Monday, 8 November 2021

JIPATIE BIDHAA ZA JAMBO!! LADHA NI NYINGI - CHAGUO NI LAKO! TAZAMA HAPA


Kampuni ya JAMBO FOOD PRODUCTS ya Mjini Shinyanga inayozalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo Juisi, Soda, Maji, Ice Cream, Pipi, Biskuti, Mikate.

Bidhaa hizi zina Ladha ni nyingi, chaguo ni lako.

Jipatie Ubora wako kwa bei ya mwananchi!!

Kama unahitaji kuwa Wakala wa Bidhaa hizi za Jambo Piga simu namba 0622666692 au 0622666693



Share:

ALL SET FOR THE SURVEY ON IMPROVEMENT OF URBAN TRANSPORT(COMMUTER RAILWAYS) IN DAR


******************** 

Dar es Salaam. Data collection survey on improvement of urban transport utilizing conventional railways in Dar es Salaam will begin soon as the Japan International Cooperation Agency (JICA), Ministry of Works and Transport and Tanzania Railways Corporation (TRC) organized a kick-off meeting to discuss the implementation plan. 

The four-month study that ends in February 2022, will examine the existing commuter railways in Dar es Salaam (Pugu line and Ubungo line) and proposing measures to improve them, according to the first meeting conducted on November 4, 2021 in Dar es Salaam. 

The meeting of 18 participants from JICA Tanzania Office, the Mistry of Works and Transport, TRC and Consultants from Japan and Tanzania proposed an improvement plan on tracking, signaling, rolling stock, stations, station plaza and transportation planning to the existing commuter train lines. 

The formulated study team will also discuss with Tanzanian government officials to revise the Dar es Salaam Urban Transport Master Plan supported by JICA in 2018. The Master Plan projects Dar es Salaam to hit more than 10million of population as early as 2030, suggesting that road transport alone will not be able to provide safe and reliable mode of transportation due to worse congestion and lengthy travel time within the city. 

The meeting recommended improvements to the existing railways system for the well-planned and balanced transport development. 

Further discussion meetings will be held, whenever necessary, until the completion of the survey in 2022. 

Japan International Cooperation Agency (JICA) has been supporting transport sector for over 40 years.
Share:

TRAFIKI APIGWA NGUMI NA MHUNI AKIONGOZA MAGARI KWENYE FOLENI, APASULIWA USO

Afisa wa polisi wa trafiki anauguza majeraha kwenye uso wake baada ya kushambuliwa na raia alipokuwa kazini.

Kisa hicho kimefanyika Jumapili Novemba 7,2021 katika mzunguko wa magari eneo la Kariokor jijini Nairobi nchini Kenya ambapo Afisa huyo alikuwa akisaidia kuelekeza magari wakati jamaa mmoja aliibuka ghafla na kumtwanga ngumi usoni.

Kutokana na ngumi hiyo nzito aliyopigwa na mhuni huyo, Askari poli alishikwa na kizunguzungu na kuanguka huku akivunja damu na ndipo Msamaria Mwema akamkimbiza hospitali

Kwa mujibu wa DCI, afisa huyo alikuwa katika mzunguko wa Kariokor jijini Nairobi wakati kisa hicho kilifanyika.

Taarifa ya DCI ilisema afisa huyo alikuwa akisaidia kufungua foleni/ msongamano wa magari kabla ya jamaa huyo kuibuka ghafla na kumuangushia ngumi nzito.

"Afisa huyo alikuwa akisaidia kuelekeza magari katika mzunguko wa Kariokor wakati mwanaume huyo alimshambulia kwa kumpiga ngumi na kisha kutoweka huku akimwacha afisa huyo amepasuka usoni karibu na jicho," DCI walisema.

Msamaria mwema aliyeshuhudia kisa hicho alimkimbiza afisa huyo hospitalini ambapo alipokea matibabu na kuruhusiwa kuondoka.

Ni kisa ambacho kiliwaacha madereva katika mzunguko huo kwa mshangao huku msongamano mkubwa wa magari ukishuhudiwa. Makachero wa DCI wanaendelea kuchunguza kisa hicho ili aliyetekeleza uvamizi huo kukamatwa.

Yeyote aliye na habari ametakiwa kusaidia makachero kumtia mbaroni mhuni huyo ili ashtakiwe kwa kosa hilo.


Chanzo - Tuko News
Share:

GGML YAENDELEZA UDHAMINI WA UPASUAJI MIDOMO SUNGURA


Meneja wa Afya, usalama na mazingira kutoka GGML, Dk. Kiva Mvungi akiwa amembeba mtoto anayetarajiwa kufanyiwa upasuaji wa midomo sungura.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo akiwa kambeba mtoto anayejiandaa kupata huduma ya upasuaji wa mdomo sungura inayofadhiliwa na GGML kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo (kulia) akisalimiana na wazazi na walezi wa wagonjwa wa mdomo sungura (kushoto) ambao wanatarajiwa kupata matibabu katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza.
**

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission ya Australia kwa mara nyingine mwaka huu imeendeleza udhamini wake wa kusaidia kugharamia upasuaji na matibabu ya wagonjwa 25 wa midomo Sungura katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza mwezi huu.

Msaada huu umekuwa ukitolewa kwa zaidi ya muongo mmoja sasa tangu mwaka 2002 ukitoa matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 1,717 wakiwemo watoto na watu wazima kutoka maeneo yanayozunguka mgodi.

Tatizo la midomo Sungura ni changamoto ya kidunia na bahati mbaya ni tatizo linalowakumba zaidi watoto kuzunguka eneo la Ziwa Victoria ambapo kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) inapatikana.

Chanzo cha midomo sungura hakijulikani lakini inasemekana ni matokeo ya jeni na sababu za kimazingira.

Akizungumzia udhamini huo jana mjini Geita kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Meneja Mwandamizi anayeshughulikia Afya, usalama, mazingira na mafunzo, Dk. Kiva Mvungi amesema GGML inatoa udhamini huu ili kurejesha matumaini na tabasamu kwa watoto na watu wazima.

Amesema udhamini huo utagharimia matibabu, malazi na usafiri katika kipindi chote ambacho watapatiwa matibabu hayo kwenye Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza.

“Udhamini huu unaendana na tunu na ahadi za kampuni hiyo ambapo afya ni kipaumbele cha kwanza cha kusaidia jamii inayozunguka mgodi,’ amesema.

Dk. Mvungi ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 17 ambayo GGML imegharimia matibabu hayo, wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji wamepata matumaini mapya na maisha yao yamekuwa tofauti kabisa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amesema kutoa ufadhili huo wa matibabu ya upasuaji wa midomo sungura kwa wagonjwa hao uliofanywa na GGML kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission, ni mwendelezo wa GGML kusaidia sekta ya afya katika wilaya hiyo na wananchi.

Shimo amewapongeza wananchi waliojitokeza hadharani kuleta watoto wao kufanyiwa upasuaji na kuachana na imani potofu za kuwaficha ndani ya nyumba na kuendelea kupata matatizo bila kutibiwa.

Amewataka wananchi kuachana na tabia ya kuficha walemavu ndani hasa watoto badala yake wajitokeze kwa ajili kutibiwa kama watu hao 25 waliojitokeza na kupata ufadhili wa matibabu kutoka mgodi wa GGML kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho ya midomo yao.

GGML imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo mkoani Geita. Kwa kushirikiana na Serikali imefanikiwa kuwekeza kiasi cha fedha za kitanzania bilioni 50 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo ya afya, elimu na miundombinu.

Kampuni ya GGML pia imelipa zaidi ya trilioni 3.9 za kitanzania kama kodi serikalini tangu kuanza shughuli zake Mwaka 2000.
Mbali na kodi na fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii,kampuni pia inao mpango wa kusaidia fursa za kukuza uchumi kwa wafanyabiashara wazawa ambapo kampuni hiyo imetumia jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 67.6 katika manunuzi ya bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni za kitanzania mwishoni mwa mwezi Septemba 2021.

Katika kuendeleza biashara za kitanzania kwenye mnyororo wa thamani ndani ya mgodi, kampuni ya GGML imeshirikiana na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) na kuwajengea uwezo wafanyabiashara zaidi ya 350 kutoka Geita kwa kuwapatia mafunzo na ujuzi mbalimbali.

Mapema mwaka huu, kampuni ya GGML iliibuka mshindi wa jumla katika kampuni zinazofanya vizuri kwenye sekta ya madini nchini Tanzania kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 baada ya kunyakua tuzo katika vipengele vya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, mazingira,usalama, mlipaji bora wa mapato (kodi) na uendelezaji wazawa.
Share:

Accoun Accounts at TANROADS

Accounts Assistant (3 Posts)   Ref. No. AB.322/267/01/02 The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) is an Agency under the Ministry of Works and Transport which is responsible for the Development and Maintenance of the Trunk and Regional Roads Network in Tanzania Mainland. Apart from this, it is also responsible in conducting Axle Load Control Operations using […]

This post Accoun Accounts at TANROADS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Office Assistant at TANROADS

Office Assistant    Ref. No. AB.322/267/01/02 The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) is an Agency under the Ministry of Works and Transport which is responsible for the Development and Maintenance of the Trunk and Regional Roads Network in Tanzania Mainland. Apart from this, it is also responsible in conducting Axle Load Control Operations using Weighbridges. […]

This post Office Assistant at TANROADS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Laboratory Assistant at TANROADS

Laboratory Assistant     Ref. No. AB.322/267/01/02 The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) is an Agency under the Ministry of Works and Transport which is responsible for the Development and Maintenance of the Trunk and Regional Roads Network in Tanzania Mainland. Apart from this, it is also responsible in conducting Axle Load Control Operations using Weighbridges. […]

This post Laboratory Assistant at TANROADS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

MAMA MZAZI WA HAMZA AFARIKI DUNIA




Mama mzazi wa kijana Hamza Mohammed aliyeshambulia na kuua askari wanne kwa risasi kabla ya yeye kuuawa kwa kupigwa katika maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa, Bi. Sofia Hassan Askari amefariki dunia.

Bi. Sofia amefariki jana Jumapili, Novemba 7, 2021 na anatarajia kuzikwa kesho saa 7 mchana kwa mujibu wa taarifa za kifamilia.

Jina la Askari ni la utani ambalo alipewa kutokana na mume wake kuwa askari (miaka ya nyuma) wakati akiishi katika maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam.

Share:

HAWA NDIYO WASHINDI NBC DODOMA MARATHON, MILIONI 200 ZAKUSANYWA KUPAMBANA NA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI


Mshindi wa kwanza mbio za km 42 wanaume NBC Dodoma Marathon Mtanzania Tumaini Habie akiiibuka akimaliza mbio hizo baada ya kutumia muda wa saa 02:17:15.
*****
Mbio za hisani za kimataifa zilizoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) “NBC Dodoma Marathon” zimefanikiwa kukusanya fedha zaidi ya Mil 200 kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama huku ikishuhudiwa wanariadha kutoka Tanzania wakifanya vizuri zaidi kwenye mashindano hayo kwa kuibuka vinara kwenye mbio za km 42 na km 21.

Katika mbio hizo zilizofanyika jijini Dodoma  na kupambwa na uwepo wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ilishuhudiwa Mwanariadha Mtanzania Tumaini Habie akiiibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za KM 42 upande wa wanaume baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:17:15, akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya Eyanae Paul aliyetumia muda wa saa 02:18:31.

Mtanzania Abrahamu Too alimaliza katika nafasi ya tatu kwa kutumia muda wa saa 02:19:04

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza katika mbio za km 42 ni Mkenya Cheruto Isgah aliyetumia muda wa saa 02:45:03 akifuatiwa na Watanzania Jackline Sakilu na Sara Ramadhani waliotumia muda wa saa 02:45:46 na 02:46:13 kila mmoja.

Mwariadha wa Kimataifa kutoka Tanzania Alphonce Simbu aliibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za KM 21 hizo baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:03:46, akifuatiwa na watanzania wengine katika nafasi ya pili na ya tatu ambao ni Joseph Panga pamoja na Daniel Giniki waliotumia muda wa saa 01:04:18 na 01:05:37 kila mmoja.

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza katika mbio za km 21 ni Mtanzania Failuna Abdi aliyetumia muda wa saa 01:14:50 akifuatiwa na Wakenya Lelei Jepkemboi na Tanui Euliter waliotumia waliotumia muda wa saa 01:15:18 na 01:17:21

Katika mbio hizo ilishuhudiwa mshindi wa kwanza wa kilometa 42 kwa wanaume na wanawake kila mmoja akiondoka na Sh milioni 5.5 huku upande wa kilometa 21, mshindi akiondoka na kitita cha Sh milioni 3.5, wakati katika kilometa 10, mshindi alipewa Sh milioni 1.5 na mshindi wa kilometa tano alipewa Sh milioni 1.

Akikabidhi hundi ya mchango huo yenye thamani ya sh mil 200 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk. Julius Mwaiselage pamoja na zawadi kwa washindi wa mbio hizo, Waziri Bashungwa pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa kuandaa vema mbio hizo alisema licha ya faida nyingine za kimichezo umuhimu wa mbio hizo unapimwa zaidi katika lengo lake la kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kina mama.

“Tangu kuanzishwa kwa mbio hizi huu ukiwa ni msimu wa pili sasa, serikali imekuwa mstari wa mbele kuziunga mkono kutokana na dhima yake kuu ya kuwasaidia kina mama dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi. Tunashukuru kuona nia hiyo imefanikiwa na sasa tunakwenda kuokoa maisha ya maelfu ya kina mama kupitia jitihada za kimichezo.’’ Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi aliwashukuru washiriki pamoja na wadhamini wa mbio hizo kwa kufanikisha lengo kuu la mbio hizo la kuchangia huduma za afya katika Hospitali ya Ocean Road, hasusani matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi, ambayo ndiyo inayoongoza kwa vifo vitokanavyo na saratani nchini.

Alisema kupitia mbio hizo mwaka jana waliweza kukusanya fedha kiasi cha sh mil 100 kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo na mwaka huu lengo lilikuwa ni kukusanya kiasi cha sh mil 200 zilizopatikana kupitia usajili wa washiriki wa mbio hizo pamoja na michango mbalimbali kutoka kwa wadhamini wa mbio hizo.

“Ndio maana pamoja na yote tunatumia fursa hii kujipongeza sisi sote tukiwemo waandaaji, washiriki pamoja na wadhamini wetu kwa kufanikisha lengo hili muhimu. Pamoja na kwamba tumepata washindi wa mbio hizi lakini bado kila mshiriki ni mshindi kwasababu amefanikisha kuokoa maisha ya mama zetu,’’ alisema.

Akipokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk. Julius Mwaiselage aliishukuru benki hiyo kwa jitihada hizo huku akibaisha kuwa msaada huo unakwenda kusaidia mapambano hayo katika maeneo mbalimbali hususani mikoani ili kuwahi matibabu kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakifika hospitalini wakiwa katika hatua ya mwisho ya ugonjwa huo.

Awali akizungumzia matokeo hayo Rais wa Shirikisho la Riadha Taifa (RT) Bw Silas Isangi alisema kufanya vizuri kwa watanzania katika mbio mbalimbali hapa nchini ni kutokana na maandalizi mazuri yanayofanywa na wanariadha hao huku akibainisha kuwa huo ni mwanzo tu kwa kuwa matokeo hayo mazuri ya watanzania yanatarajiwa hadi kimataifa.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (wa tatu kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya Tsh mil 200 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk. Julius Mwaiselage ikiwa ni mchangp wa mbio za NBC Dodoma Marathon ili kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa uzazi kwa kina mama. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tano kushoto)


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi wa mbio za Km 21wanawake katika mbio za NBC Dodoma Marathon Failuna Abdi (Kulia) zilizofanyika hii leo jijini Dodoma.



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi wa mbio za Km 21 wanaume katika mbio za NBC Dodoma Marathon Alphonce Simbu (Kulia) zilizofanyika hii leo jijini Dodoma. Kulia ni mshindi wa tatu wa mbio hizo Daniel Giniki kutoka Tanzania.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (wa tatu kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi wa mbio za Km 21 katika mbio za NBC Dodoma Marathon Alphonce Simbu (wa pili Kulia) zilizofanyika hii leo jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbasi (Kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kulia) Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (wa pili kulia) na Rais wa Shirikisho la Riadha Taifa (RT) Bw Silas Isangi (Kulia)




Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (kulia) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa mmoja wa washindi wa mbio za walemavu katika mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika hii leo jijini Dodoma.






Tupo tayari kuanza mbio!




Washiriki wa mbio za NBC Dodoma Marathon wakipoza miili yao kwenye moja ya kituo cha maji wakati wakiendelea na mbio zao.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mbio za NBC Dodoma Marathon wakiwemo wadhamini wa mbio hizo


Baada ya mbio washiriki walipata fursa ya kujipumzisha, kufahamiana na kubadilishana mawazo wakati wakisubiri zawadi zao.


Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakiendelea na mashindano


Mmoja wa washiriki wa mbio hizo upande wa walemavu akiendelea na mashindano.


Msemaji wa Benki ya NBC Bw William Kallaghe akitoa neno la shukrani kwa washiriki na wadhamini wa mbio hizo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi akiwashukuru washiriki pamoja na wadhamini wa mbio hizo kwa kufanikisha lengo kuu la kuchangia huduma za afya katika Hospitali ya Ocean Road, hasusani matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi, ambayo ndiyo inayoongoza kwa vifo vitokanavyo na saratani nchini.

Mwariadha wa Kimataifa kutoka Tanzania Alphonce Simbu aliibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za KM 21 wanaume NBC Dodoma Marathon baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:03:46
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger