Monday, 5 April 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 5,2021




















Share:

Sunday, 4 April 2021

Breaking : RAIS SAMIA ATEUA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA,NAIBU MAKATIBU WAKUU WA WIZARA NA WAKUU WA TAASISI...TAZAMA MAJINA YOTE HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana amefanya uteuzi wa Makatibu wakuu wa Wizara, Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa Taasisi mbalimbali





Share:

Video Mpya : NYUMBU MJANJA - PEKE YANGU II


Msanii Nyumbu Mjanja ameachia wimbo mpya unaitwa Peke Yangu II /Peke Yangu season 2.....Tazama Video Hapa chini
Share:

Video Mpya : NYASANI - BADO UNAISHI JPM


Msanii Nyasani anakualika kutazama Video ya wimbo wake uaitwao Bado Unaishi JPM. 
Wimbo huu ni kwa ajili ya maombolezo ya shujaa wa Afrika,Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Director ni Dave_skerah, Producer ni Sheddy the mix, Paradox empire records.

Tazama hapa chini
Share:

Various Jobs at IKUNGI District Council

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

WANANDOA WAISHI ZAIDI YA MIAKA 18 BILA KUFANYA TENDO LA NDOA DAR


Mahakama ya Mwanzo Buguruni jijini Dar es salaam imevunja ndoa ya mwanamuziki wa nyimbo za injili, Rebecca Magaba na Zabron Maselege baada ya wanandoa hao kutoshiriki tendo la ndoa kwa zaidi ya miaka 18.

Mahakama hiyo imetoa amri mali zote walizochuma wanandoa hao, ikiwamo shamba la eka 10 lililopo Bagamoyo, maduka mawili yaliyopo Bonyokwa na Mahengo na shamba la miti ya mikaratusi lililopo Kigoma zichukuliwe na Maselege na kiwanja kilichopo Madale kitabaki kwa Rebecca.

Hakimu Mkazi, Mwinyiheri Kondo amesema Mahakama imevunja ndoa hiyo baada ya kuona wanandoa hao wanafanya matendo ya ndoa ambayo si ya kawaida.

Kondo amesema katika ushahidi uliotolewa na Rebecca alidai hawakuwahi kufanya tendo la ndoa tangu wafunge ndoa kutokana na mume wake kutokuwa na korodani.

Hivyo kutokana na hilo, Mahakama hiyo imevunja ndoa hiyo, na ndani ya siku 45 haki ya kukata rufaa kwa mdaiwa ipo wazi.

Katika kesi hiyo, Rebecca aliiomba Mahakama hiyo ivunje ndoa hiyo kisheria baada ya kuishi na mume wake kwa miaka 21 bila ya kushiriki tendo la ndoa.



Share:

Picha : MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO ASHIRIKI IBADA YA MISA TAKATIFU YA KUADHIMISHA SIKUKUU YA PASAKA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na Waumini wa Dini ya Kikristo na Watanzania  katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika leo April 04,2021 katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.
Share:

Msaidizi wa Kumbukumbu II at Mbinga District Council April, 2021

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

4 Government Job Opportunities MWANZA at Buchosa District Council – Various Posts

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

4 New Government Job Opportunities SINGIDA at IKUNGI District Council – Various Posts

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

District Council Jobs Government Job Opportunities IKUNGI District Council April 2021, New Jobs Ikungi 2021, New Government Jobs 2021 Ikungi District is one of the six districts of the Singida Region of Tanzania. It is one of the 20 new districts that were formed in Tanzania since 2010; it was split off from Singida Rural […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

4 Government Job Opportunities LINDI at Liwale District Council – Various Posts

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

District Council Jobs Government Job Opportunities Liwale District Council April 2021, New Jobs Liwale 2021, New Government Jobs 2021 Liwale District Council was officially established on July 7, 1975 after being disbanded from Nachingwea due to the size of Nachingwea District. Prior to that, Liwale District was a Nachingwea District Division from 1961. Also in […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

KAMANDA MAMBOSASA AWATAKA WANAUME WANAONYANYASWA KIJINSIA KUJITOKEZA


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi katika Kata ya Pangani Ilala jijini Dar es Salaam waliojitokeza kwenye huduma za mkono kwa mkono maarufu 'Ones Stop Center' zilifofanyika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Program wa Fredrich Naumann Foundation for Freedom East Africa kwa Tanzania na Kenya, Veni Swai (wa kwanza kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi katika Kata ya Pangani Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mratibu wa One Stop Center katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Dk Christina Onyango akifuatilia.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi katika Kata ya Pangani Ilala jijini Dar es Salaam waliojitokeza kwenye huduma za mkono kwa mkono maarufu 'Ones Stop Center' zilifofanyika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza na baadhi ya wanahabari mara baada ya hafla hiyo.
Baadhi ya wananchi wakihudumiwa kwenye huduma za mkono kwa mkono maarufu 'Ones Stop Center' zilifofanyika eneo hilo.
Huduma zikitolewa kwenye hafla hiyo.
***
KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewataka wanaume wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika familia zao wajitokeze na kudai haki zao mbele ya sheria, badala ya kuendelea kukaa kimya kwa kilea kinachodaiwa wanaona aibu huku wakizidi kuteseka.

Kamanda Mambosasa ametoa wito huo juzi katika Kata ya Pangani Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga awamu ya pili ya huduma za mkono kwa mkono maarufu 'Ones Stop Center' zinazotembea kwa waathirika wa unyanyasaji na ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika kata tisa za Mkoa wa Kipolisi wa Ilala takribani kwa siku 18.

Pamoja na hayo aliongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto na unyanyasaji  watoto vikiwemo vya ubakaji, ukeketaji, utumikishaji watoto na ndoa za utoto vinavyowanyima watoto haki zao haviwezi kukubalika, kwani watoto hao ndio viongozi na wajenzi wa taifa la kesho.

“Watoto wa sasa ndio akina Rais Samia Suluhu wa kesho; ndio akina Lazaro Mambosasa wa kesho; ndio madkatari na viongozi wa kesho hivyo, lazima haki zao zilindwe na waendelezwe.” Hivyo, lazima Watanzania tuungane na kusimama pamoja kuhakikisha wanawake na watoto wanalindwa ili kesho na kesho kutwa, washike nafasi mbaimbali kutumikia taifa,” alifafanua Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa aliipongeza taasisi ya Fredrich Naumann Foundation for Freedom East Africa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanikisha huduma za mkono kwa mkono zinazotembea na kuahidi kuendelea kuunga mkono na kusaidia kufanikiwa zaidi kwa huduma hizo ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia eneo lake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Program wa Fredrich Naumann Foundation for Freedom East Africa kwa Tanzania na Kenya, Veni Swai akizungumza katika hafla hiyo, alilipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada za kupambana na uhaifu ukiwemo ukatili wa kijinsia, na hasa utaratibu wa kuwafuata wananchi mahali walipo pamoja na kutoa elimu na huduma dhidi ya ukatili wa kijinsia. 

Alisema hatua hiyo inaifanya jamii kuongeza imani yake kwa polisi hivyo, kujitokeza kueleza kero zao zikiwamo za kifamilia.

“Kitendo cha polisi kuwafuata wananchi katika maeneo yao na kusikiliza kero zao sambamba na kuwapa msaada ukiwamo wa kisheria, msaada wa kipolisi, unasihi na huduma za afya na elimu dhidi ya ukatili wakijinsia, kinaonesha uhusiano mwema baina ya polisi na raia unazidi kuimarika. Bado wadau wote kwa pamoja tuna kazi kubwa mbele yetu na sisi tunaahidi kuendelea kushirikiana na polisi kadiri inavyowezekana.” Alisema Bi. Swai.

Naye Mratibu wa One Stop Center katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Dk Christina Onyango, alisema mbali na vituo hivyo kutoa huduma za upimaji afya kama macho, sukari na shinikiza la damu, unasihi, huduma za kisheria, pia wananchi wamekuwa wakifundishwa namna ya kubaini, wahusika, dalili, aina na namna ya kuripoti na kutunza ushadidi dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Dk. Onyango alibainisha kuwa awamu ya kwanza ya huduma kama hizo ilifanyika Desemba mwaka jana katika kata saba zilizo katika mkoa huo wa kipolisi ikiwa ni mwendelezo wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia. 


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 4,2021






























Share:

Saturday, 3 April 2021

SIMBA SC YAITWANGA AS VITA 4G..... YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA KWA KISHINDO


Na Alex Sonna,Dar es Salaam

Mabingwa wa Tanzania timu ya Simba imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa  mabao 4-1 As Vita Club kutoka Kongo na kufikisha  Pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na Al Ahly ya Misri Mchezo uliopigwa uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba walikuwa wa Kwanza kuliona lango la wageni kupitia kwa winga machachari Luis Miquissone dakika ya 30 kwa shuti kali akipokea pasi kutoka kwa Bernard Morisson ,mnamo dakika ya 32 kiungo Zemanga Soze akasawazisha na kuvunja rekodi ya Simba ya kutoruhusu bao.

Kabla ya Mapumziko Simba walipata bao la pili kupitia kwa kiungo Mshambuliaji Clatous Chama dakika ya 45 na kuipeleka Simba mapumziko ikiwa kifua mbele.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Simba ilinufaika na mabadiliko hayo akitokea benchi Larry Bwalya aliipatia Simba bao la tatu akimalizia pasi ya Clatous Chama dakika ya 66.

Mnamo dakika ya 83 Clatous Chama alirudi tena kambani kwa bao safi kwa kuwachambua mabeki wa As Vita pamoja na golikipa wao mara baada ya kupokea pasi ya Luis Miquissone.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 13 na kuongoza kundi A ambapo hawawezi  kufikiwa na timu yoyote baada ya Vibonde Al-Merreikh kuwakazia  Al Ahly kwa kufungana mabao 2-2 ,Simba wamebakiza mechi moja ugenini dhidi ya Al Ahly ambao wana pointi 8 hata kama Simba atapoteza bado ataongoza kundi A.

As Vita na Al-Merreikh rasmi wameshindwa kuendelea hatua ya robo Fainali na kuwachia Simba na Al Ahly wakisonga mbele ya Michuano hiyo Mikubwa barani Afrika.

Soma zaidi <<HAPA>>

CHANZO - FULLSHANGWE BLOG

Share:

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. MWIGULU NCHEMBA AWAAGIZA TRA KUKADIRIA KODI KWA KUFUATA SHERIA

Na. Saidina Msangi na Peter Haule, WFM, Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutumia weledi na kuzingatia sheria katika kukadiria kodi kwa wafanyabiashara ili kulinda walipa kodi na kutanua wigo wa walipa kodi.

Dkt. Nchemba alitoa maagizo hayo Jijini Dodoma alipokutana na wakuu wa Idara na Taasisi za wizara hiyo, katika kikao kazi kilicholenga kutekeleza maelekezo yaliyotolewa hivi karibuni na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo aliiagiza Wizara hiyo kutatua changamoto za wafanyabiashara nchini kuhusu masuala ya kodi.

“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais ni muhimu yatekelezwe ipasavyo ili kulinda na kukuza uchumi wa nchi kwa kutoza kodi kwa staha, weledi na kwa mujibu wa Sheria na turekebishe mahali tulipoharibu”alisisitiza Dkt. Nchemba.

Aliitaka TRA kuacha kudai taarifa za miaka mingi ya nyuma ambayo iko nje ya sheria kwa wafanyabiashara ambazo zilikwishafanyiwa kazi,  kwani utunzaji wa kumbukumbu ni changamoto kwa wengi hivyo ni vema kuzingatia sheria na taratibu za namna ya kufanya ukadiriaji wa kodi.

“TRA nawataka mpeleke ujumbe makini kwa wafanyakazi wa TRA nchini nzima kwamba Serikali haijasema msikusanye kodi au mpunguze jitihada za kukusanya kodi hizo bali kinachoongelewa na kusisitizwa ni kukadiria na kukusanya kodi kwa kuzingatia sheria na taratibu, bila kuonea watu”alisisitiza Dkt. Nchemba

Aliongeza kuwa ili kuendelea kupata mapato ya kutosha nchini ni lazima kuwalea wafanyabiashara ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi akitolea mfano wa ngoómbe wa maziwa anayetakiwa kupewa huduma muhimu kabla ya kumkamua maziwa.

“Mheshimiwa Rais alielezea changamoto ya Kushika akaunti, fedha za wafanyabashara, tuache vitendo hivyo, hapa hakuna mjadala ni lazima yafuatwe na sisi Wizara tutaendelea kufuatilia maelekezo hayo” alisema Dkt. Nchemba.

Alisisitiza Mamlaka ya Mapato Tanzania kuzingatia maelekezo aliyotoa na  kurekebisha pale ambapo sheria hazikuzingatiwa ili kulinda uchumi wa nchi na kutodhoofisha biashara za walipakodi pamoja na kuangalia namna ya kuongeza walipa kodi wapya.

Kwa upande mwingine Waziri Dkt. Nchemba ametoa rai kwa Watanzania wakiwemo wafanyabiashara kulipa kodi inavyostahili kwa kufuata Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia matumizi bora ya kutunza kumbukumbu za malipo.

Alieleza kuwa utamaduni wa kulipa kodi uwe jambo la kawaida na la kila siku kwenye maisha yetu, ujanja ujanja wa kukwepa kodi ni kuvunja sheria na Serikali haitavumilia.

Aidha amewataka wafanyabiashara walioziondoa fedha zao kwenye benki wazirejeshe na kuzihifadhi kwenye benki hizo na kuahidi kuwa zitakuwa salama na hazitazuiwa na TRA kwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwa taasisi hiyo ili kurejesha ari ya ufanyaji biashara nchini.

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni, alisema kuwa kikao kazi hicho kitawawezesha kujua hatua gani imefikiwa na Wizara ili kusimamia na kuendeleza uchumi wa nchi na Maisha ya watu.

Alisema kuwa ameona timu nzuri ya wataalam ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango ambayo itasaidia kutimiza malengo ya Serikali, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni.


Share:

ASKOFU CYPRIAN KIZITO AFARIKI DUNIA



Rais Museveni na Askofu Mkuu wa Kampala Cyprian Lwanga Kizito (kulia)
****
Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki mjini Kampala Cyprian Kizito Lwanga amefariki akiwa na umri wa miaka 68, Kanisa limethibitisha.

Katika taarifa iliyotolewa na Diyosisi ya Kampala ya Kanisa Katoliki, Askofu Lwanga alipatikana chumbani mwake akiwa amefariki Jumamosi asubuhi. Chanzo cha kifo chake hakijabainishwa.

Taarifa za kifo hicho cha ghafla zimewashtua Waganda wengi ambao wametumia twitter na WhatsApp kutoa rambirambi zao.

Mapema Ijumaa, aliongoza Wakristo katika ibaada ya Ijumaa njema akishirikiana na Askofu mkuu wa kanisa la Uganda Daktari Kazimba Mugalu,kupitia Baraza la Muungano wa Madhehebu ya Wakristo nchini Uganda (UJCC), ambalo alikuwa mwenyekiti wake.

Kizito Lwanga aliyetawazwa kuwa padri wa Kanisa Katolikio 1978 alionekana kama mkosoaji wa serikali ya NRM.

ALikuwa akiangazia wazi wazi dhidi ya ufisadi, ukiukaji wa haki za binadamu na marekebisho ya katiba ya nchi ili kuondoa ukomo wa muhula na urais ili kumruhusu Rais aliye madarakani, Yoweri Museveni kuongeza muda wa utawala wake.


Mwaka 2012 aliwahi kumuandikia barua Rais Museveni akimtaka astaafu ifikapo mwaka 2016.

Kifo chake kimepokelewaje?

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine aliandika katika mtandao wa Twitter: Nimepokea kwa mshtuko kifo cha ghafla cha Dkt. Cyprian Kizito Lwanga, Askofu Mkuu wa Kampala. Itakuwa vigumu kukabiliana na msiba huu.

Mwaka 2018, Askofu huyo mkuu aliilaumu utawala wa Museveni kwa kuwatumia makasisi kumchunguza alipokuwa akipinga madai kwamba anapanga kupindua serikali.

Hivi karibuni, alilaani visa vya kukamatwa na kutekwa nyara kwa wafuasi wa upinzani.

Wakati wa uchaguzi wa mwezi Januari January 2021, alipendekeza uchaguzi kuahirishwa kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na janga la corona na kupanda kwa taharuki za kisiasa.

Mrengo wa upinzani ulipiga pendekezo hilo.

Katika Ibaada ya jana alimpongeza aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli kwa kazi alizowafanyia Watanzania na Jumuia ya Afrika mashariki kwa muda mfupi katika utawala wake.

Pia alisifu utawala uliopo kwa kuingia madarakani wakati huo mgumu baada ya kifo cha John Pombe Magufuli na kusema liwe funzo kwa mataifa mengine.

Katika ujumbe wake wa Ijumaa kuu hapo pia aliomba serikali kuwaachia huru waliowatekwa nyara au kukamatwa bila kufikishwa mbele ya sheria.

Askofu Lwanga alizaliwa mwaka 1953 wilayani Mukono mashariki ya mji wa Kampala.

Kifo cha Lwanga kimetokea wakati Uganda inakabiliwa na mgawanyiko mkubwa wa kisiasa kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali huku upinzani ukidai kuwa baadhi ya wafuasi wao wametekwa.

CHANZO- BBC SWAHILI
Share:

TFF YAMFUNGIA MWAKALEBELA MIAKA MITANO KUTOJIHUSISHA NA SOKA



KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia miaka mitano Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa makosa ya kimaadili.

Pamoja na kifungo hicho, TFF imemtoza Mwakalebela faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kutiwa hatiani kwa maneno ya uchochezi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger