Tuesday, 5 April 2022
Monday, 4 April 2022
CHUKUA SIRI HII KUTOKA KWA KIWANGA
Wananiita Priscilla Kishama na bwanaangu ni mfanyabiashara mashuhuri ambaye ana magari za abiria nyingi mno na kwa siku yeye hutengeza hela nyingi anazoziweka kwa hazina ya benki.
Kwa kweli sisi ni matajiri! Lakini kumbuka kuwa tulipopatana naye alikuwa mtu maskini asiyejiweza; hata chakula cha kila siku ikawa ni ndoto kwetu kwani mara nyingi tungelilala njaa kana kwamba hatuna kisomo chochote. Mimi nimesomea taaluma ya Marketing naye amesomea uhandisi lakini kupata kazi ikawa ni vigumu jambo lililofanya aanze kufanya biashara rejareja mtaani kwetu.
Aling’ang’ana mno kwa miaka tatu bila mafanikio na hadi tukaanza kufikiria kurudi nyumbani mashambani. Hali ilibadilika ikawa hata ngumu zaidi wakati kulipia nyumba tuliokuwa tumekodisha ilikuwa vigumu na mwenyewe akaiweka kufuli.
Tulilala kwa jirani siku hiyo na siku iliyofuata asubuhi tukafunganya virago kurudi kwetu mashamabani. Ilikuwa aibu kubwa! Maisha magumu ilituzonga na kutuandama hadi huko mashaambani hadi wakati rafiki yangu mama Zubedah alipotutembeelea na kutuambia siri ya kuimarisha maisha yetu.
Alitukariria maisha yake yalivyokuwa kwa muda mrefu hadi pale alipomtembelea daktari mmoja mashuhuri wa miti shamba. Alimuita Daktari Kiwanga. Alitupatia nambari ya simu ya daktari huyo kisha akatuambia tumtemtembelee ili atutengeneze na kutufungulia baraka zetu.
Kwa kweli sababu tulikuwa tumefika mwisho ilibidi tuende tumuone mimi na bwanangu na tulipofika kwa Kiwanga alichukuwa mda kidogo sana kutufanyia Spell Casting Services na kisha akaturuhusu turudi nyumbani.
Ajabu, siku hazikuisha tatu bwanaangu alikuwa ameitiwa kazi Nairobi na shirika moja la South Africa. Sasa hivi yeye ndiye mkubwa wao nchini Kenya. Sasa tunaishi maisha mazuri mno kwani mshahara wake ni shilingi za Kenya elfu mia mbili sihirini. Ahsante Kiwanga Doctors.
Kiwanga Doctors wanatatua shida nyingi kama Kupata mpenzi, kurudisha mpenzi, kuongezwa mamlaka kazini, kuleta furaha na amani katika familia nk. Pia wanasaidia kuimarisha nyota yako pamoja na kupata dawa ya mvuto kwa mwanaume au mwanamke.
Siyo lazima usafiri hadi ofisi zao. Ongea nao kwa njia ya simu na utasaidika kwa haraka kama vile watu wengine wanavyopata usaidizi. Kiwanga wanatibu magonjwa sugu kama Kisukari, Pressure kwa kutumia miti shamba na mengineyo. Wasiliana na Kiwanga Doctors kwa nambari +254 769404965 kwa ajili ya kupata huduma.
Pia unaweza pitia mtandao huu www.kiwangdoctors.com au kwa barua pepe yaani Email: kiwangadoctors@gmail.com
KIKAO KAZI NA MAFUNZO WENYEVITI WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA YA WILAYA CHAANZA MKOANI TANGA
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Michael Luena akizungumza katika kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022
Sehemu ya Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wakiwa katika kikao kazi na mafunzo cha wenyeviti hao kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi Benhaji Masoud akiwasilisha mada kwenye kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stella Tullo akizungumza wakati wa kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Zakariyya Kerra akizungumza katika kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Sehemu ya Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wakiwa kwenye kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti hao kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
*****************
Na Mwandishi Wetu, TANGA
Kikao Kazi na Mafunzo kwa Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya nchini kimeanza leo tarehe 4 April 2022 mkoani Tanga.
Kikao hicho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete.
Katika kikao hicho pamoja na uwasilishwaji mada, Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini watapata mafunzo ya namna bora ya kuendesha mashauri ya ardhi pamoja na uandishi mzuri wa hukumu.
Katika siku ya kwanza ya kikao hicho Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Benhaji Masoud aliwasilisha mada kuhusiana na masuala mtambuka katika uendeshaji mashauri ya ardhi.
Kikao hicho cha siku nne kinatarajiwa kumalizika siku ya alhamisi tarehe 7 April 2022.
SIMBA NA RSB BERKANE ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Na Alex Sonna
SIMBA na RSB Berkane zimetinga kibabe hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi katika mechi zao za mwisho Kundi D.
Simba akicheza uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wameichapa US Gendarmerie mabao 4-0 bao la kwanza likifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 63.
Mabao mawili yamefungwa na Chris Mugalu dakika ya 68 na 78 huku bao la nne akijifunga mlinda mlango wa US Gendarmerie Saidu Hamisu baada ya mpira kurudishiwa na beki wake.
Berkane nao wameifunga ASEC Mimosas bao 1-0 likipatikana dakika ya 28 likifungwa na Chadrack Lukombe kwa Mkwaju wa Penalti
Kwa ushindi huo Timu hizo zimemaliza zikiwa na Pointi 10 kila mmoja huku RSB Berkane wakiongoza wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa nafasi ya tatu ikishikwa na ASEC Mimosas Pointi 9 na US Gendarmerie wakimaliza wa mwisho kwa pointi zao 5.
Sunday, 3 April 2022
NIC YADHAMINI MBIO ZA BIMA MARATHON 2022, YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WATANO
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mbio za Bima marathon za kilometa 21 kwa uppande wa wanaume zilizofanyika leo Aprili 03,2022. Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa mbio za Bima marathon za kilometa 21 kwa uppande wa wanaume zilizofanyika leo Aprili 03,2022.Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mbio za Bima marathon za kilometa 21 kwa uppande wa wanawake zilizofanyika leo Aprili 03,2022.Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa mbio za Bima marathon za kilometa 21 kwa uppande wa wanawake zilizofanyika leo Aprili 03,2022.
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika la Bima la Taifa NIC limedhamini mbio za Bima Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam, ambapo NIC iliweza kutoa zawadi kwa washindi wa mbio za Kilomita 21 kwa wanawake na wanaume wa kwanza hadi watano.
Aidha kupitia mbio hizo NIC wametoa elimu ya bima kwa kueleza umuhimu wa kuwa na Bima kama NIC ili kuweza kujilinda na majanga ya moto na mahafa mbalimbali.
Akizungumza katika mbio hizo amesema kuwa ushiriki umekuwa wa kuvutia kwani washiriki wameweza kujiunga na mbio hizo wakitoka katika maeneo mbalimbali nchini na maeneo ya visiwani ambapo miongoni mwa washindi kwenye mbio hizo ametokea visiwani Zanzibar.
Amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mazoezi hasa ya mbio kwani yanasaidia kuuweka mwili vizuri na kujiepusha na maradhi nyemelezi.
PICHA ZAIDI
DKT. MABULA ATAKA USHIRIKISHWAJI UTATUZI MIGOGORO YA MATUMIZI YA ARDHI KATIKA VIJIJI 975
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdlah Ulega mara baada ya kutua na helikopta mkoani Tanga wakati timu ya Mwaziri wa Wizara za Kisekta ilipokwenda kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi ya vijiji 975 katika mkoa huo tarehe 2 April 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiongoza ujumbe wa Mawaziri wenzake wa Wizara za Kisekta baada ya kutua na helikopta mkoani Tanga walipokwenda kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwenye mkoa huo tarehe 2 April 2022.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega akizungumza kwenye kikao na uongozi wa mkoa wa Tanga wakati timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula ilipokwenda mkoani humo kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwenye mkoa huo tarehe 2 April 2022. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde.
Sehemu ya washiriki wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Tanga kuhusu utatuzi utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kilichofanyika mkoani Tanga tarehe 2 April 2022.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi akichangia hoja wakati wa kikoa baina ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Tanga kuhusu utatuzi utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 2 April 2022.
Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow akichangia hoja wakati wa kikoa baina ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Tanga kuhusu utatuzi utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 2 April 2022 (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
**********************
Na Munir Shemweta na Magreth Lyimo, WANMM TANGA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makakzi Dkt Angeline Mbuala ametaka elimu na ushirikishwaji wananchi kupewa kipaumbele wakati wa utekeleza maamuzi ya Baraza la Mawiziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975
Dkt Mabula alisema hayo mkoani Tanga tarehe 02 April 20202 wakati yeye na timu yake ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakitoa mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa viongozi wa mkoa na wilaya katika mkoa huo kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi.
Katika maamuzi yake, Baraza la Mawaziri lilipendekeza vijiji 14 katika mkoa wa Tanga kubaki maeneo ya hifadhi na kufanyiwa marejebisho ya mipaka huku vijiji viwili na mitaa miwili kufanyiwa tathmni kutokana na sehemu kubwa ya maeneo yake kuwa na umuhimu kwa maslahi ya Taifa.
Katika mkoa wa Tanga maeneo yenye mgogoro wa matumizi ya ardhi yanahusisha wananchi na Hifadhi ya Msitu wa Mikoko na Shamba la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo katika Kituo cha TALIRI,
Maeneo mengine ni kwenye Hifadhi za Misitu Chang’andu, Kwani na Gendagenda pamoja na mgogoro katika Pori Tengefu la Mto Umba na ule wa Shamba la Mwele-ASA.
‘’Rai yangu katika utekelezaji maamuzi haya ya Baraza la Mawaziri ni ushirikishwaji ili asitokee mtu akalalamika kaonewa au kafanyaje, jukumu letu kama serikali ni kuhakikisha tunatoa elimu pia ili masuala haya yasijirudie kwa sababu tumekuwa na operesheni mbalimbali ambazo mwisho wa siku utekelezaji au usimamizi wake ubakuwa siyo mzuri sana’’
‘’Kipindi hiki Mhe mama Samia asingependa kuona masuala haya ya migogoro ya matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali yanajirudia ndiyo maana katika Wizara ya Ardhi ametoa fedha nyingi ili kumalizana na migogoro ya ardhi’’.
Hata hivyo, Waziri wa Ardhi alisisitiza suala la uwajibikaji kwa watendaji wa serikali kuanzia mkoa hadi kijiji na kuwataka kila mmoja kusimamia majukumu yake ili masuala ya uvamizi kwenye hifadhi na taasisi za umma yasijirudie.
‘’Tunaporekebisha maeneo haya hatutarajii tena uvunjifu wa sheria uendelee uongozi kuanzia ngazi ya kijiji muwe walinzi wazuri wa maeneo hayo ili kuepuka migogoro hiyo ya wananchi kujimegea maeneo ambayo siyo rasmi kwa makazi’’ alisema Dkt Mabula.
Mawaziri walioko kwenye ziara hiyo mkoani Tanga walielezea hatua na mikakati ya kuchukua wakati wa utekelezaji Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa Migogoro katika vijiji 975.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega alisisitiza suala la watendaji wa serikali kuwa imara wakati wa kusimamia zoezi zima la utekelezaji maamuzi hayo ili kuepuka kupata tabu kwenye utekelezaji.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Hamis Chillo aliwahimiza watendaji wa serikali kuhakikisha wanasimamia na kutunza mazingira hususan kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na kusisitiza utumiaji busara wakati wa utekelezaji maamuzi ya baraza la Mawaziri.
Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo alielezea mikakati ya serikali kupitia wizara yake katika kujikita kwenye uzalishaji mbegu ili kukidhi mahitaji ya nchi na kuepuka uagizaji mbegu kutoka nje ya nchi sambamba na kufanya utafiti katika mashamba yake yaliyovamiwa.
Waziri wa Ardhi Dkt Mabula ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Kisekta aliwaasa wananchi hasa waliotengewa maeneo yaliyowekewa mipango ya matumizi ya ardhi kuwa, serikali haitarajii kuona tena wakiingia maeneo ya hifadhi na vyanzo vya maji yaliyozuiliwa kwa kuwa uvamizi uliofanywa ndiyo uliosababisha migogoro ya matumizi ya ardhi.
‘Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Wizara yake isingependa kuona mambo haya yanajirudia na wale wote ambao mara nyingi wanavamia maeneo na kutarajia serikali kuridhia kuendelea wawepo maeneo hayo, suala hili halitajirudia tena na kinachotakiwa sasa kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa kutii sheria bila shuruti kwani serikali haiwezi kuwa na mazoezi haya kila mwaka.