Sunday, 20 November 2022

MAKATIBU 146 WA AMCOS SHINYANGA WAHITIMU MAFUNZO YA UANDISHI WA VITABU VYA HESABU KWA VITENDO

Mratibu wa Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Justin Mogendi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya uandishi wa vitabu vya hesabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya Makatibu 146 wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya uandishi wa vitabu vya hesabu kwa vitendo ili kuboresha uandishi wa vitabu vya hesabu kwenye AMCOS zao.

Mafunzo hayo yamefanyika Ijumaa Novemba 18,2022 hadi Jumapili Novemba 20,2022 Mjini Shinyanga na Kahama Mjini yakishirikisha watendaji hao kutoka kwenye vyama vya msingi vya pamba 174.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Jumapili Novemba 20,2022, Mratibu wa Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Justin Mogendi amesema yatasaidia kuondoa Hati chafu kwenye vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS).

“Tunatarajia mafunzo haya yataboresha uandishi wa vitabu vya hesabu kwenye AMCOS ili kuondoa hati chafu, nendeni mkatumie ujuzi mliopewa kwenye mafunzo haya kuboresha utendaji katika AMCOS”,amesema Mogendi.

Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace amesema mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo watendaji wa Vyama vya Msingi vya Pamba katika shughuli zao za kila siku hivyo ana imani utendaji kazi utaboreshwa kwenye AMCOS.

Nao washiriki wa mafunzo hayo akiwemo, Regina Kulwa na Mabula Manyesha wamesema hawakuwa wanajua namna ya kuandika vitabu vya hesabu lakini sasa wamepata ujuzi hivyo watakwenda kuandaa taarifa vizuri kwenye AMCOS zao.

Mratibu wa Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Justin Mogendi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya uandishi wa vitabu vya hesabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga
Mratibu wa Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Justin Mogendi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya uandishi wa vitabu vya hesabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga
Mratibu wa Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Justin Mogendi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya uandishi wa vitabu vya hesabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya uandishi wa vitabu vya hesabu kwa vitendo kwa Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba Mkoa wa Shinyanga

 Makatibu wa Vyama vya Msingi vya Pamba wakiwa ukumbini

Mratibu wa Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Justin Mogendi (kushoto) akimkabidhi cheti katibu wa AMCOS

Katibu wa AMCOS akishikana mkono na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniphace wakati Mratibu wa Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Justin Mogendi akikabidhi vyeti kwa washiriki wa mafunzo.

Picha na Kadama Malunde 1 blog
Share:

JINSI TGNP ILIVYOJIPANGA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Share:

DK.BASHIRU AKALIA KUTI KAVU KUTOKANA NA KAULI YAKE DHIDI YA SERIKALI

KATIBU Mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 19,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kumtaka aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kujitathini na kuomba radhi wananchi na Viongozi kwa ujumla kutokana na video yake aliyoitoa Mtandaoni. 

.................................. 

Na Alex Sonna-DODOMA KATIBU Mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi,amemtaka aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kujitathini na kuomba radhi wananchi na Viongozi kwa ujumla kutokana na video yake aliyoitoa Mtandaoni. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 19,2022 jijini Dodoma Kihongosi amesema kuwa maneno aliyotumia si rafiki, si ya kiungwana, yamejaa ukakasi na yamelenga kuchonganisha Serikali na wananchi hasa wakulima. 

Dk.Bashiru alitoa maneno ya kuchinganisha Serikali na wananchi wakati akihutumia mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mjini Morogoro kwamba viongozi hawapaswi kusifiwa kuwa ‘anaupiga mwingi’ wanapotekeleza majukumu 

“Ninamtaka Dkt.Bashiru ajitathimini na kuwaomba radhi watanzania na Serikali kwa ujumla kutokana na kauli yake chonganishi ambayo imeonekana sio nzuri ikizingatiwa yeye alishawahi kuwa kiongozi na alikuwa akiipongeza Serikali Kwa mazuri inayoyafanya " amesema Kihongosi 

Amesema kuwa wao kama UVCCM hawakubaliani na jambo hilo na serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa ambayo imekwenda kuacha alama katika eneo la wakulima, katika suala hilo tunaweza kutizama kipindi hicho bei ya mbolea ilipanda bei sana na ongezeko lile ilipelekea Rais Samia Suluhu Hassan kutoa ruzuku ya Sh.Bilioni 150 ili kupunguza bei ambayo ilikuwa Sh.130,000. 

Kihongosi amesema kuwa serikali imeweka utaratibu na wakulima wananunua kwa bei nafuu jambo ambalo limegusa maisha yao na uchumi wa nchi. 

“Sasa anapotokea kiongozi ambaye alikuwa na dhamana kubwa anatoa maneno yenye ukakasi kwamba viongozi hawapaswi kupongezwa bali wanapaswa kutolewa matamko ya kuwashinikiza hii sio sawa, nitoe rai kwa viongozi wa tabia hii sio njema.”amesisitiza 

Aidha ameeleza kuwa Dk. Bashiru ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo na anajua kila kilichofanyika kwenye sekta hiyo na namna bajeti ilivyoongezeka katika mwaka huu wa fedha lakini anapofikia kutoa kauli hiyo ni jambo la kushangaza.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 20,2022

Share:

Saturday, 19 November 2022

MANISPAA YA SHINYANGA YASHINDA TUZO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA KUTOKA WIZARA YA AFYA

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imekuwa mshindi wa kwanza mashindano ya Tuzo ya Taifa ya Afya na Usafi wa Mazingira mwaka 2022, kundi la Halmashauri za Manispaa Tanzania Bara kutoka Wizara ya Afya.

Tuzo hizo zimetolewa leo Novemba 19, 2022 Jijini Dodoma.
Share:

MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MZEE ZAIDI AFARIKI DUNIA

Priscilla Sitienei amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.

MWANAFUNZI mkubwa zaidi wa elimu ya msingi nchini Kenya, Priscilla Sitienei amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.

Sitienei alikuwa maarufu kwa jina la Gogo ambalo kwa lugha ya asili ya kabila la Kalenjin linamaanisha ‘bibi’.

Mjukuu wa Sitienei, Sammy Chepsiror amelieleza gazeti la The Standard la nchini humo kuwa ‘Gogo’ amefariki dunia akiwa katika hali ya utulivu mbele ya baadhi ya wanafamilia.

Hadithi yake ya kujiunga na elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka 94 iliwavutia watengeneza filamu wa Ufaransa waliotengeneza filamu ya Gogo, ambayo ilimpa fursa “Gogo” kukutana na mke wa rais wa Ufaransa, Brigette Macron.Priscilla Sitienei akiwa na wanafunzi wenzake enzi za uhai wake

Mmoja wa waandishi wa filamu hiyo, Patrick Pessis ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huo akiandika katika ukurasa wa Twitter “ujumbe kuhusu elimu kwa wasichana unaendelea kubaki”.

Gogo Sitienei alijiunga na shule ya watoto ya Vision Preparatory School akijiunga na darasa la wanafunzi ambao ni sawa na vilembwe wake alipoamua kurejea shule akiwa na miaka 90 baada ya kufanya kazi ya ukunga wa jadi kwa zaidi ya miongo miwili.

Sitienei hakufanikiwa kujiunga na shule alipokuwa mdogo lakini serikali ya Kenya ilipoamua kuweka unafuu wa gharama za elimu ya msingi mwaka 2003 ilimhamasisha Gogo na wazee wengine kurejea darasani.

Mwaka 2015 Gogo aliiambia BBC kuwa analenga kuwahamasisha watu wazima kurejea shule “Wananiambia wao ni wakubwa [na hawawezi kurudi shuleni kusoma]” nitawajibu, “Mimi ni mzee [zaidi yao] na ninasoma darasani hivyo ni lazima warudi kusoma”. Alinukuliwa na BBC.
Share:

Friday, 18 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 19,2022

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger