Monday, 21 November 2022

TUME YA UTUMISHI YA MAHAKAMA IMEFANYA MKUTANO NA WADAU WA MAHAKAMA MKOA WA SHINYANGA



Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA 
 
TUME ya Utumishi ya Mahakama imefanya mkutano na wadau wa Mahakama Mkoa Shinyanga.

Mkutano huo umefanyika leo Novemba 21. 2022 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, amesema wamefanya ziara ya kukutana na wadau hao kuitangaza Tume hiyo, pamoja na kujadili uboreshaji wa utoaji haki kwa wananchi na kwa wakati.

Amesema Tume hiyo imekutana na wadau pamoja na watumishi wa Mahakama, kusikiliza maoni na kuboresha juu ya utoaji haki kwa wananchi kupitia Mahakama.

“Tume ya Utumishi wa Mahakama tumefanya ziara hapa Shinyanga, kwa lengo la kujadili uboreshaji na utoaji haki kwa wananchi, na Tarehe 25 mwezi huu tunazindua Mahakama za wilaya 18, na Kanda hii ya Shinyanga tutazindua Mahakama za wilaya ya Busega na Itilima,”amesema Prof Juma.

Naye Jaji Kiongozi na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mustapher Siyani, anasema matarajio ya Tume hiyo ni kuboresha utendaji kazi wa Mahakama, pamoja na kupunguza mrundikano wa mashauri.

Amewataka pia mawakili wasomi, wanasheria wawe wanawashauri wateja wao wafanye usuluhishi juu ya kesi zao, na siyo kila kesi ipelekwe mahakamani ili kupunguza mrundikano wa mashauri na kutopoteza muda.

“Mrundikano wa Mashauri uliopo Mahakamani hadi sasa kuanzia Mahakama za Mwanzo, Wilaya, hadi Mahakama kuu ni 3,419,”amesema Siyani.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma, amesema ziara hiyo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama utaboresha utendaji kazi wa mahakama pamoja na utoaji haki kwa wananchi na kwa wakati.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama akizungumza kwenye mkutano huo.

Jaji Kiongozi na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mustapher Siyani, akizungumza kwenye mkutano huo.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.
Share:

HII NDIO DAWA YA MIGOGORO YOTE NDANI YA NDOA!


Jina langu ni Debora kutoka Mwanza, Tanzania, mwaka mmoja baada ya kufunga ndoa na mume wangu Kelvin mambo yalianza kubadilika hasa kwa upendo aliokuwa nao mwanzo mume wangu alipunguza.


Hali hii ilinipa wasiwasi mkubwa sana lakini kiukweli mume wangu nilimkabidhi moyo wangu wote hivyo sikumfikilia vibaya licha ya hayo niliyokuwa napitia.

Tukiwa tumelala kitandani aliniambia mke wangu sitaki nikuone mtandaoni wewe ni mke tayari na unatakiwa kuishi kama mke kwa

Nilikuwa namheshimu na kumpenda sana mume wangu sikutaka kubishana nae japo iliniuma kwani nilikuwa nimezoea kuingia mitandao sana tangu nikiwa kwetu.

Nilimpatia simu yangu usiku ule ule kisha akafuta mafaili yote ya mtandaoni, hapo nilijiuliza maswali mengi kwanini kafanya vile au hataki niwe natumia simu, nilijiuliza ila sikuweza kupata jibu kwa muda huo mimi nilizidi kuongeza upendo katika ndoa.

Nilianza kuamka saa1 1 kila siku namuandalia chai, namchemshia maji ya kuoga huku nikijitahidi kumpatia haki yake ya ndoa kwa muda licha ya kumfanyia hayo yote sikuona muitikio mkubwa wa upendo kutoka kwa mume wangu.

Nilipitia kipindi kigumu kidogo mpaka nikaanza kuhudhuria semina mbalimbali za ndoa bila mume wangu kujua ili kikubwa niweze kumfurahisha mume wangu ambaye nilimpenda kuliko mtu yeyote katika maisha yangu.

Siku moj wakati ameenda kuoga niliweza, kuchukua simu yake kisha nikaanza kukagua kimoja baada ya kingine niliingia kwenye meseji ndipo nilipokutana na mambo mazito. Baada ya kutoka kuoga nilimwambia mume wangu samahani nimekuta meseji mbaya kwenye simu yako ni nani yako unayechati naye.

Vile mume wangu alikasilika sana na kuniambia niondoke pale nyumbani, nilimuomba msamaha lakinni hakuweza kunisikia mimi

niliondoka kwa mume wangu na kurudi kwa wazazi wangu kumbe alikuwa na mwanamke nje ila mimi sikuweza kumjua.

Baaada ya kukaa kwa wazazi kama wiki mbili, nilikutana na rafiki yangu nikamueleza jinsi nilivyofukuzwa na mume wangu, rafiki yangu alihudhunika sana, aliniambia nakupa namba hii (+254 769404965) ya Dr. Kiwanga. Wasiliana naye.

Niliwasiliana naye, kabla hajanipa tiba yake aliniuliza kwanini nimeamua kuondoka nyumbani kwangu nilimuelezea akanipa pole na kuniambia nakufanyia hii dawa itakusaidia na utaona matokeo ndani ya muda mfupi.

Baada ya siku tatu, mume wangu alinipigia simu huku akiniomba msamaha, akaomba nirudi nyumbani tuongee, nilifurahi sana kusikia vile.

Nilirudi nyumbani huku nimefurahi nilimkuta mume wangu, alinikumbatia na kunambia nimsamehe kwa yote aliyoyafanya, nilifrahi sana. Namshukuru sana, Dr. Kiwangwa kwa kunirejeshea ndoa yangu.

Ukiachana na hilo, Dr. Kiwanga ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda katika michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Vile vile anatibu magonjwa kama Kaswende, Kisonono, Kifua Kikuu, Presha na mengine mengi, kwa mawasiliano zaidi mtumie barua pepe; kiwangadoctors@gmail.com, tembelea tovuti yake; www.kiwangadoctors.com au piga simu +254 769404965.

Mwisho.
Share:

CCM YASIMAMISHA UCHAGUZI CCM SIMIYU, MBEYA, ARUSHA

 

Na Dotto Kwilasa,DODOMA.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesimamisha uchaguzi katika mikoa mitatu kwa nafasi zilizoonyesha kuwa na changamoto pamoja na kufuta uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho Kutokana na sababu za rushwa .


Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa  baada ya tukijiridhisha kama hakutakuwa na  changamoto ,chama kitaruhusu  uchaguzi kufanyika na kama watabaini  changamoto wataondosha wagombea wenye changamoto na wasio na changamoto kuendelea na uchaguzi kwa nafasi husika.


Amesema baada ya uchunguzi wa kina wa changamoto katika maeneo husika ,hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahusika kugombea na kisha kuwakabidhi katika vyombo vyenye dhamana ya kufuatilia masuala ya rushwa.


“Mikoa ambayo tumefanya  uamuzi ni pamoja na kufuta uchaguzi wa umoja wa Vijana mkoa wa Simiyu , pia tumesimamisha uchaguzi wa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mbeya kwa sababu ya tuhuma mbalimbali zikiwemo za rushwa ambako nako tunafanya uchunguzi wa kina tukikamilisha tutatoa taarifa ya uamuzi wa chama,"amesema Chongolo.


Pamoja na hayo amesema," tumesimamisha uchaguzi wa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  mkoa wa Arusha kwa sababu hiyo hiyo ya rushwa na  tukikamilisha uchunguzi tutatoa taarifa za uamuzi wa chama ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi kuendelea".


Katibu Mkuu huyo pia amezungumzia kuhusu tukio la wanachama kuondoka na boksi la kura katika uchaguzi uliofanywa jana (juzi)  mkoa wa kichama wa Magharibi Zanzibar na kueleza kuwa watu hao walienda na boksi hilo kwenye chumba kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kuhesabia kura .


 “Sasa  tunataka kuangalia uchukuaji wa boksi hilo ulilenga kuhesabu kura au ulikuwa una lengo lingine,tutafuatilia tukijiridhisha tutachukua uamuzi ukiwemo kuufuta uchaguzi na kurudiwa upya ili kutenda haki ,tukijiridhsisha kwamba lengo la  kuchukua boksi hilo ulilenga kwenda  kuhesabu kura basi tutaruhusu matokeo ya uchaguzi huo yaendelee kama yalivyo.”amesema


Aidha Chongolo amezungumzia kuhusu changamoto iliyopo sasa ndani ya chama hicho kuwa ni kuwepo kwa wajanja  wachache wanaogombea nafasi mbalimbali au wapambe wao kutengeneza msukumo wa kuonyesha wao ni maalum kuliko wengine  na wao ndio wanaotakiwa na viongozi wa juu kuliko wengine.


“Wapo humu wengine wanajiita wagombea wa katibu Mkuu ,wapo wanaojiita wagombea wa Makamu Mwenyekiti ,wengine wanajiita wagombea wa Mwenyekiti na wapo wanaojiita wagomeba wa wajumbe wa kamati kuu,sisi tulishapitisha majina,na  kama tumepitisha kwenye mkoa majina matatu ,moja ,mawili au manne na kuendelea maana yake hao ndiyo wagombea wa chama,"amesema.

Share:

POLISI SHINYANGA WAKAMATA SILAHA ZA KIVITA, VITU KIBAO ....TAZAMA HAPA, NJOO POLISI UTAMBUE MALI YAKO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha silaha walizokamata zinazodaiwa kutumika kutendea uhalifu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata Bunduki za Kivita AK47 mbili, za kiraia 27(S\gun 9, Riffle 5 pamoja na Gobole 15 zilizokuwa zinatumika kutendea uhalifu. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Novemba 21,2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema silaha hizo zimekamatwa kufuatia
misako na operesheni zilizofanywa na Jeshi la Polisi katika kipindi cha miezi mitatu (3) kuanzia mwezi Septemba 2022 hadi mwezi Novemba 2022.

"Mbali na kukamata silaha hizo pia tumefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Heroine kidonge kimoja naa kete 10kg, bangi 55kg, mirungi 10kg, mitambo miwili ya kutengenezea pombe haramu ya gongo, Tv tatu, mitungi ya gesi 5, majiko ya gesi 4, computer 3, Subwoofer 6, monitor 3, Darubini 3, king'amuzi kimoja, magodoro 3 na bidhaa mbalimbali za madukani",amesema Kamanda Magomi.

"Watuhumiwa mbalimbali wanashikiliwa na wengine wamefikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali. Jeshi la Polisi linaendelea kuwaasa wananchi kufuata sheria za nchi wakati wote na kutojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa namna yoyote ile",amesema.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawaomba wananchi kufika katika kituo kikubwa cha Polisi Shinyanga mjini kwa ajili ya kuzitambua mali zao mbalimbali kuanzia Novemba 23,2022 hadi Novemba 30,2022.

Hayo ameyasema leo kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi wakata akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema tayari watuhumiwa wameshikiliwa na wengine kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha silaha walizokamata zinazodaiwa kutumika kutendea uhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha pikipiki walizokamata 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi  akionesha pikipiki na baiskeli walizokamata 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha Darubini walizokamata 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha bangi walizokamata 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha king'amuzi walichokamata
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali mbalimbali walizokamata
Vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
Pikipiki zilizokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
Silaha zilizokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
Vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
Vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
Share:

MAAFISA WA POLISI, DAWATI LA JINSIA SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO KUPINGA UKATILI WA JINSIA.. RPC MAGOMI ATAKA WASISULUHISHE KESI


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limetoa mafunzo ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la polisi na askari polisi wa Dawati la Jinsia na Watoto ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).

Akifungua mafunzo kazini kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto leo Jumatatu Novemba 21,2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amewataka kuzingatia maadili ya kazi yao na kuchukua hatua za haraka wakati wakiwahudumia Waathirika/Madhura wa matukio ya ukatili wa kijinsia.


“Ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ni lazima askari polisi wawe na maadili na kuepuka vitendo vya rushwa na kusuluhisha kesi za ukatili ili wale waliofanya makosa waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria”, amesema Kamanda Magomi.

“Askari polisi tunapopata kesi za ukatili wa kijinsia ni lazima tusimame katika haki, tutumie lugha nzuri kwa madhura wa ukatili wa kijinsia, tusiwe na mahusiano na wahalifu, tusisuluhishe kesi, tuzipokee, tuzipeleleze na kutenda haki. Wapelelezi fanyeni kazi kwa weledi. Wakuu wa vituo vya polisi msikae na kesi, msisuluhishe na zipelekeni hizo kesi za ukatili wa kijinsia kwenye dawati la jinsia na watoto”,amesema Kamanda Magomi.

Katika hatua nyingine Kamanda Magomi amesema watapita kwenye migodi ya madini ambako kuna taarifa za kuwepo matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo biashara ya ngono ambayo hadi watoto wanashiriki.


“Tumepata taarifa kuhusu kuwepo kwa matukio ya ukatili kwenye migodi midogo. Tukiwa tunaelekea kwenye Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huko migodini tutakwenda. Polisi tutafika kwa ajili ya kutoa elimu na kuwakamata wanaofanya ukatili wa kijinsia migodini”,amesema Kamanda Magomi.


Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo maafisa wa jeshi la polisi na Watendaji wa dawati la jinsia namna ya kushughulikia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kupinga ukatili wa kijinsia.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto leo Jumatatu Novemba 21,2022 katika Bwalo la Polisi Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto.
Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere akizungumza kwenye mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto.

Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto wakiwa kwenye mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto wakiwa kwenye mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto wakiwa kwenye mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Share:

Sunday, 20 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 21,2022














Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger