Friday, 1 October 2021

Picha : DC MBONEKO AONGOZA MAHAFALI YA 5 DARASA LA SABA 2021, SHULE YA AWALI LITTLE TREASURES

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikata keki na wanafunzi wa shule ya awali Little Treasures

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameongoza Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Mahafali hayo yamefanyika leo Ijumaa Oktoba 1,2021 katika shule hiyo iliyopo eneo la Bugayambelele katika Manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 98 wamehitimu elimu ya darasa la saba na wanafunzi 87 wamehitimu elimu ya awali na sasa wataingia darasa la kwanza mwaka 2022.

Akizungumza, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta amesema serikali na wanashinyanga wanajivunia uwepo wa shule ya Msingi Little Treasures ambayo imekuwa ikiupa sifa nzuri mkoa wa Shinyanga kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.

“Shule hii imekuwa ikitutangaza vizuri kitaifa katika matokeo ya mtihani ndiyo maana sisi serikali hatusiti kuwaunga mkono na tutaendelea kuwaunga mkono kwani nia ya serikali ni kushirikiana na sekta binafsi”,amesema Mboneko.

“Ninawapongeza pia kwa kukuza vipaji vya watoto, watoto hawa wa vipaji lakini pia darasani hawakamatiki, Kusoma na burudani pamoja na mazoezi lazima vyote vifanyike kwa ajili ya makuzi ya watoto. Nawapongeza sana kwa kulea watoto na kuwa bora”,ameongeza.

Aidha amewataka wazazi kuendelea kutilia mkazo suala la elimu kwani elimu inatengeneza watalaamu mbalimbali na watoto wanataka kutimiza ndoto zao huku akiwahimiza wazazi kuwasimamia watoto na kuwapeleka shule wkwani hakuna urithi mzuri zaidi ya elimu.

“Tukiwapeleka shule watakwenda kujitegemea, wataenda kusoma kwa bidii ili wawe na vipato , wasiwe tegemezi, pelekeni watoto shule, tuwafundishe uzalendo, tuwafundishe utamaduni pia, haya lazima wakue nayo ili waje watumikie taifa lao”,amesema.

“Little treasures wana ushirikiano mzuri na wana walimu wazuri ambao wengi wao ni vijana ambao wanaleta fikra mpya wakishirikiana na wazee. Shule hii ina uongozi thabiti, walimu wanajituma na wanajitahidi kulea na kusimamia watoto hawa, ambao ni wanyenyekevu na nidhamu kwa sababu wamefundishwa shuleni”,amesema Mboneko.

“Sisi wazazi tuna wajibu wa kuwalinda watoto hawa waliomaliza shule wasiwe wazururaji kwenye mitaa yetu na wazazi tuwaleee vizuri. Kwenye shule zetu wapo ambao kwa kiasi kikubwa kuna changamoto, naomba wazazi tujinyime na kujitahidi na kulipa ada, tulipe ada”.

“Wazazi tunajipendelea sana, kila kitchen party, upo kila sherehe upo, tuweke kipaumbele pia kwa watoto wetu, tuwalipie ada na kuwapatia mahitaji mengine. Tuhakikishe tunaweka kipaumbele kwa ajili ya watoto wetu”,amesema.

Kwa upande Mkurugenzi wa shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita ameishukuru serikali kwa ushirikiano inaoutoa kwa shule hiyo ambapo sasa serikali imewapelekea umeme ili kupunguza gharama za uendeshaji wa shule hiyo.

Aidha amewashukuru wazazi na walezi kwa kuiamini shule hiyo na kupeleka watoto katika shule za Little Treasures.

Lucy amewataka wahitimu wa darasa la saba kuwa watoto wazuri kwa familia, jamii na mahali popote watakapokwenda huku akiwasihi wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao.

Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita amesema tangu shule ya Msingi Little Treasures ilipoanzishwa mwaka 2012 ikiwa na wanafunzi wanne pekee hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 800 na imeendelea kupata wanafunzi wengi kila mwaka huku ufaulu wake ukiwa mzuri kwa kufaulisha wanafunzi wote kwa kupata daraja A tangu mwaka 2017 hadi mwaka 2020.

Amesema mbali na kuwa na shule ya Msingi Little Treasures pia wameanzisha Shule ya Sekondari Little Treasures ambapo mwaka huu 2021 jumla ya wanafunzi 25 wanahitimu kidato cha nne.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures Paulo Kiondo amewaomba wazazi na walezi kuendelea kushirikiana na walimu katika kulea wanafunzi ili kutimiza ndoto zao huku akiwakumbusha kulipa ada kwa wakati.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
 Wahitimu wa darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures wakiandamana kuelekea kwenye eneo la Sherehe za mahafali ya 5 ya darasa la saba na shule ya awali leo Ijumaa Oktoba 1,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 Maandamano kuelekea kwenye eneo la Sherehe za mahafali ya 5 ya darasa la saba na shule ya awali yakiendelea
 Wahitimu wa darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures  na wahitimu wa elimu ya awali wakiandamana kuelekea kwenye eneo la Sherehe za mahafali ya 5 ya darasa la saba na shule ya awali leo Ijumaa Oktoba 1,2021.

Wahitimu wa elimu ya awali wakiandamana kuelekea kwenye eneo la Sherehe za mahafali ya 5 ya darasa la saba na shule ya awali leo Ijumaa Oktoba 1,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikata keki na watoto waliohitimu elimu ya awali leo wakati wa Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikata keki na wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakati wa Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimlisha keki mhitimu wa elimu ya awali leo wakati wa Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mhitimu wa elimu ya awali akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko wakati wa Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimlisha keki mhitimu wa elimu ya darasa la saba wakati wa Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Wahitimu wa darasa la saba wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mkurugenzi wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita akizungumza kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Meneja wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasures, Alfred Mwita akizungumza kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Msingi Little Treasures, Tilulindwa Sulusi akizungumza kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Little Treasures, Paulo Kiondo akizungumza kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wahitimu wa darasa la saba wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wahitimu wa darasa la awali wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wahitimu wa darasa la awali shule ya Msingi Little Treasures wakitoa burudani ya kucheza 
Wahitimu wa darasa la saba wakiwa wamesimama kwa ajili ya zoezi la kukabidhiwa kwa wazazi wao kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mkurugenzi wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita akiwakabidhi Wahitimu wa darasa la saba kwa wazazi wao kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa na Wahitimu wa darasa la saba kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Msingi Little Treasures, Tilulindwa Sulusi kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Meneja wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasures, Alfred Mwita (kulia) na Mkurugenzi wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita wakimkabidhi zawadi Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mkurugenzi wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita akimkabidhi zawadi Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wahitimu wa darasa la saba wakijiandaa kupokea vyeti kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi vyeti kwa mhitimu wa darasa la saba kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi vyeti kwa mhitimu wa darasa la saba Shule ya Msingi Little Treasures

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa darasa la awali kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi vyeti kwa wahitimu darasa la awali Shule ya Msingi Little Treasures
Wahitimu wa darasa la saba wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wahitimu wa darasa la saba wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wahitimu wa darasa la saba wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wahitimu wa darasa la saba wakicheza muziki
Wahitimu wa darasa la saba shule ya Msingi  Little Treasures wakisoma risala kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wanafunzi wa Kidato cha tatu Shule ya Sekondari Little Treasures wakitoa burudani
Wanafunzi wa darasa la pili wakitoa burudani
Darasa la pili
Wahitimu wa darasa la saba wakiimba na kucheza muziki
Wanafunzi wa darasa la sita wakitoa burudani
Wanafunzi wa darasa la tano wakicheza muziki kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Wazazi wakiwa neno la shukrani kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Nabii Janeth akizungumza kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wafanyakazi wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasures wakicheza muziki kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya Tano ya darasa la saba 2021 katika Shule ya Msingi Little Treasures pamoja Mahafali ya 10 shule ya awali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Little Treasures.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Jeshi la Polisi latoa taarifa kuhusiana na makampuni binafsi ya ulinzi yasiyofuata masharti ya vibali vyao

Share:

Waziri Mchengerwa Aelekeza Kuwabadilishia Vituo Vya Kazi Maafisa Ununuzi Serikalini Ili Kukabiliana Na Vitendo Vya Rushwa

 Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaelekeza watendaji wa ofisi yake kuwa na utaratibu wa kuwabadilishia vituo vya kazi Maafisa Ununuzi na Ugavi wote waliokaa muda mrefu kwenye kituo kimoja ili kukabiliana na changamoto ya maafisa hao kujihusisha na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi Serikalini.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa amesema, wapo Maafisa Ununuzi na Ugavi waliokaa muda mrefu kwenye vituo vya kazi na kuona ofisi ni zao na hatimaye kuanza kufanya kazi kwa mazoea, hivyo ofisi yake inalazimika kuwa na utaratibu wa kuwahamisha ili kuendelea kusimamia uadilifu mahala pa kazi.

“Hakuna Afisa Ununuzi na Ugavi au mtumishi yeyote wa umma mwenye hati miliki ya kukaa muda mrefu kwenye kituo kimoja cha kazi na kuongeza kuwa, ofisi yake itahakikisha inawajibika kuendelea kulinda maadili ya utendaji kazi kwa watumishi wa kada zote,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Ameongeza kuwa, Maafisa Ununuzi na Ugavi watakaohamishwa wawe tayari kufanya kazi watakapopelekwa kwani ni jukumu la Watumishi wa Umma kuwatumikia wananchi mahala popote.

Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa, kitendo cha kuwabadilishia Maafisa hao vituo vya kazi kitasaidia sana kuongeza weledi na uwajibikaji mahala pa kazi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa kutoa maelekezo ya kuwa na utaratibu wa kuwabadilishia vituo vya kazi Maafisa Ununuzi na Ugavi ili waondokane na utendaji kazi wa mazoea unaosababisha wajihusishe na vitendo vya rushwa.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda amesema kwa kuwa takribani asilimia sabini ya matumizi yapo upande wa manunuzi hivyo katika kikao kazi hicho mada ya masuala ya ununuzi na ugavi itawasilishwa ili kujenga uelewa wa pamoja kwa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali katika eneo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameendelea kukemea vitendo vya rushwa kwa Watumishi wa Umma wa kada mbalimbali ikiwemo ya ununuzi na ugavi.

Share:

Majaliwa: Serikali Inatambua Mchango Unaotolewa Na Taasisi Za Kidini Nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inaheshimu, inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za kidini katika kujenga jamii ya wacha Mungu, wenye kutii mamlaka na sheria.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa taasisi za kidini kujiepushe kutumia nyumba za ibada kama majukwaa ya siasa na badala yake ziendelee kushirikiana na Serikali katika kujenga Taifa la watu wenye hofu ya Mungu, heshima, upendo na wenye kudumisha amani na utulivu nchini.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba Mosi, 2021) kwenye hafla ya uzinduzi wa msikiti wa Jamiu Assaliheen uliojengwa na taasisi ya Istiqaama katika Kata ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Pwani.  Msikiti huo una uwezo wa kutumiwa na waumini 500 kwa wakati mmoja na una vyumba vinne vya madrasa kwa ajili ya kutoa elimu ya dini na malezi mema.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kushirikiana na taasisi zote za kidini zenye nia safi na thabiti ili kuhakikisha miradi na mipango mbalimbali ya kijamii na kiroho yenye manufaa kwa umma wa Watanzania inaendelea kutekelezwa kama ilivyokusudiwa.

“Sote ni mashahidi kuhusu mchango mkubwa unaotolewa na madhehebu au taasisi za kidini katika jamii yetu. Taasisi za kidini nchini zimekuwa zikijihusisha kwa kiwango kikubwa na utoaji wa huduma za kijamii hususan elimu, maji, afya, kusaidia watu wenye uhitaji kama vile yatima na wajane sambamba na malezi na utoaji wa huduma za kiroho.“

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Jumuiya ya Istiqaama kwa kazi nzuri wanazozifanya nchini ikiwemo ya kujenga mshikamano baina ya waislamu wa madhehebu mbalimbali lakini pia baina ya waislamu na waumini wa dini nyingine . “Hivyo basi, tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote moyo wa subra na kujitolea katika mambo ya heri.“

“Aidha niwapongeze kwa kazi nzuri ya kujenga misingi mizuri ya kiroho na kimaadili kwa vijana wetu ambao ndiyo Taifa na viongozi wetu wa kesho. Jambo hili ni la msingi sana kwani ni dhahiri kuwa hakuna Taifa lolote duniani linaloweza kufanikiwa bila ya kuwa na misingi imara ya kiroho na kimaadili.“

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Istiqaama Tanzania Sheikh Badar bin Sood amempongeza Mheshimiwa Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuendeleza umoja, amani, mshikamano na maendeleo kwenye kila nyanja kwa Watanzania wote.

Naye, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar bin Zubeir bin Ally amewakumbusha waumini wa dini ya kiislam na watanzania kwa ujumla kujitokeza kuchanja chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19 ili kuongeza kinga na kujilinda na ugonjwa huo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Jumuiya ya Istiqaama Tanzania Sheikh Khalifa, Sheikh, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Istiqaama Tanzania, Sheikh Seif Ally Seif, Naibu Balozi wa Oman nchini, Dkt. Salim Al Harbin, Mwakilishi wa Mufti wa Oman, Sheikh Dr Wail Al Harasi.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Share:

Waliovamia Eneo La Farm Chamwino Ikulu Wapewa Wiki Mbili Kuondoka

 Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Serikali imeagiza wananchi waliovamia eneo la Farm katika kijiji cha Chamwino Ikulu mkoani Dodoma kuondoka katika kipindi cha wiki mbili kuanzia Oktoba 2, 2021 kwa kuwa   kijiji hicho kilishatangazwa eneo la mpango mwaka 1992 kupitia GN Na 263 ya tarehe 25 Juni 1992 ili kuepusha sheria ya ardhi ya vijiji (Sura 114 Toleo la 2002) kutumika.

Agizo hilo limetolewa leo Oktoba 1, 2021 na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya wakati wa kutangaza maamuzi ya timu ya uchunguzi wa mgogoro wa eneo la Farm mbele ya wananchi wa kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma.

"Natoa tamko la serikali kwa niaba ya kamati ya ulinzi ya wilaya na wananchi wa kijiji cha Chamwino naagiza wanaokalia maeneo ndani ya eneo la Farm kuondoka ndani ya wiki mbili na watakaokaidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao" alisema Gift Msuya.

Sehemu ya eneo la shamba la Farm lenye ukubwa  wa ekari 640 lililoanzishwa kati ya mwaka 1971/1972 na Hayati baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa lengo la kuwafunza wanakijiji cha Chamwino ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa, mbuzi, kondoo, nguruwe na kuku lilivamiwa na kuzua mgogoro kati ya wananchi na serikali.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Chamwino, mwananchi yeyote aliyeingia ndani ya eneo hilo ni marufuku kufanya shughuli yoyote kama vile ujenzi, kilimo na serikali kupitia idara ya ardhi itaweka mabango katika eneo hilo kuonesha kuwa eneo hilo ni eneo la umma.

‘’Wanaoendelea kufanya ujenzi watakuwa wanajiingiza hasara na wananchi mwenye yeyote mwenye nyaraka za kumilikishwa sehemu ya eneo hilo la Farm afike ofisi ya mkuu wa wilaya na atapatiwa haki yake’’. Alisema Gift Msuya

Kwa upande wake Kamishna wa ardhi nchini Nathaniel Nhonge alisema, kumbukumbu katika eneo hilo zimeweka bayana kuwa, eneo lenye mgogoro la Farm lilitolewa kwa matumizi ya umma na hakuna mabadiliko yaliyofanyika kwenda kwa mtu mmoja mmoja.

"Kimsingi hakuna mtu aliyelipwa fidia ndani ya eneo la Farm na wale wananchi waliolipwa kimakosa wanatakiwa warejeshe fedha". Alisema Nhonge

Alisema, baada ya ripoti ya tume ya uchunguzi kuhusiana na mgogoro huo sasa upimaji utafanyika eneo lililotolewa kwa matumizi ya taasisi za shule ya sekondari Chamwino, Shule ya Msingi Kikwete pamoja na eneo la Mahakama na kuyamilikisha kwa wahusika kuepuka migogoro hapo baadaye.

"Serikali itaweka utaratibu wa kudumu wa kubaini na kulinda maeneo mengine ya aina hii yaliyoko ndani ya Chamwino dhidi ya uvamizi wa wananchi". alisema Kamishna Nhonge.

Hata  hivyo,  baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chamwino wameonesha kutoridhishwa na maamuzu hayo kwa kueleza kuwa maeneo hayo walirithi na kuridhiwa na serikali ya kijiji kwa nyakati tofauti ingawa hawakuwa na nyaraka zozote zinazoonesha kumilikishwa maeneo hayo.

Eneo la Farm katika kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma limekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu uliosababisha kuundwa kwa timu maalum ya kushughulikia mgogoro huo.

Wakati wa kushughulikia mgogoro timu ya uchunguzi ilielezwa kuwa, shamba la Farm lilitolewa kwa serikali ya kijiji miaka ya 1971/1972 kwa matumizi ya mradi wa mifugo na baada ya mradi kufa mwaka 1995 baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo kabla ya Farm kuanzishwa walirudi kwenye eneo hilo na wengine waliomba serikali ya kijiji kwa ajili ya kulima shamba hilo kwa muda.

Hata hivyo, Serikali ya kijiji cha Chamwino ilitoa sehemu ya eneo hilo kujengwa shule ya Sekondari ya Chanwino mwaka 1995 na sehemu ya shamba hilo lililotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Kikwete 2007.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Kijiji Na 4/1999 kifungu cha 13 (7) inaeleza kuwa ardhi iliyotengwa na halmashauri ya kijiji au mkutano wa kijiji kwa matumizi ya jumuiya/umma au ardhi ambayo wenyeji wa eneo husika wanaitumia kama ardhi ya kijiji ya umma kabla ya kutungwa kwa sheria ya ardhi, ardhi hiyo ni ya ardhi ya kijiji. Pia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 kifungu cha 12 (1) inakataza ardhi ya jumla kutolewa kwa mtu binafsi.

Share:

Hukumu Ya Ole Sabaya Na Wenzake Yaahirishwa Hadi Oktoba 15, 2021.

Hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili iliyokuwa itolewe leo imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021.

Akiahirisha hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Amalia Mushi amesema bado hukumu hiyo haijakamilika kuandikwa.

Sabaya na wenzake, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha. Inadaiwa katika shtaka la kwanza kuwa Februari 9, 2021 katika Mtaa wa Bondeni, Arusha, washtakiwa hao waliiba Sh2.769 milioni, mali ya mfanyabiashara Mohamed Saad.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa kabla na baada ya kufanya wizi huo, washtakiwa waliwashambulia Numan Jasin, Harijin Saad Harijin, Bakari Msangi, Salim Hassan na Ally Shaban kwa kuwapiga kwa kutumia bunduki, ili kufanikisha wizi huo.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger