Friday, 25 November 2022

TCRA YAKUTANA NA WATOA HUDUMA NA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA

Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imekutana na Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.

Mkutano huo uliopewa jina la ‘Consumer Forum’ umefanyika leo Ijumaa Novemba 25,2022 katika ukumbi wa TMDA Buzuruga Jijini Mwanza.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo amewataka watumiaji wa huduma za mawasiliano kufanya uhakiki wa usajili wa laini ya simu kwa kupiga *106#, kutumia namba 100 kwa ajili ya huduma kwa mteja na kutumia namba 15040 endapo watapigiwa simu au kupata ujumbe wa kitapeli.

“Ili kuhakiki namba zako za simu zilizosajiliwa kwa namba ya kitambulisho chako cha NIDA piga *106# na kama utabaini kuna namba zipo lakini hujazisajili toa taarifa kwa mtoa huduma wako wa huduma za mawasiliano ili wazuie namba hizo”,amesema Ringo.


“Siyo kila simu au SMS inayoingia kwenye simu yako ni halali. Tumia namba 15040 (Tuma neno Utapeli) endapo utapigiwa simu au kupata ujumbe wa kitapeli, sisi tutaifanyia kazi. Usitume pesa kwa mtu usiyemfahamu, hakiki Ujumbe na namba inayokutaka utume pesa kabla ya kufanya muamala na kumbuka Mawasiliano baina ya mteja wa huduma za mawasiliano ya simu na mtoa huduma wake ni kuptia namba 100 pekee”, ameongeza Ringo.


Nao Watumiaji wa huduma za mawasiliano , wameeleza baadhi ya malalamiko yao kuwa ni pamoja na namba ya huduma kwa mteja namba 100 kwenye kampuni za simu kuchukua muda mrefu kupokelewa, Laini za simu kufutwa bila mtumiaji kupewa taarifa wakisema ni bora watoa huduma za mawasiliano wangekuwa wanaziondoa tu hizo laini kwenye mfumo badala ya kumpatia mtu mwingine hali inayosababisha taarifa za mtumiaji wa awali kupelekwa kwa mtumiaji mwingine.
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano leo Ijumaa Novemba 25,2022 katika ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo  akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano leo Ijumaa Novemba 25,2022 katika ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano leo Ijumaa Novemba 25,2022 katika ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akiongoza Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akiongoza Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akiongoza Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akiongoza Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo  akiongoza Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Afisa Mkuu wa TEHAMA TCRA, Irene Kahmili akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Afisa Mkuu wa TEHAMA TCRA, Irene Kahmili akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Afisa Mkuu wa TEHAMA TCRA, Irene Kahmili akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji wa huduma za mawasiliano mkoa wa Mwanza, Jonathan Kassibu akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji wa huduma za mawasiliano mkoa wa Mwanza, Jonathan Kassibu akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.
Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

MKURUGENZI WA TGNP AFUNGA SEMINA YA UPANGAJI WA BAJETI KWA MRENGO WA KIJINSIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi amesema suala la kijinsia ni suala la maendeleo na Dunia yote ikiwemo Tanzania inazungumza na kijadili usawa wa kijinsia na hii yote ni kwasababu hata kama uko na watoto watano na kama ndani ya hao watoto hao wawili ni wakike na watu niwa kiume watakaokwenda shule ni wale wa kiume na wale wa kike watafanya kazi za nyumbani na kusubiria kuolewa.


Liundi ameyasema hayo wakati wa akifunga warsha iliyokuwa inahusu Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa Madiwani, maafisa Mipango na Bajeti, Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa madawati ya Jinsia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wawakilishi kutoka ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Halmshauri za wilaya ya Kishapu, Mbeya, Kasulu, Morogoro, Tarime, Same, Muheza na Moshi. Kwa Dar es salaam kuna washiriki kutoka manispaa za ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke


"Kwa Taifa ukiwekeza kwa mtoto wa kike na kiume kwa asilimia 50 kwa 50 maendeleo yatakuwa haraka sana kwasababu ya usawa wa kijinsia lakini ukiwekeza kwa jinsi moja maendeleo yatakuwa yanasuasua hii yote ni kuwa unaipa mzigo jinsi moja." alisema Liundi


Pia amsema sasa ni muda wa kutengeneza wawezeshaji ili kupunguza gharama za uendeshaji wa TGNP watakaotoa mafunzo kwa jamii pamoja na viongozi mbalimbali katika ngazi ya mtaa, kata, Wilaya na Mkoa kwa kuwa wa TGNP imewapa mafunzo hivyo nao wanaweza kuwa wakufunzi wazuri wa masuala ya kijinsia.


"Kwenye vikao vya ALAT tumekuwa tukipeleka wataalamu wetu ili kutoa mafunzi lakini kwasababu mmekuja na pendekezo la kujikita kwenye ARAT ngazi ya Mkoa basi tunaichukua na tutaiweka kwenye Bajeti zetu.Kutoka na mafunzo hayo basi kwenye vikao vya utengenezaji wa Bajeti wataweza kuongeza Bajeti yenye mrengi wa Kijinsia ambapo halmashauri ya Kishapu bado wameshika nafasi ya kwanza kwa kutumia ripoti ya TGNP hivyo halmashauri nyingine ziige mfano huo." Alisema Liundi


Naye Diwani wa Kata ya Ngerengere iliyopo Wilaya ya Morogoro Vijijini Kibena Kingu ameushukuru Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuweza kutoa semina kwa wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutoa maoni mbadala kwenye vikao vya upangaji wa Bajeti kwenye ngazi za Halmashauri.


Pia amasema wajumbe wa warsha hiyo watakuwa mabalozi kwenyw usawa wa kijinsia hasa kwenye utengenezaji wa Bajeti yenye mrengo wa usawa wa kijinsia na pia watakwenda kutoa elimu kwa watu wanaotoa maamuzi kwenye upangaji wa Bajeti ili kuja na mabadiliko kwenye upangaji wa Bajeti zijazo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza wakati wa kufunga wa mafunzo kuhusu Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Same, Benedict Missari akisoma mapendekezo na mkakati waliojiwekea wakatiwa kufunga kwa warsha ya Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Madiwani kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini pamoja na wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakisikiliza hituba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi alipokuwa anafunga warsha ya Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa wataalam hao yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Ngerengere iliyopo Wilaya ya Morogoro Vijijini Kibena Kingu akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuweza kutoa mafunzo ya Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia ili kujipatia ufahamu zaidi kuhusu namna ya uapangaji wa Bajeti wenye mrengo wa Kijinsia wakati wa kufunga kwa warsha hiyo iliyofanyika kuanzia terehe 21 hadi 24 Novemba 2022.
Share:

Thursday, 24 November 2022

BABU APULIZWA PESA ZAKE ZOTE BENKI NA MREMBO ALIYEMSHOBOKEA BAA


Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 kutoka Murang'a Kenya amezua gumzo mitandaoni baada ya kusimulia alivyoibiwa shilingi 700,000 na mpenzi wake.


Mwanamume huyo, Tom Waithaka Ikonya akisimulia kwa kilio na majuto alianzia kwa kusema kuwa angetaka masaibu yake kuwa funzo kwa vijana wadogo.


Ikonya mnamo Novemba 17 aliamua kwenda baa moja eneo la Maragua kaunti ya Murang’a kujiburudisha kwa siku mbili kisha kufika jijini kwa ajili ya kuanzisha biashara ya kuuza nyama.


Baada ya vileo kadhaa aliamua kutafuta chumba cha kukodi kulala bila mafanikio. Hapo alipatana na mwanadada mmoja aliyesema kuwa angempa pahali pa kulala.


Ikonya alizidi kusimulia na kusema alijaribu kuonywa na marafiki aliokuwa amewanunulia pombe ila baada ya kuwaza na kuwazua aliamua kwenda kulala kwa mwanadada huyo ambaye hakumjua.


Nyumbani kwa mpezi huyo alikula akaoga na akaamua kulala kama mfalme kwa siku 4.


Baada ya mazungumzo ya kujuana Ikoja alimwelezea nia yake ya biashara. Mwanadada huyo alimwahidi kwamba angempunguzia mzigo wa kutafuta pahali kuazisha biashara mradi tu amwamini.


Ikonja asijue hatari aliyokuwa amejiingiza, alimpa shilingi laki 7 za kusimamia bajeti ya biashara, mapato ya iwapo biashara ingeanza kwenda mrama na akamwongezea shilingi 50,000 kwa jambo mwanadada huyo alilolitaja la dharura.


Baada ya wiki moja baada ya kujuana "Nilimpa kadi ya ATM kutoa pesa hizo na kunirudishia, sikuhisi chochote kibaya kingetokea. Pia niligundua kuwa kuna kifurushi alichoacha na kilikuwa na nguo zangu. Sikufikiria sana. Niliendelea kuagiza pombe na kunywa," Ikonya alizidi kusimulia kwenye jarida hilo la Nation lililochapishwa mnamo Novemba 22.


"Nilipewa bili ya shilingi 3,100 kwenye hiyo baa na sikuwa na pesa ingine mfukoni mwangu. Pesa iliyobaki ilikuwa kwa mwanamke huyo," anasema.


Msichana huyo alikawia sana bila ya kurejea bila kujua likoenda. Ikonja aliamua kwenda kutoa pesa na kadi yake kwenye ATM.


"Kwenye ATM, alipatwa na mstuko alipoambiwa na mashine kwamba hana fedha za kutosha za kutoa shilingi 10,000 na baki yake ni shilingi 8 pekee," Mzee alisema.
Share:

MAMA ATUPWA JELA MIAKA 15 KWA KUKATA NYETI ZA MMEWE KWA KISU

Mahakama ya Maua, Meru mnamo Novemba 23 2022 iimemhukumu mama wa watoto 5 kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya jaribio la kumuua mumewe kwa kumkata sehemu zake za siri kwa kisu.


Tukio hilo lilijiri siku ya Jumamosi ya Novemba 19 eneo la Igembe Kaunti ya Meru huko Kenya.


Kulingana na hukumu iliyotolewa na jaji mkuu Tito Gesora, mama huyo alinuwia kumuua mumewe alipokuwa amelala baada ya mume wake kukataa kugawanya shamba lake la miraa.


Mwanamume huyo alisimulia jinsi alivyoshtuka alipomwona mkewe akinyanyua kisu majira ya saa 3 asubuhi, akimpiga kichwa na kiungo chake cha siri huku akilia kwa maumivu. Mkononi alishika kisu cha jikoni alichotumia kutekeleza uhaini huo.


Mkulima wa miraa mwenye umri wa miaka 60, alijaribu kupiga kengele lakini alitokwa na damu nyingi hadi kupoteza fahamu.


Mahakama ilisema mkewe huyo katili hakutosheka, alijaribu kulazimisha kunywa kemikali isiyojulikana mdomoni mwa mumewe huku binti yao akijionea na akipiga kamsa baada ya mama mzazi kumuamuru anyamaze mara moja.


Mtoto alikimbia na kuomba msaada, na kuvutia wanakijiji ambao walikimbilia nyumbani wakiwa na hamaki kuu huku mama huyo akijaribu kuzua ghasia.


Mwanamke huyo kisha alijaribu kutoroka lakini wanakijiji walimkamata na kumpiga kitutu ila akaokolewa na chifu wa eneo hilo ambaye alimpeleka katika kituo cha polisi cha Laare.


Mume huyo sasa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Chaaria Mission.


Mahakama ilipigwa na butwaa kumwona mkewe akimfanyia kitendo hicho licha ya kuoana kwa muda mrefu. Alisema alikataa kugawanya shamba lake kwa sababu watoto wote walikuwa bado shuleni.


Mama aliiambia mahakama kuwa hakufahamu alichokuwa akifanya, alijikuta tu akimshambulia mumewe huku akijitetea kwamba hakukusudia na anaugua ugonjwa wa akili.
Share:

TRA YATOA MSAADA WA MATANKI YA MAJI HOSPITALI MPYA YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA WIKI YA SHUKRANI KWA MLIPA KODI

Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kushoto)  akishikana mkono na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali hiyo.

Na Kadama Malunde -  Malunde 1 blog 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi matanki mawili ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 20,000 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi "Asante kwa kulipa kodi kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa;Kazi Iendelee". 

Matanki hayo yamekabidhiwa leo Alhamisi Novemba 24,2022 na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila katika hospitali hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi matanki hayo mawili yenye ujazo wa lita 10,000 kila moja, Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela amesema TRA imetoa matanki hayo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa walipa kodi ili kupunguza changamoto ya vifaa vya kutunzia maji katika hospitali mpya ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.

“Sisi TRA tupo katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi iliyoanza Novemba 23 hadi Novemba 25,2022. Tumeleta matanki haya ili kupunguza changamoto ya vifaa vya kutunzia maji kwenye hospitali hii ya Rufaa mkoa wa Shinyanga”,amesema Kabyemela.

Akipokea matanki hayo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila ameishukuru TRA kwa kuikumbuka hospitali hiyo mpya na kuipatia matanki ya kuhifadhia maji akibainisha kuwa hospitali hiyo inahitaji maji kila wakati.

“TRA mmefanya jambo jema kuleta matanki ya kuhifadhia maji, hili ni jambo muhimu sana kwa sababu tunahitaji maji kila wakati kwa ajili ya huduma mbalimbali katika hospitali hii mpya ambayo imeanza kufanya kazi hivi karibuni hapa Mwawaza”,amesema Dkt. Luzila.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kwenye suti katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila leo Alhamisi Novemba 24,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kwenye suti katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila leo Alhamisi Novemba 24,2022.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kushoto)  akishikana mkono na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila akizungumza wakati akipokea Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali hiyo. Kushoto ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mdesa (wa sita kulia) akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog
Share:

WAFANYAKAZI WA MGODI WA BARRICK NORTH MARA WALIVYOPOKEA TUZO YA USHINDI WA MLIPA KODI WA KWANZA NCHINI TANZANIA


Baada ya kutunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza ya Mlipa Bora na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kilele cha Wiki ya Mlipa Kodi iliyomalizika hivi karibuni,Wafanyakazi wa Mgodi wa Twiga Minerals wa Barrick North Mara, wamepokea taarifa hiyo kwa furaha na kulipokea kombe la ushindi lilipowasili mgodini hapo.

Twiga Minerals Corporation, inasimamia shughuli za: Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga; Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Tarime– pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi (Pangea) ambao pia upo Shinyanga ambao kwa sasa uko katika hali ya kufungwa.

Mnamo mwaka wa 2020, Twiga Minerals Corporation ililipa kodi ya mapato kiasi cha dola milioni $119, ambapo mwaka 2021, ililipa dola milioni $96.

Mapema mwaka huu, Wizara ya Madini iliitambua Twiga kama mchangiaji mkubwa wa mapato ya serikali kwa mwaka 2021. Kampuni yake tanzu - North Mara Gold Mine pia ilishinda tuzo ya Mshindi wa Kwanza miongoni mwa Wamiliki wa Leseni Maalumu za Uchimbaji katika Utekelezaji sera ya ushirikishwaji wazawa katika mnyororo wa uchumi wa madini (Local content) kwa mujibu wa Sheria ya Madini kifungu namba 123 mnamo mwaka 2021.

Akitoa taarifa ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha robo mwaka kwa vyombo vya habari mwezi Oktoba, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold Corporation Dk, Mark Bristow, alisema kuwa Twiga imechangia kwa zaidi ya dola bilioni 2.187 katika uchumi tangu mwaka 2019. Kati ya hizo, dola milioni 878 zililipwa katika mfumo wa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali.
Kuhusiana na kusaidia biashara za ndani, Dk. Bristow alisema kuwa asilimia 80% ya manunuzi yenye thamani ya kiasi cha dola bilioni $ 1.025 yalikuwa ya bidhaa za ndani.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo

Share:

MOTO WATEKETEZA BWENI NA KUUA WATOTO WENYE ULEMAVU KITUO CHA BUHANGIJA


Muonekano wa Bweni lililoteketea kwa moto na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Bweni lililoteketea kwa moto na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Moto ambao haujajulikana chanzo chake umeunguza bweni la Kituo cha Kulelea Watoto wenye ulemavu cha Buhangija Mjini Shinyanga na kusababisha vifo vya watoto watatu wa kike wenye ulemavu wa macho.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema moto huo umetokea jana Novemba 23,2022 majira ya saa 2 na nusu usiku katika bweni B lililokuwa na watoto 32 katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu (watoto wenye ualbino, viziwi na wasioona).

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linafanya uchunguzi wa tukio la moto ambao haujafahamika chanzo chake na kuteketeza bweni katika kituo cha kulelea watoto walemavu Buhangija kilichopo mkoa wa Shinyanga na kusababisha vifo vya watoto watatu wa kike”,amesema Kamanda Magomi.

Amewataja watoto waliofariki dunia kuwa ni Niliam Limbu (12), Caren Mayenga (10), Catherine Paulo (10) wote ni walemavu wa macho (wasioona), wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Buhangija.

Amesema kufuatia tukio hilo mali mbalimbali za wanafunzi na za shule zimeharibika ambazo bado thamani yake haijafahamika na hakuna majeruhi yeyote.

“Baada ya taarifa za tukio hili kupatikana Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio, Pia jeshi la zimamoto na uokoaji nalo lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto ule pamoja na TANESCO kufanikisha uzimaji wa umeme haraka katika eneo lile ili kuzuia madhara makubwa ambayo yangeweza kutokea kutokana na moto ule”,ameeleza Kamanda Magomi.



Amefafanua kuwa kituo cha kulelea watoto Buhangija kilikuwa na watoto 163 waliolala bwenini kituoni hapo siku ya tukio ambapo watoto wenye ualbino ni 77 kati yao wa kike 38, wa kiume 39, wasioona 20 wa kiume 9, kike 11 ambapo watatu wamefariki dunia na Viziwi 66 kati yao wa kiume ni 31 na wa kike 35.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila amethibitisha kupokea miili mitatu ya watoto waliofariki dunia kutokana na ajali ya moto katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija.
Share:

NAIBU GAVANA WA BENKI KUU YA BURUNDI AIPONGEZA BENKI YA CRDB BURUNDI KWA MIAKA 10 YA MAFANIKIO


Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni Mama ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (watatu kulia) akikabidhi tuzo maalumu ya shukrani ya maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi kwa Naibu Gavana wa kwanza Benki Kuu ya Burundi, Desire Musharitse (katikati) pamoja na Naibu Gavana wa pili, Marie Goreth Ndayishimiye. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Hosea Kashimba (wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Burundi, Fredrick Siwale (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Menard Bucumi.

========= ======== ========

Bujumbura, 24 Novemba 2022 – Benki Kuu ya nchini Burundi (BRB) imeipongeza Benki ya CRDB Burundi kwa mafanikio makubwa iliyopata katika kipindi cha miaka 10 ya uwepo wake nchini Burundi.


Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Burundi kwa niaba ya Gavana katika mkutano na ujumbe wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyeambatana na wajumbe wa Bodi ya kampuni Mama ya Benki ya CRDB pamoja na kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi. Ujumbe huo umetembelea Benki Kuu ya Burundi kutoa shukrani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya utoaji huduma za kibenki ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi.
Akizungumza katika mkutano, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Burundi, Desire Musharitse alisema Benki Kuu ya nchi hiyo inafurahia sana kwa uwepo wa Benki ya CRDB nchini Burundi kwani imekua sehemu ya uwezeshaji wa miradi mingi ya kiuchumi kwa nchi lakini pia imechangia uwezeshaji wa wafanyabiashara.


“Tulipata matatizo yaliyopelekea changamoto kubwa ya upatikanaji wa fedha za kigeni mwaka 2015 lakini tulipata msaada mkubwa sana kutoka Benki ya CRDB na hakika hilo limedhihirisha ule usemi wa rafiki wa kweli hujulikana wakati wa shida” alisema Musharitse.
Tangu ilipoingia katika soko la Burundi mwaka 2012, Benki ya CRDB imekua ikifanya vyema sokoni na katika kipindi cha miaka 10 tu imeweza kushika nafasi ya tatu kati ya benki kumi na tatu zinazotoa huduma za kibenki nchini Burundi. Katika kipindi hiko Benki imeweza kufungua matawi manne huku tawi la tano likitarajiwa kufunguliwa mapema mwaka 2023.


“Kutokana na kufanya vizuri kwa Benki ya CRDB Burundi tunatamani kuona ikifungua matawi mengi zaidi nje ya Bujumbura lakini pia kuweza kufanikisha upatikanaji wa mikopo kwa njia za kidigitali kama ambavyo wamekua wakitoa huduma nyingine kidigitali” aliongeza Musharitse.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameishukuru Benki Kuu ya Burundi kwa ushirikiano mkubwa kwa Benki ya CRDB Burundi uliopelekea kampuni tanzu hiyo kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi cha miaka 10. Sambamba na hilo Nsekela ameishukuru Serikali ya nchi hiyo chini ya Rais Evariste Ndayishimiye kwa kuipatia eneo Benki ya CRDB Burundi katika makao makuu mapya ya nchi ya Gitega ili kufanikisha ujenzi wa tawi jipya.


“Maraisi wetu wanatamani kuona ushirikiano wa sekta binafsi za Tanzania na Burundi lakini pia wamezungumza juu ya miradi ya kimkakati kati ya nchi hizi mbili ikiwemo mradi wa SGR na sisi tuko tayari kuisadia kampuni yetu tanzu kushiriki katika mradi huu kwa upande wa Burundi kama ambavyo tumeshiriki kwa upande wa Tanzania” alisema Nsekela.
Aidha, alisema Benki ya CRDB inatarajia kuingia nchini DRC hivi karibuni jambo ambalo litachangia kukuza biashara kati ya Burundi na DRC lakini pia ushirikiano wa biashara kati ya nchi hizo na Tanzania ambazo kwa pamoja ni sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


“Adhma yetu katika masoko tunayohudumia sio tu kutoa huduma bora bali kutoa mchango katika uchumi na kubadilisha maisha ya watu tunaowahudumia hivyo tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Benki Kuu ya Burundi ili kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini Burundi” aliongeza Nsekela.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Hosea Kashimba na yeye alitoa shukrani za bodi kwa Benki Kuu ya Burundi kwa ushirikiano mkubwa uliochangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Benki ya CRDB Burundi katika kipindi cha miaka 10 tangu kuingia katika soko la Burundi.


“Tunaona muelekeo mzuri wa nchi na tunaamini ndani ya kipindi kifupi kijacho tutaweza kuwa Benki kiongozi hapa nchini Burundi hivyo basi tunaomba ushirikiano huu uendelee kwani hatuwezi kufikia malengo yetu bila ushirikiano wenu” alisema Kashimba ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma PSSSF.
Maadhimisho ya miaka 10 ya Benki ya CRDB Burundi yameambatana na shughuli mbalimbali zenye lengo la kushukuru jamii ya watu wa Burundi kuiwezesha Benki ya CRDB Burundi kufanya vizuri sokoni. Sehemu ya shughuli zilizofanyika ni pamoja na kutoa misaada kwa makundi yenye uhitaji maalum, uandaaji wa shindano la mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana pamoja na ujenzi wa mradi wa usafi kwa jiji la Bujumbura.


Benki ya CRDB Burundi ilianzishwa nchini Burundi mnamo mwaka 2012 chini ya sheria ya makampuni nchini Burundi. Benki ya CRB Burundi inatoa huduma kwa wateja wa taasisi na makampuni pamoja na wateja binafsi huku ikimilikiwa na kampuni Mama ya Benki ya CRDB kwa asilimia 100. Benki ya CRDB Burundi inatoa huduma kupitia matawi manne sambamba na mawakala wa benki zaidi ya 600. Hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka 2022, Benki ya CRDB Burundi imetoa mikopo ya zaidi ya Faranga Bilioni 300 za Burundi kwa sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, viwanda na utalii.
Share:

Wednesday, 23 November 2022

SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE 1-1 MBEYA CITY


*********************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imelazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya timu ya Mbeya City, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Sokoine Mbeya.

Katika mchezo huo Simba Sc ilianza kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wao Mzamiru Yasin dakika ya 15 na kuwapelaka mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili klabu ya Mbeya City iliingia ikiwa inahitaji kusawazsiha bao kwani walicheza mpira wa kushambulia bila mafanikio mpaka dakika za lala salama kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Tariq Seif dakika ya 78.
Share:

HII NDIO DAWA YA KWELI KWA WANAOOTA NDOTO MBAYA, KUKOMESHA MAUZAUZA

Jina langu ni Nasra kutokea Tanga nchini Tanzania, miaka kadhaa nyuma iliyopita nilijikuta kwenye sehemu ya mauzauza, nilikuwa naota ndoto mbaya, nilikuwa katika mazingira ya shule, kwa kuwa mazingira yale yalijaa mauzauza sikuweza kushangaa sana.

Ilikuwa haipiti wiki mimi sijaugua, nilikuwa naota ndoto kama nakabwa, kipindi hicho bado nipo Shule, ilikuwa ni hali ya kuhatarisha katika maisha yangu, kiukweli katika dua na jamaa zangu lakini haikusaidia lolote.

Tulikuwa tunaamka pamoja na rafiki yangu muda wa saa 11 alfajiri, tunaomba dua hadi saa 12 asubuhi, kisha tunakwenda kuungana na wenzetu. Usiku saa nne kamili tunaanza dua walau nusu saa kisha tunakwenda kulala.

Siku moja nakumbuka ilikuwa Ijumaa kuamkia Jumamosi, kama kawaida yetu baada ya prepo tulikwenda kufanya dua kwenye kajumba ambako kalikuwa kama mita 50 toka mabweni yalipo.

Wakati tunaendelea kupiga dua ya nguvu, tukiwa tumeshikana mikono, ghafla ulijitokeza moto unaowaka katikati yetu,

kwa kuwa mauzauza nilikuwa nishayazoea, sikushtuka sana tuliendelea kufannya dua kwa nguvu sana mara moto ule ukatoweka.

Baada ya dakika chache akajitokeza paka pale ulipokuwa moto, tukakomaa naye kwa dua hadi akaondoka, baada ya kumaliza kusali tuliagana na kila mmoja kwenda kulala bwenini kwake.

Usiku wa manane mimi waliniibukia mazima, walinifata kitandani na kuninyanyua nikaelea angani juu ya kitanda, nilipiga kelele sana watu wakaniona naelea angani.

Hali Ile iliniogopesha sana, nilishuka na kubamizwa kitandani, cha ajabu kesho yake niliamka mwlili unaniuma, maumivu mwili mzima ila sikumbuki chochote kilichotokea.

Ilinibidi niwaombe walimu wanipe likizo ya muda nikapumzike nyumbani, kabla sijafika nyumbani nilinunua gazeti na kulisoma, kabla sijamalizia kulisoma nilikutana tangazo la Dr. Kiwanga kuwa anaweza kutuliza hali ya mauzauza pamoja na kuota ndoto za kutisha.

Nilichukua namba yake ambayo ni +254 769404965, nilipiga ile namba, akapokea nikamuelezea matatizo yangu, akanifanyia matambiko pamoja na dawa na tangu wakati ule ile hali ikakoma.

Hadi naandika ujumbe huu kwa sasa nipo shuleni na sijawahi kuona tena hali ile pamoja na wenzangu, binafsi namshukuru sana Dr. Kiwanga kwa tiba yake.

Ukiachana na hilo, Dr. Kiwanga ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda katika michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Vile vile anatibu magonjwa kama Kaswende, Kisonono, Kifua Kikuu, Presha na mengine mengi, kwa mawasiliano zaidi mtumie barua pepe; kiwangadoctors@gmail.com, tembelea tovuti yake; www.kiwangadoctors.com au piga simu +254 769404965.

Mwisho.
Share:

MFARIJI MKUU


Rais Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara iliyopo Babati katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo tarehe 23 Novemba, 2022. Picha IKULU
Share:

HII NDIO MBINU ILIYOWASAIDIA WENGI KUFAULU MITIHANI YA CHUO


Jina langu ni Pascal mkazi wa Buza, Dar es Salaam, kwa sasa nimuhitumu wa Chuo Kikuu nikiwa na Shahada ya Biashara, nafanya kazi zangu na kupata fedha nzuri.

Kipindi nasoma shule ya msingi sikuwa mwanafunzi mwenye akili darasani, kila mara nilikuwa mtu wa mwisho kiasi kwamba hadi wanafunzi wenzangu walikuwa wananicheka na kunikejeli.

Halafu walimu mwenyewe walikuwa wanatambua sikuwa na uwezo mzuri wa kimasomo na hadi naweza kusema walishakata tamaa na mimi na kuamini sitoweza kuja kubadilika.

Nilipofeli shule ya msingi wengi walisema hatukutegemea kama wewe utaweza kuja kufaulu masomo maana tunajua uwezo wako ilivyokuwa mdogo kimasomo.

Nilihitimu shule ya msingi nikiwa na miaka 12, bado nilionekana mdogo sana, ndipo wazazi wangu wakataka nikarudie tena kusema darasa la saba.

Wakati nataka kurudi tena shule ya msingi ili kurudia mtihani wa darasa la saba, kuna mjomba yangu aliyekuwa anaishi Nairobi nchini Kenya alikuja kututembelea. Aliniuliza kama nilifaulu masomo na kumjibu hapana, alishangaa sana kusikia nimefeli na nina mpango wa kurudia tena shule.

Akaniambia kuna mtu anaitwa Dr. Kiwanga toka Kericho, Kenya amekuwa akiwasaidia sana wanafunzi wengi kufaulu mitihani yao, na kana kwamba ningemwambia mapema kama nina shida katika masomo yangu, angeniunganisha naye mapema.

Mjomba alimpa mama namba ya Dr. Kiwanga ambayo ni +254 769404965, tuliweza kuwasiliana naye na kumueleza kuwa ndio naenda tena kurudia darasa la saba baada ya kufeli. Dr. Kiwanga alimueleza mama kuwa safari hii nikirejea shule nitakuwa mwanafunzi kinara katika masomo yangu.

Na kweli niliporudi shule nilikuwa nafaulu sana mitihani hadi mwenyewe nikawa nashangaa imewezekanaje, ila kiu yangu kubwa ilikuwa ni kuona nafaulu mtihani wa mwisho wa darasa la saba.

Ilifika siku ya mtihani wa mwisho, kila mtihani uliokuwa unakuja mbele yangu nilikuwa naona ni mwepesi sana tofauti na ule mtihani wa mwanzo ambao nilikuwa sielewi chochote.

Majibu yalitoka nikawa nimefaulu kwa kiwango cha juu zaidi, basi miezi kadhaa mbele nikajiunga na sekondari ambapo nako nilifanya vizuri kimasomo hadi nilipofanikiwa kujiunga na chuo kikuu.

Chuo Kikuu niliweza kukutana na wanafunzi wenzangu ambapo walikuwa wananicheka kipindi kile nikifanya vibaya shule ya msingi, walikuwa wamenizidi mwaka mmoja kimasomo lakini kuna baadhi ya mambo nilikuwa naweza kuwafundisha. Nilikuja kuhitimu Chuo Kikuu nikiwa na ufaulu mzuri sana na sasa nimeajiriwa.

Ukiachana na hilo, Dr. Kiwanga ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda katika michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Vile vile anatibu magonjwa kama Kaswende, Kisonono, Kifua Kikuu, Presha na mengine mengi, kwa mawasiliano zaidi mtumie barua pepe; kiwangadoctors@gmail.com, tembelea tovuti yake; www.kiwangadoctors.com au piga simu +254 769404965.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger