Friday, 2 December 2022

RC MJEMA AKABIDHI PIKIPIKI NA BAJAJI KWA VIKUNDI VYA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU MANISPAA YA SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akikabidhi funguo kwa mwendesha bodaboda. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imekabidhi Mikopo ya Shilingi Milioni 144.4 kwa vikundi 9 vya Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa kuwakabidhi vitendea kazi zikiwemo pikipiki 34 na Bajaji tatu kwa ajili ya biashara ya usafirishaji.


Akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki na Bajaji leo Ijumaa Desemba 2,2022 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.

“Vijana tumewapatia pikipiki hizi hakikisheni mnazitumia kujiingizia kipato kama ilivyokusudiwa. Tayari mna leseni na Pikipiki na bajaj hizi zimekatiwa bima kubwa. Msitumike na wahalifu na fuateni sheria za usalama barabarani, msipakize watu zaidi ya mmoja kwenye pikipiki ‘mshikaki’ na msibebe mizigo mikubwa”,amesema Mkuu huyo wa mkoa.


Aidha amesema pia anataka kuwepo kwa Kanzi Data ‘Data Base' ya waendesha pikipiki mkoa mzima wa Shinyanga ili kuwatambua waendesha bodaboda wote kubaini wasio waaminifu wanaoshiriki vitendo vya uhalifu.

“Hongera sana Manispaa ya Shinyanga kwa kuendelea kutoa mikopo kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu ambapo tangu mwaka 2015 mpaka mwaka 2022 mmefanikiwa kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1.5. Naomba muendelee kutoa mikopo ili wananchi waweze kuinuka kiuchumi”,amesema Dkt. Mjema.

Amesema Serikali mkoani Shinyanga inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo ujenzi wa Stendi na barabara ili kuboresha maisha ya wananchi.

“Sasa hivi Shinyanga kuna Vibe kubwa!! Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga anajitahidi kuibadilisha Manispaa ya Shinyanga. Tunatengeneza miundo mbinu hapa ili muwe mnatereza tu…ukiingia mjini hakuna vumbi na tayari tumeanzisha usafiri wa Hiace kwenye baadhi ya maeneo hapa mjini Shinyanga na hivi karibuni tutazindua Stendi ya Hiace hapa Kambarage zitakazofanya mizunguko kwenye mitaa mbalimbali mjini Shinyanga”,amesema Dkt. Mjema.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kumgusa kila mwananchi, anataka kuona wananchi wanaondokana na umaskini na ndiyo maana mikopo imeendelea kutolewa”, ameongeza.


Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amekemea tabia ya baadhi ya waendesha bodaboda kutumiwa na wahalifu huku akiwaonya kuacha kung’oa Vioo vya pikipiki ‘Side Mirror’ na wasiendeshe bila kuvaa kofia ngumu.

Naye Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SSP Debora Lukololo amewakumbusha waendeshaji wa vyombo vya moto kuepuka kuendesha wakiwa wamelewa, wasimame kwenye vivuko ‘Zebra’ na kwenye Taa za barabarani, kutobeba mizigo mikubwa na kutumia lugha nzuri kwa wateja wao.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema wataendelea kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miredi mbalimbali hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia mikopo inayotolewa na halmashauri.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha amesema Mikopo hiyo ya shilingi 144,424,000/= ambayo inatokana na Mapato ya ndani imetolewa kwa vikundi 9 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambao wamenunua pikipiki, bajaji na vifaa vingine vya kutendea kazi huku akiwasisitiza kurejesha mikopo hiyo ili wapatiwe wananchi wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza leo Ijumaa Desemba 2,2022 katika Stendi Mpya ya Hiace Kambarage Manispaa ya Shinyanga wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza leo Ijumaa Desemba 2,2022 katika Stendi Mpya ya Hiace Kambarage Manispaa ya Shinyanga wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza leo Ijumaa Desemba 2,2022 katika Stendi Mpya ya Hiace Kambarage Manispaa ya Shinyanga wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Mikopo kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa Bajaji kwa ajili ya vikundi vya Watu wenye Ulemavu katika Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa pikipiki zilizolewa kwa vijana
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akikabidhi funguo za Bajaji kwa mkazi wa Shinyanga. Jumla ya Bajaji tatu zimetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akikabidhi funguo za Bajaji kwa mkazi wa Shinyanga. Jumla ya Bajaji tatu zimetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akikabidhi funguo za Bajaji kwa mkazi wa Shinyanga. Jumla ya Bajaji tatu zimetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu
Mkazi wa Shinyanga akionesha funguo za bajaji, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema. Jumla ya Bajaji tatu zimetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu
Mkazi wa Shinyanga akishikana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema (katikati). Jumla ya Bajaji tatu zimetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Mkazi wa Shinyanga akionesha Funguo za Bajaji, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko. Jumla ya Bajaji tatu zimetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akisalimiana na mwendesha bodaboda. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko. Jumla ya Pikipiki 34  zimekabidhiwa kwa vijana 34 kupitia vikundi vya vijana 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akikabidhi funguo kwa mwendesha bodaboda. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko. Jumla ya Pikipiki 34  zimekabidhiwa kwa vijana 34 kupitia vikundi vya vijana 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza na  mwendesha bodaboda mwanamke bi. Lilian John. Jumla ya Pikipiki 34  zimekabidhiwa kwa vijana 34 kupitia vikundi vya vijana 
Bi. Lilian John akionesha funguo za pikipiki. Jumla ya Pikipiki 34  zimekabidhiwa kwa vijana 34 kupitia vikundi vya vijana 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akikabidhi hundi ya shilingi 144,424,000/= kwa ajili ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu zilizotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SSP Debora Lukololo akizungumza wakati akikabidhi Viaksi Mwanga kwa ajili ya waendesha bodaboda
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akiwahamasisha waendesha vyombo  vya moto kuzingatia sheria za barabarani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza wakati akikabidhi pikipiki kwa waendesha pikipiki 'bodaboda'
Mnufaika wa mikopo ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akitoa neno la shukrani
Waendesha bodaboda wakicheza muziki 
Awali Maafisa wa Jeshi la Polisi wakikagua pikipiki hizo
Awali Maafisa wa Jeshi la Polisi wakikagua pikipiki hizo
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kushoto) akiwa amepanda pikipiki hizo.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa tano kushoto) akiwa amepanda pikipiki hizo.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akiwa amepanda pikipiki hizo.
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga SSP Debora Lukololo akitoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda.
Madiwani na viongozi mbalimbali wakiwa eneo la tukio

Vijana na wanawake wanufaika wa mikopo ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Vijana na wanawake wanufaika wa mikopo ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa eneo la tukio.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

WAZIRI MKENDA AHIMIZA UFUNDISHWAJI WA SOMO LA MAENDELEO VYUO VIKUU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ametoa wito kwa Vyuo Vikuu nchini kufundisha Somo la Maendeleo (Development Studies) kwa namna ambayo itachochea wanafunzi kuwa wadadisi.

Akizungumza leo Desemba 2, 2022 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Waziri Mkenda amesema kuwa ufundishaji wa somo hilo uwezeshe wanafunzi hao kufanya tafukuri tundulizi.

Waziri pia ametaka ufundishaji huo uwawezeshe wanafunzi kupata fursa ya kuchambua historia ya uchumi wa nchi ili kutambua vipindi mbalimbali ambavyo nchi imepitia na tunapoelekea kiuchumi.

"nimefurahi kuona kupitia mkutano huu mnafanya tathimini ya somo la maendeleo ambalo linawawezesha wanafunzi katika fani zote kuwa wadadisi na kuweza kufanya tafakuri. amesema Prof. Mkenda

Kuhusu Mapitio ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014, amesema kwa ujumla yanalenga kuona mwanafunzi akiwa na udadisi, mahiri na mwenye kujiamini katika kufanya kazi aliyosomea anapohitimu.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Colman Msoka amesema mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini na unalenga kufanya tathimini ya ufundishaji wa somo la maendeleo chuoni hapo.

Dkt. Msoka ameongeza kuwa Taasisi hiyo Mwaka 2023 itakuwa inafikisha miaka 50, hivyo wameona ni jambo muhimu kutafakari kwa kuwa katika miaka hiyo mambo yametokea ikiwemo kuporomoka kwa ujamaa, ulibelali kuongezeka kwa kasi, utandawazi na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, vyote vimebadili namna ya kuishi hivyo umuhimu wa kubadili mbinu za ufundishaji wa somo hilo.

Mkutano huo unashirikisha wajumbe kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka nchi za Marekani, Afrika Kusini, Ethiopia, India na Nigeria.
Share:

Thursday, 1 December 2022

NECTA YAZUIA MATOKEO YA WATAHINIWA 540

Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani, Athumani Amasi (kushoto) akitangaza matokeo ya mtihani wa elimu ya shule za msingi kwa mwaka 2022, jijini Dar es Salaam.


Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limezuia matokeo ya watahiniwa 540 kutoka vituo sita vya mitihani ndani ya jiji la Dar es Salaam baada ya kugundulika kufanya udanganyifu.

Wanafunzi hao wanatoka katika vituo vya Joylanda, Castle hill, Green Acress, Maktaba, Great Vision na Mtendeni.

Share:

GGML YAWEKA REKODI MAPAMBANO DHIDI YA VVU/ UKIMWI

Baadhi washiriki Kampeni ya GGM Kili Challenge 2022 waliopanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha za mapambano dhidi ya VVU. Mwaka huu jumla ya Sh bilioni 1.1 ilikusanywa na GGML kupitia wadau mbalimbali.


NA MWANDISHI WETU

WAKATI leo ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), imesema itaendeleza mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi kutokana na msaada inaoupokea kutoka kwa wadau na kuiwezesha Kampeni ya Kili Challenge kupiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 hadi kufikia kuwa mfuko wa kimataifa.


Kampeni hiyo iliyozinduliwa na GGML miaka 20 iliyopita na inalenga kuongeza uelewa na fedha za kupambana na maambukizi ya VVU. Kili Challenge imekuwa mfuko wa kimataifa wenye kushirikisha wapanda mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.


Hayo yamebainishwa jana naMakamu wa Rais wa AngloGold Ashanti anayesimamia miradi endelevu, Ghana na Tanzania, Simon Shayo wakati akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi duniani.


“Tunafurahia mafanikio haya kwa kutuwezesha kuufanya mfuko huu kuwa endelevu katika kutimiza malengo ya Serikali dhidi ya janga hili,” amesema.


Alisema mwaka huu GGML kwa kushirikiana na Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) kupitia kampeni hiyo ya Kili Challenge ilifanikiwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 1.1 fedha zinazotumika katika kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.


Alisema fedha ambazo zimepatikana hadi sasa zimewezesha taasisi na makundi mbalimbali nchini kuboresha shughuli za mapambano dhidi ya UKIMWI.


Alisema kampeni ya GGM Kili Challenge 2022 iliyoanza Juni 29 na kumalizika Julai 21 mwaka huu, inaunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kufikia malengo ya sifuri tatu.


Sifuri ya kwanza inalenga katika kupunguza asilimia ya maambukizi mapya, sifuri ya pili katika kupunguza unyanyapaa na sifuri ya mwisho ni kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na VVU.


“Mathalani katika kampeni ya mwaka huu jumla ya washiriki 52 ambao 24 kati yao walipanda Mlima Kilimanjaro kwa miguu na 28 waliendesha baiskeli kuzunguka mlima huo kuanzia lango la Machame na kumalizia kwenye lango la Mweka,” alisema.


Alisema kwamba kampeni ya mwaka huu ilikuwa ya mafanikio makubwa.


Pia alieleza kuwa kampeni hiyo iliambatana na upimaji wa bure wa VVU na kisukari pamoja na chanjo ya UVIKO-19 kwa wakazi wa Moshi mjini na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.


“Ninafuraha kubwa kuwataarifu kuwa katika huduma hizo zilizofanyika Julai 15 hadi 18 mwaka huu jumla ya watu 463 walipimwa VVU na hakuna hata mmoja aliyekutwa na maambukizi. Aidha watu 411 walijitokeza kupima VVU. Hii ni hatua kubwa katika mwitikio wa Watanzania wanaotaka kujua hali zao za kiafya,” alisema Shayo.


Aliongeza kuwa katika utoaji wa chanjo ya UVIKO-19, wataalam hao walifanikiwa kuwachanja watu 822, wakiwemo wanaume 365 na wanawake 427.


Zoezi la kuchangia damu lilikusanya jumla ya uniti 27 za damu, huku kondomu za kiume 9,335 na za kike 200 zikitolewa kwa wananchi waliohudhuria tukio hilo.


“Ili kutoa elimu ya kutosha kwa umma kuhusu VVU, vidonge vya PrEP pia vilisambazwa ili kupunguza makali ya kwa waathirika na kuzuia maambukizi kwa wale waliopima na kukutwa hawana ugonjwa huo, pamoja na vipeperushi 204 kuhusu masuala ya afya ya uzazi,” alisema Shayo.


Aidha, Mkurugenzi wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko alisema jumla ya Sh1.1 bilioni zilipatikana wakati wa kampeni hiyo.

Pia alitoa wito kwa wadau wengine kukaa mezani na TACAIDS ili kwa pamoja kutafuta njia mpya za kutafuta fedha zaidi za kukuza mfuko wa VVU nchini.


Mmoja wa wapanda mlima, Lucina Livigha alisema licha ya changamoto za kupanda mlima huo, wanajivunia kuwa sehemu ya kampeni hiyo yenye mafanikio ambayo ni kuokoa maisha ya Watanzania.

Share:

UNESCO KUONGEZA UWEZO WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU NA KATI KUTOA ELIMU YA STADI ZA MAISHA INAYOLENGA AFYA YA UZAZI, VVU/UKIMWI NA JINSIA KWA NJIA YA MTANDAO.

Mgeni rasmi Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akisikiliza maelezo kuhusu Kozi mtandaoni ya Stadi za Maisha, VVU/UKIMWI na Jinsia kwa vyuo vya elimu ya juu na kati.

30 Novemba 2022, Lindi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imezindua kozi ya elimu ya stadi za maisha inayolenga Afya ya Uzazi, VVU/UKIMWI na elimu ya kuzuia ukatili wa kijinsia kupitia mtandao, kwaajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati.

Uzinduzi huu umefanyika tarehe 30 Novemba 2022 uwanja wa Ilulu mkoani Lindi, kwenye wiki ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani katika Kilele cha siku ya Vijana.

UNESCO kwa kupitia mradi wake wa “Haki zetu, Maisha Yetu, Mustakabali wetu” maarufu kama O3 Plus unaofadhiliwa na shirika la maendeleo la kimataifa la Sweden (SIDA) na mpango wa kudhibiti VVU wa Umoja wa Mataifa (UN Joint program on AIDS), inalenga kuhakikisha kwamba vijana waliopo kwenye vyuo vya elimu ya juu na elimu ya kati nchini Tanzania wanapata matokeo chanya ya afya, elimu, na usawa wa kijinsia kwa kupunguza maambukizi mapya ya VVU, mimba zisizotarajiwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwakuzingatia hili UNESCO inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuongeza utoaji wa elimu ya stadi za maisha kwa kuzingatia umri, utamaduni na maadili kwenye suala la elimu ya afya ya uzazi kwa kina katika Taasisi za Elimu ya Juu na Elimu ya kati.

Kama sehemu ya mpango huu, UNESCO ikishirikiana na mashirika ya Umoja wa mataifa ya UNAIDS, UNFPA na ILO pamoja na Wizara husika (Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya) na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) vikiwemo pia vyuo vikuu (Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Iringa, Chuo kikuu cha Mt. Augustine na Chuo kikuu cha Dodoma) ilitengeneza kozi hii inayoweza kusomwa mtandaoni kupitia mfumo wa tehama wa chuo husika au simu ya mkononi. Kozi hii ilifanyiwa majaribio katika vyuo vikuu vinne (UDSM, SAUT, UoI na MUCE) mwaka 2021 ambapo zaidi ya wanafunzi 17,000 walijisajili na kusoma kozi hiyo.

Kwa kupitia majaribio haya, UNESCO ilipata mapendekezo muhimu ya kuzingatia katika kuboresha wa maudhui na mtindo wa uwasilishaji wa kozi kupitia mifumo ya tehama ya kujifunzia vyuoni. Michakato ya kuboresha kozi ilifanyika na kupelekea maboresho yaliyopendekezwa kufanyika kwa wakati.

Uzinduzi wa kozi ya mtandaoni ya elimu ya afya ya uzazi kwa kina inayozingatia stadi za maisha ni hatua muhimu ya kuboresha mazingira salama ya kujifunzia na kufundishia kwa Wanafunzi na Walimu wa Taasisi za elimu ya juu na kati. Wanafunzi watakaosoma kozi hii watapata uelewa na kujenga umahiri wa kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza kwenye maisha yao wawapo vyuoni na hata baada ya kumaliza masomo hususani kwenye masuala ya VVU/UKIMWI, afya ya uzazi, jamii na uchumi.

Pia kijana atakayesoma kozi hii ataweza kufurahia maisha yake ya chuo na kuweza kufikia malengo yake ya elimu na kuweza kuchangia kwa ufanisi zaidi katika maendeleo ya nchi kama mhitimu wa elimu ya juu na kiongozi wa baadae.

Kozi hii imetengenezwa kwa maudhui na mtindo wa kuvutia ili kuwawezesha wanafunzi kuisoma kwa wepesi wakati wowote, mahali popote kwa ratiba yao wenyewe.

Katika kuchangia mipango ya Kitaifa ya sekta ya VVU/UKIMWI pamoja na Afya, baada ya kuzindua kozi hii TACAIDS kwa kushirikiana na wizara na wadau itaisambaza kwenye Vyuo vyote vya elimu ya juu na elimu ya kati nchini.

UNESCO katika kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kama moja ya lengo la maendeleo endelevu inashirikiana na wadau wa elimu kuweka mazingira salama na jumuishi ya kusomea kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu na elimu ya kati wa Tanzania, ili kufanikisha wanafunzi kumaliza safari yao ya elimu bila vikwazo.
Share:

TAKUKURU YASHIRIKIANA NA WADAU KUZIBA MIANYA YA RUSHWA, YATIA MGUU VIBANDA VYA BIASHARA MANISPAA YA SHINYANGA

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy  akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 1,2022
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy  akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 1,2022
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy  akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 1,2022


Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imeendelea kushirikiana na wadau wa sekta za umma kudhibiti mianya ya Rushwa na kufanya uzuiaji rushwa katika miradi ya maendeleo.

Akitoa Taarifa ya TAKUKURU katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 (Julai – Septemba 2022) leo Alhamisi Desemba 1,2022, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy amesema katika kipindi hicho walijikita katika kuziba mianya ya rushwa na kuzuia rushwa kwenye miradi ya maendeleo.


“Katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo TAKUKURU Mkoa wa hinyanga ilishirikiana bega kwa bega na watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga wanaousika na utekelezaji wa miradi ya maendeleo”,amesema Kessy.

Ameeleza ufuatiliaji ulihusisha kazi za kutembelea miradi na shughuli zote za ujenzi katika miradi yote inayotekelezwa inakuwa na thamani halisi na ubora unaotakiwa.

“Kwa kufanya hivyo miradi 28 yenye thamani ya shilingi Bilioni 11.5 (11,573,687,057/=) iliyotembelewa kwa kipindi cha robo ya kwanza ikiwemo ya iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2022 iliweza kukamilika kwa ufanisi na ubora na hivyo kupelekea miradi kuwa na thamani halisi ya fedha”,ameeleza.

Ameongeza kuwa, TAKUKURU pia imeendelea kushirikiana na wadau wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kunakuwepo na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ikiwemo kupangisha vibanda vya biashara kwa wafanyabiashara kwa bei nafuu.

“Tunataka kuhakikisha vibanda vinatumiwa na wafanyabiashara halisi waliogawiwa vibanda na siyo wafanyabiashara waliopewa vibanda kuwapangisha wapangaji wengine au kuviuza kwa bei kubwa na kupelekea uwepo wa mazingira magumu ya kufanya biashara yanayoweza kuathiri pato la mkoa na taifa na hivyo kupelekea mfumuko wa bei”,amesema Kessy.


Katika hatua nyingine ameitaja mikakati ya utendaji kazi wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Desemba 2022 kuwa ni pamoja na kukamilisha majukumu yake kwa kujielekeza zaidi kwenye ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa ili kuhakikisha inatekelezwa kwa thamani halisi ya fedha iliyoletwa na serikali.

“Pia tutaendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi kupitia Kampeni ya TAKUKURU inayotembea lengo likiwa ni kuwafikia wananchi walio maeneo ya ndani wanaoshindwa kufika TAKUKURU na kuwasaidia kutatua kero zao zinazowakabili hasa zinazohusiana na masuala ya rushwa”,ameongeza.
Share:

WAZIRI DKT MABULA ASIKITISHWA NA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI IRINGA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa huo jana. Sehemu ya watendaji wa sekta ya ardhi wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) alipofanya ziara katika mkoa huo kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa huo jana. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa huo jana (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

*************************

Na Munir Shemweta, WANMM IRINGA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesikitishwa na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za Manispaa na Wilaya ya Iringa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kusababisha halamshauri hizo kushindwa kukusanya maduhuli ya serikali yatokanayo na kodi ya pango la ardhi.

Akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Iringa Novemba 30, 2022 kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi, Dkt. Mabula alibaini uzembe wa baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi wakiwemo maafisa ardhi wateule kwa kushindwa kusimamia utoaji hati za ardhi na uingizaji milki za ardhi kwenye Mfumo wa Utunzaji Kumbukumbu za Ardhi kwa njia ya kielektroniki.

Amewataka maafisa ardhi wateule katika halmashauri hizo kujitathmini kutokana na kushindwa kwao kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha wananchi wanamilikishwa na kupatiwa hatimiliki za ardhi.

Aidha, Waziri wa Ardhi Dkt Mabula amewataka maafisa hao wa sekta ya ardhi katika halmashauri hizo mbili za mkoa wa Iringa kuhakikisha kufikia Desemba mwaka huu wa 2022 wawe wamewasilisha taarifa zao za makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na hatua walizochukua kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi.

"Maana hata idadi ya viwanja mlivyonavyo hamvijui hilo ni kosa, unawezaje kukaa bila kujua idadi ya viwanja vyako katika halmashauri yako. Nataka kabla sijaondoka hapa nijue idadi ya viwanja mlivyokuwa navyo ni vingapi, na vingapi vipo kwenye mfumo na kwa nini havijaingia kwenye mfumo kwa hundred percent" alisema Dkt Mabula.

Aliongeza kwa kusema kuwa, mtendaji wa sekta ya ardhi hajui idadi ya viwanja vilivyopo kwenye mfumo wa utunzaji kumbukumbu za ardhi anawezaje kudai madeni? na kubainisha kuwa wamiliki wa ardhi wanapotambulika kwenye mfumo inakuwa ni rahisi kwa watendaji kudai madeni.

"Huna idadi maalum ya viwanja na hujaingiza kwenye mfumo wa utunzaji kumbukumbu unawezaje kudai madeni? Alihoji Dkt Mabula

Amewataka wakurugenzi wa halmashauri katika mkoa wa Iringa kutimiza wajibu wao wa kuzisimamia sekta za ardhi kwenye halmashauri zao kwa kuwa idara za ardhi ni za kwao na si za wizara na kubainisha kuwa watendaji wa sekta ya ardhi ni chachu ya kutoa elimu katika masuala ya ardhi.

Katika ziara yake Dkt Mabula amekutana na watumishi wa sekta ya ardhi kutoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Iringa pamoja na wale wa halmashauri ya Manispaa na Wilaya ya Iringa lengo likiwa kuboresha utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Mkoa wa Iringa unazo jumla ya halmashauri tano ambazo ni Manispaa ya Iringa, Mafinga Mji, Irinda DC, Kilolo DC na Mufindi DC.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DESEMBA 1,2022


Magazetini leo Alhamis December mosi 2022

















Share:

UTT YATOA ELIMU KWA WAJUMBE WA TFC SINGIDA



Afisa Mwandamizi Idara ya Masoko na Mawasiliano wa UTT AMAS Grace Ngailo akizungumza alipokuwa akitoa mada kwa wajumbe wa semina ya siku moja ya viongozi wa vyama vya ushirika nchini kabla ya kufanyika kwa mkutano skuu wa Shirikisho la Vyama vya ushirika Tanzania (TFC) Mkoani Singida.
Katibu Mtendaji wa Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) Alex Domitius (aliyekaa) akimsakiliza Afisa Mwandamizi Idara ya Masoko na Mawasiliano wa UTT AMAS Grace Ngailo alipokuwa akiwasilisha mada kwa washiriki wa semina hiyo Mkoani Singida.

(PICHA NA; HUGHES DUGILO)
Share:

Wednesday, 30 November 2022

NDOTO ZANGU NA MPENZI WANGU ZIMETIMIA, NI KUPATA KAZI NA FAMILIA

Share:

WANAWAKE WANAOSUMBUKA KUPATA MTOTO, TUMIA NJIA HII

Share:

IDADI YA WAGONJWA YAONGEZEKA MLOGANZILA


Idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imeongezeka kutoka 10854 kufikia 11188 kwa wagonjwa wa nje wakati wagonjwa wanaolazwa 793 hadi 1052 katika kipindi cha miezi miwili kuanzia Septemba hadi Novemba mwaka huu.

Ongezeko hilo limechangiwa na uboreshwaji wa huduma ikiwemo kuhamia kwa Kliniki ya Magonjwa ya Moyo (Cardiology) na Kliniki ya Mishipa ya Fahamu (Neurology) kutoka Muhimbili Upanga ambapo kwa sasa wataalamu wanapatikana muda wote Mloganzila.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Mloganzila .

Prof. Janabi amesema pamoja kuhamia kwa kliniki hizo kutoka Muhimbili Upanga lakini Kliniki za Magonjwa ya Ngozi, Upasuaji, Usingizi na ganzi, Masikio, Pua na Koo zinaendelea kama kawaida na wataalamu wapo muda wote.

"Pamoja na kliniki hizo, pia kuanzia tarehe 1 Desemba Kliniki ya Magonjwa ya Sukari na Homoni itahamia hapa Mloganzila, wataalamu waliokuwa wanapatikana Upanga wote watapatikana Mloganzila" amesema Prof. Janabi

Ameeleza kwamba ongezeko hilo limekuja na changamoto ya usafiri, Magari yanayokuja Mloganzila kutoka sehemu mbalimbali yameanza kulemewa hivyo ametoa wito kwa wakala wa usafiri wa mabasi yaendayo kasi DART kuongeza idadi ya magari yanayofika Mloganzila ili kurahisisha huduma za usafiri.

Naye Bi. Marietha John ambaye ni ndugu wa mgonjwa anayehudhuria Kliniki ya Mishipa ya Fahamu ameshukuru uongozi wa MNH kwa kuhakikisha wataalamu wanapatikana muda wote na wagonjwa wanapata huduma kwa wakati.

"Mama yangu ana tatizo la kiharusi, anahudhuria hapa kliniki , kwa kweli nashukuru tunapata huduma nzuri na Mama anapata eneo kubwa na lenye utulivu la kufanyia mazoezi" ameeleza Bi. Marietha
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger