Monday, 14 February 2022

BENKI KUU TANZANIA (BoT) YAWATAKA WAANDISHI KUWA SEHEMU YA KUVUTIA UWEKEZAJI KUPITIA KALAMU ZAO


Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya akifungua semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo vya habari nchini inayofanyika kwenye tawi la BoT mkoani Mbeya katikati ni Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo na kulia ni Emmanuel Lengwa wa ITV na mtunza muda wa semina hiyo.

.............................................

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatamani wanahabari wawe sehemu ya kuvutia uwekezaji kupitia kalamu zao kwa kuandika habari zinazoibua fursa mbalimbali za kiuchumi, zinazopatikana nchini ili kuvutia wawekezaji na kuinua uchumi wa wananchi na taifa kupitia fedha za kigeni.

Amesema habari zitakazoandikwa zikiainisha fursa mbalimbali zinazoonyesha fursa zinazopatikana katika kilimo cha Parachichi Nyanda za juu Kusini zitahamasisha wakulima wengi kujiingiza kwenye zao hilo na hatimaye kujikwamua kiuchumi na kuisaidia Taifa kupata fedha za kigeni.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya, Dk. Nicholaus Kessy kwa niaba ya Naibu Gavana wa (BoT) nchini, Bernard Kibesse wakati akifungua semina kwa Wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini inayofanyika katika tawi la (BoT) jijini Mbeya.

"Semina hii imejikita kuwafundisha wanahabari kuwa wabobezi wa habari za Uchumi, fedha na biashara kwa sababu wanahabari wakibobea katika eneo hilo wataweza kuandika kwa weledi habari zinazohusu sera mbalimbali za fedha pamoja na kuchambua kupitia vipindi, na makala zinazoeleza majukumu ya benki kuu Tanzania ,” amesema Dk. Kessy.

Ameongeza kuwa wanahabari wanapaswa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana hususani Mikoa ya Nyanda za juu kusini ikiwamo vivutio vya uatlii na kilimo ili kuwavutia wawekezaji na watalii kutembelea Hifadhi za Taifa kama vile Kitulo, Ruaha, Katavi , Ziwa Ngosi na maeneo mengine yenye kuvutia.

Naye, Kaimu Meneja wa Mahusiano na Itifaki kutoka Benki ya Tanzania (BoT), Vicky Msina amesema semina inayotolewa kwa waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha inalenga kuwajengea uwezo kuchambua na kuandika habari kwa weledi zinazohusu majukumu ya benki.

Msina amesema miongoni mwa mambo wanayofundishwa wanahabari ni kutambua matumizi ya lugha za kifedha ili kuwasaidia wanahabari kuandika habari zitakazoeleweka kwa jamii.

“Hii ni semina ya tisa tangu kuanza kwa utaratibu huu, tumeona manufaa makubwa baada ya kuwapatia wanahabari mbalimbali nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayofanywa na Benki kuu ya Tanzania pamoja na masuala mengine yanayohusu biashara na uchumi,” amesema Msina.
Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BoT tawi la Mbeya akifungua semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo vya habari nchini inayofanyika kwenye tawi la BoT mkoani Mbeya katikati ni Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo kushoto ni Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki (BoT) Bi. Vick Msina na kulia ni Emmanuel Lengwa wa ITV na mtunza muda wa semina hiyo
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ili kumkaribisha mgeni rasmi.
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ili kumkaribisha mgeni rasmi kulia ni mgeni rasmi Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya akimsikiliza.
Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki (BoT) Bi. Vick Msina akitoa neno la utangulizi kabla ya mgeni rasmi kufungua semina hiyo kulia ni Dorcas Mtenga Mwenyekiti wa Semina na katikati ni Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BoT.
Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania wakiwa na majukumu mbalimbali ili kufanikisha semina hiyo hapa wakijadiliana jambo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika seminahiyo inayofanyika kwenye tawi la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mbeya.
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza na washiriki wa semina hiyo kabla ya kuanza rasmi kwa semina hiyo.
Picha ya Pamoja
Share:

Sunday, 13 February 2022

ZAMARADI MKETEMA AZUA GUMZO KUTUNDIKA BANGO BARABARANI KUELEZEA HISIA KWA VALENTINE WAKE

Zikiwa zimebaki saa chache tu kuingia Valentine’s day February 14 2022 Mtangazaji/Mjasiriamali @ZamaradiMketema ameingia kwenye trend mitandaoni baada ya kutundika barabarani bango lenye picha ya Mume wake likiwa na maneno ‘acha dunia ijue nakupenda kiasi gani, YOU ARE MY KING, happy Valentine’s day my love…… from your loving Wife”

Baada ya kusambaa kwa picha hii @ayotv_ ilimpigia simu Zamaradi ili kufahamu mengine ambapo amesema bango hili ambalo alianza kuliandaa kwa wiki mbili zilizopita bila Mume wake kufahamu, limewekwa leo February 13 saa kumi na mbili jioni na amelilipia litakaa hapo kwa muda wa mwezi mzima "hii ni barabara ambayo anapenda sana kupita yani kila siku lazima apite ndio maana nimeliweka pale"

"Baada ya kuliweka nilimchukua mpaka pale amefurahi sana, tulipofika pale alicheka sana alafu akaingia kwenye gari machozi yakawa yanamtoka akaanza kulia akawa ameinama kwenye gari akasema kwahiyo Mke wangu umeamua kuniweka hapa juu…… amefurahi sana kwakweli”

“Sasa hivi tuna miaka mitano ya ndoa lakini sita ya mahusiano, nia yangu kumuweka kwenye bango ni jinsi ninavyompenda, ninampenda sana Mume wangu, Mume wangu amekua ni Mtu flani ambae amenifanyia vitu vingi hakuna Mtu ambaye anaweza akajua” ——— Zamaradi.

“He is a special man in mylife nafikiri siku moja naweza kukupa Interview ambayo sijawahi kuitoa popote.... amekua ni Mtu ambae ananipenda sana hata maneno hayawezi kutosha kumuelezea ni Mwanaume wa namna gani kwenye maisha yangu" amemalizia Zamaradi.

 
Share:

MAMA ASHTUKA KUTAMBUA KUWA MUME WAKE NI NDUGU YAKE WALIYEZAA WATOTO WATATU


Domitila alizaliwa mnamo mwaka 1978, lakini mwaka mmoja baadaye mama yake alifariki dunia.

Kisha miaka michache baadaye alimpoteza baba yake na hivyo alikuwa na ndugu wengi ambao walikulia katika familia tofauti.

Katu hakuwa anamfahamu kaka yake japo jamaa zake walikuwa wakimuarifu kwamba ana kaka.


Baada ya miaka mingi, Domitila alianza kufanya kazi kama kijakazi na siku moja alikutana na kaka yake jijini Kigali, Rwanda, lakini hawakujua wao ni watu wa damu moja.

Jane Mugo: Kizaazaa Kortini Huku Mpelelezi Binafsi Akiangua Kilio, Adai Watekaji Nyara Walikuwa Wakimfuata
Waoana
Ndugu hao walipendana sana na kisha walioana na kujaliwa watoto watatu.

Baadaye waligundua kwamba wao ni ndugu wa damu moja waliotoka tumbo moja na baba yao ni mmoja.

Taarifa hiyo ilimdunisha Domitila na kumfanya kujidharau sana akijifungia akijificha kukutana na watu.

"Nilichanganyikiwa na kuanza kujificha kwa watu. Niliacha hata kuchota maji..." alisema katika mahojiano na AfriMax.

Domitila alisema watu walikuwa wamdhihaki pamoja na wanawe wakisema walizaliwa na damu moja na hivyo kumlazimu kutengana na kaka yake.

Mama huyo anaishi katika nyumba mbovu ambayo haijamalizwa kujengwa na hapokei msaada wowote kutoka kwa baba ya watoto wake.

Kifungua mimba wa Domitilia na mwanawe wa pili wana matatizo tofauti za kiafya.

Domitila alisema ni miaka mitano sasa tangu atengane na kaka yake ambaye hataki kujihusisha na wanao.

Anawaomba wasamaria mema kumsaidia kujenga nyumba mpya kwa ajili ya familia yake na kuwapeleka watoto wake shuleni.

Jamaa ashtuka kutambua anachumbiana na mke wa kakake
Jamaa Atekwa Nyara Dakika Chache Baada ya Kuondolewa Gerezani Wajir

Katika kisa sawia na hicho, TUKO.co.ke, iliripotia kumhusu mwanamume Mkenya mwenye miaka 36, ambaye alishtuka kutambua amekuwa katika mahusiano ya mapenzi mke wa kaka yake mdogo.


Katika mahojiano ya kipekee na mhariri wa mahusiano wa TUKO.co.ke, Gitau alifichua kwamba amekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitatu na ana hisia ya mapenzi kwa wanawake na wanaume ingawa mkewe hajui.

Baba huyo wa watoto wawili alifichua kwamba alikutana na mpenzi wake wa jinsia moja kwenye programu ya uchumba ya Tinder mnamo 2020 na alishtuka kugundua alikuwa ni mke wa kaka yake wakati wa hafla ya familia.
Share:

WATUMISHI MSAJILI WA HAZINA WABORESHA AFYA KWA MICHEZO


Michael Mzoo (wa kwanza kulia) akiwaongoza Watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea (Kushoto) akifurahia ushindi pamoja na washindi wa Mpira wa Mguu wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea (Kushoto) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili wa mbio fupi upande wa wanawake kwa Neema Matagi wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea (Kushoto) akikabidhi tuzo ya mshindi wa mbio fupi upande wa wanaume kwa Felix Ngoi, wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea (Kulia) akipokea tuzo kama shukrani kutoka kwa Irene Minja (Kushoto) akiwakilisha watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea (Kushoto) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili katika mbio za magunia upande wa wanawake kwa Avelina Rwilemera, wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea (Kushoto) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili katika mbio za magunia upande wa wanaume kwa Peter Maungo, wakati wa Bonanza Maalumu la Michezo lililofanyika jana katika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)

*********************

Na Mwandishi Maalumu

KATIKA kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na afya bora na kuboresha mahusiano mahali pa kazi, Ofisi ya Msajili wa Hazina jana ilifanya Bonanza kubwa kwa ajili ya watumishi wake lililofanyika Viwanja vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Jijini Dar es Salaam.

Zaidi ya wanamichezo 100 walifurahia Bonanza hilo lililoshirikisha mazoezi ya viungo, mpira wa miguu, kuvuta kamba, riadha, mbio za magunia na kukimbiza kuku.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha bonanza hilo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Pili Mazowea aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto, alisema lengo kuu la Bonanza hilo ni kuimarisha afya ya watumishi na kuboresha mahusiano mahali pa kazi.

Aliongeza kuwa, afya ikiwa nzuri kwa watumishi hata utendaji kazi unakuwa mzuri, hivyo amewasihi kushiriki michezo mara kwa mara ili kuimarisha afya.

Aliwapongeza pia watumishi walioshiriki katika bonanza hilo kwa kujitokeza kwa wingi, akiamini watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine katika kutunza afya zao kupitia michezo.

Washindi wa michezo mbalimbali walizawadiwa vikombe huku washiriki wakitunukiwa medali.

Hilo lilikuwa bonanza la pili kwa watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina kufanyika kati ya mwaka jana na mwaka huu na kwanza aina hiyo ya kusanyiko la kimichezo litakuwa endelevu.

Share:

WAFANYAKAZI WA AZAM MEDIA WAPATA AJALI KITONGA


Watu kadhaa wakiwemo wafanyakazi 12 wa kampuni ya Azam Media wamejeruhiwa baada ya gari la kampuni hilo walilokuwa wakisafiria kutokea mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam, lenye namba za usajili T735DHQ aina ya Toyota Hiace kugongwa na lori lililopata hitilafu katika mfumo wa breki, tukio lililotokea leo Februari 13, 2022 katika eneo la Kitonga mkoani Iringa.

Taarifa iliyotolewa na Kampuni ya Azam Media, imeeleza kwamba wafanyakazi wake hao, walikuwa wakitokea mkoani Mbeya walikoenda kwa ajili ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya NBC na kwamba, wamesaidiwa na Jeshi la Polisi na wasamaria wema na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, lori hilo lilipata hitilafu katika mfumo wa breki na kuanza kurudi nyuma kwa kasi na ndipo lilipoligonga gari hilo la Azam lililokuwa nyuma yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa jeshi la polisi lipo eneo la tukio kwa ajili ya kuwasaidia wote waliopata majeraha na kueleza kwamba taarifa kamili itatolewa baadaye.

Share:

MISA - TANZANIA YAKUTANA NA WABUNGE VINARA NA MARAFIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUJADILI SHERIA ZA HABARI


Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) imeendesha warsha kwa wabunge vinara na marafiki wa vyombo vya habari Pamoja na asasi mbalimbali za kiraia kujadili baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye sheria za habari.

Akifungua warsha hiyo ya kuwajengea uwezo makundi hayo iliyofanyika jijini Dodoma, Mwenyekiti wa MISA -TANZANIA Bi. Salome Kitomari amesema dhumuni kubwa la warsha hiyo ni kuwashirikisha wabunge na wadau wa Habari mambo mbalimbali ambayo yapo katika sheria za Habari na yanachangia kudidimiza uhuru wa kujieleza.

“Tumewaita baadhi ya Wabunge wetu vinara kuwashirikisha kile ambacho waandishi wamekuwa wanakilalamikia mara kwa mara hivyo panapotokea mapitio ya sheria wawe na uzoefu na waweze kuona madhara ya baadhi ya vifungu vya sheria katika tasnia ya Habari.” amesema Kitomari.

Kwa upande wake Halima Mdee (Viti Maalum- CHADEMA) amesema kuna baadhi ya sheria zinaminya uhuru wa vyombo vya Habari kutekeleza majukumu yao kwa kile kinachoitwa ‘maslahi ya umma’

Mdee amesema tafsiri ya maslahi ya umma katika mambo mbalimbali yanayotokea nchini haipo wazi kwani upande wa utawala unaweza ukawa na tafsiri tofauti na kile ambacho wananchi wanachokitarajia.

“Habari yenye maslahi na umma ni lazima iandikwe bila kuwekea vigezo vyovyote vile,jambo lenye maslahi ya umma lazima ujue jambo hilo sio kulificha ficha.” Amebainisha Mdee huku akiomba vyombo vya Habari vinavyotambulika kama vya umma kutoa taarifa kwa maslahi ya umma na sio kutoa muda mwingi kwa watawala tu.

Naye mbunge wa Momba(CCM),Condester Sichwale aliwataka waandishi wa Habari kuandika Habari kwa weledi ili kuaminika katika jamii,na pia ameshauri vyombo vya Habari kujikita katika kutafuta suluhisho kwa matatizo ya yanayokabili jamii.” ameeeleza Sichwale.

“Tunaomba mjitahidi kusimamia maadili na miongozo inayosimamia tasnia yenu,kuna baadhi ya mambo yanakuzwa na vyombo vya habari bila sababu ya msingi na wakati mwingine Habari hizo zinaenda kupotosha jamii”, amesema

Akizungumza kwa niaba ya wabunge hao, Mbunge wa Mlalo (CCM) Rashidi Shangazi amesema kuna umuhimu wa kuanzishwa baraza la walaji wa Habari ili wao kama watumiaji wa Habari wawe na jukwaa la kufikisha maoni yao kuhusu muenendo wa tasnia hiyo.

“Kama walaji wengine wana mabaraza yao na sisi walaji wa Habari ni bora tukafikiria kuanzisha jukwaa letu ili inapobidi tuwaambie kwamba mnachotulisha siyo tunachohitaji.”alisisitiza Shangazi.

Shangazi pia aliishukuru MISA TAN kwa kuwajengea uwezo kundi hilo la wabunge na kuwashauri kuendelea na semina hizo kwa kamati mbalimbali za bunge ili kuwaonesha namna baadhi ya vifungu vya sheria zinazopitishwa bungeni zinavyaathiri uhuru wa tasnia ya Habari nchini.

Semina hiyo iliongozwa na Wahariri Waandamizi Jesse Kwayu na Neville Meena ambao waliwapitisha washiriki katika vifungu mbalimbali vya sheria ikiwemo Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari, 2016.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARI 13,2022





 
Share:

CHELSEA FC YACHUKUA KOMBE LA DUNIA NGAZI YA VILABU



Na Emmanuel Mbatilo 

KLABU ya Chelsea imeibuka Mabingwa wa Kombe la Dunia ngazi ya klabu mara baada ya kuichapa Palmeiras ya nchini Brazili kwa mabao 2-1 katika dakika 30 za nyongeza.

Chelsea ilianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Romelu Lukaku akipokea krosi kutoka kwa Hudson Odoi dakika ya 54 ya mchezo.

Dakika ya 64 ya mchezo Thiago Silva beki wa Chelsea aliunawa mpira ndani ya kumi nane akijaribu kuokoa mashambulizi kutoka kwa Palmeiras na kuamuliwa penati ambayo ilikwenda kupigwa na Raphael Veiga na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika 90.

Dakika 30 zilivyoongezwa Chelsea ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji na dakika ya 116 mchezaji wa Palmeiras Luan Garcia nae akanawa mpira na kuamuliwa penati ambayo ilikwenda kupigwa na Kai Harvert na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger