Sunday, 10 January 2021

SAVE THE CHILDREN YAENDESHA MDAHALO WA BAJETI JUMUISHI NGAZI YA HALMASHAURI MANISPAA YA SHINYANGA


Mtaalam wa Haki za Watoto na Utawala Bora kutoka Save The Children Makao Makuu Jesca Ndana, akizungumza kwenye Madahalo huo.

Na Marco Maduhu  Shinyanga. 

Shirika la Save The Children linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto katika nchi 117 duniani ikiwemo Tanzania, limeendesha mdahalo wa utekelezaji wa bajeti jumuishi katika sekta zinazomuhusu mtoto moja kwa moja katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.

Mdahalo huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Empire Mjini Shinyanga, ambao umekutanisha maafisa elimu, maendeleo, wachumi, viongozi wa kisiasa, dini, wajumbe wa baraza la watoto, wadau kutoka mashirika na asasi zisizo za kiserikali, waandishi wa habari, pamoja na maofisa kutoka TAMISEMI wanaohusika na masuala ya bajeti, huku mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi. 

Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Utawala wa Kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, amesema wameandaa na kuwezesha mdahalo huo ,ili wadau wajadili kwa pamoja namna ya kupanga bajeti bora ambayo itazingatia maslahi mapana ya watoto. 

Amesema Shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya utetezi wa haki za watoto ikiwemo mradi huu wa mijadala jumuishi, ambao utekelezaji wake ulianza mwaka jana (2020), na umelenga zaidi masuala ya kisera ya utekelezaji wa bajeti zinazomhusu mtoto na utakoma mwaka huu (2021).

Ameongeza kuwa kupitia mradi huu Save the Children ingependa kuona ushirikishwaji wa wadau wakiwemo wanajamii wa kawaida na watoto katika mchakato wa kibajeti na kuboresha utekelezaji wa bajeti za watoto. 

"Save the Children tumeendesha mdahalo huu wa bajeti jumuishi haswa tukianzia sekta inayomgusa mtoto moja kwa moja, kwa lengo la kujadiliana namna ya kupanga bajeti ambayo itazingatia maslahi ya watoto katika sekta hizo mbazo ni afya na lishe, elimu, maendeleo ya jamii, ulinzi na usalama wa mtoto," amesema Enock. 

"Mradi huu unatekelezwa katika wilaya tano zikiwemo Unguja mjini, Magharabi “A” na “B” Visiwani Zanzibar, na wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, pamoja na manispaa ya Shinyanga, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

"Ni matarajio yetu kuwa wadau kwa kushirikiana na halmashauri husika zitaweza kuyapa kipaumbele masuala ya watoto kwenye bajeti zao, na hivyo kumuwezesha mtoto wa Kitanzania kupata haki zake", ameongeza. 

Kwa upande wake mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi, amelipongeza Shirika la Save the Children kwa kuendesha mdahalo huo, na kubainisha upo katika muda muafaka, ambapo wadau wanapaswa kuanza kujadili kuanzia sasa vipaumbele na malengo ya bajeti ngazi za chini. 

Amesema katika upangaji wa bajeti hizo ikiwamo ya watoto, kuwepo na vipaumbele vichache muhimu, ambavyo vitaweza kutekelezeka kulingana na bajeti ya fedha za halmashauri, kuliko kuwa na vipaumbele vingi ambavyo haviwezi kutekelezeka. 

Naye Makamu Mwenyekiti Baraza la watoto Manispaa ya Shinyanga Nancy Kasembo, amepongeza mdahalo huo, ambao umewapatia mwanga wa namna ya kushiriki kikamilifu kwenye utoaji wa mapendekezo ya bajeti zinazomhusu mtoto. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akiendelea kuzungumza kwenye Mdahalo huo.
Mtaalamu wa haki za watoto na utawala Bora kutoka Save The Children Makao Makuu Jesca Ndana, akizungumza kwenye Madahalo huo.
Mtaalam wa Haki za watoto na utawala Bora kutoka Save The Children Makao Makuu Jesca Ndana, akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Mchumi kutoka TAMISEM Allan Bendera, akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Gerald Ng'ong'a ambaye alikuwa mwenyekiti wa Mdahalo huo akizungumza na kutoa maoni yake.
Washiriki wakiwa kwenye Mdahalo huo.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Waandishi wa Habari nao wakishiriki kwenye Mdahalo huo, wakwanza kushoto ni Fanki Mshana Mwandishi wa ITV, katika Suzy Butondo wa Mwananchi, akifuatiwa na Malaki Philipo wa RFA.
Diwani wa Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Elias akichangia mada kwenye Mdahalo huo.
Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Gwakisa Mwasheba, akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akichangia Mada kwenye Mdahalo huo
Mwenyekiti wa Shirikisho wa vyama vya watu wenye ulemavu mkoani Shinyanga (SHIVYAWATA), Richard Mpongo, akichangia mada kwenye Mdahalo huo.
John Shija kutoka Shirika la PACESH Mkoani Shinyanga akichangia mada kwenye Mdahalo huo.
John Eddy kutoka Shirika la TAWLAE, akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Makamu Mwenyekiti Baraza la watoto Manispaa ya Shinyanga Nancy Kasembo, akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Mchumi kutoka TAMISEM Allan Bendera, akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.
Washiriki wa Mdahalo huo wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Kazi ya vikundi ikiendelea.
Kazi ya vikundi ikiendelea.
Kazi ya vikundi ikiendelea.
Uwasilishaji kazi ya vikundi ukiendelea.
Uwasilishaji kazi ya vikundi ukiendelea.
Uwasilishaji kazi ya vikundi ukiendelea.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

WANANCHI WAMUOMBA MBUNGE WAITARA KUINGILIA MGOGORO KATI YA WANANCHI WA KATA YA KWIHANCHA NA HIFADHI YA SERENGETI

Mbunge Waitara akizungumza na wananchi wa kata ya Kwihancha
Mbunge Waitara akizungumza na wananchi wa kata ya Kwihancha
**

Na Dinna Maningo,Tarime.

Wananchi wa kata ya Kwihancha wamemuomba Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mwita Waitara kuingilia kati mgogoro wa mpaka kati ya vijiji na hifadhi ya Serengeti ambao umesababisha baadhi ya watu kupoteza maisha.

Mbunge Waitara akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa alizungumza na wananchi wa kata ya Kwihancha ambapo Diwani wa kata hiyo Magita Mato alisema kuwa tangu mwaka 2015 watu 9 wameuliwa wakidaiwa kuingia ndani ya hifadhi nakwamba eneo la Tindiga ya Gong'ora,Kijito cha Sweto na mto Mara ni maeneo ambayo mifugo ukamatwa na watu kuuwawa.

Diwani huyo aliwataja waliouwawa ni Lucus Gasaya,Wambura Maisori,Goryo Ghati,Kebacho Wanko,Mwita Makuri,Nyagwisi Manga,Chacha Megoko,Wanene Masiaga,na Chacha Nyaiho.

"Sisi tunatambua mpaka wa mwaka 1968 kati ya hifadhi na kata ya Kwihancha miaka ya nyuma tuliwahi kufanya uhakiki wa mipaka na watu wa hifadhi lakini kila mara wanazidi kuongeza,nusu ya eneo la tindiga liko kifadhini na nusu liko kwenye kijiji ambalo ndilo mifugo uchungia.

" Eneo hilo lina udongo wa chumvichumvi,udongo huo ujenga mifupa ya wanyama na unatoa minyoo tumboni ni eneo linalopendwa na mifugo lakini Tanapa wamelichukua lote bado tena wameingia hadi mita 60 eneo la kijiji mifugo inateseka" alisema.

Rugura Wankaba alisema kuwa mpaka umeleta shida na migogoro mikubwa nakwamba maeneo yanayodaiwa kuwa ni hifadhi si kweli ni ya wananchi ambayo walikuwa wakilisha mifugo na kuishi tangu 1981 na sasa wamefukuzwa na hivyo kukosa maeneo ya kulima na malisho.

Msabi John alisema"Wakati wa uhakiki wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya nilishiriki kwenye uwekaji wa Bikon,na GPS zilikuwa zinaonyesha mipaka lakini nashangaa hawatumii ramani za zamani zilizokuwa zinatambulika wao wamekuwa ni kuhamisha bikoni leo iko huku siku chache baadae unakuta zimesogezwa mbele"alisema John.

Mwenyekiti wa kijiji cha Karakatonga Amos Waisahi alisema " hivi karibuni baada ya mwananchi Chacha Megoko kuuwawa  tuliitwa tukaenda Nyamwaga kuhojiwa kuhusu mauwaji lakini hadi sasa hatujapewa majibu,na kuna watu wawili waliuwawa na Tembo ambao ni Mohoni Nyagichonge na Juma Mahara lakini hatujawahi kuona Serikali ikichangia chochote mazao yanaharibika hakuna utatuzi"alisema.

Mbunge wa jimbo hilo Mwita Waitara alisema kuwa atawasiliana na Waziri wa Maliasili na Waziri wa Ardhi kufika kusikiliza kero za wananchi na kuzunguka maeneo yote yanayopakana na hifadhi ili kupitia mipaka.

"Niliambiwa nyumba zimechomwa,mazao yamefekwa na ni nje ya hifadhi ,nikiongea na hifadhi nao wanasema nyumba na mazao yaliyochomwa yako ndani ya hifadhi,nitaongea na waziri ili nao wasikilize kero zenu tupitie mipaka na tuone chakufanya " alisema Waitara.

Naye Mtendaji wa Kata ya Kwihancha David Giriri alitaja changamoto za kata hiyo zikiwemo za upungufu wa walimu 38,nyumba za walimu 65,madarasa 46,vyoo matundu 114, madawati 551, meza 63,viti 56, ofisi 12 na watoa huduma ya afya 9.

Mbunge Waitara alimwagiza mtendaji huyo kuwakamata viongozi waliopita waliofuja fedha za vibanda vya soko sh.milioni nne ambapo naye alichangia sh. milioni tano katika ujenzi wa madarasa.

Mbunge huyo akiwa katika ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa aliongozana na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya na viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tarime akiwemo katibu wa CCM wilaya Hamis Mkaruka,Katibu Mwenezi,Mrema Sollo,Katibu wa Vijana Newton Mwongi na Katibu Hamasa Remmy Mkapa.

Share:

Video Mpya: Nandy Ft. Joeboy – Number One


Video Mpya: Nandy Ft. Joeboy – Number One


Share:

Makampuni Yasiyokamilisha Urasimishaji Yanyang’anywe Kazi -Naibu Waziri Mabula


 Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza Makampuni ya Urasimishaji ambayo mikataba yake imekwisha na kushindwa kukamilisha kazi kwa wakati katika mkoa wa Arusha yanyang’anywe kazi hizo na kurejesha fedha zilizotolewa na wananchi sambamba na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Aidha, alielekeza kuwa kwa yale  makampuni ambayo muda wa kazi bado haukuisha basi yafanye kazi chini ya uangalizi ili kuhakikisha kazi waliyopewa inakamilika kwa wakati.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo tarehe 9 Januari 2021 katika mkoa wa Arusha alipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na wakurugenzi wa halmashauri akiwa katika ziara yake ya siku moja kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji kodi ya pango la ardhi.

Naibu Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, kufuatia uamuzi huo Makatibu Tawala wa Wilaya katika mkoa wa Arusha watumie mamlaka zao kuunda vikosi kazi kushirikisha halmashauri ili kuharakisha zoezi la urasimishaji kwenye maeneo ambayo makampuni ya urasimishaji yameshindwa kukamilisha kazi.

Awali Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula akizungumza na Makampuni ya urasimishaji alisema, baadhi yake yameshindwa kukamilisha kazi kwa wakati kwa visingizio mbalimbali na hata pale yalipokutana na Waziri wa Ardhi William Lukuvi Dar es Salaam na kuongezewa muda kukamilisha kazi  yalishindwa na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya zoezi hilo.

“Makampuni ambayo mikataba yake iimekwisha na kufikia Januari 31, 2021 hayajakamilisha kazi, basi yafungashe virago na kupelekwa katika vyombo vya sheria na halmashauri zishirikiane na ofisi za ardhi za mkoa kufanya kazi hiyo” alisema Dkt Mabula.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi  Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshangazwa na halmashauri kuweka malengo madogo katika ukusanyaji maduhuli ya Serikali yatokanayo na kodi ya  ardhi bila kujumuisha madeni ya wadaiwa sugu.

Alisema, mkoa wa Arusha wenye wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi zaidi ya 200 una madeni ya zaidi ya bilioni 178.943 lakini mkoa ulijiwekea malengo ya kukusanya bilioni 8.9 tu na kufanikiwa kukusanya bilioni 4.2 sawa na asilimia 47 kufikia desemba 2020.

Aliwaelekeza Maafisa Ardhi Wateule kuhakikisha inawafikisha kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi kwa kuwa tayari walishapelekewa ilani za madai kama sheria inavyoelekeza na kusisitiza kuwa, kwa wale wadaiwa wanaotaka majadiliano yafanyike ndani ya siku kumi na nne na baada ya hapo shauri lipelekwe kwenye  Baraza.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, serikali inahitaji mapato kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kusisitiza kuwa huko katika Mabaraza ya Ardhi maamuzi yake ni kulipa ama kunadiwa mali kufidia deni.

Baadhi ya Wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi zikiwemo taasisi mbalimbali katika jiji la Arusha kama vile Chuo cha Uhasibu na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) walikubali kulipa madeni yao kwa awamu ambapo Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula alielekeza kuingia makubaliano kwa maandishi.

Halmashauri ya jiji la Arusha pekee inadai jumla ya shilingi bilioni 4,134,610,533.23 za wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi na jiji hilo  limeweza kukusanya bilioni 2.27 sawa na asilimia 49.79 ya lengo kwa mwaka 2020/2021 ambalo ni bilioni 4.134.


Share:

Video Mpya: Goodluck Gozbert Ft. Bony Mwaitege – Mugambo


Video Mpya: Goodluck Gozbert Ft. Bony Mwaitege – Mugambo


Share:

Serikali Kutumia Mbinu Ya Makambi Kwa Wanafunzi Wasichana Kuwawezesha Kufikia Malengo


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imepanga kutumia Mbinu ya kuwaweka kwenye Kambi wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini,  kwa kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati, ili waweze kufanya vizuri kwenye masomo, kujitambua, kujiamini na kuweza kutimiza malengo yao.

Kwa mara ya Kwanza Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imeratibu kambi ya majaribio ya siku tano, kuanzia tarehe 4-8 Januari, 2021, Jijini Dodoma, kwa  wanafunzi wasichana 105 wa shule 18 kutoka kaya masikini zilizo chini ya mpango wa TASAF za Halmashauri ya wilaya ya Bahi, jijini Dodoma.

Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko amebainisha kuwa kufanikiwa kwa majaribio ya kambi hiyo kutawezesha serikali kupitia ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, kuendesha kambi za namna hiyo kwenye Halmashauri nyingine hapa nchini ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kaya masikini kuweza kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda, amefafanua kuwa wilaya hiyo wamepanga kuwa na utaratibu wa kuwa na kambi za wanafunzi wasichana balehe kila baada ya miezi sita kwa wanafunzi 1,324 walioko ndani ya shule. Aidha, ameeleza kuwa wilaya hiyo tayari inao mfuko wa elimu wa Halmashauri ambao utawaendeleza kieleimu wanafunzi hao hadi elimu ya chuo kikuu.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Taifa, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Audrey Njelekela, amefafanua kuwa Kambi hiyo ni sehemu ya Utekelezaji wa mradi wa TIMIZA MALENGO unaowalenga Wasichana Balehe na Wanawake Vijana walioko ndani na nje ya shule kutimiza malengo yao. Kwa sasa mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri 10 nchini za mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro ambapo mikoa ya Tanga na Geita imeongezwa kwenye mradi huo. Amesisitiza  kuwa Mradi wa kambi utatekelezwa pia katika Halmashauri za mikoa hiyo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baada ya kufunga Kambi hiyo Mratibu wa Mradi huo  wa Kambi Salum Kilipamwambu ambainisha kuwa Tafiti za elimu ya sekondari zinaonesha wanafunzi wasichana wa sekondari wamekuwa wakishindwa kuhitimu masomo yao kwa kukosa uelewa na kutojitambua na kujiamini, naye, Mwajuma Hamisi kutoka shule ya sekondari Kigwe, Bahi jijini Dodoma, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewawezesha kujitambua, kujiamini na wameongeza weledi kwenye masomo ya sayansi na Hisabati hivyo wataweza kufanya vizuri kwenye masomo na hatimaye kuweza kutimiza elimu.

 MWISHO


Share:

NHC Kuanza Kuwabana Wapangaji Wake Wasiolipa Kodi


Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA

Shirika la Nyumba la Taifa litaanza kuwabana wapangaji wake wanaodaiwa takriban Bilioni 27 ikiwa ni malimbikizo ya upangishaji nyumba zake kwa kuwatangaza na kunadi mali zao kufidia deni kufikia mwisho wa mwezi Januari 2021.

Shirika hilo la nyumba la NHC lina takriban wapangaji 17,000 katika mikoa mbalimbali nchini zikiwemo taasisi za umma na binafsi wanaodaiwa kodi nyumba kama malimbikizo ya kodi hiyo baada ya kushindwa kulipa kwa wakati.

Akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na watendaji wa Sekta ya ardhi jijini Arusha tarehe 9 Januari 2021 Meneja Huduma za Jamii na Uhusiano wa NHC Muungano Saguya alisema, kwa jiji la Arusha pekee shirika lake linadai wapangaji zaidi ya  milioni 370 na kusisitiza kuwa zoezi hilo ni la nchi nzima.

Alisema, njia pekee kwa wadaiwa wa kodi ya pango la nyumba wa Shirika hilo kuepuka kuchukuliwa hatua  ikiwemo kuwatangaza katika vyombo vya habari ni kuhakikisha wanalipa malimbikizo na kodi wanazodaiwa kabla ya januari 31, 2021.

Kwa mujibu wa Saguya, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linategemea fedha za wapangaji wake na miradi mbalimbali inayofanya kujiendesha hivyo kutolipwa fedha za upangishaji ni  kufifisha juhudi za Shirika katika  kujiendesha kibiashara.

"Shirika letu la NHC linategemea fedha za upangishaji nyumba zake na miradi kujiendesha kibiashara hivyo kutolipa kodi kunalifanya Shirika kushindwa kujiendesha kwa ufanisi" alisema Saguya.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema zoezi linaloendelea la kuwafikisha wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya liende sambamba na kuwachukulia hatua wapangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wanaodaiwa kodi ya nyumba.

Alisema, Shirika la Nyumba la Taifa linategemea kwa asilimia mia moja kujiendesha hivyo wapangaji wake kushindwa kulipa kodi kwa wakati kunalifanya kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

"Msako wa kodi ya ardhi pango la ardhi uende sambamba pia na wale wadaiwa wa Shirika la Nyumba la Taifa maana Shirika hujitegemea kwa asilimia mia moja, tusipolipa tutalikwamisha kufanya kazi" alisema Dkt Mabula.

Shirika la Nyumba la Taifa ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na mbali na upangishaji wa nyumba zake hujishughulisha pia na kazi mbalimbali kama vile ukandarasi wa miradi na upangaji miji ambapo kwa sasa linaendesha miradi ya ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mtwara na Kwangwa Mara, Ofisi za wilaya za Hai Kilimanjaro na Wanging'ombe Njombe pamoja na ujenzi wa Ofisi na nyumba 17 za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).


Share:

Wizara Ya Kazi, Vijana,ajira Na Watu Wenye Ulemavu Yakanusha Taarifa Ya Fomu Maalumu Kwa Ajili Ya Wadhamini Inayosambaa Mitandaoni




Share:

Zaidi Ya Ajira 3000 Kuzalishwa Kiwanda Cha Viatu Cha Karanga


Mwandishi Wetu
Kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi cha Karanga kinatarajiwa kuzalisha ajira 3000 katika fani mbalimbali nchini mara baada ya kukamilika ujenzi wa jengo la kuchakata bidhaa za ngozi lililo katika hatua za mwisho.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa majumuisho ya ziara yake katika kiwanda hicho alipotembelea kukagua na kuona maendeleo ya ujenzi huo tarehe 7 Januari, 2021 mkoani Arusha.

Waziri alieleza kuwa, kiwanda hicho hadi sasa kimeajiri wafanyakazi 283 kati 3000 ambapo mpaka mwezi Juni mwaka huu kinatarajia kuajiri wafanyakazi 1906 katika maeneo mbalimbali.

“Kiwanda hiki kinamanufaa kwa jamii kwakuwa kitachangia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana wetu hivyo kamilisheni kwa wakati na uzingatie thamani ya fedha zilizowekezwa,”alisema Waziri Mhagama

Waziri aliwataka kuhakikisha ifikapo Juni, 2021 mradi huo unakamilika na kuukabidhi kulingana na makubaliano ya ujenzi huo.

Aidha kiwanda kinalenga kuwa na uzalishaji mkubwa utakao changia katika uchumi wa nchi na kupata faida ili fedha zilizowekezwa na wananchi zisitumike pasipo matokeo yaliyokusudiwa.

Waziri aliwataka kuhakikisha kiwanda kinakuwa endelevu na kuzalisha bidhaa zenye viwango ili kujihakikishia soko la uhakika.

“Hakikisheni mnatoa bidhaa zenye ubora na anzeni kutafuta masoko ili kuepuka changamoto ya soko la uhakika,”alisema

Naye Msimamizi wa Ujenzi wa kiwanda hicho Dkt. Miragi Katumbili aliahidi kuendelea kisimamia na kuhakikisha kiwanda kinakamilika kwa wakati ili kusaidia ajira hizo kwa vijana pamoja na kuahidi kuendelea kusimamia kwa ufanisi wa hali ya juu.

“Tunaahidi ujenzi utakamilika kwa wakati, kama uliyotupa miezi sita,na ifikapo mwezi Juni 2021 tutakuwa tumekabidhi mradi huu,”alisema Mhandishi Mitagi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba aliahidi kutekeleza maelekezo ya waziri ikiwemo kuendelea kutoa fedha za ujenzi huo kwa wakati.

Alieleza matarajio ni kukamilisha ujenzi kwa wakati na kufikia malengo ya kuzalisha bidhaa kwa wingi zenye kuchangia kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

“Kama wafadhili wa mradi huu,tutahakikisha tunatoa fedha na malighafi kwa wakati ili kutokwamisha ujenzi huu unaoendelea,”alisema Kashimba.

Alimwakikishia Waziri uwepo wa soko kubwa la viatu ndani na nje ya nchi ambapo hadi sasa kiwanda kimepokea mahitaji ya kutengeneza viatu 48000 na kueleza ni ishara nzuri kwa kiwanda hicho.


Share:

Super Nhesha: Dawa Bora Ya Kutibu Tatizo La Kisukari


 DODOMA!! DODOMA!! DODOMA!!
KWA WALE WENYE MATATIZO YA SUKARI AU KITAALAMU: (DIABETES MELLITUS)
NINI CHANZO CHA TATIZO HILI LA SUKARI.

KUNA VYANZO VINAVYOWEZA KUSABABISHA SUKARI:
(1) Shinikizo la damu (B.P) (2) Viwango vya juu vya triglyceride (Mafuta)
(3) Vyakula vyenye mafuta mengi na wanga
(4)Utumiaji wa pombe kupita kiasi 
(5)Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi (6)Mtindo wa maisha usiofaa kiafya (7)Uzito unene uliozidi (8) Kutofanya mazoezi

NINI DALILI ZA KUWA NA TATIZO LA SUKARI
(1) Kuhisi njaa mara kwa mara (2) Kuhisi kiu mara kwa mara
(3) Kupungua uzito 
(4) Maono machafu 
(5) Uchovu mara kwa mara
(6) Ukipata kidonda hakiponi 
(7) Kushuka kwa kinga mwilini pia kwa wanaume wenye tatizo hili wanakuwa na  tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kama vile kukosa hamu ya tendo la ndoa,  kulegea na kusinyaa, kuwahi kufika kileleni, maumivu ya mgongo, Kiuno, Tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kutopata choo vizuri

SASA TIBA IMEWASILI KWA
Kwa kutumia tiba za asili Dawa ya mitishamba ilyokatika mfumo wa vidonge asilia Dawa inaitwa NHESHA POWER kwa kutumia Dawa hizi utapona tatizo hilo ndani ya siku 14 tu na hautaliona tena katika maisha yako.
 
BABU MADUHU atakuwepo Dodoma kuanzia Tarehe 25/01/2021 hadi tarehe 10/02/2021kwa hapa Dar es salaam tunaendelea   kutoa huduma zetu Ofisini hapa Magomeni, Moroco Hotel/Kanisani
Simu No. 0755 684 297, 0788 330 105, 0652 102 152
**** Karibu Tukuhudumie****
 


Share:

Naibu Waziri wa Ujenzi: Tumieni Fursa Za Ujenzi Wa Miundombinu Kukuza Uchumi


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,  amewataka wakazi wa mikoa ya Songwe, Rukwa, Katavi na Kigoma kutumia fursa za ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya barabara na bandari katika mwambao wa Ziwa Tanganyika ili kukuza uchumi katika maeneo yao.

Amesema hayo  alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za Mpanda-Vikonge (km 35), Kasinde – Mpanda (km 105.389), Kagwira – Karema (km 112) na bandari ya Karema mkoani Katavi ambayo ujenzi wake unaendelea.

Amezitaja fursa hizo kuwa ni kupata ajira kwa wale wenye taaluma, kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na biashara katika mwambao wa ziwa Tanganyika ambao umeanza kuvutia wawekezaji wengi katika siku za hivi karibuni.

“Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 47 za kitanzania kwa ajili ya kujenga bandari ya kisasa ya Karema awamu ya kwanza na mchakato wa kuijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Kagwira – Karema (km 112) inayoelekea katika bandari hiyo utaanza hivi karibuni”, amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Amezitaja bandari nyingine zinazojengwa katika ukanda wa Ziwa Tanganyika kuwa ni Kabwe na Kasanga ambazo zote zitakapokamilika zitaongeza huduma za usafiri na uchukuzi katika Ziwa Tanganyika na nchi jirani hivyo kukuza biashara katika mwambao huo.

Aidha, amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi, kuhakikisha barabara ya Kagwira -Karema (km 112) inayounganisha mji wa Mpanda na bandari ya Karema inapitika wakati wote ili kuharakisha ujenzi wa bandari  hiyo na hivyo  kuwezesha wawekezaji kufika kwa urahisi katika eneo hilo ili kuona fursa za kiuchumi na kijamii.

Naye, Meneja wa TANROADS mkoa wa Katavi, Mhandisi Martin Mwakabende, amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa kiasi cha shilingi bilioni 1.2 za kitanzania zimetengwa kwaajili ya kuiboresha barabara hiyo  kipindi hiki cha mvua nyingi wakati mchakato wa kuijenga kwa kiwango cha lami ukiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando, amesema kuwa Wilaya yake imejidhatiti kuhakikisha wakandarasi  wote wanaosimamia miradi katika eneo hilo wanapata ushirikiano wa kutosha ikiwemo ulinzi na watumishi wenye sifa ili kukamilisha miradi ya ujenzi kwa wakati.

Bandari ya Karema ambayo inatarajiwa kuwa kubwa katika ukanda wa Ziwa Tanganyika inajengwa na mkandarasi  XIAMEN ONGOING CONSTRUCTION GROUP toka China na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Kukamilika kwa bandari hiyo iliyoko wilayani Tanganyika mkoani Katavi kutachochea biashara kati ya Tanzania na nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia na Burundi na hivyo kukuza uchumi katika mikoa ya ukanda wa magharibi.


Share:

Wimbo Mpya 2021: NTEMI OMABALA 'NG'WANA KANG'WA' - NDAGU


Msanii maarufu wa Nyimbo za asili Ntemi Omabala 'Ng'wana Kang'wa' kutoka Kahama Mkoani Shinyanga ameachia wimbo mpya 2021 unaitwa Ndagu. Usikilize hapa 

Share:

MPANGO JUMUISHI WA LISHE WA TAIFA UNATAMBUA VIONGOZI WA KISIASA KAMA WADAU MUHIMU KATIKA KUIMARISHA LISHE

 

MKURUGENZI wa Shirika la Agri Thamani (MB) Mh Neema Lugangira akisisitiza jukumu la viongozi Wanawake wa UWT kuhakikisha wanasimamia malengo ya Lishe yaliyowekwa kwenye ilani ya Uchaguzi inayotekelezeka kushoto ni Mratibu wa Lishe kutoka Tamisemi Mwita Waibe
MKURUGENZI wa Shirika la Agri Thamani (MB) Mh Neema Lugangira akisisitiza jukumu la viongozi Wanawake wa UWT kuhakikisha wanasimamia malengo ya Lishe yaliyowekwa kwenye ilani ya Uchaguzi inayotekelezeka
Mratibu wa Lishe kutoka Tamisemi Mwita Waibe akisistiza jambo wakati wa semina hiyo
MSHIRIKI kutoka wilaya ya Kyerwa akiomba Shirika la Agri Thamani liandae vitini kwa ajili yao ili waingie field maana hawana muda wa kupoteza hii ni ajenda kuu
VIONGOZI wa Wanawake (UWT) kutoka wilaya za Kyerwa ,Ngara ,Karagwe na Missenyi wakifuatilia semina hiyo
Viongozi wanawake wakifuatilia semina hiyo



MPANGO  Jumuishi wa Lishe wa Taifa wa Mwaka 2016-2021 unatambua Viongozi wa Kisiasa kama Wadau Muhimu katika kuimarisha Lishe Bora na kutokomeza udumavu na aina zote za utapiamlo nchini Tanzania. 

Kulingana na utambuzi huo, Agri Thamani imeendelea na mpango unaolenga kuwajengea uelewa wa kina Viongozi wa Kisiasa ili waweze kutumia ushawishi wao kwenye jamii kuchangia kubadilisha mfumo mzima wa mahusiano yetu na chakula na pia waweze kufuatilia, kutathmini na kusimamia utekelezaji wa mipango mizuri inayowekwa na Serikali. 
 
Akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa UWT wilaya nne za Mkoa wa Kagera ,Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Neema Lugangira (MB) amesema katika jitihada za kuhakikisha kuwa mkoa huo  unatokomeza Udumavu maana ndio Mkoa unaongoza kwa Idadi Kubwa Zaidi ya Watoto chini ya Umri wa Miaka 5 wenye Udumavu; 
 
Alisema Shirika hilo  lilianzisha Programu ya kuwafikia Viongozi wa Jumuiya ya Umoja Wanawake Tanzania (CCM) ili kuwajengea uwezo kwa lengo la kupata uelewa juu ya umuhimu wa lishe bora na hatimaye kuweza kuwa chachu ya kutokomeza udumavu kwenye maeneo yao.
 
"Kama mnavyojua Makao Makuu ya Agri Thamani yapo kwenye Majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera hivyo ni muhimu kwa Agri Thamani kuweka mikakati thabiti na endelevu ili Mkoa wa Kagera uwe Mkoa wa Mfano katika Vita Dhidi ya Udumavu na Utapiamlo kwa Ujumla", alisema Mhe Neema Lugangira (Mb) - Mkurugenzi wa Agri Thamani.

Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi cha mwezi  Desemba 2020 hadi Januari 2021 Agri Thamani ilishatoa Semina za Lishe Viongozi wa UWT kutoka Kata zote za Wilaya za Muleba,  Bukoba Mjini na Bukoba Vijijini. Pia, Agri Thamani imeshatoa Semina ya Lishe kwa Madiwani wa Viti Maalumu kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kagera. 

Alisema kwa sasa Shirika hilo la Agri Thamani limekamilisha Mafunzo ya Lishe kwa Awamu ya kwanza kwa kuwafikia Viongozi wa UWT kutoka Kata zote za Wilaya za Ngara, Kyerwa, Karagwe na Missenyi. 

Mafunzo haya yalitolewa na Mbunge Neema Lugangira na Mratibu wa Lishe kutoka TAMISEMI, Ndg. Mwita Waibe. 

Hata hivyo Viongozi hao wa UWT walionekana kushtushwa na  hali ya lishe kwenye Mkoa na maeneo yao  kwa namna ambavyo watoto wanaweza kupata athari pasipo mzazi kujua kumbe ambazo zinasababishwa na masuala ya kilishe. 
 
Kwa umoja wao waliazimia kuwa wanakwenda kuhoji kuhusu hali ya lishe kwenye Kata zao, mikataba ya lishe iliyosainiwa kwenye kata zao, bajeti za lishe zinazotengwa na Halmashauri zao na pia ajenda ya lishe inakwenda kuwa ya kudumu kwenye shughuli zao. 
 
Pia Waliaidi kuanza kutoa mafunzo kwa jamii na wameiomba Agri Thamani iandae mafunzo ya vitendo hususan kwenye eneo la namna bora ya kuandaa na kupika chakula chenye lishe bora kwa mama mjamzito, mama anaenyonyesha na mtoto chini ya umri wa miaka 5. 
 
 Katika Awamu ya Pili ya Mafunzo haya, Agri Thamani inatarajia kuwafikia Viongozi wa UWT na Madiwani kutoka Mikoa ya Kigoma, Tanga, Tabora, Lindi na Geita kwa Wilaya zitakazochaguliwa. Aidha, chini ya Programu hii hatua inayofuata ni kuwafikia Wenyeviti wa Serikali za Mitaa/Vijiji/Vitongoji, Watendaji wa Kata, na Viongozi wengine Ngazi ya Kata, Kijiji, Kitongoji na Jamii kwa jumla. 

Mbunge Neema Lugangira alimalizia kwa kusema wadau wote tukishikiriana kwa karibu na kila mmoja kwa nafasi yake akaibeba Ajenda ya Lishe vita dhidi ya kutokomeza udumavu na utapiamlo tutaishinda ndani ya miaka mitano hii 2020-2025

Share:

SERIKALI YA TANZANIA YAAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA TASNIA YA HABARI


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa
**
Serikali imesema inatambua mchango wa sekta ya habari na kuahidi kuzishughulikia changamoto za tasnia hiyo kwa kufanya maboresho, kupitia sheria na mikutano na wanahabari.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dae es Salaam, Januari 9, 2021.

Baadhi ya changamoto zilizoibuliwa na waandishi wa habari ni pamoja na waandishi kukosa mikataba ya kudumu ya kazi, kufanya kazi kwa kujitolea kwa muda mrefu, bei kubwa ya kusajili ' Blogs na Online TV', wasemaji wa taasisi za serikali kutotoa ushirikiano katika masuala yanayohitaji ufafanuzi kwa kero za jamii na wavamiaji wa taaluma.

Akizijibu changamoto hizo, Waziri Bashungwa amesema atashirikiana na wizara nyingine ikiwemo ya kazi ili kutatua suala la ajira kwa wanahabari.

''Suala hili la ajira kwa mujibu wa sheria kama lilikua halisimamiwi, basi nitashirikiana na Wizara ya Ajira kuhakikisha waandishi wanapata mikataba na suala hili halina mjadala na tutalifanyia kazi'' amesema Waziri Bashungwa.

Sambamba na hilo Waziri Bashungwa, amesema wizara yake inaandaa utaratibu wa kuzungumza na wamiliki wa vyombo vya habari lengo ni kuweka ushirikiano katika kutimiza malengo ya serikali na kuboresha stahiki za wanahabari.

Chanzo - EATV

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili January 10



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger