Sunday, 19 September 2021

MBUNGE WA JIMBO LA NAMTUMBO ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA GARI



Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa amepata ajali katika eneo la Nalasi wilayani Tunduru akiwa kwenye ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme ambaye ana ziara leo huko Namtumbo, mkoani Ruvuma. Mbunge huyo alikuwa watu wengine watatu kwenye gari na wote wametoka salama.( Picha na CCM Makao Makuu)
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa akiwa amenusurika kwenye ajali ya gari lake alilokuwa akilitumia katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Christine Mdeme.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa akizungumza na Bw. Nasoro Hassan Dereva wa CCM Makao Mkuu mara baada ya kunusurika kwenye ajali ya gari lake alilokuwa akilitumia katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Christine Mdeme.

Share:

PINDA ATAKA CCM USHINDI WA KISHINDO JIMBO LA USHETU, KATA YA NDEMBEZI

 


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Shinyanga.


Na Marco Maduhu, Shinyanga

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, amekitaka Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Shinyanga, kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ushetu wilayani Kahama, na Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Alibainisha hayo jana wakati akizungumza na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Shinyanga, alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kuzindua rasmi mashindano ya michezo ya Umoja wa Vijana wa Chama hicho UVCCM GREEN CUP Kitaifa, katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Alisema Jimbo la Ushetu lilikuwa chini ya Marehemu Elias Kwandikwa, na Kata hiyo ya Ndembezi ilikuwa chini ya Marehemu David Nkulila, ambao wote walitoka Chama Cha Mapinduzi CCM, na walifariki Agosti mwaka huu siku tofauti, hivyo ni vyema kuwaenzi kwa kuwapatia viongozi wanaotokana na CCM.

“Katika uchaguzi mdogo wa wa Jimbo la Ushetu na Kata ya Ndembezi sina shaka tutashinda, na ili kuwaenzi viongozi hawa waliotangulia mbele ya haki, lazima tushinde kwa Kishindo, na nina kuomba Emmanuel Charahani ambaye umepitishwa na chama kugombea Jimbo la Ushetu, ujinyenyekeze kwa wapiga kura ili upate kura nyingi,”alisema Pinda.

Pia alikitaka Chama hicho kujiimarisha zaidi kwenye mashina, zikiwemo jumuiya za vijana, wazazi, na wanawake ili kukijenga chama, na wakifanikiwa kwenye hilo hakuna uchaguzi wowote watakaoshindwa, zikiwamo chaguzi zijazo wa Serikali za Mitaa 2024, na uchaguzi Mkuu 2025.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Shinyanga Mabala Mlolwa, alimhakikishia Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kuwa katika uchaguzi huo mdogo Jimbo la Ushetu na Kata ya Ndembezi watahakikisha wanapata ushindi wa kishindo,

Aidha katika Jimbo hilo la Ushetu lilikuwa chini ya Marehemu Elias Kwandikwa, ambaye pia alikuwa Waziri wa ulinzi, na katika Kata ya Ndembezi, ilikuwa chini ya David Nkulila ambaye alikuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga, ambapo tayari Tume ya Taifa (NEC) imeshatangaza uchaguzi mdogo kwenye majimbo yote pamoja na kata.


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akizungumza kwneye kikao hicho.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Muhsin Zikatim, akisoma taarifa ya UVCCM kwenye kikao hicho.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

Na Marco Maduhu- Shinyanga

Share:

BIASHARA YANGU, BIASHARA YAKO, PROGRAMU YA BARRICK YA KUWAJENGEA WAJASIRIAMALI UWEZO WA KUJIKOMBOA KIUCHUMI


Baadhi ya Wajasiriamali wanaowezeshwa na Barrick wakionesha bidhaa zao katika moja ya maonyesho ya biashara
Baadhi ya Wajasiriamali wanaowezeshwa na Barrick wakionesha bidhaa zao katika moja ya maonyesho ya biashara
Baadhi ya Wajasiriamali wanaowezeshwa na Barrick wakionesha bidhaa zao katika moja ya maonyesho ya biashara
Kuna msemo maarufu wa Kichina usemao kuwa Usimpe mtu samaki, mfundishe kuvua ili asiendelee kuomba Samaki bali avue mwenyewe.Kampuni ya madini ya Barrick inatekeleza msemo huu kwa vitendo kutokana na kutekeleza programu ya kuwapatia wajasiriamali wanaoishi karibu na migodi yake ijulikanayo kama ‘Biashara yangu biashara yako’.

Mafunzo haya ambayo hutolewa na wataalamu wa masuala ya biashara na ujasiriamali yamefanikiwa kuwawezesha wajasiriamali wengi wa maeneo hayo hususani wanawake kusimama kiuchumi na kuendesha shughuli zao kwa utaalamu na kujiamini.

Wajasiriamali ambao wamenufaika na programu ya mafunzo haya, ni wale wanaojishughulisha na kilimo, ufugaji wa kuku, wazalishaji wa uyoga,ushonaji,watengeneza nguo za batiki, mafundi ujenzi na shughuli nyingineo nyingi.

Katika mahojiano yaliyofanyika karibuni, mmoja wa wanufaika wa progarmu hii,Clementina Felix, mkazi wa Bugarama wilayani Kahama, anayejishughulisha na biashara ya ushonaji kwa niaba ya wenzake ,aliishukuru kampuni ya Barrick, kwa uwezeshaji mkubwa inaofanya kwa wajasiriamali wa wilaya hiyo kwa kuwapatia mafunzo ya biashara na kuwaunga mkono katika shughuli zao za ujasiriamali.

“Barrick, inawezesha wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka vijiji 14 vilivyopo katika kata za Mwingiru, Bulyanhulu na Bugarama, ambapo tumekuwa tukipatiwa mafunzo ya biashara na kuwezeshwa kushiriki maonyesho mbalimbali pia bidhaa tunazozalisha soko letu kubwa tunalitegemea kutoka kwa wafanyakazi wa mgodini”, alisema Clementina.

Akiwa fundi wa ushonaji anasema amefanikiwa kubuni makoti ambayo yanavutia watu wengi katika soko, ambapo pia amefankiwa kupata soko kutoka kampuni ya Barrick kwa ajili ya wafanyakazi wake na amekuwa na masoko ya nje ambayo amekuwa akiyapata kutokana na kuwezeshwa kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya biashara.

Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19,wapo wajasiriamali wenzake ambao wanashona barakoa na kuweza kuziuaza katika masoko mbalimbali na kujikwamua kiuchumi sambamba na kuboresha maisha ya familia zao ikiwemo kuboresha makazi yao na kusomesha watoto.

Mjasiriamali mwingine,Berita Nyawanga anasema kuwa tangu aanze kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na Barrick kupitia programu ya Biashara yangu biashara yako ,shughuli zake zinaenda vizuri na ameweza kugundua kuwa sio mtai pekee unahitajika kufanikiwa kibiashara bali mafunzo ya uendeshaji biashara ni muhimu na ndio nguzo kubwa ya mafanikio.

Nyawanga, aliongeza kusema kuwa Barrick imeleta ukombozi katika maeneo yao, hususani kwa wanawake ambao walibaki nyuma katika shughuli za kujikwamua kiuchumi lakini kwa sasa wamekuwa na mwamko mkubwa kushiriki katika shughuli za ujasiriamali na wanaweza kujipatia vipato badala ya kuwa tegemezi kwa wenzawao kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa upande wake Ester Lali, ambaye anashughulika na ufugaji wa nyuki katika kijiji cha Kakola wilayani Kahama,alisema Barrick, inaendelea kuwezesha wana vijiji kuchangamkia ufugaji wa nyuki kupitia kuwaleta wataalamu wa kuwafundisha ufugaji bora wa nyuki.

“Mwamko wa ufugaji wa nyuki unaendelea kuwa mkubwa na wapo wafugaji wameanza kupata asali bora na wanaendelea kuiuza katika masoko mbalimbali nchini na kinachofurahisha anawake wengi na vijana wanaendelea kujitokeza kuchangamkia fursa hii”,alisema Lari.

Afisa Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu, Sebastian Antony, amesema programu ya mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali imepokelewa vizuri na inaendelea kuwanufaisha,ambapo wapo ambao biashara zao zinazidi kukua siku hadi siku na baadhi yao wamefikia hatua ya kuzalisha ajira kutokana na shughuli zao.

Antony alisema kuwa pia wanavijiji wanaoishi jirani na mgodi kupitia mafunzo haya wameweza kutambua fursa za kibiashara zilizopo katika maeneo yao ambapo wameanza kuzichangamkia na kuweza kujipatia vipato kupitia kujiajiri.

Barrick imedhamiria kuhakikisha wananchi wanaoishi jirani na maeneo yake ya kazi wanaendelea kunufaika na shughuli za uchimbaji wa madini, kupitia sera ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa madini kupitia kupewa kipaumbele katika kuuza na kutoa huduma migodini.
Share:

MBUNGE WA MASWA MAGHARIBI MASHIMBA NDAKI AZIDI KUTOA MISAADA KWA JAMII



Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Ndaki agawa jezi 13 kwa timu za mpira katika jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ahadi zake katika kukuza sekta ya michezo katika jimbo hilo na kuwahamasisha vijana kucheza kwa bidii na kuhakikisha wanafikia malengo ya kucheza katika timu kubwa ndani na nje ya nchi.

Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa kwenye picha ya pamoja na vijana kutoka katika timu 13 za mpira wa miguu baada ya kugawa jezi na mipira katika timu hizo zilizopo katika Jimbo la Maswa Magharibi na kuwataka kuhakikisha jezi na mipira inatumika katika malengo yaliyokusudiwa ya kukuza sekta ya michezo katika jimbo hilo.


Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Ndaki akitoa msaada wa magongo ya kutembelea kwa mmoja wa walemavu wa miguu ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa watu wenye mahitaji maalum katika jimbo hilo.


Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Ndaki akitoa msaada wa baiskeli maalum kwa ajili ya walemavu wa miguu kwa mmoja wa walemavu ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa watu wenye mahitaji maalum katika jimbo hilo.


Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Ndaki akitoa msaada wa fimbo malum ya kumuongoza mlemavu asiyeona ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa watu wenye ulemavu huo katika jimbo lake ikiwa ni muendelezo wa misaada mbalimbali ambayo amekuwa akitoa kwa wenye mahitaji maalum.

Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Ndaki akitoa msaada wa fimbo malum ya kumuongoza mlemavu asiyeona ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa watu wenye ulemavu huo katika jimbo lake ikiwa ni muendelezo wa misaada mbalimbali ambayo amekuwa akitoa kwa wenye mahitaji maalum.



Share:

VYAMA 16 VYACHUKUA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA USHETU

NEC Habari, Ushetu- Shinyanga
Vyama 16 vya siasa vimejitokeza kuchukua fomu za uteuzi kugombea kiti cha Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Ushetu Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga unaotarajiwa kufanyika tarehe 9 Oktoba mwaka 2021.

Vyama vilivyojitokeza kuchukua fomu za uteuzi hadi kufikia tarehe 18 Septemba mwaka 2021 saa 10:00 jioni ni Chama cha DP, Chama cha CHAUMMA, NRA, ADC, AAFP, Sauti ya Umma (SAU),

Vyama vingine vilivyochukua fomu ni Cha cha ADA TADEA, UPDP, TLP, Demokrasia Makini, UMD, NLD, UDP, CCK, CCM na Chama cha ACT Wazalendo.

NEC Habari imeshuhudia baadhi ya wagombea wakichukua fomu za uteuzi huku kikuwepo na ushindani kati ya wanawake na wanaume ambapo kati ya vyama 16 vilivyochukua fomu, vyama nane (8) vimewakilishwa na wanawake.

Vyama vilivyoteua wawakilishi wanawake kuchukua fomu za uteuzi ni Chama cha ADC, AAFP, SAU, ADA-TADEA, UPDP, UMD, NLD na Chama cha CCK.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ushetu Bw. Linno Pius Mwageni amesema fomu za uteuzi kwa wagombea wa kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo zimeanza kutolewa tarehe 13 hadi tarehe 19 kesho Jumalipi itakuwa ni siku ya Uteuzi wa wagombea.

Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi  wa Jimbo la Ushetu Godfrey Samwel Lwambura amewataka wagombea hao kuhakikisha wanajaza fumo za uteuzi kwa usahihi na siku watakaporejesha fomu hizo watajaza Fomu Namba 10 ya kuheshimu Maadili ya Uchaguzi.

Kwa mujibu wa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Ushetu iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 20 Septemba, 2021 hadi tarehe 8 Oktoba, 2021 na Siku ya Kupiga Kura itakua tarehe 9 Oktoba mwaka 2021.



Share:

WAZIRI MKUMBO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI


...................................................................................

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Profesa Kitila Mkumbo amekutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu maendeleo ya Sekta ya viwanda na biashara nchini.

Waziri Mhe. Mkumbo amekutana na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries, Mark Ocitti pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Alfonso Velez leo tarehe 17/09/2021.

Katika Mkutano wake na Bakozi Concar, wawili hao walizungumzia maandalizi ya Kongamano la Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza linalotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Aidha, Balozi Concar amebainisha kuwa, Kongamano hilo limapata hamasa kubwa na kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi wa Uingereza na kuahidi kuja kushiriki hapa nchini na wengine kushiriki kwa njia ya mtandao.

Balozi Concar ameongeza kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya mwamko mkubwa wa kibiashara na uwekezaji uliopo nchini Tanzania katikabuongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Kwa upande wake, Waziri Mkumbo amemuhakikishia Balozi huyo kuwa, maandalizi yanaendelea vizuri na wafanyabiashara wa Watanzania wana shauku kubwa kushiriki Kongamano hilo kwa lengo la kutumia fursa zilizopo na kubaini fursa mpya za ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili hususan kuangalia namna gani bidhaa za Tanzania zinaweza kuuzwa nchini Uingereza.

Awali akikutuna na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti, Waziri Mkumbo alitumia fursa hiyo kupokea taarifa ya uzinduzi wa mradi wa upanuzi wa kiwanda cha Sengereti Breweries Kilimanjaro ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 23, 2021 ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa na manufaa makubwa nchini ikiwemo kuongeza ajira na kuchochea kilimo cha shayiri na mazao mengine ambayo kiwanda hicho hutumia kama malighafi.

Vile vile, Waziri Mkumbo alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, Alfonso Velez, na kukitaka kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa saruji nchini kulingana na mahitaji yanayohitajika nchini hususan katika kipindi hiki cha utekelezaji wa miradi kitaifa ya kimkakati ya kimaendeleo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 19,2021




















Share:

FKF YAMFUTA KAZI KOCHA MKUU WA TIMU YA TAIFA KENYA 'HARAMBEE STARS' JACOB MULEE GHOST

 
Shirikisho la mpira wa miguu Kenya (FKF) limefuta kazi kocha mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Harambee Stars Jacob Mulee maarafu Ghost.

Cha kushangaza ni kuwa, FKF imefanya uamuzi huo ikiwa ni wiki tatu tu kabla ya mchezo wa Kenya dhidi ya Mali wa kufuzu kushiriki kombe la dunia uliopangwa kufanyika octoba 6 mwaka huu nchini Morocco.

Katika toleo kwa waandishi wa habari, FKF walisema,

“Kocha mkuu wa Harambee Stars Jocob Mulee na msaidizi wake Twahir Muhiddin na kocha wa walindamlango Haggai Azamde wamekubaliana kuondoka”.

Toleo hilo liliongeza na kusema pia, “Wasaidizi wa makocha Ken Odhiambo na William Muluya watabaki kufanya kazi katika benchi la ufundi wakati Kenya ikijiandaa kuminyana na Mali ili kufuzu kushiriki kombe la dunia 2022”.

Share:

Saturday, 18 September 2021

WAZIRI JAFO ATAKA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA, KUIFANYA DODOMA KUWA YA KIJANI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wakazi wa Kongwa kuhusu agenda ya mazingira mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani hapo.
Baadhi ya wakazi wa Kongwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) aliyefanya ziara ya siku moja Wilaya hapo leo kuhamasisha utunzaji mazingira.

Na Dotto Kwilasa, Dodoma.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ametoa rai kwa wakazi wa Kongwa kutoa msukumo wa dhati katika agenda ya mazingira kwa  kupanda miti rafiki kwa mazingira.

Akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Kongwa Waziri Jafo ametoa rai hiyo leo  na kuwataka kuunga mkono juhudi za Serikali za kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani.

"Ndugu zangu Kampeni ya kukijanisha Dodoma ni endelevu, na Kongwa ni sehemu ya Mkoa wa Dodoma, natoa rai kwenu mpande miti kwa wingi, sambamba na kilimo cha Korosho kama zao la kimkakati" Jafo amesisitiza.

Amesema agenda ya mazingira iende sambamba na upandaji wa miti kwa kila kaya walau miti mitatu ikiwemo ya kivuli na matunda ili jamii iweze kunufaika nayo sambamba na hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na ulinzi endelevu wa miundombinu kama vile barabara na madaraja.

 "Kongwa ya sasa si sawa na Kongwa ya zamani kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu kama Ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa,"amesema Jafo.

Pamoja na hayo Waziri Jafo amesema Ofisi yake imezindua Kampeni Kabambe ya Kitaifa ya Uhifadhi na Usafi wa Mazingira kwa lengo la kunusuru taifa na majanga yatokanayo na uharibifu wa mazingira huku akisisitiza  kuwa kila kaya inapaswa kupanda miti walau mitatu ya kivuli pamoja na matunda hali itakayosaidia kuhifadhi miundombinu ya barabara na madaraja.

Kutokana na hayo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa  Remidius Emmanuel amesema Wilaya  yake inaendelea kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuhimiza kutokata miti, kutoharibu vyanzo vya maji, kutovamia misitu.

Amesema kwa kutilia mkazo jambo hilo tayari Wilaya hiyo  imepanda miti na kuhifadhi visiki asili 1,470,252 ambavyo vimeainishwa na kutunzwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo
Share:

WACHIMBAJI WATAKIWA KUKATA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI GEITA


Mtakwimu wa tume ya madini Azihar Kashakara akieleza utendaji kazi na maboresho ya tume hiyo kwa kamati ya siasa ilipotembelea kwenye banda hilo. Picha zote na Alphonce Kabilondo
Mwenyekiti wa Chama Cha wachimbaji wadogo mkoa wa Geita Christopher Kadeo akitoa maelezo mbele ya kamati ya siasa ilipotembelea kwenye banda hilo.
Kamati ya siasa ikipata maelezo kutoka kwa afisa masoko mwandamizi wa mfuko wa bima ya afya (NHIF) Flora Mataba


Na Alphonce Kabilondo,Geita

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita mkoani Geita imewataka wachimbaji wadogo kukata leseni za uchimbaji katika maeneo yao ili kuondoa migogoro pindi yanapoibuka madini ya dhahabu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Barnabas Mhoja Mapande ametoa kauli hiyo leo alipotembelea mabanda ya maonesho ya nne ya teknolojia ya uchimbaji madini yanayoanyika eneo la EPZ mjini Geita.

Mapande amesema kuwa hao wachimbaji wadogo hawana budi kufika ofisi ya tume madini kuomba leseni ya uchimbaji ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea pindi madini yanapoibuka kwenye maeneo yao.

Aidha kamati hiyo ikiwa kwenye banda la tume ya madini imetumia fursa hiyo kuipongeza tume ya madini kwa kuboresha utoaji wa leseni kwa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wananchi wachimbaji wadogo wa madini kujitokeza kwenye maonesho haya kuona na kujiunza teknolojia ya uchimbaji wa kisasa”, alisema Mwenyekiti.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Mkoani Geita (GEREMA) Christopher Kadeo ameiambia kamati hiyo kuwa baadhi ya wachimbaji wameingiwa na sintofahamu baada serikali ya kuwapa notisi za kukusudia kuwafutia leseni zao.
Share:

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AONDOKA NCHINI KUELEKEA MAREKANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo tarehe 18 Septemba, 2021. PICHA NA IKULU

Share:

POLISI ARUSHA YANASA MTANDAO WA WIZI WA PIKIPIKI , RPC AWAITA WANANCHI 'CENTRAL'


Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sita wa wizi wa pikipiki baada kufanya operesheni katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Justine Masejo alisema Operesheni hiyo iliyoanza tarehe 12 Septemba 2021 ni endelevu. 

Kamanda Masejo alisema watuhumiwa watano walikamatwa jijini Arusha na mmoja alikamatwa katika maeneo ya Mto wa Mbu wilayani Monduli, huku mmoja wao ambaye ni mkazi wa Kwa Mrefu jijini Arusha alikutwa na pikipiki nne, kadi nane za pikipiki pamoja na mikataba ya mauziano. 

“Jumla ya Pikipiki zilizopatikana ni tisa ambazo ni Toyo yenye namba za usajili MC 201 ABB, Toyo Power yenye namba za usajili MC 816 BHX rangi nyeusi, Honda Daz yenye namba za usajili T. 744 AZP rangi nyeusi.

Zingine ni Kinglion yenye namba za usajili MC 763 CBU, Sinoray yenye namba za usajili MC 600 CBR, Kinglion nyekundu yenye namba za usajili MC. 783 CFW, Kinglion yenye namba za usajili MC 306 CGD, Sinoray yenye namba za usajili MC 492 BPZ na Sinoray yenye namba za usajili MC 718 CHU.”

Kamanda Masejo alibainisha kwamba, wakati wa mahojiano watuhumiwa hao walikiri kushiriki kutenda matukio hayo ya uhalifu mkoa hapa na kisha kuuza mikoa ya jirani.

Aidha kupitia taarifa hiyo, Kamanda Masejo amewaarifu wananchi walioibiwa Pikipiki kufika katika kituo kikuu cha Polisi Arusha wakiwa na viambatanisho  vya umiliki kwa nia ya kuzitambua.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa waendesha Pikipiki maarufu kwa jina la “Boda Boda” kuendelea kuchukua tahadhari za usalama wao na mali zao pindi wanapowahudumia abiria hasa nyakati za usiku.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger