Friday, 15 July 2022

WAJUMBE AUWSA WATEMBELEA CHANZO CHA MAJI YA ZIWA VICTORIA, WAVUNA MADINI YA KUTOSHA KASHWASA

WAJUMBE wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA),wametembelea na kukagua mtambo unaochakata na kusambaza maji ya ziwa Victoria kutoka mkoa wa Mwanza hadi Shinyanga na Tabora kwa kutumia mtambo huo.


Wajumbe hao wa Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) wamefanya ziara hiyo Julai 14, 2022, wakiwa wameambatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) mhandishi Patrick Nzamba na wajumbe wa bodi ya Maji Arusha, kwa lengo la kujifunza na kubadilishana mawazo juu ya utendaji kazi na Mamlaka ya Maji (KASHWASA).

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka Mamlaka hiyo ya Maji Arusha (AUWSA) Dk. Jackline Mkindi, amesema wamefanya ziara katika Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Kahama ,Shinyanga (KASHWASA), ili kujifunza jinsi gani wanavyoweza kuendesha mamlaka yao na kupata matokeo chanya kama ilivyo KASHWASA.


Dk. Mkindi amesema katika ziara hiyo wamejifunza vitu vingi vizuri kutoka (KASHWASA), ambapo wao kama Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) watakwenda kuvifanyia kazi na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwenye Mamlaka hiyo ya Maji Arusha.

“Tunaipongeza KASHWASA) kwa ubunifu wao mkubwa, wakutoa maji mkoa wa Mwanza hadi Shinyanga na kusambza huduma hiyo mikoa jirani ya kiwa safi na salama, huu ni ubunifu wa hali ya juu sana ambao sisi tumejifunza,”amesema Mkindi.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba akizungumza na wajumbe wa bodi ya maji kutoka AUWSA ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mwaka 2009 ilikuwa ni kutatua changamoto ya maji katika mji wa Shinyanga na Kahama lakini hivi sasa miji mingi inahitaji maji hayo kama vile (MwanzaNgudu,Shinyanga na Tabora) baadaye Isaka,Kishapu,Kagongwa,Igunga na Tabora.

Amesema wao ni wazalishaji wa maji wala siyo wasambazaji kwani kazi ya kusambaza maji kwa mteja mmoja mmoja inafanywa na mamlaka za maji katika miji husika kama vile KUWASA NA SHUWASA ambao ndiyo wateja wakubwa wa maji pamoja na kamati za maji za vijiji

Hata hivyo Mhandisi Nzamba amesema katika ziara hiyo imekuwa na mafanikio pia kwao, ambapo wamebadilishana mawazo na kupeana ushauri wa kiutendaji kazi hali itakayo saidia kuboresha utendaji kazi wa KASHWASA katika mkoa wa Shinyanga.

Baadhi ya mitambo katika jengo karibu na Ziwa Victoria,hii inatumika kusukuma maji hadi katika kituo cha Kutibu Maji cha Ihelele kilomita chache kutoka Ziwani





Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA) Jackline Mkindi, akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yao Mkoani Shinyanga kwa kutembelea KASHWASA.










Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 15, 2022


Magazetini leo Ijumaa Julai 15, 2022


Share:

Wednesday, 13 July 2022

UGONJWA WA AJABU WAIBUKA TANZANIA.. RAIS SAMIA "HATUJUI NI KITU GANI....WATAALAMU WAMEPIGA KAMBI"

 Na Veronica Mrema

Homa kali, mwili kuchoka, shida ya kupumua na kutoka damu puani, ndizo dalili za awali ambazo zimeripotiwa za ugonjwa usiojulikana uliozuka huko Kusini mwa Tanzania.


Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichwale amebainisha dalili hizo alipozungumza na EAST Africa Radio.


"Timu bado ipo 'site', wakija {na ripoti kamili}, tutaeleza Umma sasa bado ni mapema.


"Mkoa wa Lindi wanajaribu kufuatilia hii shida ni nini?


"Dalili tulizoambiwa homa kali, mwili kuchoka, kupata shida ya kupumua na kutoka damu puani, ndizo  wanazosema," amesema.


Dkt. Sichwale ameongeza"Timu yetu ya idara ya magonjwa ya dharura na majanga na nyingine kutoka Idara ya Kinga katika Kitengo cha epidemiolojia.


"Timu ya afya ya Mkoa na halmashauri na idara ya mifugo wanaendelea na ufuatilia, taarifa itatolewa na Waziri wa Afya, tuwe na subra" amesema.


Julai 13, 2022 {jana}, akizungumza katika Maadhimisho ya Mkutano wa 20 wa AMECEA, Rais Samia Suluhu Hassan alisema ugonjwa umeingia huko Kusini mwa Tanzania, watu wengi wanatoka damu puani na kudondoka.


"Ingekuwa mmoja tungesema labda ana 'presha' {Shinikizo la damu} au 'veins' zimepasuka {puani}, Lakini ni wengi wanadondoka kwa mara moja," alisema.


Ingawa hakubainisha takwimu, Rais Samia alithibitisha kwamba tayari wataalamu wa afya wamehamia {wamepiga kambi} huko wakifuatilia kwa kina ugonjwa huo.


Rais Samia ameongeza "Hatujui kitu gani wataalamu na wanasayansi wamehamia huko wanaangalia.


Chanzo : Matukio na Maisha blog

Share:

AJALI YA GARI MCHOMOKO YAUA WATU WATANO SIMIYU.

 

Watu watano wamefariki dunia na wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Magereza nje kidogo ya mji wa Bariadi Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu usiku wa kuamkia leo Julai 13, 2022.


Kamanda wa Polisi Mkoa Simiyu, Blasius Chatanda amesema kuwa ajali hiyo imehusisha magari madogo ya abiria.

"Nimefika eneo la ajali nimeona waliofariki wote ni wanaume. Gari moja mchomoko lilikuwa likitokea Lamadi na lingine Bariadi. Dereva aliyekuwa akitoka Lamadi aliova-take ndipo akakutana na mwenzake. Chanzo ni mwendo kasi. Madereva wamejeruhiwa na wapo chini ya ulinzi,"amesema
Share:

RAIS SAMIA ARIDHIA WADAIWA SUGU KODI YA ARDHI KUSAMEHEWA RIBA


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Nyachoka wilayani Serengeti mkoani Mara wakati wa zoezi la kukabidhi hati miliki za kimila tarehe 12 Julai 2022 Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Nyachoka wilayani Serengeti mkoa wa Mara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipokwenda kutoa hatimiliki za kimila tarehe 12 Julai 2022Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi kitabu cha mpango wa matumizi ya ardhi Mwenyekiti wa kijiji cha Nyichoka wilayani Serengeti mkoa wa Mara Imanuel Cairo Sochora wakati wa zoezi la kukabidhi hati miliki za kimila tarehe 12 Julai 2022.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara Vicent Mashinji akizungumza wakati wa zoezi la kugawa hatimiliki za kimila tarehe 12 Julai 2022. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Na Munir Shemweta, SERENGETI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia kusamehewa riba ya kodi ya pango la ardhi kwa wadaiwa sugu kwa masharti kwamba wadaiwa hao wawe wamelipa madeni yq msingi ndani ya miezi sita kuanzia mwezi julai hadi desemba 2022.

Hayo yamebainishwa tarehe 12 Julai 2022 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Nyachoka wilayani Serengeti mkoani Mara wakati wa zoezi la kukabidhi hati miliki za kimila.

Jumla ya hatimiliki za kimila 6,155 zimekamilika na kutolewa kwa wananchi wa vijiji 22 katika wilaya ya Serengeti ambapo hati 1621 sawa na asilimia 26 zimekamilishwa kwa ajili ya akina mama na hatimiliki 1519 sawa na asilomia 25 ni za umiliki pacha kati ya wanaume na wanawake.

Dkt Mabula alisema yeye pamoja na Waziri wa Fedha ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusamehe watakutana na kupanga namna bora ya kutekeleza msamaha huo.

"Najua kuna wengi wanadaiwa madeni ya muda mrefu kwa hiyo kumetokea msamaha kuanzia mwezi julai mpaka desemba mwaka huu, watakaoweza kulipa ndani ya miezi hii sita, wale ambao madeni yao yana miaka mitano kurudi nyuma watalipa bila ile tozo ya riba" alisema Dkta Mabula.

" Mhe mama samia ameridhia kupitia waziri wa fedha kwa kushirikiana na waziri wa ardhi waweke utaratibu mzuri wa ninyi kuondolewa tozo ile na msamaha ni wa miezi sita tu kama una ndugu mpigie simu mwambie serikali ya awamu ya sita chini ya mama samia imetoa msamaha kwa wadiwa sugu ili watoke katika jina baya la wadaiwa sugu kwenda kulipa madeni bila riba" alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, mmiliki wa ardhi atakayeshindwa kulipa madeni yake katika kipindi cha miezi hiyo sita basi atadaiwa madeni yake pamoja na riba na akishindwa kufanya hivyo atafikishwa kwenye vyombo vya sheria ambako huko uamuzi wake ni kulipa ama kunyang'anywa ardhi anayoimiliki.

Akigeukia zoezi la utoaji hatimiliki za kimila Dkt Mabula alisema, hatua ya kumilikishwa ardhi kwa nyaraka kuna faida kubwa katika maisha ya kila siku na kutaja baadhi ya faida hizo kuwa ni pamoja na usalama wa ardhi, uhakika wa milki, kupunguza migogoro pamoja na nyaraka hiyo kutumika kama dhamana.

Zaidi ya wananchi 6000 katika vijiji 22 wamepangiwa matumizi bora ya ardhi katika maneo yao na kuwekewa mipaka ya kudumu ili kuepuka migogoro ya mipaka kwenye ardhi zao

Serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Serengeti, Shirika la Hifadhi la Taifa Serengeti (SENAPA) na Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) kupitia mradi wa utunzaji na uendelezaji wa Ikolojia ya Serengeti waliingia makubaliano ya pamoja kwa ajili ya kuwezesha uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya vijjji vinavyopakana na maeneo yaliyohifadhiwa yanayounda ikolojia ya serengeti inayojumuisha hifadhi za taifa na mapori ya akiba.

Madhumuni ya mradi huo ni pamoja na kupunguza migogoro ya matumizi ya ardhi kati ya vijiji na eneo la hifadjhi , kutatua migogoro ya mipaka kati ya maneo ya kiutawala pamona na kutoa elimu ya uhifadhi na sheria mbalimbambalj zinazosimamia mipango ya matumiZi ya ardhi nchini
Share:

WAZIRI DKT MABULA AIPA WIKI MBILI HALMASHAURI YA SERENGETI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza na uongozi wa wilaya ya Serengeti na watendaji wa sekta ya ardhi tarehe 12 Julai 2022Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti (aliyevaa Kaunda) Ayoub Mwita akimuonesha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi eneo la kijiji cha Nyichoka katika ramani ya Sereneti wakati wa ziara ya siku moja katika wilaya hiyo tarehe 12 Julai 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiangalia moja ya hati za kimila alizozikuta katika ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Serengeti wakati wa ziara yake ya siku moja tarehe 12 Julai 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

***************

Na Munir Shemweta, SERENGETI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameipa wiki mbili halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara kumpatia taarifa ya hali ya mashamba 36 yaliyopo katika halmashauri hiyo ili yale mashamba yasiyoendelezwa yaweze kubatilishwa umiliki wake.

Hatua hiyo inafuatia kuelezwa kupitia taarifa ya sekta ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Serengeti kuwa wilaya hiyo ina mashamba yaliyopimwa 36 kulingana na taarifa iliyopatikana kutoka wizarani kutokana na kutokuwepo kumbukumbu za kutosha mashamba hayo katika wilaya hiyo.

Taarifa hiyo iliyosomwa na nAfisa Ardhi Mteule wa Halmasahauri hiyo ya Serengeti Orwaka Nyamsusa ilieleza kuwa, mashamba hayo yalipimwa vijijini bila kufuata taratibu za uhaulishaji na ilipotakiwa yamililishwe kwa kupewa hati za kawaida ilishindikana.

"Ninawapa Serengeti wiki mbili nijue status ya mashamba hayo na kama ni suala la kuanza kuyabatilisha, mchakato uanzie katika halmashauri ambayo ni mamlaka ya upangaji ili tuitangaze fursa kwa wawekezaji kama Serengeti tunayo mashamba 36 na kati ya hayo ni matano tu yenye umiliki halali’’. Alisema Dkt Mabula

Akizungumza na uongozi wa wilaya ya serengeti na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo tarehe 12 Juala 2022 wilayani humo, Dkt Mabula alisema haingii akilini mashamba pamoja na ardhi kuwa katika halmashauri hiyo lakini halmashauri husika haina kumbukumbu iwapo imeyapima mashamba hayo na badala yake inaenda kutafuta kumbukumbu wizarani.

Alibainisha kuwa, kama utaratibu wa kuisimamia sekta ya ardhi kwa halmashauri ya Serengeti utakuwa ni wa aina hiyo basi halmashauri hiyo haiwezi kufika popote katika masuala ya ardhi na itaendelea kuwa na changamato.

" Halmashauri ni mamlaka za upangaji kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mipango miji ya 2007, ni mamlaka za upangaji zinazotakiwa kupanga miji yao wanataka iwe ya namna gani wizara kazi yake ni kusimamia na kuangalia kama shughuli za ardhi zinaenda kwa utaratibu au shetia zinafuatwa.

Alisema, halmashauri nyingi hazifuati takwa la sheria huku zikifahamu ni mamlaka za upangaji na kueleza kuwa halmashauri zote zinatakiwa kutekeleza takwa hilo na zisipotekekeza migogoro yq ardhi haiwezi kuisha.

Katika taarifa yake, halmashauri ya wilaya ya serengeti ilieleza kuwa wilaya hiyo ina jumla ya vijjji 78 ambapo kato ya hivyo vijjji 61 vimepimwa huku vijiji 10 kati ya hivyo vikitakiwa kufanyiea marejeo kutokana na makosa katika ramani za upimaji.

Aidha, jumla ya vijiji 29 kati ya 78 vina mpango wa matumizj bora ya ardhi ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/ 2023 halmashauri hiyo imetenga kiaai cha shilingi 15,000,000 kwa ajili ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji 3
Share:

Tuesday, 12 July 2022

AJALI YAUA WATU NANE, KUJERUHI WATANO BUHARAMULO


Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, William Mwampaghale

**
Watu nane wakiwamo watano wa familia moja ambao ni mama na watoto wake wanne, wamefariki dunia baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso usiku wa kuamkia Julai 11, 2022, katika eneo la Busiri barabara kuu ya kutoka Lusahunga kuelekea Nyakahura wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera William Mwampaghale, amesema kuwa ajali hiyo imeyahusisha gari la mizigo lililokuwa likitokea nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam, likiendeshwa na Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda, na Toyota Succeed lililokuwa likitokea eneo la Nyamalagala wilayani Biharamulo kuelekea Benaco wilayani Ngara likiendeshwa na Nyawenda Bihela (35) ambaye alifariki wakati wa ajali hiyo.

"Uchunguzi wa awali umeonesha ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa lori kutokana na kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara na kuendesha gari upande wa kulia, kitendo kilichosababisha magari hayo kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo, miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika kituo cha afya Nyakanazi Biharamulo" amesema Kamanda William.

Kamanda huyo amesema kuwa mbali na dereva pia watu wote waliokuwa katika gari aina ya Toyota Succeed walipoteza maisha, na kutaja majina yao kuwa ni Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo (6), Vedastina Sekanabo (8), Michael Charles (28) na Majaliwa Kanundo (32).

Chanzo - EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger