Monday, 11 January 2021

MTU TAJIRI ZAIDI DUNIANI AANIKA SIRI 6 KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA ZAKO..HIZI HAPA


Ni nini kinachompatia Elon Musk ufanisi katika biashara?

Siku chache zilizopita Elon Musk alitangazwa kuwa mtu tajiri zaidi duniani, akimpiku mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos.

Utajiri wa mfanyabiashara huyo wa magari ya Tesla na SpaceX umepita dola bilioni 185 sawa na euro 136 bilioni baada ya bei ya hisa za kampuni yake ya magari kupanda.

Lakini je ni nini siri ya ufanisi wake katika biashara? Miaka michache iliopita alizungumzia suala hilo kwa karibu saa moja alipohoijwa na BBC.

1. Cha msingi sio pesa

Kulingana na mtazamo wa biashara wa Elon Musk - cha msingi sio pesa.

Alipohojiwa mwaka 2014 alisema hajui kiwango cha utajiri wake.

"Sio kwamba kuna rundo la pesa zilizohifadhiwa mahali," alisema. "Ukweli ni kwamba nina hisa kadhaa katika Tesla, SpaceX, na SolarCity, na katika soko la hisa kila hosa niliyo nayo ina thamani yake ."
Aina ya gari ya Tesla X 90D ikiwa katika onyesho la kibiashara mjini Brussels.

Hapingi mbinu zozote za kutafuta mali "ikiwa inafanyika kwa kuzingatia maadili na njia nzuri", lakini anasema sio jambo linalompatia msukumo.

Mbinu hiyo bila shaka inonekana kufanya kazi.

Kampuni yake ya magari ya umeme Tesla, imefanya vyema baada ya thamani ya hisa zake kuongezeka hadi zaidi ya dola 700 bilioni katika miaka ya hivi karibuni.

Fedha hizo zinatosha kununua Ford, General Motors, BMW, Volkswagen na Fiat Chrysler, na bado asalie na fedha za kununua gari la Ferrari.
Robert Downey Jr anasema ametumia mbinu ya Musk katika aonyesho lake la Iron Man

Lakini Musk, ambaye anafikisha umri wa miaka 50 mwaka huu, hatarajii kufariki akiwa tajiri.

Anasema fedha zake zitatumika kujenga majumba katika sayari ya Mars na anasema hatoshangaa kuona utajiri wake wote ukimalizikia katika mradi huo.

Sawa na Bill Gates, huenda akachukulia kama ishara ya kufeli maishani akiwa atasalia na mabilioni kadhaa kwa sababu atakuwa hajatumia fedha hizo kwa njia nzuri.

2. Fuatilia ndoto zako

Ndoto ya kuwa na majumba katika sayari ya Mars ni kidokezo ambacho Elon Musk anaamini ndio ufunguo wa mafanikio.

"Unataka vitu vijavyo maishani kuwa vizuri," aliambia BBC. "Unataka vitu hivi vipya ambavyo vitafanya maisha kuwa bora."

Kwa mfano SpaceX. Alisema alibuni kampuni hiyo baada ya kuhisi kwamba mpango wa Marekani wa anga za mbali haukuwa na malengo ya juu zaidi.

"Nilitarajia kuona vitu vya hali ya juu zaidi ambavyo havipatikani duniani vikibuniwa, binadamu kuishi katika sayari ya Mars, kuwa na makao mwezini, na safari za ndege za mara kwa mara kwenda anga za mbali," alisema.

Wakati hilo halikufanyika, alizindua mpango wa "Mars Oasis Mission", ambao ulilenga kuanzisha kilimo cha kisasa cha kutumia nyumba katika sayari nyekundu.

Lengo lilikuwa kuwapa matumaini watu kuhusu masuala ya anga za mbali, na kuishawishi serikali ya Marekani kuongeza mgao wa bajeti ya Nasa.

Ni wakati alipokuwa anajaribu kuanzisha mradi huo ndiposa aligundua tatizo sio "kutokuwa na utashi, bali ni ukosefu wa njia" - teknolojia ya anga za mbali ni ghali zaidi kuliko jinsi inavyotakiwa kuwa.

Na kutokana na wazo hilo! Biashara ya bei rahisi zaidi ya utengenezaji roketi ilizaliwa.
Roketi ya SpaceX ikiandaliwa kufanya majaribio ya kwanza katika kiwanda cha kampuni hiyo mjini Boca Chica, Texas mwezi

Na cha kushangaza katika mradi huo ni kwamba haukubuniwa kwa lengo la kutengeza pesa, bali kumpeleka binadamu katika sayari ya Mars.

Musk alisema anajichukulia kama mhandisi kuliko mwekezaji, na kuongeza kuwa kile kinachomuamsha kila asubuhi ni kusuluhisha matatizo ya kiufundi.

Ni hilo ndilo limekuwa lengo lake la kwanza badala ya kuwa na dola kwenye benki na ametumia kanuni hiyo kama kigezo cha kujiendeleza maishani.

Anafahamu kila kizingiti anachovuka katika biashara yake kinamsaidia akiwa mtu anayejaribu kutafuta suluhisho la tatizo sawa na hilo - na kuendelea hivyo daima.

3. Usiogope kuwa na mawazo makubwa

Moja ya mambo makuu kuhusu biashara ya Elon Musk ni udhubutu wake.

Anataka kubadilisha kabisa kampuni ya magari, kuwa na koloni Mars, kutengeza treni za mwendo kasi kupitia bomba la hewa, kujumuisha AI katika ubongo wa binadamu kuimarisha nguvu ya jua na kampuni za betri.

Hii inamaanisha miradi yake yote inalenga siku za usoni sawa na vitu ambavyo ungesoma katika majarida ya watoto mapema miaka ya 1980.

Kwa mfano, biashara yake ya bomba inaitwa ''The Boring Company''.

Musk bila shaka hafanyi siri kuwa mawazo yake yalichangiwa na vitabu na filamu alizotazama akiwa mtoto nchini Afrika Kusini.
Kiwanda kipya cha Tesla kikijengwa mjini Shanghai, China mwaka 2019

Hatua hiyo inatupeleka katika kidokezo cha Musk cha tatu cha biashara - usijinyime.

Anaamini kuwa na malengo madogo ni changamoto kwa kampuni nyingi' hali ambayo inachangia miundo ya motisha.

Kampuni nyingi zinaangazia "kujiongeza", alisema. "Ukiwa Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni kubwa na malengo yako ni ya ukuaji wa kadri, itachukuwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa, na matokeo yasiwe mazuri kama ilivyokusudiwa, basi hakuna atakaye kulaumu," aliambia BBC.

Unaweza kusema haikuwa kosa lako, ni kosa la wasambazaji.

4. Kuwa tayari kuchukua hatua ya hatari

Hii bila shaka ni jambo la kweli.

Lazima uwe mkakamavu kuchukua hatua hii, lakini Elon Musk amezidisha hatua hiyo kuliko wafanyabiashara wengi.

Kufikia mwaka 2002 alikuwa ameuza biashara zake mbili, muongozo wa jiji kupitia intaneti unaoitwa Zip2 na kampuni PayPal ambayo ni ya malipo mtandaoni.

Alikuwa ndio mwanzo ametimiza miaka 30 na tayari alikuwa na karibu dola milioni 200 kwenye benki.

Anasema mpango wake ulikuwa kuwekeza nusu ya utajiri wake kwenye biashara na kujiwekea nusu nyingine.

Mambo haykuwa hivyo alipokutana na mwandishi wa BBC, alikuwa ndio mwanzo anaibuka katika kipindi kibaya zaidi cha biashara maishani mwake.

Kampuni zake mpya zilikabiliwa na kila aina ya changamoto. Safari tatu za kwanza za roketi ya SpaceX zilitibuka, na Tesla ilikumbwa na kila aina ya matatizo ya uzalishaji, usambazaji na masuala ya muundo.
Vituo kadha wa kadha za kuchaji magari ya umeme zinabuniwa kati kati ya miji

Halafu mzozo wa kiuchumi ukaibuka.

Musk anasema alilazimika kufanya maamuzi magumu. "Ima aamuwe kuhifadhi pesa zake na kuacha kampuni zifilie mbali ama awekeze fedha zote alizosalia nazo kujaribu bahati yake ."

Aliendelea kumimina pesa.
Wakati mmoja alikuwa na madeni na kulazimika kuchukua mkopo kwa marafiki kujikimu kimaisha, aliambia BBC.

Je hofu ya kufilisika ilimtia uoga?

Anasema la hasha: "Watoto wangu huenda wakajiunga na shule za umma. Hiyo si hoja, hata mimi mwenyewe nilisomea shule ya serikali."

5. Puuza wakosoaji

Kilichomshangaza zaidi - na ambacho kilionekana wazi kumkera hata mwaka 2014 - ni jinsi wataalamu wengi na watoa maoni walivyoonekana kufurahia masibu yake.

"Ukosoaji ulikuwa wa kushangaza na hali ya juu sana," alisema Musk. "Blogu nyingi ziliangazia jinsi mradi wa Tesla unavyoelekea kuangamia."

BBC ilipendekeza kwamba watu walitaka mradi wake ufeli kwasababu alikuwa na kiburi.

Alipinga pendekezo hilo. "Nadhani ingelikuwa kiburi laiti tungelisema lazima tutafanikiwa, ukilinganisha na jinsi tulivyokuwa na hamu ya kufanikisha azma yetu na kujitolea kila tuwezavyo kufikia lengo hilo."

Hii inatupeleka katika kidokezo kingine cha ufanisi wa Musk katika biashara - usiwasikilize wakosoaji.

Aliambia BBC kuwa hakuwahi kuamini SpaceX au Tesla itawahi kurudisha kiwango cha fedha alichotumia karibuni - na ukweli ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyedhani hilo lingewezekana.

Lakini aliwapuuza wakosoaji na kuendelea mbele na mradi wake.

Kwa nini? Kumbuka huyo ni mtu ambaye anapima ufanisi wake kulingana na matatizo anayosuluhisha, na wala ni fedha kiasi gani anachopata.

Hii bila shaka ni kanuni ambayo inamweka huru. Hana hofu ya kuonekana mjinga kwa sababu fedha alizotumia hazikumnufaisha, kile anachoangazia ni umuhimu wa kufikia lengo.

Hali hii inafanya kazi kuwa rahisa kwasababu anaelekeza nguvu zote katika kitu ambacho anaamini kina umuhimu zaidi.

Na soko linaonaoneka kuvutiwa na kile anachofanya.

Mwezi Oktoba mwaka jana, Morgan Stanley ambayo ni benki ya uwekezaji ya Marekani ilikadiria thamani ya SpaceX kuwa dolabilioni 100 ($100bn).

Kampuni hiyo imeimarisha uchumi wa usafiri wa anga za mbali, lakini kile kitakachomfanya Musk kujivunia zaidi ni jinsi kampuni yake ilivyoimarisha nafasi ya Marekani katika mpango wa angaza mbali.

Mwaka jana roketi yake ya Crew Dragon iliwapeleka wanajimu wakimataifa katika kituo cha angani, katika mpango wa kwanza wa aina hiyo kutoka ardhi ya Marekani tangu safari hizo zilipositishwa mwaka 2011.

6. Furahia unachofanya

Fuata muongozo huu ukiambanisha na bahati kidogo bila shaka utapata utajiri na umaarufu. Na baada ya hapo utaanza kutoka katika ganda lako.

Elon Musk anafahamika kuwa mchapa kazi kupita kiasi - anajivunia kufanya kazi kwa takriban saa 120 - kwa wiki ili kufanikisha uzalishaji wa gari la Tesla Model 3 hadi lilipoingia barabarani - na tangu wakati huo anaonekana kufurahia anachofanya.

Mwaka 2018 ilijipata mashakani na wasimamizi wa Marekani wa masuala ya fedha alipoweka ujumbe kwenye Twitter kwamba anapanga kubinafsisha kampuni ya Tesla, na wakati janga la corona lilipoilazimuTesla kufunga kiwanda chake cha San Francisco, alipinga vikali marufuku ya kutotoka nje.

Alitaja hofu kuhusu virusi hivyo kuwa "ujinga" katika Twitter, na kuelezea amri ya kukaa nyumbani kama "kifungo cha lazima", akisema ''haifai'' na kwamba inakiuka haki ya kikatiba.

Alitaja hofu kuhusu virusi hivyo kuwa "ujinga" katika Twitter, na kuelezea amri ya kukaa nyumbani kama "kifungo cha lazima", akisema ''haifai'' na kwamba inakiuka haki ya kikatiba.

Msimu wa joto alitangaza mpango wa kuuza mali yake akisema "zinakurudisha nyuma".

Siku chache baadaye aliandika katika Twitter kwamba atamuita mwanawe wa kiume aliyezaliwa X Æ A-12 Musk.

Licha ya hayo mwenendo wake usiotabirika ukionekana kutoathiri biashara zake huku mfanyabiashara huyo akiendelea kuwa na ndoto kubwa kama zamani.

CHANZO - BBC SWAHILI


Share:

Angalia Picha : MUONEKANO WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA CHATO MKOANI GEITA


Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita ambayo imewekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita leo tarehe 11 Januari 2021.

Ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Chato umekamilika kwa asilimia 90 katika awamu ya kwanza ambayo makabidhiano ya miundo mbinu ya awamu hiyo ya kwanza yamepangwa kufanyika mapema mwezi Machi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Hospitali hiyo ya Ukanda wa Chato lililowekwa na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi.

Dk Gwajima amesema hospitali hiyo ikikamilika itakuwa nauwezo wa kuhudumia wananchi milioni 14 kutoka Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora, Rukwa, Geita, na wilaya za Mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Share:

WAZIRI BASHUNGWA AAHIDI MAPINDUZI SEKTA YA UTANGAZAJI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashugwa akizungumza na wamiliki wa vyombo vya habari na Wamiliki wa Kampuni za Visimbuzi Leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Innocent Bashugwa akipata maelezo ya simu zilivyotumika zamani kutoka kwa Mhifadhi Mwandamizi wa Makumbusho wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Raphael Mwango wakati waziri huyo alipoafanya ziara katika Makumbusho hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashugwa akizungumza katika Makumbusho ya TCRA na kudai Mamlaka imepangilia Makumbusho hayo.
Picha ya mbalimbali za Makumbusho TCRA.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano wa wadau wa Wamiliki wa vyombo vya Habari na Kampuni za Visimbuzi Jijini Dar es Salaam.
Wadau wakichangia mkutano kuhusiana na sekta ya utangazajiKaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Joannes Karugura akitoa akizungumza kuhusiana na masuala ya utangazaji katika mkutano wa wadau wa vyombo vya habari vya utangazaji na wamiliki wa kampuni za visimbuzi.

*******************

WAZIRI wa Habari,Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema kuwa mfumo wa dijital una nafasi kubwa ya mapato hivyo vyombo vya habari vinaweza kutumia fursa katika kuatangaza bidhaa mbalimbali katika kanda.

Hayo aliyasema Waziri wakati alipokutana na Wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na wamiliki kampuni za visimbuzi pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni ziara ya kukutana na wadau kujadili masuala mbalimbali ikiwemo na changamoto mkutano wa wadau hao umefanyika Makao Makuu ya TCRA

Amesema kuwa kukutana na wadau ni hatua iendelevu aliyopanga katika kuangalia vitu mbalimbali vya sera pamoja na sharia kwa lengo ya kukuza sekta ya habari na utangazaji nchini.

Bashungwa amesema kuwa maoni ya wadau watayafanyia kazi na kuwataka kuendelea na majadiliano ya mara kwa mara na wadau wa utangazaji kuingia katika mfumo mmoja wa kuwa na king’amuzi kimoja kwa siku zijazo.

Aidha Bashungwa amesema kuwa mapato mengi yanapotea kutokana mifumo ikiwemo kwa wasanii kupata haki zao. Waziri Basshungwa katika ziara hiyo pia alifanya ziara katika Makumbusho ya TCRA na ambapo alisema ni sehemu nzuri ya watu kujifunza historia ya Mawasiliano tangu ilivyoanza.

Amesema kuwa katika Makumbusho hayo watengeneze na kuweza kutangaza ambapo Mamlaka hiyo ilishaanza kufanya hivyo.

Waziri huyo amezungumza na Cosota,Basata na TCRA kuangalia wanavyoweza kufikia malengo ya Serikali katika kutangaza Tanzania Pamoja na kujadili maslahi ya wasanii.

Share:

MANISPAA YA SHINYANGA YAKUTANA NA WATENDAJI WA KATA KUJADILI VIPAUMBELE VYA MAPENDEKEZO YA BAJETI

Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Gwakisa Masyeba, akizungumza kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Na Marco Maduhu -Shinyanga. 
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imefanya kikao na watendaji wa Kata kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti katika mwaka wa fedha ujao (2021-2022), ili kubaini vipaumbele muhimu ambavyo vitatekelezeka na kutoa huduma.

Kikao hicho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano katika shule ya Msingi Balina iliyopo Kata ya Ndembezi, na kuhudhuriwa pia na wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Shinyanga. 

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema watendaji hao wanapaswa kuainisha vipaumbele vichache na muhimu, ambavyo vitaweza kutekelezeka kuliko kubainisha vitu vingi na kushindwa kutekelezwa kulingana na ufinyu wa bajeti. 

“Kipindi hiki ni muhimu sana kwa wananchi cha utoaji wa maoni yao ya mapendekezo ya bajeti ijayo kabla ya kwenda kwenye ngazi za juu, hivyo naomba wananchi watoe mapendekezo yao kupitia kwenye ofisi za watendaji wa kata ili yafanyiwe kazi, kuliko kuanza kulalamika kwenye mitandao ya kijamii,”amesema Mwangulumbi. 

Pia amewataka watendaji hao kusimamia kwa ukamilifu zoezi la ukusanyaji mapato, pamoja na wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kulipa kodi na ushuru kwa hiari, ili zipatikane fedha za utekelezaji wa mapendekezo hayo ya bajeti. 

Kwa upande wake Mchumi wa manispaa ya Shinyanga Gwakisa Mwasyeba, alisema kikao hicho ni muhumi sana, ambacho kitasaidia kuchambua vipaumbele vya mapendekezo ambavyo ni muhimu vitakavyo zingatia maslahi mapana ya wananchi. 

Nao baadhi ya watendaji hao wa Kata akiwamo Rose Matunda kutoka Kitangili na Joshua Masengwa kutoka Kizumbi, wametoa wito kwa wananchi kipindi wanapokuwa wakiitwa kwenye mikutano ya hadhara kutoa maoni ya mapendekezo ya Bajeti, wawe wana hudhulia ili kuondoa malalamiko pale bajeti itakapopitishwa. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kikao hicho cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Gwakisa Masyeba, akizungumza kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Gwakisa Masyeba, akizungumza kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Watendaji wa Kata manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ijayo ngazi ya Kata.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto Mwakaluba Wilison, akitoa vipaumbele vya mapendekeo ya Bajeti ijayo kwenye Kata yake.
Ponsian Mgodita Afisa Mtendaji Kata ya Chibe, akitoa vipaumbele vya mapendekezo ya bajeti ijayo kwenye Kata yake. 
Gaudiozi Mwombeki, akitoa vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ijayo kwenye Kata yake.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI DK. CHAMURIHO AWATAKA WAFANYAKAZI SEKTA YA UCHUKUZI KUJIENDELEZA KIELIMU


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  Dk. Leonard Chamuriho akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi katika ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Mwanza  Januari11, 2021.
Kaimu Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi  Gabriel Migire akizungumza kwenye Mkutano huo
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini
Wajumbe wa Baraza wakiwa ukumbini.


Na Hellen Mtereko Mwanza

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ,Dkt. Leonard Chamuriho amewataka  wafanyakazi wa sekta ya Uchukuzi kujenga tabia ya kujiendeleza kielimu ili  wafanye kazi kwa weledi.

Ameyasema hayo leo  Januari 11,2021 wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa sekta hiyo Jijini Mwanza  wenye lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu ya kazi, utawala na wajibu wa wafanyakazi.

Alisema kila mtumishi ana wajibu wa kufanya kazi kwa weledi na  ushirikiano ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya sekta hiyo.
 
Alisema hatutasita kuchukua hatua pale tutakapobaini mazoea yanawekwa mbele badala ya weledi katika utendaji wa kazi.

Aliongeza kuwa ni lazima wajibu uambatane na uelewa wa majukumu ya kila mmoja  pamoja na uhusiano mwema kazini Kati ya viongozi na wafanyakazi.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa sekta hiyo Gabriel Migire alisema  katika mpango wa tatu wa maendeleo ya Taifa unaoendelea kuandaliwa sekita hiyo imepewa dhamana ya kutekeleza miradi ya kielelezo ikiwemo ujenzi wa reli ya Kati, uboreshwaji wa Bandari ya Dar -es Salaam na uimarishaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo unasimamiwa na wajumbe  wa sekta hiyo hivyo amewaasa  kutekeleza miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa na kulinda thamani ya fedha iliyowekezwa.

Naye Mjumbe kutoka Sekta ya Uchukuzi Stella Katondo alisema  atahakikisha wanafanya kazi kwa weledi na bidii ili waweze kukamilisha miradi iliyopo kwenye sekta hiyo.
Share:

WANANCHI SIRARI WAMUELEZA MBUNGE BEI KUBWA INACHANGIA SARUJI YA KENYA KUINGIA KWA MAGENDO

Mbunge Waitara akisaini kitabu cha mahudhurio baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kata ya Sirari. Kushoto ni katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka
Mkutano wa mbunge Waitara uliofanyika uwanja wa Tarafa Sirari
Mkutano wa mbunge Waitara uliofanyika uwanja wa Tarafa Sirari
Mkutano wa mbunge Waitara uliofanyika uwanja wa Tarafa Sirari

Na Dinna Maningo,Tarime

Wananchi wa kata ya Sirari wamesema kuwa kinachosababisha wafanyabiashara kuingiza bidhaa nchini kwa njia za Magendo badala ya kupitisha katika mipaka halali ukiwemo mpaka wa Sirari ni kutokana na ushuru mkubwa wa bidhaa zitokazo nchi jirani ya Kenya ikiwemo Saruji,Sukari na Mafuta ya chakula.

Ili kupunguza tatizo la bidhaa za Kenya kuingia nchini kwa njia za panya,wananchi wameiomba Serikali kushusha bei ya Saruji ya Kenya ili iwe rafiki kwa wafanyabiashara ikizingatiwa kwamba wilaya ya Tarime imepakana na nchi ya Kenya na Saruji ya Tanzania ni gharama ikilinganishwa na ya nchi hiyo jirani.

Wananchi walieleza hayo kwa Mbunge wao wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,alipokuwa kwenye ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na kisha  kuzungumza na wananchi katika uwanja wa Tarafa kufahamu kero zinazowakabili ili zitatuliwe.

Diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara (CCM) alisema kuwa wananchi hawakwepi kulipa kodi ila kinachosababisha wapitishe bidhaa kwa njia za panya wanakwepa ushuru mkubwa kwa kuwa unawaumiza kibiashara.

"Saruji ya Tanzania mfuko mmoja unauzwa sh.22,000 bado usafiri na wakati mwingine upatikanaji wake ni wa shida, Boda ya Kenya Saruji inauzwa kwa sh.12,000-13,000 ikiingia Tarime inauzwa sh 17,000 na upatikanaji wake ni rahisi ukichukua ya Kenya kila mfuko unaokoa sh.5,000,cha kushangaza ukipitisha  saruji mpakani Saruji ya Kenya mfuko mmoja unatozwa kodi sh.8,500 ndiyo maana wanakwepa",alisema Chacha.

Bhoke Marwa alisema"Mnunuzi anaangalia unafuu wa bei, tunaomba Serikali ishushe bei bidhaa zake kwani ushuru ni mkubwa matokeo yake wananchi nao wanabuni njia za kuingiza bidhaa kukwepa ushuru mkubwa".

Wananchi wanaiomba Serikali kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinakuwa na bei nafuu na zipatikane kwa urahisi hususani kwenye wilaya zinazopakana na nchi za jirani kwa kufanya hivyo itasaidia wananchi kupenda na kununua bidhaa za ndani badala ya kwenda kununua bidhaa za nchi jirani kwa sababu ya unafuu wa bei na itasaidia kupunguza uingizaji wa bidhaa za nje kwa njia ya magendo.

Mbunge Waitara alisema kuwa Saruji imekuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi wilayani Tarime hivyo kuna haja ya kulitizama suala hilo kwa mapana zaidi kwa kuwa linawaumiza wananchi na kuahidi kulifikisha mamlaka husika ili litatuliwe.

Mbali na suala hilo wananchi waliomba kuwepo kwa mnada wa ng'ombe ,na wengine kulalamikia vitendo vya uonevu kwa askari wa usalama barabarani,lakini pia Waitara aliwasisitiza viongozi wakiwemo Madiwani kufanya mikutano ya wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na ushirikishwaji wa miradi ya maendeleo.
Share:

Lukuvi Ataka Usimamizi Wa Ardhi Katika Ngazi Ya Mitaa


Na Munir Shemweta, WANMM SINGIDA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha zinashusha usimamizi wa masuala ya ardhi katika ngazi za mitaa na vijiji ili ziweze  kusimamia kuepuka ujenzi holela na kurahisisha ufuatiliaji makusanyo ya kodi ya pango la ardhi.

Akizungumza wakati akikagua ofisi ya ardhi katika halmashauri ya Manispaa ya Singida akiwa katika ziara ya siku moja kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Singida tarehe 10 Januari 2021, Lukuvi alisema ni vyema wakurugenzi katika halmashauri nchini kuwapa wajibu watendaji wa mitaa na vijiji kwa barua kusimamia misingi ya ardhi yenye lengo la kusimimia sheria katika masuala ya ardhi.

Hata hivyo, Waziri Lukuvi alisema Watendaji wa Mitaa na Vijiji watakaokasimia mamlaka ya usimamizi ardhi katika maeneo yao hawatakuwa na jukumu la kugawa, kupanga, kupima na kumilikisha ardhi bali kuangalia yanayoendelea katika mitaa yao na wakikuta ukiukwaji wowote kama vile ujenzi holela basi watakuwa na wajibu wa kusitisha.

” Afisa ardhi katika wilaya hawezi kujua yale yanayoendelea kwenye mtaa au kijiji na hata suala la kodi  mkiwatumia watendaji wa mitaa wataweza kusaidia kuwabaini wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi kirahisi”

Ametaka watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri kuhakikisha wanatengeneza majedwali maalum yenye orodha inayoonesha kila mmiliki wa kiwanja kwa lengo la kuwawezesha watendaji wa mitaa kuwajua wamiliki katika maeneo yao.

” Kumbukumbu zote za masuala ya ardhi wajulishwe watendaji wa mitaa na vijiji ili waweze kufuatilia katika mitaa yao maana katika suala la hati za kimila tumefanya vizur ngazi ya vijiji ila suala la Hati Miliki za Ardhi bado tuko nyuma maana tumeficha taarifa wilayani” alisema Lukuvi.

Waziri Lukuvi alizitaka ofisi za ardhi za mikoa kuhakikisha zitatoa elimu kwa watendaji wa mitaa na vijiji ili kuwajengea ufahamu wa masuala ya ardhi na kuwawezesha kusimamia vyema masuala hayo katika maeneo yao.

Kwa mujibu wa Lukuvi, hata kama Manispaa imepanga matumizi bora ya ardhi ni vyema matumizi yake yakawekwa kwenye vipande vya ngazi ya mitaa na kusisitiza kuwa kazi hiyo ni ya halmashauri kwa kuwa mitaa ni jicho lake la kutoa taarifa katika masuala mbalimbali yakiwemo yale ya ardhi.

Katika ziara yake Waziri wa Ardhi mbali na kutembelea halmashauri za wilaya ya Singida na Ikungi na kusisitiza kuwa halmashauri ndizo zenye jukumu la kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika maeneo yake na jukumu hilo siyo la maafisa ardhi.

Lukuvi alisema Halmashauri zote zijue zina wajibu wa kusimamia ardhi katika maeneo yao na ilichofanya Wizara ya Ardhi ni kuwapatia wataalam watakaowasaidia kujua namna bora  ya kutumia ardhi vizuri.


Share:

RAIS WA MSUMBIJI NYUSI ATUA TANZANIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI KANDA YA CHATO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshuhudia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akimwagilia maji mti alioupanda baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato mkoani Geita alikowasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumatatu Januari 11, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumatatu Januari 11, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora ya THE BIG FIVE mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumatatu Januari 11, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato mkoani Geita alikowasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumatatu Januari 11, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakisikiliza maelezo toka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato mkoani Geita leo Jumatatu Januari 11, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha kwa viongozi mbalimbali mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi alipowasili ili kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato mkoani Geita leo Jumatatu Januari 11, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakifurahia ngoma za utamaduni katika Uwanja wa Ndege wa Geita mara alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Jumatatu Januari 11, 2021
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger