Wednesday, 7 July 2021

MWANAFUNZI WA CHUO CHA KMTC AUAWA KWA KUCHOMWA KISU


Mwanafunzi wa taasisi ya kimatibabu kaunti ya Homa Bay, KMTC nchini Kenya Emily Chepkemoi (23) aliyeripotiwa kutoweka kwa siku mbili amepatikana akiwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake ya kupanga.

Kulingana na wanafunzi wenzake, Chepkemoi ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza alitoweka siku ya Ijumaa, Julai 2 baada ya kuwa darasani, mwili wake ulipatikana Jumapili, Julai 4 baada ya kutafutwa na familia.

"Marehemu alikuwa darasani siku ya Ijumaa na akaenda nyumbani kwake majira ya jioni, alibadilisha nguo na kuenda kuteka maji, baada ya hapo sikumsikia tena hadi nilipopokea habari kwamba alikuwa ameaga dunia," Mwanafunzi mwenzake alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za Daily Nation, milango ya nyumba yake ilikuwa imefungwa na mwili wake ulipatikana ukiwa umefungwa kwenye blanketi ukiwa na majeraha kadhaa.

Marafiki wake waliambia maafisa wa polisi kwamba, Chepkemoi alikuwa ameweka muziki kwa sauti ya juu na hawangeshuku kwamba alikuwa hatarini.

"Mimi sikusikia chochote, nilidhani kulikuwa na sherehe kwake kwa sababu pia sikusikia kelele zozote za kutisha," Mmoja wa marafiki wake alisema.

Kwa mujibu wa taarifa ya chifu msaidizi wa Homa Bay mjini, Dancan Oketh, Chepkemoi alidunga kisu mara kadhaa kabla ya kufariki dunia.

"Alikuwa na majeraha kadhaa ya kisu kwenye kichwa chake, mgongo na shingo, alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi, Chifu huyo alisema.

Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Homa Bay huku upasuaji wa maiti ukisubiriwa kufanyika.

Chanzo - Tuko News
Share:

DKT.NDUGULILE AHIMIZA WANANCHI KUHAKIKI NAMBA ZAO ZA LAINI ZA SIMU


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akizungumza kuhusiana na uhakiki wa laini za simu za mkononi wakati alipotembelea Banda la TCRA maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari Katika Banda la TCRA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akikabidhiwa mfuko wenye machapisho mbalimbali na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bi.Lucy Mbogoro wakati alipotembelea Banda la TCRA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

*******************

Na Mwandishi Wetu

*Wakati ukifika laini hizo zitafungwa.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile amesema kuwa wananchi wahakiki laini zao za simu kwa usalama wao katika matumizi ya mawasiliano.

Dk.Ndugulile ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam, amesema kuwa laini hizo wakati ukifika zitafungwa hawawezi kutumia laini hizo pamoja na simu kinachofuata ni kwenda Mamlaka Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dk.Ndugulile amesema wananchi wahakiki laini zao kutokana na muda ulioopo itafika wakati hawataweza kutumia laini hizo pamoja na simu.

Amesema kuwa uhakiki wa namba ni kumtambua mmiliki wa namba na pale anapobaini kuna namba zingine ambazo sio zake basi anatakiwa kutoa kwa kwenda kwa mtoa huduma wa simu za mkononi kutokana na laini anayoitumia.

Katika maonesho hayo Dk.Ndugulile aliwataka wananchi kutumia fursa ya maonesho kupata taarifa katika mamlaka ya Udhibiti TCRA.

Aidha Dk.Ndugulile amesema kuwa kuendelea kutumia laini ambayo hajakikiwa kwani kuna wakati mwingine baadhi ya watu walisajiliwa kwa kwa kitambulisho cha mtu mwingine hivyo chochote kikitokea atahusika mwenye jina katika kitambulisho.

"Nitoe rai wananchi wahakiki namba zao za simu kwa usalama wao katika matumizi ya mawasiliano kwa kuweza kujiepusha madhara watayoyapata kutokana na kutosajili namba zao"amesema Dk.Ndugulile.
Share:

SHIRIKA LA POSTA LAANZA KUTOA HUDUMA YA PAMOJA CENTRE KWA TAASISI ZA SERIKALI


Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Zainab Chaula alipotembelea ofisi za Shirika la Posta na kuangalia namna walivyojiandaa kwa ajili ya huduma ya One stop Centre (Huduma Pamoja Centre) itakayotoa huduma taasisi zote za Kiserikali nchi nzima.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknlojia Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Taasisi mbalimbali wa Kiserikali watakaokuwa wanatoa huduma zao ndani ya ofisi za Shirika La Posta Nchini.

……………………………

Na Mwandishi wetu

SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC) limeanza kutoa Huduma Pamoja Centre kwa taasisi za kiserikali ili kurahisha na kupunguza usumbufu kwa wananchi.

Huduma hiyo iliyoanza kutolewa Julai Mosi mwaka huu inazihusisha taasisi zote za kiserikali za zitatoa huduma zote ndani ya ofisi moja.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Zainab Chaula amesema mpango huo ni mkakati wa muda mrefu wa serikali katika kuziunganisha taasisi za kiserikali kufanya kazi kwenye ofisi moja.

Akizungumza na waandish wa habari baada ya kutembelea ofisi za Shirika la Posta Jijini Dar es Salaam, Chaula amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi yake kidigitali kwa kuzileta taasisi zote muhimu pamoja ndani ya ofisi moja ambayo nayo ni Shirika la Posta.

Amesema Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia imeweka mikakati katika kusimamia mifumo ya kidigitali ili kupunguza usumbufu kwa wananchi pindi wanapotaka huduma kwa uharaka zaidi.

Chaula amesema amefanya kikao na wakuu wa taasisi zote na kuwataka waongeze muda wa kufanya kazi ili wananchi wengi waweze kupata huduma.

Huduma hizo zote zitakuwa zinatolewa ndani ofisi za Posta ambapo kwa sasa imeanza katika mkoa wa Dodoma na Dar es salaam na amezipongeza taasisi zote kwa kuweza kuamua kwa pamoja kuweka ofisi za Posta kwasababu kila siku wanataka huduma na njia rahisi ni kuwasogezea karibu

Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo amesema hadi kufikia Septemba mwaka huu watakuwa wamefikia ofisi 10 zitakazokuwa zinatoa huduma hizo.

Amesema Shirika la Posta lipo nchi nzima na huduma hizo zitakuwa zinapatikana ndani ya ofisi zao zote na kwa hilo itaondoa usumbufu na gharama kwa wananchi. Amesema shirika wamejipanga kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi wote

Kaimu Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Usajili Vizazi na Vifo RITA Emmy Hudson amesema katika ofisi za Posta watakuwa wanatoa huduma ya vyeti vya kuzaliwa na vifo. Amesema kwa sasa ukifika katika ofisi za Posta ndani ya Jiji la Dodoma na Dar es salaam utakuta ofisi zao na huduma zote utazipata na itapunguza usumbufu kwenda ofisi za RITA.

Ameishukuru na kuipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa wananchi kupata huduma zote muhimu ndani ya ofisi moja.

Kwa sasa ndani ya ofisi za shirika la posta litakua linatoa huduma mbalimbali za kitaasisi kama NIDA, BRELA, RITA, NSSF, uhamiaji na zinginezo.
Share:

RUWASA YAANZA KUTEKELEZA KWA KISHINDO MIRADI YA MAJI BUDUHE NA KADOTO SHINYANGA


Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi (kulia) wakiangalia mabomba ya maji yakipakiwa tayari kusafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto.

***
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga imeanza kutekeleza miradi ya maji safi Buduhe kata ya Salawe na Kadoto kata ya Lyamidati katika katika halmashauri ya wilaya Shinyanga ambapo tayari imesafirisha mabomba ya kusambazajia maji ili kuhakikisha inatatua changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili wakazi zaidi ya 8,000 wa maeneo hayo.

Akizungumza leo Jumatano Julai 7,2021 wakati wa kusafirisha mabomba ya maji kutoka ofisi za RUWASA zilizopo Mjini Shinyanga kwenda kwenye maeneo ya miradi, Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi amesema utekelezaji wa miradi hiyo unaanza Julai 2021 hadi Oktoba 2021 ikigharimu jumla ya shilingi milioni 381.

Ameeleza kuwa miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga inatekelezwa na RUWASA ikitarajia kuwanufaisha wananchi zaidi ya 8,000 huku akisisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi.

“Tayari zoezi la kuchimba mitaro limeanza na haya ni mabomba ya maji kwa ajili ya mradi wa maji safi wa Buduhe kata ya Salawe ambao pia utanufaisha kijiji cha Nzoza ambao utakuwa na vituo 10 vya kuchotea maji (DP), ukiwa na mtandao wa bomba Kilomita 9.85 ukigharimu jumla ya shilingi milioni 195. Pia tunapeleka mabomba haya katika maradi wa maji safi wa Kadoto kata ya Lyamidati ambapo mtandao wake wa bomba ni kilomita 7.8 ukiwa na vituo vya kuchotea maji (DP) 6 ukigharimu jumla ya shilingi milioni 186”,amesema Nkopi.

Kwa upande, Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi ambaye ameshuhudia zoezi la kusafirisha mabomba ya maji kuelekea kwenye maeneo ya miradi ya maji amesema sasa wananchi wa Buduhe na Kadoto wategemee kupata huduma ya maji safi na kuondokana na tabia ya wizi wa maji kwa kutoboa mabomba ya maji kutoka Ziwa Victoria yaliyokuwa yanapita kwenye maeneo yao lakini wakawa hawapati huduma ya maji.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje amesema ni faraja kubwa kwa wakazi wa Kadoto na Buduhe kupata huduma ya maji ambayo imekuwa changamoto ya muda mrefu kwenye maeneo hayo licha ya bomba la maji kupita kwenye maeneo hayo.

“Maji hayana mbadala, tunafarijika sana kuona serikali inatatua kero za wananchi. Kupatikana kwa huduma ya maji katika maeneo haya itasaidia pia kuongeza uchumi kwani wananchi walikuwa wanatumia muda mwingi kufatuta huduma ya maji na kujikuta hawafanyi shughuli za maendeleo”,amesema Mboje.

Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi (kulia) wakiangalia mabomba ya maji yakipakiwa tayari kusafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kushoto) akimwelezea Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi kuhusu mabomba ya maji kwa ajili ya miradi ya maji safi ya Buduhe na Kadoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi mabomba ya maji kwa ajili ya miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (kulia) akimuonesha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi mabomba ya maji kwa ajili ya miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi akimuonesha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi akimuonesha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (wa katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon wakiangalia mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi (wa pili kushoto) akifurahia jambo n Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (wa kwanza kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon wakati wakikagua mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi na wafanyakazi wa RUWASA wakiwa kwenye mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga, Mhandisi Emael Nkopi akikagua mabomba ya maji yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka ofisi za RUWASA kwenda kwenye miradi ya maji safi Buduhe na Kadoto leo Jumatano Julai 7,2021.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

MSHINDI WA KAMPENI YA SIMBANKING AKABIDHIWA GARI AINA YA TOYOTA IST

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili akimkabidhi zawadi ya gari mshindi wa kampeni ya SimBanking “Mzigo Promosheni,” Kevin Ngao katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha CRDB Wakala (wapili kushoto), Ericky Willy na Meneja Biashara Kanda ya Mashariki, George Yatera.
Dar es Salaam Tanzania, July 7, 2021 – Benki ya CRDB imekabidhi gari aina ya Toyota IST kwa mshindi wa kwanza wa kampeni ya “SimBanking Mzigo Promosheni,” anayejulikana kwa jina la Kelvin Ngao. Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Stephen Adili alisema mshindi huyo amepatikana kwa kufanya miamala mingi zaidi kupitia huduma ya SimBanking.


“Kampeni yetu inalenga katika kuwahamasisha wateja kujenga utamaduni wa kutumia mifumo ya kidijitali ikiwamo SimBanking kufanya miamala yao. Tumekuwa tukitoa zawadi ya Sh. 100,000 kwa wateja wetu wenye miamala mingi zaidi kila siku na leo hii tunakwenda kutoa zawadi ya gari kwa mshindi wa jumla wa mwezi Juni, Kevin Ngao,” alisema Adili.

Adili aliongezea kuwa katika kampeni hiyo Benki ya CRDB pia inatoa elimu kwa wateja wake juu ya matumizi ya huduma ya SimBanking ambapo pia wateja wamekuwa wakiulizwa maswali kupitia mitandao ya kijamii na radio na kujishindia zawadi ya Sh. 30,000. Mpaka sasa tayari benki hiyo imeshatoa jumla ya shilingi milioni 15 kwa washindi 500.
Akielezea mafanikio ya kampeni hiyo alisema katika kipindi cha mwezi Juni matumizi ya huduma ya SimBanking yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 20 kutokana na uelewa wa wateja juu ya urahisi na unafuu wa SimBanking katika kupata huduma.


Adili alisema kampeni hiyo pia imezaa matunda katika upande wa elimu ya kufungua akaunti kupitia SimBanking App ambapo hadi sasa zaidi ya wateja 30,000 wameshafungua akaunti kupitia mfumo huo wa kidijitali.


Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo Kevin Ngao aliishukuru Benki ya CRDB kwa zawadi hiyo ya gari huku akibainisha siri ya ushindi ni kujenga utamaduni wa kutumia SimBanking kufanya miamala yake.
“Ninafurahia sana kufanya miamala kupitia SimBanking iliyoboreshwa, imekuwa rahisi na nafuu sana kutumia. Sasa hivi miamala yangu yote nakamilisha kupitia SimBanking, iwe kufanya malipo kupitia CRDB Lipa Namba, kutuma pesa, kulipia bima, kulipia kodi na kutoa fedha kwa CRDB Wakala/ ATMs na Tawini bila ya kadi,” alibainisha Kevin.


Akihitimisha hafla hiyo Meneja wa Biashara Kanda ya Mashariki Benki ya CRDB, George Yatera alimpongeza mshindi huyo pamoja na washindi wengine wote ambao wamepata zawadi kupitia kampeni hiyo huku akitoa rai kwa wateja wengine wa benki hiyo kushiriki kampeni kwa kuendelea kufanya miamala kupitia SimBanking.
“Kampeni yetu bado ina miezi miwili zaidi hadi mwezi Agosti, zawadi bado ni nyingi hivyo nitoe rai kwa wateja wetu kuendelea kufanya miamala kwa wingi Zaidi lakini pia kufuatilia mitandao yetu ya kijamii ambapo pia tunatoa zawadi,” alihitimisha Yatera.
Share:

Benki Kuu Yaagizwa Kuongeza Kasi Mchakato Wa Taasisi Za Fedha Kupunguza Riba Za Mikopo


Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itekeleze haraka maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kuhusu Taasisi za Fedha kupunguza riba za mikopo ili kuwawezesha wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla kukopa na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Mhe. Masauni ametoa maagizo hayo alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Benki hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Alipongeza jitihada zinazofanywa na Benki Kuu ya Tanzania za kukutana na wadau ili kuhakikisha kuwa Taasisi za Fedha zikiwemo Benki na Watoa huduma wa Sekta Ndogo ya Fedha wanapunguza riba za mikopo yao ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo isiyo na gharama kubwa.

“Niwapongeze kwa juhudi zilizoanza kuchukuliwa kuwezesha riba kupungua na ikiwezekana mwishoni mwa mwezi huu wananchi waanze kuona matokeo ya juhudi hizo kwa riba kuanza kupungua, kwa kuwa kupungua kwa riba ni jambo linalowezekana”, alieleza Mhandisi Masauni.

Aidha, ameitaka Benki hiyo kuhakikisha inaweka mikakati mahususi ya kuongeza akiba ya Fedha za kigeni kwa kuwa na mbinu za kibunifu zikiwemo kuanza kununua na kuhifadhi dhahabu pamoja na kuongeza uuzaji wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi na kusimamia kikamilifu shughuli za utalii.

Kuhusu suala la fedha za wananchi waliokuwa wateja wa Benki ya FBME Limited iliyowekwa chini ya uangalizi wa Bima ya Amana za Wateja inayosimamiwa  na Benki Kuu ya Tanzania ikiwa katika hatua za kufilisiwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Yussuf Masauni, ameitaka Benki hiyo kuhakikisha wateja wa Benki hiyo wanarejeshewa fedha zao haraka baada ya kukamilisha taratibu za kisheria zinazoendelea nchini Cyprus.

Kwa upande wake Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Bernard Kibesse, alimhakikishia Mhe. Naibu Waziri Masauni kwamba Benki yake inakamilisha mazungumzo na mabenki ili washushe riba kama alivyoelekeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan jijini Mwanza.

Alisema Benki Kuu pia inaendelea kurekebisha kanuni mbalimbali za mikopo inayotolewa na Benki hiyo kwa Mabenki ili kuziongezea ukwasi Benki hizo ili na zenyewe zitumie fursa hiyo kushusha riba za mikopo.

Aidha, Naibu Gavana Dkt. Kibese alieleza kuwa Benki Kuu ya Tanzania itaanza kununua na kuhifadhi dhahabu baada ya Kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Mwanza kilichozinduliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan jijini Mwanza hivi karibuni kupata hati ya uthibitisho ya uzalishaji wa dhahabu wa viwango vya kimataifa ambavyo ili cheti hicho kitolewe, kiwanda kinatakiwa kuzalisha dhahabu yenye ubora wa asilimia 99.9.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Masauni yupo jijini Dar es Salaam katika ziara yake kikazi ambapo atatembelea ofisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.



Share:

Rais Samia Akutana Na Afisa Mtendaji Mku Barrick



Share:

BANDA LA BARRICK LAENDELEA KUVUTIA WENGI MAONESHO YA SABASABA


Banda la Barrick laendelea kuvutia wengi maonesho ya Sabasaba
Kampuni ya madini ya Barrick inashiriki katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 45 yanayaoendelea jijini Dar es Salaam ambapo banda lake la maonyesho na wajasiriamali inaowawezesha kutoka vijiji jirani na mgodi wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga linaendelea kuwavutia wananchi na viongozi mbalimbali na wadau wa sekta ya madini.
Mmiliki wa mgodi wa madini ya Tanzanite,bilionea Laizer Saniniu,(wa tatu kutoka kulia) akiwa na wafanyakazi wa Barrick na wajasiriamali wanaowezeshwa na kampuni hiyo baada ya kuwatembelea katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es salaam.
Mfanyabiashara wa madini,Laizer Saniniu (Kulia) akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la maonesho la Barrick.
Waziri wa Ardhi,Mh.William Lukuvi,(kulia) akiongea na Wafanyakazi wa Barrick alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya Sabasaba.
Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda,Dk.Exaud Kigahe(Kulia)akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wanaowezeshwa na kampuni ya Barrick.
Share:

Picha : KLABU YA MAZOEZI PJFCS YATOA MSAADA WA MITUNGI YA OKSIJENI, KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

Share:

Waajiri Waaswa Kuzingatia Usalama Na Afya Katika Maeneo Ya Kazi


Na; Mwandishi Wetu – Dar Es Salaam
Waajiri nchini waaswa kuzingatia maswala ya usalama na afya katika maeneo ya kazi ili kuwalinda wafanyakazi dhidi ya ajali, na madhara ya kiafya kwa kuwa na mazingira yenye usalama na ustawi kwa wafanyakazi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha Fujian Hexiawang na Kiwanda cha Lodhia Group of Companies vilivyopo Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Akiwa katika ziara hiyo iliyolenga kufuatilia uzingatiaji wa sheria na kanuni za usalama na afya katika maeneo ya kazi Waziri Mhagama alieleza kuwa waajiri wote wanawajibu wa kuhakikisha masuala ya usalama na afya katika maeneo ya kazi yanazingatiwa ili wafanyakazi waweze kutekeleza shughuli zao kwenye mazingira ambayo ni salama.

“Tulipokea malalamiko kuhusu kiwanda cha Fujian Hexiawang kinachozalisha nondo kuwepo kwa mapugufu katika mazingira ya utendaji kazi kwa wafanyakazi waliopo katika kiwanda hicho ambao walikuwa wakibeba vyuma chakavu na kuweka kwenye tanuri la moto (Jiko la kuyeyusha Vyuma chakavu) hali ambayo ilikuwa hatarisihi kwa wafanyakazi hao,” alisema Waziri Mhagama

“Serikali katika kuwajali wananchi wake kupitia Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) ilikutana na mwekezaji wa kiwanda hicho na walijadiliana pamoja kuona teknolojia bora ya kuwalinda wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa kuwa na mtambo maalumu wa kubeba na kuweka vyuma chakavu kwenye tanuri la moto badala ya wafanyakazi kufanya kazi hiyo ambayo ilikuwa hatarishi kwao,” alieleza Waziri Mhagama

“Vilevile jukumu la mwajiri kugawa vifaa kinga kwa wafanyakazi ikiwemo maovaroli maalumu, vifunika uso, glovu, kofia ngumu n.k ili kulinda wafanyakazi katika mazingira ambayo ni hatarishi,” alieleza

Aliongeza kuwa lengo la kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ni kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na mazingira mazuri ya kazi na kiafya ili waweze kutekeleza majuku yao kwa weledi na ufanisi.

“Mnatambua kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa akihamasisha uwekezaji nchini ambao utazalisha ajira zaidi kwa vijana. Lakini kupitia uwekezaji huo serikali imekuwa ikihamasisha wawekezaji kufuata Sheria na Taratibu zilizopo nchini kwa kuzingatia usalama na afya za wafanyakazi katika kujenga uchumi wa nchi” alieleza

Katika kutekeleza hayo, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imekuwa na jukumu la kuhakikisha maeneo ya kazi yanazingatia usalama na afya ya wafanyakazi nchini kwa kudhibiti, kusimamia utekelezaji na kuendeleza viwango imara vya usalama na afya kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Aidha, Waziri Mhagama alipongeza viwanda hivyo kwa kuzalisha nondo imara ambazo zimekuwa zikitumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa nchini ikiwemo Miradi ya Kimkakati (reli ya Kisasa ya SGR, mradi wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere na Daraja la Tanzanite), Barabara na Vituo vya Afya vinavyojengwa katika maeneo mbalimbali.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Mhagama amewataka wafanyakazi watumie haki yao ya kutoa taarifa kuhusu majanga mbalimbali ambayo yanatokea katika maeneo ya kazi ikiwemo kuumia kwa mfanyakazi, ugonjwa au kifo kutokana na kazi ili hatua na taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Sambamba na hayo ameutaka Uongozi wa viwanda hivyo kufanya tathmini ya vihatarishi akitolea mfano vilipuzi ambavyo vimekuwa hatarishi kwa wafanyakazi waliopo katika maeno ya uzalishaji katika kiwanda hivyo.

“Tuliwapa miongozo ikiwemo kuweka utaratibu wa kubeba vyuma chakavu na kupeleka kwenye tanuri pamoja na kuweka mtu wa kuweza kutambua vyuma salama, alieleza

Waziri Mhagama ametaka Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) kuendelea kutoa elimu na mafunzo ya usalama kwa waajiri na wafanyakazi. Pia alihimiza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wafike katika viwanda hivyo na kutoa elimu na ufafanuzi juu ya masuala ya fidia kwa wafanyakazi ili waweze kutambua taratibu zikoje.

Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe.Abdallah Ulega alieleza kuwa ziara hiyo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, imekuwa ni faraja kwa wafanyakazi wa viwanda hivyo kwa kuwa wanatambua changamoto zao zitafanyiwa kazi kwa ufasaha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Hadija Ally alieleza kuwa maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri watahakikisha wanayasimamia na kuyafanyia kazi ili waweze kulinda maslahi ya wafanyakazi, kuhakikisha wanakuwa na mikataba na wanafanya kazi katika mazigira ambayo ni rafiki kwa lengo la kuimarisha ustawi wao.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda alisema kuwa Taasisi hiyo itaendelea kufanya kaguzi za kufuatilia utekelezaji wa usalama na afya katika maeneo ya kazi.

“OSHA itaendelea kushirikiana na wawekezaji, waajiri na wafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya kazi nchini ili kuhakikisha vihatarishi vinatambulia na kutengenezewa mikakati ya kidhibiti kwa ajili ya kuzuia madhara kwa wafanyakazi na mitambo iliyowekezwa,” alisema Mwenda


Share:

RM – Local Large Corporates at Absa Bank

RM – Local Large Corporates   Bring your possibility to life! Define your career with us With over 100 years of rich history and strongly positioned as a local bank with regional and international expertise, a career with our family offers the opportunity to be part of this exciting growth journey, to reset our future and […]

This post RM – Local Large Corporates at Absa Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Rais Samia Azungumza Kwa Simu Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Marekani



Share:

Head of Debt at Absa Bank

Head of Debt    Bring your possibility to life! Define your career with us With over 100 years of rich history and strongly positioned as a local bank with regional and international expertise, a career with our family offers the opportunity to be part of this exciting growth journey, to reset our future and shape […]

This post Head of Debt at Absa Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Head Business Advisory at Absa Bank

Head Business Advisory     Bring your possibility to life! Define your career with us With over 100 years of rich history and strongly positioned as a local bank with regional and international expertise, a career with our family offers the opportunity to be part of this exciting growth journey, to reset our future and shape […]

This post Head Business Advisory at Absa Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

ICT Officer II – Information Systems Auditor at TCAA

POST: ICT OFFICER II – INFORMATION SYSTEMS AUDITOR (RE-ADVERTISED) – 1 POST POST CATEGORY(S) IT AND TELECOMS EMPLOYER Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) APPLICATION TIMELINE: 2021-07-06 2021-07-19 JOB SUMMARY To participate in ensuring effective and efficient functioning of ICT Auditing for better achievement of TCAA Vision and Mission. DUTIES AND RESPONSIBILITIES   To assist financial auditors in […]

This post ICT Officer II – Information Systems Auditor at TCAA has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Data Centre & Network Specialist at NBC

 Data Centre & Network Specialist     NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Summary To plan, organize, upgrade and deliver cost effective and efficient network infrastructure services (WAN/LAN) that meets and […]

This post Data Centre & Network Specialist at NBC has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Technician II – Mining (9) at Mining Commission

POST: TECHNICIAN II (MINING) – 9 POST POST CATEGORY(S) WATER, MINING AND NATURAL RESOURCES EMPLOYER Mining Commission APPLICATION TIMELINE: 2021-07-06 2021-07-19 DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i. To assist in collecting and analyzing mining and explosives information and data; ii. To assist in preparation of inquiries and other logistics related to investigations in mining accidents and incidences; iii. To […]

This post Technician II – Mining (9) at Mining Commission has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger