Wednesday, 20 July 2022

UTEUZI; RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU

Share:

Breaking : RAIS SAMIA ATEUA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA...IGP SIRRO AONDOLEWA.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura na Kumteua kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Kupita taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Uteuzi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 20, 2022 ambapo kabla ya kuteuliwa alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (CDI).

Pia Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe.

Wakati huo huo amempadisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamis Kingai kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (CDI).

Uteuzi mwingine ni kama ifuatavyo:





Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 20,2022



Magazetini leo Jumatano July 20,2022



Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI USIKU HUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi ufuatao;
Share:

DIAMOND PLATNUMZ ATHIBITISHA KUNUNUA NDEGE


Diamond Platnumz akitumbuiza Jijini Berlin Ujerumani

KAMA ulikuwa unadhani ni stori stori tu za mtandaoni, habari ikufikie Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amethibitisha kununua ndege.


Ndio, kwa kinywa chake Diamond ametamka akiwa nchini Ujerumani akiwa ameshika kipaza sauti cha chombo cha habari cha kimataifa cha DW nchini Ujerumani.
Diamond alikuwa akizungumzia namna msanii unatakiwa kuishi au kuwa ili kupata ile heshima unayostahili na kuingiza mkwanja wa kutosha (msanii unavyotakiwa kujiwekeza mwenyewe).


“Mfano kwa mtu kama mimi ambaye nimetokea mtaani, kwa sasa nanunua gari la kifahari lenye thamani hadi tsh. bilioni 2.3…kwa hiyo itabidi ufanye hivyo kwani usipofanya hivyo hawatakuona wewe ni wa thamani (watakuchukulia poa)… na sasa tayari nimeshanunua ndege binafsi (private jet),” Diamond Platnumz.
Share:

JIWE MBARONI TUHUMA ZA KUUA MKE WAKE UKWENI

 

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limemkamata Seleman Malima maarufu “Jiwe” mkazi wa Keko Mwanga kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Husna Majaliwa mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa maeneo ya Goba kwa Awadhi kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali Tumboni.


Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo huku akisema tukio hilo limetokea Juni 12, 2022 maeneo ya Goba kinondoni.

Amesema mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na juhudi za kumtafuta zilianza na kufanikiwa kumkamata Julai 18, 2022 katika maeneo ya Mbande Jijini Dodoma.

Kamanda Muliro amesema uchunguzi wa awali umethibitisha kulikuwa na mgogoro wa kifamilia baina ya wawili hao na mtuhumiwa alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu kumsalimia mzazi mwenzake pamoja na mtoto.

Wakati wakiwa kwenye maongezi ndipo mtuhumiwa Seleman alimshambulia mke wake kwa kisu na kumsababishia kifo.
Share:

KIMAMBO FASHION NDIYO HABARI YA MJINI!! NGUO BORA KWA BEI NAFUU 0762 656 192


Karibu Kimambo Fashion kwa nguo nzuri zenye ubora wa kiwango cha juu kwa gharama nafuu kabisa!! Duka la Nguo la Kimambo Fashion lipo Soko Kuu Shinyanga mkabala na Duka la Shirima.

Kimambo Fashion 'Quality Brand' :  Jeans, T - shirt, shirt, socks, belt,boxers, shoes.

Tupigie 0762 656 192

Share:

Tuesday, 19 July 2022

RUWASA KUTEKELEZA MIRADI 1,029 KUONDOA UHABA WA MAJI

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi  Clement Kivegelo akizungumza na Waandishi wa habari leo Julai 19,2022 Jijini Dodoma.

Na Dotto Kwilasa, DODOMA 
KWA mwaka wa fedha  2022/23 Wakala wa Maji Vjijini (RUWASA) umepanga kutekeleza jumla ya miradi 1,029 huku kati ya miradi hiyo 381 ni mipya na miradi 648 ile ambayo utekelezaji wake unaendelea kutoka mwaka wa fedha uliopita.

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi  Clement Kivegalo amesema hayo leo Julai 19,2022Jijini Dodoma  wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wake,utekelezaji,mwelekeo na mafanikio yake na kueleza kuwa  jumla ya kiasi cha Shilingi bilioni 387.7 imeidhinishwa na Bunge kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. 

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo, kutawezesha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kuongezeka kwa wastani wa asilimia sita na kwamba utekelezaji wa shughuli zake unaongozwa na Mpango Mkakati wa miaka mitano, yaani 2020/2021 hadi 2024/2025 utakaongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini hadi kufikia kiwango kisichopungua asilimia 85 kwa mwaka 2025.

Akieleza hali ya upatikanaji wa maji kabla na baada ya kuundwa RUWASA,Mhandisi Kivegalo amesema,wakati wa kuanzishwa kwake, RUWASA ilirithi jumla ya skimu za maji 1,379 zilizokuwa zimekamilika na kulikuwa na miradi 632 ya ujenzi wa skimu za usambazaji wa maji katika maeneo mbalimbali nchini na kueleza kuwa kati ya skimu hizo zilizokuwa zimekamilika 177 zilikuwa hazitoi huduma ya maji kwa wananchi kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukauka kwa vyanzo vya maji.

Amefafanua kuwa mwezi Julai 2019 upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ulikuwa ni wastani wa asilimia 64.8 ambapo pamoja na kiwango hicho cha upatikanaji wa maji, kwa ujumla, hali ya huduma ya maji vijijini haikuwa ya kuridhisha. 

Sambamba na hayo alisema ujenzi wa miradi ulikuwa ukichukua muda mrefu na kwamba hata miradi iliyokuwa ikikamilika na kuzinduliwa, ilidumu muda mfupi na kusababisha wananchi wa vijijini kuendelea na adha ya maji huku akieleza kuwa miradi hiyo ilikuwa ikijengwa kwa gharama kubwa ikilinganishwa na uhalisia wa soko.

Mhandisi hiyo pia amesema pamoja na utekelezaji wa mpango wa bajeti 2021/2022, kuliibuka pia uhitaji wa mradi wa maji kwa wananchi wa Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni ambacho  wananchi kutoka Ngorongoro walihamia kwa hiari.

Kutokana na hayo ameeleza kuwa RUWASA inatekeleza ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji hicho, ambapo mpango wa utekelezaji uligawanywa katika awamu mbili (awamu ya muda mfupi na awamu ya muda mrefu).

"Awamu ya muda mfupi imekamilika na vituo vya kuchotea maji 12 vimeshaanza kutoa huduma ya maji, awamu ya pili imefikia asilimia 70 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai, 2022,kukamilika kwa awamu hiyo kutawezesha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 17,000 pamoja na mifugo yao ,

Aidha hali hiyo itapelekea idadi ya vituo vya maji kuongezeka kutoka 12 hadi kufikia vituo vya kuchotea maji 30 kwa matumizi ya binadamu na vituo 3 vya kunyweshea maji mifugo,"amesisitiza 

Sambamba na hayo ameweka wazi kuwa Wakala huo  unafanya jitihada kuboresha huduma ya maji katika Kijiji cha Msomera na kwamba Serikali kupitia RUWASA inaendelea na ujenzi wa bwawa la maji kwa gharama ya Shilingi bilioni 1.99 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 15.

Share:

DKT.MPANGO-UNAHITAJIKA MUONGOZO ENDELEVU WA BIASHARA ILI UCHUMI WA BAHARI UENDANE NA MAZINGIRA YA BAHARINI

Makama wa Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifuatilia Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makama wa Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifungua Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Makama wa Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.Makama wa Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifuatilia Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akizungumza wakati Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Aboud Selemani Jumbe Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvivu Zanzibar akizungumza wakati Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mkutano ukiendelea wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifuatilia Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC uliofanyika Leo Jumanne Julai 19, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 19 Julai 2022 amefungua Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini, usimamizi na utunzaji wa mazingira ya Bahari Kongamano lililofanyikia katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 19 hadi 27 Julai 2022.

Akizungumza na Viongozi na washiriki wa Mongamano hilo Makamu wa Rais amesema umoja baina ya Mataifa pamoja na kujitolea ni mambo muhimu yatakayopelekea matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari pamoja na kuepusha kupotea kwa rasilimali hizo.

Amesema ni lazima kuzuia na kupunguza uchafuzi wa Bahari kwa kila namna kuanzia vyanzo vya ardhini hadi baharini.

Ameongeza kwamba unahitajika muongozo endelevu wa biashara ili uchumi wa Bahari uendane na mazingira ya Baharini.

Pia Makamu wa Rais amesema kwa sasa katika kulinda Bahari vinahitajika vitendo zaidi vitakavyokwenda sambamba na sayansi, uvumbuzi na teknolojia pamoja na ushirikishwaji wa wadau wote unaojumuisha vijana na wanawake katika mijadala ambao ni sehemu ya suluhu.

Hali kadhalika Makamu wa Rais amesisitiza kwamba Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kulinda mazingira ikiwemo mazingira ya Bahari kama vile kupiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki inayotumika mara moja, kutenga asilimia 6.5 eneo la Bahari ya Hindi kuwa eneo tengefu la bahari, kudhibiti kwa asilimia 99 uvuvi haramu pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa shughuli za uvuvi wa Bahari kuu.

Amesema umefika wakati wa kutafuta njia sahihi za kudhibiti na kusimamia shughuli zinazofanyika Baharini, pamoja na namna bora ya kuweka uwiano wa kiuchumi, kijamii na kimazingira wakati wa kutumia rasilimali za Bahari.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamiu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Dkt. Sulemani Jafo amesema kuwa Tanzania imepewa fursa na Umoja wa Mataifa ya kuwa mwenyeji na kuratibu Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya Hali ya Mazingira ya Bahari ikiwemo Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambao unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC.

Asema kuwa kwa sasa dunia inajielekeza katika kuangalia mambo ya Bahari kwa ujumla kama nyenzo muhimu ya kujenga uchumi na masuala mbalimbali ya kijamii.

Amesema Katika mkutano huo kutakua na mambo tofauti tofauti yatakayojadiliwa kwa takribani wiki mbili ili kuona taarifa mbalimbali zinazohusiana na uchumi wa Bahari na utaratibu wa kutoa takwimu mbalimbali za mwenendo wa kiuchumi na kijamii ukihusiana na bahari.

" Mikutano ya Kimataifa inapofanyika kunakuwa na Agenda mbalimbali miongoni mwa jambo chini ya Mkutano huu ni kujadili mambo mbalimbali yanayotokea katika sekta ya uchumi wa Bahari Duniani" amesema Waziri Jafo

Ameongeza kuwa zaidi ya Nchi 22 zimeweza kushiriki mkutano huu ambao washiriki zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali Duniani wameshiriki ambao utasaidia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu katika masuala ya kibahari , kujengeana uwezo na kujifunza namna Mashirika mbalimbali Duniani yanavyoweza kuratibu masuala ya Bahari na uchumi wake .

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Aboud Jumbe amesema kinachohitajika ni kuendelea kufanya kazi pamoja Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau, watumiaji wa Bahari pamoja na jamii inayoishi pembezoni mwa Bahari kwa ajili ya kuwawezesha kunufaika kiuchumi na mazao yanayotokana na Bahari (Blue economy).

Ameongeza kwamba Wataalam wanapaswa kuzingatia mahitaji ya watumiaji wa Bahari ambao wanaishi pembezoni kwa kuwa wamebeba wajibu wa ulinzi wa rasilimali za baharini.

Awali mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Kitengo cha mambo ya Bahari na Sheria za Kimataifa za Bahari Bi. Alice Hicuburundi amesema kwamba uelewa ni jambo muhimu zaidi katika kulinda na kuhifadhi kwa ajili ya matumizi endelevu ya Bahari.

Amesema matumizi ya sayansi na teknolojia yakiungana na uelewa ndio yanapaswa kuwa msingi wa ulinzi na utawala wa Bahari kwa maendeleo endelevu hasa katika kufikia lengo la 14 la Umoja wa Mataifa. Madhumuni ya Kongamano hilo ni kuwajengea uwezo washiriki juu ya usimamizi wa Bahari ikiwemo kuonesha hali na mwelekeo wa Bahari, vihatarishi vikuu vinavyoikabili Bahari na mazingira yake, matokeo ya vihatarishi hivyo, na hatua mbalimbali za kupunguza athari hizo.
Share:

WANANCHI KISHAPU WACHANGAMKIA KILIMO CHA MKONGE…. FURSA MPYA ILIYOJIFICHA


Mhasibu wa Shirikisho la wakulima na wasindikaji Mkonge Kishapu (SHIWAMKI), Joseph Kulwa akielezea namna wanavyosindika zao la mkonge. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Usindikaji zao la mkonge ukiendelea katika Shirikisho la wakulima na wasindikaji Mkonge Kishapu (SHIWAMKI)
Mhasibu wa Shirikisho la wakulima na wasindikaji Mkonge Kishapu (SHIWAMKI), Joseph Kulwa akionesha mkonge uliosindikwa tayari kusafirishwa kwenda kwa wanunuzi
Mwenyekiti wa Shirikisho la wakulima na wasindikaji Mkonge Kishapu (SHIWAMKI), akielezea kuhusu usindikaji wa mkonge.
Mbunifu wa mitambo ya kuchakata zao la mkonge Daud Magili Magolyo mkazi wa Kishapu akielezea kuhusu  mtambo mpya wa kisasa zaidi wa tatu kubuniwa duniani aliotengeneza kwa ajili ya kutumika kusindika mkonge.
Mbunifu wa mitambo ya kuchakata zao la mkonge Daud Magili Magolyo mkazi wa Kishapu akionesha namna mtambo mpya wa kisasa unavyofanya kazi ya kusindika mkonge.
Msaidizi wa Mbunifu wa mitambo ya kuchakata zao la mkonge Daud Magili Magolyo mkazi wa Kishapu akionesha mkonge uliosindikwa kwenye mtambo mpya wa kisasa wa kusindika mkonge.
Muonekano wa bango katika kitalu cha miche ya mkonge Kishapu
Muonekano wa miche katika kitalu cha miche ya mkonge Kishapu

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wananchi katika Halmashauri ya Kishapu wamehamasika kulima zao la Mkonge huku changamoto kubwa sasa ikiwa ni uhaba wa miche ya mbegu licha ya kwamba halmashauri hiyo imeanzisha kitalu chenye ukubwa wa ekari 20 kinachokadiriwa kuwa na miche 640,000.

Hamasa hiyo imetokana na maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipokutana na wadau wa mkonge mkoani Tanga mwaka 2021 ambapo alihamasisha Mikoa yenye ukame kama Kishapu kuona zao la Mkonge kama fursa ya zao la biashara badala ya kuwa zao mbadala jambo ambalo amekuwa akilihamasisha kila mara ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa serikali kuhamasisha kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo mkonge.


Kufuatia agizo hilo, wananchi wa Kishapu wamehamasika kulima zao hilo na sasa mahitaji yao ni miche milioni 13 juu ya kiwango cha miche iliyopo sasa 640,000 katika kitalu cha miche ya mkonge kilichoanzishwa na Halmashauri ya Kishapu.


Akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo waliotembelea wadau wa kilimo wilayani Kishapu, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika (Afisa Ugani) wilaya ya Kishapu, George Kessy amesema wakulima wa Kishapu wamehamasika kulima zao la mkonge na kinachohitajika sasa ni miche.


“Tumelima kitalu cha miche ya mkonge chenye ekari 20 kwa ajili ya kuzalisha miche tutakayoisambaza kwa wakulima, tayari wakulima wamejitokeza kwa wingi wakihitaji miche zaidi ya milioni 13 na mwezi Oktoba miche iliyopo tutaanza kuisambaza kwa wananchi ”,amesema Kessy.


“Tayari tuna Shirikisho la wakulima na wasindikaji Mkonge Kishapu (SHIWAMKI) ambao walima na kusindika mkonge na tunaye mbunifu wa mitambo ya kuchakata zao la mkonge Daud Magili Magolyo ambaye serikali imekuwa bega kwa bega naye katika kuhakikisha teknolojia hiyo inakuwa bora zaidi na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya teknolojia na viwanda wamekuwa wakimtembelea na kumpa ushirikiano na sasa amehama kutoka kwenye mashine za kwanza za kawaida na ametengeneza mtambo mpya wa kisasa zaidi wa tatu kubuniwa duniani”,ameeleza afisa ugani huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson amesema wananchi wamehamasika kulima zao la mkonge na mahitaji ya miche ni makubwa hivyo ili kupata miche mingi ya mkonge wanaendelea kuhamasisha wananchi kuanzisha vitalu vyao binafsi.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude amesema hivi sasa kuna mabadiliko makubwa kwani wananchi wameanza kuchangamkia kilimo cha mkonge zao ambalo linastahili ukame kulingana na mabadiliko ya tabia nchi.


Mhasibu wa Shirikisho la wakulima na wasindikaji Mkonge Kishapu (SHIWAMKI), Joseph Kulwa amewashauri wananchi wakiwemo vijana kuchangamkia fursa ya zao la mkonge kwani halina msimu na linavumilia ukame na soko lake ni kubwa ili kujikwamua kiuchumi.

“Soko la mkonge sasa ni kubwa na kupitia SHIWAMKI tumefanikiwa kuuza tani 240,000 na sasa tunauza kilo moja shilingi 2500”,amesema.

Share:

MWEKEZAJI KIWANDA CHA JIELONG AFUNGUKA CHANGAMOTO YA UHABA WA MALIGHAFI..ASHAURI UZALISHAJI MAZAO YA MAFUTA

Share:

Monday, 18 July 2022

UGONJWA ULIOLIPUKA LINDI NI 'HOMA YA MGUNDA' UNAAMBUKIZWA KUTOKA KWA WANYAMA KWENDA KWA BINADAMU


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
**
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa upimaji wa sampuli za wagonjwa waliokuwa wakiugua Ugonjwa Usiojulikana katika Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi umethibitisha mlipuko huu kuwa ni ugonjwa wa Leptospirosis, ama Homa ya Mgunda.

Waziri Ummy amesema hayo leo mara baada ya kutembelea Wilaya ya Ruangwa katika Mkoa wa Lindi ambako kumezuka mlipuko wa ugonjwa huo na kuzungumza na waandishi wa habari ambapo amesema Homa ya Mgunda ni miongoni mwa magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa Binadamu na unasababishwa na Bakteria aina ya Leptospira interrogans.

Ummy amesema “Ugonjwa huu umekuwepo katika maeneo ya kitropiki ambayo ni yenye hali ya joto katika mabara ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Afrika, Asia na Australia, wanyama aina za panya, kindi, mbweha, kulungu, swala, na wanyamapori wengine wameripotiwa kupata maambukizi ya vimelea hivi na kuwa chanzo cha maambukizi kwa Binadamu”

Amesema kuwa Ugonjwa wa Homa ya Mgunda huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa Binadamu kupitia uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji kutoka katika mkojo wa wanyama wenye maambukizi.

Wizara inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huu na kuendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu. Hivyo Serikali inawaasa Wananchi kutokuwa na hofu kwani ugonjwa huu unaendelea kudhibitiwa” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Chanzo - Global Publishers
Share:

IJA YAENDESHA MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA


Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbard Chuma akifungua mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Mahakama ya Tanzania yanayofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Picha mbalimbali za watumishi wapya wa Mahakama ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka wa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbard Chuma.

………………………………………………

Mhe. Wilbard Chuma Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania leo tarehe 18/07/202 amefungua rasmi mafunzo elekezi kwa watumishi wapya 58 wa Mahakama Tanzania. Mafunzo hayo yanaendeshwa na kufanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA). Hili ni kundi la kwanza kati ya waajiriwa 227 waliofanyiwa usaili na kuajiriwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama hivi karibuni ambapo kuna kada mbalimbali kama Mahakimu, Maafisa Utumishi, Maafisa TEHAMA, Makatibu Mahususi, Watunza Kumbukumbu Wasaidizi na Madereva.

Akitoa hotuba ya ufunguzi, Mhe. Chuma alianza kwa kuwapongeza waajiriwa hao wapya kwa kuwaeleza kuwa ajira waliyopata hawakupata kama hisani ila imepatikana kutokana na ubora waliouonesha wakati wa usaili hivyo wanapaswa kuwa waaminifu, waadilifu na wachapakazi kwa kuzingatia mikataba ya ajira, viapo na sheria za nchi katika utumishi wao.

Mhe. Chuma aliendelea kwa kuwasisitiza Watumishi hao wapya wa Mahakama kwa kumnukuu Jaji Mkuu wa Mahakama wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma tarehe Mei 31, 2021 katika hotuba yake aliyoitoa wakati akifungua rasmi Mafunzo elekezi kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya Tanzania pamoja na Mahakama Kuu Zanzibar hapa Chuoni kwa kusema watumishi wa Mahakama wanatakiwa kuwa na uadilifu na maadili ili wafanye kazi kwa kuzingaia Katiba na masharti ya viapo.

“Watu husahau kuwa mara nyingi sheria sio mbaya bali ni nafsi, maadili na tabia za wanaotekeleza sheria hizo. Hivyo nawakumbusha kila jalada utakalokuwa ukilitolea uamuzi ukumbuke kuwa linagusa watu halisi, linagusa uhuru wao, biashara zao, mali zao na familia zao. Kumbukeni kuwa wananchi kupitia katiba wametupa sisi Majaji mamlaka ya utoaji haki lakini wananchi wamebaki na haki zao zote za msingi” alinukuu.

Mhe. Chuma aliendelea kwa kuwakumbusha watumishi hao kuwa maadili ni kiini cha haki, na hivyo wakati wa kutekeleza jukumu la utoaji haki na wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi na kutoa maamuzi kwa kuzingatia misingi ya haki, sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.

Mhe. Chuma aliwaeleza watumishi hao wapya kuwa malengo ya mhimili wa Mahakama yatafikiwa iwapo watakuwa na nia moja na ushirikiano baina yao na watumishi wengine watakaowakuta kwenye vituo vya kazi watakavyopangiwa. Alieleza kwamba ushirikiano huo utasaidia kufanikisha jitihada zinazoendelea za maboresho ya Mahakama ya Tanzania. Mhe. Chuma aliwasisitiza watumishi hao kuwa na ushirikiano na wadau wengine kwa kuchukua mawazo mazuri na bora kutoka kwenye taasisi au idara zingine kwa kuyafanyia kazi au kuyafikisha mahali panapostahili ili yalete mabadiliko kwa kuwa kazi ya kulijenga taifa ni wote.

Mhe. Chuma aliendelea kwa kuwasisitiza watumishi hao kuwa dhana ya uhuru wa mahakama haina maana ya kuvunja sheria kwa kuwa kanuni hii ya kikatiba inaenda sanjari na kanuni ile ya Utawala wa Sheria. Hivyo, amewataka Mahakimu kuwa ni wajibu wao kufanya kazi zao chini ya kivuli cha uhuru wa Mahakama, kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria za nchi na sio kwa kuzivunja. Aliendelea kwa kuwaasa watumishi wengine ambao sio mahakimu wakawasaidie maafisa wa Mahakama wa ngazi mbalimbali katika kufikia azma ya kutenda na kutoa haki kwa mujibu wa sheria ili wasiwe chanzo cha malalamiko au kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na utendaji kazi ambao unakiuka misingi ya utu na katiba.

Mafunzo haya yanafanyika kwa makundi matatu ambapo kundi la kwanza la Mahakimu Wakazi na Maafisa Kumbukumbu Wasaidizi yamenza leo tarehe 18 Julai ,2022. Makundi mengine ya kada nyingine yatafuata na kutegemea kumalizika 12 Agosti, 2022.

IJA inajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wote wa mahakama kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao pia kwa mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yanayotoa huduma za utoaji haki nchini. Pamoja na mafunzo hayo Chuo kimebobea katika kutoa mafunzo ya Stashahada na Astashahada ya sheria. Vilevile Chuo kinafanya shughuli za kutoa ushauri wa kitalaamu, machapisho na tafiti mbalimbali.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger