Saturday, 6 November 2021

HESLB YAFUNGUA DIRISHA LA RUFAA KWA SIKU TANO KUANZIA NOVEMBA 6, 2021




Na Mwandishi Wetu, HESLB,Dar es salaam

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Jumamosi, Novemba 6, 2021) imefungua dirisha la rufaa ili kuwawezesha waombaji ambao hawajapangiwa mikopo au wanahitaji kuongezewa viwango vya mikopo kwa mwaka wa masomo 2021/2022 kuwasilisha maombi ya rufaa zao.

“Dirisha hili litakuwa wazi kwa siku tano, kuanzia leo, Novemba 6 hadi 10, 2021 na ni fursa kwa wanafunzi wote, wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea, kuwasilisha maombi yao ya kuongezewa viwango vya mkopo au kupangiwa kwa wale ambao hawajapangiwa hadi sasa,” amesema Dkt. Veronica Nyahende, Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa HESLB.

Kuhusu utaratibu wa kuwasilisha maombi ya rufaa, Dkt. Nyahende amesema maombi yote ya rufaa yanapaswa kuwasilishwa kwa njia ya mtandao kama yalivyowasilishwa maombi ya msingi.

“Kupitia dirisha hili, tunawasihi waombaji mikopo kusoma maelekezo kwa makini na kuyazingatia … ikiwemo kuweka nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao ambazo awali hawakuwa wameziweka,” amesisitiza Dkt. Nyahende.

Wakati huohuo, Dkt. Nyahende amefafanua kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo na ambao walikuwa wameomba mkopo kwa mwaka 2021/2022 na kusema kuwa maombi yao yamechambuliwa na wale wenye sifa tayari wameshapangiwa mkopo.

“Hawa tunawaita ‘first time continuing applicants’, na tumeshawapangia na kuweka taarifa zao katika SIPA na kwa kuwa ni wazoefu, wakiingia wataona … maafisa mikopo wa vyuo pia wana taarifa zao,” amesema Dkt. Nyahende.

Kuhusu malipo ya fedha kwa wanafunzi waliopangiwa mikopo, Dkt. Nyahende amesema HESLB imeshatuma vyuoni fedha za wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza ambao wamepangiwa mikopo na kuwakumbusha wanafunzi hao kufika katika ofisi za mikopo vyuoni ili kukamilisha taratibu za kupokea fedha hizo.
Share:

TUME YATAKIWA KUTENGENEZA MFUMO WA MAWASILIANO





Mkuu wa kitengo cha ICT, Geofrey Mwakijungu  (aliyekaa) akimwonyesha Mwenyekiti wa Bodi ya Tume Prof, Mahoo baadhi ya matukio katika Tovuti ya Tume.
Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akikagua
Mtambo aina ya EXCAVATOR katika Ofisi za Tume Mkao Makuu Dodoma.
 ***
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof. Henry Mahoo, ameshauri Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutengeneza Mfumo wa kiteknolojia utakaopokea taarifa za kila siku za utekelezaji wa majukumu ya watumishi kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Makao makuu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Tume.

Akizungumza katika kikao chake na Menejimenti jijini Dodoma Prof, Mahoo amesema, mfumo huo utamsaidia Mkurugenzi Mkuu, Wakuu wa Idara na Vitengo kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya mtumishi mmoja mmoja na kubaini mapungufu yaliyopo ama, ubora katika utendaji wake.

“Mfumo huo utaonyesha majukumu waliyopangiwa watumishi,utekelezaji wake, sanjari na kubadilishana taarifa baina ya viongozi wa idara na vitengo na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.Mfumo huo pia utasaidia katika kuboresha eneo la ufuatiliaji na tathmini ya uwajibika wa Watumishi.”

Aidha Prof. Mahoo amepongeza juhudi za kutanua eneo la Ofisi kwaajili ya Wataalam wa Tume na kuongeza kuwa Ofisi hizo zitabakia kuwa Ofisi za Tume Mkoa wa Dodoma mara ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu zitakapokamilika katika eneo la Njedengwa mjini Dodoma.

Katika hatua nyingine Prof. Mahoo ameitaka Idara ya Uendelezaji Miundombinu kuongeza kasi ya kuifanyia matengenezo Mitambo yote ya Tume inayohitaji kutengenezwa ili iweze kutumika kibiashara na katika shughuli za ukarabati na ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji.

Ameishauri Idara hiyo kuboresha eneo la maegesho ya Mitambo pamoja na Stoo ya kuhifadhia vipuli vya Mashine wakati wa Matengenezo katika karakana ya Tume.


Share:

KIJANA HOHEHAHE APATA KAZI YA HELA NYINGI MNO

Mohamed ni mzaliwa wa Nyali na ambaye hakufika hata kidato cha pili. Wazazi wake walishindwa kumlipia karo ya shule sababu mwanzo babake alianza kuugua ugonjwa wa Kisukari hivyo kazi yake ikaisha. 

Familia yao ina watoto saba ambapo mama mzazi alikuwa na umri mkubwa na pia hakuwa na kazi. Maisha ya Mohamed kwa kweli yakabadilika na kumbidi aanze kutoka nje kutafuta kipato ili kukimu mahitaji ya familia yao.

 Ikawa sasa yeye ndiye kila kitu yaani tegemeo. Alienedelea kupitia shida baada ya nyingine hadi kila mtu kijiji akajuwa kuwa yeye ndiye baba wa familia sasa. Ikumbukwe kuwa Moha – vile alivyokuwa akiitwa - alikuwa kijana mdogo mwenye umri wa miaka 24 pekee na kuanza kuchukua majukumu ya mtu mzima lilikuwa jambo ngumu kwake lakini hakuwa na namna nyingine. 

Ya Mungu ni mengi na sasa tunapoongea hivi maisha yake yalibadilika pale alipokutana na rafiki yake waliyekuwa naye shule ya upili ambaye alimchukua na kumpelea kwa Daktari flani wa kienyeji ambaye alimfamnyia Money Spells ili kufungua njia zake za kikazi na maisha. 

Amini usiamini baada ya siku tatu tuu Mohamed alifanikiwa kupata kazi kule Dar es Salaam ambako sasa yeye anafanya kazi huku akisoma ili kujiongezea masomo. Juzi mamaye alisikika akisema kuwa kijana wake analipwa kima cha shilingi elfu themanini pesa za Kenya yote kwa sababu ya dawa za daktari Kiwanga.

 Kiwanga wamesaidai watu wengi mno duniani kupokea baraka na nyota zao za maisha. Wengi wamepata kazi na kuongezwa vyeo kupitia Spells zao. Pia kama una matatizo na ndoa, au kesi kortini, wizi na kadhalika tafadhali pigia Daktari Kiwanga ili upate kusaidiwa haraka iwezekanavyo. 

Wengi ambao walikataliwa na wapenzi wamepata usaidizi wa Dakatari Kiwanga na sasa ndoa zao zimetulia. Ninatoa wito kwa wenye shida za magonjwa, mapenzi, ndoa, biashara, kikazi na afya kuharakisha kuwatembelea madaktari was Kiwanga. Tuvuti au Website yao ni: www.kiwangadoctors.com; Simu: +254 769404965 au wasiliana kwa barua pepe yaani Email kiwangadoctors@gmail.com.

 Sio lazima usafiri hadi ofisi zao. Ongea nao kwa njia ya simu na utasaidika kwa haraka kama vile watu wengine wanavyopata usaidizi. 

Share:

MWANA MUZIKI MAARUFU MARILIA MENDONCA AFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE



MWIMBAJI maarufu wa Brazil ambaye pia mshindi wa tuzo la Grammy 2019 kwa Amerika ya Kusini, Marilia Mendonca (26) amefariki dunia baada ya ndege aliyokuwemo kupata ajali.

Watu wengine wawili ambao ni mjomba wake, producer wake na wengine kutoka kwenye crew yake nao wamepoteza maisha kutokana na ajali hiyo iliyotokea Kusini Mashariki mwa mji wa Minas Gerais, uchunguzi bado unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Huyu ni miongoni mwa wasanii wakubwa sana nchini Brazil ambaye alikuwa akiimba muziki wa country maarufu kama sertanejo kwa Brazil, Mendonça alianza kujihusisha na muziki tangu akiwa mtoto na umaarufu wake ukaibuka mwaka 2016 na ngoma yake iliyokuwa ikizungumzia michepuko kwenye mahusiano, alifahamika kama “Queen of Suffering” ama Malkia wa Mateso.

Mwaka jana aliahirisha matamasha yake yote kutokana na kusambaa kwa janga la Corona, lakini ndiye alikuwa msanii aliyesikilizwa zaidi kwenye Mtandao wa Music wa Spotify na kutazamwa zaidi YouTube.
Mendonça, ambaye ameacha watoto wawili, alikuwa amepanga kufanya bonge la shoo jana Ijumaa jioni katika jiji la Caratinga, ambalo lipo kilomita 12 pekee kutoka eneo alipopata ajali, muda mfupi kabla ya ajali aliposti video akijiandaa na safari.

Licha ya taarifa za awali za mmoja wa wafanyakazi wake aliyedai kuwa Mendoca ametoka akiwa mzima, simanzi iliibuka baada ya staa wa Soka wa Brazilian, Neymar kuandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa: “Siwezi kuamini, siwezi”. Mwanamuziki aitwaye Anitta naye aliandika: “Siwezi kuamini huu msiba. Nataka kuamini kwamba bado kuna matumaini”.
Share:

HAWA NDIYO MABABU WA MOJA KWA MOJA WA BINADAMU


Kuna kipindi katika historia ya mabadiliko ya mwanadamu ambayo wanasayansi bado hawayaelewi vizuri.

Ni kidogo kinachojulikana kuhusu enzi hizi, ambazo zinajulikana kuwa mkanganyiko , kwasababu wataalamu bado hawakubaliani kuhusu spishi ya binadamu aliyekuwepo na kwamba wanawakilisha enzi zisizojulikana kati ya Homo erectus na binadamu wa sasa.

Na sasa kundi moja la watafiti limetaja spishi mpya ambayo inaweza kuangaza kuhusu mkanganyiko, huo ambao kulingana na uchanganuzi wao, ndio mababu wa moja kwa moja wa binadamu.

Ni kuhusu Homo bodoensis , ambao waliishi barani Afrika miaka 500,000 iliopita na ambao kulingana na wanzilishi wa utafiti huo , wanasaidia kukamilisha fumbo kuhusu wakati muhimu katika mabadiliko ya binadamu.

Lebo mpya

"Mkanganyiko huo unahusiana na enzi za Middle Pleistocene, muda unaojulikana kama Chibanian tangu 2020 , na ambao ulitokea kati ya miaka 774,000 na 129,000 iliopita.

Watalaamu hatahivyo hawaelewi mabaki yanatoka kutoka kwa spishi katika kipindi hicho. Na haijulikani ni spishi ipi ilizaa nyengine.

Kipindi cha Chibanian ni muhimu kwa sababu huo ndio wakati Homosapiens waliibuka Afrika na Neanderthals huko Uropa.

Tatizo ni kwamba mabaki ya wakati huo ambayo yalitangulia Homo sapiens na Neanderthals, "hayajaelezewa vizuri na yanaeleweka kwa njia tofauti," kulingana na waandishi wa utafiti huo.

Kwa hili, watafiti wanamaanisha kuwa mabaki yaliopo kutoka enzi za Chibanian yamepewa jina kama Homo heidelbergensis au Homo rhodesiensis , aina mbili ambazo, kulingana nao, mara nyingi zimeelezewa kukinzana.



Via BBC Swahili
Share:

BABU ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MIWILI KAHAMA


Na Ali Lityawi - Kahama

MKAZI wa Kata ya Nyihogo katika Manispaa ya Kahama, Maduhu Tarasisi Chubwa (60),amehukumiwa kwenda Jela maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka miwili.

Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 5,2021 na Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Kahama,Christine Chovenye, baada ya kukubaliana na ushahidi wa upande wa mashtaka na kumtia hatiani mshtakiwa.

Hakimu Chovenye alisema ametoa adhabu hiyo baada ya kukubaliana na ushahidi wa upande wa mashitaka ambao haujaacha shaka,kuwa mshtakiwa alitenda kosa kinyume cha kifungu namba 130(1)na (2) (e) na kifungu cha namba 131(3) kinyume na kanuni ya adhabu namba 16 kama kilivyorekebishwa RE 2019.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka wa serikali, Mercy Ngowi,kuwa mtuhumiwa huyo alimbaka Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mwili,mnamo tarehe 11/10/2021,majira ya mchana katika eneo la Nyihogo.

Hata hivyo wakati wa mwenendo wa kesi hiyo mshatakiwa Chubwa aliposomewa shitaka hilo mbele ya mahakama hiyo alikana kutenda kosa hilo.

Akitoa hukumu hiyo,Hakimu Covenye,alisema mahakama imejiridhisha na ushahidi wa walioshuhudia kitendo hicho kutoka katika eneo la Chumba jirani na alichokuwa akiishi Mtuhumiwa,ikiwa ni pamoja na mtoto huyo kukutwa na mbegu za kiume sehemu za siri.

Chovenye aliieleza kuwa upande wa mashitaka ulifunga ushahidi uliotolewa na Dkt, Idd Ramadhani kutoka katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama, aliyemfanyia uchunguzi wa kitabibu binti huyo na kumkuta akiwa na mbegu za kiume na michubuko katika sehemu zake za siri.

Aidha Hakimu huyo alieleza ushahidi mwingine ulikuwa ni wa mazingira pamoja na majirani ambao waliutoa mahakamani na hivyo Mahakama hiyo kujiridhisha na ushahdi huo na kutoa adhabu hiyo ya mshtakiwa kutumikia kifungo cha maisha jela.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo,Mwendesha mashitaka Ngowi,aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo kwani kitendo alichomfanyia mtoto huyo hakivumiliki katika jamii,na kwamba kimesababisha majeraha makali na makovu ya milele kwa mtoto huyo mdogo.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo Maduhu Tarasisi Chubwa alipotakiwa kujitetea mahakamani hapo alisema kuwa yeye ni mzee na kuiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na mahakama hiyo kuamua kutoa adhabu kali iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo.
Share:

POLISI SHINYANGA WACHUNGUZA TUKIO LA KIJANA KUUAWA, KUTOBOLEWA MACHO NA KUTUPWA NGOKOLO MITUMBANI


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

****

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limesema linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mauaji ya kijana ambaye hajafahamika jina wala makazi yake (25-30) ambaye amekutwa ameuawa na kutobolewa macho usiku wa kuamkia leo Jumamosi Novemba 6,2021 katika ghuba la kuhifadhia uchafu la Ngokolo Mitumbani Mjini Shinyanga.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema bado wanafanya upelelezi ili kuwabaini chanzo cha mauaji na wahusika wa mauaji hayo

"Jeshi la Polisi tumefika eneo la tukio, tumekuta pembeni ya mwili wa marehemu kuna vyuma ambavyo huenda ndivyo vimetumika kufanyia mauaji. Tunaendelea kufanya upelelezi ili kujua chanzo cha tukio lakini pia kuwabaini wahusika wa mauaji haya",amesema.

"Tumechukua mwili wa marehemu na tuumepeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi, bahati mbaya huyu mtu hajulikani jina wala makazi yake, hatujajua kama  aliuawa pale, au aliuawa mahali pengine akaja kutupwa pale, tunaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini nini hasa hasa kilitokea",ameongeza Kamanda Kyando.


Baadhi ya mashuhuda waliofika eneo la tukio wamesema  wameukuta mwili wa kijana huyo akiwa ameuawa kinyama na kutobolewa macho na watu wasiojulikana majira ya saa moja asubuhi kisha Jeshi la polisi lilifika na kuuchukua mwili huo na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.


Share:

Head of Marketing at School of St Jude

Head of Marketing Want to work for one of the largest charities of its kind in Africa? Do you love creating engaging and successful content for a good cause? Are you passionate about fundraising? Do you have experience leading a team? Does it sound like we’re talking about you… Keep reading! The School of St […]

This post Head of Marketing at School of St Jude has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Sales Agents at Biss Company

Sales Agents    COMPANY: BISS COMPANY We are a B2B and B2C e-commerce platform that that deals with selling clothes & accessories. We provide hassle free shopping experience to both consumers and businesses by providing a seamless integration of service. Location: Dar es Salaam Job Title: Sales Agents (Wakala Wa Mauzo) Job requirements:   Must have a […]

This post Sales Agents at Biss Company has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 6,2021














Share:

Friday, 5 November 2021

MVUA YAUA MTU MMOJA SONGWE, YAJERUHI NA KUHARIBU MALI


Mtu mmoja amepoteza maisha na watatu kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kuanzia siku ya tarehe 2 hadi 3 Novemba, mwaka huu katika wilaya za Momba na Ileje Mkoani Songwe.

Mvua hizo zilizoambatana na upepo mkali zimesababisha pia maafa makubwa ikiwemo kubomoa na kusomba nyumba 46 za wakazi wa eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amewatembelewa wahanga hao na kuwapa pole akisema kuwa nyumba 36 zimebomolewa katika wilaya ya Ileje na 10 katika wilaya ya Momba huku akitaja kuwa chanzo cha mvua hizo ni mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotokana na shughuli za kibinadamu.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey M. Kasekenya, amekutana na viongozi wa Kijiji Cha Yuli kata ya Mlale kutathmini kutathmini madhara yaliyotokana na Mvua zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha Nyumba 36 kuezuliwa na kifo cha mtu mmoja.

Share:

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAADHIMISHO MIAKA 10 YA LSF


Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (katikati) akiwa na mnufaika wa mradi wa upatikanaji wa haki, Asia Shemdoa pamoja na wadau wengine wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya LSF yanayotarajiwa kufanyika Novemba 11, 2021.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya LSF yanayotarajiwa kufanyika Novemba 11, 2021.


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika madhimisho ya miaka 10 ya Shirika la Legal Services Facility (LSF) yanayotarajiwa kufanyika tarehe 11 Novemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

LSF ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kukuza upatikanaji wa haki nchini Tanzania kupitia utekelezaji wa program ya upatikanaji wa haki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana tarehe 4 Novemba, 2021, Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema tukio hilo linalenga kusherehekea matokeo na mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa program mbalimbali.

Ametaja progamu hizo kuwa ni upatikanaji wa haki nchini Tanzania (Access to Justice Program), Mradi wa Uwezeshaji wa Kisheria Maeneo ya Mijini (Urban Legal Empowement Project) pamoja na miradi mingine ya kimkakati.

“LSF imejikita katika maeneo makuu manne ikiwemo; upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kupitia kwa watoa huduma za msaada wa kisheria takriban 4,000; kuwa na jamii iliyowezeshwa kisheria; kuboresha mazingira Rafiki ya upatikanaji wa huduma bora za msaada wa kisheria; pamoja na kujenga mazingira ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria endelevu katika ngazi ya kitaasisi,” amesema.

Aidha, amesema tukio hilo linakwenda sawia na maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria, ambapo wadau nchi nzima hususani wasaidizi wa kisheria wanaendelea kutoa bure katika kila wilaya nchi nzima.

Amesema katika kipindi cha miaka 10, LSF imetoa ruzuku kwa mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria zaidi ya 200 Tanzania bara na Visiwani Zanzibar. 

Amesema LSF imekuwa ikishirikiana na serikali katika ngazi ya chini mpaka juu serikalini kupitia Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) na kufanikiwa kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi milioni sita na kjutatua migogoro 90,000 kwa mwaka.

“Pia imekuwa ikifanya kazi na Wizara ya Mambo ya Ndani katika mradi wa haki jinai (Criminal Justice Project) ambao unatekelezwa na shirika mdau wetu wa kimkakati ENVIROCARE wakati kwa upande wa Jeshi la Polisi Tanzania, LSF inashirikiana nao kupitia makubaliano yaliyolenga kuwezesha zoezi la kupitia upya mwongozo wa jeshi hilo (General Police Orders – PGO,” amesema.

Amesema LSF imekuwa ikifanya kazi na Wizara ya Afya katika mpango wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na Watoto.

Vilevile LSF imekuwa ikifanya kazi na Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Visiwani Zanzibar katika kukuza upatikanaji wa haki visiwani humo pamoja na kuboresha sera ya wasaidizi wa kisheria Zanzibar.

Amesema katika kutambua tija iliyo nayo sekta ya kilimo nchini Tanzania, katika kipindi cha miaka 10, LSF imekuwa na makubaliano na Benki ya Taifa ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa kusaidia kuvijengea uwezo wakulima, vyama vya msingi vya wakulima (AMCOS) na wajasiriamali wengine katika sekta ya kilimo.

“Kubwa zaidi katika kipindi hiki, LSF ni sehemu ya mafanikio ya upatikanaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria iliyopitishwa mwaka 2017 ili kuwatambua rasmi wasaidizi wa kisheria nchini.

“Hivyo, tukielekea kuadhimisha miaka 10 ya LSF, tunawashukuru wadau wetu muhimu wa maendeleo ikiwemo DANIDA, Umoja wa Ulaya, UKAID, DFiD, ambao tumekuwa nao katika hatua mbalimbali za safari hii katika kukuza upatikanaji kwa watu wote hususani wanawake na Watoto,” amesema Afisa Mtendaji huyo.

Share:

LSF NA MPANGO WA UWEZESHAJI WANAWAKE KUTAMBUA HAKI ZAO KIUCHUMI


Mratibu wa Mradi wa Ajira –WLAC, Abia Richards, akiwakabidhi machapisho yanayohusu sheria ya Ajira na Haki za wafanyakazi, wafanyakazi wa kazi za ndani walioshiriki kwenye kampeni ya Boss Mama na Supa Dada.
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubongo, Beatrice Dominuo (kushoto) akikabidhi hati ya kibali cha utekelezaji wa mradi wa Hati Yangu Maisha Yangu katika Wilaya ya Ubungo wakati wa uzinduzi wa mradi huu wenye lengo la kuwawezesha wanawake kupatiwa hati miliki ya ardhi zao na elimu ya sheria za ardhi ili kuwawezesha wanawake kiuchumi. Anayepokea ni Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala wakati anayeshuhudia Mary Richard, Mkuu wa program TAWLA.


****

· 2000 wapatiwa msaada kutatua migogoro ya ardhi

Na Mwandishi wetu
Mwaka 2018 LSF ilizindua mpango wake wa uwezeshaji wa wanawake waishio mijini ili wapate uelewa wa kisheria kuhusu masuala ya haki za mazingira, uchumi, makazi na kazi kwani ni mojawapo ya haki ambazo hukiukwa sana katika maeneo ya mijini nchini.

Ili kuwezesha utekelezaji wa mpango huu, LSF ilishirikiana na mashirika yanayofanya shughuli zake mijini na kutoa ufadhili uliowezesha mashirika hayo kuchangia katika maeneo muhimu na kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa na LSF.

LSF ilishirikiana na Taasisi ya Chama Cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) ili kuhakikisha kila mwananchi mkazi wa Dar es Salaam anafurahia haki yake ya msingi ya kuishi katika mazingira safi na yenye afya bora kupitia mradi uliotekelezwa katika wilaya tano za jiji hilo.

Akizungumzia ufadhili huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala anasema chini ya ufadhili wa mradi huu mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kutunga sheria ndogondogo zinazowezesha jamii kuweka vituo vya kuzolea taka mitaani, kuweka sheria kali dhidi ya uvujishaji wa maji taka na kuwatoza faini watu wanaokiuka sheria hizo ndogo. Mpango huu umeboresha kwa kiasi kikubwa usafi wa jumla wa mazingira katika maeneo mengi ya jiji na kuondoa milipuko ya magonjwa.

Kuhusu masuala ya makazi miongoni mwa jamii maskini za mijini, anasema LSF ilishirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) na kutoa elimu ya sheria kwa wananchi kwa ujumla ili kuwasaidia kuelewa haki yao na kuhakikisha wanaingia mikataba ya kupangisha ili kuwazuia wamiliki wa nyumba wasikiuke haki za wapangaji.

Aidha, programu maalum inayolenga kuwawezesha wanawake kiuchumi imezinduliwa na inaendelea kufanyiwa kutekelezwa katika Manispaa ya Ubungo.

Anasema mpango huo utashuhudia zaidi ya wanawake 300 wakisaidiwa kupata hati miliki zao, na zaidi ya 2,000 wakiwezeshwa katika masuala ya kisheria yanayohusu masuala ya ardhi ambayo ni muhimu katika kushughulikia migogoro ya ardhi inayoshamiri katika maeneo mengi ya nchi.

Kwa msaada wa LSF, Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) kinatekeleza mradi wa uwezeshaji jamii katika haki za ajira ambao walengwa wake ni wanawake na vijana wanaofanya kazi katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

Mratibu wa mradi huo, Abia Richard anasema chini ya mradi huu jumla ya watu 1,192 wamepata msaada wa kisheria kupitia uhamasishaji, mafunzo, maigizo na usambazaji wa jumbe mbalimbali za uhamasishaji.

“Zaidi ya hayo, wafanyakazi wanapata uelewa kuhusu uvunjaji wa mikataba ya ajira, ukiukwaji wa haki za uzazi, na unyanyasaji wa kijinsia mahali pa kazi,” anasema.

Mradi wa “Wanawake na Ajira” unaotekelezwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) unaoshughulikia changamoto za haki za ajira zinazowakabili wanawake, vijana na wasichana walioajiriwa katika sekta ya viwanda jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa WiLDAF, Anna Kulaya anasema chini ya mradi huu viwanda kadhaa vimeweka utaratibu wa kuzuia aina zote za ukatili na ubaguzi mahali pa kazi, kama inavyothibitishwa zaidi na maombi ya wafanyabiashara 12 wa viwanda jijini Dar es Salaam wanaotaka kuandaliwa sera za kupinga unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yao ya kazi.

Mafanikio mengine ya mradi huo ni mpango wa mwaka mmoja ambao uliandaliwa na WCPC - Ubungo ili kukabiliana kikamilifu na ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake mahali pa kazi.

Mkoani Mwanza - LSF imeunga mkono shirika la Railway Children Africa ambalo linatekeleza mpango ulioandaliwa kwa ajili ya kuboresha na kubadilisha maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Lengo ni kuwaongezea uelewa ili kukbailiana na changamoto zinazowasukuma na kuwaweka watoto katika mazingira yasiyo salama kwa kutumikishwa kufanyiwa unyanyasaji mwingine katika mazingira hayo ya mijini katika wilaya za Ilemela na Nyamagana.

Kupitia usaidizi wa kisheria na mafunzo juu ya haki za watoto wa mitaani na wafanyakazi wa nyumbani, taratibu za usaidizi wa haki zimetolewa ikiwamo haki ya malezi ya wazazi au ya ulezi kwa watoto wa mitaani pia zimetolewa kwa kujumuisha.

Nambari maalum ya simu kwa wafanyakazi wa nyumbani imetolewa ili kuripoti matukio yoyote ya ukatili wanayotendewa na watu wengi wanaitumia kuripoti matukio hayo na kupata msaada.

Mjini Dodoma kulianzishwa mradi wenye lengo la kuboresha na kuwezesha haki za kuishi katika mazingira safi na salama kwa wakazi wa kipato cha chini waishio halmashauri ya jiji la Dodoma.

Mradi huo umetekelezwa na Shirika la Reaching Unreached Tanzania (RUT) ulianza mwaka jana kwa ufadhili wa LSF.

Afisa mradi kutoka RUT, Getrude Kigala anasema halmashauri ya jiji hilo imepewa mafunzo ya namna ya kutumia sheria za taka ngumu na kusaidiwa kuitekeleza. Hatua hiyo inakuza haki za wakazi wa jiji kuishi katika mazingira safi na yenye afya.

Kwa upande mwingine jijini Mbeya, LSF inashirikiana na Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) kuwajengea uelewa na kuwapa ujuzi wa kutosha wanawake wa mijini ili kumudu masharti ya mikopo katika kata 36 za jiji la Mbeya.

Mmoja wa maofisa wa LSF waliotoa elimu hiyo mkoani Mbeya, Aggripa Senka anasema hadi sasa mradi huo umetoa umewafikia watu 11,000 na kutatua changamoto zinazowakabili wanawake kama vile kutambua na kukataa muda usiofaa wa mkataba wanapopata mkopo kwa shughuli zao za kiuchumi au kijamii.

Kwa upande wa Zanzibar, LSF inaunga mkono Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Zanzibar (ZAPAO) kwa kuwawezesha wafanyabiashara wadogo hususani wanawake na vijana katika mkoa wa Mjini Magharibi ili kuboresha mazingira yao ya kibiashara.

Kupitia ZAPAO wafanyabiashara hawa wamefaidika katika nyanja mbalimbali ikiwamo kupata maeneo yaliyotengwa na serikali ambapo wanafanya biashara zao bila vikwazo.

Meneja Miradi kutoka LSF, Deo Bwire anasema kwa ujumla, mpango wa LSF kuhusu uwezeshaji wa kisheria katika maeneo ya mijini, kwa kiasi kikubwa umeshughulikia changamoto katika mazingira ya mijini hivyo kuongeza fursa za kuendelea kufanya kazi na serikali za mitaa na washirika wengine katika masuala ya kila siku mijini na kuwasaidia wanawake na vijana kutambua haki zao.

“Tunaposherehekea kumbukumbu ya miaka 10 tunaona haja ya kuendelea kusaidia na kupanua program hii katika mikoa mingi zaidi,” anasema Bwire.
Share:

Intern – Information Technology at Absa

Intern – Information Technology   Bring your possibility to life! Define your career with us With over 100 years of rich history and strongly positioned as a local bank with regional and international expertise, a career with our family offers the opportunity to be part of this exciting growth journey, to reset our future and […]

This post Intern – Information Technology at Absa has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Government Banking at CRDB Bank

Relationship Manager; Government Banking    Reporting line- Senior Manager; Local Government Job Summary To drive the Government business portfolio both in volume and value through building a positive relationship with the Government and its stakeholders within Zanzibar (Unguja and Pemba) by generating/identifying new business opportunities/avenues for the Bank. Key responsibilities:   Grow unit’s profitability through […]

This post Government Banking at CRDB Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

📲DOWNLOAD APP MPYA KABISA YA MALUNDE 1 BLOG.... UPATE HABARI NA MATUKIO YOTE HARAKA ZAIDI KWENYE SIMU YAKO


Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>



Share:

Design software application for WASH monitoring at SNV

Company Description SNV is a not-for-profit international development organization that applies practical know-how to make a lasting difference in the lives of people living in poverty. We use our extensive and long-term in-country presence to apply and adapt our top-notch expertise in agriculture, energy and WASH to local contexts. SNV has an annual turnover of […]

This post Design software application for WASH monitoring at SNV has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger