Tuesday, 22 November 2022

TGNP YATOA YA MAFUNZO UANDAAJI WA BAJETI YENYE MRENGO WA KIJINSIA KWA MADIWANI, MAAFISA MIPANGO, MAENDELEO YA JAMII NA WARATIBU WA MADAWATI YA JINSIA


Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu Uandaaji wa Bajeti kwa Mrengo wa Kijinsia kwa maafisa mipango na bajeti, maendeleo ya jamii na waratibu wa madawati ya jinsia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wawakilishi kutoka ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Halmshauri za wilaya ya Kishapu, Mbeya, Kasulu, Morogoro, Tarime, Same, Muheza na Moshi. Kwa Dar es salaam kuna washiriki kutoka manispaa za Ubungo, Kinondoni, Ilala na Temeke.
Afisa Programu Idara ya Mafunzo kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai akizungumza kuhusu namna Mtandao huo unavyofanya kazi na jamii hasa kwenye uandaaji wa Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia wakati wa warsha ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini inayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Lihoya Chamwali akitoa mada kuhusu namna wanavyoweza kuweka usawa wakjinsia pamoja na kuweka bajeti yenye mlengo wa kijinsia kwa Wataalam wa Bajeti za Halmashauri ambao ni Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Madiwani kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini leo tarehe Novemba 22, 2022.
Baadhi ya Madiwani, Maafisa Mipango na Bajeti pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Harmashauri mbalimbali za hapa nchini wakichangia mada kwenye warsha ya kuwajengea uwezo kuhusu Bajeti yenye mlengo wa jinsia inayofanyika kwa siku nne jijini Dar es Salaam.
Semina ikiendelea
Share:

TUME YA UTUMISHI YA MAHAKAMA YAKUTANA NA WAJUMBE KAMATI ZA MAADILI


Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahimu Juma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

TUME ya Utumishi ya Mahakama yakutana na wajumbe wa kamati za maadili ngazi ya Mkoa na wilaya mkoani Shinyanga, kujadili maadili na utoaji haki kwa wananchi.

Mkutano huo umefanyika leo Novemba 22, 2022 katika ukumbi wa mikutano Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, ambao umeongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahimu Juma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Amesema jana walifanya kikao na watumishi wa mahakama pamoja na wadau, ambapo leo wamekutana na wajumbe wa kamati za maadili kuanzia ngazi ya wilaya hadi Mkoa, ili kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kuzingatia maadili na utoaji haki kwa wananchi.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kujadiliana kwa pamoja, kubadilisha uzoefu, na kuona namna ya kujadili changamoto ambazo zinasababisha ukwamishaji wa utoaji haki kwa wananchi na kwa wakati.

“Taarifa ambayo tumeipata jana kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma kuwa, kumekuwa na changamoto ya matimizi ya mtandano katika usilikizwaji wa mashauri, upungufu wa vitendea kazi ikiwamo Kopyuta na kushindwa kutoa pia nakala za hukumu mapema,”anasema Jaji Mkuu Ibrahimu Juma.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu kamati za maadili Mkoa wa Shinyanga, amesema kumekuwa na changamoto ya uelewa mdogo kwa wananchi kuwasilisha malalamiko yao kujua namna ya kudai haki ambapo elimu inahitajika zaidi.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahimu Juma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama akizungumza kwenye mkutano huo.

Jaji wa Mahakama ya Rufani na Kamishna Tume ya Utumishi wa Mahakama Dk Gerald Ndika, akiwasilisha muundo wa majukumu ya kamati za maadili.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama Timothy Ndanya akiwsilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya kamati za maadili Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Pfof Siza Tumbo.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.
Share:

BODABODA AFIKISHWA MAHAKAMANI TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI 'KUMBAKA' BINTI YAKE WA MIAKA 11


Na Walter Mguluchuma,Katavi.

Mwendesha Boda boda Idrisa Said Bayaga(32) wa Kituo cha waendesha pikipiki cha Nyerere Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya(mapenzi) tendo la ndoa(MAHARIMU)na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe mwenye umri wa (11).


Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu mfawidhi mwandamizi Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Gosper Luoga.

Mwendesha mashtaka mwanasheria wa Serikali Gregoli Mhangwa ameiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe kwa nyakati tofauti kuanzia kipindi cha mwezi Aprili   mwaka huu hadi mwezi Septemba .

Aidha kuwa kitendo hicho cha kufanya tendo la ndoa na mtoto wake mwenye umri mdogo wa miaka 11 ni kutenda kosa kinyume na kifungu cha sheria Namba 158(1) (a) cha kanuni ya adhabu sura 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019.

Mtuhumiwa huyo baada ya kusomewa mashitaka hayo na mwanasheria wa Serikali alikana na mashtaka hayo ya kutenda kosa la kufanya tendo la ndoa kwa nyakati tofauti na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe.

Baada ya mtuhumiwa kukana mashtaka hayo mwendesha mashtaka Gregoli Mhangwa aliiambia Mahakama kuwa upande wa mashtaka umeishakamilisha upelelezi wa kesi hiyo .

Hivyo aliiomba Mahakama iweze kuendelea na hatua zinazofuata za kimahakama kufuatia kukamilika kwa upelelezi uliofanywa na pande wa mashtaka .

Kufutia maombi hayo ya upende wa mashitaka Hakimu Luoga alikubaliana na hoja hiyo iliyotolewa mbele yake na upande wa mashitaka ambapo mtuhumiwa Idrisa Said Bayaga alisomewa hoja za awali za mashtaka .

Baada ya kutolewa mahakamani hapo hoja za awali kuwasilishwa Mahakani hapo Hakimu Mkazi mfawidhi Mwandamizi Gosper Luoga aliiambia mhakama kuwa mdhamana wa mshitakiwa upo wazi na anatakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyo hamishika na dhamana kuwa wazi Huku mtuhumiwa kushindwa kutimiza masharti hayo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo Desemba 5 itakapoanza kusikilizwa ambapo mtuhumiwa amekwenda rumande kwenye gereza la mahabusu la Mpanda Mjini.

Chanzo - Katavi Press club blog
Share:

Video Mpya Kali : NTEMI OMABALA - ZUNYAGA


Msanii maarufu Ntemi Omabala anakualika kutazama video ya wimbo wake mpya wa Mapenzi unaitwa Zunyaga (Kubali). Katika wimbo huu ameimba kwa Lugha ya Kisukuma lakini maneno yametafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili
Tazama Video Hapa Chini
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 22,2022

















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger