Tuesday, 12 July 2022
TEITI YATOA ELIMU KWA WANANCHI NAMNA INAVYOTIMIZA MAJUKUMU YAKE KWA MUJIBU WA SHERIA
KUHANI MWAKIBINGA : JITOKEZENI KWA WINGI KUHESABIWA SIKU YA SENSA

Kuhani Ayubu Mwakibinga
Na Derick Milton, Bariadi.
Amesema kuwa zoezi hilo ambalo litafanyika Agosti 23, 2022 ni muhimu sana kwa nchi ambayo inataka kuwaletea watu wake maendeleo, ambapo ameeleza yeye atakuwa mstari wa mbele siku hiyo kwenda kuhesabiwa.
Kiongozi huyo wa Dini amesema hayo jana mjini Bariadi wakati wa mkutano wake wa injili uliofanyika mjini Bariadi na kuhudhuliwa na mamia ya wananchi wa mji wa Bariadi wakiwemo wahumini wake.
Alisema kuwa zoezi la sensa linatakiwa kuungwa mkono na kila mtanzania mpenda maendeleo, kwani serikali haiwezi kuleta miundombinu mbalimbali kwa wananchi bila ya kujua wako wangapi na wanahitaji nini.
Aliongeza kuwa watu wengi wamekuwa wakilalamikia serikali kwa kushindwa kuwaletea huduma za mbalimbali za kijamii, ambapo ameeleza ili serikali iweze kutimiza jukumu hilo lazima ijue ina watu wangapi.
Amewataka wahumini wake kila mmoja kuhakikisha anamwasisha mwezake kwenda kuhesabiwa Agosti 23, 2022, ili serikali iweze kuweka mipango yake ya kuwaletea watanzania maendeleo.
“ Agosti 23, 2022 ni siku ya sensa kitaifa, na sisi kama raia wa nchi hii, ambayo inaoongoza na mmama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan tunao wajibu wa kumuunga mkono Rais wetu kwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhesabiwa, Mimi nitakuwa mstari wa mbele kuhesabiwa.” Alisema Kuhani Mwakibinga…..
“ Nchi lazima iwe na takwimu, tukipanga maendeleao tujue wako wangapi, tunaweka pale kulingana na takwimu na watu wako pale, tusipohesabiwa tutajua watu wako wangapi?....
Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa Dini amewataka wahumini wake kuendelea kumwombea Rais Samia kwani amekuwa kiongozi mwenye maono wa kuletea maendeleo kwa kasi wananchi wake.
“ Tumemwona Rais wetu kwa kipindi hiki kifupi amejenga shule, vituo vya Afya kwa wingi sana, tunao wajibu wa kumlinda kiongozi wetu kwa kumwombea na wale wenye nia mbaya na yeye” ,alisema Kuhani Mwakibinga
WAZIRI WA NISHATI AANZA UHAMASISHAJI WA MATUMIZI SAFI YA NISHATI NCHINI

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (kushoto) akizungumza na Bi.Tereza Stephano wa Kijiji cha Kisamwene wilayani Butiama kuhusu athari za matumizi ya kuni na mkaa katika mfumo wa upumuaji pamoja na faida za kutumia nishati safi ya kupikia. Waziri wa Nishati aligawa mtungi wa Gesi kwa kaya ya Bi. Tereza Stephano ili iweze kutumia kwa matumizi ya kupikia.
Waziri wa Nishati, January Makamba akizindua mradi wa umeme wa BUTUGURI wilayani Butiama mkoani Mara ambao utasambaza umeme katika Nyumba 287 na utagharimu Shilingi milioni 385. Mradi huu utawasaidia wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kufunga mashine za kusaga na kukoboa nafaka, uchomeleaji na upatikanaji wa huduma bora za kijamii ikiwemo maji baada ya umeme kufika katika miradi ya maji.
Bi.Tereza Stephano kutoka Kijiji cha Kisamwene wilayani Butiama mkoani Mara akimshukuru Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba baada ya kumkabidhi mtungi wa gesi utakaomwezesha kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo yanaleta athari katika mfumo wa upumuaji. Kulia kwa Waziri wa Nishati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ambaye pia ni Mbunge wa Butiama.
Dkt. Mary Mahenge kutoka Hospitali ya Mkoa wa Mara iliyopo wilayani Musoma akimweleza Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ( wa Pili kutoka kushoto) kuhusu magonjwa ya mfumo wa hewa ni yanayotokana na kuchomwa kwa kuni na mkaa wakati Waziri wa Nishati alipofanya ziara mkoani Mara kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.MWENYE NYUMBA AEZUA PAA KWENYE VYUMBA VYA WAPANGAJI WAKE NGOKOLO SHINYANGA
Monday, 11 July 2022
JITIBU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER
MAJAMBAZI YAVAMIA BAA NA KUUA WATU 15

Watu 15 wameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine 11 wakijeruhiwa baada ya kuvamiwa na majambazi katika baa moja iliyopo kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo ya habari nchini humo, tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Jumapili, Julai 10, muda mfupi baada ya saa sita usiku.
Watu wengine 11 walijeruhiwa katika kisa hicho ambapo walikimbizwa hospitali huku nane kati yao wakiwa mahututi.
“Ndio, ninaweza kuthibitisha kuwa kisa hicho kilitokea mwendo was aa sita na nusu asubuhi hii,” Kamishna wa Polisi wa Gauteng Elias Mawela amenukuliwa na eNCA, ambalo ni shirika la habari la nchini humo.
Kamishna huyo wa polisi vilevile alisema kuwa waathiriwa ni wa kati ya umri wa miaka 19 na 35. Washukiwa wanaripotiwa kutoroka punde tu baada ya kutekeleza kisa hicho.
“Mwanzo wa upepelezi unaonyesha kuwa watu walikuwa wanaburudika katika eneo moja la burudani. Waliingia na kuwamiminia risasi kiholela,” Mawela alisema.
Sunday, 10 July 2022
ELIMU MATUMIZI SAHIHI UTUMIAJI CHANDARUA CHA MBU YATOLEWA KWA WAKAZI WAPYA MSOMERA
Tabibu Mwandamizi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Grace Vincent akeieleza jambo wakati akitoa elimu kwa WANANCHI wa kaya 104 waliohamia Kijiji cha Msomera wilayani Handeni wakitokea Hifadhi ya Ngorongoro namna ya kutumia vyandarua kwa usahihi ili kujikinga na malaria pamoja na magonjwa mengine yanayotokanayo na mabaadiliko ya hali ya hewa.Chini ni picha mbalimbali zikionesha namna gani ya kutumia vyndarua hivyo kutoka kwa Wataalamu wa NCAA.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MSOMERA-HANDENIANAYETAKA KUNUNUA MTANDAO WA TWITTER AANZA KUZINGUA






























