Wednesday, 13 January 2021

Results Based Mgmt Specialist at UNDP

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Background The UN Resident Coordinator’s Office (RCO) in Tanzania supports the Resident Coordinator in promoting attainment of the Sustainable Development Goals and the Africa Agenda 2063. It provides strategic guidance and coordination assistance for the design and delivery of the UN’s Cooperation Framework, UN Development Assistance Plan 2015-2022 (UNDAP II). Under the direct guidance and […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Teacher – Early Childhood at Kazini Kwetu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

EARLY CHILDHOOD TEACHER On behalf of a client who runs a reputable school in Kigamboni, we are looking for Teacher – Early Childhood to work in Kigamboni. The desired candidate should have at least 2 years of experience and either Certificate or Diploma in Early Childhood Development. Duties and Responsibilities Organizes and provides developmentally appropriate […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Sales Consultant at Kazini Kwetu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

SALES CONSULTANTS On behalf of client, Kazini Kwetu Ltd is looking for two Sales Consultant whose main role will be to increase sales volumes and for the company. The desired candidate should have prior work experience of sales in pest management, construction, agriculture and similar sectors.    Responsibilities and Duties Visit potential/existing customers to demonstrate […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Primary Education Teacher at Kazini Kwetu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

PRIMARY EDUCATION TEACHER Provides a stimulating, safe, and developmentally appropriate educational environment where children have the opportunity to develop cognitive, social, emotional, and physical skills. Provides a block and lesson plan by which classes are conducted. Responsibilities: Develop and issue educational content including notes, tests, and assignments. Supervise classes to ensure all students are learning […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Store Keeper at Kazini Kwetu

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

STORE KEEPER A reputable service company is looking for Store Keeper to be based in Dar es Salaam. An ideal candidate should have at least two years experience of working in a store or warehouse with a good command in both English and Swahili. Responsibilities Oversees and administers the operations of a store. Receives, identifies […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

STORE OFFICER at WASSHA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

STORE OFFICER   JOB BRIEF:   The main responsibility to receive, store and issue supplies and equipment for the day to day WASSHA operations. Work closely with other departments, ensure cleanliness and arrangement of all store areas, keeping storage and receiving areas clean and tidy at all times.   He/she also verifies that all supplies […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AHOJI KUNA MAHUSIANO GANI KATI YA LISHE BOIRA NA VIFO VYA WAKINA MAMA WAJAWAZITO VINAVYOTOKANA NA UZAZI

 

Mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga" ambao umeandaliwa na Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani ukiendelea
Mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga" ambao umeandaliwa na Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani ukiendelea

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia NGOs Mhe Neema Lugangira ameandaa mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga"
 
Mkutano huo ulilenga kujadiliana kuhusu uhusiano kati ya vifo vya wakina mama wajawazito wanapojifungua na lishe bora kwa maana ya upungufu wa damu "Anemia".

Katika mkutano huo zaidi ya watu 50 walishiriki kupitia Mtandao wa Zoom ambapo watoa mada waliwakilisha makundi muhimu . 

Watoa mada waliwakilisha makundi muhimu kama Dr. Grace Moshi - Msimamizi wa Masuala ya Lishe; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Dr. Lilian Mnabwiru - Katibu; Chama Cha Madaktari Tanzania huku Anna Sengoka wa Chama Cha Wakunga Tanzania naye akiwasilisha mada.

 Pia katika mkutano huo uliwashirikisha Dr. Ali Said - Daktari Bingwa wa Masuala ya Wanawake na Mwalimu MUHIMBILI na Dr. Isihaka Mwandalima - Mkurugenzi (Technical) - Shirika lisilo la Kiserikali (NGO); Pathfinder International

 Mkutano huu uliendeshwa na Wenyeviti Wawili Mhe Neema Lugangira (Mb.) na Dr. Frank Minja; Rais wa Diaspora ya Watanzania wanaoishi Marekani.

Akizungumza baada ya mkutano Mbunge Neema Lugangira alisema ni  dhahiri mkutano huu wa kwanza kwa hakika umedhihirisha umuhimu wa lishe bora kwa mama mjamzito kabla, wakati na baada ya kujifungua. 

Mhe Mbunge alipoulizwa nini mchango wake katika kufanikisha suala hilo, alisema kuwa Shirika la Agri Thamani Foundation ambalo yeye ni Mkurugenzi lipo mstari wa mbele kuhamasisha ulaji wa matunda na mbogamboga ngazi ya kaya hususan kwa vijana balehe.
 
Alieleza ndio maana shirika hilo limekuja na programu ya kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa sekondari huku msaada huu ukiendana na elimu ya lishe bora ikiwemo kuanzisha bustani za mfano za mbogamboga shuleni na kaya.

Hata hivyo Mhe Neema alisema ni dhamira yake kuendelea kuandaa mijadala ya namna hii kwa njia mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha ajenda ya lishe bora inapata kipaumbele inachostahili".

Kama hukubahatika kushiriki katika majadiliano haya LIVE unaweza kusikiliza mjadala mzima kupitia link hii http://bit.ly/3s9rNjU na ukasoma chat nzima kupitia link hii http://bit.ly/35q9Dki


Share:

CHAMA CHA WANAUME WACHOYO CHAANZISHWA...GUMZO MTANDAONI



Taarifa kuhusu chama cha wanaume wachoyo cha Nigeria- Stingy Men Association of Nigeria (Smen), imeenea kwenye mtandao wa kijamii waTwitter nchini Nigeria huku wanaume maarufu wa Nigeria wakishirikisha umma kadi za uanachama wao wa kikundi hicho.

Ujumbe wa Twitter wa mzalishaji wa muziki Don Jazzy wa kadi yake ya uanachama ulishirikishwa tena na wafuasi wake mara 11,000.

Nyota wa muziki wa Afrobeats Bw Eazi pia alituma kati yake ya uanachama katika chama cha wanaume wachoyokupitia mtandao wa Twitter.

Akaunti rasmi ya chama cha wanaume wachoyo kwenye mtandao wa Twitter ilionekana kwenye mtandao huo kwa mara ya kwanza Jumatatu.

Wanaotuma jumbe za Twitter wamekuwa wakitania kuwa watabuni wimbo wao maalumu, makao makuu na kiapo.

Haijawa wazi ni vipi taarifa ya chama cha wanaume wachoyo iliyoshirikishwa zaidi kwenye Twitter ilivyoanza nchini Nigeria. Wazo hilo tayari limesambaa katika mataifa mengine ya Afrika.

Mwezi Disemba taarifa ya gazeti la Uganda la Daily Monitor iliainisha pendekezo la kikundi hicho nchini Uganda.

Katika taarifa hiyo iliyoandikwa na , Ian Ortega aliandika: "Katiba hii iliandikwa katika mwaka wa janga la corona itaelezea maana ya hatua kali ."

Sehemu ya"katiba yake " iliwalenga marafiki wa kike wanaowaomba wapenzi wako wa kiume pesa.

"Kila binti wa Eva ambaye anaomba pesa atachukuliwa kama muhamiaji haramu na kuepukwa; ‘hafai kuwa mke ,’" aliandika.

Aliendelea kusema kuwa “mjumbe hapaswi kuhisi aibu yoyote katika kukataa ombi lolote la pesa linalowasilishwa kwake.”

Hii ni pamoja na maombi ya pesa za usafiri au salio la simu.
Share:

Taarifa Ya Kukamatwa Kwa Waethiopia 61 Kwa Kosa La Kuingia Nchini Bila Kibali.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata Waethiopia 61 kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata taratibu za nchi.

Ni kwamba tarehe 12.01.2021 majira ya saa 23:00 usiku huko Kijiji cha Gari Jembe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Askari Polisi wakiwa kazini katika kizuizi [Barrier] kilichopo barabara kuu ya Mbeya – Tukuyu walilisimamisha Gari yenye namba za usajili T.509 AZZ Scania Lori lililokuwa likiendeshwa na dereva RABDI RAMADHANI [48] Mkazi wa Unga Limited Arusha.

Askari walianza kufanya ukaguzi kwenye Gari hilo na kumtaka dereva kufungua mlango wa nyuma ya Gari hilo na ndipo walimkamata DAWAT TADESA [22] Raia na Mkazi wa nchini Ethiopia akiwa na wenzake 60 kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Awali katika mahojiano, dereva wa Gari hilo alidai kuwa amepakia bidhaa mbalimbali za dukani lakini baada ya kuamriwa kufungua mlango wa nyuma wa Gari hilo ndipo ilibainika amepakia/anasafirisha wahamiaji haramu kuelekea Kasumulu mpaka wa Tanzania na Malawi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, tunaendelea na mahojiano dhidi ya mtuhumiwa RABDI RAMADHANI [48] Dereva aliyekuwa akisafirisha wahamiaji hao ili kubaini mtandao mzima wa mawakala wa kusafirisha wahamiaji.

Mtakumbuka Oktoba 22, 2020 huko Wilaya ya Mbarali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata Waethiopia 22 kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Sambamba na hilo Disemba 15, 2020 huko Wilaya ya Rungwe Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji lilifanikiwa kuwakamata Waethiopia 57 kwa kosa la kuingia nchini bila kibali pamoja na mawakala wawili waliokuwa wakiwasafirisha.

WITO WA KAIMU KAMANDA:

Ninatoa wito kwa wasafirishaji wa wahamiaji haramu nchini kujiepusha kufanya biashara haramu ya binadamu kwani ni kinyume cha sheria za kimataifa na hata maadili na dini pia inakatazwa.

Kwamba wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wajue kwamba kusafirisha wahamiaji haramu ni kosa la jinai lenye adhabu kali na vyombo vinavyotumika kuwasafirishia hutaifishwa kwa amri ya Mahakama.

Kwamba Mbeya hapapenyeki na iwapo utajaribu tu biashara hiyo haramu utaishia mkononi mwa vyombo vya dola kwani tumejipanga vilivyo kuzuia na kupambana na uhalifu na wahalifu wa kila aina.


Share:

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Uamuzi Wa Kufungua Mashtaka Katika Mashauri Ya Jinai Mikoa Mbalimbali



Share:

VYUO VIKUU NCHINI VYAASWA KUTOA WATAALAMU WENYE UJUZI WA KUJIAJIRI

Katibu Mkuu wa Elimu,Sayansi Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizungumza katika kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa Elimu,Sayansi Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizungumza katika kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Vyuo Vikuu nchini vimeaswa kutoa wataalamu wenye ujuzi wa kuweza kujiajiri na kuajirika ikawa lengo ni kuwa na mitaala yenye kulenga soko nyumbulifu kwa kadri ya mabadiliko ya teknolojia.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Elimu,Sayansi Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo katika kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Akwilapo amesema kunatakiwa kufanyike maboresho makubwa ya mfumo wa utoaji wa elimu ya juu ambayo yatasababisha kuwe na mabadiliko chanya kwenye nyanja zote zinazohusiana na ukuzaji wa uchumi wa nchi yetu.

"Uwepo wa mradi huo utaleta madiliko na mapinduzi katika kujenga uchumi wa kisasa hapa nchini Tanzania". Amesema Dkt.Akwilapo.

Aidha amesema kuwa Serikali ina lengo la kukopa fedha kutoka Benki ya Dunia ili kutekeleza mradi wa kuboresha elimu ya juu kwa ajili ya kuimarisha uchumi nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wanafunzi Wenye mahitaji Maalumu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Bw.Kelvin Mkude amesema mradi wa HEET umekuja katika wakati muafaka kwani umelenga kwa wale wahitimu wa Vyuo Vikuu wawe vizuri katika upande wa ajira hasa kujiajiri.

Naye mwakilishi wa Taasisi ya Serikali ya wanafunzi DARUSO Bi.Ntoteba Hassani amesema mradi huo utawasaidia wanafunzi ambao wapo Vyuo Vikuu kuboresha zaidi mnyororo mzima wa elimu ya Vyuo Vikuu lkiwemo miundombinu kwa kuwezesha watu kupata ajira na kuweza kujiajiri.

Share:

GARI LA KUBEBA MIILI YA MAREHEMU LAKAMATWA LIKIWA NA MIRUNGI BUNDA 1685 TANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda akuzungumza na waandishi wa habari leo kwenye kituo cha Polisi Chumbageni Jijini Tanga kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa anasafirisha mirungi kwenye gari la kubebea miili ya marehemu

 

Gari la kubebea miili ya marehemu ambalo limekamatwa likiwa na mirungi


JESHI la Polisi Mkoani Tanga limemkamata mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam Simon Pasian Tarimo(37) akiwa amebeba mirungi bunda 1685 ambazo ni sawa na kilogramu 133  ikiwa imehifadhiwa ndani ya mifuko sita ya Salfate kwenye gari la kusafirishia miili ya marehemu .

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blausis Chatanda alisema kwamba gari hilo lilikamatwa Januari 12 mwaka huu saa nane usiku huko kwenye Kijiji cha Manga Kata ya Mkata Tarafa ya Mazingira wilayani Handeni.

 

Akieleza namna walivyofanikiwa kukamatwa na gari hilo alisema askari waliokuwa doria walilishtukia na walipotaka kulilisimamisha dereva akataka kukimbia na wakamkimbiza na kufanikiwa kumkamata na walimuhoji sababu za kukimbia akiwa amesimamishwa na Polisi.

 

Alisema baada ya hapo Askari hao walitaka kulipekua na walipolipekua gari wakakuta kwenye eneo la kuweka mwili wakakuta mafurushi sita yakiwa yamehifadhiwa mirungi ndani yake na ni eneo ambalo wakati wa kwenda lilikaa Jeneza na wakati wanarudi ndipo walipoweka mirungi.

 

Kamanda huyo alisema katika mahojiano na dereva huyo alisema baada ya kupelekea mwili  Makanya Usangi wakati wa kurudi njiani eneo ambalo alilweka maiti akaaamua kuweka mirungi akiamini kwamba angeweza kusafiri salama asipekuliwe kwa sababu anaamini watanzania hawana utamaduni wa kukagua na kupekua magari ambayo yamebeba maiti.

 

Alilitaja gari la kusafirisha  miili ya marehemu ambalo limekamatwa na mirungi hiyo kuwa ni lenye namba za usajili T.569 DSZ aina ya Volvo ambalo ni maalumu kwa kubebea miiili ya marehemu ambalo linamilikiwa na mali ya Nuru Funeral Service iliyopo Jijini Dar es Salaam.

 

Kamanda Chatanda alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha mirungi hiyo akitokea Usangi kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo mbinu iliyotumika ni kuweka mfuko kwenye Jokofu linalotumika kuhifadhia Jeneza lenye maiti wakati wa kusafirisha.

Share:

Fisi Azua Taharuki Shinyanga..... Ajeruhi Mzee Wa Miaka 70 Na Mwanae wa Miaka 17


SALVATORY NTANDU
Wakazi wawili wa  Kijiji cha kilimawe kata ya Mwantini mkoani  Shinyanga, Mabuga Ndakuna (70) na Timotheo Mabuga ( 17) wamejeruhiwa na mnyama aina ya fisi wakati wakijaribu kuokoa mifugo yao iliyokuwa kwenye banda la nyumba yao isishambuliwe na mnyama huyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana na kusema kuwa  tukio hilo limetokea Januari 11 mwaka huu majira ya saa 10 alfajiri ambapo fisi huyo alivamia banda la  kuku katika familia ya Mzee  Mabuga na kushambulia kuku ndipo katika harakati za kumfukuza alianza kuwashambulia.

“Mzee Mabuga Ndakuna aling'atwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani,miguuni na kuvunjwa mkono wa kushoto huku mwanae Timotheo aking'atwa sehemu mbalimbali za mwili wake kama vile mikono,miguuni na mabegani,”alisema Magiligimba.

Kamanda Magiligimba alisema kuwa  chanzo cha tukio hilo ni  mnyama huyo aina ya fisi kuvamia banda la kuku na wanafamilia hao kutoka nje kwenda kuokoa mifugo yao isiendelee kushambuliwa ambapo baada ya kutekeleza tukio hilo alikimbilia vichakani.

“Majeruhi wanaendelea kupatiwa  matibabu katika  hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, hali zao zinaendelea vizuri na jitihada za kumtafuta mnyama huyo zinaendelea ili kuwaondoa wanyama wakali katika kijiji hicho kwa kushirikiana na maafisa  wanyama pori,”alisema Magiligimba.

Mwisho.


Share:

Vijana Walilia Ajira Ujenzi Wa Daraja La JPM


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amemtaka Mkandarasi anayejenga Daraja la Magufuli  jijini Mwanza, kutoa ajira nyingi za vibarua kwa vijana wazawa ili wanufaike na mradi huo.

Agizo hilo amelitoa Waziri huyo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo yaliyofikiwa had sasa.

“Miradi yote ambayo tunalipa pesa zetu wenyewe tuhakikishe wakandarasi wazawa wanajumuishwa kwenye kazi, ili kuweza kupata uzoefu kwa vijana wetu wa kitanzania”.amesisisitiza waziri chamuriho

Waziri Chamuriho pia amewataka Bodi ya Wakandarasi nchini (CRB), kuhakikisha inawaongezea uwezo wakandarasi wazawa ili waweze kuwa pamoja katika Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa barabara, na madaraja.

“Katika miradi yote mikubwa lazima tuweke asilimia kubwa kwa wakandarasi wazawa ili tuweze kupata wakandarasi wenye weledi”.aliongezea waziri chamuriho

Aidha, Waziri Chamuriho amewapongeza wakandarasi kwa kazi nzuri ya ujenzi wa daraja hilo na kumuagiza mkandarasi wa daraja hilo kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa wakati.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)Mkoa wa Mwanza ,Mhandisi Fedestus Malibe, amesema kuwa Daraja la JPM linajengwa kwa lengo la kuunganisha barabara kuu ya Isagara-sengerema-Geita- katika ziwa Victoria na litakapokamilika litarahisisha usafirishaji baina ya pande zote mbili.

Naye, Afisa Utumishi wa kampuni ya CCE onesphory Ngonyani, amemhakikishia Waziri huyo kuendelea kutoa ajira kwa vijana wazawa wa eneo hilo, hadi pale ujenzi huo utakapokamilika.


Share:

Serikali Yaanza Mchakato Ujenzi Mradi Mkubwa wa Umeme Mto Ruhuji Njombe


 Timu ya Watalaamu wa Serikali imefika na kufanya ukaguzi wa kwanza katika maporomoko ya mto Ruhuji katika kijiji cha Itipula mkoani Njombe ambao unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa umeme utakaozalisha megawats 358 za umeme.

Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unaotarajiwa kuanza mwezi juni au julai mwaka huu ulifanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza 1998 na kisha kusimama kwa muda mrefu jambo ambalo lilisababisha wananchi kupoteza matumaini na kuanza kurudi kwenye maeneo waliotakiwa kupisha.

Naibu katibu mkuu wizara ya nishati mhandisi Leonard Masanja akizungumza mbele ya timu ya watalaamu kutoka wizara ya nishati,TANESCO na wakazi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mradi amesema katika mradi huo uliosubiriwa kwa zaidi ya 22 kutajengwa mabwawa 2,Intake moja pamoja miuondombinu ya umeme na barabara.

Tito Muinuka ambaye ni mkurugenzi wa shirika la umeme TANESCO nchini anasema kitendo cha kufika hapo ni mwanzo wa kuanza utekelezaji wa mradi huo na kwamba kukamilika kwake kutaongeza kiwango cha hazina ya megawats nchini huku Wangwe Elieza Mjiolojia wa TANESCO akisema kutajengwa Zanziber DAM ,Storage Dam na Intake moja

Kwa upande wao wakazi wa kijiji cha Itupula na vijiji jirani akiwemo Eleteus Mkolwe,Josphat Mwenda ambao ni miongoni mwa waliosimama kufanya shughuli za mendeleo ya kudumu katika la mradi kwa zaidi ya miaka 22 wanasema wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali na kwamba wana amini wanakwenda kupata ajira kwa vijana kupitia mradi huo


Share:

Vikao vya Kamati za Bunge Kuanza Januari 18


Vikao vya kamati za Bunge la Tanzania vinatarajiwa kuanza Januari 18 hadi 31, 2021 jijini Dodoma

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Januari 13, 2021 inaeleza kuwa shughuli zitakazofanywa ni pamoja na uchaguzi wa wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati.

Pia mafunzo kwa wajumbe wa kamati za kudumu kuhusu majukumu na taratibu za uendeshaji wa kila kamati na mafunzo kuhusu Bunge mtandao na usalama wa mitandao ya kamati zote.

Shughuli nyingine ni kamati za kisekta kupokea maelezo ya wizara kuhusu muundo, majukumu ya taasisi pamoja na sera na sheria zinazosimamiwa na wizara hiyo.

Nyingine ni mafunzo kwa kamati za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati za Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati za Uwekezaji na Mitaji kwa Umma (PIC) na Kamati ya Bajeti.

Taarifa hiyo imesema mafunzo hayo yatahusu uchambuzi wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Msajili wa hazina (TR) na namna bora ya kuhoji maofisa masuhuli.

Nyingine ni mafunzo kwa Kamati ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo na uzoefu wa mabunge mengine ya nchi zinazofuata mfumo wa kibunge wa jumuiya ya madola.

Kwa upande wa kamati ya Bajeti, taarifa hiyo imesema watapokea tathimini ya utekelezaji wa mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano wa 2016/2017 hadi 2020/2021.

Pia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2021/22 hadi 2025/26 na mwongozi wa kuandaa mpango na bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Shughuli nyingine ni utekelezaji wa bajeti ya Serikali pamoja na Sheria ya Fedha kwa kipindi cha nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

 



Share:

Mawaziri Wawili Wafariki Kwa Corona Nchini Malawi


Rais Lazarus Chakwera wa Malawi ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia vifo vya Mawaziri mawili, ambao wamefariki dunia baada ya kuugua Corona.

Mawaziri hao ni wa wizara ya Uchukuzi Sidik Mia na Lingson Belekanyama ambaye ni Waziri wa Serikali za Mitaa.

Hivi karibuni Rais Chakwera alilihutubia Taifa kupitia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Serikali na kuwataka Raia wa Malawi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Alisema kuwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini Malawi kwa sasa yako juu, hivyo ni lazima tahadhari ikachukuliwa.

Watu 50 wamethibitika kufariki dunia baada ya kuugua Corona nchini Malawi, katika kipindi cha kuanzia mwezi huu hadi sasa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger