Sunday, 17 January 2021

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA GEOFFREY MWAMBE ATAKA WAHITIMU CBE WAJIENDELEZE KIELIMU


Waziri wa Viwanda na Biashara Geoffrey Mwambe akizungumza kwenye mahafali ya 13 ya Chuo Cha Biashara (CBE) Kampasi ya Mwanza Januari 16 2021

Na Hellen Mtereko Mwanza

Waziri wa Viwanda na Biashara Geoffrey Mwambe amewataka wahitimu wa Chuo Cha Biashara (CBE) kuhakikisha wanajiendeleza kielimu katika ngazi tofauti na kuwa wabunifu ili kuacha dhana ya kuajiriwa.

Hayo aliyasema jana Januari 16 2021 wakati akizungumza kwenye  mahafali ya 13 ya chuo hicho kampasi ya Mwanza. 

Mwambe alisema wahitimu wenye Diploma wajiendeleze ili wafike ngazi ya Stashahada ili kuweza kuwa na nchi yenye wasomi watakaokuja kusaidia taifa.

Aliwataka wahitimu kutumia utalamu wao walioupata  kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii .

 Aliomba mashirika binafsi na ya Serikali yalete  wafanyakazi wao  ili waweze kupata Elimu katika chuo hicho. 

Aidha alisema Serikali itaboresha miundombinu ya Elimu katika vyuo vya CBE nchini kutokana na ongezeko la Wanafunzi wenye uhitaji wa kujiendeleza na sera ya Elimu bure inayoendelea kuinua wasomi wengi.

Aliiomba CBE kuhakikisha inafungua kampasi katika maeneo ya nyanda za Kaskazini na Kusini(Ruvuma/Lindi na Mtwara). 

Pia alikiagiza Chuo hicho kuhakikisha kinakuja na mkakati  wa Kukuza Ujasiriamali ili kupata wafanya biashara wenye Elimu na ujuzi kutoka chuoni hapo.

Mkuu wa Chuo cha CBE,Kampasi ya Mwanza Profesa Emmanuel Mjema alisema jumla ya wahitimu 447 wamehitimu katika ngazi tofauti. 

Mjema alisema chuo chao kipo katika mkakati wa kuweza kuanzisha kozi mpya ya Stashahada ya masoko na Utalii ili kwendana na kasi iliyopo.

Alisema Chuo chao kipo kwenye mkakati wa kuanzisha chuo  katika mkoa wa Iringa na Zanzibar kutokana na maombi mengi anayopokea kutoka kwa wananchi wenye kufahamu umuhimu wa Elimu.

Aliipongeza Serikali kwa kuwezesha kuongeza bajeti ya mikopo kwa Elimu ya juu ambapo na Chuo chao kimenufaika pia  ameipongeza Serikali kwa kuwalipia fedha za kununua eneo la chuo hicho katika eneo la Kangae mkoani Mwanza
Share:

Tanzia : MSANII WA BONGO FLEVA CPWAA AFARIKI DUNIA

Msanii Cpwaa enzi za uhai wake
Msanii wa Bongo Fleva Ilunga Khalifa maarufu 'C Pwaa'amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 17,2021 akiendelea na matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam.
CPWAA ambaye aliwahi kuunda kundi la Park Lane akiwa na msanii mwenzake Suma Lee kabla ya kundi hilo kuvunjika mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Tutawaletea taarifa zaidi hivi punde
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 17,2021

Share:

Saturday, 16 January 2021

HEWA YA UKAA YAWAPAISHA KIUCHUMI WANANCHI WILAYA YA TANGANYIKA

Share:

YOWERI MUSEVENI ATANGAZWA MSHINDI UCHAGUZI WA URAIS UGANDA



Yoweri Museveni ametangazwa kuwa rais mteule Uganda baada ya kupata ushindi wa kura asilimia 58.64.

Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) imemtangaza Yoweri Kaguta Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamisi tarehe 14 Januari 2021.

Kwa mujibu wa EC Bw Museveni amepata kura 5,851,037 sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa.

Mpinzani mkuu wa Museveni, mwanamuziki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 3,475,398 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote.

Bobi Wine hata hivyo alitangaza kutokukubaliana na matokeo hapo jana wakati tume ya EC ilipokuwa ikiendelea kutangaza matokeo.



Idadi kamili ya watu waliopiga kura ni 9,978,093 ikiwa ni sawa na asilimia 57.22 tu ya idadi ya watu waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Hii inamaana kuwa zaidi ya asilimia 40 ya waliojiandikisha hawakujitokeza kupiga kura.

Rais Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 akiwa atakuwa anaingia kuongoza kwa muhula wa sita.

Bwana Museveni mwenye miaka 76-anasema kuwa amelifanya taifa hilo kuwa na maendeleo wakati Bobi Wine, ambaye ana miaka 38- jina lake alisi likiwa Robert Kyagulanyi, anasema anawakilisha vijana ambapo Uganda likiwa ni taifa ambalo lina vijana wengi zaidi duniani.

Ijumaa, wakati matokeo yakianza kutangazwa bwana Wine alisema askari walikuwa wameizingira nyumba yake.

Lakini msemaji wa serikali alimshutumu kwa kuweka taharuki isiyo na ukweli ili kupata huruma ya watu.

 CHANZO - BBC SWAHILI

Share:

WAZIRI JAFFO ATAKA VIONGOZI NA WASIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI WA MAJENGO YA UVINZA KUKAMATWA NA KUWEKWA NDANI


Jengo la Utawala la halmashauri ya wilaya Uvinza ambalo ujenzi wake umekwama
Jengo la nyumba ya Mkuu wa wilaya Uvinza ambalo limekwama tangu mwaka 2013 licha ya watekelezaji wa mradi wakala wa majengo (TBA) kupokea milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huo
**

Na Editha Karlo,Uvinza

WAZIRI wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa Suleiman Jaffo ameamuru kukamatwa na  kuwekwa ndani kwa viongozi na wasimamizi wa miradi wa wakala wa majengo nchini (TBA) mkoa Kigoma kwa kushindwa kukamilisha miradi ya ujenzi waliyopewa wakati walichukua kiasi kikubwa cha pesa.

Jaffo ameyasema hayo leo kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Kigoma 

Akiwa kwenye ziara ya kukagua majengo ya Utawala ya viongozi na watumishi walio chini ya wizara hiyo Wilayani Uvinza alikerwa na taarifa ya ujenzi wa majengo hayo.

Akiwa wilayani Uvinza Waziri  Jaffo alieleza kukerwa   na taarifa ya  TBA kupewa kiasi Cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza miaka mitano iliyopita ambapo hadi Sasa nyumba hiyo imefikia usawa wa msingi.

Pamoja na hiyo Waziri Jaffo alionyesha kukerwa kutokana na kukwama jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya Uvinza ambapo kiasi Cha shilingi milioni 900 kimetolewa lakini mradi umekwama kwa miaka zaidi ya mitatu na kwa sasa ujenzi upo usawa wa madirisha.

Akitoa taarifa kwa Waziri Jaffo Meneja wa miradi ya ujenzi katika ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma, Masawika Kachenje alisema kuwa miradi hiyo ilianza mwaka 2013 na ilipaswa kukamilika mwaka 2018 na waliomba pesa kwenye miradi hiyo kama malipo ya awali.

Kachenje alisema kuwa pesa kwenye miradi hiyo zimeingizwa kwenye akaunti ya TBA makao makuu lakini taarifa zinaonyesha kuwa pesa hizo hazipelekwi kwenye miradi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Uvinza,Mwanamvua Mrindoko alimweleza Waziri Jaffo kuwa analazimika kuishi kwenye nyumba za kontena zilizoachwa na mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami wa Kidahwe Hadi Uvinza kutokana na kukwama kwa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa wilaya.

Mrindoko alisema kuwa wamefanya jitihada kuhakikisha TBA wanarejesha fedha lakini hakuna jitihada iliyofanyika.

Kutokana na hali hiyo Waziri Jaffo ameagiza kuorodheshwa kwa miradi yote iliyokwama kwa mkoa wa Kigoma ambayo ilikuwa inatekelezwa na TBA, kueleza thamani ya kazi iliyofanyika na kiasi Cha pesa kilichoelekwa na taarifa hiyo iwasilishwe ofisini kwake aweze kuifanyia kazi.
Share:

WANACHUO 13 WASHIKILIWA KWA RUSHWA NA UDANGANYIFU WAKIFANYA MTIHANI WA 'SUP' DODOMA

 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 13 wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) cha Jijini Dodoma kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu wakati wa kufanya mtihani.

Imedaiwa kwamba wanafunzi hao kwa  kutumia rushwa waliweza kurudia kufanya mtihani  nje ya chumba cha mtihani na baadae walijaribu kuingiza karatasi za kujibia  mtihani kwenye mfumo rasmi ambapo alidai Chuo kiliwabaini na kutoa taarifa Takukuru.

Hayo yameelezwa leo Januari 16 ,2021 na  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sostenes Kibwengo wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari juu  ya utendaji wa Takukuru Mkoa wa Dodoma kwa robo ya Oktoba hadi Desemba mwaka 2020.

Kibwengo amesema wanawashikilia wanafunzi hao wa mwaka wa tatu kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu wakati wa kufanya mtihani marudio (supplementary examination) wa somo la Applied Statistics II uliofanyika Novemba mwaka jana chuoni hapo.

Amesema uchunguzi wa awali umeonesha kwamba wanafunzi hao kwa kutumia rushwa waliweza kurudia kufanya mtihani huo  nje ya chumba cha mtihani na baadae walijaribu kuingiza karatasi za kujibia  mtihani kwenye mfumo rasmi ambapo alidai Chuo kiliwabaini na kutoa taarifa Takukuru.

Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Dodoma amewataka waliokuwa wanafunzi wa Chuo hicho,Evarist Nyaki na Lameck Kawinga kuripoti mara moja kwenye ofisi za Takukuru Mkoani Dodoma kwa ajili ya kusaidia uchunguzi huo.

CHANZO - C FM
Share:

Video Mpya : ROGETI - MAGUFULI

Msanii Rogeti ameachia wimbo mpya unaitwa Magufuli..Tazam Video hapa chini

Share:

Wimbo Mpya : KEMA HEWA - MIKOPO

Hii hapa ngoma mpya ya Msanii Kema Hewa inaitwa Mikopo...Sikiliza hapa chini
Share:

Wimbo Mpya : KEMA HEWA - NZALA

 

Msanii wa Nyimbo za asili Kema Hewa Kutoka Ushetu Kahama mkoani Shinyanga ameachia wimbo mpya unaitwa Nzala...usikilize hapa chini

Share:

Wimbo Mpya : MAGAMBO MACHIMU - MICHANGO

Huu hapa wimbo mpya wa Msanii Machimu Magambo unaitwa Michango...Sikiliza hapa chini
Share:

MICHUANO YA MATAIFA YA AFRIKA - CHAN 2021 KUANZA RASMI LEO CAMEROON


Nembo ya shirikisho la soka barani Afrika CAF na picha ya tuzo ya kombe la Mashindano ya CHAN.

Sherehe za uzinduzi wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani yaani CHAN kwa msimu huu wa mwaka 2021 zinataraji kufanyika usiku wa leo wa tarehe 16 januari 2021 nchini Cameroon ambapo michuano hiyo inataraji kuanza kwa michezo miwili ya ufunguzi.

Sherehe za uzinduzi wa michuano hiyo ambayo inafanyika kwa msimu wa sita tokea kuanzishwa kwake mwaka 2009, zitaambatana na tukio maalum ya kumkabidhi tuzo ya heshima ya uongozi uliotukuka kwa Issa Hayatou aliyekuwa rais wa CAF kuanzia mwaka 1988 hadi 2017.

Hayatou anatazamiwa kukabidhiwa tuzo hiyo ndani ya ardhi ya nchini kwake Cameroon na muwakilishi wa shirikisho la soka la barani Afrika anayekaimu nafasi ya Ahmad Ahmad aliyefungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa miaka mitano kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.

Sherehe ya ufunguzi wa michuano hiyo itazinduliwa na mgeni rasmi wake rais wa shirikisho la soka Duniani FIFA, Gianni Infatino ambaye ataambata na viongozi wa mashirikisho mbalimbali Afrika na mwenyeji wake Seydou Mbombouo anayekaimu nafasi ya urais wa shirikisho la soka nchini Cameroon

Michuano hiyo inashirikisha timu za taifa kutoka mataifa 16 ambazo zipo kwenye mfumo wa makundi 4 kila kundi likiwa na timu 4 ambapo vinara na washindi wa pili wa kila kundi watafuzu kucheza hatua za mtoano kuanzia robo fainali mpaka fainali kwa wale watakaokuwa wanashinda.

Michezo miwili ya ufunguzi ni ile kutoka kundi A, wenyeji Cameroon kufungua pazia na Zimbabwe saa 1:00 usiku ilhali timu ya taifa ya Mali itakipiga na timu ya taifa ya Burkina Faso mchezo mishale ya saa 4:00 usiku yote kwenye dimba la Amadou Ahidjo jijini Yaounde.

Michezo miwili mingine itaendelea tena usiku wa kesho jumapili ya tarehe 17 Januari 2021 kwa michezo miwili, kutoka kundi B, Libya itakipiga na Niger saa 1:00 usiku, DR Congo dhidi ya Congo saa 4:00 usiku, kundi C Morocco bingwa mtetezi atapepetuana na Togo saa 1:00 usiku wa Jumatatu.

Rwanda na Uganda ni mchezo mwingine kutoka kundi C utakaochezwa siku ya Jumatatu tarehe 18 Januari 2021 mishale ya saa 4:00 usiku ilhali michezo ya kundi D itachezwa siku ya Jumanne tarehe 19 Januari 2021 ambapo Zambia itaumana na Tanzania saa 1:00 usiku na Guinea na Namibia 4:00 usiku.

Mshindi wa kwanza wa michuano hiyo anatazamiwa kuondoka na kitita cha dola za kimarekani milioni 1,250,000 ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni 2, milioni 890 za kitanzania, mshindi wa pili atapata dola 700,000 za kimarekani ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni 1, milioni 600 za kitanzania.

Mshindi wa nne atapata dola za kimarekani 400,000 ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 926 na laki 400 ilhali mshindi wa nne atapata dola 300,000 za kitanzania ambazo ni sawa na milioni 694 na laki 800 a kitanzania. Zawadi hizo zitatolewa mwisho wa mashindano hayo tarehe 7 februari 2021.
Share:

HAYA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020

Share:

HAYA HAPA MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA DARASA LA NNE (SFNA) 2020

Share:

HAYA HAPA MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020

Share:

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (CSEE) MWAKA 2020

Share:

MZEE ABDUL : "MSINIITE TENA BABA DIAMOND, AKITUMIA JINA LANGU NAMSHTAKI....NI JEURI YA PESA, ANAJIONA HATOKUFA"


IKIWA ni saa chache baada ya mama mzazi wa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Sanura Kassim maarufu Mama Dangote, kuanika kuwa Mzee Abdul Juma ambaye wengi wanamjua kama baba mzazi wa Diamond, si baba Mzazi wa Diamond kwani wakati wanaingia kwenye mahusiano, tayari mama huyo alikuwa na ujauzito wa mwanamuziki huyo, basi mzee Abdul naye amejibu mapigo.

“Sasa hivi inabidi msiniite Baba Diamond, niiteni Mzee Abdul peke yake, kama alivyoongea mama na mimi najibu kwa ufupi, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa Baba mlezi, nimepata thawabu hata kama ni ndogo.

“Kwa aliyozungumza najisikia faraja moyoni mwangu kwa sababu nilikuwa najiuliza, kwa nini nikihitaji kitu nakosa, halafu wengine wanapata. Kumbe walikuwa wamekaa na mtoto wake wamepanga mambo yao na leo napata jibu kamili kwamba mimi sio baba mzazi ni baba mlezi.

“Kwa hiyo atakuwa Diamond Platnumz na siyo Naseeb Abdul, akitumia jina langu nitamshitaki, lakini upande wa Queen Darleen kama yeye atakuwa tayari kubaki na mimi kama baba yake, nipo tayari, Diamond tumeachana asitumie tena jina langu, nitabaki kuwa baba mlezi.

“Leo Watanzania wamejua kwa nini nilikuwa sipati misaada kwa sababu siyo mhusika. Lakini alichofeli huyo mama ni jambo moja tu, mimi nimeishi naye tangu mwanzo, akawa mjamzito, nikalea mpaka nampeleka hospitali anakwenda kujifungua, nimelea mtoto mpaka tukaja kugombana akiwa form one, lakini leo ametoa kauli kama hizo inaonekana walikaa wakapanga na mtoto wake wafanye hivyo.

“Mama Diamond hakuwa na mahusiano mengine, kimsingi mimba ya kwanza tulitoa, mpaka nikauza mkanda wangu wa deki ili tukatoe mimba ile. Baadaye tukafanya tena ndipo akapata ujauzito wa Diamond. Kumbe nilikuwa napigwa picha za kudharirishwa? Na mimi nazungumza kwamba Diamond Platnumz siyo mwanangu, sihusiki naye na sipo kwenye familia yao.

“Mtoto hagombaniwi, hata mpaka wa nyumba haugombaniwi, kama sio riziki yako achana nacho, najua kama asingekuwa na pesa yasingetokea haya, pengine kwa sababu anajiona hatokufa, wamenivunjia adabu, kama ni mambo ya kifamilia wangeniita tukayamaliza kumbe ndiyo maana nilikuwa nababaishwa.

“Diamond alizaliwa Hospitali ya Amana, nilihusika mwanzo mpaka mwisho, malezi na kila kitu lakini hii ni kiburi tu cha pesa, bahati nzuri Diamond hajawahi kunisaidia chochote, nina maisha yangu napata kidogo kinanitosha. Wakamwonyeshe kaburi la baba yake basi, kama atamfanya Queen Darleen ni mfanyazi wake sawa tu,” amesema Mzee Abdul.

Januari 15,2021 Mama Dangote alifunguka kupitia kipindi cha MashamSham, kinachoruka kupitia Wasafi FM baada ya kupigiwa simu LIVE kufuatia mahojiano ya Ricardo Momo ambaye ameelezea kuwa ni kaka yake na Diamond kwani wanashea baba mmoja ambaye anaitwa Salum Iddy Nyange (marehemu kwa sasa).

Sanura Kassim maarufu mama Dangote ambaye ni mama mzazi wa msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz amesema baba halisi wa mwanaye ni Salum Iddi Nyange na si Abdul Juma ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifahamika kama baba wa mkali huyo wa Bongofleva.

Katika majibu yake, mama Dangote amesema Ricardo na Diamond ni ndugu na baba yao ni Nyange ambaye kwa sasa ni marehemu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger