Wednesday, 17 August 2022

BARRICK NORTH MARA YAFANIKISHA UKARABATI WA BARABARA KOROFI TARIME

Kampuni ya Barrick, kupitia Mgodi wake wa North Mara, imeanza kutekeleza kwa vitendo ahadi iliyotolewa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Mark Bristow la kurekebisha kipande cha barabara korofi katika eneo la vijiji vya Nyamongo na Kewanja wilayani Tarime mkoani Mara, iliyokuwa imeharibika sana na kuleta usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo wanaotumia barabara hiyo.

Viongozi wa eneo hilo walitoa ombi la kusaidiwa kutengenezewa kipande cha barabara hiyo hivi karibuni wakati walipokutana na Bw. Bristow, alipokuwa nchini hivi karibuni.

Kipande hicho kinachokarabatiwa na Barrick, kina umbali wa kilometa 3.6 kuanzia katika kijji cha Kewanja kwenye kitongoji cha Kwinogo, kuanzia makutano ya barabara ya kwenda Serengeti, hadi kwenye makutano ya barabara ya kwenda Tarime.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiongelea hatua hiyo jana baada ya kushuhudia mkandarasi kampuni ya ujenzi ya Stanley, ameanza kazi ya kuchonga na kumwaga vifusi, walisema kuwa barabara hiyo iliharibika na kuwasababishia usumbufu mkubwa na hasara na walishukuru uongozi wa Barrick kwa ukarabati wa barabara hiyo.

Akiongea kwa niaba ya Wananchi wenzake, Perusi Masiaga Chacha ,mkazi wa eneo hilo alisema ubovu mkubwa wa barabara hiyo ulisababisha kuishi kwa hofu kuitumia hasa watoto wao kuvuka wakati wa kwenda shule, kusababisha kusafiri mwendo mfupi kwa muda mrefu pia kusababisha uharibifu mkubwa wa vifaa vya usafirishaji hasa pikipiki na magari.

Aliishukuru kampuni ya Barrick, kwa kuamua kuwaondolea kero hii ya barabara mbovu ‘’Tunayo furaha kuona barabara hii inatengenezwa kwa kuwa mbali na kuwarahisishia maisha watumiaji wake itasaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo haya yaliyokuwa yanafifishwa na ubovu wa miundo mbinu.Tunaishukuru Barrick, kwa kudhihirisha kuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika eneo hili.

Naye Samwel Wambura, akiongea kwa niaba ya madereva wa vyombo vya moto wanaotumia barabara hiyo alisema kuwa kwa muda mrefu imewasababishia hasara kubwa ya kuharibika kwa vyombo vyao na alishukuru Barrick kwa kuona umuhimu wa kuifanyia ukarabati ili iweze kupitika vizuri.


Kwa upande wake, Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Mgodi wa North Mara, Gilbert Mworia, alisema barabara hiyo inakarabatiwa kutokana na ombi la viongozi wa eneo hilo pia kutokana na ubovu wake uliosababisha utumiaji wa barabara za mgodini kuwa mkubwa hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya Wananchi kutokana na barabara nyingi za Mgodini kutumiwa na mitambo mikubwa ya shughuli za uchimbaji.
Kazi ya ukarabati wa barabara korofi katika eneo la vijiji vya Nyamongo na Kewanja,wilayani Tarime ikiendelea

Share:

Tuesday, 16 August 2022

AJALI YAUA 19 , KUJERUHI 10 MBEYA


Ni kwamba mnamo tarehe 16.08.2022 majira ya saa 02:00 asubuhi huko maeneo ya Inyala Pipeline, Kijiji cha Shamwengo, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya – Njombe, Gari lori lenye namba za usajili T.387 DFJ lenye tela namba T.918 DFE aina ya Dayun likiendeshwa na Dereva MUHSIN GUMBO, Mkazi wa Dar es Salaam mali ya kampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga likitokea Mbeya liligonga kwa nyuma Gari T.966 DUQ aina ya Fuso basi mali ya kampuni ya Super Rojas likitokea Mbeya kuelekea Njombe likiendeshwa na ALEX MGIMBA [51] Mkazi wa Jijini Mbeya na kisha kugonga Gari T.836 DRE Mitsubish Benz iliyokuwa ikiendeshwa na NEDIM PREMJI, Mkazi wa Dar es Salaam na kisha kugonga Gari linguine T.342 CHG/T.989 CGS Scania iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu 19 kati yao wanaume ni 12, wanawake 06 na mtoto 01. Aidha katika ajali hiyo majeruhi ni 10 kati yao wanaume ni 07, wanawake ni 02 na mtoto 01.


Chanzo cha ajali ni Gari kufeli breki kwenye eneo lenye mteremko mkali na kisha kugonga magari mengine. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali ya Igawilo.


Imetolewa na:
Ulrich Matei – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Share:

MTANDAO WA TELEGRAM SALAMA ZAIDI KULIKO WHATSAPP KWENYE UDUKUZI


Na Mwandishi Wetu

Mtandao wa kijamii wa Telegram umeonekana kuwa salama zaidi kuliko mtandao wa WhatsApp ambao umejizolea umaarufu zaidi duniani.


Wataalamu wa masuala ya usalama wa kidijiti na mitandao ya jamii wamesema kuwa utafiti wao umeonesha kuwa mtandao wa Telegram unaweza kuhimili mashambulizi kutoka kwa wadukuzi kuliko mtandao wa WhatsApp.


Nchini Nigeria, moja ya nchi za Afrika zenye watumiaji wengi zaidi wa mitandao ya jamii, wananchi wengi wanahamia kwenye mtandao wa Telegram ili kukwepa kudukuliwa.


Waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakilalamika nchini Nigeria kuwa mawasiliano yao ya WhatsApp yanadukuliwa na kusababisha wanyanyaswe au kukamatwa na polisi.


Vitendo hivyo vya udukuzi vimepelekea wananchi wengi nchini humo waamue kuacha kutumia mtandao wa WhatsApp na kuhamia Telegram, ambayo ni salama zaidi.


Telegram, ambayo inazindua huduma mpya ya "premium" imepata watumiaji wapya zaidi ya milioni 700 kutoka sehemu mbalimbali duniani ndani ya mwaka mmoja tu, huku watumiaji wengi wakihamia mtandao huo baada ya kuvutiwa na umadhubuti wake wa kuzuia udukuaji wa taarifa zao za siri.


Maabara ya wananchi nchini Canada inayojulikana kama the Citizen Lab at the University of Toronto, imebaini kuwa vyombo vya dola nchini Nigeria vimekuwa vikitumia teknolojia ya kijasusi kutoka nchi ya Isreal kudukua taarifa za faragha za wananchi kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.


Wananchi ambao wamekuwa wakidukuliwa na vyombo vya dola kupitia WhatsApp ni pamoja na waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati.

Share:

RAILA ODINGA APINGA MATOKEO YA URAIS KENYA

Kiongozi wa Muungano wa Azimio nchini Kenya Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi uliomtangaza naibu wa rais William Ruto kuwa ndiye rais Mteule.


Raila amesema kwamba hakubaliani na matokeo hayo kwa sababu mwenyekiti wa tume hiyo alikiuka sheria ya tume hiyo kabla ya kumtangaza mshindi


Amesema kwamba makamishna wa tume hiyo hawakukubaliana kuhusu hesabu ya mwisho ya matokeo hayo yaliompatia ushindi William Ruto.


''Takwimu zilizotangazwa na Chebukati ni batili kwa maoni yetu, hakuna mshindi kisheria, aliyetangazwa kihalali wala rais mteule''.


Hata hivyo Raila amewasihi wafuasi wake kujizuia akiongezea kwamba atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.


''Jana, demokrasia yetu changa ilikumbwa na msukosuko mkubwa, kwa sababu hiyo, Kenya inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisheria na kisiasa kutokana na matendo ya Wafula Chebukati''.


''Tunafuatilia njia za kisheria na za amani. Tuna hakika kwamba haki itatendeka. Tunaelewa kuwa ni Bw Chebukati pekee ndiye aliyepata kujumlisha kura za urais. Aliwanyima makamishna wote kupata taarifa hizo'', aliongeza Raila akizungumza na vyombo vya habari jijini Nairobi.
Share:

JAMAA AKATA NYETI ZAKE AKIOTA ANACHINJA MBUZI

Mwanaume mmoja nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 42 anapambania kuokoa maisha yake baada ya kuzikata sehemu zake za siri na kisu ndotoni, baada ya kuota anachinja mbuzi kwa ajili ya kumsaidia mke wake kuandaa chakula cha jioni.


Tukio hilo limetokea Agosti 12, 2022, na kusema kwamba baadaye alikuja kushtuka na kugundua kwamba alikuwa akizikata sehemu zake za siri badala ya mbuzi kama alivyokuwa anaota.

Imeelezwa kwamba mke wa mwanaume huyo hakuwepo nyumbani na ndipo alipopigiwa simu na majirani zake kumuarifu kwamba mume wake amejeruhiwa na ndipo alipowahi kurudi nyumbani na kumkuta amezishikilia sehemu zake za siri na kisha kumpeleka hospitali.
Share:

STENDI MPYA YA HIACE, BAJAJI SOKO KUU MJINI SHINYANGA YAZINDULIWA


 
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (katikati) akikata Utepe kuzindua Stendi ya Hiace, Bajaji na Bodaboda iliyopo Soko kuu Manispaa ya Shinyanga, (kulia) Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema, (kushoto) Diwani wa Chibe John Kisandu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAFANYABIASHARA wa usafirishaji katika Stendi ya Hiace, Bajaji na Bodaboda iliyopo Soko kuu Manispaa ya Shinyanga, wameipongeza Serikali kwa kuifanyia ukarabati Stendi hiyo, na kuwaboreshea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao.


Stendi hiyo imezinduliwa leo Agost 16, 2022, ambapo awali ilikuwa ikikabiliwa na uchakavu wa miundombinu, lakini Serikali ikaifanyia ukarabati kuanzia Juni mwaka huu, na imekamilika Agosti na sasa imeanza kutumika rasmi na imegharimu Sh.milioni 147.

Mmoja wa Wafanyabiashara hao Paschal Mboje, amesema awali Stendi hiyo ilikuwa na vumbi na kipindi cha mvua tope linakuwa jingi na maji kutwama, lakini sasa hivi changamoto hizo hazipo tena na watafanyabiashara zao katika mazingira mazuri.

“Tunaipongeza Serikali kwa kuikarabati Stendi hii, na kutatua Changamoto ambazo tulikuwa tukikabiliana nazo za uchakavu wa miundombinu na tutafanya biashara zetu kwa raha mstarehe,”amesema Mboje.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amewataka wafanyabiashara hao waitunze miundombinu ya Stendi hiyo ili waendelee kufanyabiashara zao katika mazingira rafiki.


Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza mara baada ya kumaliza kuzindua Stendi ya Hiace, Bajaji na Bodaboda iliyopo Soku kuu Manispaa ya Shinyanga.

Mfanyabiashara wa usafirishaji Paschal Makoye akizungumza mara baada ya kumaliza kuzinduliwa Stendi hiyo.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (katikati) akikata Utepe kuzindua Stendi ya Hiace, Bajaji na Bodaboda iliyopo Soko kuu Manispaa ya Shinyanga, (kulia) Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema, (kushoto) Diwani wa Chibe John Kisandu.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (katikati) akikata Utepe kuzindua Stendi ya Hiace, Bajaji na Bodaboda iliyopo Soko kuu Manispaa ya Shinyanga, (kulia) Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema, (kushoto) Diwani wa Chibe John Kisandu.
Madereva wa Bodaboda wakiingia kwenye Stendi hiyo.

Madereva wa Bajaji wakiingia kwenye Stendi hiyo.

Hiace ikiingia ndani ya Stendi hiyo.

Hiace ikiingia ndani ya Stendi hiyo.

Hiace zikiwa ndani ya Stendi.

Bajaji zikiwa ndani ya Stendi.

Share:

BENKI YA EXIM YAADHIMISHA MIAKA 25 KWA KUPONGEZA NA KUTAMBUA JITIHADA ZA WAFANYAKAZI WAKE



Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo iliyofanyika Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Exim, Fredrick Kanga, akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo iliyofanyika Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo (wa tatu kulia) sambamba na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo wakishirikiana na wateja kukata keki ikiwa ni ishara ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (kushoto) akisaidiana kukata keki na Mkuu Uendeshaji wa matawi ya benki hiyo Bw Eugine Massawe wakati wa hafla fupi ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo iliyofanyika Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Bw Massawe ni mmoja wa watumishi wa benki hiyo waliohudumu kwa kipindi cha miaka 25


Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania waliofanya kazi na benki hiyo kwa zaidi ya miaka 20 wakijipongeza wakati wa hafla hiyo.


Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa benki hiyo wakati wa hafla hiyo.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (wa pili kulia) akijipongeza sambamba na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo iliyofanyika Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (kushoto) akimlisha keki Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Exim Bi Zainabu Nungu wakati wa hafla fupi ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo iliyofanyika Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Cheers! “Benki ya Exim Tanzania ilianzishwa mwaka 1997 jijini Dar es Salaam ikiwa ni huduma rafiki zenye ubunifu ikiwa na wafanyakazi 16 tu wanaojituma sambamba na wateja waaminifu kwa huduma za benki. Leo hii, Benki ya Exim imekua na kuwa moja ya benki imara zaidi nchini ikiwa na matawi 30 maeneo mbalimbali nchini Tanzania na zaidi ya wafanyakazi 900 katika mataifa matano’’ - Fredrick Kanga - Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Exim

........................................

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

BENKI ya Exim Tanzania imeadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa hafla fupi iliyolenga kutambua jitihada na mchango wa wafanyakazi wa benki hiyo katika kufanikisha ustawi wa benki hiyo.

Kivutio kikubwa kwenye hiyo iliyofanyika leo Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhiriwa na viongozi waandamizi na wafanyakazi wa benki hiyo ilikuwa ni utambuzi na pongezi za heshima zilizotolewa kwa watumishi waliohudumu katika benki hiyo tangu kuanzishwa kwake miaka 25 iliyopita.

"Benki ya Exim imejitolea kwa dhamira yetu ya dhati kuwaweka wadau wetu muhimu wakiwemo wafanyakazi na wateja mbele," alisema Jaffari Matundu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo.

"Wafanyikazi wetu ndio wanaosimamia dira yetu ya kila siku wakitoa huduma ya kipekee kwa wateja wetu. Tukio hili linatoa fursa kwetu kutambua juhudi zao za pamoja, na kusherehekea mafanikio ambayo yasingewezekana bila wao.’’

Alisema maadhimisho hayo yanahusisa matawi yote ya benki hiyo nchi nzima na itahusisha mpango wa benki hiyo katika kusaidia jamii kwa namna mbalimbali.

Kwa mujibu wa Bw Matundu benki hiyo imejipanga zaidi kuendelea kuwapa wateja wake bidhaa na huduma za kibunifu huku ikijiweka katika nafasi ya ushindani mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

"Ili kuendelea kufikia malengo yetu, miaka ijayo tunahitaji kuwa na uvumbuzi zaidi, teknolojia salama na yenye ufanisi, huduma bora kwa wateja na zaidi ya yote, ushirikiano mkubwa na msaada wa wateja wetu, washirika wa biashara, mamlaka mbalimbali na wadau wengine wote." Alitaja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Exim, Fredrick Kanga, aliwashukuru wafanyakazi hao kwa mchango wao katika ukuaji wa benki hiyo huku akibainisha kuwa uongozi unaheshimu na kutambua umuhimu wa kila mfanyakazi katika kuleta maendeleo ya benki hiyo.

Alisema muda mrefu wa utumishi miongoni mwa baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo unaonyesha kiwango cha uaminifu na kujitolea kwa pande zote mbili yaani wafanyakazi wenyewe pamoja na uongozi wa Benki na hivyo kudhihirisha uaminifu baina ya pande hizo muhimu.

"Tangu mwanzo, tumefungua milango yetu kwa vijana ambao wanataka kuishi ndoto zao na kufuata kazi zinazoakisi ujuzi na shauku yao.’’ Alisema.

Alibainisha kuwa benki hiyo ilianzishwa mwaka 1997 jijini Dar es Salaam ikiwa ni huduma rafiki zenye ubunifu ikiwa na wafanyakazi 16 tu wanaojituma sambamba na wateja waaminifu kwa huduma za benki hiyo.

"Leo hii, Benki ya Exim imekua na kuwa moja ya benki imara zaidi nchini ikiwa na matawi 30 maeneo mbalimbali nchini Tanzania na zaidi ya wafanyakazi 900 katika mataifa matano ambao bado wanaendeleza utamaduni uliotukuka wa kusaidia familia na biashara kuimarika kiuchumi.’’ Aliongeza.

Akiwashuhudia mbele ya wafanyakazi wengine wa benki hiyo, Bw Eugine Massawe, Mkuu Uendeshaji wa matawi ya benki hiyo ambaye ni mmoja wa watumishi wa benki hiyo waliohudumu kwa kipindi cha miaka 25 alisema uhusiano wake na benki hiyo katika kipindi chote ni wa ushirika zaidi.

"Na ninafuraha kuendelea kujitoa niwezavyo kwa ushirikiano huu kwa manufaa ya benki, na pia kwa ajili yangu mwenyewe. Malengo yangu ya kibinafsi na kitaaluma yanawiana na ramani ya ukuaji wa muda mrefu ya benki ya Exim na mazingira mazuri ya kazi yananipa motisha zaidi" alisema
Share:

RAIS SAMIA AMPONGEZA RUTO



Viongozi mbali mbali wa kimataifa wameendelea kutuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Kenya William Ruto kufuatia kutangazwa kwake Jumatatu kama mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 9 Agosti,2022.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema:’’ Ninawapongezaa Wakenya kwa uchaguzi wao mkuu wa amani na kutangazwa kwa Dr William Ruto kama Rais mteule. Tunatazamia kuendelea kufanya kazi na makaka na madada zetu nchini Kenya kuimarisha uhusiano wetu wa karibu. Tuko pamoja’’:


Katika ujumbe wake wa Twitter Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema ”Ningependa kumpongeza rais mteule wa Kenya William Ruto na watu wa Jamuhuri ya Kenya kwa kuendesha uchaguzi wa huru, haki na wa amani.”



Naye Rais wa Nigeria Mahammadu Buhari amesema "Ningependa kuwapongeza watu wa Kenya kwa uchaguzi wa amani, na matokeo yenye uwazi, ambayo kwa mara nyingine tena yanaonyesha kuwa mchakato wa demokrasia ,maadili na kanuni vinasalia kuwa njia bora kwa watu kwa kuwachagua viongozi wao na kuwawajibisha
Share:

Monday, 15 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 16,2022















Share:

SHY TOWN NYAMA CHOMA FESTIVAL KUFANYIKA AGOSTI 26 - 28, 2022


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger