuma salamu za pole na rambirambi kufuatia vifo vya watu 250 katika za Malawi na Msumbiji kutokana na Kimbunga Freddy.

Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira amesema Bunge la Afrika limehuzunishwa na tukio la Kimbunga Freddy hivyo linatoa pole kwa nchi za Malawi na Msumbiji

Aidha, Chifu Charumbira amesema Bunge la Afrika lipo pamoja na Wamalawi na Msumbiji wote katika kipindi hiki kigumu. 

Rais huyo wa Bunge la Afrika pia ameshauri hatua madhubuti na maksudi zinapashwa kuchukuliwa ikiwa ni sehemu ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Akitoa taarifa kuhusu taarifa kuhusu madhara ya Kimbunga Freddy kilichoikumba ya Malawi na Msumbiji wakati wa Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini, Mbunge kutoka Malawi Mhe. Steven Mikaya amesema idadi ya watu waliofariki kutokana na Kimbunga Freddy nchini Malawi na Msumbiji hadi sasa ni watu 250 na manusura ni wengi na huduma za kijamii zimekosekana barabara zimeharibiwa, hakuna huduma ya maji , umeme umekatika, uharibifu mkubwa umefanyika hivyo panahitajika misaada ya kibinadamu.

Watu wengi na nyumba zao wamesombwa na matope katika mji mkuu Blantyre nchini Malawi ulioharibiwa zaidi baada ya kimbunga Freddy kupiga kusini mwa Afrika kwa mara ya pili, na kusababisha mafuriko ambayo yamewaua watu zaidi ya 250.


Vikosi vya uokozi vinaonya juu ya uwezekano wa kuwepo waathirika zaidi wa kimbunga hicho wakati vikiendelea kuwatafuta manusura kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na kimbunga Freddy.


Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Malawi Felix Washoni amesema waliwapata watu kwenye miti, kwenye mapaa ya nyumba au katika maeneo ya miinuko.


Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) ukiongozwa na Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Chief Fortune Charumbira unaendelea leo Machi 16, 2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini ambapo wabunge wanajadili mambo mbalimbali kuhusu Bara la Afrika.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira akizungumzia tukio la Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji na kusababisha vifo vya watu 250
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira akizungumzia tukio la Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji na kusababisha vifo vya watu 250
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira na Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu 250 waliofariki kufuatia Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji.
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira na Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu 250 waliofariki kufuatia Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji.
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) Mhe Chifu Fortune Charumbira na Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu 250 waliofariki kufuatia Kimbunga Freddy kilichotokea nchini Malawi na Msumbiji.
Mbunge kutoka Malawi Mhe. Steven Mikaya akitoa taarifa kuhusu Kimbunga Freddy kilichosababisha vifo vya watu 250 nchini Malawi na Msumbiji
Mbunge kutoka Malawi Mhe. Steven Mikaya akitoa taarifa kuhusu Kimbunga Freddy kilichosababisha vifo vya watu 250 nchini Malawi na Msumbiji

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI



Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) ,Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) ,Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) ,Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 
Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) ,Mhe. Chief Fortune Charumbira akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 
 Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika ukiendelea leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya AfCFTA , Wamkele Mene, akihutubia Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP)
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya AfCFTA , Wamkele Mene, akihutubia Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP)
Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika ukiendelea leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 
Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika ukiendelea leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini 



Mkutano wa Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika ukiendelea leo Machi 16,2023 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Afrika Kusini


Share:

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA HIFADHI YA KILIMANJARO YAFANA


Na John Mapepele 

Shamrashamra za hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro zimepambamoto katika Makao Makuu ya Hifadhi hii Mkoani Kilimanjaro. Maadhimisho haya yanafanyika leo Machi 16, 2023 ambapo Mgeni Rasmi ni Waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii Mhe Mohamed Mchengerwa. 

Katika hafla hii Mhe. Mchengerwa anatarajia kutoa Tuzo kadhaa kutambua mchango wa watu mbalimbali walioutoa katika Hifadhi hii maarufu duniani. 

Miongoni mwa watu watakaokabidhiwa Tuzo hizo ni pamoja na familia ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 

Aidha, Mhe. Mchengerwa atashuhudia tukio la kusaini mkataba wa kusaidia uhifadhi katika Hifadhi hii kutoka Serikali ya China. 

Kwa upande wa Tanzania Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Anderson Mutatembwa atawakilisha wakati kwa upande wa Kenya, Mhe. Balozi wa China nchini atasaini mkataba huo. 

Pia Mhe Mchengerwa anatarajiwa kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Dola za kimarekani milioni moja kutoka Serikali ya China kama msaada kwa Hifadhi ya Kilimanjaro. 

Hifadhi hii ni ya pili kwa makusanyo ikiongizwa na Serengeti kwa Hifadhi zinazosimamiwa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA). 

Kwa mwaka wa fedha 2021/22 ilikusanya bilioni 581.8 kutoka kwa watalii 467,190 waliotembelea Hifadhi hiyo. 

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ilianzishwa rasmi Machi 16, 1973 na ni miongoni mwa Hifadhi maarufu duniani.
Share:

Wednesday, 15 March 2023

KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI KUWANUFAISHA VIJANA ZAIDI YA 2000


Zaidi ya vijana 2000 nchini wanatarajia kunufaika na ujenzi wa kiwanda cha Mkulazi kilichopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kwa kupatiwa ajira mbalimbali kulingana na ujuzi wao.

Hayo yamebainishwa Februari 14 mwaka huu na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho na kueleza namna ambavyo vijana watanufaika na ajira kupitia kiwanda hicho.

Amesema licha ya kiwanda hicho kutoa ajira kwa vijana kitasaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa sukari kwa matumizi ya binadamu na viwandani ambapo kitazalisha tani 50,000 kwa siku.

“kwa niaba ya kamati hii tumeridhishwa na ujenzi wa kiwanda hiki ambao umefikia asilimia 89, tunaamni kuwa kukamilika kwake mbali na kupunguza changamoto ya upungufu wa sukari pia vijana wetu watapa ajira na kujikwamua kiuchumi,"amesema.

Aidha Mwenyekiti huyo ampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha kwa ajili ya ujezi wa kiwanda.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce ndalichako amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inaimalisha uzalishaji wa viwanda, kupunguza upungufu wa sukari nchini na kuttoa fursa kwa watanzania kupata ajira hususani vijana.

Aidha amewataka wakandarasi kukamilisha ujezi wa kiwanda hicho kwa wakati ili kianze kufanya kazi kwa wakati ifikapo Julai mwaka huu.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho Selestine Some amesema mradi huo hadi kukamilika utagharimu shilingi bilioni 344.47 na kufikia februari 28 mwaka huu jumla ya fedha zilizotolewa kama mtaji ni shiling bilioni 263.60 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 19.38 ni thamani ya ardhi na shilingi bilioni 127.00 fedha taslimu kwa ajili ya kazi ya kilimo cha miwa.

Hadi kufikia februari 2023 mradi wa mbigiri umetoa ajira kwa wafanyakazi 1,025 kati ya hao,wafanyakazi 340 wanafanya kazi mbalimbali za ujenzi wa kiwanda, 450 wanafanya kazi za mashambani na kitakapokamilika kitaajiri wafanyakazi zaidi ya 2315.

Hata hivyo kamati hiyo imetembelea kiwanda cha nyama cha ngulu hills na kukagua maendeleo ya kiwanda hicho na kukiri kuridhishwa na maendeleo ya kiwanda hicho yaliyofikia asilimia 98.
Share:

NEMC YAONESHA ULIMWENGU JINSI YA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI YALIYOBORESHWA KUVUTIA UWEKEZAJI TANZANIA KWENYE MAONESHO QATAR

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanashiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kutoa elimu na kuonesha ulimwengu jinsi mazingira ya uwekezaji yalivyoboreshwa na kurahisishwa kwa ajili ya kuvutia uwekezaji nchini. Vilevile wanaeleza fursa zilizopo za uwekezaji hasa katika kilimo endelevu kinachozingatia uhifadhi wa mazingira pamoja na utalii kwa ajili ya maendeleo endelevu. Baraza linaelimisha wawekezaji wa Kimataifa juu ya kufanya Tathimini ya Athari kwa Mazingira (TAM)
Share:

TWIGA MINERALS NA BARRICK DHAMINI MKUTANO WA JUKWAA LA PILI LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI


Meneja wa Barrick nchini, Dk. Melkiory Ngido (katikati) akifuatilia mada za ufunguzi wa mkutano huo,(kushoto) kwake ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Max Steel,Purvita Vadgama na (kulia) ni Mhasibu Mwandamizi wa kampuni ya Apex,Christina Padilla. Barrick na Twiga ni wadhamini wakuu wa mkutano huo
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia matukio
Watendaji Waandamizi kutoka taasisi mbalimbali wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa mkutano huo.
Watendaji Waandamizi kutoka taasisi mbalimbali wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia mawasilisho ya mada mbalimbali za ufunguzi.


Kampuni ya Serikali Twiga Minerals Corporation, yenye ubia na kampuni ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick Gold Corporation, ni mdhamini mkuu wa mkutano wa Jukwaa la Pili la utekelezaji wa ushirikishwaji Watanzania katika sekta ya madini.


Mkutano huu unaofanyika kila mwaka umeandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Madini chini ya Wizara ya Madini na unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha International Conference Centre (AICC), na kukutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta hiyo ya madini kwa lengo la kujadili na kufanya tathmini ya ushirikishwaji watanzania katika mnyororo wa sekta hiyo.

Waziri wa Madini, Mh. Dkt. Doto Biteko, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mkutano huo kesho.


Mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini kwa kufungamana na sekta nyingine kwa uchumi imara wa nchi” unaambatana na maonyesho ya makampuni mbalimbali yanayojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini nchini.
Share:

KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YAANZA UPASUAJI KITETE

Kiongozi wa Madakatri Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Tumbi Dkt. Amani Malima .

Na. Catherine Sungura-Tabora


Kambi maalumu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Dodoma imeanza kufanya upasuaji kwa wagonjwa waliokutwa na uhitaji wa huduma hiyo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora-Kitete.


Hayo yamesemwa leo na Kiongozi wa Madakatri hao ambaye pia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Tumbi Dkt. Amani Malima ambapo zoezi hilo limeanza siku ya jumatatu na litadumu kwa siku tano. 


Amesema kuwa kwa siku ya kwanza walianza kuwaona wagonjwa na kuweza kuwachambua na kwa wale waliohitaji upasuaji, wameanza huduma hiyo toka siku ya jumanne  katika idara ya Mifupa, Masikio, Pua na Koo pamoja na matumbo.


“Jana tulifanya upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya Masikio, Koo na Pua pamoja na matumbo, kwahiyo leo tunaendelea  kwa upande wa idara Mifupa hususani kwa  watoto wenye matatizo ya mifupa ambayo wamezaliwa nayo, pia kuna watu waliopata ajali lakini wamekuwa na ulemavu ambao unaweza kurekebishika hivyo tupo hapa kwa nia ya kuwasahihisha”. Aliongeza Dkt. Malima.


Aidha, Dkt. Malima amesema lengo kubwa  la kambi hiyo ni kutoa huduma za matibabu ya kibingwa wa wananchi wa mkoa wa Tabora na kuwapunguzia  gharama za kuzifuata huduma hizo nje ya mkoa kwani wananchi wengi wamekuwa wakifuata huduma  Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro na Dodoma.


“Serikali yetu kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekua ikifanya vizuri na mambo makubwa katika sekta ya afya, hivi sasa kuna maboresho ya miundombinu yakiwemo majengo na ununuzi wa vifaa tiba hivyo tumewaleta madaktari mabingwa hawa ili kuweza kutoa huduma hizi kwa fani mbalimbali.


“Sisi kama wataalamu wa hospitali za rufaa za mikoa tumeona ni vyema kujiongeza licha ya  kuwapunguzia gharama watanzania wa kuzifuata huduma hizi nje ya Tabora lakini tutawajengea pia uwezo wataalamu wa hospitali hii ili kuhakikisha wananchi wa hapa wanaendelea kupata huduma kama hizi, hivyo tumeuda kikundi cha madaktari bingwa kutoka fani mbalimbali zaidi ya ishirini”.


Hata hivyo Dkt. Malima amesema kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya uliofanyika kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo vya Afya, hospitali za wilaya na hospitali za rufaa za mikoa, hivyo amewataka wananchi kuhakikisha wanafika kupata huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na si kwingineko.


Dkt. Malima pia amewaomba wafanyabiashara, makampuni na watu wenye uwezo wajitokeze  kusapoti huduma kama hizo kwenye maeneo yao waliyozaliwa ili kuweza kuwasaidia wananchi katika huduma za afya.


Naye, Mkazi wa Uyui Bi.Christina Lukwiza ambaye amemleta mtoto wake anayesumbuliwa na tatizo la kupumua kwa miaka minne sasa amesema alifurahi mara baada ya kusikia kuna madaktari bingwa kwenye hospitali ya Kitete.


“Nimeshazunguka kwenye hospitali mbalimbali na kuambiwa mwanangu ana vinyama kwenye pua na tumekuwa tukipewa dawa na kuzitumia ila tatizo halijaisha na hivyo kusababisha mahudhurio hafifu shuleni na wakati mwingine tunashindwa kumpeleka hospitali nyingine kwani hatuna uwezo wa kifedha”amesema Bi. Christina


Ameongeza kuwa amekimbilia hospitalini hapa kwakuwa hakuna gharama za kumuona daktari bingwa pia hata huduma zingine ni kuchangia kidogo.


“Nimekimbilia hapa ili mwanangu aonane na madaktari bingwa, kwani nilikua nawaza sana lini mwanangu ataonana na madakari bingwa, kwakweli ujio wao umenifurahisha sana kwani najua watatusaidia hasa sisi wenye kipato kidogo”.


 

Share:

NHIF YATOA UFAFANUZI FAO LA TOTO AFYA

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga  akizungumza na Waandishi wa habari Dodoma.

Na Dotto Kwilasa,Malunde I Blog-DODOMA


KUTOKANA na maboresho yanayoendelea kufanyika kwenye Mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF), Mfuko huo umewatoa hofu wanachama wake kufuatia taharuki iliyojitokeza kuhusu  Mfuko huo kutangaza kuondoa fao la "Toto Afya Kadi".

Akiongea na wananchi kupitia vyombo vya habari  Jijini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard H.Konga amesema hali hiyo haiwezi kuathiri huduma za afya na kwamba hayo ni maboresho ya utaratibu wa usajili na huduma kwa watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa bima hiyo.

Amesema kutokana na maboresho hayo, kwa sasa wazazi na walezi wanashauriwa kuwasajili watoto wao kama wategemezi wao kwenye bima ya afya au kuwasajili kupitia shule wanazosoma Ili kuongeza wigo wa wanachama katika mfumo wa bima ya afya kuelekea bima ya afya kwa wote.

Amefafanua kuwa wanachama katika makundi hayo watatakiwa kujiunga kama familia au kaya au makundi ya wanafunzi kupitia shule wanazosoma.

"Mpango wa Toto Afya Kadi ulianza rasmi 2016 baada ya kufanyiwa upembuzi lengo likiwa ni kuwajumuisha watoto kupitia shule zao,nia yetu ni kuwafikia kundi kubwa la watoto chini ya miaka 18 ambao takwimu ni zaidi ya nusu ya wananchi wote na kufikia azma ya Serikali ya watu wote kuwa na bima ya afya,"amesema

Pamoja na hayo amesema uzoefu wa miaka saba wa kulihudumia kundi hilo la watoto kupitia Toto Afya Kadi umewezesha Mfuko huo kufikia watoto 210,664 walio chini ya miaka 18 na kupelekea Mfuko kujifunza mengi yanayohitaji kufanyiwa kazi na kuyaboresha.

"Kati ya hayo ni pamoja na usajili wa mtoto mmoja ambayo inachelewesha utekelezaji wa dhana ya bima ya afya ambayo inataka watu kujiunga kwa wingi,aidha NHIF umeendelea kushirikiana na shule za msingi na Sekondari ili kusajili wanafunzi na mwitikio unaonekana,tunaamini hii ndo njia sahihi ya kuendelea nayo Ili kuhakikisha watoto wengi wanufaika,"amesisitiza

Amesema, maboresho ya utaratibu wa usajili wa hiari kwa kundi hilo la watoto walio chini ya miaka 18 mzazi au mlezi anashauriwa kuandikisha mtoto kama mtegemezi kupitia bima zao kwa mwajiri au vifurushi vya Najali afya,wekeza afya na Timiza afya pamoja na wazazi wao.

Aidha vifurushi hivyo vinawezesha mtu yeyote mwenye umrí wa zaidi ya miaka 18 kujiunga yeye mwenyewe au na mwenza wake au na watoto wake wasiozidi wanne Wenye umrí usiozidi miaka 18 na wanufaika na huduma za matibabu popote nchini kwenye vituo vilivyosajiliwa na NHIF.

"Kundi la watoto watakao Kosa sifa na vigezo vya kuandikishwa kupitia bima ya afya ya wazazi kwa mwajiri au vifurushi vya Najali afya, wekeza afya na Timiza afya wanaweza kuandikishwa kupitia vyuo , shule au vituo rasmi vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu,"anafafanua 

Kwa watoto walio chini ya miaka mitano Mkurugenzi huyo amefanua kwamba ambao watashindwa kuandikishwa kupitia machaguo hayo wanapaswa kutumia fursa ya matibabu bila malipo katika vituo vya Umma kama ilivyoainishwa kwenye sera ya afya ya mwaka 2007.

Akieleza faida za usajili wa watoto kupitia shule zao ni pamoja na kuwezesha utekelezaji wa dhana ya bima ya afya kwa wote utaratibu utakaowapa nafuu wazazi kugharamia matibabu ya watoto wao na kuwa na uhakika wa matibabu ikiwa ni pamoja na kuwajenga watoto dhana ya bima ya afya tangu wakiwa wadogo.

"Manufaa ya kusajili watoto kupitia kaya au familia ni kuwezesha familia nzima kunufaika na si mtoto tu au baadhi ya watoto tu utaratibu huu pia utawezesha wazazi  kupanga mipango ya kugharamia nafuu wa afya na hivyo kuepuka umaskini usio wa lazima,"amesema.

Aidha Mkurugenzi huyo wa NHIF ameeleza kuwa utekelezaji wa mpango huo umeanza juzi Machi 13,2023 na Mfuko ulitoa taarifa rasmi Kwa Umma na kwamba Mfuko Katika Ofisi zake zote upo tayari kuelimisha na kutoa ufafanuzi Kwa wote wanaohitaji kufahamu zaidi.

Kutokana na hayo jamii inapaswa kuelewa kuwa vifurushi vya bima ya afya ni mpango unawezesha mwananchi mmoja mmoja au familia kuchagua na kuchangia huduma za matibabu kabla ya kuugua na Kisha kuwa na uhakika wa matibabu kwa kutumia Kadi ya bima ya afya bila kikwazo Cha pesa.




Share:

BUNGE LA AFRIKA LAHAMASISHA MATUMIZI YA DAWA ZA ASILI

Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika iliyoshirikisha Wabunge wa Bunge la Afrika na Wadau mbalimbali wa afya katika Ukumbi wa Bunge la Afrika, Mdrand Afrika Kusini.
Dkt. Gayo amesema kuna uhitaji mkubwa kukuza dawa za asili ili kuwezesha kuunganishwa kwake katika mifumo ya afya barani Afrika.


"Tunataka kukuza tiba asilia katika nchi zetu za Afrika ili kuchangia katika kuboresha huduma ya afya ya watu wetu lakini pia kuhakikisha nafasi ya dawa za asili katika mifumo ya afya inatambuliwa. Tunataka pia kuhakikisha dawa za asili zinaboreshwa kisasa lakini pia Sheria zinaimarishwa ili kudhibiti utafiti katika dawa za asili",amesema Dkt. Gayo.


Nao washiriki wa warsha hiyo wamesema WaAfrika wanatakiwa kuzipa kipaumbele dawa za asili na kuondokana na mtazamo hasi kwamba kutumia dawa za asili ni ushamba/uchawi/zimepitwana wakati wakibainisha kuwa hata wakati wa janga na Covid - 19 dawa za asili zimesaidia sana kutibu afya za watu lakini pia dawa hizo zimekuwa zikitumiwa na mababu zetu hivyo ni vyema utamaduni ukaenziwa kwa kuwekewa nguvu zaidi pia kwenye Idara za Afya/Wizara za Afya katika nchi.
Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 
Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger