Monday, 23 January 2023

MKUDE AFANYA ZIARA MGODI WA MWADUI KUFAHAMU HATUA ZILIZOCHUKULIWA TANGU BWAWA LA MAJI TOPE LIBOMOKE...."FIDIA ILIPWE MAPEMA, UZALISHAJI UANZE"


Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akiangalia maji tope akiwa juu ya tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude ametembelea Mgodi huo ili kufahamu hatua gani zimechukuliwa tangu Bwawa hilo la Maji Tope lilipobomoka na kuharibu makazi na mashamba ya wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo katika Kata ya Mwadui Luhumbo kwa kufunikwa na tope Novemba 7,2022.


Mkude ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu amefanya ziara hiyo katika Mgodi wa Almasi wa Mwadui leo Jumatatu Januari 23,2023 akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati ya Usalama Mkoa wa Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Sabinus Chaula na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Ayoub Mwenda.


Mkude amesema ziara hiyo imelenga kutaka kufahamu hatua gani zimefikiwa baada ya kupata janga la kubomoka kwa kingo za bwawa la Maji Tope katika Mgodi Almasi wa Mwadui tangu Novemba 7,2022 ikiwa ni miezi kadhaa sasa imepita.

“Leo nimefanya ziara ya kujiridhisha kwamba ni hatua gani zimefikiwa, Wenzetu wa Mgodi wa Williamson Diamond Limited wamechukua hatua mbalimbali kwanza za kuwanusuru wananchi waliokutwa na matope katika maeneo yao ya makazi na maeneo ya mashamba.

Hatua ya pili waliyofanya ni kuwapatia huduma zote muhimu wananchi waliothirika na janga hilo ikiwemo za afya, elimu kwa watoto waliokuwa wanasoma na kwa watu waliokosa makazi sasa hivi wote wamehifadhiwa kwenye nyumba za kupanga ambapo wamepangishiwa na Mgodi wa Mwadui mpaka hali yao itakapokuwa sawa wengine wanaendelea kupata huduma ya chakula tangu Novemba 7,2022”,ameeleza Mkude.
Muonekano wa tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi.

Amebainisha kuwa hatua zaidi zilizochukuliwa ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu la kutafuta eneo mbadala la kuishi ambalo ni salama kuliko lile wananchi walikuwa wanaishi ambapo eneo limepatikana katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge lenye ukubwa wa Hekari 400.

“Tumefika kwenye eneo hili na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ametueleza ukubwa wa eneo kuwa ni la hekari 400 ambazo kwa kweli wananchi walioathirika na tope zitawatosha wao makazi na kilimo kwa sababu eneo lina rutuba, lilikuwa eneo la serikali na halina mgogoro wowote”,amesema Mkude.

“Natumia fursa hii kuushukuru Mgodi wa Williamson Diamond Limited kwa kutimiza yale yote ambayo walielekezwa na serikali kwa kuweka miundo mbinu ya kuhifadhi maji tope yasizagae tena na mengine, lakini pia namshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu kwa kutafuta eneo mbadala ambalo kwa kweli ni matumaini yangu hapa utaanza mji ambapo wananchi watapata huduma zote za msingi, shule zipo,kituo cha afya kipo, maji yapo, miundombinu ya barabara nitamsisitiza Mkurugenzi aiweke na umeme n.k”,ameongeza Mkude.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula akionesha eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu

Mkude ameusisitiza Mgodi wa Williamson Diamond Limited  suala la kulipa fidia kulipeleka haraka zaidi, akieleza kuwa amebaini kwamba bado hatua ya kufanya Tathmini haijakabidhiwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali hivyo kuelekeza ndani ya wiki mbili wawe wamefikisha taarifa hizo ili zirudi mapema waweze kulipa fidia kwa wananchi.

“Hivi karibuni Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa mkoani Shinyanga alitamka wazi kwamba tuchukue hatua ili kuhakikisha wananchi waliopatwa na janga hili la Maji tope wanalipwa mapema kadri inavyowezekana na ndiyo maana nimefanya ziara hata wiki moja haijapita, nimefanya ziara ili kujua hatua gani kwanza zimechukuliwa na nimegundua kuwa bado Mthamini Mkuu hajapata Nyaraka ili kuzisaini, Mgodi nimewapa wiki mbili hili ikamilike”,amesema Mkude.


Mwenyekiti huyo wa kamati ya uchunguzi wa kubomoka kwa bwawa la maji tope amefafanua kuwa suala la ujenzi wa nyumba watakaohitaji nyumba litatumia utaratibu utakaofaa, hivyo ameusisitiza Mgodi kufanya haraka na kutia umuhimu kwa maisha ya watu waliopatwa na janga hilo.

“Pia tumezungumza kwa undani sana kuhusu maendeleo ya Mgodi, siyo tunaangalia tu upande wa fidia na ubinadamu ni pamoja na kuendelea kufanya kazi kama kawaida. Mgodi kwa kweli ulisimama shughuli zake, tumesisitiza pia kuna maeneo ya mbadala au ujenzi wa bwawa jipya uendelee kwa kasi zaidi, hilo tumelifanya na tumekubaliana na wamesema kati ya miezi mitatu hadi mitano watakuwa wamekamilisha ujenzi wa bwawa na shughuli za uzalishaji zitaanza”,ameongeza Mkude.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda  akielezea hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka.


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda amesema tangu bwawa la maji tope lilipobomoka kingo Novemba 7 mwaka 2022, licha ya kuendelea na taratibu za tathmini ili wananchi walipwe fidia pia wameendelea kutoa huduma zote za kibinadamu kwa waathirika wa tope hilo kwa kuwapatia chakula, malazi na huduma zingine za elimu na afya na kwamba nyumba watakazowajengea wananchi zitakuwa bora.

“Jumla ya kaya 171 zitalipwa fidia, kati ya hizo kaya 46 tutazijengea makazi na tunaendelea kuzipatia huduma ya chakula kaya 50 zenye watu 286 mpaka pale watakapopata fidia na kupata makazi”,amesema Mwenda.
Mchoro unaoonesha hatua zilizochukuliwa na Mgodi wa Mwadui baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka

Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo amesema wamejenga kuta na kuweka matuta ya kuzuia tope lisiendelee zaidi kwenda kwenye makazi ya watu pamoja na kutengeneza mifereji ya kuchepusha maji yaliyokuwa yanaingia kwenye bwawa la New Almasi walilokuwa wanalitumia wananchi kwa huduma za kijamii na wanaendelea na ujenzi wa bwawa jipya.

“Tumejenga tuta kwenye bwawa la maji tope lililobomoka lakini pia tumekarabati bwawa la New Almasi ambalo lilikuwa linatumiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali ambalo lilijaa tope kwa kuliwekea tuta”,ameongeza Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo Shagembe Mipawa.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula amesema halmashauri hiyo imetenga eneo la halmashauri lenye ukubwa wa hekari 400 kwa ajili ya wananchi walioathiriwa na maji tope huku akisisitiza kuwa eneo hilo ni salama na halina mgogoro wowote na huduma za kijamii zinapatikana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude  akizungumza leo Jumatatu Januari 23,2023 wakati akipokea taarifa ya hatua zilizochukuliwa tangu Bwawa hilo la MajiTope lilipobomoka na kuharibu makazi na mashamba ya wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo katika Kata ya Mwadui Luhumbo kwa kufunikwa na tope Novemba 7,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude  akizungumza leo Jumatatu Januari 23,2023 katika mgodi wa Mwadui.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda  akielezea hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akifafanua kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akifafanua kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akifafanua kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo Shagembe Mipawa akielezea kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Mchoro unaoonesha hatua zilizochukuliwa na Mgodi wa Mwadui baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Juu ya tuta lililojengwa kudhibiti maji tope yasisambae kwa wananchi
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akiangalia maji tope akiwa juu ya tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi
Muonekano wa tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akitembelea mgodi wa Mwadui, aliyevaa miwani ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akiangalia mtaro/mfereji unaochepusha maji yaliyokuwa yanaingia kwenye bwawa la New Almasi walilokuwa wanalitumia wananchi kwa huduma za kijamii 
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akionesha mfereji unaochepusha maji yaliyokuwa yanaingia kwenye bwawa la New Almasi walilokuwa wanalitumia wananchi kwa huduma za kijamii 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu, eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu, eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akitembelea eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akitembelea eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula akionesha eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Share:

NEMC YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA TAASISI INAYOJIHUSISHA NA MASUALA YA KIMAZINGIRA INDIA KUDHIBITI TAKA NGUMU


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Taasisi inayojishughulisha na masuala ya kisayansi na kimazingira kutoka nchini India ambapo ushirikiano huo utasaidia kufanya maboresho katika ukusanyaji wa taka ngumu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amesema NEMC pamoja na Center for Science and Environment wamekusudia kujengeana uwezo na uzoefu kuwa pamoja na kufanya tafiti zinazohusiana na miji yetu katika ukusanyaji taka lakini vilevilekubadilishana uzoefu ambapo baadhi ya wataalamu wao wanaweza kupewa mafunzo.

Amesema nia ya mkataba huo uwe wa miaka mitatu kuanzia sasa lakini kutakuwa na uwezekano kuupeleka mbele zaidi lengo kubwa ni kuzipa nguvu Mamlaka za Serikali za Mitaa hasa katika majiji, miji pamoja na Wilaya ndo maana wakurugenzi wameweza kushiriki kwenye mkutano huo ili waweze kubadilishana mawazo na uzoefu ili baadae tuwe na mifumo ya kisasa kuhakikisha taka ngumu zinazozalishwa ziwezwe kutengwa na zisionekane kwenye madampona zile zinazooza ziweze kuwa mbolea.

"Suala la taka ngumu limekuwa changamoto katika miji mingi sio Tanzania tu,lakini katikanchi mbalimbali kwahiyo tumekuwa na wenzetu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Eswatini, Ghana , Zambia ambao na wao wametuma wawakilishai wao hapa kuja kujadili na kuweza kubadilishana uzoefu". Amesema

Aidha amesema madampo imekuwa mojawapo ya sehemu ambayo ni changamoto na ni gharama katika kuyaendesha katika uksanyaji wa taka ngumu na matokeo yake miji yetu mingi imekuwa ni michafu hivyo kupitia Taasisi hiyo kutoka India ambao wao wamekwenda mbali katika teknolojia hivyo kusaidia kutengeneza mifumo rafiki kwaajili ya kutenga taka ngumu zisiweze kuleta madhara kwenye mazingira.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka OR TAMISEMI, Bi.Hawa Mwechaga amesema TAMISEMI inasimamia halmashauri 184 ambako huko kote kuna taka ngumu kwahiyo kwa kila halmashauri wana idara zinazoratibu uzalishaji wa taka ngumu hivyo wanashirikiana na NEMC kuona ni namna gani wanaenda kuboresha Majiji na miundombinu mbalimbali.

Share:

POLISI SHINYANGA WAKAMATA MALI ZA WIZI, NYARA ZA SERIKALI...IMO MIKIA YA NYUMBU & KUCHA NA NGOZI ZA PAKA PORI , MBUZI MAWE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha ganda la yai la mbuni na kipande kimoja cha pembe ya korongo.
 
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata, mali za wizi, dawa za kulevya pamoja na Pikipiki nane zinazodaiwa kutumika kwa wizi na nyara za serikali yakiwemo maganda ya mayai ya mbuni,mikia ya nyumbu,  ngozi na kucha za paka pori, ngozi ya mbuzi mawe na Fungo.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Januari 23,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema vitu hivyo pamoja na vielelezo vimekamatwa wakati wa misako na doria zilizofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Desemba 20,2022 hadi Januari 23,2023.

“Tumefanikiwa kukamata pikipiki 8 zilizokuwa zinatumika kwa wizi au za wizim bangi kilo 10,kete 278. Vitu vingine ni nyara za serikali ambazo ni mikia 21 ya nyumbu, maganda 5 ya mayai ya mbuni,ngozi moja ya paka pori, kipande kimoja ca ngozi ya mbuzi mawe, miiba 44 ya nungunungu, vipande vitatu vya mkonga wa tembo, mikia 3 ya ngiri,vipande 3 vya magamba ya kobe,kucha 5 za paka pori,kipande kimoja cha jino la tembo, kipande kimoja cha ngozi ya fungo na kipande kimoja cha pembe ya korongo”,amesema Kamanda Magomi.

“Vile vile tumekamata meter 1 ya TANESCO, Solar panel 1,control box 1 ya mtambo, Tv 4, Subwoofer 1, mafuta ya petrol lita 225, bidhaa mbalimbali za dukani, seti moja ya muziki wa Disco, Pombe kali aina mbalimbali, pombe ya moshi lita 10,computer 1, godoro 1, viti 10 vya plastic, nyaya za miundombinu ya mawasiliano ya TTCL, battery 2 kubwa za gari, vyuma vya miundombinu ya barabara, madumu 42 yaliyotaka kutumika katika wizi wa mafuta kwenye Ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa katika eneo la Seke wilayaNI Kishapu”,ameeleza Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amesema pia Jeshi la Polisi liliokota pikipiki 9 ambazo zinadaiwa kusahaulika au kutupwa katika maeneo mbalimbali kutokana na sababu tofauti kama vile uhalifu na ulevi.

Kamanda huyo wa Polisi amewataka wananchi kuacha vitendo vya uhalifu na washirikiane na Polisi katika kutokomeza uhalifu na kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu wahalifu na badala yake kuwafikisha katika vituo vya polisi kwani kitendo hicho ni kosa la jinai na linahatarisha usalama wa raia.

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawataka wananchi kufika katika kituo kikuu cha Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutambua mali mbalimbali zilizokamatwa kuanzia Januari 23,2023 hadi Januari 30,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 23,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha  vifaa vilivyokamatwa na jeshi la polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha nyara za serikali walizokamata
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha seti moja ya muziki wa Disco waliyokamata
Seti ya muziki wa Disco iliyokamatwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali walizokamata
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali walizokamata
Miundombinu ya TTCL na barabara 
Mali zilizokamatwa
Mali zilizokamatwa
Nyara za serikali na vifaa vya kufanyia uganga
Muonekano wa pikipiki zilizokamatwa
Share:

Sunday, 22 January 2023

MBOWE : MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI, NAMSHUKURU RAIS SAMIA


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe amesema yeye sio kiongozi ambaye anaweza kununuliwa kwa chochote kama ambavyo baadhi ya wanachama wa chama hicho walivyomtazama baada ya kuonekana akifanya vikao mara kwa mara na Rais Samia.

Mbowe ameyasema hayo leo Januari 21 jijini Mwanza kwenye mkutano wa kwanza wa hadhara baada ya takribani miaka saba kwa vyama vya kisiasa kuwekewa katazo la kufanya mikutano ya hadhara.


Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini humo

"Wakati nyinyi mnaona kulikua na ugumu upande wenu upande wa CCM kulikua na ugumu kuliko CHADEMA kwasababu wanajua, yaani nyinyi badala ya kunipongeza Mbowe mnakuja kusema mambo ya kiharamia kwamba Mbowe anakula asali, hivi mnajua Mbowe anapoteza bilioni ngapi kwa CHADEMA"

"Nilivumilia kwasababu nilisema nina mambo makubwa ya kuyatafuta kuliko kauli za propaganda, nilisimama kuanzia miaka 30 iliyopita kuitafuta haki na ustawi wa nchi yangu nitasimama hapo kwa gharama yoyote hakuna idadi ya fedha wala mali itakayofanya niwasaliti watanzania," amesema Freeman Mbowe

Hata hivyo Mbowe amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu vyama vya siasa nchini kufanya mikutano ya hadhara baada ya mazungumzo yao ya muda mrefu ya kumshawishi na baadae kukubaliana naye licha ya baadhi ya wanachama wa chama tawala kutokubaliana na hatua hiyo.

"Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni nasimama mbele ya watanzania kumshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo alikuwa mvumilivu kwenye vikao mfululizo nilivyokaa nae kumshawishi atambue kwamba nchi inahitaji maridhiano, huyu Rais akakubali maridhiano"

"Watu walitamani maridhiano yasifanikiwe kwasababu kuna kitu wanafaidi lakini Rais Samia nimempelekea kwa niaba yenu wote alafu watu wanataka nimtukane siwezi kufanya hivyo" amesema Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo kinaadhimisha mika 30 tangu kuanzishwa kwake ambapo Maelfu ya Wanachama wa Chama hicho wameujaza uwanja wa Furahisha jijini Mwanza huku Askari wa jeshi la polisi wakionekana wakiwa maeneo ya uwanja huo ili kuimarisha ulinzi kwa wanachama.

Chanzo - EATV
Share:

SIMBA SC YAONDOKA NA ALAMA TATU MBELE YA DODOMA JIJI



NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu ugenini wakiinyuka Dodoma Jiji 1-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Jamhuri Jijini Dodoma.

Katika mechi hiyo tumeshuhudia Simba Sc ikiwaanzisha wachezaji wao wapya waliowasajili kwenye dirisha dogo ambao ni Sawadogo pamoja na mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Baleke.

Bao hilo pekee limefungwa na mshambuliaji wao mpya Jean Baleke akitumia makosa ya beki wa Dodoma Jijini na kuweza kufunga bao kwenye mchezo huo muhimu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger