Monday, 12 July 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 12,2021




 

 

















Share:

Sunday, 11 July 2021

SIMBA BINGWA VPL MARA NNE MFULULIZO



Mabao mawili ya John Bocco na Chriss Mugalu kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Coastal Union uliopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa yametosha kuifanya Simba kutangaza ubingwa baada ya kufikisha alama 79 ambazo hakuna timu yeyote ya ligi inaweza kuzifikisha kwa msimu huu.

Simba wamechukua ubingwa huo kwa mara ya nne mfululizo tangu walivyofanya hivyo msimu wa 2017/2018.Simba imekuwa bingwa baada ya kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, huku bado ikiwa na michezo miwili kibindoni ligi kumalizika.

Mbali na ubingwa, Nahodha wa Simba, John Bocco ndiye anaongoza kwa ufungaji magoli akiwa na magoli 15 hadi sasa akifuatiwa Prince Dube wa Azam FC mwenye magoli 14.

Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama yeye anaongoza kwa assists ambapo amehusika kwenye magoli 15.
Share:

ASKOFU JACOB OLE AWATAKA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI YA CORONA


Na Jackline Lolah Minja Morogoro.

Waumini wa Dini ya Kikristo nchini wamesisitizwa kutouogopa ugonjwa Corona badala yake wachukue tahadhari ili kuweza kuushinda kwa maslahi ya Watanzania wote.

Akitoa  salamu kwenye Ibada maalumu ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa katika mtaa wa Bethania Usharika wa Mji Mwema Morogoro ,Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Morogoro Jacob Ole Mameyo amesema kwa sasa janga hilo limekuja kwa utofauti kuliko awali hivyo ni vyema kujilinda na kulinda wengine.

"Mwanzo Corona ilinyanyasa wazee , lakini sasa inamaliza hadi watoto hivyo nawasihi kujilinda na tusiiogope , Makuhani tuhakikishe tunalinda waumini wetu kutokana bila wao hatutaweza pata mapato kwa kuendeleza Kanisa." Alisema mameyo

Katika hatua nyingine  Askofu Mameyo amesema lazima Wakristo kudumisha upendo ili kutimiza kusudi la Mungu kwa wanadamu na kuepusha migogoro katika kanisa.

"Baadhi ya watu wamebadilisha maneno ya Biblia kuwa mpende jirani yako kama nafsi yako wanasema mpende jirani yako kama unanafasi hii sio sahihi, hivyo sio agizo la Mungu tusifanye ujanja ujanja badala yake tuzidi kumbembeleza Mungu atupokee kwenye uzima wa milele kwa kuwa hili ni agizo kuu kwetu wanadamu", alisema askofu Mameyo.
Share:

MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI YA UKWELI WILAYA YA SHINYANGA…LUTENI MWAMBASHI ATIA NENO

 


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude, kushoto, akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, tayari kwa kukimbizwa wilayani humo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi, ameweka mawe ya msingi na kuona miradi mbalimbali ya maendeleo Wilaya ya Shinyanga (Manispaa ya Shinyanga na wilaya ya Shinyanga), ambapo ameridhishwa na miradi hiyo na hakuna ambao ameukataa.

Zoezi la Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru kitaifa wilayani Shinyanga limefanyika leo Jumapili Julai 11,2021 mara baada ya Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude, kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko katika viwanja wa michezo Shule ya Sekondari Mwalukwa wilayani humo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi yote sita Luteni Mwambashi amesema ameridhishwa na miradi hiyo ambayo imeendana na thamani ya fedha (Value for Money), huku kukiwa na salio la fedha kwenye baadhi ya miradi, na kuagiza ile ambayo haijakamilika kujengwa ikamilishwe haraka ili ianze kutoa huduma.

“Nimekagua miradi yote iko vizuri, na nimeweka jiwe la msingi, na ile ambayo nimetoa maelekezo yafanyiwe kazi, pamoja na kuikamilisha ile ambayo bado ipo kwenye hatua ya ujenzi ili itoe huduma haraka kwa wananchi,”amesema Luteni Mwambashi.

Pia amewapongeza wananchi wa Bushushu kwa kujitoa kuchangia ujenzi wa Zahanati, ambayo itawasaidia kuondokana na adha ya kufuata huduma za matibabu umbari mrefu.

Akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, amewataka Watanzania, kudumisha amani, kuendeleza mapambano ya Rushwa, madawa ya kulevya, virusi vya Ukimwi, Malaria, kuzingatia lishe bora kwa watoto, pamoja na Halmashauri kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kieletroniki.

Kwa upande wao Wabunge wa Shinyanga, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, Patrobas Katambi Jimbo la Shinyanga mjini, pamoja na Christina Mzava wa viti maalum, kwa nyakati tofauti waliahidi kuendelea kuwaletea maendeleo wananchi, pamoja na kukamilisha maboma yaliyosalia kujengwa.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisoma taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, amesema umekimbizwa Kilomita 136, pamoja na kukagua miradi sita yenye gharama ya Sh. milioni 855.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni, Ujenzi Maabara ya Sayansi katika shule ya Sekondari Mwalukwa, Zahanati ya Bushusu, Nyumba nne za watumishi, Jengo la Uthibiti ubora wa shule Kanda ya Magharibi, chumba cha Tehama katika Shule ya Sekondari uhuru, pamoja na kuona maendeleo ya mradi wa maji Ziwa Victoria Masekelo.

Katika hatua nyingine Mboneko amewashukuru wananchi wa Shinyanga, kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizo za Mwenge wa uhuru, huku akiwataka kuendelea kushirikiana na Serikali kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2021 inasema “Tehama ni msingi wa Taifa endelevu, Itumike kwa usahihi na uwajibikaji"

Tazama Picha hapa chini.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude, kushoto, akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Tayari kwa kukimbizwa wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiushika Mwenge wa Uhuru tayari kwa kukimbizwa wilayani humo leo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zikianza wilayani Shinyanga kwa kukagua miradi na kuweka jiwe la msingi.
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akikagua ujenzi wa Maabara ya Sayansi katika shule ya Sekondari Mwalukwa.
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akiweka Jiwe la Msingi katika Zahanati ya Bushushu.
Muonekano wa Jengo la Zahanati ya Bushushu.
Kiongozi wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi, akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba za Watumishi mkoani Shinyanga zilizopo Negezi Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa nyumba za watumishi.
Kiongozi wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akiweka jiwe la msingi katika Jengo la Uthibiti ubora wa Shule Kanda ya Magharibi.
Muonekano wa Jengo la Uthibiti ubora wa Shule Kanda ya Magharibi.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vija na Ajira, akifungua maji katika mradi wa maji Masekelo wa mtandao wa Ziwa Victoria ambao ulitembelewa na Mwenge wa Uhuru kuona maendeleo yake ya utoaji huduma kwa wananchi.
Koplo Rehema Ali Haji ambaye ni Miongoni mwa viongozi wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru, akimtwisha ndoo ya Maji Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, kwenye mradi huo wa maji wa Masekelo unotekelezwa na Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA.)
Ukaguzi wa mfumo wa TEHAMA katika Shule ya Sekondari Uhuru ukiendelea na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kushoto Jasinta Mboneko, akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi katikati wakiendelea na ukaguzi wa miradi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

RAIS SAMIA ATOA POLE HASARA WALIYOPATA WAFANYABIASHARA SOKO LA KARIAKOO






Share:

MAJALIWA AIPA SIKU SABA TUME KUCHUNGUZA CHANZO CHA MOTO SOKO LA KARIAKOO

Waziri Mkuu Kaasim Majaliwa ameipa siku saba za awali tume aliyoiunda kuchunguza chanzo cha moto katika soko la kimataifa la Kariakoo ili kubaini nini kimesababisha au nani kasababisha moto huo.

Ametoa kauli leo (Jumapili Julai 11, 2021) alipokuwa anaongea na wafanyabiashara na wakazi wa eneo la Kariakoo baada ya kukagua hatua zinazoendela kuchukuliwa kudhibiti moto huo, Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kamati iliyoundwa ambayo itafanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo itajumuisha Ofisi ya Rais-Ikulu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo itawakilishwa na Mkurugenzi wa Maafa.

Wengine ni Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikujumuisha Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Zimamoto pamoja na Taasisi ya Kupambana na Rushwa. Pia Waziri Mkuu alizitaja Wakala wa Majengo, Shirika la Umeme (TANESCO), Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

“ Endapo itagundulika kama kuna mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, hatua kali za kisheria zitachukuliwa moja kwa moja, kitendo cha kuungua kwa soko hili la miaka chungu mzima lazima kuwe na uchunguzi wa kina, kwanini leo lishike moto”

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara katika soko hilo wawe watulivu wakati Serikali inafanya kazi yake ya kujua chanzo cha moto huo na amewahakikishia usalama wa mali zilizo ndani ya soko hilo.

Waziri Mkuu pia aliwataka wafanyabiashara kutoingia ndani ya soko hilo katika kipindi hiki ambacho udhibiti unaendelea hadi pale timu zilizoundwa zitakapojiridhisha na utulivu na kufanya sensa ya watu wenye mali kuingia mmoja baada ya mwingine ili wakatoe vitu walivyoviacha.

“Tunachoshukuru kule chini shimoni hakuna moto, mali zote zinalindwa, msiwe na mashaka milango yote imefungwa na makamanda wako ndani na nje wanalinda, mali zote zimehifadhiwa, msiwe na mashaka”

Kadhalika Waziri Mkuu amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa Serikali itaongea na Mabenki yaliyowakopesha wafanyabiashara waliounguliwa na mali zao kuwaongezea muda wa kulipa mikopo yao baada ya kuunguliwa.

“Tumezitapata taarifa za kila mmoja mwenye mkopo rasmi kwenye taasisi za fedha ili tuzungumze nao waongeze muda waache kipindi hiki ili uweze kulipa hapo baadae utakapo kuwa umetulia,biashara imeungua naamini mabenki yatatuelewa na kuweka utaratibu mzuri”
Share:

WAZIRI NDAKI AMALIZA MGOGORO WA ARDHI RANCHI YA KAGOMA

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na viongozi na wataalam kutoka wizarani upande wa sekta ya Mifugo, sekretarieti ya mkoa wa Kagera na Wilaya ya Muleba kuhusu migogoro iliyopo kwenye Ranchi ya Kagoma na Mwesa ambapo ameagiza upimaji ufanyike katika eneo hilo ili kutatua migogoro iliyopo sasa ili wawekezaji waweze kuyatumia maeneo hayo kwa ajili ya kufugia mifugo na wananchi waendeleze shughuli zao za kiuchumi. Kikao hicho kimefanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na wananchi na wawekezaji waliopo kwenye Ranchi ya Kagoma kuhusu mgogoro wa ardhi ambapo ameagiza maeneo yaliyovamiwa na wananchi yapimwe ili wawekezaji waweze kubakiwa na eneo ambalo halitakuwa na mgogoro na kwamba baada ya kupimwa atakae vamia eneo la mtu atachukuliwa hatua.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akifafanua jambo kuhusu upandaji wa malisho kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhe. Toba Nguvila (katikati) wakati walipokua wanakagua baadhi ya maeneo kwenye Ranchi ya Kagoma iliyopo wilayani Muleba Mkoa wa Kagera.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akizungumza jambo Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora (katikati) wakati wa mkutano wa kutatua mgogoro kati ya wananchi na wawekezaji kwenye Ranchi ya Kagoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Peter Msoffe.

Wananchi na wawekezaji katika Ranchi ya Kagoma wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (hayupo pichani) wakati alipofanya mkutano kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi katika ranchi hiyo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wataalam kutoka wizarani upande wa sekta ya Mifugo, sekretarieti ya mkoa wa Kagera, Wilaya ya Muleba, Chama cha Mapinduzi na wananchi wa Kijiji cha Rutoro mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichojadili hali ya migogoro kwenye Ranchi za Kagoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wataalam kutoka wizarani upande wa sekta ya Mifugo, sekretarieti ya mkoa wa Kagera, Wilaya ya Muleba, Chama cha Mapinduzi na wawekezaji katika Ranchi ya Kagoma mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichojadili hali ya migogoro kwenye Ranchi hiyo.

........................................................

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki ameumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi waliovamia kwenye vitalu katika Ranchi ya Kagoma na wawekezaji ambao wanamiliki vitalu hivyo.

Waziri Ndaki ameumaliza mgogoro huo leo (10.07.2021) baada ya kuwasikiliza wananchi na wawekezaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Rutoro wilayani Muleba Mkoa wa Kagera.

Akizungimzia kuhusu mgogoro huo, Waziri Ndaki aliwaeleza wananchi kuwa maeneo hayo waliyoyavamia ni mali ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ambayo tayari yalikuwa yameshakodishwa kwa wawekezaji wanaofanya shughuli za ufugaji hivyo walipaswa kuondolewa. Lakini kutokana na busara za Mhe. Rais Samia ameridhia eneo hilo lipimwe na wananchi wabakizwe kwenye vijiji vinne vilivyopo ambavyo ni Kijiji cha Rutoro, Byengeregere, Chobuheke na Mishambya vilivopo katika Kata ya Rutoro.

“Ninyi wananchi mnatakiwa kumshukuru sana Rais Samia kwa maamuzi yake ya kuwabakiza katika maeneo haya. Lakini niwasihi kuwa watulivu wakati wa zoezi la upimaji wa maeneo na kutoa ushirikiano kwa wataalam watakao kuja kutekeleza zoezi hilo,” alisema Waziri Ndaki.

Vilevile amewataka wananchi kutoendelea kuvamia maeneo mengine katika ranchi hiyo kwani wakifanya hivyo kwa sasa watachukuliwa hatua. Waziri Ndaki pia ametoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kuuza maeneo hayo wakati wao wenyewe hawajamilikishwa.

Pia kwa upande wa wawekezaji hao amewahakikishi kuwa zoezi hilo la upimaji wa maeneo halitaathiri shughuli zao za ufugaji kwa kuwa utawekwa utaratibu mzuri. Vilevile amewaeleza kuwa maamuzi hayo ya kupima maeneo na kuweka alama za mipaka yatasaidia sana kupunguza migogoro ya ardhi na kufanya pande zote kuishi kwa amani.

Katika mkutano huo yalitolewa malalamiko kuwa wafugaji wanalisha mifugo kwenye mashamba yao na kuwasababishia hasara. Kutokana na hilo Waziri Ndaki aliwaagiza wafugaji hao kuacha tabia hiyo kwani ni moja ya vitu vinavyosababisha tatizo la njaa kwa wananchi na kuleta migogoro baina ya pande zote mbili.

Vilevile wawekezaji wametakiwa kuhakikisha wanayatumia maeneo waliyopewa kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo. Aidha, uongozi wa wilaya ya Muleba umetakiwa kuweka utaratibu utakaotumika kuwaondoa wavamizi kwenye vitalu ambao wameingiza mifugo yao wakati hawajamilikishwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhe. Toba Nguvila amemuhakikishia Waziri kuwa maelekezo aliyoyatoa watakwenda kuyasimamia kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kagera na uongozi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).

Kutokana na uamuzi uliochukuliwa wa kupima maeneo hayo kwenye ranchi ya Kagoma, wawekezaji na wananchi wote wameonesha mtazamo chanya kwani hata wao wenyewe hilo ndio wameliona ndio suluhisho.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger