

















Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Silvest Arumasi akizungumza na wateja katika mkutano walipokutana hivi karibuni Mkoani Mwanza
Wateja wa Benki ya Akiba Comercial Tanzania wakifurahia jambo patika mkutano na uongozi wa benki hiyo hive karibuni Jijini Mwanza
Wafanyakazi wa Benki ya Akiba Comercial Tanzania wakiwa tayari kuwapokea wateja mbali mbali wa Benki hiyo hivi Runde Jijini Mwanza
Meneja wa Tawi la Mwanza Herieth Bujiku akizungumza na wateja wa Benki ya Akiba Comercial Tanzania mara baada ya kukutana nao hivi karibuni Jijini Mwanza[/caption] Meneja wa Tawi la Mwanza Herieth Bujiku akizungumza na wateja wa Benki ya Akiba Comercial Tanzania mara baada ya kukutana nao hivi karibuni Jijini Mwanza
Wateja wa Benki ya Akiba Comercial Tanzania wakipata Chakula mara baada ya kukutana na Uongozi wa Benki hiyo hivi karibuni Jijini Mwanza .



Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma ya magonjwa ya moyo kwa wananchi katika hospitali ya Msoga ,Halmashauri ya Chalinze****
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
TAASISI ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na halmashauri ya Chalinze, Mkoa wa Pwani wametoa huduma ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wenye matatizo hayo hivi karibuni.
Huduma hiyo iliyochukua siku mbili, ikiendeshwa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Halmashauri ya Chalinze ilihudumia wananchi kutoka mkoa wa Pwani pamoja na mikoa jirani katika hospitali ya Msoga iliyopo Chalinze.
Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi hiyo Dkt.Peter Kisenge alieleza kuwa zoezi hilo limefanyika katika hospitali hiyo na idadi ya watu waliofika katika zoezi hilo kwa ajili ya upimaji, wapo waliopatikana na magonjwa hayo na wengine walikuwa salama.
“Tangu tumefika hapa mpaka leo tunamalizia zoezi hili la upimaji na tumeweza kupata idadi ya watu 422, ambapo kati ya hao asilimia 60 ya wagonjwa tumewaona wana matatizo ya shinikizo la damu kwa misuli yao ya moyo kutanuka na kutofanya kazi vizuri, na tumeweza kuwapeleka wagonjwa 20 katika Taasisis yetu kwa ajili ya kupata uchunguzi zaidi”.Alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge aliwashauri wananchi kujikinga na magonjwa ya moyo kwa kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora na kuepuka vyakula vinavochangia unene wa kupitiliza kiasi, hususani vyakula vya wanga, nyama kwa wingi, unywaji wa pombe pamoja na uvutaji wa sigara uliiokithiri.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Dkt.Allen Mlekwa aliwapongeza wananchi wa Chalinze kwa kujitokeza kupata huduma ya vipimo vya moyo pamoja na mikakati ya Halmashauri ya Chalinze juu yakuendeleza vipimo hivyo.
Dkt. Mlekwa kwa niaba ya Halmashauri ya Chalinze aliishukuru Serikali ya awamu ya sita pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa ushirikiano wa kutoa huduma hizo.
Kwa niaba ya wananchi waliopatiwa vipimo hivyo, Bi.Gabriela Mtwale aliishukuru Halmashauri ya Chalinze kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa huduma walizozipata na kuomba zoezi hilo liwe linafanyika mara kwa mara ili kuokoa maisha ya nguvu kazi ya Taifa.
Kaimu meneja wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS )Kanda ya Magharibi Bw.Rodney Alananga akiwa katika zoezi la kuteketeza bidhaa za vyakula na vipodozi katika dampo la Manispaa ya Mpanda mapema jana.

Makani Mkuu wa Chuo cha DMI akiwa na timu kutoka DMI tayari Kwa maonyesho ya NACTVET katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
Mhe. Jumanne Kishimba, Mbunge wa Kahama Mjini atembelea banda la DMI.
Bi. Winfrida Ngallu, mwanafunzi wa Marine Engineering, mwaka wa tatu akitoa elimu kuhusiana na taaluma ya ubaharia.
Capt. Azan Azan kutoka chuo cha DMI akitoa elimu ya kujiokoa wakati wa dharula melini.
Umati wa wananchi umefurika katika banda la DMI wakipatiwa elimu ya bahari.
Watumishi kutoka chuo cha DMI wakijioanga kutoa huduma Kwa wananchi katika viwanja vya Jamhuri - Dodoma.
Prof. Zacharia Nganilo, Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) atembelea banda la DMI.