Friday, 2 September 2022
WAWEKEZAJI ARUSHA WAMWAGIA SIFA RAIS SAMIA UJENZI WA BARABARA ZA TARURA
Thursday, 1 September 2022
WATOA HUDUMA ZA AFYA, WANACHAMA WACHANGIA KUHATARISHA UHAI WA MFUKO WA NHIF
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
Kutokana na hayo imesema ipo katika hatua za mwisho kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ambayo itaweka mazingira kwa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuwezesha dhana ya kuchangiana gharama za matibabu hali itakayo saidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Hayo yameelezwa leo Jijini hapa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu hali ya mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) na kueleza kuwa Serikali haitakubali kuona Mfuko huo unatetereka hivyo kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wote kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya.
Amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya wataaluma 65 wamefikishwa katika mabaraza yao kutokana na kukiuka taratibu na miongozo ya taaluma za afya hivyo kuitaka NHIF kuimarisha mikakati yake ya kupambana na vitendo vya udanganyifu pamoja na kuimarisha matumizi ya Mifumo ya TEHAMA.
Hata hivyo Waziri huyo amewatoa hofu wanachama wa NHIF na wananchi kwa ujumla kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuuimarisha Mfuko huo ili kuwa endelevu na kuwanufaisha wananchi walio wengi zaidi.
Pamoja na kuimarisha huduma za afya,Waziri huyo amekiri kuwa bado kuna changamoto ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya wananchi wenye magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo gharama zake ni kubwa hali inayohatarisha uhai na uendelevu wa Mfuko wa NHIF.
Vilevile, changamoto nyingine iliyopo ni uwepo wa kundi kubwa la wananchi wanaojiunga na NHIF kwa hiari ambao, takribani asilimia 99 ni wagonjwa hatua inayotokana na kutokuwepo kwa Sheria ya ulazima kwa wananchi kujiunga na Bima ya Afya na kuondokana na kuelemewa kwa mfuko huo kunakotokana na gharama za matibabu kuongezeka kwa idadi ya wanufaika wenye magonjwa yasiyoambukizwa na gharama zake, hali inayoweza kuathiri uhai na uendelevu wa Mfuko.
"Kama mnakumbuka tarehe 29/08/2022 wakati nikifungua Mkutano wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu jijini Dar es Salaam, niliweka msisitizo wa kuweka nguvu na jitihada katika kuzuia magonjwa badala ya kusubiri kutibu;
Katika muktadha huo nilitoa angalizo kuwa hivi sasa nchini kwetu tunashudia ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo matibabu yake ni gharama kubwa na hivyo kama tutachelewa kuchukua hatua stahiki katika kudhibiti magonjwa hayo, basi kuna hatari pia kwa Mfuko wetu wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuelemewa na gharama za matibabu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanufaika wenye magonjwa yasiyoambukizwa na gharama zake, hali inayoweza kuathiri uhai na uendelevu wa Mfuko,"Amesema.
Kulingana na takwimu zilizopo, amesema gharama za magonjwa yasiyo ya kuambukizwa zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 35.65 mwaka 2016/17 hadi shilingi bilioni 99.09 mwaka 2021/22 na kwamba Gharama za kuhudumia wagonjwa wa saratani wanaopata tiba za mionzi na chemotherapia (chemotherapy services), kupitia Mfuko ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 9 mwaka 2015/16 hadi kufikia shilingi bilioni 22.5 mwaka 2021/22,"amesema
Kwa upande wa huduma za matibabu ya figo kwa wanachama wanaopata huduma ya kuchuja damu (hemodialysis services) Waziri Ummy amesema gharama ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 9.5 mwaka 2015/16 kufikia shilingi bilioni 35.44 mwaka 2021/22 huku idadi ya wagonjwa wa figo imeongezeka kutoka 280 mwaka 2014/15 hadi kufikia 2,099 mwaka 2021/22.
"Gharama za matibabu ya moyo kwa wanachama wa Mfuko wanaopata matibabu ya upasuaji wa moyo (minimal and invasive cardiac procedures), ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 0.5 mwaka 2015/16 hadi kufikia shilingi bilioni 4.33 mwaka 2021/22,gharama za vipimo vya CT scan na MRI ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 5.43 mwaka 2015/16 hadi kufikia shilingi bilioni 10.87 mwaka 2021/22,"amefafanua
Sambamba na hayo ameeleza kuwa ni wazi hali ya ustahimilivu na uendelevu wa Mfuko ipo mashakani endapo hatua stahiki hazitachukuliwa ambazo ni pamoja na kuimarisha afua za kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika hatua za awali ikiwemo kuyatambua mapema kabla ya kuwa na athari kubwa,kuongeza idadi ya wanachama na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.
Ametaja hatua nyingine ni kudhibiti matumizi ya huduma yasiyo na tija,kupunguza gharama za matibabu nchini,kuwa na Mfumo endelevu wa kuhakikisha Mfuko unakuwa na fedha wakati wote kutoka katika vyanzo vyake vya mapato na katika hatua hii tunaishukuru serikali kwa kuwasilisha michango ya watumishi kwa wakati.
"Niwatoe wasiwasi wadau wa NHIF wakiwemo wanachama, watoa huduma pamoja na watanzania wote kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki kuhakikisha kuwa Mfuko huu unakuwa imara, endelevu na stahimilivu kwani kwa sasa, ni moja kati ya mfumo unaotumika katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa nchini,"amesema
Amesema mfuko wa NHIF ndio umekuwa tegemeo la watanzania wengi hususani wa kipato cha chini pia umekuwa tegemeo la vituo vya kutoa huduma za afya nchini pamoja na kuwa na wanachama asilimia nane (8) tu ya Watanzania wote, vituo vingi vya kutolea huduma vinategemea mapato kutoka katika Mfuko kwa zaidi ya asilimia 70.
"Katika kuhakikisha kuwa maamuzi yote yahusuyo Mfuko huu yanazingatia taratibu na miongozo ya kuendesha chombo hiki, tumefanya tathmini ya uhai na uendelevu wa mfuko kwa mujibu wa sheria na, hivyo tunatambua ni yapi yanapaswa kufanyika ili kuhakikisha mfuko wetu unakuwa endelevu na imara zaidi na matokeo ya awali yanaonesha uendelevu wa Mfuko huu unategemea sana ongezeko la wanachama watakaoandikishwa katika Mfuko huu,"amesema.
Akizungumza uzoefu kutoka katika nchi nyingine ,Waziri huyo alisema unaonesha kuwa, kadri idadi ya wanachama inavyokuwa kubwa katika Mifuko hii ya bima za afya za umma kama NHIF, ndipo uwezo wake katika kugharamia matibabu unaongezeka na hivyo kuwa stahimilivu na endelevu kwa muda mrefu.
MWANZA HOTEL NI SALAMA... HAIJAUNGUA
MMILIKI wa New Mwanza Hotel Mwita Gachuma amekanusha uvumi ulikuwa umesambazwa wa kuungua kwa eneo hilo lililoko katika mwa Jiji kwa kusema ni sehemu ya eneo hilo ndiyo ilipata tatizo hilo.
Amesema hayo leo jijini Mwanza kuwa ni sehemu ya eneo la nyuma ya hotel hiyo iliyokuwa inatumiwa kama ukumbi wa harusi na kasino ambayo yameungua kwa moto unaohisiwa kutokana na hitilafu ya umeme.
Moto huo ulitokea usiku saa 1.30 siku ya tarehe 31 mwezi wa Nane kwa kile kinachohisiwa kuwa hitilafu ya umeme.
Gachuma ametoa shukurani kwa serikali ya mkoa huo, watendaji wa idara mbalimbali na wananchi kwa kuwezesha kuzimwa kwa moto huo kabla ya kuleta madhara makubwa kwa nyumba zilizopo karibu na sehemu hiyo.
Alisema madhara yaliyotokana na moto huo ni makubwa na watalaamu wa vyombo mbalimbali wamefika kufanya tathimini ya hasra hiyo kwani eneo hilo limeharibiwa vibaya na hivyo kuhitajika ujenzi upya.
"Watu wa Mamlaka Bima wamefika kwa ajili ya kufanya tathimini kuweza kujua ni kiasi gani cha hasara kimepatikana kutokana na moto huo hivyo siwezi kusema kiwango halisi cha hasara kilichopatikana" alisema Gachuma.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima aliyefika tena kufatilia athari iliyotokana na moto huo alisema kuwa anashukuru vyombo vyote vya ulizi kwa kazi yao nzuri waliyofanya usiku wa tarehe 31 Agosti ilipoungua jengo hilo.
Alisema kutokana na jengo hilo kuwa katikati mwa majengo mengine madhara yake yangeweza kuwa makubwa zaidi endapo moto huo usingezibitiwa haraka.
'Nilikuwepo jana usiku kwenye tukio la moto huo hata hivyo nimeona nipite tena leo asubuhi kuona hali hiyo ambayo ingeweza kuleta madhara kwa moto huo kusambaa kwenye nyumba zingine' alisema Malima
Malima alitoa wito kwa watu wote kujenga majengo yao kwa kuweka tahadhari ya vitu vinavyozuia moto katika maeneo yao ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
KINANA ATUA KIGOMA KWA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu Abdulrahman Omari Kinana amewasili leo Alhamisi tarehe 01 Septemba, 2022 mkoani Kigoma kwa ziara ya siku moja mkoani humo ya kukagua uhai wa chama, utekelezaji wa ilani pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Kinana amewasili uwanja wa ndege wa Kigoma na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Ndg Amandus Dismas Nzamba, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Ndg Thobias Andengenye, wanachama na viongozi wa chama na serikali.
Kinana ameanza leo ziara ya siku moja mkoani Kigoma ambapo ataendelea katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza. Katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.
#CCMImara
#KaziIendelee