Wednesday, 20 April 2022

KAFULILA AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA VYAMA VYA USHIRIKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila akiongea na wadau wa zao la Pamba mkoani Simiyu.

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila ameitaka Taasisi ya Kupambana na Kuziua Rushwa Mkoani humo kuhakikisha wanakamilisha uchunguzi juu vyama vya ushirika ambavyo vilipokea fedha na kuwalipa wakulima ili kujiridhisha kama malipo hayo ni sahihi.

Kafulila ameyasema hayo leo (Aprili 20,2022) kwenye mkutano wa kujadili tathimini ya zao la pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Bariadi Conference na kuwakutanisha wadau wa pamba mkoani humo.

‘’Nataka nione kama Amcos zimewalipa wakulima kulingana na fedha walizopokea toka kwenye makampuni ya ununuzi wa pamba, tusiache jiwe juu ya jiwe, tusiache mtu hata mmoja aliyekula fedha za mkulima’’, amesema Kafulila.


Hata hivyo Kafulila ameshangazwa kuona Taasisi hiyo haijafanya uchunguzi tangu alipotoa maagizo jambo ambalo amesema limesikitisha sana, na kwamba ameitaka TAKUKURU kufanya uchunguzi huo haraka na aipate ripoti hiyo.


Aidha Kafulila amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika bado wanawaibia wakulima kupitia vyama vya ushirika ambapo si lengo la serikali kuwaibia wakulima kupitia ushirika.


‘’Tunataka kuona Mnunuzi hamwibii mkulima, Mkulima anataka bei stahiki na mnunuzi anataka kutoa bei stahiki…’’ amesema Kafulila.

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga amesema mkoa wa Simiyu ndio wazalishaji wakubwa wa pamba nchini na kwamba changamoto nyingi za zao la pamba ziko mkoa wa Simiyu.


Alisema viongozi wa Amcos hawaambii wakulima juu ya mabadiliko ya bei, wanalipwa fedha kidogo wakati makampuni yanatoa bei kubwa kwa wakulima.


‘’kuna genge linagawana fedha za wakulima, ushirika mlitakiwa kufanya vizuri ili wakulima wapate fedha zao, ushirika mnawaibia wakulima ndio maana haiutaki ushirika’’ amesema Mtunga.


Alisema kuna Usimamizi mbovu sana kutoka kwa viongozi wa vyama vya ushirika, ambapo aliwataka kufanya vizuri ili kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.


‘’Msitumie ilani kuharibu mambo ya watu, Ushirika ni Ilani, hata kama mnafanya vibata tung’anga’ane tu na ushirikia…’’ amesema Mtunga.


Gilang’hinda Busiga kutoka Kampuni ya Lugeye kutoka Mwanza, aliomba wafuate mfumo wa Amcos kuajiri wapimaji kulingana na makampuni yaliyofika kwenye Amcos, waajiri wahasibu ili kila kampuni liwe na mlango wake.
Share:

AJALI YA NOAH, LORI YAUA WATU SITA ARUSHA






Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha

Watu sita (06) wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyo husisha gari Toyota Noah kugongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameseama ajali hiyo imetokea tarehe 19.04.2022 muda wa saa nne usiku na  kuyataja magari hayo kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY likitokea Arusha mjini kwenda Karatu  na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva amabapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufamu majina halisi ya abiri waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.

ACP Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ilikupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha
Share:

MKURUGENZI JIJI LA DODOMA ASHIKILIA MSIMAMO WAKE KUHUSU SOKO LA SABASABA

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo Dodoma kuhusu msimamo wa kuwahamisha wafanyabiashara wa soko la Sabasaba kupisha ukarabati wenye lengo la kuboresha soko hilo kuwa la kisasa linalokidhi vigezo vya makao makuu ya nchi.


 Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA.
 
LICHA ya wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba Jijini  kutishia kuandamana hadi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ili kumfikishia kilio chao cha kuondolewa katika eneo hilo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru ameendelea  kuwataka wafanyanishara hao kupisha ukarabati wa soko hilo huku akieleza lengo la serikali ni jema kwa maslahi ya wafanyabaishara hao na siyo vinginevyo.

Hayo yanajiri ikiwa ni hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka kuagiza Jiji la Dodoma kufanya mkakati wa Uboreshaji wa Soko hilo kwa kuwaorodhesha wafanyabiasha wote katika mfumo maalum ili kuweza kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza hapo baadaye.

Akiongea na waandishi wa habari leo Aprili 20, 2022 Ofisini kwake amesema lengo la Jiji ni kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara hao ili kufanya ukarabati wa soko hilo na baada ya ujenzi huo kukamilika watawarudisha kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

"Zoezi hili tunalifanya kwa uwazi,tuliwashirikisha wafanyabiashara wote na kilichobaki sasa ni kuhakiki ili kuwatambua nani anamiliki nini na anafanya nini na kuwaondoa hofu kuwa tunakwenda kuwahamisha kwa muda ili kupisha ujenzi wa eneo hilo kwa muda wa mwaka mmoja au miwili kulingana na mchoro wetu”amesema Mafuru

Aidha amesema soko hilo ni la historia na limechakaa kutokana na kuwa  ni la muda mrefu tangu mwaka 1996 halijafanyiwa ukarabati wa miundominu yake hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha linakarabatiwa kisasa zaidi kulingana na mahitaji na kuweza kuhudumia zaidi ya wafanyabiashara 7000 .
"Lengo la jiji ni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na si kuwadhulumu,imefika wakati wafanyabiashara kuelewa Dodoma Sasa ni Jiji na ndiyo Makao makuu ya nchi na soko la Sabasaba limekuwa halina hadhi lazima tufanye ukarabati,"amefafanua na kuongeza;

Mvua ikinyesha pale Sabasaba watu wanashindwa kufanya shughuli zao kwa utaratibu  tope linakuwa la kutisha na nimekuwa nikipokea  malalamiko mengi kuwa tunachukua ushuru lakini hatufanyi ukarabati”amesema Mafuru

Amesema jiji halina lengo la kuwaonea wafanyabiasahara bali kinachotakiwa ni kuwashirikisha kila hatua ili kuweza kupata uelewa wa pamoja na kila mtu kuridhika na maamuzi hayo.

Hata hivyo amesema malalamiko ambayo wamekuwa wakiyapata yanaonyesha kuwa wafanyabiashara hao hawana imani na jiji katika kutekeleza mpango huo hivyo Kutoa nafasi ya kuwahudumia huku akitoa maelekezo kwa  wapangaji waliojimilikisha zaidi ya kibanda kimoja kuwa  watamiliki kibanda kimoja tu ili kuwapa nafasi watu wengine .

"Kuna baadhi ya wafanyabiashara wamejimilikisha zaidi ya vibanda 20 na kuvipangisha kwa watu wengine kwa bei ya juu niseme wazi kuwa baada ya ukarabati huo Kila mfanyabiashara atakuwa na haki ya kumiliki kibada kimoja ili kila mfanya biashara awe na fursa,"amesema

Naye Afisa biashara wa Jiji la Dodoma Donatila Vedasto amesema lengo la  kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara ni kupisha uboreshaji wa miundombinu na kwamba mpango huo ni wa kitambo lakini haukutekelezwa kwa wakati kutokana na ufinyu wa bajeti uliokuwepo.

Amesema ili kupata kauli moja wanapanga kuendelea na vikao vya kujadilina baina ya jiji na uongozo wa soko hilo ili kupata namna bora ya kufikia mwafaka.

“Kuna watu wanahofu kupoteza vibanda vyao hasa wale wenye maeneo zaidi ya moja lakini ni wahakikishie kuwa kupitia mazungumzo tutafikia mwafaka na hakuna atakaye poteza haki yake waelewe tuu tunafanya uhakiki ili kujilidhisha na idadi ya wafanyabiasahara iliyopo”amesema

Amesema "Soko la sababasa miundombini yake imechakaa na hata ukienda sasa hivi kuko wazi lakini pia hili ni jiji na makao makuu hatuwezi kuwa na soko la aina ile  kama jiji tukasema kuwe na kitu cha kufanya kuboresha soko kama hadhi ya jiji na kuendana na makao makuu ya nchi,

Tukawaza kuweka mkakati kwa maana katika mradi huu tutanza ujenzi mwezi wa saba na  huwezi kuanza bila kuwashirikisha wadau ,vikao vimeanza tangu mwaka jana kuhusiana na changamoto kikubwa miundombinu vikao vya kuanza kujenza tumeanza mwezi wa kwanza wtaalam walikuja tukawashirikisha," amesema Afisa huyo wa Biashara .


 

Share:

Tuesday, 19 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 20,2022


















Share:

NABII Dkt. JOSHUA ASISITIZA RAIS SAMIA NI KIONGOZI HODARI


RAIS wa Umoja wa Mitume na Manabii Tanzania, Nabii Dkt.Joshua Aram Mwantyala amesema katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan madarakani ameonesha uhodari mkubwa ikiwemo kusimamia kikamilifu uendelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoachwa na mtangulizi wake hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.


Kutokana na uhodari huo, Nabii Dkt. Joshua amewatoa shaka waliodhania Mheshimiwa Rais asingeweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ambapo amesisitiza Watanzania wote waendelee kumuunga mkono na kumpa ushirikiano wa dhati.


Sambamba na kumuombea ili azidi kulitumikia taifa kwa ufanisi mkubwa, kwani nafasi hiyo ya Urais anayohudumu amepewa na Mungu na kwamba Mungu ameiangazia njia yake ya uongozi mwanga mzuri wa kuliletea mafanikio makubwa taifa na wananchi kwa ujumla.


Nabii Dkt. Joshua ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania yenye makao yake makuu mjini Morogoro ameyasema hayo leo Aprili 19,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kueleza mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia na mikakati waliyonayo kama mitume na manabii katika kufanikisha juhudi mbalimbali za kuliletea Taifa maendeleo.


Pamoja na mambo mengine, Nabii Dkt.Joshua amebainisha kuwa, Umoja wa Mitume na Nabii nchini utaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kutoa mchango wa maendeleo ya nchi ikiwemo kusaidia ujenzi wa huduma za kijamii kama vituo vya afya na elimu kama ambavyo baadhi ya taasisi za dini zilizotangulia likiwemo Kanisa Katholiki ambalo limefanikiwa kufanya hivyo kwa ufanisi.


Amesema,umoja huo umedhamiria kuchagiza maendeleo ya nchi kupitia ujenzi wa viwanda ambavyo vitasaidia kutoa ajira kwa vijana na kuhamasisha Watanzania wazidi kujituma kufanya kazi mbalimbali halali za maendeleo katika kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.


Nabii Dkt. Joshua pia amesema miongoni mwa majukumu aliyonayo baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mitume na Manabii nchini, ni kuhakikisha anawaunganisha Mitume na Manabii kusudi wawe pamoja na kwamba umoja wao uwe na tija kwa nchi ikiwemo kuhamasisha maadili mema, kuendelea kuliombea Taifa, kufundisha mafundisho ya kiroho kwa kuzingatia kikamilifu misingi ya Neno la Mungu.


Pia, Nabii huyo amewataka Mitume na Manabii nchini, kujiepusha na tabia mbaya ikiwemo kutumia vipawa walivyopewa bure na Mungu kuvitumia kama kitega uchumi na kwamba wazingatie misingi ya Neno la Mungu, kwani vipawa hivyo wamepewa bure, hivyo wavitumie bure.


Huku akiwaonya Mitume na Manabii wenye nia ovu na wanaochafua imani kuacha kufanya hivyo badala yake wasimamie kweli ya Neno la Mungu.


"Msingi wa Biblia tumepewa bure vipawa, vipawa vimetolewa na Mungu tuvitumie bure havina chuo tuvitumie bure. Ni kosa kubwa Mtumishi wa Mungu kuuza kipawa, msingi wa wokovu wetu ni upendo ni vizuri watumishi wa Mungu turithi tabia ya mwanzilishi wa imani yetu Yesu Kristo. Sisi Mitume na Manabii tunajipambanua kwa watu kwa kutoa faraja la suluhisho la matatizo yao na siyo kuleta hofu." amesema Nabii Dkt.Joshua.


Ameongeza kuwa, chombo hicho kitasaidia kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kudumisha amani kwa njia mbalimbali ikiwemo kuelimisha jamii kujiepusha na matendo yote maovu,kabla sheria za nchi hazijafuata mkondo wake.

Share:

KIVULINI YAHAMASISHA WANAUME KUJENGA MAKAZI BORA....YASIN ASEMA 'MSIWEKE HESHIMA BAA NA KUHONGA'

Wanaume katika Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wametakiwa kuacha tabia ya kwenda kuweka heshima baa wakitumia vibaya fedha nyingi na badala yake watumie fursa hiyo kujenga makazi bora na kuishi kwa upendo na wake zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally alitoa rai hiyo Jumapili Aprili 17, 2022 wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' lililofanyika katika Msikiti wa BAKWATA wilayani Kwimba.


"Kuna baadhi ya wanaume msimu wa kilimo wanalima pamoja na wake zao, wakivuna wanapata kuanzia milioni mbili hadi tano kisha wanatokomea na hela kwenda kuweka heshima baa na kuhonga, kuanzia leo heshima ya kwanza iwe kujenga nyumba nzuri",alisema Ally.


"Unakuta mwanaume anatafuta sifa baa, mnadani ama kwenye vijiwe vya mpira wakati nyumbani ni chenga tupu, kaone anapolala utashangaa", alisema Ally akiwasihi baadhi ya wanaume wilayani Kwimba wasiowajibika kwa maendeleo ya familia kubadilika.

Pia aliwasihi wanaume kuishi kwa maelewano na wake zao na kuacha kauli tata zinazochochea migogoro kwenye familia na kusababisha kukosekana kwa malezi bora hususani kwa watoto na matokeo yake linaibuka wimbi la watoto wanaokimbilia mitaani.


Kwa upande wake Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke alisema kukosekana kwa mafunzo kwa vijana kabla ya kuoana ni chanzo cha ndoa nyingi kukosa maelewano na kuvunjika na kusisitiza kuwa suala hilo litapewa kipaumbele.


"Hatuwezi kuwa na jamii ambayo haina mafunzo, tuanzishe mafunzo hata ya siku 14 kwa vijana kabla ya kufunga ndoa, lakini pia wanaofungisha ndoa hizo wahakikishe wanazifuatilia na kuzilea", alisisitiza Sheikh Kabeke.


Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo akiwemo Amina Mussa na Maneno Hassan walisema walitoa rai kwa wanandoa hususani wanaume kurejea misingi ya dini, kuwa na utamaduni wa kusali ili wawe na hofu ya Mwenyezi Mungu jambo litakalosaidia kuishi kwa maelewano na kulea familia pamoja.


Kongamano hilo ni sehemu ya makongamano ya 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa" ambayo yameandaliwa na BAKWATA Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na shirika la KIVULINI yakitarajiwa kufanyika katika Wilaya zote mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha maadili katika jamii ili kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, kulea familia na kuondoa watoto wanaokimbilia mitaani pamoja na kupambana na utoro mashuleni.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wakifuatilia kongamano hilo lililofanyika katika Msikiti wa BAKWATA wilayani Kwimba.
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke akizungumza kwenye kongamano hilo.
Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
BAKWATA kwa kushirikiana na KIVULINI wameandaa makongamano 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' katika Wilaya zote mkoani Mwanza.
Mshiriki wa kongamano hilo, Amina Mussa akichangia hoja kwenye kongamano hilo ambapo aliwasihi wanaume kurejesha upendo kwa wake zao na kulea familia kwani wengi wao upendo umepungua ndiyo maana wanatelekeza familia.

"Tumetelekezewa majukumu ya kulea familia na wanaume" alisema Bi. Fatuma Idrisa wakati akichangia mada kwenye kongamano hilo ambapo aliwasili wanaume kuwa na upendo kwa wake zao ili kulea familia kwa pamoja.
Mshiriki wa kongamano hilo, Maneno Hassan aliwasihi wanawake kuwa na upendo wa dhati kwa waume zao hatua itakayosaidia kuishi kwa amani na furaha akisema "unampa mtaji wa biashara mkeo, siku mtaji wako ukikatika, yeye hawezi kukusaidia, hilo nalo ni tatizo".
Share:

Monday, 18 April 2022

AUAWA KWA KUUMWA NA NYOKA ANAOWAFUGA


Mwanaume mmoja huko nchini Marekani David Riston, ambaye alikutwa amefariki ndani ya nyumba yake imegundulika kuwa alikuwa mfugaji wa nyoka na kifo chake kimesababishwa na kuumwa na nyoka aliokuwa anawafuga.

Uchunguzi wa Polisi umebaini nyoka zaidi ya 120 ndani ya nyumba yake huku mwili wake ukibainika kuwa na sumu kali ya nyoka hao.

Maafisa wa Ofisi ya Mkaguzi wa Matibabu wa Jimbo la Maryland wamethibitisha kwamba David Riston, (49), alikufa kutokana na kuumwa na nyoka.

Polisi walifanya ukaguzi baada ya jirani wa Riston kuonyesha wasiwasi kwamba hakuwa amemuona Riston kwa takriban saa 24.

Baada ya kuukaribia mlango wa mtu huyo, jirani huyo aliona Riston akiwa ameanguka chini.

Maafisa hao walipokuwa wakiendelea kuingia ndani ya nyumba hiyo, zaidi ya nyoka 100 wenye sumu na wasio na sumu wa aina tofauti waligunduliwa kwenye nyumba hiyo.
Share:

MITIHANI YA KITAIFA KUSAHIHISHWA KIDITALI - 2025


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde akifafanua jambo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) wakati akikagua Mfumo wa kidijitali utakaotumika kusahihisha mitihani ya Vyuo vya Ualimu mwaka huu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) akifuatilia kwa makini namna Mfumo wa kidijitali unavyofanya kazi wakati wa ukaguzi wa majaribio ya usahihishaji mitihani kwa kutumia Mfumo huo yaliyofanyika katika ofisi za Baraza la Mitihani Tanzania.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) akifafanua jambo kwa baadhi ya wataalamu waliopo katika majaribio ya usahihishaji mitihani kwa kutumia Mfumo wa Kidijitali ulioandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania.

***********

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Aprili 18 2022 amekagua na kuridhishwa na majaribio ya Mfumo wa Kidijitali wa Usahihishaji Mitihani ya Kitaifa ya Ualimu ulioandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi na kujionea Mfumo huo unavyofanya kazi, Prof. Mkenda amesema kukamilika na kufanya kazi kwa mfumo huo kutasaidia Serikali kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika wakati wa usahihishaji wa mitihani ya kitaifa.

Waziri huyo amesema ameridhishwa pia kuona mafunzo kwa vitendo ya wasahishaji na wakaguzi wakati wa mchakato nzima wa usahihishaji wa mitihani na wahakiki wa ubora wa usahihishaji wake.

"Nimeambiwa Mfumo huu wa usahishaji mitihani ya Ualimu unatarajiwa kuanza rasmi kutumika mwaka huu kwa kusahihisha mitihani ya ualimu ya vyuo vyote na mwakani utaendelea katika hatua nyingiine ya kusahihisha mitihani ya kidato cha sita na tayari waalimu na wakaguzi wameandaliwa na kupatiwa vifaa husika," amesema Waziri Mkenda.

Mkenda amesema mfumo huo ni wa kwanza katika Afrika na umeandaliwa na vijana wa Kitanzania ambao ni wataalamu kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ambapo amesisitiza kwamba lengo la Serikali ni kuiona NECTA inafanya shughuli zake zote kidijitali ifikapo 2025.

Waziri Mkenda ameongezea kuwa kwa kutumia mfumo huo Serikali itaokoa zaidi ya Shilingi bilioni 37 kila mwaka pamoja na kupunguza mlolongo mkubwa wa usahihishaji wa mitihani.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema wametengeneza mfumo huo kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Sita na maelekezo ya Waziri ya kuona namna bora ya kuandaa mifumo ya kijiditali ambayo inaweza kutumika katika kusahihisha mitihani pamoja na shughuli nyingine za Taasisi hiyo.

Dkt. Msonde amesema kuwa wataalamu wa TEHAMA wa Baraza hilo walianza kazi ambayo imeleta matokeo ya kuanzishwa kwa mfumo huo ambayo unafanyiwa majaribio ili uweze kutumika kusahihisha mitihani ya Ualimu mwaka huu.

"Kwa Mfumo huu tunaendelea kufikia azma ya Wizara yetu ya kuwa na mifumo ili kuendesha shughuli zote kidigitali na kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita la kuwa na uchumi wa kidigitali na kwetu sisi tumeamua shughuli zote za mitihani kuwa za kidijitali ifikapo mwaka 2025," amefafanua Dkt. Msonde.
Share:

WASIOJULIKANA WAUA NA KUIBA MAFUTA YA KULA



Polisi katika eneo la Uranga kaunti ya Siaya nchini Kenya, wanachunguza mauaji ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19, baada ya watu wasiojulikana kumvamia dukani na kumuua kisha kuondoka na mafuta ya kula.

Tukio hilo limetokea Jumatano, Aprili 13, 2022, ambapo kwa mujibu wa polisi wameeleza kwamba mwili wa kijana huyo uliokuwa umekatwakatwa vibaya, ulipatikana kando ya barabara, karibu na duka hilo, siku tatu baada ya kuripotiwa kutoweka.

Taarifa zimeeleza kwamba kijana huyo alikuwa amemaliza mtihani wake wa kidato cha nne (KCSE) 2021, akisubiri matokeo.
Share:

BARRICK YADHAMINI KONGAMANO LA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU


Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa makampuni mbalimbali wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa makampuni mbalimbali wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiuliza swali wakati wa wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick
Baadhi ya watendaji waandamizi kutoka makampuni mbalimbali wakisikiliza hoja za wanafunzi wakati wa kongamano la Wanafunzi la AISEC lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya Barrick

***
Kampuni ya Barrick imedhamini na kushiriki maonesho ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliyoandaliwa na taasisi ya AISEC Tanzania, na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kampasi ya Mlimani.

Kupitia maonyesho hayo wanafunzi huweza kujua jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kujifunza, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Mameneja Waandamizi wa Barrick, walishiriki katika maonesho ya kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake sambamba na mpango wake wa ukuzaji wa vipaji kwa wafanyakazi wake.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger