Monday, 2 August 2021

SERIKALI KUPELEKA CHANJO YA CORONA MAKAMBI YA WAKIMBIZI

 Na Abubakari Akida,MOHA
Serikali imesema iko katika mpango wa kupeleka Chanjo ya UVIKO 19 katika Makambi na Makazi ya Wakimbizi katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi ikiwa ni mpango mkakati wa kukabiliana na wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Katumba kinachotumiwa na wakimbizi na raia wapya wanaokadiriwa kufikia 86,233  toka nchini Burundi ambao walikimbia mapigano ya kikabila yaliyotokea nchini kwao 1974.

“Katika kukabiliana na janga la UVIKO 19 tayari Wakuu wa Makambi washaanza  kutambua idadi ya watu ambao wanauhitaji wa hiari wa kupata chanjo hiyo ili jamii ya wakimbizi wanaokaa katika makambi yaliyopo nchini ili muda ukifika tuwe na takwimu sahihi za wanaohitaji kuchanjwa na tayari kama mnavyoona tayari zoezi la chanjo lishaanza baada ya siku chache kuzinduliwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu,wito pekee naotoa kwa wakimbizi kufuata ushauri wa wataalamu wa afya katika kujikinga na maradhi hayo ambayo dunia sasa inapitia” amesema Naibu Waziri Chilo

Akizungumzia idadi ya wagonjwa wa UVIKO 19 katika Kituo cha Afya Katumba, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,Dkt.Veneranda Msati amesema hawana mgonjwa aliyefika kituoni huku akielezea utolewaji wa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwa wagonjwa na mama wajawazito wanaofika katika kituo hicho kupata huduma.

“Kwasasa katika kituo chetu hatuna mgonjwa yoyote wa Corona tunachofanya ni kutoa ushauri wa kujikinga na maradhi hayo kwa wagonjwa wanaofika hapa kupata huduma za afya ikiwemo na akina mama wajawazito lakini pia tunatuma wataalamu wetu wa afya kwenda kuwafundisha wananchi katika makazi yao jinsi ya kunawa kwa maji safi tiririka na kukaa umbali unaoshauriwa ili kuepuka maambukizi ya UVIKO”amesema Dkt. Veneranda

Awali akisoma taarifa ya makazi hayo,Mkuu wa Makazi ya Katumba,John Mwita amesema hali ya usalama ni shwari huku wakiendelea kutoa elimu na kufuata sheria za kuishi katika makazi kwa wakimbizi hao.

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA

Share:

MREMBO AKAMATWA BAADA YA JAMAA ALIYEKUWA ANACHONYA NAE ASALI HOTELINI KUFARIKI

Polisi katika kaunti ya Kiambu Ndumberi nchini Kenya wamemkamata mwanamke mmoja baada ya jamaa aliyekuwa akipalilia mgomba wakiwa kwenye chumba cha anasa kufariki dunia.

Wawili hao walikuwa katika chumba kwenye hoteli ya Konteina walipokuwa wakionja tunda la penzi. 

Moses Muiruri aliamua kukodi chumba hicho baada ya wawili hao kuonja chupa kadhaa Ijumaa Julai 30,2021.

 Duru kwenye mkahawa huo ziliambia gazeti la Standard kuwa wawili hao waliingia kwenye chumba nambari saba saa 4:30 asubuhi.

 Kufikia Jumamosi Julai 31, kipusa huyo alijaribu kutoroka kutoka hoteli hiyo baada ya mambo kuenda sege mnege.

 Polisi waliitwa baada ya Muiruri kupatikana kwenye chumba hicho akiwa amefariki dunia.

Mkuu wa polisi Ndumberi Badel Mohammed alisema mwendazake alipatwa akivuja damu kutoka mdomoni.

Kisa sawa na hicho kiliripotiwa Murang'a ambapo buda alizimia na kufariki dunia katika chumba alipokuwa na mpenziwe.

 Frederick Opiyo alikuwa kwenye mkahawa wa Rurago saa tatu usiku Julai 27 akiwa na mpenzi wake Mary Mwende Munyalo kabla ya kuzirai na kuzima. 

Mwende alisema alikuwa akuioga wakati ambapo aliskia dume huyo akiunguruma huku akiwa na matatizo ya kupumua.

 Polisi walisema walifika katika eneo la mkasa na kupata vifaa vya kazi vikiwamo mipira ya kondomu na pia dawa za kuongeza nguvu za mapenzi.
Share:

SERIKALI YAAGIZA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI KUTOA AJIRA VIJIJINI

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili uliofanyika tarehe 01/08/2021 katika Kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akitoa maagizo kwa wakandarasi na wasimamizi wa miradi kuhakikisha kuwa kifaa mbadala cha wiring UMETA kinapatikana ili wananchi wasiomudu gharama za wiring waweze kuvitumia kwa ajili ya kuunganishiwa umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge akiongea na umati wa wananchi wa Kijiji cha Nalasi kilichopo Wilaya ya Tunduru ambako uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili uliofanyika tarehe 01/08/2021.
Watoto wakifuatilia matukio ya uzinduzi.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwakabidhi wazee kifaa cha UMETA ambacho ni mbadala wa wiring ili waweze kuunganishiwa umeme katika nyumba zao.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mkuu wa Ruvuma Brigedia Jenerali,Balozi Wilbert Ibuge pamoja na viongozi mbalimbali wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Agosti 1,2021.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mkuu wa Ruvuma Brigedia Jenerali,Balozi Wilbert Ibuge pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga Makofi mara baada ya kuzindua Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Agosti 1,2021.

........................................

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ameagiza wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini kutoa kipaumbele cha ajira kwa vijana waliopo katika vijiji ambapo miradi hiyo inatekelezwa.

Dkt. Kalemani alitoa agizo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Agosti 1,2021 katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru.

“Wakandarasi chukueni vibarua kutoka katika vijiji ambavyo mnapeleka umeme” alisema na kuongeza kuwa lengo ni kufanya miradi hiyo iwe na tija kwa kuwashirikisha wananchi katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.

Aidha, Mhe. Kalemani amesema Serikali itatumia zaidi ya Shilingi bilioni 71 kwa ajili ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vijiji 265 ambavyo havina huduma ya nishati hiyo katika Mkoa wa Ruvuma.

“Katika Mkoa wa Rvuma, vijiji vyenye umeme ni 289 kati ya 554. Kwa kutambua hilo leo ninawakabidhi wakandarasi waushambulie Mkoa wa Ruuma na kuhakikisha vijiji vyote vilivyosalia 265 vinapatiwa umeme kupitia mradi huu. Nipende kutoa rai kwa Watanzania wote kuwa kila Mtanzania atapata Nishati ya Umeme” alisema Waziri Kalemani.

Waziri Kalemani alisema kuwa Wilaya ya Tunduru ambako Mradi umezinduliwa kuna vijiji 85 ambavyo hadi sasa bado havijafikiwa na huduma ya umeme na kwa kutambua hilo, Serikali imetenga takribani Shilingi bilioni 23.52 kwa ajili ya kuvifikishia umeme vijiji hivyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge aliwataka wananchi wasihujumu miundombinu ya kusambaza umeme kwa kuiba nyaya na vifaa vingine na wawe walinzi wa miundombinu hiyo.
Share:

Relationship Manager; SME at NMB Bank

Relationship Manager; SME     Job Purpose Responsible for growing both Liabilities (Deposits) and Assets from Small and Medium Enterprises (SMEs) for Business banking; advising Business Banking department on business strategy, assisting SME Business Bankers /Relationship Officers/Branch Managers in recruiting business customers to ensure SME business growth. Main Responsibilities   Actively selling SME deposits, lending and […]

This post Relationship Manager; SME at NMB Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde Mhe.Sheha Mpemba Faki ajiuzulu.

Share:

Jengo la kudhibiti mifumo la kituo cha kupokea na kusambaza umeme cha Msamvu - Morogoro Lateketea Kwa Moto

Ofisi za Kituo kikubwa cha kupokea na kusambaza umeme Msamvu - Morogoro limewaka moto na kusababisha Mkoa wa Morogoro kukosa umeme.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, lakini taarifa ya TANESCO imeeleza kuwa wataalamu  na mafundi wanaendelea na kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa haraka. 

Share:

Mbunge wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpemba Faki ajiuzulu

Share:

PICHA: Rais Samia Awasili Nchini Rwanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali Nchini Rwanda kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Paul Kagame leo Agosti 02,2021.

Share:

Waziri Mkuu Atoa Rai Kwa Waliopata Ufadhili Wa Mafunzo Ya Ufundi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana waliopata ufadhili wa Serikali kupitia programu maalumu ya kupata mafunzo ya ufundi stadi watumie vizuri fursa hiyo ili wanufaike.

Amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fungu la fedha kwa ajili ya kuwasomesha vijana katika fani mbalimbali za ufundi stadi kwa muda wa miezi sita.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumapili, Agosti 1, 2021) wakati wa uzinduzi wa chuo cha Ufundi Stadi kilichopo katika kijiji cha Kipapa kata ya Lufilyo wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya.

“Kilichotuleta hapa ni kuja kushuhudia vijana wetu wa Kitanzania ambao wameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuwapatia ujuzi ili wakaendeleze kazi hizo.”

Amesema Tanzania nzima kuna vijana takribani 45,000 ambao wamesambazwa katika vyuo vyote vya Serikali na vya binafsi ambapo watapatiwa mafunzo ya ufundi stadi kwa miezi sita.
 
Waziri Mkuu amesema mbali na kupatiwa ujunzi katika vyuo hivyo pia vijana wengine wamepelekwa kwenye maeneo ya kutolea huduma kama za utalii, hoteli ili wapate ujuzi.

Amesema chuo hicho cha VETA Busokelo ni kimojawapo kati ya vyuo walivyovichagua ili kipokee vijana wa maeneo ya wilaya za Rungwe, Kyela, Chunya na Mbeya ili kuwapa ujuzi.

“Matarajio yangu vijana wote waliopata nafasi hii hawataipoteza, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatamani kuona kila Mtanzania akijishughulisha na shughuli za ujasiriamali.

Amesema mkakati wa Serikali kwa mwaka 2021 ni kusomesha vijana 80,000 ambapo asilimia 60 ya mafunzo hayo watayapata kwa vitendo na asilimia 40 watafundishwa darasani.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu alisema chuo cha Ufundi Stadi cha Busokelo kimedahili wanafunzi 127 ambao watapa mafunzo ya ufundi kupitia program hiyo.

Alisema kati ya wanafunzi hao 26 wanasomea ufundi seremala, 45 ushonaji nguo, 28 umeme wa majumbani, 18 ukarabati wa vitarakimishi na 10 utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki.

Alisema mafanikio ya programu hiyo ni pamoja na kuwawezesha wanafunzi waliopata ujuzi kuweza kujiajiri katika fani za useremala, ushonaji, udereva na matumizi ya vitarakinishi.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Share:

Manager, Mobile Lending and Analytics at Absa

Manager, Mobile Lending and Analytics    Bring your possibility to life! Define your career with us With over 100 years of rich history and strongly positioned as a local bank with regional and international expertise, a career with our family offers the opportunity to be part of this exciting growth journey, to reset our future […]

This post Manager, Mobile Lending and Analytics at Absa has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

People & Culture intern at Sokowatch

People & Culture intern   Dar Es Salaam, About Us: Sokowatch is transforming communities across Africa by revolutionizing access to essential goods and services. By connecting small shops to the digital economy, we fix inefficient supply chains and provide services that were previously unavailable. Sokowatch aims to provide everything a retailer needs, no wholesalers or […]

This post People & Culture intern at Sokowatch has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Field Sales Manager at Sokowatch

Field sales Manager Mbeya, About Us: Sokowatch is transforming communities across Africa by revolutionizing access to essential goods and services. By connecting small shops to the digital economy, we fix inefficient supply chains and provide services previously unavailable to informal businesses. Sokowatch aims to provide everything a retailer needs, no wholesalers or banks necessary. Thousands […]

This post Field Sales Manager at Sokowatch has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Director of People and Culture at European Management Solutions

Position: Director of People and Culture Duty station: South Africa or one of other country offices in Rwanda, Kenya, Nigeria, Ethiopia, Tanzania Hours: Full-time position; Reporting to: Regional Director of Africa Start date: As soon as possible Travels: Some occasional international travel post COVID-19 Salary package: Competitive salary, plus benefits (medical insurance and annual performance-based bonus). […]

This post Director of People and Culture at European Management Solutions has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Production Manager at Blue Recruits Limited

Production Manager   Blue Recruits Limited  Dar es Salaam Recruitment Consultant at Blue Recruits Limited We’re looking for a competent and experienced manager. Experience in the meat process industry is a requirement (meat/Poultry/Abattoir/Processed meat factory/food manufacturing, storage or handling industry etc.) Will be overseeing the day-to-day operations at food processing to ensure optimal product quality […]

This post Production Manager at Blue Recruits Limited has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

HAWA NDIYO WAKURUGENZI WAPYA WA HALMASHAURI SHINYANGA...MKRISTO ATUA MANISPAA YA SHINYANGA, MSUMBA ABAKI KAHAMA

Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson David Msumba
 ***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendji wa Halmashauri za Jiji, Miji, Manispaa na Wilaya ambapo kwa upande wa Mkoa wa Shinyanga amemteua Nice Remen Munissy kuwa Mkurugenzi wa wilaya ya Shinyanga, Charles Edward Fussi wilaya ya Msalala akichukua nafasi ya Simon Berege aliyepelekwa wilaya ya Maswa, Lino Pius Mwageni wilaya ya Ushetu, Jomary Mkristo Satura Manispaa ya Shinyanga huku akimbakiza  Emmanuel Johnson Matinyi katika wilaya ya Kishapu na Anderson Msumba katika Manispaa ya Kahama.
Share:

RAIS SAMIA ATEUA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI....TAZAMA MAJINA YOTE HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani

Share:

WAZIRI BITEKO ATEMBELEA BANDA LA SHUWASA AKIFUNGA MAONESHO SHINYANGA

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimwelezea Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kuhusu huduma zinazotolewa na SHUWAS alipotembelea Banda la SHUWASA akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021 . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akimwelezea Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kuhusu huduma zinazotolewa na SHUWAS alipotembelea Banda la SHUWASA akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021 .
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akizungumza kwenye Banda la SHUWASA akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021.

Soma pia:
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger