Friday, 29 January 2021

RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI ISAKA-KAGONGWA MKOANI SHINYANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungulia maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka leo tarehe 29 Januari 2021 katika eneo la Kagongwa, Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungulia maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka leo tarehe 29 Januari 2021 katika eneo la Kagongwa, Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishika maji mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka leo tarehe 29 Januari 2021 katika eneo la Kagongwa, Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungulia maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka leo tarehe 29 Januari 2021 katika eneo la Kagongwa, Kahama mkoani Shinyanga.
Sehemu ya Matanki ya kusambazia maji katika mradi huo wa maji Kagongwa -Isaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuzindua upanuzi wa Mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika mji mdogo wa Kagongwa na Isaka Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 29 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Meneja mradi Mhandisi Felister Lyimo kuhusu mradi wa maji wa Isaka-Kagongwa kabla ya kuzindua mradi huo wa maji mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Meneja mradi Mhandisi Felister Lyimo kuhusu mradi wa maji wa Isaka-Kagongwa kabla ya kuzindua mradi huo wa maji mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kagongwa mkoani Shinyanga mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji. 

PICHA NA IKULU
Share:

MHUBIRI ALIYEJIGAMBA KUFUFUA WAFU SIKU YA ALHAMIS AKAMATWA



Mhubiri Onyebuchi Okocha kutoka Nigeria ambaye alidai kwamba angewafufua wafu siku ya Alhamisi, Januari 28, 2021, amekamatwa na maafisa wa polisi.

Onyebuchi Okocha ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Amafor alikamatwa siku ya Jumatano, Januari 2021, hii ni kwa mujibu wa taarifa za Anambra Broadcasting Servicen nchini humo.

Hata hivyo, nabii huyo ameomba msamaha ingawa serikali ya Anambra imesema itakabiliana naye kisheria kwa sababu anawapotosha wananchi.

Video zake kadhaa zimekuwa zikienezwa mitandaoni zikimuonyesha Nabii huyo akifanya miujiza kadhaa. 

Video ya hivi punde, ilimuonyesha mhubiri huyo akiwarushia noti wanaume waliokuwa uchi wakiwa ndani ya mto.

 Serikali ya Anambra ilighadhabishwa na video hiyo, maelfu ya wananchi wa Nigeria pia walitoa maoni tofauti wakikashifu vitendo vya mhubiri huyo. 

Mhubiri huyo amekuwa akionywa kwa mara kadhaa kuhusiana na vitendo vyake lakini inaonekana hajakuwa akitilia maanani, serikali ya Anambra imeapa kukabiliana naye kisheria.

Via Tuko News

Share:

MHUBIRI ALIYEJIGAMBA KUFUFUA WAFU SIKU YA ALHAMIS AKAMATWA



Mhubiri Onyebuchi Okocha kutoka Nigeria ambaye alidai kwamba angewafufua wafu siku ya Alhamisi, Januari 28, 2021, amekamatwa na maafisa wa polisi.

Onyebuchi Okocha ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Amafor alikamatwa siku ya Jumatano, Januari 2021, hii ni kwa mujibu wa taarifa za Anambra Broadcasting Servicen nchini humo.

Hata hivyo, nabii huyo ameomba msamaha ingawa serikali ya Anambra imesema itakabiliana naye kisheria kwa sababu anawapotosha wananchi.

Video zake kadhaa zimekuwa zikienezwa mitandaoni zikimuonyesha Nabii huyo akifanya miujiza kadhaa. 

Video ya hivi punde, ilimuonyesha mhubiri huyo akiwarushia noti wanaume waliokuwa uchi wakiwa ndani ya mto.

 Serikali ya Anambra ilighadhabishwa na video hiyo, maelfu ya wananchi wa Nigeria pia walitoa maoni tofauti wakikashifu vitendo vya mhubiri huyo. 

Mhubiri huyo amekuwa akionywa kwa mara kadhaa kuhusiana na vitendo vyake lakini inaonekana hajakuwa akitilia maanani, serikali ya Anambra imeapa kukabiliana naye kisheria.

Via Tuko News

Share:

DIAMOND PLATNUMZ AFUNGUKA KUHUSU BABA YAKE MZAZI

Mwanamuziki nyota wa Tanzania maarufu kama Diamond Platnumz, ameweka bayana ukweli kuhusu baba yake mzazi.

Akizungumza katika mahojiano na Wasafi Radio,jana Diamond amesema licha ya kuishi vizuri na mzee Abdul ambaye awali alifahamika kama baba yake, lakini mwaka 2000 aligundua kuwa baba yake mzazi ni mzee Nyange ambaye kwa sasa ni marehemu.

''Nikiwa na kama miaka 11 hivi niliambiwa na mmoja wa majirani zangu kwamba nenda pale kwenye soko la Tandale, halafu muulizie Salum Bubu au Iddi Nyange, nikafika akanipa shilingi mia mbili na mchele, kwa sababu alikua anauza mchele wa ujumla'',alisema Diamond.

''Mwanzoni nilikuwa naona utofauti kwenye vitu vingi, lakini sikuweza kuelewa baadhi ya vitu kwa sababu ya utoto'' ,aliongeza Diamond.

Katika maelezo yake leo, Diamond amesema alilitambua suala hilo tangu mwaka 2000 baada ya mama mzazi wa msanii Rommy Jones ambaye pia ni ndugu yake kumuelekeza kuhusu Salum Nyange.

“Alinieleza kuwa kipindi hicho baba alikuwa anauza mchele katika soko la Tandale. Nilipofika Tandale sokoni nilionana naye na kumueleza kwamba nimeelekezwa kuwa yeye ni baba yangu akanipa mchele na Sh200, ule mchele niliupeleka nyumbani.”

“Kipindi hicho hawakuwa na ukaribu na mama yangu hivyo ukawa ndio utaratibu wangu naenda kila mara kumuona hali iliyopelekea yeye na mama wakarudisha mahusiano,” amesema Diamond.

Katika maelezo yake msanii huyo anayewania tuzo za MTV Mama mwaka 2021 amesema alipelekwa Kariakoo na kukutana na ndugu zake wengine akiwemo Ricardo na Iddy Santus na waliishi kwa upendo.

“Tukawa na upendo wa ajabu..., tangu kipindi hicho nikawa sikai tena Tandale nikawa nakimbilia Kariakoo. Ila kipindi hicho chote nilikuwa sina uhakika familia yangu halisi ni ipi,” amesema Diamond.

Amesema alipokuwa mkubwa alibaini kuwa wale ni ndugu zake kwa kuwa walikuwa wakiendana na kubainisha kuwa hakuwahi kuishi na msanii Queen Darlin ambaye ni mtoto wa mzee Abdul.

“Miezi minne iliyopita ndiyo nilizungumza na mama yangu kuhusu hili jambo na kupata uhakika kuwa baba yangu mzazi ni nani baada ya kuangalia tena zile picha za mzee wangu.”

“Kuna kipindi mzee Abdul alikuwa anaumwa na nilikuwa nikienda kumsalimia lakini mama yake (mzee Abdul) alikuwa ananifukuza. Kuna siku nilikwenda na Queen Darlin akatuambia tumetumwa na mama zetu kwenda kumchora tukidhani atakufa turithi mali. Nikawa nawaza mbona yanatokea hayo lakini upande ule mwingine (wa Nyange) wananipenda na mwanzoni hilo lilikuwa linanisumbua sana,” amesema.

Amedai licha ya mzee Abdul kutokuwa naye karibu hakikumzuia kumsaidia jambo ambalo mama Dangote hakulipenda kwa madai kuwa mzee huyo alikuwa anamzungumzia vibaya Diamond kwenye vyombo vya habari.

Siku ambayo mama Dangote alieleza kuhusu baba yake Diamond, mzee Abdul alihojiwa na televisheni mbalimbali na kusema kuwa kama jambo hilo limezungumzwa na mama Dangote, yeye hana cha kuongeza licha ya awali kupinga kwamba yeye si baba wa Diamond.

Takribani wiki mbili zilizopita,  kulikuwa na gumzo mtandaoni kuhusu baba aliyefahamika kama mzazi wake Diamond kuwa si baba halisi wa mwanamuziki huyo.

Gumzo hilo lilianza mara baada ya mama yake Diamond kuongea kwenye radio kuwa baba ambaye anadai Diamond amemtelekeza si baba wa kumzaa, baba yake Diamond ni marehemu na alikuwa anaitwa Nyange na si Abdul.

Mama huyo aliweka picha ya Diamond ikiwa pamoja na Nyange, kuonesha jinsi wanavyofanana.

Hatua hiyo imeendelea kuzua mijadala katika mitandao ya kijamii nchini humo, haswa baada ya baba anayedai kuwa ndiye mzazi wake ''Abdul'' kutoridhishwa na tukio hilo kwa madai ya kwamba aliukataa ujauzito.

''Kama niliukataa ujauzito, iweje nimlee Diamond miaka yote hiyo? alihoji Mzee Abdul ambaye alimlea Diamond tokea akiwa mdogo na watu wengi kudhani kuwa ndiye baba yake mzazi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 29,2021


























Share:

TMDA INAVYODHIBITI UTENGENEZAJI NA UINGIZAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA KUHAKIKISHA USALAMA KWA WATUMIAJI


Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Kanda ya Ziwa Sophia Mziray akielezea kuhusu wanavyodhibiti Dawa na Vifaa tiba vinapotengenezwa au kuingizwa nchini na kwenye masoko
Ofisi ya Mamlaka ya Dwa na Vifaa Tiba Kanda ya Ziwa.

………………………

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa imesema inafanya kazi ya kudhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata Dawa na Vifaa vyenye ubora,Usalama na Ufanisi.

Imesema kuwa imekuwa na ufatiliaji dawa katika mnyororo mzima wakati inaingia na wakati usambazi kutoka chanzo Kikuu na kwenda kwa watumiaji.

Hata hivyo amesema wafanyabiasha wafuate taratibu kwani hawawezi kupitisha dawa na ikaendelea kuumiza wananchi wamejipanga kila sehemu ya mipaka ili khakikishakila kitu kinakwenda sawa.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi za Kanda ya Ziwa hivi karbuni Meneja Meneja wa TMDA Sofia Mziray Kanda hiyo amesema kuwa udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba unahitaji ushirikiano na wadau mbalimbali kwani madhara yatokanayo na Dawa wakati kunapotokea tatizo hayawezi kugusa mtu mmoja Bali yatagusa watu wote kutokana dawa ilivyosambaa.

Amesema Kanda ya Ziwa ina Mikoa Sita pamoja na mipaka ya nchi zilizo katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo bila kuwa na utaratibu wa kufuatilia uingizaji wa Dawa kunaweza kutoa mwanya kwa wafanyabiashara kuingiza dawa bandia ,au zilizoisha muda na kuleta madhara katika jamii.

Mziray amesema kutokana na Ofisi ya Kanda ya Ziwa kuwa Mwanza wameweza kusogeza huduma Bariadi mkoani Simiyu ambapo watahudumia Mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki.

Amesema wamekuwa na ukaguzi aina tofauti ukiwemo ukaguzi elekezi wa majengo mapya ya kutengenezea dawa ,Uhifadhi wa dawa ,Vifaa Tiba pamoja na vitendanishi kwa kutoa ushauri wa kitaalam kabla kuanza uzalishaji.

Amesema pia kuna ukaguzi wa kawaida katika kujihakikishia kuwa bidhaa zinaendelea kuzalishwa ,kuhifadhiwa kwa kutoa utaratibu zikiwa na ubora,salama na zenye ufanisi.
Share:

Thursday, 28 January 2021

WADAU WA HABARI KANDA YA ZIWA WAAHIDI KUENDELEA KUFANYA KAZI NA VYOMBO VYA HABARI

Wadau wa Habari wa Kanda ya Ziwa wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na vyombo vya Habari Nchini  ili kuifikia jamii na kuihabarisha juu ya shughuli wanazofanya.

Hayo yamesemwa kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliondaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) kuelekea tukio la hafla ya usiku ya Waandishi wa habari na wadau wa Habari iliyopangwa kufanyika Februari 1 mwaka huu.

Mwakilishi wa NHIF  Paul Bulolo alisema kuwa, Vyombo vya Habari na Waandishi wa habari wamekuwa na mchango mkubwa kwa kuwa daraja la kufikisha taarifa kwa jamii zinazofanywa na NHIF juu huduma za afya.

Naye Mkurugenzi wa shirika la EMEDO Editrudith  Lukanga amesema kuwa, Waandishi wa Habari wana nafasi kubwa ya kufikisha taarifa kwa jamii na hivyo kuwaomba waandishi kupitia klabu ya Mwanza kushirikiana na EMEDO ili kujua programu zinazowagusa wanawake na vijana zinavyotekelezwa.

Kuwa upande wake, Mkurugenzi wa Yuhoma Education Limited Bwana Yussuf Yuhoma amesema kuwa, vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa hasa kwenye kuemimisha, kuhabarisha na kuburudisha hivyo amesema wataendelea kufanya kazi na waandishi wa habari.

Bwana Makwaya Makani kutoka kampuni ya Jambo alisema  kuwa, kampuni yao inatambua mchango wa vyombo vya habari na hata wao wana mpango wa kufungua kituo cha redio kitakachoitwa Jambo FM ili kuchangia maendeleo ya Taifa na  kufanya kazi na klabu ya Waandishi ya Mwanza kwa ukaribu.

Mwakilishi wa kampuni ya bia ya TBL Diamond Mawai alisema kuwa,wao walianza zamani kufanya kazi na waandishi wa habari hivyo anatambua umuhimu wao na wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha.

Bwana Kalebe   Luteli mwakilishi toka Hospitali ya Bugando ameweka wazi kwamba  kwenye sekta ya afya Bugando imefanya mambo makubwa kupitia ushirikishwaji wa waandishi wa habari hivyo wataendelea kufanya kazi kwa karibu na waandishi.

Naye Mwenyekiti wa MPC bwana Edwin Soko alisema kuwa, wadau wa habari wasiviogope vyombo vya habari kwani waandishi wa habari sio maadui wa wadau wa habari bali ni marafiki zao.

Soko aliongeza kuwa, kukiwepo ushirikiano baina ya wadau wa habari na vyombo vya habari basi ni rahisi wananchi kupata maendeleo.

Usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari utafanyika Februari 1 kwenye Hotel ya Gold Crest Mwanza.

Share:

SILINDE : TAMISEMI TUTAPAMBANA NA WANAOWANYANYASA MACHINGA

Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema Wizara ya TAMISEMI imejikita kwenye Kuondoa kero na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara Wajasiriamali wadogo wadogo almaarufu kama Machinga.

Ameyasema hayo leo Mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa Kongamano la Machinga lililo fanyika jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwashukuru kwa kuiamini Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kutatua kero na changamoto zinazowakabili Machinga

"Kama Wizara ya TAMISEMI Tumepokea na kusikiliza changamoto za Machinga na tunazifanyia kazi. Changamoto ya Mikopo tumetoa nafasi kwa Machinga wakiwa na vitambulisho vya ujasiriamali mkajiunga vikundi mnapewa mikopo",amesema Silinde

Pia amegusia Tatizo la unyanyasaji wa Wafanyabiashara hao unaofanywa na Mgambo na kuahidi kulifanyia kazi.

"Kuna kero pia ya Mgambo kuwasumbua Machinga na sio kwamba wanatumwa na Serikali kuwanyanyasa wananchi bali ni hulka zao binafsi. Serikali ya Rais Magufuli haitavumilia wananchi wake kunyanyaswa tutashuka na kuwashughulikia",amesema.

Pia ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafanya mikutano ya Hadhara kila mwaka na Machinga ili kusikiliza kero zao na kuzitatua.

"Machinga wamekuwa wakiomba mikutano na viongozi wa wilaya ili kusikiliza Changamoto na kero na tumeahidi kila mwaka mikutano miwili hadi mitatu ili kuwaskiliza",amesema Silinde.

 

Share:

UMMY MWALIMU : NEMC MSIFANYE KAZI YA UPOLISI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa umma ili kuwasaidia wenye viwanda na wawekezaji kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Amesema hayo hii leo, Jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Majukumu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Waziri Ummy amesema kuwa kumekuwa na malalamiko ya ucheleweshaji wa vibali, utozwaji wa faini kubwa hivyo ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kufanya kazi kwa weledi zaidi na kuwaelekeza wawekezaji kufuata taratibu.

“NEMC mna kazi ya kuwasaidia wawekezaji kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na si vinginevyo, mkiwa wakali watu hawatatii Sheria lakini mkielimisha jamii itatii” ,Waziri Ummy alisisitiza.

Awali akiwasilisha taarifa ya Majukumu ya NEMC Mkurugenzi Mkuu Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa Sheria ya Mazingira, 2004 na Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Tathmini ya Athari na Ukaguzi wa Mazingira) (marekebisho), 2018 zinataka miradi yote inayowekezwa nchini kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) kabla ya kuanza kutekelezwa. Miradi iliyowekezwa kabla ya kuwepo Sheria ya Mazingira inatakiwa kufanyiwa Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Audit).

“Baraza limesajili jumla ya Wataalam elekezi wa mazingira 908 kwa ajili ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na  423 wa Ukaguzi wa Mazingira. Kati ya hao Makampuni yaliyosajiliwa kufanya EIA ni 173 na EA ni 94”, Dkt. Gwamaka alisisitiza.

Amesema, Baraza limeendelea kuboresha kanzidata ya wataalamu hao na kupata wataalam Washauri 299 wenye sifa za kutoa ushauri wa masuala ya mazingira na kuwasilisha miradi yao. Kati ya Wataalam hao 191 ni wataalam binafsi (Individual Environmental Experts) na 108 ni kampuni  (Firms of Environmental Experts).

Kutokana na azma ya Serikali ya kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, Baraza limekuwa likipokea miradi mingi na linatarajia ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta hiyo. 

Katika kukabiliana na malalamiko ya wadau kuhusu Tozo, kanuni ya ada na tozo za Mazingira ya mwaka 2016, 2018, 2019 imepunguza baadhi ya tozo katika Sekta ya Kilimo, Usajili wa Miradi ya Tathmini ya  athari kwenye Mazingira (TAM).

Kwa upande mwingine Mjumbe wa Kamati hiyo Askofu Josephat Gwajima ametoa ushauri kwa Serikali kubuni miradi ya kuchakata taka ili kuzalisha nishati. “Ndugu zangu taka hivi sasa ni mali, naishauri Serikali kutazama suala hili kwa kina na kuhimiza utenganishaji wa taka kuanzia ngazi ya kaya”, Gwajima alisisitiza.


Share:

MOI YAWEKA HISTORIA KWA MARA YA KWANZA.... YAANZA KUTOA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA MISHIPA YA DAMU KWENYE UBONGO BILA KUFUNGUA FUVU


Mgonjwa akifanyiwa uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila ya kufungua fuvu katika maabara ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo (Angio Suite ) iliyopo MOI. Huyu ni mgonjwa wa kwanza toka ujenzi wa maabara hiyo yenye thamani ya Tsh Bilion 7.9 ikamilike.
Madaktari bingwa wakifanya huduma ya uchunguzi wamishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akiwa na Mkurugenzi wa tiba MOI Dkt Samuel Swai pamoja na madaktari wengine wakifuatilia huduma ya uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu wakiwa katika chumba maalum ambacho waliweza kushuhudia upasuaji moja kwa moja. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akiwa katika picha ya pamoja na jopo la madaktari bingwa, wauguzi na wataalamu wa radiolojia kutoka MOI, MNH, AGHAKHAN na JKCI walioshiriki katika tukio la kihistoria la kuchunguza ubongo bila kufungua fuvu.

*******************************************

Taasisi ya Mifupa Muhimbili- MOI Imeandika Historia ambapo kwa mara ya kwanza imeanza kutoa huduma ya uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu la kichwa katika maabara ya kisasa ya upasuaji wa ubongo (Angio Suite).

Uchunguzi huo umefanywa kwa masaa 3 na jopo la madaktari bingwa, wauguzi, watalamu wa radiolojia wazalendo 6 kutoka MOI, MNH,JKCI pamoja na hospitali ya Aghakhan. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema kuanza kwa maabara hii ni ishara ya mageuzi makubwa katika sekta ya afya hapa nchini kwani maabara ya kisasa kama hii haipo kwenye nchi nyingine kwenye ukanda wa afrika mashariki kati.

“Leo ni siku ya furaha sana kwani tumeanza kutumia maabara yetu ya upasuaji wa ubongo (Angio suite) ,hii imewezekana kutokana na dhamira ya dhati ya Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini kwani maabara hii imejengwa Serikali ya awamu ya Tano kwa zaidi ya Tsh Bilioni 7.9, kwakweli tunamshukuru sana Mh Rais” Alisema Dkt Boniface

Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo MOI Dkt Lemery Mchome amesema kuanza kwa maabara hii kumeleta mageuzi makubwa katika huduma za uchunguzi na upasuaji wa ubongo hapa nchini kwani hakuna mgonjwa atakayelazimika kwenda nje ya nchi kufuata huduma hii ambayo ilikuwa haipatikani hapa nchini.

“ Tunashukuru upasuaji umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa, tumeweza kufika kwenye ubongo wa mgonjwa bila kufungua fuvu, tumefanya upasuaji huu katika mazingizra mazuri kwani mitambo hii ni ya kisasa sana, kama mnavyoona mgonjwa yuko macho na anaongea vizuri kabisa ,hana kovu wala maumivu, hii ni hatua kubwa sana kwetu kama wataalamu.

Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji huo Bwana Hafidhi saidi kutoka mkoani Singida amemshukuru Mungu kwa huduma aliyopata kwani amakuwa akipata maumivu kwa kipindi kirefu bila kujua anasumbuliwa na ugonjwa gani.

“Namshukuru sana Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua vifaa hivi ambavyo vimesaidia leo nimehudumiwa hapa MOI, Nawashukuru madaktari na wataalamu wote walionihudumia, nimefurahi sana na nawaambia watanzania wenzangu wenye shida kama yangu waje wahudumiwe hapa MOI,” Alisema Hafidhi

Huyu ni mgonja wa kwanza kupata huduma katika maabara hii ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo iliyojengwa na Serikali ya awamu ya Tano Kwa zaidi ya Tsh Bilioni 7.9

Share:

NAIBU WAZIRI UMMY NDERIANAGA: TUNACHUKUA HATUA MADHUBUTI KULINDA NGUVU KAZI YA NCHI


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderianaga, akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya Huduma ya Kwanza ambao ni watumishi wa TANESCO alipohitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderianaga, akikabidhi vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya Huduma ya Kwanza ambao ni watumishi wa TANESCO alipohitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, akitoa maelezo ya awali mbele ya Mgeni Rasmi (Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu) wakati wa kufunga mafunzo ya Huduma ya Kwanza yaliyotolewa na OSHA kwa watumishi wa TANESCO.
Mkufunzi kutoka OSHA, Nathanael Mbwambo, akifundisha somo la Huduma ya Kwanza kwa vitendo katika mafunzo hayo yaliyotolewa kwa watumishi wa TANESCO jijini Mwanza.

********************************************

Na Mwandishi Wetu

Serikali imesema inachukua hatua za maksudi za kulinda nguvu kazi yake dhidi ya majanga, ajali na magonjwa yatokanayo na kazi ambayo yanaweza kutokea na kuwaathiri wafanyakazi hususan katika kipindi hiki ambacho nchi inajenga uchumi imara wa viwanda.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Ummy Nderianaga, ameyasema hayo wakati akihitimisha mafunzo ya Usalama na Afya kazini yaliyokuwa yakitolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Nderiananga amesema TANESCO ina nafasi muhimu katika kuliwezesha Taifa kufikia agenda yake ya kujenga uchumi wa viwanda ambapo ufanisi wa shirika hilo unategemea uwepo wa wafanyakazi ambao watakuwa salama na wenye afya njema.

“Bila shaka mnatambua umuhimu wenu na Shiriki lenu katika kufanikisha agenda ya nchi yetu ya kuimarisha uchumi kupitia mageuzi ya viwanda ambapo ili kufikia azma hiyo ni lazima kuwe na umeme wa uhakika. Hata hivyo, upatikanaji wa uhakika wa nishati hiyo muhimu unategemea uwepo wa watumishi wenye afya njema na wenye ujuzi stahiki kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao,”alisema Naibu Waziri huyo.

Aidha, Nderianga amesema ili jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kuleta maendeleo hususan ujenzi wa miradi mikubwa ya umeme na miradi mingine ziwe na tija ni lazima kuhakikisha kwamba nguvu kazi yake inalindwa ipasavyo.

“Ni kutokana na sababu hii ya msingi ndio maana leo mko hapa ili kupewa nyenzo za kujiepusha na madhara ya ajali na magonjwa yanayoweza kujitokeza katika maeneo yenu ya kazi. Kwasababu hiyo, ninaupongeza uongozi wa Shirika pamoja na OSHA kwakuliona hilo na kuchukua hatua kwa wakati,”aliongeza Naibu Waziri.

Akitoa maelezo ya awali kwa Mgeni Rasmi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema mafunzo hayo ambayo yalijikita katika masuala ya utoaji wa Huduma ya Kwanza mahali pa kazi yalitolewa kwa takribani siku tisa kwa makundi matatu tofauti ya watumishi wa TANESCO ambapo kila kundi lilipata mafunzo hayo kwa siku tatu.

Kwa mujibu wa Mtendaji huyo mkuu wa OSHA zaidi ya watumishi 120 wa TANESCO kutoka katika mikoa mbali mbali hapa nchini wamepatiwa mafunzo ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao katika hali ya usalama na afya.

“Tunafahamu TANESCO mnafanya kazi ambazo ni hatarishi hivyo pamoja na kwamba mna fahamu lakini tumeona kuna umuhimu wa kuendelea kukumbushana ili kuweza kuokoa maisha au kupunguza madhara pale ajali au magonjwa yanapotokea katika sehemu zetu za kazi,” alieleza Mwenda.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt.Phillis Nyimbi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo amesema OSHA imekuwa ikifanya vizuri katika Kanda ya Ziwa hususan katika kutoa miongozo na maelekezo kuhusu masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

Aidha, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Dativa Mahembe na Elton Mwashala wamebainisha kwamba mafunzo waliyoyapata yataleta tija katika kazi zao za kila siku hususan katika kuokoa maisha au kupunguza athari miongoni mwa wafanyakazi wanaopata ajali au changamoto mbali mbali za kiafya wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Japo mafunzo haya yamefanyika kwa siku tatu tu, kiukweli tumejifunza mambo mengi sana ambayo ni muhimu si tu katika sehemu za kazi lakini pia hata majumbani na mahali pengine,” alisema Dativa Mahembe ambaye ni mshiriki na pia mratibu wa mafunzo hayo.

OSHA ni taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) ambayo majukumu yake ya msingi ni pamoja na kufanya ukaguzi wa Usalama na Afya katika sehemu za kazi na kutoa mafunzo mbali mbali yakiwemo ya Huduma ya Kwanza, usalama na afya katika shughuli za ujenzi, usalama na afya katika shughuli za mafuta na gesi, Kozi ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Uchunguzi wa ajali katika sehemu za kazi na kufanya kazi katika majukwaa (Working at Height).

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger