Thursday, 28 April 2022

HAYA NDIYO MAHARAGE YANAYOONGEZA NGUVU ZA KIUME


Maharage aina ya Jesca

KUTOKANA na kuwa na ongezeko kubwa la wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume tafiti zimeonesha kuwa kuna aina ya maharage yanayopatikana jijini Arusha na Tanzania kwa ujumla ambayo ni suluhisho la tatizo hilo.


Maharage hayo yanafahamika kwa jina la Jesca ambalo kimsingi limetokana na muunganiko wa herufi za kwanza za majina ya vijana wanne ambao waliamua kuungana na kufanya utafiti pamoja na kufanya uzalishaji wa maharage hayo ambayo wanadai yanapatikana kote nchini tena kwa bei ambayo ni rafiki kwa mteja.
Maharage aina hii yanaongeza nguvu za kiume

Vijana hao ni John, Elizabeth, Sostenes, Clement na Alex.

Maharage hayo yameongezwa viini lishe vya madini ya zinki na chuma ambavyo vinasaidia kuongeza uzalishaji wa homoni aina ya testosteroni pamoja na kuongeza damu mwilini,


Licha ya kwamba maharage hayo yamekuwa yakipewa majina mbalimbali kutokana na maeneo husika mathalani majina kama Iringa au Punda, lakini jina halisi ambalo watafiti hao wameliweka wazi kama jina la Kampuni ni JESCA.


Naye mtaalamu kutoka Taasisi ya Lishe Celestin Mgoba amesema maharage ya Jesca yameongezewa kwa wingi madini chuma na madini ya zinki kwa njia ya kilimo ambayo amedai kwa madini chuma ni lazima iwe miligramu 74 hadi 92 kwa kilo moja na zinki iwe miligramu 26 hadi 43 kwa kilo moja.
Share:

Wednesday, 27 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 28,2022












Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 27,2022

















Share:

Tuesday, 26 April 2022

TANZANIA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA DUNIANI


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), Bw. Junaid Kamal Ahmad, Makao Makuu ya Benki hiyo, Jijini Washington DC, Marekani.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), Bw. Junaid Kamal Ahmad, kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania, Makao Makuu ya Benki hiyo, Jijini Washington DC, Marekani.

Makamu wa Rais wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), Bw. Junaid Kamal Ahmad, akizungumza wakati wa mkutano wake na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania, Makao Makuu ya Benki hiyo, Jijini Washington DC, Marekani.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), Bw. Junaid Kamal Ahmad, Makao Makuu ya Benki hiyo, Jijini Washington DC, Marekani.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), ukiongozwa na Makamu wake wa Rais Bw. Junaid Kamal Ahmad (wa tatu kulia), Makao Makuu ya Benki hiyo, Jijini Washington DC, Marekani. Kushoto ni Mshauri Mwandamizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Dkt. Zarau Kabwe, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Bi. Sauda Msemo.

Ujumbe wa Tanzania (kulia) ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba ukiwa katika kikao na ujumbe wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), ukiongozwa na Makamu wake wa Rais Bw. Junaid Kamal Ahmad, kilichojadili masuala ya fursa ya uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania, Makao Makuu ya Benki hiyo, Jijini Washington DC, Marekani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Washington DC)

******************************

Na Benny Mwaipaja, Washington DC

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania katika sekta mbalimbali.

Bw. Tutuba ametoa rai hiyo mjini Washington DC, Marekani, alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), Bw. Junaid Kamal Ahmad.

Alisema kuwa Serikali imeweka vivutio vingi vya uwekezaji ili kuvutia mitaji na teknolojia kutoka nje ya nchi na kuiomba taasisi hiyo itoe dhamana kwa kampuni, taasisi au mashirika yanayotaka kuwekeza nchini Tanzania.

“Tuna maeneo ya uwekezaji kwenye nishati, uendeshaji wa mabasi, reli ya kisasa ambapo wawekezaji wanaweza kuleta vichwa vya treni na mabehewa lakini pia kwenye sekta ya kilimo kwenye miundombinu ya uwagiliaji, pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya utalii kwa kujenga hoteli za kisasa na miundombinu mingine” alisema Bw. Tutuba

Bw. Tutuba alisema kuwa MIGA inatakiwa kutoa dhamana kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu na wawekeze kwenye maeneo hayo.

Alisema kuwa Tanzania imeialika Taasisi hiyo kufanya majadiliano ya pamoja na wawekezaji kutoka pembe zote za dunia mwezi Julai, 2022 nchini Tanzania, hatua itakayochochea masuala ya uwekezaji ambao lengo lake ni kukuza uchumi wa nchi, ajira na hatimaye kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja.

“Kikao kimekuwa na mafanikio makubwa kama watakuja na kutoa dhamana kwa wafanyabiashara wa ndani, ninaamini wafanyabiashara wa chini watakuwa wa kati na wa kati watakuwa wafanyabiashara wakubwa ambao uwekezaji wao utazalisha ajira, kukuza uchumi na kuchangia mapato na kodi nyingine za Serikali na kuongeza kipato cha mtanzania mmoja mmoja” alisema Bw. Tutuba

Kwa upande wake, Makamu wa Rais anayesimamia masuala ya uendeshaji wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayoshughulika na utoaji Dhamana katika Uwekezaji kwa Sekta Binafsi (MIGA), Bw. Junaid Kamal Ahmad, aliipongeza Tanzania kwa hatua zake za kuboresha mazingira ya uwekezaji ambayo anaamini yatavutia wawekezaji wengi kuwekeza nchini humo.

Alisema kuwa Taasisi yake iko tayari kufanya mkutano wa majadiliano na wadau wa sekta binafsi nchini Tanzania na kuahidi kuendelea kuwashawishi wawekezaji wengi kwenda kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati pamoja na maeneo mengine yatakayochangia kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.

Alisema kuwa Sekta Binafsi ndiyo injini ya ukuaji wa uchumi wan chi yoyote duniani na kwamba mazingira mazuri ya uwekezaji ynyofanywa na Tanzania yatasababisha wawekezaji wengi kufulika nchini humo na kwamba watatumia mkutano huo wa majadiliano kuchadili furs ana changamoto za uwekezaji huo na kuzipatia ufumbuzi wa Pamoja.
Share:

Monday, 25 April 2022

MREMA NA MKEWE WAHITIMISHA FUNGATE LAO KIBABE

 MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Taifa, Dkt.Augustine Lyatonga Mrema ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye hifadhi zilizopo nchini kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi ili kuweza kukabiliana na tatizo la ujangili.

Ametoa wito huo wakati akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita kwenye hifadhi nne za wanyama akiwa na mke wake Doreen Kimbi kwa ajili ya kukamilisha fungate yao.

Mrema amesema pamoja na kwamba kumeimarishwa kwa vikosi vya ulinzi kwenye hifadhi lakini bado wananchi ambao vijiji vyao vipo karibu na hifadhi wana nafasi ya kusaidia ulinzi ili kumaliza tatizo la ujangili.
Aidha, Mrema amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za wanyama badala ya kidhani kuwa kazi hiyo ni kwa ajili ya wageni tu kutoka nje.

Amesema Watanzania wanapaswa kumuunga mkono rais Samia Suluhu Hassan ambaye amejipanga vizuri kwa ajili kutangaza vivutio vyetu vya utalii ndani na nje ya nchi kupitia filamu ya Safari Royal Tour kwa kutembelea mbuga za wanyama.
"Nimekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani y Nchi, nimekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, nimekuwa Naibu Waziri Mkuu, nimekuwa mbunge Vunjo lakini sikuwahi kutembelea kwenye mbuga za wanyama lakini kiukweli kuna mambo mazuri ya kujifunza unapopata fursa usikose kutembelea hifadhi zetu,"amesema.


Naye mke wake Mrema, Doreen Kimbi, amesema katika mbuga za wanyama kuna vitu vingi vizuri vya kujifunza hivyo wananchi kila mwezi wewe wanapanga ratiba kutembelea hifadhi zetu.
Doreen amesema wazo la kufanya fungate kwenye hifadhi za wanyama alilitoa yeye na mume wake (Mrema) kulikubali haraka kwani hiyo ndio njia mojawapo ya kumuunga mkono rais Samia ambaye amekuwa akisisitiza umuhimu wa wananchi kutembelea hifadhi zetu zilizopo nchini.

Naye Afisa Uhifadhi Utalii wa Hifadhi ya Ziwa Manyara, Renard Twinzi amesema, katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Aprili 2022 hifadhi hiyo imetembelewa na watalii 57,485.

Amesema, hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wa utalii imeweka mikakati ya kuhamasisha utalii wa ndani ili kuweza kufikia malengo ya hifadhi kutembelewa na 100,000 kwa mwaka.
Mrema na mke wake katika ziara hiyo iliyopewa jina la Mr&Mrs Mrema Honeymoon Tour walitembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tarangire, Manyara na Ngorongoro ambazo zimezungukwa na maliasili nyingi nchini.
Share:

KATAMBI AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini akizungumza kwenye futari hiyo.

Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, amewaomba viongozi wa dini mkoani Shinyanga, kuliombea Taifa amani na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassani afya njema ili aendelee kuitumikia nchi na kuleta maendeleo.

Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, alibainisha hayo jana wakati akishiriki futari iliyoiandaa kwa viongozi wa dini ya kiislamu mkoani Shinyanga.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassani ameichukua nchi katika kipindi kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Rais Hayati John Magufuli, hivyo watanzania wanapaswa kumuunga mkono katika majukumu yake ya kuwaletea maendeleo, pamoja na viongozi wa dini kuliombea Taifa amani na Rais Samia kuendelea kuwa na afya njema.

“Nawaomba viongozi wa dini tuendelee kuliombea Taifa letu amani na kumuombea Rais Samia Afya njema ambaye anafanya kazi kubwa ya kutuletea maendeleo na ameichukua hii nchi katika kipindi kigumu, hivyo tumuunge mkono kwa kila hatua ambayo anaipiga,”alisema Katambi.

Naye Naibu Waziri wa Afya Dk, Godwin Mollel, ambaye alishiriki Futari hiyo, alisema mataifa mengi ambayo yameendelea yamemtanguliza mwenyezi Mungu mbele, na kuwaomba watanzania kila jambo wanalolifanya wasimsahau mwenyezi mungu sababu yeye ndiyo ufunguo wa kila kitu.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya, alisema anashukuru viongozi hao kujumuika kula nao futari, huku wakiahidi kuwa wataendelea kuliombea taifa amani na kuuombea Rais Samia Suluhu Hassani aendelea kuwa na afya njema ili awatumikie vizuri.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini akizungumza kwenye Futari hiyo.

Naibu Waziri wa Afya Dk, Godwin Mollel, akizungumza kwenye Futari hiyo.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye Futari hiyo.

Viongozi wa dini wakiwa kwenye Futari hiyo.

Viongozi wakishiriki Futari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akishiriki Futari.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger