Tuesday, 1 November 2022

BEI YA MAFUTA YAENDELEA KUSHUKA ZAIDI TANZANIA...TAZAMA BEI MPYA HAPA


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini, bezi hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Novemba 02, 2022 saa 6:01 usiku.






Share:

WFT-TRUST WAENDESHA KIKAO CHA TATHIMINI MTAKUWWA AWAMU YA KWANZA, UKATILI WAPUNGUA SHINYANGA


Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MFUKO wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) umefanya kikao na mashirika ambayo wameyapatia Ruzuku ya kutekeleza mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, wanabadiliko ngazi ya jamii, pamoja na viongozi kutoka Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi Maluum, kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mtakuwwa awamu ya kwanza.

Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 1, 2022 katika ukumbi wa mikutano Karena Hotel.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia, amesema wameendesha kikao hicho na mashirika ambayo huyapatia Ruzuku, wanabadiliko ngazi ya jamii pamoja na viongozi kutoka Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi Maalumu, kwa ajili ya kufanya tathimini ya mpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) awamu ya kwanza ambao umeishia june mwaka huu.

“Mpango Mkakati wa kitaifa wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ulianza mwaka 2017,na umeisha June mwaka huu (2022), hivyo ikiwa sisi ni sehemu ya kutekeleza mpango huu tumefanya kikao hiki kufanya tathimini ya utekelezaji wake na kutoa mapendekezo ya mpango mwingine ujao, kutokana na uzoefu na utafiti tuliofanya” amesema Mbia.

“Katika Mkoa wa Shinyanga tulianza kutoa Ruzuku kwa Mashirika ambayo yanajihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto mwaka 2020, ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na shughuli hizi zilikuwa zikitekelezwa katika kata 18 halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,”ameongeza.

Naye Mkurugenzi mwenza wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) Rose Marandu, akizungumza kwenye kikao hicho kwa njia ya mtandao (zoom), amesema wamekuwa wakitoa Ruzuku kwa mashirika hayo kutokana na Mkoa wa Shinyanga kuwa na kiwango kikubwa cha matukio ya ukatili wa wanawake na watoto.

Amesema katika utoaji wa Ruzuku hizo, wameshaanza kuona mafanikio makubwa, ambapo vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimeanza kupungua, huku akitoa mapendezo kwa Serikali kuondoa Sera au Sheria ambazo zinakinzana katika utetezi wa haki za wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku, ameipongeza WFT-Trust kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya kwa kuyafadhili mashirika na kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kutoa elimu juu ya madhara ya vitendo vya ukatili.

Pia ameupongeza Mkoa wa Shinyanga kuwa Mkoa wa kwanza katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ikiwamo kuzindua mpango wake mkakati wa kutokomeza ukatili wa wanawake na watoto na kuwa mkoa wa mfano.

Aidha, amesema kutokana kazi kubwa ambayo wameifanya Mkoa huo waShinyanga kwa kuweka juhudi kubwa katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ndiyo sababu kubwa ambayo imewafanya kufanya ziara kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mtakuwwa.

Mratibu wa Mtakuwwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary, halmashauri ambayo ilikuwa ikitekelezewa mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa mashirika ambayo yalipewa Ruzuku na WFT-Trust, amesema ukatili wilayani humo umepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka ya nyuma.

Amesema pia kumekuwepo na utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa jamii, pamoja na watoto kutoa taarifa kupitia mabaraza ya watoto na wamefanikiwa kuzui ndoa za utotoni 14, pamoja na kumfunga Jela miaka 30 Mwalimu wa Skauti aliyekuwa akilawiti watoto.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza.Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza.


Mkurugenzi wa idara sera na mipango kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Sayi Katwale akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Sebastian Kitiku akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Mtakuwwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Joel Mangi akizungumza kwenye kikao hicho.

Pastory Mfoi akizungumza kwenye kikao hicho kwa niaba ya Mtaribu wa Mtakuwwa Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa Mtakuwwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa Shirika la ICS mkoani Shinyanga Kudely Sokoine akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

WFT-Trust kutoka Makao makuu Dar es Salaam wakishiriki kikao kwa njia ya mtandao (zoom).
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa kikao.


Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa kikao.

Kwa mawasiliano zaidi kwa WFT Trust, Piga simu +255 753 912 130, tuma barua pepe kwa info@wftrust.or.tz au tembelea tovuti www.wft.or.tz

Share:

TUMIA NJIA HII WATOTO WAKO WAFAULU MITIHANI SHULENI

Share:

Live : KIKAO CHA PILI CHA MKUTANO WA KWANZA WA KAWAIDA WA BUNGE LA SITA LA AFRIKA 'PAP'


Kikao cha Pili cha Mkutano wa Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika (Pan African Parliament - PAP) kinaendelea muda huu leo Jumanne Novemba 1,2022 kikiongozwa na Kauli mbiu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2022 "Kujenga Uthabiti  katika Lishe katika Bara la Afrika : Kuharakisha mtaji wa watu, maendeleo ya kijamii na kiuchumi". Fuatilia hapa chini
Share:

Monday, 31 October 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 1,2022













Share:

SERIKALI KUFANYA MABORESHO MAKUBWA KATIKA MIFUMO YA UNUNUZI.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Hamad Hassan Chande (Mb) akiwataka wataalamu wa maboresho makubwa ya Mfumo wa Ununuzi Serikalini, kuhakikisha wanamaliza kazi kwa wakati, alipofanya ziara ya kukagua mfumo huo, mkoani Iringa.

Mkurugenzi wa Mifumo na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Michael Moshiro, akieleza changamoto katika Mfumo wa sasa Ununuzi wa Umma (TANePS), wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Hamad Hassan Chande (Mb) (kushoto) ya kukagua mfumo wa ununuzi wa umma, mkoani Iringa.
Baadhi ya wataalamu wa uboreshaji mkubwa wa Mfumo wa Ununuzi wa Umma, wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Hamad Hassan Chande (Mb) (hayupo pichani), alipofanya ziara ya kukagua mfumo huo, mkoani Iringa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa nne kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Bw. Eliakimu Maswi (wan ne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa maboresho ya Mfumo wa Ununuzi wa TANePS, mkoani Iringa.

(Picha na Kitengo cha Uhusiano kwa Umma-PPRA)



*******************

Na Zawadi Msalla-Iringa

Naibu Waziri, wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande ameipongeza PPRA kwa juhudi wanazoendelea nazo za maboresho makubwa katika mfumo wa ununuzi wa kielektroniki. Maboresho hayo yaliyolenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Sekta ya Ununuzi nchini yanafanyika kwa kutumia wataalam wa ndani ya nchi wa ujenzi wa mifumo ya TEHAMA . Akizungumza baada ya kutembelea kambi ya wataalam hao mkoani Iringa katika Chuo kishiriki cha Elimu Mkwawa Mhe. Chande alisema ni imani yake kuwa maboresho hayo yatasaidia taasisi nunuzi kuweza kufanya michakato ya ununuzi kwa uwazi na ubora unaotakiwa.

Mhe. Chande aliongeza kuwa zipo faida nyingi ambazo Serikali itazipata baada ya maboresho haya kukamilika ikiwemo kuondoa changamoto ambazo zipo katika mfumo wa sasa wa TANePS. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kuwa mfumo huu si rafiki kwa watumiaji. Hivyo basi katika kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa wataalamu wapo kazini kuona mfumo huu uweze kufanya kazi mpaka kwa kutumia vishikwambi, alieleza.

“Kama watu hawafundishwi jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii lakini wanaweza kutumia, hata mfumo huu itakuwa rahisi kutumia kwa kila mtu” alisema Mhe. Naibu Waziri

Akiongea na wataalam wa mifumo alisema ni lazima wafahamu nia ya Serikali ya kuamua kufanya maboresho hayo kuwa ni kuhakikisha taasisi nunuzi zinatoka katika mazoea ya kufanya michakato ya ununuzi nje ya mfumo kwani ununuzi wa nje ya mfumo unaongeza uwezekano wa rushwa na upotevu wa thamani ya fedha.

“Kumekuwa na usiri mkubwa katika michakato ya ununuzi, hali inayofanya mtu uwaze huu usiri una nini katikati yake, ununuzi unatakiwa ufanyike kwa uwazi na haki, ni nyie mliopo hapa mnayofanya haya maboresho mnaweza kututengenezea mfumo unao akisi uwazi katika ununuzi na utakaosaidia manunuzi yoyote yanayofanyika kuwa ya haki” alisema.

Mfumo huu kama utatumiwa ipasavyo uchumi wa nchi utaenda kuimarika, kwani asilimia 70 ya matumizi yote ya bajeti ya nchi umejikita katika ununuzi. Maboresho haya yataweza kuleta upatikanaji wa thamani ya fedha kwani kama mchakato wote utafanyika ndani ya mfumo utaondoa mianya ya rushwa katika ununuzi.

Hatahivyo alimtaka mtendaji Mkuu wa PPRA, Eliakumu Maswi kujipanga na kuangalia jinsi ya kuweza kuutunza mfumo huo ulioboreshwa ilikuhakikisha unakuwa na unatenda kazi unaoimarika kila siku. Alisema itasikitisha kuona wataalamu wametumia muda na nguvu zao kwa kiwango cha juu na baada ya hapo mfumo ushindwe kutunzwa.

Naye Mbunge wa jimbola Iringa mjini , Mhe Jesca Msambatavangu aliipongeza Serikali kwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango na kwa kushirikiana na PPRA umeufanya, alisema si jambo rahisi kuingia katika maboresho makubwa kama yanavyoendelea sasa bila kuwa na msaada kutoka kwa wataalam wa nje ya nchi.

Alisema Faraja yake ni kuwa wataalamu waliofanya maboresho haya ni wazawa ni imani yake kuwa mfumo utakuwa umeangalia hali halisi ya mtanzania na soko la ndani. Alisema mafanikio ya maboresho haya yametokana na wataalam wazawa kujiamini kuwa inawezekana bila wataalam kutoka nje ya nchi.

Aliwakumbusha wataalam hao kuwa uzalendo waliouonesha wakati wakiendelea na maboresho ya mfumo utakumbukwa kwa vizazi vyao vyote. Hata hivyo aliwataka uzalendo waliouonesha usiishie wakati wa huu, hata baada ya kumaliza kazi hii ni vema wakumbuke bado Taifa linawahitaji. Moyo wa uzalendo uwe mbele zaidi katika kulitoa Taifa katika umaskini na kulifanya liwe ni moja ya taifa linalotegemewa.

Uamuzi wa maboresho ya Mfumo wa Ununuzi nchini ulitokana na agizo la Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya mwaka 2022/23 bungeni. Maboresho hayo yaliyoanza mwezi julai 2022 yanatarajia kufanyika kwa awamu sita ambapo mpaka sasa awamu ya kwanza tayari imekwisha kamilika na inatarajiwa majaribio yake yaanze mwezi desemba 2022.






Share:

NIMEMRUDISHA MPENZI WANGU ALIYECHEPUKA NA BOSSI WAKE!

Share:

RAIS SAMIA ATANGAZA MATOKEO YA SENSA..IDADI YA WATANZANIA NI 61, 741,120

Idadi ya Watanzania ni 61,741,120

Idadi ya Watanzania ni 61,741,120


Hayo yamebainishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, muda mfupi uliopita wakati akitangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iliyofanyika kuanzia Agosti 23 mwaka huu.

Amesema watu 59,851,357 wapo Tanzanzia Bara na watu 1,889,773 wapo Tanzania Zanzibar.

Kuhusu idadi hiyo wanawake wapo 31,687,990 sawa na asilimia 51 ya watu wote na wanaume ni 30,530,130 sawa na asilimia 49 ya watu.

Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini, kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu.

Sensa hufanyika kila baada ya miaka 10, ambapo sensa ya mwaka 2022 ni ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012. Matokeo ya sensa ya mwaka 2012 yalionesha kuwa Tanzania ilikuwa na watu 44,929,002 wakiwamo 43,625,434 Tanzania Bara na 1,303,568 Zanzibari.
 
Chanzo habari leo
 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger