Tuesday, 13 July 2021
Monday, 12 July 2021
RC SENGATI ASEMA LAZIMA KIONGOZI WA CHADEMA ALIYESEMA SHINYANGA IMEELEMEWA NA WAGONJWA WA CORONA ACHUKULIWE HATUA KALI ZA KISHERIA
Waziri Gwajima Awataka Wahudumu Wa Afya Nchini Kuwa Wakarimu
Na Mwandishi Maalum – Dar es Salaam
Wahudumu wa afya nchini wametakiwa kuwa wakarimu wakati wanapowahudumia wateja na wagonjwa kwani kufanya hivyo wataongeza idadi ya watumiaji wa huduma watakaokwenda kutibiwa katika vituo vyao na kuvutiwa wajiunge na bima za afya na hivyo kuongeza mapato ya vituo husika na kupitia kuvutia wateja wa kimataifa watainua uchumi wa nchi kwa ujumla wake.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima wakati akizindua timu ya kuratibu hatua za Tanzania kuelekea kwenye utalii wa tiba katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Waziri Dkt. Gwajima alisema asili ya binadamu yeyote yule anahitaji kujaliwa, kuthaminiwa na kutambuliwa kama wahudumu hao wa afya wakifanya hivyo watapiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa.
“Hospitali zetu zina majengo mazuri, zina wataalamu wa kutosha na vifaa tiba vya kisasa vya kutosha kitu kinachokosekana ni ukarimu kwa wagonjwa, ili tuingie katika utalii wa matibabu kwa kila hospitali tunatakiwa kuwe na mabadiliko katika utendaji wa kazi ili mgonjwa achaguwe kwenda kutibiwa katika Hospitali yako”,.
“Imefika wakati sasa kwa hospitali kufungua kitabu cha utoaji huduma kwa mteja ili kila mfanyakazi anayelalamikiwa kwa kutoa huduma mbaya na anayesifiwa kwa kutoa huduma nzuri jina lake liandikwe humo, yule atakayelalamikiwa mara nyingi aweze kuchukuliwa hatua na yule ambaye jina lake litaongoza kwa kutoa huduma nzuri apongezwe”, alisema Dkt. Gwajima.
Waziri huyo wa Afya alisema utalii tiba siyo ngeni hapa nchini na tayari umeanza kufanyika, katika utalii huu mgonjwa anachagua hospitali ambayo inatoa huduma bora na nzuri na kwenda kutibiwa huko. Utalii huu unafanyika kwa watanzania wenyewe na kwa wagonjwa wanaotoka nje ya nchi na kuja kutibiwa hapa nchini kwa kufanya hivyo nchi inaongeza mapato pia tunaimarisha undugu kati ya nchi na nchi.
Dkt. Gwajima pia aliipongeza timu hiyo ya kuratibu hatua za Tanzania kuelekea katika utalii wa tiba na kusema inawataalamu wa kada mbalimbali wakiwemo kutoka sekta binafsi na kuwaagiza katika utekelezaji wa utalii tiba wasiziache Hospitali binafsi kwani nazo zina majengo mazuri, wataalamu wa kutosha na vifaa vya kisasa jambo la muhimu ni kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya utalii tiba kama zilivyo nchi zingine Duniani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Prof. Mohamed Janabi alisema kamati hiyo imependekeza utalii huo uanze kufanyika katika tiba ya moyo inatolewa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), matibabu ya figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), tiba ya upasuaji wa ubongo inayotolewa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na matibabu ya mionzi ya saratani yanayotolewa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road na baadaye ufanyike katika hospitali za kanda, mikoa na wilaya.
Prof. Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI alisema katika utalii tiba kuna watalii wa aina tatu ambapo kuna wagonjwa wanakuja kutibiwa nchini kutoka nje ya nchi na baada ya kupona wanarudi nchini kwao, kuna wagonjwa watakuja kutibiwa na baada ya kupona watakwenda kutalii katika vivutio mbalimbali vya utalii na kuna watalii ambao wanakuja kutalii nchini ambao wakipata matatizo ya kiafya watapata huduma za matibabu hapa nchini.
“Jambo la muhimu ni kuangalia ni jinsi gani Hospitali zetu zitatoa huduma ambazo zitawavutia watanzania pamoja na nchi mbalimbali za Afrika kutibiwa hapa nchini na siyo kwenda kutibiwa mahali pengine kwani tuna wataalamu wa kutosha, vifaa tiba vya kisasa na majengo mazuri”, alisema Prof. Janabi.
Naye Abdulmalik Mollel ambaye ni mjumbe wa timu hiyo na mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya utalii tiba ya GEL alisema hapa nchini kuna huduma nzuri za matibabu lakini kitu kinachokosekana ni lugha zinazotolewa kwa wagonjwa na wahudumu wa afya pamoja na namna ya utoaji wa huduma husika.
Alitoa mfano wa raia wengi wa visiwa vya Comoro wanavyotegemea kupata huduma za matibabu hapa nchini lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni lugha wao wanazungumza lugha ya Kifaransa na Tanzania lugha zinazotumika ni za Kiswahili na Kiingereza.
“Umbali kutoka uwanja wa ndege hadi zilipo Hospitali zetu za Taifa ambazo ni Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Saratani Ocean Road ni kilomita kama 10, Hospitali tatu kati ya hizi zipo katika eneo moja mahali ambapo mtu anatembea kwa miguu kutoka hospitali moja hadi nyingine”,.
“Mahali ilipo Taasisi ya Saratani Ocean Road siyo mbali na zilipo hospitali hizi zingine, hii ni tofauti na nchi zingine ambako umbali wa kutoka uwanja wa ndege hadi hospitali ni mrefu pia ilipo hospitali moja na nyingine ni mbali. Tatizo lililopo hapa kwetu ninamfahamu nani ili niende kupata huduma nzuri za matibabu lakini kama tutaamua kubadilika utalii wa matibabu unawezekana kabisa kufanyika”, .
Katikati ya mwezi wa sita mwaka huu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizindua mtambo wa Cathlab uliopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alisema ni wakati sasa umefika kwa Tanzania kuwa nchi ya utalii tiba kwani vifaa tiba vya kisasa vipo, wataalamu wapo pamoja na hospitali nzuri zipo.
Timu ya kuratibu hatua za Tanzania kuelekea kwenye utalii tiba inawajumbe 13 kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road, Bodi ya Utalii na sekta binafsi.
MWANAMKE AKUTWA MTUPU , AMEUAWA SHINYANGA MJINI
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mwanamke Lucia Michael maarufu Mama Kulwa, mkazi wa Majengo Manispaa ya Shinyanga, amekutwa ameuwa na watu wasiojulikana, na mwili wake kutupwa nyuma ya msikiti wa Majengo ukiwa hauna nguo 'mtupu'.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo aligundulika na majirani majira ya saa 12 asubuhi mara baada ya kuuona mwili wake ukiwa nyuma ya msikiti wa Majengo jirani na makazi yao akiwa mtupu.
Akielezea tukio hilo mmoja wa majirani Anastazia Amos, alisema baada ya kupata taarifa, alifika eneo la tukio na kumkuta jirani yake akiwa mtupu huku ameuawa, ndipo wakamfunika nguo na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa.
"Mwanamke huyu ni jirani yetu ana watoto watatu, na kazi yake ni msusi maarufu sana hapa mtaani kwetu, tunasikitika sana kumkuta akiwa ameuawa tena kavuliwa nguo zote," alisema Amosi.
Naye Mwenyekiti wa Majengo Manispaa ya Shinyanga Iddi Bwana, alisema mwanamke huyo huenda aliuawa na vibaka, na kisha mwili wake kutupwa nyuma ya Msikiti jirani na makazi ya watu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha kuwa Jeshi bado linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo chake na wahusika.
LHRC YAWAPIGA MSASA WA SHERIA , HAKI ZA BINADAMU WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA
TIGO YATOA FEDHA KUSAIDIA MATIBABU YA MIGUU PINDE
Mchango huu pia hutumika kama mpango wa uhamasishaji kwa umma juu ya umuhimu wa kufuata matibabu ili kuhakikisha wenye matatizo wanapona na kuzuia ulemavu.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika CCBRT, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema: "Mchango wetu unathibitisha zaidi kujitolea kwetu kusaidia jamii zinazotuzunguka. Matibabu ya miguu pinde nchini ni mada ambayo inahitaji utangazaji na kama kampuni ya simu inayoheshimika, tuko hapa leo kubadili hadithi, tunahitaji ushiriki wa jamii na nguvu ya kuhakikisha kwamba kila mtoto aliye na miguu pinde Tanzania, anapata matibabu bora na kwa wakati kwa kutumia njia ya Ponseti, kama matibabu ya kiwango cha juu na hivyo kuwapa fursa sawa ya kuishi maisha yenye tija kama walivyo wengine,".
Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi, aliishukuru Tigo kutokana na msaada huo endelevu ambao umekuwa ukisaidia kuokoa maisha ya watoto wengi Watanzania.
“Tigo Tanzania imeonyesha mfano kwa jukumu muhimu ambalo sekta binafsi imeamua kulichukua katika kuhakikisha inapunguza na kutatua shida za jamii.
“CCBRT, kwa miaka mingi imeweza kushughulikia moja ya mambo magumu zaidi ya matibabu ya miguu pinde, kuhakikisha matibabu yanakuwa endelevu na ufuatiliaji, kupitia uvumbuzi na msaada wa Tigo, kuna jukwaa la kukumbushana kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS), la CCBRT linaweza kutuma njia ya simu za mkononi kukuza ufuatiliaji ili wagonjwa watibiwe kikamilifu, bila athari yoyote.
“Kwa hivyo ningependa kuwahimiza sekta binafsi kuendelea kutupatia misaada ili kuhakikisha tunatokomeza tatizo hili na kulimaliza kabisa,” alisema.
Miaka mitatu iliyopita ya ushirikiano huu imeshuhudia karibu kesi 1,500 mpya za miguu pinde kwa watoto, wanaofaidika na matibabu ya miguu yanayobadilisha maisha kwa njia ya Ponset na mamia wamefanyiwa upasuaji CCBRT.
Katika miaka ya hivi karibuni, kesi hizo zimezidu kupungua na kwamba CCBRT inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kwa ajili ya kuhakikisha wanafikia malengo.
Fahamu Uwezo Wa Battery Wa Simu Ya Infinix Hot 10i.
Kampuni ya simu Infinix imekuwa ikitoa matoleo mbalimbali ya simu kulingana na kila rika na kipato cha Mtanzania. Infinix HOT 10i inamlenga zaidi mwanafunzi na Mtanzania mwenye kipato cha kati ambaye kutumia Tsh.320,000 ni sahihi kwa simu yenye sifa hizi;
Infinix HOT 10i imezingatia umuhimu wa kuangalia matukio mbalimbali kupitia simu endapo upo ambali na nyumbani basi kupitia wigo mpana wa kioo cha inch 6.51 unaweza kuangaza yote pasipo kupitwa na chochote.
Infinix HOT 10i ilizinduliwa rasmi tarehe 6/7/2021 na sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania kwa huduma ya haraka tafadhali piga 0744606222.