Haya siyo mafuriko! Bali ni Bomba la Maji la Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) linalopita katika eneo la Soko Kuu Mjini Shinyanga likiwa limepasuka baada ya mtambo wa kuchonga barabara (Greda) uliokuwa unang’oa kisiki katika eneo ambalo ujenzi wa stendi ya mabasi unaendelea.
Tukio hilo lililozua kizaazaa limetokea jioni hii leo Jumamosi Juni 18,2022 majira ya saa 12 jioni ambapo maji hayo yanayotiririka kuelekea maeneo mbalimbali yameendelea kupotea kwa zaidi ya saa moja na kusababisha uharibifu/uhalifu wa mazingira na upotevu mkubwa wa maji.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Tazama Video hapa chini











Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji azungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akitoka katika ofisi za kiwanda cha 21st Century Textiles Limited mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji (hayupo pichani) baada ya kufanya ziara kwenye kiwanda hicho leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam













Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiagana na Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yanayolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; Mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiagana na mgeni wake Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian muda mfupi baada ya kuhitimisha mazungumzo yaliyolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akipokea utambulisho wa wasaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati alipokutana nae kwa mazungumzo. Mazungumzo yalilenga kutazama maeneo ya ushirikiano ili kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam. Picha: TCRA
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akisisitiza jambo mbele ya Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati wawili hao walipokutana kwa mazungumzo yanayolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; Mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam


