Sunday, 7 November 2021

RC HOMERA ASHIRIKI MAKABIDHIANO YA TREKTA NDOGO 24I KWA WAKULIMA MBARALI - MBEYA


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera hivi karibuni akiwa mgeni rasmi amekabidhi Trekta ndogo (Powertillers) aina ya Kubota 241 zenye thamani ya Tshs. 2.6 Billion, vifaa hivyo vimetolewa na kampuni ya Agricom Africa Kwa udhamini wa mkopo kupitia CRDB Bank kwa wakulima wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matrekta yaliyotolewa na Agricom Africa ltd Kwa udhamini wa mkopo kupitia CRDB Bank Ltd
Mtendaji Mkuu wa Agricom Africa Ltd Bw. Alex Duffar akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matrekta yaliyotolewa na Agricom Africa ltd kupitia udhamini wa mkopo wa CRDB Bank
Mwakilishi wa Meneja wa kanda WA Benki ya CRDB nyanda za juu kusini akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matrekta yaliyotolewa na Agricom Africa ltd kupitia udhamini wa mkopo wa CRDB Bank Igurusi mbeya
Mkuu wa mkoa akiwasha mojawapo ya trekta
Picha ya pamoja Kati ya mkuu wa mkoa wa Mbeya na wakulima waliokabidhiwa trekta ndogo aina ya Kubota Powertillers

Mkuu wa mkoa wa Mbeya,mwakilishi wa Meneja wa kanda WA Benki ya CRDB na Mtendaji Mkuu wa AGRICOM AFRICA LTD wakiwa na funguo kama ishara ya makabidhiano ya matrekta yaliyotolewa na Agricom Africa ltd kupitia udhamini wa mkopo wa CRDB Bank.
Mtendaji Mkuu wa AGRICOM AFRICA LTD akifurahia picha ya pamoja na wakulima waliokabidhiwa trekta ndogo aina ya Kubota Powertillers kwenye ofisi za Agricom Africa ltd Igurusi
Wakulima waliokabidhiwa trekta ndogo aina ya Kubota Powertillers
Share:

Uanzishwaji Holela Wa Masoko Na Minada Ya Mazao Ya Mifugo Na Uvuvi Wapigwa Marufuku


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amepiga marufuku uanzishwaji holela wa masoko na minada ya  mazao ya mifugo na uvuvi ambapo amesema masoko na minada hiyo inatumiwa na wafanyabiashara  kukwepa kulipa kodi ya Serikali.

Ndaki ameyasema hayo jana (06.11.2021) wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya makusanyo ya maduhuli ya sekta ya Uvuvi kutoka kwa Maafisa wafawidhi wa vituo vya ulinzi wa rasilimali za uvuvi  nchini kilichofanyika kwenye hoteli ya Morena jijini Dodoma.

“Kiutaratibu ni lazima tukague na tusajili masoko na minada yote hapa nchini lakini Kuna watu wanajianzishia tu masoko kule halafu analiita soko lake la kimataifa, hapana hatuwezi kuendelea na hiyo habari ni lazima sheria na taratibu zifuatwe” Ameongeza Ndaki.

Ndaki amemuelekeza katibu Mkuu wa wizara hiyo anayesimamia sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah kupitia upya masoko yote ya mazao ya uvuvi yaliyopo hapa nchini na kujiridhisha kama yanastahili kusajiliwa nay ale ambayo hayastahili yafutwe mara moja.

“Kinachosikitisha ni kwamba, huko wanakoanzisha haya masoko na minada hakuna wataalam wetu hivyo kila mtu anaenda sokoni na kuchukua anachotaka bila kufuata utaratibu wowote ule, hatuwezi kuwa na serikali ya namna hiyo na Mhe. Rais hatotuelewa ikiwa kila mahala tutakuwa na masoko na minada inayoendesha shughuli zake kiholela” Amesisitiza Ndaki.

Wakati huo huo Ndaki amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  anayesimamia sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah kuwaandikia barua ya onyo maafisa wafawidhi wa vituo vyote vilivyokusanya maduhuli chini ya asilimia 50 ya lengo walilowekewa ambapo amesema kuwa hatua zaidi dhidi ya maafisa hao zitachukuliwa endapo hawatoongeza kiwango hicho.

“Ila huyu wa Mtera ambaye ameshindwa kukusanya hata shilingi, Katibu Mkuu naomba umuondoe kule na umpangie kazi nyingine kwa sababu ameshaonesha wazi kuwa kazi hiyo imemshinda” Amesema Ndaki.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesisitiza kupitiwa upya kwa kanuni zinazoongoza biashara ya mazao ya uvuvi nchini ambapo amesema kuwa zilizopo haziendani na mahitaji ya soko kwa hivi sasa.

“Samaki wengi hawaingii viwandani kwa sababu ya mabadiliko ya kanuni tuliyoyafanya mwaka 2020 hivyo ninashauri tuboreshe kanuni hizo kwa sababu tumeshaona hasara kubwa tunayoipata na kama hivi viwanda vikifungwa kwetu itakuwa ni aibu na fedheha,   kuna viwanda visivyo vingi visivyo rasmi katika ukanda wa ziwa Victoria kwa ambavyo vinahifadhi samaki aina ya sangara kwenye ubaridi bila kumchakata na ukichunguza utaona hawalipi hata ushuru wa Serikali  ” Amesisitiza  Ulega.

Ulega amemuomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki kuridhia mapitio ya kanuni hizo ili ziweze kufanyiwa mabadiliko huku akitolea mfano wa kanuni ya “whole fish” ambayo amesema kuwa inapaswa kufanyiwa mabadiliko na kusimamiwa ipasavyo ili samaki aina ya sangara aweze kuchakatwa na hatimaye Serikali kunufaika na  tozo 13 zinazotokana na uchakataji huo.

“kwenye hii biashara ya mabondo Mhe. Waziri mbali na kupoteza hizo tozo 13 pia tunapoteza nafasi za ajira kwa watu ambao wangehusika na uchakataji wa samaki hawa hivyo ni lazima turudi na kupitia upya kanuni zetu ili tuweze kwenda sambamba na uchumi wa blue” Amemalizia Ulega.

Akielezea sababu za kutofikisha lengo la makusanyo, Afisa Mfawidhi wa kituo cha Ulinzi wa rasilimali za Uvuvi kilichopo mpaka wa Tunduma, Francis Mpatama amesema kuwa hali hiyo imetokana na kitendo cha ofisi yake kuhamia mpakani badala ya ndani kidogo ya nchi ya Malawi alipokuwa akikusanyia hapo awali ambako ndiko kwenye wanunuzi wengi wa dagaa wanaotoka Tanzania.

Naye Afisa Mfawidhi kutoka kituo cha Namanga, Christine Maganga amesema kuwa kushuka kwa makusanyo ya maduhuli katika kituo chake kulitokana na kitendo cha kufungwa kwa ziwa Eyasi ili kuongeza wingi wa samaki katika ziwa hilo.

“Sababu nyingine Mhe. Waziri ni mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19 ambapo idadi ya wateja ilipungua hasa wale wanaotoka nje ya nchi kutokana na taratibu zilizokuwa zimewekwa nchini mwao” Amesema Maganga.

Kikao cha kupokea taarifa ya makusanyo ya maduhuli hufanyika kila robo ya mwaka kwa lengo la kutahmini hali ya makusanyo kulingana na malengo ambayo yamewekwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.


Share:

Waziri Ndumbaro Awataka Wadau Wa Utalii Nchini Kupaza Sauti Dhidi Ya Majangili Na Wavamizi Maeneo Ya Hifadhi


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amewataka Wadau wa sekta ya Utalii  nchini kuungana na Serikali katika vita dhidi ya ujangili pamoja na uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa baadala ya kuiachia Serikali pekee

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mkoani Ruvuma  mara baada ya kufanya doria kwa kutumia  ndege ndogo katika maeneo yaliyohifadhiwa na kujionea uharibifu mkubwa unaoendelea kufanywa na Wavamizi wakiwemo wakulima na wafugaji.

Amewataja wadau hao kuwa ni Chama cha Wasafirishaji wa Watalii ( TATO), Chama cha Mahotelia ( HAT) Chama cha Wawindaji wa Kitalii ( TAHOA) Shirikisho la Vyama vya Utalii nchini ( TCT )  pamoja  Chama cha Waongoza Wataii ( TTGA)

Katika doria hiyo, Dkt.Damas Ndumbaro aliongozana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Ruvuma pamoja na Mkuu wa mkoa huyo  ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge

 Kwa mujibu wa takwimu sekta ya Utalii nchini inategemea zaidi ya asilimia 80 ya  utalii wa wanyamapori

Kufuatia takwimu hizo, Dkt.Ndumbaro amesema  kutokana na kasi ya Wafugaji kuingiza mifugo  na huku Wakulima kuendelea kulima  ndani ya maeneo ya Hifadhi kunatishia kupungua  au kuisha  kabisa kwa Wanyamapori ambao watalii hutoa pesa nyingi  kuja nchini kwa ajili ya kuwaona

Amesema katika vita ya kupambana na Wavamizi katika maeneo ya Hifadhi hususan Wafugaji kunahitaji ushirikiano mkubwa kutoka Sekta binafsi kwani Wafugaji ni watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii, watoa rushwa na wanakikundi cha Wanasiasa wakiwemo wabunge wanaowatetea pindi wanapokamatwa wakiwa wameingiza mifugo katika maeneo ya  Hifadhi.

" Ili muendelee na biashara za utalii nchini sisi kama Serikali pamoja na ninyi Wadau wa Utalii ni lazima tuzungumze lugha moja tuwakemee wale wote ambao hawautakii mema uhifadhi, huwautakii mema utalii wetu, hawautakii mema uchumi wetu," alisisitiza Ndumbaro.

 Amesisitiza kuwa kama   Wadau wa Utalii nchini wataendelea kuitegemea serikali pekee ndiyo yenye jukumu la kulinda maeneo yaliyohifadhiwa, itafika muda watalii wataacha kuja nchini kwani maeneo yote yaliyohifadhiwa yatakuwa yamejaa mifugo pamoja na mashamba ya mazao badaala ya wanyamapori.

" Nawasihi Wadau wote wa utalii nchini pazeni sauti zenu , naamini sauti zenu zina nguvu sana waambieni  Wafugaji hili suala la kuingiza mifugo hifadhini kwa kisingizio kuwa hakuna maeneo ya malisho  halikubaliki hata kidogo" alisisitiza Dkt.Ndumbaro

Amefafanua kuwa ili Wadau wa utalii nchini waendelea kufanya biashara zao katika sekta ya utalii wanategemea  sana uimara wa maeneo yaliyohifadhiwa kutokana na uvamizi mkubwa unaoendelea  serikali ni lazima ishirikiane na Wadau hao katika kupambana na Wavamizi hao.

Amewatahadhalisha Wadau hao kuwa kama wataendelea kukaa pembeni na kunyamazia wafugaji kuingiza mifugo yao basi  biashara ya utalii nchini ipo hatarini  kutoweka na watu zaidi milioni 1.5 walioajiriwa katika sekta hiyo watapoteza ajira zao  kwani kutokana na uvamizi pamoja na ujangili  wanyamapori wanazidi kupungua siku hadi siku.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amesema kumeibuka aina mpya ya majangili ambao hujidai kama wachungaji kwa kuingiza mifugo maeneo ya Hifadhi  lakini hubeba bunduki kwa ajili ya kuua wanyamapori

Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro amesewatahadharisha  Wadau wa Utali nchini  wasifikirie kuwa wapo salama kwani uchumi wao unawategemea sana   watalii bila kuungana na serikali kupaza sauti na kukemea Wafugaji wanaoingiza mifugo ndani ya Hifadhi uchumi wao utakuwa matatani siku za usoni

Akizungumzia maeneo aliyofanya  doria kwa kutumia ndege,  Dkt.Ndumbaro amesema hali ni mbaya wafugaji wameokana wakiwa na maelfu ya ng'ombe katikati ya maeneo ya Hifadhi huku  wakulima wakiwa  katikati ya maeneo ya Hifadhi wameonekana wakilima  katika vyanzo vya maji huku wakiwa wakikata miti kwa kasi pamoja na wachimba madini wakiwa wamevamia maeneo hayo  hali ambayo sio salama kwa Wanyamapori

Akitaja maeneo yaliyofanyiwa doria kuwa ni Pori la Akiba la Selous, Hifadhi ya  Wanyamapori ya Jamii ya Mbalang'andu, Pori la Akiba la Litambyandosi pamoja na Pori la Akiba la Liparamba.

Naye, Mkuu wa mkoa wa Ruvuma pamoja na Mkuu wa mkoa huyo  ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema Wafugaji ni lazima wapeleke mifugo yao katika maeneo yaliyopangwa na sio kuvamia maeneo ya hifadhi huku akiwaonya wakulima kuacha kuvamia maeneo ya hifadhi kwani ni hatari kwa ajili ya maisha yao

Amewataka wavamizi wote wajiandae kuondoka mara moja kabla ya kusbiri kuanza kuondolewa.


Share:

HIZI NDIYO DALILI ZA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE


Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu ,shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;


1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo

2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe

3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi

4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

5. Kisukari

6. Kuwa na mawazo na wasiwasi

7. Matumizi ya madawa mbalimbali

8. Umri hasa wazee

9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

10. Kuwa na tatizo la kibofu

11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu

12. Kutopata usingizi kamili

13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine


DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;


1. Kuwahi kufika kileleni

2. Kukosa hamu ya mapenzi

3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa

4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha

5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)

8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.


ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.


Pia tunatibu Magonjwa mengine kama


Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonda vya tumbo, Kisukari, Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kung’oa


Ndugu mteja Epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahihi kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO


Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27 utatumiwa sehemu yoyote ulipo
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 7,2021






Magazetini leo Jumapili November 7 2021














Share:

Saturday, 6 November 2021

SIMBA SC YAPATA KOCHA MPYA, REKODI ZA TIMU AMBAZO AMEZIFUNDISHA ZINAMBEBA


***************



Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi Pablo Franco Martín raia wa Hispania kuwa kocha wao mkuu akichukua nafasi ya Didier Gomes da Rosa aliyeachana na timu hiyo hivi karibuni. 




Franco (41) aliyewahi kuwa kocha msaidizi Real Madrid 2018 amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC.




Kabla ya kujiunga Simba SC alikuwa kocha wa Al Qadsia ya Kuwait na amewahi kuwa kocha wa Getafe 2015
Share:

WATATU WAKAMATWA KWA KUFUKUA KABURI,KUKATA MGUU WA MAREHEMU TANGA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia Jongo
**
Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga limefanikiwa kuupata mguu wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi, uliokatwa hivi karibuni na watu waliokwenda kufukua kaburi lake wilayani Lushoto kwa madai kuwa ukiwa na kiungo cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi utajiri unakufuata.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia Jongo, amesema kuwa hadi sasa jumla ya watu watatu wamekamatwa wakiwa na kiungo hicho.

Katika hatua nyingine, Jeshi hilo limewakamata watoto 117 wanaojiita watoto wa Ibilisi na wazazi kutokana na kujihusisha na matukio ya kihalifu na baadhi yao tayari wameshafikishwa mahakamani.

Chanzo - EATV
Share:

LORI LA MAFUTA LAUA WATU ZAIDI YA 80 SIERRA LEONE




Takriban watu 84 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown. Mlipuko huo ulitokea baada ya lori la mafuta lenye urefu wa futi 40 kugongana na gari jingine kwenye makutano yenye shughuli nyingi jijini humo.

Picha za video zilizorushwa na vyombo vya habari vya ndani zilionesha miili iliyoungua vibaya. Rais Julius Maada Bio alisema “amesikitishwa sana na moto huo mbaya na vifo vya kutisha vya watu”. Katika ukurasa wake wa twitter, alisema serikali yake itafanya “kila kitu kusaidia familia zilizoathirika”.

Meya wa Freetown Yvonne Aki-Sawyerr alieleza kuwa aliona picha “za kutisha” lakini akasema ukubwa wa athari za tukio hilo hazijafahamika


Katika chapisho lake wenye ukurasa wa Facebook alisema kulikuwa na “uvumi kwamba zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha”, ingawa bado hakuna idadi rasmi ya vifo. Chumba cha kuhifadhia maiti kinachosimamiwa na serikali kimepokea miili 91 hadi sasa, meneja wake ameliambia shirika la habari la Reuters.

Mlipuko huo unaaminika ulitokea kwenye makutano nje ya Duka Kuu la Choitram lililo na shughuli nyingi katika eneo la Wellington mjini siku ya Ijumaa. Ripoti moja ilisema basi lililojaa watu liliteketea kabisa, huku maduka ya karibu na maduka ya soko yalishika moto huo wakati mafuta yalipomwagika barabarani.



Brima Bureh Sesay, mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga la Sierre Leone, aliviambia vyombo vya habari kuwa tukio hilo lilikuwa “ajali mbaya”.


Mji huo wa bandari, ambao ni makazi ya watu zaidi ya milioni moja, umekabiliwa na majanga kadhaa makubwa katika miaka ya hivi karibuni.



Mwezi Machi, zaidi ya watu 80 walijeruhiwa baada ya moto mkubwa katika mojawapo ya vitongoji duni vya jiji hilo kuwaacha zaidi ya watu 5,000 kuyahama makazi yao.



Na mwaka 2017 zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maporomoko ya matope yaliyokumba jiji hilo, na kuwaacha karibu watu 3,000 bila makazi.
Share:

USHIRIKA WA ZABIBU KUONGEZA FURSA KWA WAKULIMA- WAZIRI MKUU


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisoma hotuba wakati akifungua rasmi Tamasha la mvinyo Dodoma Wine Festival Katika Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma, tamasha lililofanyika kwa lengo la kuhamasisha na kutangaza zao la zabibu na bidhaa zake.


Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akipata maelezo ya Mvinyo kutoka kwa Elias Mtiwabi Mkulima na Msindikaji wa Zabibu wa Wilaya ya Bahi (katikati) ni Afisa Ushirika Ndimolwo Laizer akifuatilia maelezo.


Bw. Elias Mtwabi Mkulima wa zabibu na msindikaji wa mvinyo wa zabibu kutoka Wilaya ya Bahi akitoa elimu kwa wadau mbalimbali waliofika katika Tamasha la mvinyo jinsi usindikaji wa zabibu unavyofanyika.


Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akifungua rasmi Tamasha la mvinyo Dodoma Wine Festival Katika Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma, tamasha lililofanyika kwa lengo la kuhamasisha na kutangaza zao la zabibu na bidhaa zake.

............................................................................

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali inafanya jitihada kuboresha na kuendeleza zao la zabibu kwa kuanzisha na kuendeleza Vyama vya Ushirika wa zabibu ili kuongeza fursa za masoko na tija kwa wakulima wa zabibu nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo Dodoma Wine Festival katika Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma Novemba 5, 2021 amebainisha baadhi ya hatua mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa na Serikali katika kuhakikisha zao la zabibu linaimarika miongoni mwa mazao ya kimkakati.

Hatua hizo ikiwa ni Pamoja na wakulima wa zabibu kujikusanya Pamoja na kuanzisha vyama vya ushirika ili Serikali iweze kuwafikia kwa urahisi kwaajili ya huduma mbalimbali za kilimo pamoja na utafutaji wa masoko. Waziri Mkuu pia ameanisha kuwa mahitaji ya miche ya zabibu kwa wakulima ni laki tatu wakati uzalishaji ni laki moja. Hivyo, amevitaka vyama vya Ushirika kuanza kuzalisha miche hiyo kwaajili ya wakulima wa vyama hivyo.

“Tunaanzisha Vyama vya Ushirika ili iwe rahisi kupata huduma za ugani, mikopo na vyama hivi vihimizwe kuzalisha miche ya zabibu ili wakulima waweze kupata huduma ya miche bora kutoka kwenye vyama itakayosaidia kuongeza uzalishaji,” alisema Waziri Mkuu

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi wengi kuchangamkia fursa ya kilimo cha zabibu kwani bado uzalishaji ni mdogo huku akitaja kuwa Mkoa wa Dodoma una jumla ya eka Milioni 2.1 zinazofaa kwa kilimo na uwekezaji wa zabibu ambao ni fursa ya kujikwamua kiuchumi.

Hatua nyingine alizozibainisha kuendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuendeleza zao la zabibu ni Pamoja na kuimarisha tafiti ya zao hilo, upatikanaji wa mbegu bora, kuongeza upatikanaji wa huduma za ugani, kuhamasisha viwanda vya usindikaji wa zabibu, usajili wa wakulima wa zabibu, kusimamia na kufufua vyama vya Ushirika wa zabibu sambamba na kuweka miundombinu ya umeme kwenye miradi ya mashamba ya zabibu.

Akielezea malengo ya Tamasha la Mvinyo Jijini Dodoma Bi. Atitwe Makweta mratibu wa tamasha hilo amesema, tamasha hilo ni la nne kufanyika mkoani Dodoma likilenga katika kuhamasisha zao la zabibu na bidhaa zake ili kuongeza tija ya mnyororo wa thamani ya uzalishaji zabibu. Akiongeza kuwa mwaka huu Kauli Mbiu ya Tamasha hiyo ni “Onja Kila Siku pata ladha tofauti”

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde ameshukuru wadau wa zao la zabibu kwa kuitika wito wa kushiriki tamasha hilo huku akiiomba Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuendelea kusaidia wakulima katika upatikanaji wa masoko, uhifadhi mzuri wa zabibu pamoja na masuala ya utaalamu wa Kilimo cha zabibu ili kuongeza thamani ya mnyororo wa zabibu utakaochangia kuongeza uchumi na pato la Taifa.
Share:

TGNP YAKUTANA NA WASAIDIZI WA KISHERIA, VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA MSALALA...WATENDAJI BADO KIKWAZO KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA umefanya kikao na Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kuboresha namna ya ushiriki wa kuzuia na kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia hususani wanawake na watoto.

Akizungumza leo Jumamosi Novemba 6,2021 wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Nitesh Manispaa ya Kahama,Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija amesema nia kuu ni kuchochea njia bora za kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia hasa yanayowakumba wanawake na watoto ili kuongeza ustawi wa wanawake na watoto katika jamii.

“Kikao hiki kinacholenga kujadili mafanikio,changamoto, kujifunza na mikakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA tangu mwezi Julai 2020 katika kata za Shilela na Lunguya halmashauri ya Wilaya ya Msalala. Tunataka tupate matokeo chanya ili kuwapatia haki waathirika wa matukio ya ukatili wa kijinsia”,amesema Shija.

Shija ametumia fursa hiyo kuwataka Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya taarifa na maarifa kutoa rufaa kwa kesi za migogoro ya ardhi na ndoa badala ya kukaa nazo.

“Kuna kesi ambazo hupaswi kuzisuluhisha bali zipelekwe ngazi zinazotakiwa. Usihangaike na jambo ambalo huhusiki nalo, mfano migogoro ya ndoa na ardhi ipelekwe kwenye mamlaka zingine, msiwe kama baadhi ya maafisa watendaji ambao wanakaa na kesi hizo. Usikae na kesi isiyokuhusu, kama imekushinda kabisa achana nayo”,amesema Shija.

Aidha amefafanua kuwa Mahakama ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kuvunja ndoa na kugawanya mali za wanandoa  hivyo kuwataka baadhi ya viongozi ngazi za vijiji, mitaa, vitongoji, kata wakiwemo maafisa watendaji kuacha tabia ya kusuluhisha kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji, mimba na ndoa za utotoni.

Hata hivyo amesema Wasaidizi wa Kisheria wana wajibu wa kutoa ushauri wa kisheria kwa wana vituo vya taarifa na maarifa kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia na wana vituo vya taarifa na maarifa kuomba ushauri pindi wanapokutana na changamoto katika kushughulikia matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Nao washiriki wa kikao hicho akiwemo Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya, Loyce Kabanza na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Lameck Manyesha wamesema wananchi wameanza kuachana na baadhi ya mila na desturi zisizofaa mfano Wacheza ngoma ya Ukango ambao sasa wamepunguza matumizi ya matusi wanapocheza ngoma zao.

Kwa upande wao, Wasaidizi wa Kisheria Phillip Jackson Sesawanga na Jacob Paul Nyalulu wamesema bado kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanapoteza ushahidi wa matukio ya ukatili wa kijinsia hali inayokwamisha kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Lakini pia bado wananchi wanakumbatia matukio ya ukatili,baadhi ya wanawake wakibakwa hawatoi ushirikiano kwa kutoa ushahidi, wanaume nao wanafanyiwa ukatili wa kijinsia mfano kupigwa lakini hawasemi, wanaona aibu kusema na bado kuna wazazi wanawataka watoto wao kufeli kwenye mitihani ili waolewe”,amesema Sesawanga.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA leo Jumamosi Novemba 6,2021 katika ukumbi wa Nitesh Manispaa ya Kahama. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija akizungumza kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya, Loyce Kabanza akizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Shilela, Lameck Manyesha akizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Msaidizi wa Kisheria David Mlyandili akizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakifanya majadiliano kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wakifanya majadiliano kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA
Msaidizi wa Kisheria kutoka kata ya Shilela, Jacob Paul Nyalulu  kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga  kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA.
Msaidizi wa Kisheria Phillip Jackson Sesawanga akichangia hoja kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga  kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA.
Mwana kituo cha taarifa na maarifa kutoka kata ya Lunguya Gaudensia Macheye akichangia hoja kwenye kikao cha Wasaidizi wa Kisheria na Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga  kilichoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA.

Picha na Kadama Malunde - Malunde  1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger